Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1273 | 1274 | (Page 1275) | 1276 | 1277 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na mke wa tajiri namba moja duniani na mwenyekiti mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Melinda Gates kwa pamoja wamelipongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kwa kufanya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kama moja ya mbinu za kumkomboa mwanamke mnyonge kiuchumi.

  Wawili hao waliyasema hayo kwenye mdahalo uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika bustani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo walikuwa wageni waalikwa waliopata fursa ya kuzungumzia jinsi ya kumuwezesha kiuchumi mwanamke mzalishaji na namna ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Akizungumza kwenye mdahalo huo, Melinda Gates alisema kuwa yeye kupitia Bill and Melinda Gates Foundation wamelenga kusaidia nchi nyingi hasa za ukanda wa Afrika Mashariki kama Tanzania katika kubadilisha maisha yao kwa kutengeneza fursa za ajira na kuwasaidia vitendea kazi.

  Aliongeza kuwa kwa nchi kama ya Tanzania ambayo asilimia 25 ya mapato yake yanatokana na kilimo, taasisi yao imejikita katika kuwawezesha wakulima wadogowadogo ambao hata hivyo huwezi kuwaacha wakina mama kwa kuwa ndiyo wanaotoa mchango mkubwa kwenye sekta hiyo.

  Akizungumzia kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Melinda Gates alitoa pongezi zake za dhati kwa shirika la Oxfam na kuongeza kuwa, ikiwa nchi za Kiafrika hususan Tanzania itataka kupiga hatua lazima iwawezeshe kiuchumi wanawake kwa kuwa wao ndiyo wenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na hilo ndiyo jambo muhimu zaidi. 


  Naye Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye mdahalo huo alisema kuwa; kwa kipindi kirefu amekuwa mfuatiliaji wa mashindano hayo na kuahidi kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni kuongeza vipaumbele kwa mwanamke kwa kutoa mianya kwa taasisi zinazomsaidia mwanamke ikiwemo shirika la Oxfam kupitia shughuli zake hasas shindano la mama shujaa wa chakula. “Nikiri tu kuwa nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa shindano hili tangu zamani, naahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwenu kwa kila jambo kwa kuwa mnaisaidia sana serikali,” alisema Ummy.

  Aidha mdahalo huo pia ulioongozwa na mwanaharakati, Maria Sarungi Tsehai ulihudhuriwa na wanaharakati wengine wa masuala ya jinsia akiwemo Mkurugenzi wa Msichana Initative, Rebecca Gyumi, Mwanaharakati wa Mtandao wa Masuala ya Kijinsia, Marjorie Mbilinyi, Mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Issa na Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2011, Anna Oloishuro.

  Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
  Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
  Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
  Mshereheshaji katika Hafla hiyo Maria Sarungi Tsehai akiendelea kutoa muongozo.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea  katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, pamoja na ziara rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini leo  asubuhi.

  Wakati mazungumzo yakiendelea.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (kulia)  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo baada ya mazungumzo yao. Kushoto ni balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Ureno imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Poland kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 baada kumaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1.

  Mpambano ulianza kwa kasi sana, mpira mrefu uliopigwa na beki wa kulia wa Poland Piszczek unamfikia Maczynski wingi ya kushoto naye bila ajizi anampelekea Lewandowski ambaye bila ajizi anaukwamisha mpira huo kimiani, hii ni dakika ya pili tu ya mchezo.
  Baada ya hapo mashambulizi yanakuwa kwa pande zote mbili lakini kunako dakika ya 32 pasi safi ya kisigino toka kwa Nani inamkuta Renarto anayefunga kwa shuti kali la mguu wa kushoto na kuipatia Ureno bao la kusawazisha.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika bao lilikuwa 1-1.

  Dakika 45 za kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya timu zote kushambuliana kwa zamu huku Ronaldo kwa upande wa Ureno na Lewandowski kwa upande wa Poland wakionesha umahiri wao ila bahati haikuwa yao kwani walikosa magoli mengi.
  Muda wa nyongeza (extra time) zilikwisha kama zilivyomalizika dakika 90,hivyo ikabidi mshindi apatikane kwa miguu 12 ya mtu mzima yaani mikwaju ya penati, ndipo Ronaldo,Renarto,Moutinho,Nani na Quaresma walipoifungia Ureno penati zote 5 na Lewandowski,Milk na Glik wakipata kwa upande wa Poland,aliyekosa ni Blaszczykowski.

