Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1293 | 1294 | (Page 1295) | 1296 | 1297 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) leo amefanya ziara katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro kwa kukagua shughuli za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko.

  Akihutubia wanawake na wananchi walio jitokeza katika maonyesho ya shughuli hizo, Mhe Ummy alieleza kuwa Serikali imejipanga katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

  Alisema, uwezeshaji huo utafanyika kupitia mifuko mbalimbali ya kuwawezesha wanawake, ikiwamo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) uliopo katika kila Halmashauri nchini na Benki ya Wanawake Tanzania.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akiendelea akiangalia moja ya mashine ya kufyatua matofali wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Morogoro.Kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia)

  Katika hadhara hiyo Mhe Ummy alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bibi Agness Martin Mkandya, kuhakikisha Halmashauri hiyo inatenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ili fedha hizo ziweze kutumika katika kukopesha wanawake wajasiliamali.

  Aidha, aliwaeleza wananchi kuwa serikali itatekeleza ahadi yake ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-20 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji kama Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) katika vijiji husika; hivyo wanawake nao wazichangamkie fedha hizo kwa kuanza kujiandaa kujiunga katika vikundi ili fursa hiyo isiwapite.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akikagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro

  Katika kukabiliana na changamoto ya masoko kwa bidhaa zinazotengenezwa na wanawake, Mhe Ummy alisema, Ilani ya uchaguzi ya ccm pia inaelekeza Halmashauri zote kutenga asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yake kwa ajili ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya vijana au wanawake. Aidha, mbunge wa Jimbo la Gairo, Mhe Ahmed Shabiby aliwaeleza wananchi kuwa wataandaa utaratibu wa kuwa na maonyesho rasmi ya kutangaza kazi za wanawake wajasiliamali wa Wilaya hiyo.

  Baadhi ya Wanawake walioshiriki katika shughuli hiyo walieleza kuwa kupitia shughuli za vikundi wameweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi hivyo, wakilenga pia kuwaelimisha vijana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha, wanawake hao waliainisha moja ya changamoto kubwa inayo wakabili kuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutosha kuendesha biashara zao.

  Kupitia hadhara hiyo Mhe Ummy aliwataka wazazi kutilia mkazo elimu kwa watoto wa kike. Alieleza kuwa Wilaya ya Gairo inakabiliwa na tatizo kubwa la mimba na ndoa za utotoni, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa linafifisha jitihada za serikali katika kumpatia mtoto wa kike Elimu.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akiendelea kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia)

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson (wa nne kulia),akiongoza mbio za Tulia Marathon KM 5 akiwa sambamba na baadhi ya Wabunge mbalimbali vikiwemo na vikundi vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae kuishi katika viwanja vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.Dkt Tulia na washiriki wa mbio hizo. Baada ya mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR-MMG DODOMA.
  Dkt Tulia akishirikia na Wabunge na vikundi mbalimbali wakifurahia kumaliza mbio hizo za kuhamasisha jamii kusaidia watoto Yatima na waishio katika Mazingira Magumu.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson (wa tatu kulia),akiwa ameongoza na Wabunge mbalimbali vikiwemo na vikundi vya kuhamasisha mbio hizo zilizoanzia geti la Bunge na baadae kuishi katika viwanja vya Vya Nyerere Skwea mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wabunge wakishiriki mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo,ambapo mbio hizo zilikomea katika viwanja vya Nyerere Skwea.

  Vikundi mbalimbali vikiunga mkono mbio za Tulia Marathon KM 5 mapema leo asubuhi.
  Baadhi ya vikundi mbalimbali vikisubiri kuanza mbio za Tulia Marathon KM 5 zikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kusaidia watoto Yatima na waishio katika Mazingira Magumu,ambapo baada ya mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa vikawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
   Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
    Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisisitiza jambo mbele ya Wajumbe wa Mutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodomam leo Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula . 
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba  wimbo wa CCM katika kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.
    Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwakaribisha viongozi wa Meza Kuu,mara walipokuwa wakiingia ukumbini wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete 
   Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.
    Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA


  0 0   Waziri wa afya akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo,mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha afya gairo(picha na wizara ya afya)

    Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi ya wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya Gairo.
   Waziri Ummy Mwalimu akiwasikiliza watumishi wa kituo hicho cha afya(hawapo pichani),kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo Mhe.Ahmed Shabiby(wa kwanza kushoto)Mkuu wa Wilaya hiyo mhe.Siriel Mchembe(wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri  Bi.Agnes Mkandya.


