Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1286 | 1287 | (Page 1288) | 1289 | 1290 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza muda zaidi kuimarisha idara zake ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa Watanzania wenye sifa za Idara ya Masoko na Habari ili kuongoza Idara hiyo.

  Awali tarehe ya  mwisho ilikuwa Julai 11, 2016 lakini kwa sasa tarehe ya mwisho itakuwa Julai 19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF imetangaza ajira.

  Lengo hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira wa miguu duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu popote duniani.

  Pili ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na soka na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati mwafaka.

  Kwa nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz

  Mbali ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko, pia TFF imepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi. Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).

  Akizungumza na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.

  Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah leo ametembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo.
   Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe ambapo pamoja na mambo mengine alimwambia kuwa  wanatamani sana kuwa na vifaa vya kufanyia kazi kama vile Full Blood Picture Machine, Ultra Sound, Na X-ray ambavyo anasema kwa wilaya nzima hakuna huduma ya X-ray hivyo inawawia vigumu kukamilisha tiba kwa wagonjwa wenye kuhitaji huduma hiyo.
   DC Asia pia alikutana na wazee wa mji wa Kilolo ambao  wameiomba serikali kuwapatia watalaamu pamoja na vifaa vya upasuaji kwa kuwa tayari walishapata jengo la upasuaji kutoka kwa mdau wa maendeleo ila  wanakwama kuanza kutumia huduma hiyo ya upasuaje kufuatia ukosefu huo wa wataalamu na Vifaa. 
  Mhe Mkuu wa Wilaya huyo aliwaahidi kufuatilia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu iliyopo wilayani humo kwa faida yao
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah leo ametembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah akiwa na Dkt. Selemani Jumbe mwenye koti jeusi na Bw. Ephron msuva mtaalamu wa maabara. alipotembelea zahanati ya Kilolo mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. Akiwa hapo alikutana na Daktari mfawidhi Dkt.  Selemani Jumbe
    
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah akipata maelezo ya jinsi vipimo mbalimbali vinavyopimwa katika maabara ya zahanati ya Kilolo alipotembelea mapema asubuhi kwa lengo la kujionea mazingira ya zahanati hiyo. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah

  0 0

   Waziri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, akikata utepe, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa na Kampuni ya Swissport Tanzania. Aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Swissport, Bw. Mark Skinner akifuatiwa na Bw. Gaudence Temu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Bw. Raymond Mbilinyi
  Bw. Gaudence Temu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania, akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa na Kampuni ya Swissport Tanzania.

  0 0

  Aliekuwa Mpinzani wa karibu wa Bi.Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kupewa ridhaa ya kubombea Urais wa Marekan kupitia Chama Cha Democrats, Bernie Sanders, amemuidhinisha Mwanamama huyo ambaye pia ni mke wa Rais wa zamani wa Marekani,(Billy Clinton), kupeperusha bendera ya Chama chao kwenye kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo lenye nguvu duniani unaotazamiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

  Bernie Sanders amemuidhinisha Bi.Hillary Clinton wakati wa mkutano wa pamoja wa kampeni uliofanyikia Portsmouth, New Hampshire.

  Kwa kumuidhinisha huko Bi. Hillary Clinton, Sanders amesema kuwa amezika moja kwa moja fununu na tetesi zilizokuwa zinaenea kwamba hatomuidhinisha Clinton na huenda akachagua kuwa mgombea binafsi. Habari hizi pia ni pigo kwa mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump ambaye alikuwa na matumaini ya kuwapata wapenzi wa Bernie Sanders kwa njia moja au nyingine.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (kushoto), akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa uendelezaji milki uliofanyika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Usimamizi Milki, Hamad Abdallah, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa Nyumba wa wizara hiyo, Charles Mafuru na Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maaly. Mkutano huo uliandaliwa na NHC.
   Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula kuufungua.
   Mwonekano wa meza kuu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
  Wadau wa uendelezaji milki wakiwa kwenye mkutano huo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa mapato kutokana na nyaraka hizo kutumika.

