Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUFUNGUA OFISI KIGALI,RWANDA.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli.

Na Daudi Manongi, MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli  amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) watafungua ofisi nchini Rwanda ili kuraisisha  uhakiki wa bidhaa  kwa  wafanyabiashara  wa  Rwanda wanaoingia nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ikiwemo ufunguzi wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa Serikali imetoa eneo la bandari kavu (ICD) kwa ajili ya kuhifadhia Bidhaa kutoka nchi ya Rwanda ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya biashara hapa nchini na kwa namna hiyo biashara itakua kwani tunategemea uchumi utapanda kutoka asilimia 7 ya sasa mpaka asilimia 7.2.

Pia amesema kuwa Serikali imepunguza vituo vya ukaguzi barabarani kutoka Tanzania kwenda Rwanda kufikia vitatu na kwa kufanya hivyo itarahisisha safari za magari ya biashara njiani na hivyo kufikisha bidhaa kwa haraka. 

Aidha amesema kuwa serikali iko mbioni kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya mapato badala ya kila sehemu kuwa na mfumo wake ambao unapoteza mapato mengi kwa kuwa mifumo hiyo haina uthibiti mmoja na hivyo serikali ya Rwanda itasaidia kwa kuleta wataalamu wa Tehama ambao watasaidia kutoa mafunzo ili kusaidia mapato yetu kuwa katika udhibiti mmoja.

Kwa upande Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza Uchumi wa nchi izi mbili kwani zina historia ndefu na kwa kuendelea kufanya biashara pamoja nchi izi mbili zimejenga taswira mpya katika mahusiano.

Awali Mawaziri wa mambo ya Nje wa nchi za Tanzania na Rwanda walitia saini Muhtasari wa Tume ya Ushirikiano wa pamoja baina ya nchi hizi mbili.

GAZETI LA MTANZANIA LAJA NA MWEONEKA MPYA

$
0
0
Warembo kutoka Kampuni ya New Habari wakiuza gazeti la Mtanzania lenye mwonekano mpya katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo.
Muonekano wa mbele.
Muonekano wa Nyuma.

DIRA YA DUNIA ALHAMISI 30/06/2016

MASHINDANO YA ROLLING STONE YAANZA RASMI JIJINI ARUSHA.

$
0
0
TIMU 20 kutoka ndani ya nchi na Nje ya nchi Tatu zilizothibitisha kushiriki mashindano ya Rolling stone zimeanza kuwasili mkoani Arusha kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Iilboru sekondari na Arusha Meru.

Mikoa hiyo ni Simiyu, Mara, Singida, Dodoma, Lindi, Pwani, tanga, Kigoma, Geita, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Dar es Salaam na Arusha ikiwa ni wenyeji na nchi za nje ni Burundi, Kenya Congo na Zanzibar kama nchi.

Akizungumza mjini hapa Mwenyekiti wa Rolling stone Ally Mtumwa alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na wageni kutoka mikoa mbalimbali wameanza kuwasili.

Alisema mpaka sasa kuna mikoa imeanza kuwasili kwa ajili ya mashindano hayo ingawa idadi tuliyoitarajia kwenye mashindano hayo imekuwa pungufu tofauti na mialiko tuliyoitoa.

“ Tulialika mikoa yote ya Tanzania na nchi zote za Afrika masharika lakini nchi zilizotoa majibu kwa njia ya barua ni hizo tatu tu huku zilizotoa majibu kwa njia simu ni nying lakini hatuna uhakika nazo kwani mpaka leo hii ambapo timu nyingine zimeanza kuwasili lakini nchi hizo hazijathibitisha kwa maandisha” alisema Mtumwa.

Mtumwa alisema wametoa nembo itakayowakilisha mashindano hayo ya Rollingstone kuwa ni Tembo kwani mnyama huyo ni wa bahati ambae kwa sasa serikali inapinga ujangili wa mnyama huyo.

“Tumemtumia mnyama tembo kwasababu kwenye mashindano haya tunataka kutoa elimu ya kupinga ujangili unaoendelea nchini na kwa nchi jirani hivyo kupitia mashindano haya najua elimu itafika kwa wakati”alisema Mtumwa.
Habari picha na woinde shizza globu ya jamii Arusha 

TPA YAKABIDHI MSAADA WA SH.MILIONI 250 KWA AJILI YA MADAWATI.