  Na.Catherine Sungura,Gairo
  Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao  ujenzi wa Hospitali ya wilaya.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi  inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.

  Waziri Ummy amesema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na vijiji vya jirani  kufika kituoni hapo kujifungua"suala ya uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua"

  Aidha,amesisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
  "Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya,pia muweke  dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu mlitekeleze"

  Kwa upande wa watumishi,Waziri Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.
  "Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri  uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi,  likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa"

  Awali akisoma taarifa ya Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa hospitali ya wilaya,  gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.
  Sent from my Huawei Mobile

  0 0

   Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”.  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam. 
   Mkurugenzi wa Masoko TBL, Kushila Thomas (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicolas John (katikati) pamoja na mgeni mwaliko aliyefika katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam. 

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge).

  Makubaliano hayo ya awali yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying.

  Akizungumza katika hafla hiyo ya utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.

  Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.

  Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Msanii wa Vichekesho ISMAIL MAKOMBE maarufu kama KUNDAMBANDA ambae pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Masasi kupitia Chama cha wananchi CUF amefariki Dunia mapema hii Leo. 
  Mungu ametoa na Mungu ametwaa. 
  Tutakukumbuka Milele Daima.
  TAZAMA HAPO CHINI MOJA YA KAZI ALIZO ZIFANYA.

  0 0

  East African Legislative Assembly.
   A bird’s eye view of the Assembly at the Special Sitting yesterday
   Hon Dora Byamukama pays tribute to the late Hon Hafsa Mossi
   A section of Members at the tree-planting ceremony in honour of the late Hon Hafsa Mossi.

  …Condemns killing, asks for speedy investigations
  East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: July 22, 2016: It was an emotional send-off for the late Hon Hafsa Mossi at a one-day Special Sitting held in Arusha yesterday with EALA legislators condemning in the strongest terms possible, the despicable, brutal and dastardly murder.   With that, the Assembly underscored the need for instituting independent investigations by credible organization(s) to unearth the killers of the late Hon Mossi, while remaining resolute that peace, security and stability should be immediately restored in Burundi.

  The Resolution which condemned the killing of the fallen legislator while paying special tribute to her, was moved by the Chair of the Committee on Legal Rules Privileges, Hon Peter Mathuki, seconded by Hon Dora Byamukama and supported by the entire House.

  In the foregoing, the Assembly urged the Summit of EAC Heads of State to ensure the on-going mediation deliberations are taken seriously by all parties.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Madaba mkoani Ruvuma, Joseph Mhagama (wa tatu kulia) akipokea moja ya madawati 540 kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari katika jimbo hilo.
  Mkuu wa kikosi cha 842 KJ Mlale kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Meja Absolomon Shaushi (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Madaba wilayani Songea, Joseph Mhagama (kulia) mara baada ya kukabidhi madawati 540 ili kukabilianana upungufu wa madawati katika jimbo hilo.
  Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi akimuonesha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea, Mennas Komba (kulia), baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikosi hicho ambayo yatasambazwa kwa baadhi ya shule za msingi na sekonadri zenye upungufu wa madawati. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Bulenganija.
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama, Mennas Komba (kulia) akipokea moja ya madawati 534 kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi, ambayo yametengenezwa na kikosi hicho ili kukabiliana na upungufu wa madawati katika jimbo la Peramiho,katikati mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilayaya Songea vijijini Simon Bulenganija. Picha na Muhidin Amri

  0 0

  In memory of the late Abel Yanga
  Sunshine June 28, 1968 Sunset July 22, 2015
  One year has passed since that sad morning of July 22, 2015
  when our loved one was called by his Creator. 

  God took him,  it was his will as he always picks the best of flowers from his Garden. Abel, you slipped like water between fingers, but again that was God's will. Though we do not see you in flesh anymore, in our hearts you will live forever.

  You are deeply missed by your parents Mzee Charles Yanga and Mama Lucy Yanga,  your young  brothers and sisters, in laws,  relatives and friends. We will cherish the memories you left till we meet again. Amen.

  0 0

   Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya unyang’anyi kwa kutumia nguvu.