  Watu hao wamekuwa wakitengeneza nyaraka ambazo ni vyeti vya kuzaliwa ,Cheti cha Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita, vyeti vya kuhitimu, Kadi za bima mbalimbali pamoja na mihuri mbalimbali ya taasisi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa watu hao wanawahoji juu ya watu walionufaika na vyeti bandia.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) kuhusu Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa mapato,leo jijini Dar es Salaam

  Kamanda Sirro amesema kuwa watafatilia watu wote wenye vyeti bandia ambao watatajwa na wameajiliwa na serikali katika sehemu mbalimbali.

  Aliwataja watu hao kuwa ni Ashrafu Maumba (37) Mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) Mkazi wa Mnyamani pamoja na Mahamudu Zuber (24) Mkazi wa Buguruni.

  Nyaraka walizowakuta nazo ni vyeti bandia vya kidato cha nne 50, stika za SUMATRA 20, Vyeti vya Vyuo vya Uuguzi, Vyeti vya Kuzaliwa 10, VETA 10, Cheti cha Darasa la Saba, Siri au Rakili bandia za vyeti vya CBE 10. Leseni za Biashara, nyaraka za bima 100 pamoja na nyaraka za COMESA 100.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akiwaonesha waandishi wa habari nyaraka za serikali bandia,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka.

  Katika upekuzi huo waliweza kukamata mihuri mbalimbali ya Ofisi za Serikali na Binafsi, Muhuri wenye nembo ya bibi na bwana, Karatasi maalum zilizo na nembo za TRA kwa ajili ya kutengeneza kadi za vyombo vya moto Zaidi ya 500, Computa nne, Monitor Screen tatu, printer tatu Generator moja na stabilizer moja.

  Baada ya uchunguzi watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote.

  Wakati huo huo jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki aina ya Short Gun Pump Action ikiwa na risasi sita pamoja na pikipiki aina Fekon .

  Silaha na pikipiki hiyo walikamata wakati majambazi walikuwa wakitaka kwenda kuvamia na jeshi la polisi lilipata taarifa na kutumia mbinu zao za kuwakamata baada ya kuwakimbiza na kuweza kuacha vitu hivvyo.Na Chalila Kibuda.

  0 0

  Every year ZIFF “pauses” the event for an evening to host a public forum on a topical and often difficult topic. A panel of experts is invited to the discussion and engages directly with the public at the Old Fort Ampitheatre in Stone Town. 
  The Difficult Dialogues program is our marquee event and a unique program of the festival, made possible this year with the generous support of the Italian NGO ACRA. The event will also be broadcast live on ZENJ TV, enabling an even wider audience to benefit from the event. 
  The discussion is conducted in both English and Swahili giving all festival visitors opportunity to join in the conversation. This year the topic for the Difficult Dialogue will be the state of Stone Town’s Heritage site status. In recent years this status has been jeopardized by a number of developments creating major concern for many stakeholders. 
  Development and tourism can often come into conflict with culture and heritage and yet they are all interdependent. This complex issue will be discussed further by a panel of experts including Professor Ikaweba Bunting and Mr. Mugheiry Sheha Mkungzini and event will be hosted by Maryam Mansab. 
  The event will take place live at the Old Fort on Wednesday July 13th from 19:20 and also be broadcast live on ZENJ TV. Please also tune in to ZENJ TV daily until July 17th at 10am and 5pm for the best of ZIFF!

  For all the festival details please visit www.ziff.or.tz www.facebook.com/zanzibarinternationalfilmfestival , twitter @ZIFF_2016 and Instagram Zanzibarinternationalfilmfest

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, akikata utepe, wakati wa ufunguzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa Katika Uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere na Kampuni ya Swissport Tanzania. Aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Swissport, Bw. Mark Skinner.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania,Bw. Gaudence Temu (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa na Kampuni ya Swissport Tanzania.

  0 0

  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.

  Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.
  Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame.

  Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai.
  Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
  Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.

  Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya Matangazo.
  Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manidpaa na Majiji 185 kabla ya hawajakula kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano ulioitishwa  na Rais John Magufuli kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya na baadhi ya Wakuu wa  wilaya  ikulu jijini Dar es salaam Julai 12, 2016.
  Wakuu wa wilaya za Kongwa Mhe deo Ndejembi (kushoto), Siriel Shaidi Mchembe (DC Gairo) na Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe (DC Manyoni) wa kila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukosa kufanya hivyo na wenzao wiki iliyopita. 

  Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji 185 wakila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Kituo cha TBC Manyara Bw. Mganga Mwanja (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo (katikati) Mhe. Anastazia Wambura changamoto ya mitambo waliyo nayo alipotembelea eneo la mitambo ya kurusha matangazo leo katika Mji wa Babati katika ziara yake ya kikazi.
  Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mji wa Manyara Bi. Rena Urio leo kabla ya kuanza kwa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (katikato) kutembelea vivutio vya kiutamaduni vilivyoko katika Wilaya ya Babati.

  0 0  0 0

  Na Chalila Kibbuda, 
  Globu ya Jamii.

  BODI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza kufanya kazi kwa kasi katika utoaji  wa huduma kwa wananchi.

  Akizungumza na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo  Mwenyekiti bodi hiyo Spika Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa utaratibu wa awali wakurugenzi walikuwa wanaajiliwa kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu.

  Amesema kuwa wakurugenzi waliokuwa wanafanya kazi ambapo wengine kwa mikataba na wengine wamemaliza na ambao walikuwa wanaendelea wamesitisha mikataba yao.

  Makinda amesema kuwa NHIF imekaa kwa muda ikiwa haina bodi kwa mwaka mmoja na nusu hivyo baadhi ya vitu havikuwa sawa.

  Amesema kuwa watu ambao wamemaliza mikataba na weengine kusitisha mikataba yao wanaweza wakaomba tena kama wana sifa ya kazi watazoomba na kuangalia weledi wao


   Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani)   juu ya maboresho ya muundo wa safu ya wakurugenzi leo jijini, Dar es Salaa,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani)  juu   ya hatua ya bodi waliochukua katika shirika hilo katika kubadili muundo wa wakurugenzi, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF Spika Mstaafu, Anne Makinda.
  Wajumbe wa bodi na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda. Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

  0 0

  Picha na habari na 
  Emmanuel Masaka
  Taasisi ya Kutetea uhai (Pro Life) imesema kuwa utoaji mimba na vidhibiti mimba una athari kwa wanawake kupoteza maisha kutokana na kufanya hivyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Taasisi hiyo, Padre Shenan Boquet amesema kuwa watu wamepandikizwa vitu vibaya juu ya uzazi kuendelea kujengwa vizazi na vizazi.

  Amesema kutoa mimba na kuweka vidhibiti kunahitajika kuwepo kwa elimu katika kuibadilisha jamii kutoondokana vitu hivyo vya kunyima uhai.

  Aidha amesema kuwa baadhi ya nchi zinahamasisha utoaji mimba na vidhibiti mimba wakiwa wanajua ni kunyima haki viumbe vingine.

  Amesema katika kupinga hatua hiyo taasisi imeandaa kongamano litakalofanyika Mbagala Julai 18 ikiwa ni kutoa elimu na kuwepo kwa maada mbalimbali.

   Rais wa Taasisi ya kutetea uhai (Pro -life), Padre Shenan Boquet  akizungumza na waandishi habari  juu ya kutetea haki ya uhai katika kupinga vidhibiti mimba na utoaji mimba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mtafiti wa Elimu wa Shirika hilo,Brian Clowes
   Mtafiti wa Elimu wa Shirika hilo,Brian Clowes, akizungumza na waandishi habari juu ya kutetea haki ya uhai katika kupinga vidhibiti mimba na utoaji mimba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Rais wa Taasisi ya kutetea uhai (Pro -life), Padre Shenan Boquet
  Waandishi wa habari  wakimsikiliza Rais wa Taasisi ya kutetea uhai (Pro -life), Padre Shenan Boquet    leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mfahamu binti Johari Swedy, mwanafunzi na mkazi wa Jiji la Mwanza. Ni binti anaestahili kuigwa na wengine kutokana na juhudi na malengo yake maishani. 
  Johari Swedy (kushoto) akizungumza na GB @BMG (kulia) alipokuwa katika eneo la Ahsante Moto Jijini Mwanza.

  Kutana na binti Johari Swedy (19), mkazi wa Jiji la Mwanza. Alizaliwa mwaka 1997. Ni mwanafunzi ambae historia ya masomo yake ilianzia shule ya msingi Mabatini aliposoma darasa la kwanza hadi darasa la saba na baadae akajiunga na shule ya sekondari Mtoni zote za Jijini Mwanza ambapo alisoma kidato cha kwanza hadi kidato cha na nne.

