Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1285 | 1286 | (Page 1287) | 1288 | 1289 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Dar es Salaam wa Vodacom Tanzania,Domician Mkama(kulia)akimpongeza mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam,Evans Mwenewanda(wapili kushoto)wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita cha Shilingi Milioni 5/= alichojishindia kupitia promosheni ya”Kamata Mpunga” inayoendeshwa na kampuni hiyo,Kushoto ni Ofisa wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Prestin Lyatonga na mshindi mwingine wa shilingi Milioni 5/=mkazi wa Goba jijini,Serena Sanga(watatu kushoto)Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
  Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/=kupitia promosheni ya”Kamata Mpunga” inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam,Serena Sanga ambaye ni mfanyakazi wa ndani(watatu kushoto) akipokea kitita chake mwishoni mwa wiki toka kwa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Dar es Salaam wa kampuni hiyo,Domician Mkama(kulia)wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi mbalimbali wa vitita hivyo.Kutoka kushoto ni Ofisa wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Prestin Lyatonga na mshindi mwingine wa shilingi Milioni 5/=mkazi wa Mwananyamala jijini, Evans Mwenewanda. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
  Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/=kupitia promosheni ya”Kamata Mpunga” inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam,Serena Sanga ambaye ni mfanyakazi wa ndani,akionesha kitita chake kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa washindi mbalimbali vitita vyao mwisho mwa wiki. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
  Sekela Kanganda(wapili kushoto)pamoja na Winfrida Bernard(watatu kushoto)ambao ni washindi wa shilingi milioni moja moja kupitia promosheni ya”Kamata Mpunga” inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Wakifurahia baada ya kukabidhiwa pesa zao na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Dar es Salaam wa kampuni hiyo,Domician Mkama(kulia)katika hafla fupi ya makabidhiano ya pesa zao walizojishindia kupitia promosheni hiyo mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Ofisa wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Prestin Lyatonga. Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), David Mgwassa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari.


  Na Dotto Mwaibale

  SHIRIKA la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kaunzia Julai 30 mwaka huu kuwa ni mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa abiria badala yake zitatumika kadi.

  Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi.

  " Tiketi zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwassa.

  Alisema Udart imepunguza bei ya kadi hizo kutoka sh.4500 ya awali hadi kufikia sh.2000 ili kutoa fursa kwa kila mwananchi wa kuweza kuipata kadi hizo na kuzitumia.

  Mgwassa alisema kadi ziliuzwa ni 55,000 na zilizobaki ni 150,000.

  Mkuu wa idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari alisema wateja wataweza kulipia kadi hizo kupitia kwa mawakala wao waliopo katika vituo vyote vya udart na kwa njia ya mitandao yote ya simu. 


  Mabasi ya Shirika la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART) yakiwa makao makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
  Meneja wa Uhusiano wa Udart, Deus Bugaywa (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kutokana na kifo cha Elizabeth Mayemba - Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.

  Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo nchini kilichotokea Julai 09, 2016 na habari zake kuanza kusambaa majira ya jioni jana kabla ya kuthibitishwa na wanafamilia na uongozi wa TASWA kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.

  Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Elizabeth Mayemba.

  Elizabeth Mayemba, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika gazeti la Majira na wakati fulani magazeti ya Kampuni ya New Habari House 2006.

  Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Elizabeth Mayemba mahala pema peponi.

  Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.  0 0

  Mama Maria Tereza akisisitiza jambo wakati akitoa shukrani zake kwa wanawake wa Tanzania wanaofanya miradi mbalimbali ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

  MAKAMU wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Tereza Fernandes de la Vega Sanz (67), amesema kwamba amefurahishwa mno na mafanikio ya wanawake 15 wa Tanzania katika kipindi kifupi baada ya mafunzo waliyoyapata jijini Madrid mapema mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa chakula cha usiku alichowaandalia akinamama hao wanaotekeleza mradi wa Green Voices katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam usiku huu mara baada ya kutua kutoka Hispania, Mhe. Maria Tereza amesema amefarijika kuona wazo lake lililoibuka mwishoni mwa mwaka 2015 la kuwawezesha wanawake kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi limeweza kuzaa matunda.


