Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu wa India awasili nchini Usiku huu

$
0
0
Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akipunga mkono  kusalimia wananchi waliojitokeza kumlaki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Modi atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 09-10 Julai, 2016
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili nchini. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.
Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana (wa kwanza kulia) akiwaongoza Waheshimiwa Mawaziri Wakuu wakati wa mapokezi 
Mhe. Modi akipunga mkono kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

ELIMU YA JUU YA NCHI KUCHUKUA SURA MPYA -Naibu Waziri Jaffo.

$
0
0
 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za elimu ni nyingi katika vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.

Jaffo ameyasema hayo wakati wa maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) katika banda la Global Education Link (GEL), amewataka Watanzania kutumia maonyesho ya Sabasaba kuwa ni kipindi muafaka kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo suala la elimu katika vyuo vya nje.

Jaffo amesema kuwa, maonesho ya sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa bure.Aidha amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya nje ya nchi kwa gharama nafuu watumie fursa hiyo kupita katika banda la Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.

‘’Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imejipanga hivyo kama wasaidizi wake lazima tujipange kuhakikisha kwamba tuangalie jinsi ya kubadilika kwa kasi na kubadilika huko kwa kwa kasi lazima tuhakikishe tuna teknolojia yakutosha kabisa kwanza kiushindani, tuanzishe vitu ambavyo vitakuwa na soko kubwa”amesema .
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik S.Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni yao hata baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya fedha anayetoa kwa kusomesha mtoto nje ya nchi.

Mollel amesema kuwa vyuo vya nje wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL ya kufatilia mienendo ya wanafunzi wao kwa kipindi chote wanachosoma na taarifa zao zinatumwa na kisha mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.

Amesema kuwa watoto wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na vinatambuliwa na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na uhakika wa elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.

Global Education Link (GEL) inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi anaweza kumudu gharama hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik S.Mollel  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo alipokuwa akiagana nae mara baada ya kulitembelea banda hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TASWA yaomboleza kifo cha Elizaberth Mayemba

$
0
0
Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba kilichotokea jana  jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai.

TASWA imestushwa na kuhuzunishwa  sana kutokana  na kifo hiki cha  Elizaberth ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa unahitajika sana.

Waandishi wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na ucheshi,kujituma na  uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa mfano kwa waandishi chipukizi.

TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa habari na kuwatakia moyo wa  subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA

WATENDAJI MKOA WA PWANI WATAKIWA KUONESHA USHIRIKIANO WA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0

Na Anitha Jonas – MAELEZO

Watendaji wa Mkoa wa Pwani watakiwa kuwa wawazi kwa waandishi wa habari pale wanapotaka kupata taarifa kutoka kwao.

Hayo yamesemwa leo Mjini Kibaha, Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo kufuatilia utekelezwaji wa maendeleo ya kisekta kwa wizara yake. 

“Kwa kuwapa ushirikiano wakutosha waandishi wa habari kutasaidia kuepuka kuandikwa kwa habari zisizona taarifa kamili ambazo huleta mkanganyiko kwa jamii na kuharibu taswira ya ofisi, hivyo ni vyema mshirikiane nao”,alisema Naibu Waziri Wambura.

Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri aliangiza kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Kitengo cha Habari kipewe kipaumbele na kitengewe bajeti itakayokidhi mahitaji pamoja na kununuliwa vitendea kazi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kutangaza shughuli za maendeleo ya Mkoa.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw.Shangwe Twamala alisema mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Maafisa Michezo kwa baadhi ya Wilaya pamoja na Maafisa Utamaduni ila suala hilo kwasasa limeshawasilishwa kwa ngazi husika na wanalifanyia kazi.

Pamoja na hayo Kaimu wa Mkoa huyo aliendelea kusema Mkoa huo unakabiliwa pia na changamoto ya usikivi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa baadhi ya maeneo kama Rufiji,Mafia na mengineyo.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Bw.Bernard Haule alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kukatwa kwa matangazo katika chaneli zote pale malipo yanapoisha katika ving’amuzi vya Azam na Zuku kwa kusema leseni zao ni tofauti na zile za Startimes na Continental ambazo mbali na malipo ya kifurushi yanapokwisha wao bado huonyesha chaneli tano za taifa bure ambazo ni ITV,Star Tv,Channel Ten, EATV na TBC 1.

