Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1276 | 1277 | (Page 1278) | 1279 | 1280 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0

  Na Mchambuzi wetu Geofrey Chambua.

  Jana ziliripotiwa taarifa kupitia BBC kwamba ndege za kivita za Israeli zimetekeleza msururu wa mashambulizi ya asubuhi mapema huko Gaza Likishambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas.

  Huenda ni vyema kuutumia wasaa huu kujuzana KWA KINA NA VINA kuhusu hali halisi ya Ukanda huu wa Gaza

  Ukanda wa Gaza (Strong City) ni eneo dogo kwenye mwabao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya mamlaka ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya 6 km na 14 km. Eneo lote halizidi 360 km². Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi milioni 1.4 na ni moja ya nchi zinazoongoza kwa msongamano duniani (the most crowded on earth)
  Kanda hili ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israel wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizokuwa Israel

  1. Gaza imezungukwa katika pande zake zote tatu na Israel ambao wameblock pande hizo zote tatu kwa kutumia jeshi lao la anga na jeshi la majini. Upande wa nne ni borderpoint ya Egypt ambapo jeshi la Misri pamoja na majeshi ya Israeli na lile la wasimamizi wa UN na walinda amani wamefunga njia hizo na yeyote haruhusiwi kutoka ama kuingia ndani ya Gaza.

  2. Gaza ni kama gereza kubwa sana ambapo huenda hata sisimizi hana ruhusa ya kuweza kutoka ama kuingia humo bila ruhusa ya Israel. Hii ni kwa sababu wanamgambo Wapalestina maarufu kama HAMAS ambao ndio wanaoongoza Serikali ya nchi hiyo, wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza kwenda Israel.
  3. Gaza haina kiwanja cha ndege, bandari wala hata japo kituo cha treni.

  4. Wakazi wa Gaza hawawezi kuondoka nchini mwao kwenda mahali popote kwa kuwa hawana passport . Pia kuna vituo vya ukaguzi vya Israeli kila mahali. Pili hakuna mtu yeyote toka nchi yeyote anayeweza kuingia Gaza pasipokuwa na kibali maalumu ama ruhusa toka kwa serikali ya Israel ambayo hata hivyo pia ni ngumu sana kuipata ruhusa hiyo. Hii pia inawahusu wanasiasa nguli duniani kuingia Gaza ni mbinde. Hata David Cameroon aliwahi kuifananisha Gaza na ‘Kambi ya Wafungwa’ (Prison Camp)

  5. Gaza ni sehemu ambayo kiujumla imetenganishwa mbali sana na sehemu kubwa ya nchi zingine za dunia hii haya yamefanywa na israel. Kila siku inayopita bidhaa zote zinazotumika kwa mahitaji ya watu wa Gaza ni lazima zipitie katika vituo vya ukaguzi vya Israeli. Hata maziwa,ngano,madawa na bidhaa zote hupitishwa kwanza katika check point za Israel. Israel hutoza kodi kwa bidhaa zote hizi zinazopita katika vituo vyao vya ukaguzi kwenda Gaza
  6. Umoja wa Mataifa UN umewasihi mara kadhaa serikali ya Israel kuondoa vizingiti hivyo na mamlaka yake ndani ya Gaza Israel imekuwa kama sikio la kufa haisikii. Zaidi ya maazimio 50 yamepitishwa na UN dhidi ya Israel lakini Israel hawajali wala kusikiliza.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Wanafunzi wa chuo Cha Uhasibu (TIA), jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo lililoko jingo la Wizara ya fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwenye jingo la wizara ya fedha viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016 ambako yanafanyika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Hapa waziri akipatiwa maelezo na Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari

  Afisa Kumbukumbu wa Mfuko Pensheni wa PSPF, Lupakisyo J. Mwaipungu (kushoto), akimsikiliza Mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo na kuamua kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS Julai 2, 2016

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba akisalimiana na baadhi ya  Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group, kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipokwenda kutoa msaada wa Baiskeli na Vyakula mbalimbali kituoni hapo.Kulia ni mkuu wa fedha Samson Katemi.
  Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya Woolworths nchini, Joehans Mgimba akiwa amempakia kwenye baiskeli kijana Majaliwa Anthony, ambaye ni miongoni mwa Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuonyesha jinsi watoto hao watakavyokuwa wanabebana wakati wa kwenda shule ili kuwahi masomo.kampuni hiyo ilitoa msaada wa baiskeri na vyakula mbalimbali kituoni hapo.
  Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaamwa wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Woolworths, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli na vyakula mbalimbali.  