  0 0

  Baada ya jana timu ya soka ya Pamba ya Jijini Mwanza, kupata nafasi ya kucheza ligi daraja la kwanza kutokana na timu ya Abajalo Fc ya Jijini Dar es salaam kupoteza pointi sita kwa kosa la kumchezesha mchezaji wa Kagera Sugar katika michuano ya ligi daraja la pili, timu hiyo imeeleza furaha yake sambamba na mikakati iliyopo katika kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.
  Akibonga na VesterJtz wa BMG, Msemaji wa timu ya Pamba, Gervas Mbaya, amesema wamepokea maamuzi yaliyotolewa na TFF kwa shangwe kubwa baada ya kushinda rufaa waliyokuwa wameikata wakilalamikia ushindi wa timu ya Abajalo Fc.
  Amesema ndani ya siku mbili zijazo, uongozi wa timu hiyo utakutana ili kupanga mikakati ni lini timu ya Pamba ianze kufanya mchakato wa usajili ili timu iingie kambini kwa ajili ya maandalizi ya mapema kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.
  Msemaji wa Pamba, Gervas Mbaya (kushoto), akiteta na Slyvester Joseph-VesterJtz @BMG (kulia).

  Itakumbukwa kwamba timu ya Pamba SC ya Mwanza na The Mighty Elephant ya Songea zilikata rufaa TFF kuilalamikia timu ya Abajalo FC kwa kumtumia mchezaji wa Kaliua City ya Tabora, Laurence Mugia, wa Kagera Sugar katika michezo ya mtoano wa Ligi daraja la pili kwa ajili ya kupanda daraja la kwanza ambapo baada ya kushinda rufaa hiyo timu zote zilijinyakulia pointi tatu na magoli matatu huku Abajalo ikipoteza pointi sita na hivyo kupoteza nafasi ya kucheza ligi daraja la kwanza.

  Bonyeza HAPA Kusikiliza Zaidi. Au Bonyeza Play Hapa Chini.

  0 0

   Mwanariadha wa zamani aliyewahi kushiriki  katika mashindao ya         Olimpiki nchini Ugiriki  Bw. John Stephen Akhwari  (wa kwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) Mwenge aliyoukimbiza katika viwanjani vya Beijing nchini China wakati wa kufungua mashindano ya Olimpiki mwaka 2008 alipomtembelea nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu Mjini Mbulu,(wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.

   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) akiwa ameshikilia kikombe cha ushindi wa Mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari alichoshinda shinda katika Mashindano yaya Olimpiki yaliyofanyika nchini Ugiriki kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga (wa kwanza kushoto)  na  John Steven Akhwari mwenye (wa kwanza kulia) wakiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu.
   
   Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akisalimiana na Daktari wa Timu ya Jeshi la Wananchi Andrew Panga leo alipotembelea timu hiyo kambini Mjini Mbulu  akiwa katika ziara ya kikazi (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(wasita kulia) akiwa katika picha ya pamoja leo na Timu ya wanariadha wa Jeshi la Wananchi waliyoko kambini Wilayani Mbulu alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi (wasita kushoto) ni mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga

  0 0
  0 0

   Waamuzi wa Mchezo wa leo kati ya Yanga ya Tanzania na Medeama ya nchini Ghana, wakiziongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1-1. ambapo Goli la Yanga liliwekwa kimyani na Mshambuliaji Donald Ngoma dakika ya pili tu ya Mchezo kipindi cha kwanza huku Medeama wakisawazisha dakika 17 baadae kupitia mwa Mshambuliaji wake Benard Danso.
   Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia ushindi wao pamoja na Washabiki wao, baada ya Mshambuliaji wake Donald Ngoma kuipatia timu yake goli la kuongoza ikiwa ni dakika ya pili tu Mchezo dhidi ya Medeama ikiwa ni Mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
   Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Medeama, Samuel Adade.
   Mwamuzi wa Mchezo huo, Ibrahim Nour El Din akimzawadia kadi ya njano, beki wa Timu ya Medeama.
   Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akijiandaa kuachia shuti kuelekea langoni mwa Timu ya Medeama, wakati wa Mtanange wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa Uwanja wa Taifa leo. timu hizo zimetoka sare ya kufungana 1-1.


older | 1 | .... | 1286 | 1287 | (Page 1288) | 1289 | 1290 | .... | 3282 | newer