Pamoja na hayo Mhe.Wambura aliagiza kuwa watendaji wahakikisheni wanatenga maeneo ya viwanja vya michezo yasiyo na mgogoro kwani michezo ni ajira na inasaidia vijana kujikwamua kiuchumi,hivyo ni vyema ipewe kipaumbele.

Halikadhalika Naibu Waziri Wambura alitoa wito kwa wasanii Muziki wa Mkoa wa Pwani kuiga mfano wa marehemu Baraka Mwishehe kwa kutunga nyimbo zenye maadili na zenye kubeba ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha jamii.

Hata hivyo Naibu waziri aliendelea kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kuenzi lugha ya Kiswahili kama yanavyofanya mataifa mengine duniani kuenzi lugha zao mfano China.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa Pwani (hawapo pichani) alipofanya ziara yake ya kikazi leo mkoani kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta kwa upande wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa Pwani Bw.Shangwe Twamala akitoa taarifa maendeleo ya kisekta kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo leo Mjini Kibaha.
Afisa Tawala Wilaya ya Kibaha Bi. Sozy Mgate akieleza changamoto za sekta ya michezo kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kibaha kujionea maendeleo ya kisekta katika Mkoa huo.

SHEREHE ZA MWENGE WA UHURU ZAFANA WILAYANI NKASI

$
0
0
Hatimaye mwenge wa Uhuru umewasili Wilayani Nkasi huku sherehe hizo zikishereheshwa na mihemko ya wakazi wa maeneo mbalimbali wilayani humo wakiwa na shauku ya kujua ni miradi ipi itazinduliwa ndani ya jamii zao ambayo huenda miradi hiyo ikawa muarobaini wa matatizo chungu mzima yanayo wakabili.

Shauku ya wakazi wa Wilaya hiyo inaondolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Said M.Mtanda ambapo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo katika risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ana ainisha kwamba mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zimepitia miradi 11 yenye thamani ya Tsh.7,056 (Bil) huku vipaumbele vikiwaa ni uwezeshwaji wa vijana na wanawake pamoja na makundi maalum huku elimu ikipewa kipaumbele.
Mkuu wa Wilaya Sumbawanga Dr.Halfan Boniface Haule (Kushoto) Akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh.Said Mohamed Mtanda
Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa kwa shule mbalimbali Wilayani Nkasi wakati wa Sherehe za mbio za Mwenge wilayani humo.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO

MAANDALIZI YA NANE NANE KITAIFA KANDA YA KUSINI YAANZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Kikao cha Nanenane na Kamati ya Maandalizi wakati akifunga Kikao cha Wadau Kilichofanyika Banda La Naliendele,Viwanja vya Ngongo.
Mhasibu wa Kamati ya Nanenane Kanda ya Kusini,Bw Mkulasi akiwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kwa wajumbe wa kikao.
Wajumbe wa Kikao cha Wadau wa Nanenane wakiwa wanamsikiliza Mwenyekiti wa kikao ambaye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi ( hayupo pichani).
Moja ya barabara inayotengenezwa ili kuwekewa lami ndani ya eneo la uwanja.
Kazi ya utengenezaji wa barabara katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane – NGONGO ikiwa inaendelea.

Zuriel Teaches Youths Film Making/Speaks @ TEDx in Lagos

$
0
0
A firm believer in the need for all children but especially Girls to get educated, Los Angeles/ Nigerian native Zuriel Oduwole has expanded her skill transfer program, this time to children from the low income Ibeju - Lekki area of Lagos State and kids from the Makoko slum area of Lagos mainland. She was also the keynote speaker at a TEDx conference in Gbagada - Lagos.

Earlier in June in parts of Abuja, she spent it teaching children elements of her Film Making '101' program, as part of her DUSUSU Foundation's efforts to reduce the number of out of school and non skilled youths in the country.

