Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1292 | 1293 | (Page 1294) | 1295 | 1296 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Ayoub Nyenzi amekana kujiengua na klabu hiyo kama vyombo vya habari vinavyosema hasa baada ya kutofautiana na moja ya viongozi wakati wa ugawaji wa mapato ya Uwanja kati ya mechi ya Kimataifa ya Yanga dhidi ya Medeama ya nchini Ghana.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Nyenzi amesema kuwa kauli yake ilichukuliwa sivyo na vyombo vya habari kwani yeye alikuwa anatetea maslahi ya watendaji wengine na hata hivyo suala hilo lilimalizika baada ya kesho yake kufanyika kwa mgawanyo huo wa mapato na kila mmoja kupata stahiki zake. "Ni kweli  nilisema kauli hiyo hasa baada ya kuona ule utaratibu uliokuwa umepangwa wa kila siku wa mgawanyo wa fedha pale pale uwanjani kushindikana na kushindwa kuelewana na kufikoa kusema vile ila kwa kila kitu kipo sawa,".

  Amesema, kwa sasa anaendelea na majukumu yake ya ujumbe wa kamati ya utendaji na hajaandika barua yoyote ya kusema kuwa anataka kujiengua katika klabu ya Yanga ila zaidi amewataka wana Yanga wote wawe na imani nae.

  Nyenzi amesisitiza na kusema kuwa yeye bado ana majukumu ndani ya klabu ya Yanga na amewaomba wanachama kuendelea kumuamini kwani pale alikuwa anawatetea ila kwa sasa yameshaisha waendelee kuijenga timu.

  0 0


  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakipita kukagua ndani ya ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma leo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Kikwete akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kushoto) na wajumbe wengine wakipita kukagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jakaya Kikwete akitoa ufafanua wa jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi,anaefuta ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonesha Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete moja ya alama ya wajumbe watakaokuwa wamefika kutoka mikoa mbalimbali
  . PICHA NA MICHUZI JR-MMG

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  TANZANIA imeshika nafasi ya nne katika ripoti ya utafiti wa matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kukosa sera ya uratibu fedha kutoka ngazi ya juu hadi chini.

  Akizungumza leo na wadau wa mabadiliko ya Tabianchi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga amesema kuwa kama hakuna nia ya dhati kuwa na sera ya matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi Tanzania itaendelea kuwa nafasi hiyo.

  Amesema kuwa nchi ya Rwanda ndio imeshika nafasi ya kwanza kutokana na kuweka sera nzuri katika uratibu na ufatiliaji wa matumizi ya fedha kutoka ngazi ya juu hadi chini.

  Mwanga amesema nchi ya Burundi ndio imekuwa ya mwisho katika ripoti hiyo ambapo kutokana na Tanzania na Burundi zinahitaji kuwa na mkazo wa kuwa na sera ya matumizi ili kuweza nchi zinazofadhili zisiwe kuacha.

   Aidha amesema nchi ya Uganda ndio inamfumo mzuri kutokana na kuwa na kituoa cha taarifa ya fedha za matumizi ya mabadiliko ya tabianchi.

  Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thabit Jacob,amesema kuwa kunahitajika elimu zaidi katika maeneo ya vijijini juu ya mabadiliko ya tabianchi.

  Amesema Tanzania ikiweka mkakati wa kuwa na sera ya matumizi ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi tunaweza kuondoka na nafasi kutokana na kuwa na sera vitu vingi na vimeweza kufanikiwa.
  Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga akizungumza na wadau wa mabadiliko ya Tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.
   Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma, Thabit Jacob akifafanua jambo  kwa wadau wa kupambana na mabadiliko ya Tabia ya Nnchi jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (CAN), Sixbert Mwanga  akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Mwene Said, Globu ya Jamii.
  Upande wa utetezi, katika rufani ya kesi inayomkabili Kamishna wa zamani wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wanaokabiliwa na mashtaka ya kujipatia Dola za Marekani million sita, leo uliomba kuahirisha kusikilizwa rufani hiyo baada ya mawakili wawili kuwa na udhuru ikiwamo ugonjwa.