  0 0

  Mkazi wa kitongoji cha Mkoani kilichopo Nyamagana jijini Mwanza,Shomari Almas ameibuka mshindi mwezi wa kitita cha shilingi milioni 20 kupitia promosheni ya ”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.

  Akiongea kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa ameibuka kuwa mshindi wa droo ya mwezi Shomari Almasi ambaye anajishughulisha na kilimo na ufugaji alisema kuwa ndoto yake ya kuboresha maisha yake imetimia.

  “Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii kwa kuwa wakati nashiriki sikujua kama nitaibuka na ushindi.Nikipatiwa fedha hizo nitaendeleza shughuli zangu za kilimo na ufugaji pia mipango yangu ya kuoa na kuazisha familia yangu itafanikiwa”.Alisema.

  Meneja Uhusiano  wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa promosheni hii ambayo inaendelea imeishawezesha wateja 61 wa Vodacom kujishindia vitita vya mamilioni ya fedha.Washindi 58 wamejinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja,washindi watatu wa mwezi wamejinyakulia shilingi milioni 5 kila mmoja.

  “Napenda kutoa wito kwa wateja wetu  na watanzania wote kwa ujumla ambao hawajajiunga na mtandao wetu waweze kujiunga na kuchangamkia promosheni hii kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/- na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na mwisho wa mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/= “Alisema

  Aliongeza kusema kuwa ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi  300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”.

  maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi.

  Kwa wateja ambao hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni hii alisema wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa kiasi cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila watakuwa wameingizwa kwa droo moja kwa moja.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya mwezi ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Shomari Almasi, mkazi wa Mwanza,aliibuka mshindi wa mwezi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- Wengine katika picha kushoto ni Ofisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe.
  Meneja Uendelezaji wa Masuala ya Kibiashara wa Vodacom Tanzania(Business continuity Management),Ajit Mistry (kushoto) na Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed (wa pili kushoto)wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiwaonyesha namba ya simu ya Shomari Almasi mkazi wa Mwanza aliyeibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- katika droo ya mwezi ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 61 wamepatikana kupitia promosheni hiyo.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

  0 0


  Familia ya Bwana William H. Shelukindo, inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Beatrice Matumbo Shelukindo (pichani) kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko Arusha. 

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street,Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha.

  Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha.
  Bwana ametoa. 
  Bwana ametwaa.
   Jina la Bwana na lihimidiwe.
  AMINA.


  0 0


  Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza Mpiganaji mwenzetu aliekuwa Mpiga picha wa Kampuni ya Azam Tv, Marehemu Omar Masoud aliefariki Dunia jana kwa ajali ya pikipiki aliyoipata eneo la Makongo Jijini Dar es salaam wakati akielekea kazini. Mazishi yamefanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Boko, jijini Dar.
  Marehemu Omar Masoud enzi za uhai wake.
  Ibada ya mazishi ya ndugu yetu Omar Masoud ikiendelea kwenye Makaburi ya Boko, Jijini Dar es salaam mchana huu.
  Waombolezaji.
  Waumini wa Kiislam wakiuswalia Mwili wa Marehemu kabla ya kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya Milele kwenye Makaburi ya Boko, Jijini Dar es salaam.

  Innalilahi wa inna ilaihi rajiun

  0 0

  Hatimae mdau mkazi wa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, amevuta rasmi jiko a.k.a mwandani wake baada ya kukaa vikao kwa muda mrefu na hatimae mambo yamejipa leo. hizi ni baadhi ya taswira mbalimbali za shamrashamra za harusi hiyo ya kukata na shoka kama uonavyo hapo juu katika taswira ikiwa ni bwana na bibi harusi wakiongoza msafara kwa kuimbiwa nyimbo kedekede za kuwapongeza wawili hao.PICHA ZOTE NA MR.PENGO - MMG RUKWA.
  Dereva wa Boda boda akiwawahisha Wasindikizaji maarufu kwa jina la Wasafisha njia huku shamra shamra zikiendelea..
  Mambo yamenoga barabarani.

  0 0

  Baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa , timu ya soka ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, imebakiza mitihani miwili kabla ya kuandika historia ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, imefahamika.