According to the UN, Nigeria has the largest number of out of school children in Africa - just over 10 million.
Speaking after the last Film-making program yesterday in Lagos, the world's youngest film maker according to CNBC, explained that education is not just core subject like English, Geography, Science or History, but any opportunity that allows one prepare to be a productive member of society. According to her, many youths have smartphones already, so that takes care to a degree of the camera issue, so she focused on teaching editing and production of what they have shot.
Zuriel believes that in less than a year, some of the youths should be able to film relatives small events like birthdays or baby dedications, which is common in Nigeria, and if the work is good, then they could get paid for it. She conducted her first film making class in Namibia earlier in February 2016, which got her invited to meet the country's leader - H.E. President Hage Geingob at the State House in Windhoek. LINK: www.namibian.com.na/index.php?page=archive-read&id=147955

Her third and fourth countries planned for elements of the project roll out in 4Q 2016 are Ghana and South Africa.
Zuriels last film "A Promising Africa" released in November 2014 has showed in movie theater chains [Genesis Deluxe Cinema & Film House Cinema Chain] and screened as well across 3 continents, including in Ghana, South Africa, the United Kingdom, Nigeria and Tokyo - Japan.

DAR JOGGING WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA VIONGOZI KULETA MAENDELEO

$
0
0
Na Zainab Nyamka

KIKUNDI cha Dar Jogging kimetakiwa kutumia vizuri fedha walizozipata kwa kuanzisha miradi itakayowaletea maendeleo na kuinua zaidi kikundi chao ikiwemo kufika mbali zaidi kiuchumi na kutumia fursa ya viongozi wa siasa waliokuwa nao kuweza kuwawezesha na sio kusubiri wao wawatumie kwa manufaa hayo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye pia ni katibu mkuu wa chama  cha kuogelea nchini TSA Ramadhan Namkoveka amesema kuwa wamefurahi sana kuona vijana wanaungana na kutengeneza umoja ambao utakuja kuwa na mlengo wa maendeleo na hasa kwa hatua waliyofikia ya kuungana na vikundi nane kutoka maeneo mbalimbali ikijumlisha wilaya ya Temeke na Kinondoni na kuanzisha mchezo wa upatu.
 Mbunge wa jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea amewataka wanavikundi vya Jogging kuwatumia ili kutengeneza fursa za ajira na kuweza kuinua vipato vyao ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali itakayokuwa na manufaa kwao na kuacha kutumiwa na wanasiasa hususani wakati wa kampeni unapofika. Hayo amesema leo katika viwanja vya shule ya Mabatini mbio zilipoishia ikiwa ni katika kuendeleza fursa waliyoipata takribani vikundi nane vilivyoamua kujiunga na kuanzisha mfuko wa kupeana ujulikanao kama upatu.

Akizungumza na vikundi hivyo, Mtolea amesema kuwa mchango mkubwa wa maendeleo unaletwa na vijana na kama watashindwa kutumia nafasi ya miaka mitano kwa viongozi wao basi bila shaka watatumiwa wao katika kipindi cha kampeni. "Nawataka vikundi vyote viweze kututumia sisi wanasiasa katika kuleta maendeleo na katu msikubali kutumiwa kwani mtakapopata nafasi ya kuanzisha miradi mbalimbali itakuwa ni mafanikio makubwa sana kwa taifa letu hususani kwenye kuinua uchumi pamoja na sekta ya ajira kutanuka zaidi na kupunguza upungufu wa vijana kukaa bila kazi,"

Vikundi vilivyoungana na kutengenza umoja huo  ni Dar Jogging, Temeke Family, Dovya Jogging, Wasafi Jogging, Tupo Jogging, Ferry Jogging kutoka wilaya ya Temeke, Mzimuni Jogging na Barafu Jogging kutoka Magomeni wilaya ya Kinondoni na utaratibu wao ukiwa ni kila kikundi kuwasilisha laki moja (100,000) kila mwisho wa mwezi na kimoja wapo kupatiwa fedha taslimu laki nane. (800,000)
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (kati) akijumuika na wanajogging wengine kufanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa mpaka Uwanja wa shule ya Mabatini, Tandika magorofani
Wanajogging wafanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa mpaka Uwanja wa shule ya Mabatini, Tandika magorofani.
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (kati) akizungumza na wanajogging mara baada ya kukabidhi fedha taslimu kiasi cha laki nane (800,000) kwa mweka hazina wa Dar Jogging Mariamu Mkama (kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Dar Jogging Ramadhan Namkoveka (kushoto)

Zoezi la Utafutaji wa Miili ya Watu tisa wa ajali ya Boti Ruvuma lafikia tamati, Miili yote yapatikana

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Satano Mahenge, amesema kuwa kazi ya kuwatafuta watu waliozama maji katika ajali ya boti kwenye kivuko cha mto Ruvuma kutoka kijiji cha Mkenda Songea kwenda kijiji cha Mitomoni Nyasa iliyotokea Julai 02, 2016 imekamilika. Boti hiyo inayokadiliwa kubeba watu kati ya 30 hadi 50 ilipata dhoruba iliyopelekea kupinduka na kusababisha vifo vya watu tisa (9) huku wengine 36 kuokolewa.

