Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1275 | 1276 | (Page 1277) | 1278 | 1279 | .... | 3270 | newer

  0 0
  0 0


  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu), Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, na kushoto ni Mhasibu wa Mfuko huo, Grace Tarimo

  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, ameutaka Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kujiweka tayari kulipa mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi kama ambavyo Sheria ilivyoelekeza.Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Julai 2, 2016 wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayoshiriki kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya Ofisi yake.

  “Najua mnatakiwa kuanza kulipa fidia mwezi huu wa Julai, vipi mko tayari na kama bado basi mjiweke tayari kufanya hivyo.” Alisema Waziri.

  Akimjibu Waziri Mhagama ambaye alifuatana na maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Sarah Kibonde Msika, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera alimwambia Waziri kuwa Mfuko umejiandaa kikamilifu kutoa fidia kwa wafanyakazi ambapo elimu ilitolewa kwa wadau wengi wakiwemo madaktari kote nchini watakaowafanyia tathmini wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi.

  Sebera pia alitoa wito kwa wadau kutembelea banda la WCF ili kujipatia maelezo ya kina ,kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo ikiwemo Fidia kwa Wafanyaakzi ambayo inaanza kutolea Julai mosi mwaka huu wa 2016.Banda la WCF liko kwenye ukumbi wa Sabasaba kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere.
  Waziri akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa WCF, na maafisa wa SSRA.

  Waziri akiagana na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, baada ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Jengo la Wizarabya Fedha, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha SSRA, Sarah Kibonde Msika.


  0 0

  RAIS wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwa tayari kukabidhi tuzo  kwa Wizara, taasisi za Serikali, kampuni, nchi washiriki pamoja na mashirika yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Ijumaa Julai 1, 2016. Kushoto kwake ni mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli na kulia kwake ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharlesMwijage akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  Na Immaculate Makilika, MAELEZO
  Rais Paul Kagame alikabidhi tuzo  hizo Ijumaa Julai 1, 2016  wakati alipokuwa akifungua maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwl Nyerere maarufu kama Sabasaba, vilivyopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
  Wizara na taasisi za Serikali, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali yalishiriki maonesho hayo kwa kushindana katika kuonesha bidhaa bora  na kueleza huduma nzuri  wanazotoa, ambapo baadae Rais Paul Kagame aliwakabidhi washindi hao tuzo mbalimbali.
  Baadhi ya  washindi hao walioganywa katika makundi mbalimbali ni pamoja na,  kundi la bidhaa za kilimo nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na  kampuni ya farm equip Tanzania limited, nafasi ya mshindi wa pili ilishikwa  na  kampuni Asas dairies na nafasi ya  mshindi wa kwanza ilishikwa na  Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).
  Katika kundi la usindikaji wa vyakula na huduma za vinywaji, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na kampuni ya  Bakhresa Group, ikifuatiwa na kampuni ya P&P, na nafasi ya  mshindi wa kwanza ilishikwa na  kampuni ya Afri tea and coffe blenders limited.
  Kwa upande wa taasisi za kifedha, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na  benki ya TIB, ikifuatiwa na Benki ya CRDB huku Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ikishika nafasi ya  kuwa  mshindi wa kwanza. Vilevile katika kundi la Mifuko ya hifadhi ya jamii nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, nafasi ya mshindi wa  pili ilishikwa na Mfuko wa Pensheni wa  LAPF na nafasi ya mshindi wa kwanza ikiwa ni Mfuko wa  Pensheni wa  PPF.
  Kwa upande wa nchi za kigeni zilizoshiriki maonesho hayo ya 40 tuzo zilienda kwa nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya  mshindi wa tatu, Ujerumani ikishika nafasi ya mshindi wa pili huku  nafasi ya mshindi  wa kwanza ikiwa  ni nchi ya  Afrika Kusini. Aidha, washindi wa jumla walioshiriki katika  maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilichoshika nafasi ya mshindi wa tatu , ikifuatia  Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Chuo cha Cha Ufundi  Stadi (VETA) kilichoshika nafasi ya mshindi wa kwanza.
  Baada ya kuwakabidhi tuzo hizo na kufungua rasmi maonesho hayo ya 40 ya biashara ya kimataifa Rais Kagame alitoa wito kwa washiriki wa maonesho hayo ya 40, kushirikiana ili kubuni mawazo mapya ya biashara ikiwa ni pamoja na  kutambua fursa zilizopo katika soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, katika kukuza biashara zao na kusaidia ukuzaji wa uchumi wa pamoja katika nchi wanachama wa  Jumuiya hiyo.


  0 0

   


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika hilo.
  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifashi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akisalimiana na Waziri Jenista Mhagama.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akisalimiana naOfisa Uhusiano wa NSSF, Devota.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati), akiwa katika banda la NSSF.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), akishiriki kutoa huduma kwa wateja waliofika katika banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo. 
  (Picha na Francis Dande)

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari  alipotembelea banda la CRDB na kushiriki kutoa huduma kwa wateja waliofika katika banda hilo. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
   Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Robertius Twijuke (kushooto)akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo waliofika kwenye banda la benki hiyo wakati wa maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa VETA wakati alipotembelea maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa ya Sabasaba.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa  ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa  Mashekhe wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana Dhishan  Haidar  na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar
   Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo  kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Pangani, Mhe. Zainabu Abdallah Issa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo. 
  Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Martine Shigella 

  Mkuu wa wilaya mpya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi 
  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanaisha Rajabu akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella 

  0 0

  Anaitwa Devota Sotel kutoka 91.0 Passion Fm Mwanza. Kwa muda mrefu amekuwa king'ang'anizi katika umahiri miongoni mwa watangazaji bora wa vipindi vya taarabu Jijini Mwanza na hata Kanda ya Ziwa.