$
0
0
MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipokea mfano wa hundi ya sh.miliioni 250, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya  Mamlaka ya  Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa  Ignas Rubaratuka. Fedha hizo ni kwaajili ya mchango wa madawati, Dar es Salaam leo. Wakwanza kulia ni  Mkurugenzi  Mkuu TPA, Mhandisi  Deusdetit  Kakoko. 
(Picha na Christopher  Lissa).

 Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa
Sh. milioni 250 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili 
ya kuchangia kampeni ya madawati Mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na tatizo la kukaa chini wanafunzi.

Licha ya kukabidhi msaada huo mamlaka hiyo pia imechangia kiasi cha Sh
milioni 165 katika Halmashauri 11 nchini zenye uhaba wa madawati ambazo walizianisha katika uhitaji wa msaada huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi (TPA) Profesa Ignas Rubaratuka alisema, msaad huo ni
kutekeleza jukumu katika kuunga mkono kampeni ya Rais katika
kuhakikisha wanatatua tatizo la ukosefu wa madawati katika Wilaya za
Mkoa huo ili watoto wa kitanzanbia wwasome katika mazingira bora.

“Pamoja na shughuli zake za kupakua na kupatia mizigo pia mamlaka
imekuwa mstari wa mbele kuchangia masuala ya kijamii kupitia sera yake
ya msaada kwa jamii (CSR) ambapo inashiriki kikamilifu kurudisha faida
yake kwa jamii,” alisema

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo Makonda ameishukuru mamlaka
hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia sekta ya elimu ambayo imekuwa
ikukabiliwa na changamoto kubwa hasa ya uhaba wa madawati.

Amesema msaada uliotolewa na TPA utasaidia kupunguza uhaba wa madawati 
zaidi ya laki nane unaolikumba jiji la Dar es Salaam ambao utasaidia 
kupunguza adha wanayoipata wanafunzi.

“Tunachangamoto kubwa ya madawati na tumeambiwa mpaka ifikapo juzi
tuwe tumekamilisha kampeni ya madawati najua Mkoa wangu ni miongoni
mwa mikoa yenye uhaba mkubwa lakini ninyi bado mmenipa nguvu ya
kuamini tutafanikiwa na kibarua changu kitaendelea kuwa salaama,”
alisema Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu TPA Deusdedit Kakoko alisema wameamua 
kutoa msaada lengo ni kurudisha kiasi kwa jamii na msaada uliotolewa 
umetolewa kwa makubaliano yao pamoja na wafanyakazi wa TPA ili kuondoa 
uhaba wa madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa mingine .

“Kampeni ya madawati mnayoifanya tunaiona na ndio maana tumeamua kutoa 
msaada huu kama mchango wa kampeni fedha zote tayati tumeshaweka 
katika akaunti za Mkoa naamini zitakwenda kufanya yale
yaliyokusudiwa,” amesema.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA RWANDA MH.PAUL KAGAME LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kufanya Mazungumzo.

Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi rasmi ya maonesho ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba  leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride la heshima uwanjani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais Paul Kagame akiwapungi mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO

RAIS DKT. MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA WATU 12 WALIOPOTEZA MAISHA AJALINI DAKAWA


Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson afungua Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akifungua Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa tatu toka kushoto) akiongea na Viongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) (kushoto) kutoka Afrika Kusini wakati wa Kikao Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.


Baadhi ya Wajumbe na Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda za kikao kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) (aliyekaa mbele) akiongea Viongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.


Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda za kikao kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika Kikao cha Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda ya kikao hico kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.


Wajiumbe wa Kikao cha Uongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia waliokaa mbele) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016. Picha na Ofisi ya Bunge)

MBINGA YAMALIZA KAZI YA KUTENGENEZA MADAWATI

$
0
0
Na Muhidin Amri,Mbinga

Wilaya ya Mbinga kupitia halmashauri zake mbili za halmashauri ya mji na wilaya, imefanikiwa kukamilisha mradi wa utengenezaji madawati kwa ajili ya kukabiliana na upungufu katika shule za msingi na sekondari wilayani humo.

Kazi hiyo, ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt John Magufuri kwa wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa apa nchini kuhakikisha wanatumia rasimali za maisitu zilizopo katika maeneo yao ili kumaliza tatizo kubwa la madawati lililosababisha baadhi ya watoto waliopo shuleni kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Mkurugenzi mtendaji wa hamashauri ya wilaya ya Mbinga Venance Mwamengo alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili ambapo alifafanua kuwa,wilaya hiyo ilikuiwa na upungufu wa madawati 12,952 kati ya hayo kwa shule za msingi ni 8452 na kwa shule za sekondari kulikuwa na upungufu wa viti na meza 4500.