  Mtihani wa kwanza ni mchezo dhidi ya Afrika Kusini unaotarajiwa kufanyika ama Agosti 5, 6 au 7, 2016 ambako mechi ya kwanza itapigwa ugenini kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam, Tanzania wiki moja baada ya mchezo huo. Hivyo mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamzi Agosti 14, 2016 saa 9.00 alasiri.
  Mshindi wa jumla katika michezo hiyo, itacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville. Wakati Afrika Kusini imepitishwa moja kwa moja Namibia imepenya kwa kuiondoa Botswana licha ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wake uliofanyika jana Julai 2, 2016 huko Botswana.

  Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Namibia, Juni 24, mwaka huu wenyeji (Namibia) walishinda 1-0. Kwa msingi huo, Namibia imepenya kwa bao la ugenini ililolivuna katika mchezo wa jana. Bao la ugenini imefanya kuwa na mabao 3-2.
  Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime, ameangalia ratiba ya mlolongo huo na kusema “Ushindani utakuwa mkubwa, lakini mimi nimelenga kushinda michezo yote iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu kwenda Madagascar tu kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii niipeleke Kombe la Dunia.”

  Fainali za Kombe la Dunia, mwakani zitapigwa India ambako kama Serengeti Boys itafuzu kucheza fainali za Afrika na ikaingia nusu fainali kwa maana timu nne bora zote zitashiriki fainali hizo ambazo tayari Tanzania imejiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.
  “Timu hii nimeanza nayo zaidi ya mwaka mmoja. Sioni kama itakuwa kikwazo kuifanikisha kufika fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu atunyooshee mkono wake, nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu hii, lakini pia wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au kuchagua mtu anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote,” amesema Shime maarufu kama Mchawi Mweusi.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Na Selemani Semunyu - JWTZ

  KLABU ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi  wa Tanzania ya  Lugalo Jijini Dar es Salaam imeahidi  kuendeleza Uwanja na klabu hiyo na kuwa na mafanikio makubwa kimataifa ukilinganisha na klabu zingine za Golf  na kuwa kitovu cha Michezo na Uchumi  kutokana na uwekezaji katika Uwanja huo.

  Hayo yamesemwa  leo na Mwenyekiti Mpya wa klabu hiyo Brigedia Jenerali  Michael Luwongo wakati akikagua Uwanja wa Klabu hiyo ikiwa ni mara ya Kwanza tangu kuteuliwa na kushika nafasi hiyo Jijini Dar es Salaam.
  “Uwanja wa Klabu ya Golf ya Lugalo ndio uwanja wa Kwanza uliojengwa na Wazalendo hivyo tunataka kuhakikisha unakuwa na hadhi ya kimataifa na kuzalisha wachezaji watakaoletea taifa Ushindi” AlIsema Brigedia Jenerali Luwongo.

  Brigedia Jenerali Luwongo alisema uwekezaji wenye lengo la kuwa kitovu cha Michezo yote kwa kuwa viwanja bora licha ya kuendeleza michezo lakini inaweza kuwa kitovu cha kiuchumi kutokana na wageni na wazawa kutumia viwanja hivyo vitakavyokuwa na ubora wa Kimataifa.

  Mwenyekiti huyo alisema mbali na Uboreshaji Miundombinu  kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuhakikisha Mchezo wa golf unachezwa na watu wa rika zote lakini hasa vijana na Watoto ambao watakuwa tegemeo na hazina kubwa kwa Taifa.

  Alisema kumekuwa na dhana isiyosahihi kuwa mchezo wa golf ni kwa matajiri dhana ambayo ameipinga na kutaka watu wajitokeze katika Uwanja huo unaomilikiwa na JWTZ ambao gharama za uchezaji wake ni ndogo ukilinganisha na klabu zingine.

  “Uwanja ni wa Jeshi lakini sio kwamba Wanajeshi pekee ndio wa naruhusiwa kuja kucheza hata ukiangalia wanajeshi wanaotumia uwanja huo ni ndogo ukilinganisha na raia na wageni toka nje ya Nchi” Alisema  Mwenyekiti.

  Aidha alitoa Wito kwa Maofisa na Askari wa JWTZ kujitokeza kuwa wanachama katika Klabu hiyo lakjini pia kushiriki mchezo wa Golf.