Kazi ya kutafuta miili hiyo iliyopotea ilianza Julai 03, 2016 na kufikia tamati jana Julai 09, 2016.  
“Napenda kuwajulisha wananchi wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla kuwa miili yote tisa ya watu waliozama imepatikana. Taratibu za mazishi zimefanyika kwa familia zikishirikiana na Serikali”. Alisema Dkt. Mahenge.

Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni Omari Jela (miaka 11) alipatikana Julai 05, 2016, Fadhili Hamis Fadhili (miaka 8) alipatikana Julai 05, 2016, Hadija Said (miaka 41) alipatikana Julai 06, 2016, Zulfa Ally (miaka 14) alipatikana Julai 06, 2016, Awetu Mohamed (miaka 14) alipatikana Julai 06, 2016.

Wengine ni Omar Waziri (miaka 13) alipatikana Julai 06, 2016, Stumahi Abdallah (miezi 5) alipatikana Julai 07, 2016, Rajabu Said Machupa (miaka 17) alipatikana Julai 08 ,2016 pamoja na Tupishane Mustafa (miaka 5) alipatikana tarehe 09 Julai, 2016.

Mkuu wa Mkoa amewapongeza  wale wote walioshiriki na kufanikisha zoezi la utafutaji wa miili hiyo, na kuwashukuru wananchi wa vijiji vya Mkenda na Mitomoni kwa ushirikiano wao walioutoa kwa kikosi kazi alichokiunda kusimamia zoezi la utafutaji miili. Pia  Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kutoa boti ya kisasa iliyofanya kazi kubwa na nzuri ya kutafuta miili ndani ya mto Ruvuma.  Boti hii imesaidia sana kufanikisha kazi ya upatikanaji wa maiti ndani ya Mto Ruvuma.  

Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya zote za Ruvuma, kuwa wafanye kazi ya kuvitambua na kuanisha vivuko vyote vilivyopo ndani ya maeneo yao, wafanye sensa ya vyombo vya usafiri vinavyotumika kuvusha abiria na mizigo na kuona umakini wake, wawatambue wamiliki na waendeshaji wa boti kwenye mito na Ziwa Nyasa na waweke utaratibu wa abiria wote kujisajili kila watumiapo vyombo vya majini.

Pia amewasihi wananchi wote kuzingatia Sheria na Taratibu kila watumiapo vyombo vya moto ili kuepusha ajali zinazosababisha vifo na ulemavu.

NEWS ALERT: LINDI SEKONDARI YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi

Shule ya Sekondari ya Lindi imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Moto huo ambao ulianza majira ya saa saba usiku na Uliweza Kudhibitiwa kutoleta Athari zaidi baada ya Jeshi la Polisi, Kikosi cha Zimamoto na Wananchi kushirikiana kwa pamoja na kufanikiwa kuudhibiti saa Moja asubuhi ya leo.
Moto ukiendelea kuwaka katika moja ya majengo ya Shule hiyo.

Mpaka moto huu ulipodhibitiwa mali zifuatazo zilikuwa tayari zimeshaungua:-

• Madarasa tisa yameungua, ambapo matano yameungua pamoja na samani zilizokuwa ndani na mengine manne ni majengo peke yake Vifaa viliwahi kuokolewa na wananchi.
• Ofisi nne za walimu.
• Maabara mbili za kemia na fizikia zimeungua kwenye paa tu, hivyo samani za ndani hazijaungua.
• Takribani madawati zaidi ya 300 yameteketea kwa moto.

Majengo mengine ya shule yapo salama yakiwemo mabweni. 