  Mama Maria Tereza ndiye anayefadhili miradi hiyo kupitia taasisi yake ya Women for Africa Foundation.
   Mama Maria Tereza Fernandes de la Vega Sanz (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi Getrude Mongella katika hafla hiyo.

  “Ni mwaka jana tu mwishoni nilipowaza namna ya kuwawezesha wanawake, hasa wa Tanzania, katika vita ya dunia ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, lakini nafarijika kusikia kwamba wanawake wachache ambao tuliwapatia mafunzo nchini Hispania leo hii wameweza kufanikiwa kuliko hata tulivyotarajia, ni muda mfupi na mafanikio ni makubwa,” alisema.


  Mama Maria Tereza alikuwa makamu wa rais wa Hispania kati ya Aprili 18, 2004 hadi Oktoba 20, 2010, na ndiye alikuwa msemaji wa serikali ya Waziri Mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero. Yeye ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika historia ya Hispania.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Akcson amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ulioongozwa na Spika Mhe Zuberi Ali Maulid na kuahidi kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina na Vyombo hivyo viwili vya kutunga sheria.

  Akizungumza na ugeni huo uliomtembelea kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi Naibu Spika amesema ili mahusiano ya Vyombo hivi viwili yaboreke zaidi kuna haja ya kuwa na mafunzo ya pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ambazo nyingi zinafanana.

  Naibu Spika aliongeza pia kuwa Bunge la Jamhuri ya Muuumgano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni Vyombo vinavyofanya kazi zinazofanana hivyo kujifunza na kubadilishana uzoefu ni jambo la muhimu katika katika kuboresha utendaji kazi.

  “Mahusiano tuliyonayo yanawekewa nguvu tunapokuwa na mafunzo yale ya pamoja kwa sababu fursa inapatikana ya kubadilishana uzoefu lakini pia kujifunza mambo kwa pamoja kuliko kukiwa na uendeshaji ambao ni tofauti sana wakati Vyombo hivi vinafanya kazi inayofanana,” alisema Naibu Spika wakati akizungumza na Ugeni huo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

  Dkt Tulia pia ametumia fursa hiyo kumpongeza Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuchaguliwa kushika nyadhifa hizo na kusema kuwa Bunge lipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote utakapohitajika.

  Kwa upande wake Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid amesema Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kitu kimoja hivyo wameona ni muhimu kuja kusalimiana, kufahamiana na kuimarisha mahusiano yaliyopo ili kurahisisha utendaji kazi wa Vyombo hivyo.

  Adiha alisema kuwa Baraza la Wawakilishi litaendelea kujifunza na kuomba ushauri toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ili hilo lifanikiwe kuna haja ya kuboresha zaidi mahusiano ya mihimili hiyo miwili ya kutunga sheria.

  Pia Mhe. Maulid amempongeza Naibu Spika Dkt Tulia kwa umahiri wake wa kupambana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uendeshaji vikao vya Bunge na kusema kuwa kuna mambo mengi wamejifunza kutoka kwake.

  Pamoja na Watendaji wengine wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Spika wa Baraza hilo aliamabatana pia na Naibu Spika wa Baraza Mhe Mgeni Hassan Juma na Katibu wa Baraza Ndg. Raya Issa Msellem.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akizungumza na Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid( katikati) pamoja na Naibu Spika wa Baraza la Wakilishi Mhe Mgeni Hassan Juma (kulia) walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ugeni kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akimsikiliza Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid wakati alipofanya mazungumzo naye Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson (katikati ya waliokaa) katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar wakiongozwa Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid (wa pili toka kulia).( Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Azam Fc, Saad Kawemba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KLABU ya Azam FC, ambao tayari wameanza mazoezi yao ya  kujiandaa na msimu ujao (2016-17) ikiwa chini ya benchi jipya la ufundi chini ya makocha kutoka nchini Hispania, linaoongozwa na Zeben Hernandez, Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia na Msaidizi wake, Pablo Borges na Kocha wa Makipa Jose Garcia huku Daktari wa timu, Sergio Perez, akitarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa.