Hata hivyo alisema, hadi kufikia tarehe 30/6/2016 ambao ni muda wa mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo tayari wamefanikiwa kutengeneza madawati 8000 hivyo kubakia madawati 450 ambayo wanatarajia kukamilisha ndani ya siku tatu zijazo kwa sababu vifaa vyote muhimu kama vile nondo na mbao viko tayari.

Pia Mwamengo alisema, kwa shule za sekondari wamekamilisha kabisa kazi hiyo na kubakiwa na ziada ya viti na meza 1000 ambazo zitasambazwa katika shule za msingi zinazokabiliwa na upungufu ili kumaliaza tatizo hilo la madawati katika wilaya hiyo.

“ apa tayari tumefanikisha kumaliza kazi ya viti na meza kwa shule za sekondari na sasa tunaendelea kumalizia kuunganisha madawati yaliyobaki ambapo ndani ya siku tatu tayari tutakuwa tumeshamaliza kazi yote,hata hivyo hilo sio tatizo kubwa sana kwa sababu tuna ziada ya viti na meza 1000 ambazo tulikusudia kupeleka katika shule za sekondari tutapeleka kwenye shule za msingi ili kufidia upungufu uliopo”alisema Mwamengo.

Kwa mujibu wa Mwamengo ni kwamba wilaya ya Mbinga, ilitenga kiasi cha shilling milioni 475.820 kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati,meza na viti kwa shule za msingi na sekondari hatua akwa kiasif ulani imesaidia kupunguza tatizo hilo.

Mwamengo alisema, kiasi hicho cha fedha ni gharama za kununulia mashine za kuranda,kukata na kukunja vyuma,mashine za kupasulia mbao,umeme, na gharama za zingine ndogo ndogo na yametengenezwa kwa kutumia mbao pamoja na chuma ili kuyafanya yawe imara zaidi ikilinganisha na madawati yanayotengenezwa kwa mbao tupu ambayo uharibika haraka.

Mwamengo alisema, wilaya ya Mbinga ilikuwa na upungufu wa madawati 12,952 ambayo katika shule za msingi upungufu ulikuwa madawati 8,452 na viti na meza kwa shule za sekondari upungufu ulikuwa 4,500,ambapo ilianza kutengeneza madawati mwezi januari mwaka huu na kadri ya agizo hilo walitarajia kukamilisha kazi hiyo tarehe 30 mwezi huu lakini kutokana na changamoto mbalimbali kazi hiyo itakamilika rasmi mwezi huu.
Madawati ya shule ya msingi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma yakisubiri kuunganishwa katika karakana mojawapo inayotumika kwa ajili ya kutengeneza madawati ili kukabiliana na upungufu huo kwa shule za msingi wilayani humo, ambapo wilaya hiyo imefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 95 agizo la Rais Dkt John Magufuri.
Baadhi ya meza na viti kwa ajili ya shule za sekondari wilayani Mbinga zikiwa katika karakana ya wilaya hiyo zikisubiri kusambazwa mashuleni ili kumaliza upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari,wilaya ya Mbinga imefanikiwa kumaliza uhaba wa madawati yote 12,850 ambayo yalihitaji kwa shule za msingi na sekondari wilayani humo.
Baadhi ya mafundi wakipandisha madawati kwenye gari kwa ajili kusambaza katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wiayani humo, ambapo wilaya ya Mbinga kupitia halmashauri zake mbili za halmashauri ya mji na wilaya zimefanikiwa kumaliza uhaba wa madawati kwazake, hivyo kuwa wilaya ya kwanza katika mkoa wa Ruvuma kutekeleza kwa asilimia 95 agizo la Rais Dkt John Magufuri alilotoa kwa wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa hapa nchini kuhakikisha wanatumia rasilimali za misitu kumaliza tatizo la upungufu wa madawati.Picha na Muhidin Amri.

KAMATI YA MAADILI YA TFF YATUPILIA MBALI KESI YA JERRY MURO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMATI ya maadili ya TFF imetupilia mbali shauri la Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro baada ya kuona mapungufu kibao kwenye barua ya wito pamoja na kushindwa kuanbatanisha sababu za kuitwa kwake, na katika.barua ya Juni 29 Muro alitumiwa wito wa kuitwa kwenye kamati ambayo haikuwekwa wazi ni kamati gani pia hakukuwa na viambatanisho vyovyote vya mashataka dhidi yake kitu kilichopelekea kutupiliwa mbalo.