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amewaomba wananchi na uongozi wa shule kuwa watulivu wakati Uongozi wa Mkoa Ukitafuta namna ya Kusaidia Wanafunzi Kuendelea na Mafunzo baada ya kufunguliwa kwa Shule hiyo kesho Julai 11, 2016
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kuuzima moto huo kwani haikuwa kazi rahisi, pia amewashukuru Polisi na Jeshi la zimamoto kwa jitihada walizochukua katika kuudhibiti moto huo.

Kwa sasa inafanyika tathmini ya mali zilizoteketea kutokana na moto huo sambamba na uchunguzi wa chanzo cha moto. Taarifa kamili ya uchunguzi na tathmini itatolewa pindi itakapokamilika.

Katika hatua nyingine mtu mmoja alietaka kuiba Komputa mpakato katika tukio hilo amekamtwa na Polisi Baada ya Wananchi kuanza kumpa adhabu.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoani Lindi, wakiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

KAMPUNI YA MANTRA YAMWAGA MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI WILAYANI SONGEA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilnith Mahenge (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Frederick Kibodya alipofika katika kata ya Majengo kupokea msaada wa madawati 500 yaliyotolewa na kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge wa kwanza mbele akikagua sehemu ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo mkoani humo,katikati nni mkuu wa wilaya ya Songea Oraleti Komando Mgema na wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Mantra Frederick Kibodya.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mantra inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo, Frederick Kibodya (kushoto), akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge moja kati ya madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 40 ili yasaidie kupunguza tatizo la madawati kwa shule za msingi mkoani Ruvuma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BURIANI ELIZABETH MAYEMBA

$
0
0

Uongozi wa Kampuni ya Business Times Limited (BTL), inayozalisha Magazeti ya Business Times, Majira na Spoti Starehe, inapenda kutangaza kifo cha mfanyakazi wake Elizabeth Mayemba (pichani).


Elizabeth Mayemba ambaye alikuwa ni Kaimu Mhariri wa Michezo Gazeti la Majira alikutwa na mauti Jumamosi ya Julai 9, 2016 saa 2 usiku, akiwa nyumbani kwake Tabata Kisukulu, Dar es Salaam.



Kabla ya kukutwa na mauti, marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote ya kila siku bila kuonesha dalili za kuumwa.



Akiwa nyumbani kwake saa 2 usiku, alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Amana, akiwa njiani alikutwa na mauti.



Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Elizabeth Mayemba atazikwa siku ya Jumanne ya Julai 12, 2016, mkoani Morogoro kwenye Makaburi ya Kola.



Elizabeth Mayemba ataagwa Jumatatu ya Julai 11, 2016 saa 5.00 asubuhi nyumbani kwake Tabata Kisukulu. Baada ya Misa mwili utasifirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.



Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kila mara ili kuwapa nafasi watu wengi wajue ratiba zote zilivyopangwa.
Kampuni imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth Mayemba, ambaye mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi na ulioonekana kwa kila mtu. Marehemu ameacha mume na watoto watatu wa kiume.
Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. 
Amina



Meneja Mkuu
Business Times Limited

Helium: 10 things you may not have known about Tanzania's new chemical wealth

$
0
0
Last week researchers discovered large quantities of helium in the Tanzanian East African Rift Valley. Helium is found in much more than just balloons and the periodic table of elements. Here’s 10 stats you may or may not have known about this chemical element and why this discovery matters for healthcare.
  1. Helium is used in telescopes, spacecrafts and radiation monitors.

  2. In the medical world, helium is essential to operate MRI machines.

  3. Tremendous amounts of energy flow through the superconducting wire throughout the key component of an MRI system, a powerful magnet cooled to 4.2 kelvin, or 452 degrees below zero Fahrenheit. Liquid helium is the only element that is feasible for cooling a magnet to the degree where the superconducting properties of the wire can work.

  4. Depending on the type of MRI being produced, a machine may need in the range of several thousand liters of helium stored in a sealed vacuum system surrounding the magnet.

  5. There are over 30 million MRI scans performed in the US each year. That’s a lot of patients and doctors who need MRI every day for diagnosis.

  6. This newly expanded resource from the Tanzanian East African Rift Valley has the potential to fill more than 1.2 million MRI scanners and should continue to support the supply to meet the demand of the industry.