  Mtendaji mkuu wa Azam Fc Saad Kawemba amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mikakati ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwa kusajili wanne wa kimataifa baada ya Didier Kvaumbagu, Allan Wanga kuondoka. Zaidi pia tunahitaji golikipa wa kimataifa ambaye atasaidiana na Aishi Manula na hasa pia atakuwa msaada kwetu kwenye michuano ya kimataifa na pia hata kweny ligi msimu ujao ambao tunahitaji ubingwa na hilo linawezekana kwani nia ninayo.

  "Tunahitaji kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na hata katika ligi pia ndiyo maana tunataka kufanya usajili utakaokuwa na manufaa kwetu na tumeonelea kwanza tunahitaji golikipa wa kimataifa, beki wa kati na washambuliaji wawili wa kimataifa ambao watachukua nafasi za Kvumbagu na Allan Wanga,"amesema Kawemba. 

  Amesema kwa sasa tiulichoamua kingine ni kupandisha vijana wetu wanne kutoka timu ya vijana pia tumefanya mchanganuo wa vikosi kwa sasa Azam watakuwa na vikosi viwili ambapo kila kimoja kitakuwa na wachezaji 22.

  Makocha hao wataongezewa nguvu na makocha wengine wazawa waliokuwepo na kikosi hicho msimu uliopita, Kocha Msaidizi Dennis Kitambi na Idd Abubakar, aliyekuwa akiwapata maujuzi makipa wa Azam FC.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali (Mstaafu), Salum Kijuu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaotekelzwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara kwa ushirikiano wa baina ya  Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) na Serikali ya Tanzania. Mradi huo utazihusisha Halmashauri 93 katika mikoa hiyo.
  Mtaalam wa fedha wa mreadi wa PS3 ambaye ndie msimamizi wa uzinduzi huo Mkoani Kagera, Abdul Kitula akielezea maeneo mbalimbali ambayo mradi huo utahusika na kufanya kazi. 


  Kitula alisema PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.

  Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Kagera wakifuatilia uzinduzi huo.
  Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.


  0 0  Pichani wa kwanza kushoto ni Afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni msimamizi wa mahabusu ya watoto mkoa wa Arusha Mussa Mkamate akiwa anabadilishana jambo na baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha mara baada yakukabidhi magodoro kama msaada katika mahabusu hiyo.

  Na Woinde Shizza wa globu ya jamii Arusha

  Kamati ya utekeleza ya wazazi wa CCM wilaya ya Arusha leo wamekabidhi jumla ya magodoro 25 katika mahabusu ya watoto iliyopo jijini hapa ikiwa ni ahadi walioiweka ya kusaidia baadhi ya changamoto zilizopo katika mahabusu hiyo.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni meneja masoko wa Radio ya Triple A iliopo jijjini Arusha Phidecia Mwakitalima alisema kuwa hii ni mara ya tatu wao kama kamati ya wazazi wa wilaya kukabidhi msaada huo kwani mara ya kwanza walishatoa chakula na mashuka kwa ajili ya watoto hao na sasa hivi wameamua kuwaletea msaada wa magodoro.

  Alisema kuwa magodoro hayo 25 yametokana na msaada ambao wao kama kamati ya wazazi waliuomba kwa wadau mbalimbali ambapo katika wadau hao kampuni ya magodoro ya Tanform iliopo arusha iliwaunga mkono na kuamua kuwapa magodoro hayo kwa ajili ya watoto hao wa mahabusu ya watoto Arusha.

  Aidha Phidecia alimalizia kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali ,wafanyabishara ,viongozi pamoja na wananchi kujijengea tabia ya kutembelea mhabusu mbalimbali za watoto zilizopo hapa nchini ili kuweza kugundua changamoto walizo nazo watoto hao na kuweza kuwasadia kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwapa baadhi ya mahitaji ambayo watoto hao walioko mahabusu hawayapati pamoja na kutatua kero walizo nazo.

  Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Arusha Ally Mtumwa alisema kuwa juhudu za jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha hazitaishia hapo kwani huu ni mwanzo wataendelewa kuwasadia watoto wa mahabusu hii pamoja na watoto wengine wanao ishi katika mazingira magumu na wale yatima waliopo ndani ya mkoa wa Arusha.