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya TFF, Wilson Ogunde amesema kuwa walikuja kukutana wakiwa na mashauri matatu ambapo shauri la kwanza na la pili limeweza kusikilizwa na mashahidi kupewa nafasi ya kujitetea lakini katika shauri la Jerry Muro tumeambiwa yupo ila amesema kuwa hataweza kuingia ndani kwa sababu barua haijamuelekeza ni wapi anatakiwa kwenda pia hakukuwa na uambatanisho wa mashtaka dhidi yake ila tumepewa taarifa kuwa ametumiwa na Email pia Julai 01 inawezekana akawa hajaisoma na kwa mamlaka kabisa tumejadiliana tumeamua kulirudisha suala hili kwenye sekretarieti ya TFF kama watahitaji kuendelea basi wamuandikie barua ya wito uliojitosheleza.

Amesema, Muro ana haki ya kujitetea na kuleta ushahidi wake na katika kusikiliza shauri lazima.upande wa mshtakiwa aridhike na mashtaka yake na kama kuna mapungufu anaweza kuomba kusogezwa mbele na katika hali ya kujitetea kwa upande wake amesema kuwa hawezi kuingia kwenye hiyo kamati kwani hakutambua kama anaitwa huko pili ajajiandaa kisaikolojia na hajaambatana na wakili wake.

Naye baada ya shauri dhidi yake kutupiliwa mbali, Muro amesema kuwa aliyeandika barua ile alikurupuka na zaidi kama angekubali kuingia kwenye kamati ile basi haki isingetendeka na zaidi wametuma taarifa ya kwanza ambayo ni Juni 29, wakatuma Email Julai 01 na hajaitumia kwa muda mrefu. Kwahiyo kama watanihitaji waandike shauri lingine sio kutaka kumfanyia mtu njama ilimradi asijihusishe na masuala ya mpira tena.

Hii mara ya tatu kwa Muro kuitwa ila mara zote amekuwa akishinda kesi hizo za maadili

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANYAKUA TUZO MBILI KATIKA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016 - SABASABA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akikabidhi tuzo mbili za ushindi ilizoshinda Wizara yake katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa viongozi wa Kamati ya Maonesho ya Wizara hiyo jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza katika kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa pili katika kundi la Mshindi wa Jumla wa Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyekuwa Mgeni Rasmi akiongozana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi la Mshindi wa Jumla.
Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia ushindi wa tuzo hizo. Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni moja ya mabanda yanayovutia zaidi katika Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2016, kwa kuwa na mchanganyiko wa mambo mbali mbali yanayoelimisha kuhusu uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Utalii. Katika banda hilo zipo pia fursa za kuwaona wanyama hai kama vile Simba, Nyati, Chui, Mamba, Ndege mbalimbali n.k. Kwa upande wa Utalii wa Ndani zipo fursa za kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ya Tsh. 10,000 kwa watoto na Tsh. 20,000 kwa watu Wazima ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi, Aidha kwa wale watakaopenda kulala itawagharimu Tsh. 50,000.
Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia tuzo hizo katika banda la Wizara hiyo.
Taswira ya tuzo hizo.(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii) 

CCM ZANZIBAR YAENDELEA KUFANYA UHAKIKI WA MALI ZAKE

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yanayomilikiwa na chama hicho kuhakikisha wanafunga mikataba rasmi ili kuepuka usumbufu wakati maeneo hayo yatakapohitajika kwa ajili ya shughuli za kichama.

Kimesema kuna baadhi ya wananchi waliopewa maeneo ya kuishi kwa muda kwa nia ya kuwasaidia na badala yake wameyageuza kuwa makaazi yao ya kudumu jambo ambalo sio sahihi.Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Vuai Ali Vuai kwa nyakati tofauti katika mwendelezo wa ziara ya kuhakiki mali na maeneo mbali mbali yanayomilikiwa na CCM huko Mbweni Mkoa wa Magharibi Kichama.

Alisema chama kinaendelea na zoezi la kuhakiki mali zake kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wanaotengeneza hati na mikataba bandia ya kujimilikisha mali za chama hicho kinyume na utaratibu.