  Kwa upande wake Msimamizi wa Miundombinu wa Klabu hiyo Kanali Mstaafu   Jackson Nsigaye amesema sasa wana viwanja 18 ambavyo ndio sahihi vya Golf toka Viwanja Tisa walivyokuwa navyo awali na muelekeo ni kuwa na Viwanja vya michezo mingine pia ili kiwe kituo cha michezo.

  Naye Meneja wa Uwanja huo Kanali Omary alisema mpaka sasa ndio uwanja pekee wenye mashindano mengi kuliko vilabu vyote na wataendeleza mafanikio hayo katika mwaka huu.

  Brigedia Jenerali Luwongo ameteuliwa kushika wadhifa huo  na  Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuziba nafasi  iliyoachwa wazi na Marehemu Brigedia Jenerali  Mstaafu Ernest Galinoma.

  0 0
  0 0

  Bwana Harusi, Richard Jeremiah Gwapulukwa (kushoto) wa Kasamwa mkoani Geita, amefunga ndoa na Happness Daniel Kulola (kulia) ambae ni binti wa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

  Ndoa imefungwa katika Kanisa hilo hii leo na Mchungaji Paul Thomas Bagaka ambae pia ni msajili wa ndoa Manispaa ya Ilemela. Hafla ya ndoa hiyo inafanyika katika Ukumbi wa New Sun City Hotel Jijini Mwanza.
  Na BMG
  Maharusi wakiingia Kanisani kwa ajili ya Kufunga ndoa leo mchana
  Maharusi wakiingia Kanisani kwa ajili ya Kufunga ndoa leo mchana
  Maharusi wakisalimia wakiwa na wapambe wao.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.Wilson Masilingi, kizungumza na Watanzania wa Jumuiya ya Kiislamu waishio Washington DC (TAMCO) mara baada ya Iftar ilioandaliwa rasmi na jumuiya hiyo Siku ya Jumamosi July 2, 2016 ndani ya ukumbi wa Lawndale Dr. Silver Spring, Maryland U.S

  0 0

  Bwana Philemon Anamwikira Ikaa Munuo,
  Anayeoneka Kwenye Picha Hapo juu anaitwa Philemon Anamwikira Ikaa Munuo, umri miaka (61) ametoweka kuuanzia siku ya juma tano tar.29.06.2016 Nyumbani kwake Bunju B Dsm, Tafadhali yeyote atakaemuona apige simu Police au Kwenye number zifuatazao..0713449666 (Rich) 0754226760 (Tumsifu) 0713552828(Rodrick) 0718555909 (lucas) 0713481648 (Tumaini)..Tafadhali sambaza ujumbe huu.

  0 0

  Wakufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea wa klabu bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East) ijulikanayo kwa jina la Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin ma Katy Morris wamesema kuwa Tanzania inaweza kupata sifa kubwa katika michezo duniani kupitia mchezo wa kuogelea.

  Wakufunzi hao walisema hayo katika semina inayoendelea ya mchezo huo kwa waogeleaji na makocha wa klabu marufu ya Dar Swim Club (DSC).Durkin alisema kuwa amefuraishwa na vipaji vya mchezo huo kutoka kwa waogeleaji wa DSC na anaamini kuwa siku moja, Tanzania itatoa bingwa wa dunia kupitia mchezo huo.

  “Nimefurahi kuona kuwa mchezo una mwamko sana na wachezaji wanaupenda, pia Tanzania ina makocha wazuri wenye elimu ya kutosha, naamini kama juhudi hizi zitaendelezwa, nchi itapata wawakilishi wazuri katika mashindano ya kimataifa na kuweza hata kutwaa ubingwa wa Dunia,” alisema Durkin ambaye ni raia wa Serbia.Alifafanua kuwa amefuraishwa na waogoeleaji chipukizi ambao umri wao ni chini ya miaka minne.

  “Nimevutiwa kuona hata Tanzania hasa klabu ya DSC ina waogeleaji watoto ambao wanaupenda mchezo, hii imenivutia sana, hapa utapata wachezaji ambao wataupendea mchezo kuanzia utotoni na huu ndiyo mwamko ambao utaleta matunda katika mchezo,” alisema.Kwa upande wake, Katy ambaye ni mwanadada alisema kuwa wadau wa mchezo huo wanatakiwa kusaidia kufikia malengo hayo kwani bila uwekezaji mkubwa, bado mchezo utakuwa chini kutokana na ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kisasa.