  Mambo yake si ya kitoto ukimsikiliza katika kipindi cha "Ambaa na Mwambao" kinachoruka 91.0 Passion Fm Mwanza kila siku jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane mchana.
  Lakini pia jumamosi kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni na jumapili kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa mbili usiku.
  Uwepo wake katika tasnia ya utangazaji hususani katika vipindi vya taarabu, kumeibua watangazaji wa taarabu wapya Mwanza ambao wamekuwa na ndoto za kufanya kazi kwa juhudi zaidi ili kumtoa Devota kwenye ubora wake alioukomalia kwa miaka mingi sasa.
  Wapo watangazaji wengi wa taarabu ambao wanaibuka kwa kasi ya ajabu Jijini Mwanza na hivyo kuongeza mvuto kwa mashabiki wa taarabu Mwanza ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu ni mtangtazaji yupi wamsikilize na ni yupi wamuache. 
  Ubunifu pekee ndio utakaobainisha nani bora zaidi kwa mwaka huu 2016 na hivyo kumuondoa Devota kwenye ubora wake.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wa wilaya tano za mkoa huo pamoja na watendaji wa ofisi yake baada ya kiapo

   Mmoja wa Wakuu wa wilaya akila  kiapo


  Na Mathias Canal, Lindi 

  Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi husika.

  Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha madawati yanatimia kama ambavyo agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la kuhakikisha wanafunzi wanaketi katika madawati pasipo kuwa na mbanano.

  Wakuu wa Wilaya  walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngumbiagai na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango.

  RC Zambi amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm ili kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba mawaka jana.

  Pamoja na hayo mkuu huyo pia amesema kuwa anatarajia kuanzishaTuzo ya Mkuu wa wilaya kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo watakubaliana na kamati hiyo.

  Wilaya ya lindi ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha zaidi na kilimo kuliko masomo Muwango amesema kuwa atahakikisha anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya wilaya ambapo Kamati hiyo itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya Nachingwea na kamati hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu wa Wilaya atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo inafanikiwa.


  0 0

  Usikose kuangalia kipindi cha Mizani ya Wiki hii leo saa mbili na nusu usiku kupitia  Azam 2 ambapo baadhi ya wabunge na wanaharakati wajitokeza kupongeza kikao cha bunge kilichomaliza hivi karibuni na kuharishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


  0 0

   Asubuhi hii Magari mawili yote ya aina ya Toyota Rav4 yamegongana katika makutano ya barabara ya Samora na Pamba karibu na Benki ya NMB Bank House na Shirika la Bima la Taifa (NIC)  Jijini Dar es Salaam.
   Wapita njia wakiangalia ajali hiyo ambayo hakuna aliyeumia zaidi ya magari
  Wana usalama barabarani wamefika eneo la tukio mara moja.
  PICHA NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM

  0 0

  Gari la kufagia barabara la Kampuni ya Green Waste Pro. Ltd likisafisha barabara ya mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam katika juhudi za kuliweka jiji safi kwa njia ya kisasa. Picha na Benedict Liwenga wa WHUSM

  0 0


  By Saidi Yakubu,
  Bunge Staff

  My heart goes out to Beatrice Shellukindo and my thoughts are with her children whom she loved and cared deeply.Beatrice was a charming woman and courageos leader.
  In my many engagement with her she would always say "in my vocabulary,impossible doesn't exist" and she lived by that statement.

  At one time we were travelling together  in Nigeria and upon reaching Lagos from Port Harcourt my ticket was not confirmed in our onward journey and the flight was full, she collected all other MPs passports and approached the flight supervisor and told her  "we are travelling as a group with him as delegation secretary he has the documents and our welfare arrangements if he cant travel please cancel all our onward journey as well" she said it in her usual sharp Beatrice tone such that the manager reluctantly upgraded one passenger to another class for me to travel with all other MPs. It was a lesson that always don't give up.


  Beatrice was keen to understand something and once she does she will be a vocal advocate to the point of being labeled radical,her speeches in Parliament are a testimony to that.
  Beatrice was a Parliamentary Service Commissioner and she fought hard for MPs welfare as well as staff but she was very hard on staff she knew they can do better.
  Beatrice was a leader in high levels of Commonwealth Parliamentary Association in Africa Region and she championed women causes and made her name in the continent and beyond where she traveled to build alliances and goodwill for Africa's voice to be heard within the Commonwealth.
  She was one of the very few MPs whom I talked to regularly after they finished their term and she was still in a fighting spirit though the body was weak few months ago when I last spoke to her.  We have lost an exemplary woman.

  May God rest her soul in eternal peace.
  Amin.

older | 1 | .... | 1275 | 1276 | (Page 1277) | 1278 | 1279 | .... | 3270 | newer