Ndg. Vuai alifafanua kwamba katika hatua za kupunguza kero hizo chama kimeamua watu wote ambao wamepewa kibinadamu sehemu za kuishi ama kufanya biashara kwa muda katika maeneo yanayomilikiwa na CCM wafunge mikataba rasmi ili chama kiweze kunufaika na rasilimali zake.

“ Watu waliopewa kwa dharura sehemu za kuishi na kufanya biashara kama hatujawapa mikataba rasmi inayotambulikana kisheria, ambayo ni kielelezo cha kumtambulisha nani mmiliki halali wa maeneo hayo baadae inaweza kuwa fursa ya kufanya utapele na kusababisha usumbufu na lawama kwa chama. 

Tujaalie kwamba mtu anaishi katika kiwanja cha Chama bila mkataba wa kisheria na imetokea ameondoka au amehama watoto, ndugu na jamaa zake hawatokubali mali hizo zirudishwe kwa CCM na kitakachotokea hapo ni ugomvi na kupelekana mahakamani hali ambayo chama hakipo tayari kuona inatokea ”,. Alifafanua Vuai na kuongeza kuwa CCM haitokuwa tayari kuona mali zake zinatumiwa na watu wachache bila ya makubaliano ya kimaandishi ama mikataba ya kisheria.

Jumuiya Shia Wamkabidhi Madawati Rais Dk.Shein

$
0
0
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar .
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar.
[Picha na Ikulu.] 

HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA

$
0
0


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU



TAARIFA KWA UMMA

KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA





Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.


IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016

Msama awatahadharisha wauza CD Feki

$
0
0
KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewatahadharisha wanaouza kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini kuachana na mfumo huo kwa sababu kuanzia mwezi huu watawakamata wanaofanya biashara hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema wametoa siku 30 kwa wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo kabla hawajawashukia. “Tunatoa siku 30 kwa wanaofanyabiashara ya kazi feki za wasanii, hiyo biashara waachane nayo kwa sababu inapoteza pato la Taifa,” alisema Msama.

Msama alisema kwa kuanzia watapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mkoa kwa mkoa ili kusaka computer zinazotumika kuiba kazi za sanaa. Msama alisema ili kufanikisha kazi hiyo wanashirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo sambamba na Kampuni ya Msama Promotions ili kufanikisha zoezi hilo ambalo litakuwa ni la kusafisha tatizo hilo.

Aidha Msama alisema ili kukomesha zoezi hilo wakikuta kazi feki kwenye duka wanabeba mzigo mzima wa kazi za sanaa. Naye Inspekta Jenera wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu alisema jamii inatakiwa kutoa ushirikiano na Polisi katika jambo hilo ambalo linaumiza nguvu kazi ya Taifa.

IGP Mangu alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Polisi ili kazi ifanyike inavyotakiwa kwa lengo la maendeleo ya wasanii ambao wanasaka namna ya kuendeleza maisha yao.

SERENGETI BOYS YATINGA HATUA YA PILI,YAITUNGUA SHELI SHELI 6-0

$
0
0
KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’ kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-0 dhidi ya timu ya Shelisheli  na  Ushindi huo unaifanya Serengeti kuwa na jumla ya goli 9-0 baada ya kushinda mchezo wa awali uliopigwa katika uwanja wa Taifa na baada ya kushinda mchezo huo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika sasa Serengeti itavaana na timu ya Taifa ya Afrika Kusini mwezi ujao.

Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana lakini Serengeti ilionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku Timu hiyo ambayo ni wawakilishi pekee wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa ilipata goli lake la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa Ibrahim Abdallah baada ya golikipa kutema shuti lililopigwa na Asadi Ally.

Serengeti inapata goli la pili lililofungwa na Mohemmed Abdallah dakika ya 43 pale alipoachia shuti kali lililomshinda kipa wa wapinzani wao na kuzama wavuni. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika serengeti walikuwa kifua mbele kwa goli 2 huku wakionekana kuutawala vilivyo mchezo huo wa ugenini.