  Dk. Masumbuko Lamwai alitoa maombi hayo leo mbele ya Jaji Edson Mkasimongwa aliyepangiwa kusikilizwa rufani ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na maombi ya dhamana ya washtakiwa hao katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

  Dk. Lamwai alisema kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa rufani ya Jamhuri kupinga kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha lakini Wakili Majura Magafu alikuwa na kesi nyingine katika Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. Pia, alidai kuwa mwingine mwenye udhuru ni, Wakili Alex Mgongolwa ni mgonjwa ameshindwa kufika mahakamani kuendelea na kesi hiyo kwamba ni busara Mahakama ikapanga tarehe nyingine ili kusikiliza rufani pamoja na maombi ya dhamana.

  Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Osward Tibabyekomya akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Awamu Mbaga na Theophil Mutakyawa, alidai kuwa hana pingamizi na ombi la utetezi.

  Mbali na Dk. Lamwai, mawakili wengine wa utetezi ni, Dk. Ringo Tenga, Misangi Nzerahula, Godwin Nyaisa na Alex Mshumbusi.

  Jaji Mkasimongwa alisema baada ya pande zote mbili kukubaliana kuahirisha kesi hiyo, Mahakama yake itasikiliza rufani pamoja na maombi ya dhamana Julai 29, mwaka huu.
  Awali Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, ilifuta shtaka la nane la kutakatisha fedha dhidi ya washtakiwa.

  Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga uamuzi wa kuliondoa shtaka hilo kwamba haukuridhika na uamuzi uliotolewa na Hakimu Mchauru.

  Hoja nyingine, Hakimu Mchauru alikosea kusema hati ya mashtaka ina dosari wakati siyo kweli.

  Hoja ya tatu, upande wa Jamhuri unaeleza kwamba uliomba nafasi kwa kuwa kifungu cha 234 kidogo cha (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), hakimpi hakimu madaraka ya kuruhusu kubadilisha hati kama kweli mahakama iliona ina dosari za kisheria.

  Mbali na Kitilya, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ambao wote wanasota rumande ni aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996 Shose Sinare na mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon. 
  Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani hapo kwa mara ya kwanza Aprili mosi, mwaka huu, wakikabiliwa na mashitaka manane likiwemo la kutakatisha fedha Dola za Marekani milioni 6 mali ya Serikali. 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu, Dkt.Heren Kijo Bisimba wakati wakizungumza na waandishi wa habari wakati wakitoa hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha nusu mwaka jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwanasheria  Mtafiti wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu, Paul Mikongoti.
  Mkurugenzi wa uwezeshaji wa uwajibikaji, Imelda Urio akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa Haki ya haki za binadamu kwa kipindi cha nusu mwaka, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu, Dkt.Heren Kijo Bisimba 

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum(watatu kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea kwa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani.Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani jijini.Kutoka kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Janester Emily,Kaimu Afisa elimu shule za msingi kinondoni,Chitegese Dominic, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ally Salum akimsalimia mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mchangani iliyopo Mwananyamala Kisiwani jijini, Hashim Jumanne baada ya kupokea msaada wa madawati 500 kwa niaba ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation jana.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondo jijini Dar es Salaam, Ally Salum akiongea na wanafunzi pamoja na Uongozi wa Shule ya msingi Mchangani iliyopo mwananyamala Kisiwani, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa madawati 500 yaliyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule za 5 za kata ya Mwananyamala Kisiwani,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza.


  0 0

   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
  Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Na Ally Daud-Maelezo
  Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.

  “Tunatambua vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.

  Aidha Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha  wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.

  Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo haja ya  watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima.

  Mkutano huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu.

  0 0

  Na Mwene Said, Glogu ya Jamii.
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepiga kalenda kesi inayomkabili Kamishna wa Kodi na Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki  na wenzake  hadi Agosti 23, mwaka huu baada ya upande wa Jamhuri kudai upelelezi wake bado haujakamilika.

  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  Alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

  Hakimu Shahidi alisema dhamana ya washtakiwa inaendelea na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 23, mwaka huu.

  Mbali ya Masamaki, washtakiwa wengine ni, Haroun Mpande wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi Mrema,  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary , Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis  na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan .

  Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Juni Mosi na Novemba 17, 2015 walikula njama kwa kuidanganya serikali.

  Washtakiwa hao, wanadaiwa kudanganya kuwa  Makontena 329 yaliyopo katika Bandari Kavu ya Azam (AICD) yalitolewa baada ya kodi zote kufanyika wakati wakijua si kweli.

  Katika shitaka la pili,  wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho hicho jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 12.7 bilioni.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
   Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki  kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.

  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
  Serikali imewataka wataalam wa vyuo Vikuu vinavyotoa mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi waitumie taaluma yao katika kutafuta suluhisho la migogoro ya Ardhi inayowakumba wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.


  Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila amesema kuwa wataalam hao wanalo jukumu la kufuatilia migogoro inayotokea nchini na kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalam utakaotoa majibu ya utatuzi wa migogoro hiyo.


  “Ninyi kama watalaam wa sekta ya Ardhi lazima mtoe majibu kwa nini migogoro ya ardhi inaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali licha kuwepo kwa kanuni, Sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya Ardhi nchini” Amesema Prof.Msanjila.


  Ameeleza kuwa wao kama watalaam wa sekta hiyo wanatakiwa kwenda zaidi kwenye matatizo halisi na kuwawafikia wananchi wengi zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili  kuondoa changamoto zao kuliko kucheza na vitabu na kuongea kwenye Ofisi.


   Amewataka wataalam hao hasa wale walioko nchini Tanzania kufika katika maeneo yenye migogoro ya Ardhi ikiwemo Morogoro na maeneo mengine ili kuangalia kwa nini wananchi wanaendelea na mapigano tunajua ipo migogoro ya Ardhi inayotokea katika mikoa ya Morogoro, Pwani na mikoa mingine.


  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali suala la ufumbuzi wa migogoro ya Ardhi linaendelea kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa ardhi inaendelea kutolewa kwa kuzingatia sheria pia kushughulikia changamoto zote zinazokwamisha ustawi wa sekta ya ardhi hususan uondoaji kero zote zinazokwamisha matumizi bora ya ardhi kwa jamii.


  Akifafanua kuhusu nafasi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika mkutano huo ameeleza kwamba kupitia mkutano huo wa kitaalam wa masuala ya Ardhi, Wizara hiyo inajifunza kuhusu  changamoto zitakazojitokeza na kuibuliwa ili ziwekwe kwenye mitaala kwa lengo la kuwaandaa watalaam watakaokuwa na uwezo wa kusuluhisha matatizo yote yanayojitokeza kwenye sekta hiyo.


  Amesema kuwa Sekta ya Elimu kupitia mkutano huo itaboreshwa kwa kupata nyongeza ya utalaam kutoka kwa wataalam kutoka Vyuo vikuu vya nchi mbalimbali za Bara la Afrika waliohudhuria mkutano huo na kuongeza kuwa Chuo Kikuu Ardhi nchini Tanzania ambacho kimebobea kwenye masuala ya Ardhi kitapata taarifa zaidi katika uboreshaji wa mitaala na mafunzo ya Programu za Utawala wa Ardhi, Ugawaji wa Ardhi na Upimaji wa Ardhi”


  Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza mara baada katika mkutano huo amesema kuwa wataalam wa Ardhi nchini Tanzania bado wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya sekta ya Ardhi na kufafanua kuwa wao kama chuo kinachozalisha watalaam wa Ardhi wanalo jukumu kuzalisha watalaam watakaofanya usimamizi thabiti wa Ardhi kukabiliana na changamoto zilizopo.


  “Sisi nafasi yetu kama Chuo Kikuu Ardhi ni kujua ni namna gani tunavyoweza kuzalisha wataalam wa kutosha wenye weledi watakaoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizoko kwenye sekta ya Ardhi pia kuhakikisha wataalam tunaozalisha wanakidhi ubora na matarajio ya wananchi” Amesema Prof. Mshoro.


  Amesema kuwa wanataaluma kutoka Tanzania watanufaika kutokana na mkutano huo kwa kuwa unawajumuisha watalaam wa Ardhi kutoka takribani nchi 9 watakaobadilishana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali za ardhi zinazojitokeza katika maeneo yao na namna wanavyozitatua.