  Watuhumiwa hao  ni wapiga debe katika sehemu mbalimbali za vituo vya daladala, watengenezaji pombe haramu ya Gongo waliokamatwa na lita 952 ikiwemo na mitambo mitatu ya kutengezea pombe hiyo, Kikosi cha mbwa mwitu 10, wauzaji na wavutaji bhangi puli 277, Kete 210, misokoto 144, pamoja na  wacheza kamari.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro amesema kuwa watuhumiwa 1,065 walikamatwa katika operesheni inayofanywa na jeshi hilo.

  Amesema katika operesheni Julai  21 wameweza kufanikiwa kupata silaha aina ya gobore yenye namba za usajili HD 201-2014 kutoka kwa watuhumiwa wanaotumia silaha katika matukio ya uhalifu iliyotelekezwa na watu wasiofahamika baada ya raia wema kuhisi kuna mtu anamiliki silaha na msako ukaendelea.

   Aidha amesema mnamo Juni 16 hadi 19  Polisi wamemkamata lita 952 za Gongo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kati ya lita hizo 420 zilikamatwa katika maeneo ya Kinzudi Wazo Hill kutoka kwa watu sita, mitambo mitatu ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo pamoja na kukamata sukari kilo 100.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya  operesheni walioifanya na kufanikiwa kukamata watuhumiwa sugu 1,065 wa makossa mbalimbali  jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha  waandishi wa habari  vitu mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha simu zilizoibwa na majambazi mbalimbali jijini Dar es Salaam waandishi wa habari.
  (Picha na Emmanuel Massa,Globu ya jamii).

  0 0

  Na Jonas Kamaleki, MAELEZO.
  SERIKALI iko mbioni kutoa hatimiliki zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa urasimishaji wa makazi holela Kata za Kimara na Saranga, Bi Grace Masatu wakati wa zoezi la ukaguzi wa maeneo ya mradi.

  “Zoezi za la upimaji linaenda sanjari na utambuzi wa mipaka,ujazaji wa madodoso, uchoraji wa ramani za upimaji na mipangomiji,”alisema Masatu.

  Viwanja zaidi ya 25,000 vinatarajiwa kupimwa katika kata za Kimara na Saranga ambapo hadi leo ramani za upimaji 14 na ramani sita (6) za mipangomiji zenye jumla ya viwanja1028 ziko tayari na zimeshawasilishwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajli ya kupitishwa, alisema Masatu. 

  Aidha, Masatu amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kuongeza thamani ya makazi kwa kutoa hatimiliki na kutambua mipaka ya wakazi wa maeneo husika.

  Kwa upande wake, Afisa Mipango miji Mkuu, Bi Anna Macha, alisema kuwa hadi sasa maeneo yaliyopimwa katika kata ya Kimara ni mtaa wa Kilungule A wote pamoja na viwanja 724 vya mtaa wa Kilungule B, ambavyo vimechukuliwa mahesabu ya upimaji kwa ajili kuandaa ramani.

  Ameongeza kuwa umetengenezwa mfumo maalum ambao unachukua taarifa za madodoso zinazojazwa wakati wa utambuzi wa mipaka ya wamiliki wa maeneo husika. Mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa Kamishna wa Ardhi (MOLIS) utakaorahisisha kufahamu idadi ya viwanja vilivyopimwa na kumilikishwa.

  Naye Mjumbe wa Mtaa wa Kilungule B,  Bwana Claud Misri Silayo ameonyesha kuridhishwa na zoezi zima la utambuzi na upimaji wa maeneo.

  “ Nimefurahishwa na zoezi la upimaji kwani nitamiliki ardhi kisheria, kihalali na nitafaidika na ardhi ninayomiliki kwa sababu mwisho wa zoezi hili nitapata hatimiliki ambayo itaniwezesha kupata mikopo kwenye taasisi za fedha,”alisema Silayo.

  Urasimishaji ni mwendelezo wa utambuzi wa makazi holela katika jiji la Dar es Salaam unaotekelezwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 pamoja na Sheria ya Mipangomiji.


  0 0

  Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
  Ligi kuu ya Uingereza almaarufu EPL inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa sana hasa kutokana na usajili unaoendelea kufanywa na vilabu mbali mbali ili viweze kufanya vizuri na hatimaye kupata ubingwa wa ligi hiyo.

  Sajili nyingi zinazoendelea zimewashitua wengi hasa sajili inayosemekena kufanyika usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Julai 22, 2016 ni ya Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United ambao utaweka rekodi ya dunia ya ada ya uhamisho, kiasi cha Pounds Milioni 120 kimetajwa kulipwa ili kufanikisha uhamisho huo.