Kipindi cha pili kinaanza kwa Serengeti kuingia kwa kasi ambayo inazaa matunda dakika ya 50 pale Asad Juma anapoandika goli la 3 baada ya kupiga faulo inayotumbukia moja kwa moja wavuni.Wageni hao katika uwanja wa Stade Linite  wanapata goli la 4 kwa penati dakika ya 61 inayopigwa na Issa Makamba na Asad Juma anaandika bao la tano dakika ya 70 huku Yohana Mkomola akiandika goli la sita dakika ya 90

Kikosi cha Serengeti Boys
Ramadhani Kambwili
Israel Mwenda
Nickson Kibabage
Enrick Nkosi
Ally Msengi
Ally Ng'anzi
Mohameed Abdallah
Shaban Ada
Ibrahim Ally
Rashid Chambo
Asad Juma

Kikosi cha Shelisheli.
Gino Pusureuse
Juninno Mathiot
Stan Estner
Brandon Molle
Mathew Basset
Churtill Rose
Emmanuel Lesperance
Julius Joseph
Ryan Henriette
Aaron Havolock
Brandon Fanchette

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI DDI AKUTANA NA BALOZI WA CHINA ZANZIBAR

$
0
0
Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania Bwana Lu Youqing ameahidi kufanya jitihada za makusudi katika kufuatilia taratibu za Mikataba ya makubaliano kwa upande wa Nchi yake ili kuona kwamba miradi yote ya Zanzibar iliyopata ufadhili wa Nchi hiyo inaanza, inaendelea na kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Akizungumza na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea Ofisini kwake katika Jengo la SMZ Magogoni Jijiji Dar es salaam Balozi Lu Youqing aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, ukamilishaji wa ujenzi wa eneo la maegesho ya Ndege kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar pamoja na Mradi wa Kisasa wa mawasiliano kwenye ofisi zote za SMZ { E government }.

Balozi Lu Youqing. alisema zipo taratibu za ukamilishaji wa Miradi iliyoanzishwa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili ambayo imeonekana kuchelewa kiasi kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya China kwa Uongozi wa Benki ya Taifa ya China { Exim Bank }.
Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha kwa mazungumzo Ofisini kwake katika Jengo la SMZ Magogoni Jijiji Dar es salaam Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing.
Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing kati kati akielezea mikakati atakayoitekeleza katika kuratibu usimamizi wa miradi ya Zanzibar iliyopata ufadhili wa Nchi yake ya China.
Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing mara baada ya mazungumzo yao ya kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na China.Picha na – OMPR – ZNZ.


YALEE YALEEE:GARI LAHAMA NJIA NA KUMGONGA MUENDESHA BAISKELI

$
0
0
Pichani ni  Usafiri wa Baiskeli Ukiwa nyang'a nyang'a mara baada ya Muendesha Baiskeli hiyo 'hayupo pichani' kugongwa na Gari aina ya Fuso alipo kuwa akielekea Nyumbani kwake na kupelekea hali Mbaya kwa Upande wake na Kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa iliyopo Sumbawanga Mjini, Majerui hakuweza kutambulika kwa Majina na Mara baada ya Tukio hilo kutokea Dereva wa Gari aina ya Fuso lenye Nambari za usajiri (T 688 DDV) aliingia Mitini na kutelekeza Gari hilo Pembezoni mwa barabara ya Sumbawanga kuelekea Wilayani karambo Eneo la Sumbawanga Enyeji.
Baadhi ya shuhuda wa tukio hilo akijaribu kumuelezea mwenzake jinsi hali ilivyo kuwa.
Jeshi la Polisi lilifika Mapema na kufanya Uchunguzi zaidi ni kipi kilicho pelekea kutokea kwa Ajali hiyo ni Mara baada ya Majerui kuwahishwa Hospitali.
Namba ya Gari lililo fanya tukio hilo la Kumgonga Muendesha Baiskeli Eneo la Sumbawanga Enyeji Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa.
PICHA NA MR.PENGO MMG RUKWA.

PPF YAENDELEA KUNG'ARA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA

$
0
0
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sostenes Lyimo, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi  Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara, na wasaidizi wake wakati walipotembelea katika Banda la Maonesho la Mfuko huo kwenye Viwanja vya  Sabasaba jana. Picha na Mafoto Blog
Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janeth  Ezekiel,  akizungumza na mwananchi aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho katika Viwanja vya Sabasaba wakati akimwelekeza jambo kuhusu mafao ya Mfuko huo. 
 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele,  akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara (katikati) walipokuwa wakitembelea Banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Sabsaba.
 Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Saluna Aziz Ally (kulia) na Glory Maboya, wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao waliofika katika Banda la maonesho Sabasaba la mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio akihojiwa na Waandishi wa habari baada ya Mfuko wake kukabidhiwa Kikombe cha ushindi wa kwanza wa Kundi la Mifuko ya Hifadhi ya jamii na Makampuni ya Bima katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.



Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images