  Aidha, amesema kuwa Sekta ya Ardhi nchini Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa watalaam wa kutosha  ambao wangeweza kusimamia maamuzi katika masuala ya Ardhi ngazi za chini na kuongeza kuwa ili kupata maamuzi na taarifa sahihi za ardhi ni lazima suala la uwepo wa watalaam hao liendelee kupewa kipaumbele.


  Kuhusu mchango wa watalaam hao katika utatuzi wa migogoro ya Ardhi amesema kuwa ipo haja ya watalaam waliopo kutumika ipasavyo kutatua migogoro inayojitokeza na kuwaletea manufaa wananchi ambao wanahitaji huduma za wataalam hao.


  Amesema kuwa kwa upande wa Serikali tayari watalaam wa sekta husika wamejipanga kuhakikisha kuwa wanapata suluhisho la mgogoro inayojitokeza kupitia sheria zilizopo.


  Mkutano huo unaohusisha Mtandao wa vyuo Vikuu ni wa nane  tangu kuanzishwa Mtandao wa EALAN mwaka 2009 ambapo kwa mwaka huu Chuo Kikuu Ardhi, Tanzania kimekuwa mwenyeji wa Mkutano huo kufuatia kuteuliwa kuwa kituo Maalum Cha Mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi Barani Afrika.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Watetezi haki za watoto wakiwa katika picha ya pamoja baada katika mkutano wa kujadili juu ya kutaka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe  uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurgenzi wa Shirila Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti akichangia maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano wadau wa masuala ya watoto uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa masula ya watoto wakisikiliza maada katika mkutano wa kujadili ndoa za utotoni katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  TAKWIMU zinaonyesha kwamba mimba za utotoni zimeongezeka kwa wastani wa asilimia nne kutoka asilimia 23 mwaka 2010,hadi kufikia asilimia 27,mwaka Jana kutokana na kukosa uwekezaji kwa watoto wa kike.

  Akizungumza kwenye mkutano wa Nijali Media Dialogue ulioandaliwa na Shirika la C-SEMA, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA),Christina Kwayu, amesema wasichana wenye umri chini ya miaka  18 wamekuwa wakiolewa kwa idadi kubwa.

  Amesema ndoa hizo zinasababisha  kuwepo kwa mimba za utotoni na ndio nas kufanya wadau wa masuala ya watoto kupigia kelele juu ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe ili kuweza msichana kutimiza malengo yake.

  "Japo baadhi ya imani ya dini zinasema mtoto chini ya miaka 18 anaweza kuolewa lakini haijatoa nafasi ya kumlazimisha msichana kuolewa",amesema Kwayu.

  Naye Mkurugenzi Wa Shirika la Utu wa Mtoto, Koshuma Mtengeti, amesema kati ya watoto watano,watoto wawili wanaolewa hapa nchini.

  Amsema hukumu iliyoyolewa na mahakama kuu kuhusu umri wa mtu kuolewa kuwa ni miaka 18, itumiwe kama sehemu ya kuwashitaki wale wote wanaooa watoto.

  Mtengeti, mchakato wa kubadilisha sheria ya ndoa umefika katika hatua nzuri na kuwataka wadau wote kuwa na nguvu ya pamoja katika kumtetea msichana waTanzania.

  Amesema utekelezaji wa hilo litafanikiwa pale wadau wote wataposhinikiza wabunge kubadilisha sheria hiyo na kuwataka watunge Sera na sheria walichukue hilo na kulifanyia kazi.

  Kwa upande wake,Afisa Jinsia kutoka Shirika la Kimataifa  la Vijiji vya Watoto(SOs), Catherine Kasimbazi, alisema kubadilishwa kwa vipengele ambavyo vina mkandamiza mtoto ni hatua nzuri katika msichana kuweza kupata utu wake.

  Amesema dhamira ya Nijali ni kuwajali watoto na kwamba sheria ya ndoa ikibadilishwa usawa kati ya mtoto wa kike na wakiume utakuwepo.

  Mkutano huo ulioandaliwa na Csema kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Australia uliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za watoto.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo, amewataka waalimu wenye tabia ya kujihusisha katika mahusiano ya kingono na wanafunzi wao, kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaatarisha ajira na maisha yao.

  Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua madarasa ya kidato cha tano na sita (5 -6) katika shule kongwe ya Sekondari ya Mdabulo iliyopo katika kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo akizindua kuanza kwa madarasa ya kidato cha 5-6.

  Mh. Jaffo amesema, katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano Mwalimu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu za maadili ya mtumishi wa umma sanjari na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na kubainisha kuwa tayari zaidi ya Waalimu 10 wamebainika na kuadhibiwa.

  Aidha, Waziri Jaffo ameuagiza uongozi wa halmashauri na Wilaya hiyo kusimamia haki na sitahiki za waalimu Wilayani huo ikiwepo kero sugu ya kutopandishwa madaraja inayolalamikiwa na waalimu nchini kote na kuangeza kuwa, kwa kutatua kero zao, itawajengea hali na shauku ya kufanya kazi kwa bidii hivyo kuinua kiwango cha elimu nchini.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo alipowasili katika hospitali ya Wilaya Mafinga.

  Shule ya Sekondari Mdabulo imeanza rasmi kutoa elimu ya juu ya sekondari  kwa wanafunzi wa kike pekee wapatao 70 kupitia michepuo ya HGL na HKL.

  Pamoja na uzinduzi huo, naibu waziri JAFO alifanya ziara katika Zahanati ya Idunda, chamzo cha maji katika mji wa Mafinga, kukagua  utoaji huduma na kuzindua ufanyaji kazi wa mashine mbili za Ultra sound katika Hospitali ya Mafinga kisha akahitimisha kwa kuzungumza na watumishi wa Halmshauri za Mufindi.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo akizungumza na umati wa wanafunzi na wazazi katika shule ya Sekondalri Mdabulo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KATIBU Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kupata kikosi cha timu B cha vijana wa chini ya miaka 20 kwani kwa sasa wameshateua wachezaji na wanatarajia kumfanya mchujo kamili ili kuunda kikosi hicho.

  Maboresho hayo yanafanywa kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho cha vijana na hasa baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kuanzisha ligi ya vijana Kwa timi zote zinazoshiriki ligi kuu na itakwenda sambamba na ratiba ya ligi kuu Vodacom itakayoanza Agosti 20 mwaka huu.

  Deusdedit amesema kuwa kwa sasa Kocha wa vijana anaendelea na programu yake kama kawaida na atakapokuwa tayari atatoa tathmini yake juu ya wachezaji wote na kisha kufanya mchujo wa mwisho na kisha kuendelea na na mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo ya vijana.

  "Kwa sasa kocha anaendelea na kazi ya kuwaangalia wachezaji waliopita mchujo wa kwanza, programu imaendelea katika uwanja wa Kaunda na itakapokuwa tayari mwalimu ataweka wazi wachezaji watakaoonesha kiwango kizuri na kuanza mazoezi rasmi ya ligi ya vijana,"amesema Deusdesit.

  Wakati huo, Deusdedit amesema kuwa uongozi wa Yanga hauna taarifa zozote juu ya mkataba wa kurusha haki za matangazo kwa kampuni ya Azam kuwa wao hawana taarifa hizo na wala hawakuhusishwa wakati wa makubaliano yoyote. Kwa sasa tupo kwenye mikakati ya kujadiliana na tutaoa tamko letu juu ya mkataba huo na zaidi tutaongelea suala la kutokuchukua fedha zile za awali.

  0 0

  WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

  MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM

  1.0.  MAISHA YAKE

  Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke  na watoto saba.  Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

  Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora  za jamii na kero zao zinaondoka.

  2.0.  ELIMU NA MAFUNZO

  Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera.  Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza  na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na  Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa  .

  Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati.  Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi  katika Jeshi la  kujenga Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha.  Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.

  Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988.  Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

  3.0.  UZOEFU WA NDANI YA  SERIKALI

  Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati.  Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu  hadi mwaka  1995.

  Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa Kagera.  Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia  hadi mwaka 2000.  Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa.  Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005. 

  Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa.   Baada ya uchaguzi, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya   Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka 2010.

  Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne  kuwa  Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato.  Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

  Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa  ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

  Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

  4.0.  UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

  Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa. 

  Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi.  Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

  Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

  5.0.  UFANISI KATIKA UONGOZI

  Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile.  Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini. 

  Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba. 

  Akiwa Waziri wa Ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha, alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

  Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi zake.  Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote.  Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”.  

  Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini. Wakati  akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo,  kama vile samaki,  ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake.  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”. 

  Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

  6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 – 2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI

  Ilani ya uchaguzi ya CCM  ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

  Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:

  ·    Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.

  ·    Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya  uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.  Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;

  ·     Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;

  ·     Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;

  ·     Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;

  ·      Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;

  ·      Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;

  ·       Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.

  ·       Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;

  ·       Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.

  HITIMISHO
  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania  washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa  ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati uaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

  0 0

  Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, akizungumzia maandalizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza, ambao tayari wameanza kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 23,2016 ambapo pamoja na mambo mengine pia Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

  Katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatarajiwa kumpitisha kwa kura za ndiyo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, akipokea Uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoani Mwanza, wamesema wana imani kubwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ambaye anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa.


  Katibu Mwenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, ameyasema hayo hii leo, wakati akizungumzia maandalizi ya wajumbe hao ambao baadhi yao tayari wamewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 23 mwaka huu.


  “Sisi wajumbe tunaotoka Mkoa wa Mwanza tunaamini kwamba anatosha (JPM) na yuko makini na chama chetu kitaendelea kuimarika zaidi akikabidhiwa uongozi. Amesema Mangelepa na kuwasihi viongozi wengine wa CCM kuanzia ngazi ya Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa, kuendelea kukiimarisha chama, ikiwemo kusimamia vizuri Ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge kama Rais Magufuli anavyosisitiza.


  Ametanabaisha kwamba wananchi wakiwemo wanaccm, wanayo matumaini makubwa kwa Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi, na kwamba wapenda amani na maendeleo wanaochukia rushwa pamoja na ubadhirifu wanampenda sana.


  Katika hatua nyingine Mangelepa amepuuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba hiyo inaashiria hofu waliyo nayo baada ya kukabidhiwa uongozi wa CCM kwa kuwa watakosa hoja za kuzungumza kisiasa.
  Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na madiwani katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, ambapo alionesha kukerwa na halmashauri hiyo kushindwa kufungua Zahanati kwa wakati, huku zahanati hizo zikiwa zimeshakamilika, Kikao hicho hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. kulia ni Katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS), Z.M Samataba.
  Katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS)Z.M Sabatama akizungumza na madiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magawa, Juma Abed akizungumza na madiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
  Sehemu ya madiwa walio fika kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani. (picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  0 0

  Na Eleuteri Mangi

  Mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika wametembelea chanzo cha maji cha Ruvu Chini uliopo Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujionea namna Tanzania ilivyojizatiti katika kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika wakati wote.

  Akizungumzia ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwewe amesma kuwa mradi wa Ruvu Chini unahudumia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
  Mhandisi Kamwewe aliwaambia Mwaziri hao kuwa chanzo hicho cha maji kinauwezo wa kuzalisha maji yapatayo lita milioni 275 kwa siku ambapo jiji la Dar es salaam peke yake wakazi wake wapatao zaidi ya milioni tano wanatumia maji kiasi cha lita milioni 450 kwa siku.

  Kiasi kingine cha maji mengine ambayo yanatumika jijini dare s salaam Mhandisi Kamwewe alisema kuwa yanazalishwa katika chanzo cha maji cha Ruvu Juu ambapo zinazalishwa lita milioni 186 kwa siku.

  Mhandisi Kamwewe aliongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika kwa wakazi wa mikoa ya Pawani na Dar es salaam kwa manufaa ya maendeleo yao na kwa ujmla taifa.

  Aidha, Serikali inaendelea kuhakikisha miundombinu ya maji inakuwa imara na bora wakati wote ambapo kwa sasa uboreshaji wa mabomba unafanyika mara kwa mara ambapo mabomba ya zamani yanaendelea kubadilishwa na kuimarishwa matanki ya maji yaliyopo eneo la chuo kikuu cha Ardhi, Kimara na Kibamba.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mawaziri wa Maji waliotembelea mradi huo wa Ruvu Chini Mhe. Anna Shiweda kutoka nchini Namibia amesema kuwa wamefurahishwa na Tanzania jinsi ilivyojipanga kuwahakikishia wananchi wake wanapata maji kwa maendeleo yao na wame wamevutiwa kwa jinsi chanzo hicho cha maji kilivyo na vifaa vya kisasa.