  Katy alisema kuwa DSC imeonyesha nia ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na kuomba wadau waunge mkoni. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni za Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom.
  Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro amesema kuwa lengo lao ni kuona Tanzania inafanya vizuri katika mchezo huo kimataifa. Alisema kuwa DSC imeamua kupambana katika kuleta maendeleo ya mchezo wa kuogelea hapa nchini.

  “Tunahitaji sapoti katika mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo makubwa kwa kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom kwa kutuunga mkono, gharama za kuwaleta walimu kutoka nje ni kubwa sana,” alisema Inviolata. 

  Mkufunzi klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji chipukizi jinsi gani ya kuanza kuogelea kwa staili ya backstroke.
  Waogeleaji chipukizi chini ya miaka minne wakishiriki katika mafunzo hayo kwa vitendo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya DIA yaliyoandaliwa na klabu ya Dar Swim Club chini ya ukufunzi kutoka klabu bingwa ya mchezo huo nchini Dubai, Hamilton Aquatics. 
  Mkufunzi wa klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji chipukizi jinsi gani ya kuelea ndani ya maji kwa staili ya backstroke.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na viongozi wa Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam wakati alipowasili msikitini hapo kushiriki katika fuatari Julai 3, 2016.  Kushoto  ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum na  kushoto kwa Waziri Mkuu  ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi wakishiriki  katika swala  kabla ya kufuturu kwenye Msikiti wa  Khona Shia Ithna-Asheri  wa jijini Dar es salaam  Julai 3, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alipozungumza katika futari iliyoandaliwa katika  Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Wanne kushoto ni  ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukakary Zubery bin Ally  na watano kushoto ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri,  Azim Dewji.
   Mwenyekiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri,  Azim Dewji akizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
  Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri  jijini Dar es salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza Julai 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0
 • 07/04/16--02:21: TANGAZO LA KIFO

 • Marehemu Mr. Amani Mshana  (1982 – 2016)
  Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Misungwi Bwana Nathan Mshana anasikitika kutangaza kifo cha mototo wake AMANI MSHANA, kilichotokea jumapili tarehe 03/7/2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza.

  Habari ziwafikie wafanyakazi wote wa Halimashauri ya Wilaya ya Kongwa, ndugu, jamaa na marafiki wote popote pale walipo.

  Mazishi yatafanyika jumatano tarehe 6/7/2016 huko Vudee Msanga, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

  0 0

  Baadhia wakina Mama Wajasiliamali wafanyao Biashara zao kandokando ya Barabara ya kuelekea Bandari ya Kasanga kutokea Sumbawanga Mjini wakiwa katika Eneo lao la Biashara kama ambavyo waonekanavyo hapo juu katika Taswira.
  Wakina Baba nao wakiwa Sambamba na Vipandwa vyao katika Pilika Pilika zao za kila Siku kando kando ya Barabara ya kutokea Sumbawanga Mjini kuelekea Bandari ya Kasanga Wilayani Karambo Mkoani Rukwa.
  Mwanaume wa Shoka akijikongoja kandokando ya Barabara hiyoo.
  Gari hii Pichani ikiwa katika matengenezo mara baada ya kupata Hitirafu katikati ya Barabara hiyo..
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG.

  0 0

  Jina: Philbart Patrick Gwagilo
  Umri miaka kwa sasa 29 alipotea akiwa na umri wa miaka 27.
  Kabila: Muha
  Dini: Mkristo
  Mkoa alipozaliwa: Kigoma Wilaya ya Kasuru.
  Maeneo anayopenda kutembelea: Sinza, Kibamba na Arusha.

  Alikuwa anafanya kazi ya uwakili wa kujitegemea katika kampuni ya Declam jijini Dar es Salaam.

  Mtajwa hapo juu anatafutwa na ndugu zake. Kwa mara ya mwisho alikuwa anaishi Sinza Lion jijini Dar es Salaam ilikuwa siku ya Jumamosi Machi 28, 2015.

  Wajihi (Rangi yake ni Mweusi) mrefu kiasi na mnene kiasi.
   Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-

  Peter P. Gwagilo: 0784390904
  Paul P.Gwagilo: 0659649891
  Yohanes  P.Gwagilo: 0714514103

older | 1 | .... | 1276 | 1277 | (Page 1278) | 1279 | 1280 | .... | 3284 | newer