  Alisema wao kama wazazi wanaguswa sana na baadhi ya matatizo yanayowapata watoto hao wanaoishi katika mahabusu hii ya watoto pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu hivyo watajitaidi kwa kila njia kuwasadia .

  “hii sio mara ya kwanza kuwasadia watoto hawa na wala sio watoto hawa tu tunawasaidia na pia atutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia watoto hawa sisi kama wazazi adi pale tutakapoona sasa watoto hao wanaishi katika hali nzuri kama wale watoto wana wazazi wanaoishi majumbani kwao.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akifungua mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini Dar es salaam kwa lengo la kuanzisha Chama chao kwa ajili ya kusimamia masula mbalimbali ya Uendelezaji wa Miliki , Moja ya mambo yaliyojadiliwa katika mkuta no huo ni Katiba Pendekezwa ya Chama hicho ambapo wajumbe wamepata muda wa kuchangia mawazo yao na kurekebisha baadhi ya vifungu ili kuipitisha mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
   Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula ili  akifungua mkutano huo.
   Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia kwa karibu masuala kadhaa ambayo yamezungumziwa katika mkutano huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeitisha mkutano Jumamosi Julai 16,2016 kwa wanachama wake waliokamilisha nyumba zao, waliochangia ujenzi na waliogaiwa mashamba ili kujadili umuliki na maendeleo ya maeneo ya makazi na kilimo.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa mkutano huo utakaofanyika ukumbi la Chuo cha Splendid, Ilala \Bungoni utaanza saa tatu asubuhi ili kujipanga kuhamia kijijini kwao Mwanzega Mkuranga ambapo mpaka sasa kuna nyumba 185 ambazo tayari zimejengwa na wanachama hao kwa njia ya kuchangishana.

  Alisema wanachama ambao watahamia katijka nyumba zao watapewa ekari moja bure kwa ajili ya kulima na ufugaji kwa ajili ya kuwaendeleza wajasiriamali wa SHIWATA.

  Taalib alisema SHIWATA inakusudia kuwapokea wadau na wajasiriamali mbalimbali wa sanaa na michezo ambao watapatiwa fursa ya kujiunga na mtandao huo kwa gharama ya sh. 100,000 kuanzia Julai 18, 2016 hadi Septemba 30,2016 itawafaidisha wajasiriamali na wadau hao kupata eneo la makazi lenye ukumbwa wa mita 35 kwa 35 pamoja na ekari moja bure kwa wale ambao wamejenga na kuhamia.

  Alisema kwa upande wa shamba, SHIWATA inampango maalum wa kuendesha kilimo cha pamoja kutumia wataalamu wa kilimo wawilaya ya Mkuranga ili kufanikisha mradi wa kilimo kwa njia ya kuchangiana.

  Pia SHIWATA inakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga shule, hospitali pamoja na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ambapo baada ya kujiunga na mtandao huo watapewa maeneo bure.

  Mwenyekiti Taalib alisema Ujenzi wa awamu ya sita unatarajiwa kuanza Julai 30 mwaka huu na nyumba zitagaiwa kwa wanachama watakaokuwa wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao.

  0 0

  Bernie Sanders endorsed Hillary Clinton on Tuesday, saying “I intend to do everything I can to make certain she will be the next president of the United States.”

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya bango la picha zilizopigwa na baadhi ya Waandishi wa Habari waliowahi kujengewa uwezo na Tanzania Media Foundation toka kwa Mkufunzi wa Picha, Bw. Mwanzo Millinga 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea bahasha yenye mafanikio ya Tanzania Media Foundation ambayo yamefanywa nchini katika kuwajengea uwezo Waandishi wa habari toka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura 12 Julai, 2016 jjijjini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya unzinduzi wa Miradi Nane inayofadhiliwa na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla maalum ya ilyofanyika kumpongeza yeye Rais iliyofanywa na Wazee hao katiika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu, Zanzibar.
  Wazee wa Wilaya ya Kusini Unguja nao walihudhuria katika hafla ya kumponheza na kumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwawezesha kupata mafao ya kufikia umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.
  Msoma utenzi Bw.Mohamed Abdalla Zungu kutoka Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akighani Utenzi wake wakati wa hafla ya Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein zilizotolewa leo na Wazee wanaopokea pencheni kwa kutimiza umri wa miaka 70 katika Viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mzee Bi Mtumwa Ali Khamis ambae alishiriki katika mchezo wa kuigiza wakati wa Shukrani na Pongezi maalum kwa Rais wa Zanzibar zilizotolewa na Wazee waliotimiza umri wa miaka 70 katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya makaazi ya Wazee Sebleni Mjini Unguja.