  Akizunguzia upatikanaji wa maji katika nchi yake, Mhe. Anna amesema kuwa nchi yao ni miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo eneo kubwa linakabiliwa na ukame ambapo wakazi wa nchi hiyo maji hupatikana kwa zaidi ya kilometa 250.

  “Mkutano wetu umekuwa wa manufaa sana, tumefurahishwa na Tanzania kwa namna ilivyojidhatiti kuwapatia wananchi wake maji, tumejifunza na tunayachukua mawazo haya kwa manufaa ya nchi zetu” alisema Mhe. Anna.

  Mhe. Waziri Anna amesema kuwa Namibia ina changamoto ya kuwa na ukame ambao unalikumba taifa hilo lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3, kutoka Tanzania wamejifunza mambo muhimu kupitia mkutano huo na Namibia imejipanga kutumia teknolojia inayotumia Tanzania ili nao waweze kuwahudumia raia wake waweze kupata maji safi na salama.

  Maonesho ya wiki ya maji yanayofanyika Dar es salaam yanahudhuriwa na Mawaziri wa Maji kutoka nchi 38 zikiwemo Tanzania ambayo ni mwenyeji wa maonesho hayo, Sudan, Kongo, Lesotho,Madagaska, Burundi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegal, Togo, Liberia, DRC na Zimbabwe.

  Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Libya, Kenya, Misri, Ivory Coast, Cameroon, Msumbiji, Zambia, Sudan Kusini, Bukina Fasso, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Benin, Mauritania, Uganda na Djibouti.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Iran nchini Mhe. Mehdi Agha Jafari alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimweleza Balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na Iran hususan katika kuhakikisha Diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo inaimarika kwa manufaa ya mataifa hayo. 
  Mhe. Balozi Mehdi Agha Jafari akizungumza ambapo alieleza kuwa Serikali ya Iran itazidi kushirikiana na Tanzania katika sekta za Elimu, Biashara, Afya na Kilimo. 
  Mhe. Balozi Mehdi Agha Jafari akimkabidhi ujumbe maalum Mhe. Waziri Mahiga 
  Mazungumzo yakiendelea 

  0 0

  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia (CFR), Dkt. Bernard Achiula. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi za Chuo hicho zilizopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam. 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi(wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Mhe. Balozi Abdallah Kilima wakiwa pamoja na Mhe. Jasem Al-Najem na Dkt. Achiula ambao waliiwakilisha Wizara katika makabidhiano hayo. 

  Balozi Mwinyi akiongea na Mhe. Jasem Al-Najem ambapo katika mazungumzo yao walizungumzia namna ya kuimarisha uhusiano uliodumu kwa muada mrefu baina ya mataifa ya Tanzania na Kuwait na alimshukuru kwa kukisaidia chuo hicho ambacho kipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kumwomba kupanua wigo katika sekta ya Elimu ikiwemo kuwa na program za mafunzo na kubadilishana uzoefu baina y anchi hizi mbili. 


  0 0

  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma Paul Chacha akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Kakonko madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati katika Shule za Msingi wilayani humo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko mkoani Kigoma Lusubilo Mwakabibi (aliyesimama kati kati) akizungumza muda mfupi kabla ya benki ya CRDB haijakabidhi madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 kwa ajili ya shule za msingi wilayani humo. 

  Mkuu wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza kabla hajapokea madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule za Msingi wilayani humo. 


  0 0

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili kulia) alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.
    Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia) sehemu ya fukwe za hifadhi hiyo ambazo ni makazi ya Mamba na Ndege wa aina mbali mbali alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma. 
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (kulia) katika fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto anaesaini kitabu cha wageni ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

older | 1 | .... | 1292 | 1293 | (Page 1294) | 1295 | 1296 | .... | 3272 | newer