  7. There are efforts underway to develop innovative ways to reduce MRI manufacturers’ reliance on this element, including an investigational, research device that was developed under a National Institutes of Health Bioengineering Research Partnership between GE Global Research and the Mayo Clinic. This new magnet technology requires only 1% of the liquid helium to operate compared to a conventional system and does not need refilling.

  8. Liquefaction is a process used to recapture helium lost during the MRI manufacturing process so it can be reused it—it’s essentially a major recycling system.

  9. GE Healthcare built a new 5,000-square-foot helium liquefaction facility in Florence, South Carolina to further liquefaction efforts.

  10. The U.S. Geological survey estimates that there are about 35 billion cubic meters worth of helium left on the plant with the majority of it coming from the U.S.
This article first appeared at GE Healthcare's The Pulse - on health, science and technology

RAIS DKT. MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA INDIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akikagua gwaride la Heshima katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wakiwasili kwenye lango kuu la Ikulu jijini Dar es Salaam.


WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA INDIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji wawekezaji kwenye mashamba makubwa ya kibiashara pamoja na viwanda vya usindikaji mazao ili iweze kuboresha uzalishaji nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Julai 10, 2016) wakati akifungua kongamano la siku moja la wafanyabiashara baina ya Tanzania na India lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kongamano hilo   lililojumuisha wafanyabiashara 50 kutoka India ambao wameambatana na Waziri Mkuu wa India, Bw. Narendra Modi, Waziri Mkuu Majaliwa alisema Tanzania inayo fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi zikiwemo miundombinu, kilimo, utalii, viwanda na madini.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lakini pia imelenga kuzalisha malighafi za viwanda ambavyo tunahimiza vijengwe. Lakini pia tumewaita waje kuwekeza kwenye sekta za uvuvi na utalii kwani nazo bado hazijaendelezwa vya kutosha,” alisema.

“Tanzania inazo kilometa 1,424 za fukwe za bahari, pia ina kilometa za mraba 223,000 za eneo la kiuchumi la bahari kuu (EEZ) na kilometa za mraba 54,337 za mito, mabwawa na maziwa ambayo ni sawa na asilimia 6.1 ya eneo la nchi nzima. Kuna fursa nyingi kwenye uvuvi, usindikaji wa samaki na ufugaji wa samaki kwenye mabwawa,” amesema.

Amesema washiriki pia wamepata nafasi ya kusikia fursa za uwekezaji zilizoko upande wa Zanzibar na kwamba kupitia vituo vya uwekezaji TIC na ZIPA wanaweza kupata huduma zote palepale bila kuhangaika kwenye ofisi mbalimbali.

Mapema, akihutubia washiriki wa mkutano huo, Waziri Mkuu amesema kuna fursa nyingine nyingi za kuwekeza kwenye sekta ya mifugo hasa katika uanzishaji wa ranchi za mifugo, usindikaji wa maziwa na nyama, usindikaji wa ngozi na utengenezaji wa bidhaa za ngozi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema urari wa kibiashara baina ya Tanzania na India umeegemea upande mmoja ambapo India inauza zaidi bidhaa zake hapa nchini Tanzania inavyouza bidhaa zake India. “Ninaamini njia mojawapo ya kurekebisha hali hii ni kwa wafanyabiashara kutoka India kuamua kuwekeza kwa kiwango kikubwa hapa nchini,” aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Charles Mwijage alisema Tanzania inahitaji India kama ambavyo India inahitaji Tanzania katika kufanya biashara zake. “India inaongoza kwa kuuza bidhaa zake hapa nchini lakini pia ni miongoni mwa nchi 10 ambazo zinanunua kwa wingi bidhaa zake kutoka Tanzania,” alisema.

Naye, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa India (Federation of Indian Chambers of Commerce and Industries - FICCI), Bw. Harshavardhan Neotia alisema biashara kati ya Tanzania na India inaendelea kukua na kwamba fursa zilizopo ni lazima zichangamkiwe mapema. “Fursa za kibiashara ni kama mawio ya jua, ukiendelea kusubiri sana unaweza usiyaone,” alisema.

Mkutano umejadili mada mbalimbali zikiwemo fursa za uwekezaji Tanzania bara na Zanzibar, fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya kiuchumi, na uzoefu wa baadhi ya wafanyabiashara kutoka India walioko nchini.