  Tukiacha mambo ya usajili tuangazie suala zima la makocha ambao wanatarajiwa kuviongoza vikosi vyao katika ligi hiyo ya nchini Uingereza, duru za kispoti zinasema kuwa ligi hiyo itakuwa na utamu wake ambao utachagizwa kwa kuwepo na makocha mbali mbali wenye sifa tofauti hasa wawapo kwenye mstari unaowatenganisha wao na uwanja.

  Baadhi ya makochaa hao ni Jurgen Klopp wa Liverpool (Majogoo wa jiji), Jose Mourinho wa Manchester United (Mashetani wekundu), Pep Guardiola wa Manchester City (Matajiri wa mafuta), Antonio Conte wa Chelsea (The Blues) na Arsene Wenger wa Asernal (Washika mitutu). Makocha hawa wana sifa tofauti ndani na nje ya uwanja, lakini leo tutatazama sifa zao za ndani ya uwaja.
  JURGEN KLOPP:

  Anasifika zaidi kwa kuwahamasisha Wachezaji sambamba na Watazamaji, mara nyingi utakuta akiwakumbusha wachezaji wake wawapo uwanjani kujituma zaidi kukaba kuanzia (juu) yaani kwenye eneo la adui, na papo hapo yeye utamuona kana kwamba naye ni sehemu ya wachezaji kwa jinsi anavyokuwa na mdadi, jinsi anavyoshangilia pindi wanapopata goli na wakati fulani badala ya kutazama mpira huwa anawatazama watazamaji kuona namna gani wanawapa sapoti wachezaji wao.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Na. Mwandishi wetu, Bahi

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewahimiza wananchi wa wilaya ya Bahi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

  Waziri Ummy alisema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani BAHI kwa kutembelea kituo cha Afya cha Mundemu.

  Akijibu maswali ya wananchi kuhusu kutopewa dawa licha ya wao kuwa na kadi za CHF, Waziri Ummy amewahakikishia wananchi wote kuwa, wizara yake kupitia Bohari ya Dawa (MSD) itahakikisha dawa za kutosha zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma ili wananchi na wanachama wa CHF waweze kupata dawa wakati wote."kupitia CHF iliyoboreshwa mtaweza kupata huduma hizo hadi ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa"alisema

  Katika ziara hiyo,Waziri Ummy pia alitembelea mradi wa usafi wa mazingira mashuleni, katika jamii na maeneo ya kutolea huduma kwa jamii unaofadhiliwa na PLAN INTERNATIONAL .

  Waziri wa afya akiongea na wagonjwa waliofika kituoni hapo kupata huduma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kituo hicho cha afya

  0 0

   Kocha Jose Mourinho hakuamini macho yake alipoishuhudia timu yake ya Manchester United ikipokea kichapo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 toka kwa vijana wa Borussia Dotmund kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita huko nchini China.

  Alikuwa ni mchezaji Castro katika dakika ya 19 aliyeanza kuwakosesha raha mashabiki wa Manchester baada ya kuandika bao la kwanza kufuatia piga nikupige langoni mwa Manchester. 

  Dakika 36 mlinzi Antonio Valencia aliunawa mpira ndani ya kumi na nane na mwamuzi akaamuru Upingwe mkwaju wa penati na mshambulizi hatari wa Dotmund Mkhitaryan Aubemayang akapiga kiufundi penati hiyo na kuandika bao la pili.

  Kipindi cha pili dakika ya 57 Dembele akawafungasha tela mabeki wa Manchester na kufunga goli zuri sana na kufanya matokeo kuwa goli 3-0. Manchester walijitahidi kufurukuta na kujipatia goli la kufutia machozi lililofungwa na Malta.
  Dakika za mwishoni wa mchezo Castro aliyekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Man U alidhihirisha ubora wake pale alipofunga bao la nne na kumfanya kocha Jose Mourinho aduae nafikiri akidhani yumo ndotoni.Wachezaji wa Man U wanaonyesha bado wanahitaji muda mrefu wa kucheza kitimu kwani hawakuwa na muunganiko mzuri wa kitimu.

  0 0

  Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

  Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

  Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

  A/C No. 2011100205 – NMB

  A/C No. 01J1028467503 – CRDB

  A/C No. CCA0240000032 – TPB

  Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

  Imetolewa na:

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

  0 0


older | 1 | .... | 1293 | 1294 | (Page 1295) | 1296 | 1297 | .... | 3278 | newer