Na Mwandishi Wetu, Songwe.
Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amesema wanawake wa mkoa huo ni nguvu kuu, wazalishaji mali wakubwa na wenye ushawishi katika familia, hivyo amewataka kukaa na vijana wao kuwaeleza maadili mema na umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na utegemezi usiokuwa na tija.
Shonza alitoa rai hiyo, jana wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (Uwt) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songwe, alipokutana nao kujadili na kupeana mikakati ya wanawake hao kuanzisha na kujiunga kwenye vikundi vya ujasariamali kwa kila kata kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato katika familia.
Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (CCM) akilakiwa na wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (Uwt) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songwe, jana alipokutana nao mji mdogo wa Mkwajuni.Shonza alikutana na wanawake hao ili kujadili na kupenana mikakati ya kuuunda na kuimarimasha vikundi vya ujasiriamali.
Alisema wanawake na watoto ndio waathirika wa kwanza endapo amani itatoweka eneo husika, lakini pia ndio wenye ushawishi mkubwa kuhakikisha wanawaweka sawa vijana wao, kutambua umuhimu wa kuipigania amani isivurugwe.
“Mtoto wenu leo nimekuja kuwashukuru kwa kunichagua kuwa mwakilishi wenu bungeni. Na nimekuja na mkakati wa kutaka nyinyi mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali kwenye kata zenu. Lakini niseme ni lazima tukumbuke kuilinda amani iliyopo. Wanawake tuhakikishe tunakaa na vijana wetu tuwaeleze maadili mema, tusiache wakavurugwa akili na mwisho wa siku wanakuja kuvuruga amani.
Mbunge Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na wanawake wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songwe, jana alipokutana nao mji mdogo wa Mkwajuni. Shonza alikutana na wanawake hao ili kujadili na kupenana mikakati ya kuuunda na kuimarimasha vikundi vya ujasiriamali.
Kwani hata amani ikitoweka hata hii mipango tunayopanga leo ya kuanzia miradi kwenye kata zetu haitafanikiwa kwakuwa kila mmoja atakuwa mafichoni. Hivyo niwaombe tujikite kwenye ujasiriamali huku tukidumisha amani yetu,” alisema Mbunge Shonza.
Kuhusu uanzishwaji wa vikundi vya ujasiriamali, Shonza alisema tayari ametoa Sh30,000 kwa kila Kata kwa ajili ya kusajilia vikundi watakavyounda lakini pia alitoa mtaji wa Sh200,000 kwa kila kata husika za kuanishishia miradi watakayokuwa wameibuni na baada ya kukamilisha zoezi hilo sasa atarajia kuanza kupeleka elimu ya ujasriamali kwa wanawake hao ambapo atawatafutia wataalamu wa masuala ya elimu.
Mbunge Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Songwe Juliana Shonza, akiwa amepiga magoti akiwasalimia wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (Uwt), wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songwe jana alipokutana nao mji mdogo wa Mkwajuni.Shonza alikutana na wanawake hao ili kujadili na kupenana mikakati ya kuuunda na kuimarimasha vikundi vya ujasiriamali.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Opulukwa na Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo walisema kina mama ndio wenye ushawishi mkubwa katika mambo mbalimbali ya kijamii hivyo waliwaahidi kuhakikisha vikundi watakavyounda kwa kushirikiana na Shonza vinakuwa endelevu na vyenye tija.
Opulukwa alisema ‘Kina mama mimi ni mgeni kabisa hapa Songwe, na mipango yangu ni kupiga vita umasikini Songwe, hivyo nimefajirika sana kuona Mnbunge Shonza amekuja na mikakati ambayo ndio kipaumbele change na katika hili ninawaahidi kuwapa ushirikiano kwa hatua mnayofanya, mkikwama sio lazima mmpigie simu Shonza, njoo kwangu kwanza’.
Mbunge Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (CCM) akiserebuka muziki na Wajumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania (Uwt) wa Chama cha Mapinduzi 9CCM) Wilaya ya Songwe, jana alipokutana nao mji mdogo wa Mkwajuni.Shonza alikutana na wanawake hao ili kujadili na kupenana mikakati ya kuuunda na kuimarimasha vikundi vya ujasiriamali.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Songwe na Chunya, Mboka Konzo alisema Mbunge Shonza amekuja na ukombozi wa kiuchumi kwa mwanamke wa Songwe na mkoa kwa ujumla katika muda mwafaka na wao kama viongozi watahakikisha wanamtumia Shonza kwenye mipango ya kimaendeleo na si vinginevyo.
Aliwataka madiwani wa viti maalumu kwa kila kata kuhakikisha wanakuwa walezi wa karibu kwenye vikundi hivyo na kuwasaidia wanakikundi pindi wanapokwama kwa kufanya mawasiliano na viongozi wa ngazi juu kwa tatizo lolote ili mradi usiweze kukwama.