CCM ZANZIBAR YATAKA MIKATABA YA MALI ZAKE KUSIMAMIWA NA WANASHERIA

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA cha Mapinduzi  (CCM)  Zanzibar kimewataka viongozi na watendaji wa chama hicho kuhakikisha mikataba ya kibiashara wanayofunga inapitiwa na kuwashirikisha wanasheria ili kuepuka vitendo vya utapeli.

Kimesema kuwashirikisha wanasheria wakati wa kufunga mikataba ya aina mbali mbali ya kukodisha Mali za Chama hicho kutasaidia kumaliza kero na migogoro ya matumizi mabaya ya Rasilimali za CCM.

Hayo aliyasema  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai katika mwendelezo wa ziara ya  kukagua na kuhakiki mali za Chama hicho huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema matatizo ya matumizi mabaya ya Mali za chama hicho yanayojitokeza katika maeneo nchini ni kutokana  na baadhi ya viongozi na watendaji kufunga mikataba ama makubaliano na wafanyabiashara bila ya kuwashirikisha wanasheria ama kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu  hali inayopelekea baadhi ya watu kutumia nafasi hiyo kujinufaisha wenyewe badala ya kuangalia maslahi ya CCM.

EVANS MASHIMI NA THERESIA 'TEDDY' SAKAYA WAMEREMETA LEO AZURA BEACH JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wadau Evans na Teddy wa Atlanta MarCb ul  ekani usiku huu wako Azura Beach jijini Dar es salaam wakiwa katika mnuso wa nguvu baada ya kumeremeta hapo hapo ufukweni Azura katika sherehe iliyofurika ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila pembe ya dunia. Picha zifuatazo zinaongea.
Picha na Frenja Digital Production.



15MIL. ZA RADIO 93.7 EFM ZASAKWA NA WAKAZI WA DAR ES LAAM NA PWANI

$
0
0
Zaidi ya wakazi 55 kutoka mkoa wa Dar es salam na Pwani wamejishindia pesa taslimu zenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kupitia mchezo wa sakasaka ulioandaliwa na EFM redio.

Mchezo huu wa sakasaka ulianza tarehe 12/06/2016 katika wilaya ya kinondoni na kwenda katika wilaya ya Temeke, Ilala, Mkuranga na kumalizika leo tarehe 10/07/2016 katika wilaya ya Kisarawe. Wakazi zaidi ya kumi kutoka katika kila wilaya waliweza kusaka vitu vyenye thamani tofauti tofauti ya pesa kuanzia shilingi elfu hamsini hadi milioni mbili.

EFM redio huchezesha mchezo huu kila mwaka tangu redio ianzishwe kwa lengo madhubuti la kusaidia jamii inayotuzunguka, kwani pesa walizojishindia zitasaidia kuinua maisha yao kwa kufanyia biashara pamoja na kusaidia familia zao.
Mkazi wa Kimara-Temboni John Joseph akikabidhiwa pesa taslimu na meneja matukio na mawasiliano wa EFM redio Neema Godlays Mukurasi baada ya kusaka vitu vyenye thamani ya shilingi laki tatu. Wengine ni watangazaji wa kituo hicho cha redio kutoka kushoto ni Chogo akifuatiwa na Swebe Santana.
Mshindi mwingine akikabidhiwa pesa taslimu.
Mtangazaji wa EFM redio Chogo akimuhoji Bw. Sadam Raha mshindi wa shilingi milioni mbili wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.
Umati wa watu walioshiriki kusaka saka vitu vilivyofichwa katika eneo hilo wakishuhudia washindi.
Baadhi ya washiriki wakisaka saka vitu vilivyofishwa.

Benki ya NBC yazindua Program ya Wajibika kusaidia ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo na taasisi ya elimu ya juu

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde, akishiakana mikono na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Neema Rose-Singo (kushoto), baada ya kuzindua program ya Wajibika ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wapili kushoto ni; Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (wa pili kulia), na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), James Kinyanyi (wa pili kushoto), wakibonyeza kitufe cha kompyuta kuashiria uzinduzi wa program ya Wajibika ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo na Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (kulia), akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa program ya Wajibika ya Benki ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program ya Wajibika ya benki hiyo yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni; Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC,James Kinyanyi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images