  0 0

  Na Benedict Liwenga, WHUSM.

  Serikali kwa kushirikiana na Uongozi wa Tanzania Media Foundation itaendelea kushirikiana bega kwa bega katika kuwawezesha Waandishi wa Habari nchini kupenda kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kuhusu changamoto za maeneo hayo.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akizindua Miradi Nane ambayo inafadhiliwa na Taasisi hiyo ambayo unahusisha Waaandishi wa Habari kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kwa lengo la kuelimisha Umma.

  Mhe. Nnauye amesema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi hiyo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari na kuwawezesha kifedha kwa ajili ya kwenda kutafuta habari mbalimbali katika maeneo ya vijijini.

  ‘’Ni muhimu kwa waandishi wa habari kufika maeneo ya vijijini na kuapata habari mbalimbali kwa jili ya kuhabarisha umma, hivyo Serikali bado iko na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na endeleeni na kazi hiyo nzuri’’, alisema Mhe. Nnauye.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea bahasha yenye mafanikio ya Tanzania Media Foundation ambayo yamefanywa nchini katika kuwajengea uwezo Waandishi wa habari toka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura 12 Julai, 2016 jjijjini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya bango la picha zilizopigwa na baadhi ya Waandishi wa Habari waliowahi kujengewa uwezo na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeitisha mkutano Jumamosi Julai 16,2016 kwa wanachama wake waliokamilisha nyumba zao, waliochangia ujenzi na waliogaiwa mashamba ili kujadili umuliki na maendeleo ya maeneo ya makazi na kilimo.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa mkutano huo utakaofanyika ukumbi la Chuo cha Splendid, Ilala \Bungoni utaanza saa tatu asubuhi ili kujipanga kuhamia kijijini kwao Mwanzega Mkuranga ambapo mpaka sasa kuna nyumba 185 ambazo tayari zimejengwa na wanachama hao kwa njia ya kuchangishana.

  Alisema wanachama ambao watahamia katijka nyumba zao watapewa ekari moja bure kwa ajili ya kulima na ufugaji kwa ajili ya kuwaendeleza wajasiriamali wa SHIWATA.

  Taalib alisema SHIWATA inakusudia kuwapokea wadau na wajasiriamali mbalimbali wa sanaa na michezo ambao watapatiwa fursa ya kujiunga na mtandao huo kwa gharama ya sh. 100,000 kuanzia Julai 18, 2016 hadi Septemba 30,2016 itawafaidisha wajasiriamali na wadau hao kupata eneo la makazi lenye ukumbwa wa mita 35 kwa 35 pamoja na ekari moja bure kwa wale ambao wamejenga na kuhamia.

  Alisema kwa upande wa shamba, SHIWATA inampango maalum wa kuendesha kilimo cha pamoja kutumia wataalamu wa kilimo wawilaya ya Mkuranga ili kufanikisha mradi wa kilimo kwa njia ya kuchangiana.

  Pia SHIWATA inakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga shule, hospitali pamoja na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ambapo baada ya kujiunga na mtandao huo watapewa maeneo bure.

  Mwenyekiti Taalib alisema Ujenzi wa awamu ya sita unatarajiwa kuanza Julai 30 mwaka huu na nyumba zitagaiwa kwa wanachama watakaokuwa wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao.

  0 0


older | 1 | .... | 1285 | 1286 | (Page 1287) | 1288 | 1289 | .... | 3270 | newer