  Ni wazi kuwa Ureno atamsubiri mshindi kati ya Wales na Ubelgiji katika mtanange wa nusu fainali siku ya jumatano tarehe 6/7/2016.

  0 0

  Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yafanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa majukumu ya kazi za Mamlaka.
    Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
   Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe wakiangalia utendaji kazi wa studio ya kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku unaosambazwa kwenye vyombo vya mbalimbali vya habari. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.

  0 0

  Na: Lilian Lundo-MAELEZO Dodoma.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri zote Nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato kuanzia Julai 01, 2016.

  Majaliwa aliyasema hayo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja Juni 30, 2016.
  “Napenda kutumia fursa hii kuziagiza Halmashauri zote Nchini kwamba kuanzia tarehe Mosi Julai, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kieletroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboreshha makusanyo,” alifafanua Mhe. Majaliwa

  Aidha Majaliwa amezitaka Halmashauri hizo kutoelekeza vyanzo vyote vya mapato kukusanywa na mawakala kwani vipo vyanzo ambavyo vinaweza kukusanywa kwa ufanisi na Halmashauri zenyewe bila kutegemea mawakala.

  Aliendelea kusema kuwa, Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia mawakala na vingine vitakusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali.

  Majaliwa aliitaja miongozo hiyo kuwa ni pamoja na Halmashahuri aidha kwa kutumia mawakala  au Halmashauri zenyewe kuweka kwenye akaunti ya Halmashauri  fedha zote zinazokunywa kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza na kumaliza kabisa masuala ya (cash transactions).

  Vile vile Halmashauri zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

  Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa sura 290, inazipa uwezo mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua Mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za  Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.

  0 0

  Bi Julieth Mwasi kushoto akimvisha pete ya ndoa mumewe Bwana Pius Mateso Ndimbo wakati wa ibada yao ya ndoa iliyofanyika katika kanisa la Mt Alois Gonzaga Mjini Mbinga mkoani Ruvuma.
  Maharusi Pius Mateso na Julieth Mwasi katikati wakiwa na wasimamizi wao katika kanisa la Mt Alois Gonzaga wakati wa ibada yao ya ndoa iliyofanyika mjini Mbinga. 
  Maharusi Bwana Pius Mateso Ndimbo na mkewe Julieth Mwasi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mt Alois Gonzaga Parokia ya Mbinga , na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Uvikambi Mbinga mjini mkoani Ruvuma.

  Picha zote na Muhidin Amri

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman (kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya makamo wa Pili wa Rais Joseph Abdalla Meza(kulia)  wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika  kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika  kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  MWAMUZI msaidizi kutoka Tanzania mwenye beji ya Shirikisho la Soka duniani FIFA, Frank Komba amehitimu mafunzo yake ya sheria na kuapishwa kuwa wakili wa kujitegemea na Jaji Mkuu Othman Chande leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam. 

  Komba ambaye ni mwamuzi wa kimataifa anaingia kwenye mlolongo wa wana michezo waliosomea sheria ambapo kwa anaamini hatua hii aliyofikia atatitumikia vizuri pia itamsaidia hasa katika kushughulikia vizuri masuala ya mpira pamoja na mambo mengine.

  Akizungumza baada ya kuapishwa, Komba amesema kuwa ametimiza moja ya malengo yake lakini zaidi bado anahitaji kuendelea mbali na hapa halipo ila msingi mkubwa ni kuhakikisha anatendea haki hiki alichokipata kwa sasa. "Nina imani kutokana na kazi yangu nitaitumia vyema nafasi hii niliyokuwa nayo pia bado ninahitaji kuendelea mbele zaidi ya hapa,".

  Komba amehitimu shahada yake ya uwakili mbali na hilo ni moja ya waamuzi wanaotegemewa na FIFA hapa nchini na ameshachezesha mechi mbalimbali za kimataifa na zaidi atasaidia kuinua mpira pamoja na kutumia nafasi yake kutoa ushauri kwa vyama vya michezo.

  "Nitatumia nafasi yangu kutoa ushauri kwa vyama vya mpira na hata klabu pia kwani kumekuwa na sintofahami nyingi sana katika sheria za mpira,"amesema Komba.

  0 0
 • 07/01/16--02:44: Article 16

 • 0 0
 • 07/01/16--02:47: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Viongozi wapya wa TUGHE tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uchaguzi.

  ABBAS Rweyumamu amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE), tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

  Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE mkoa wa Dar es Salaam, Gaudence Kadyango , ulishirikisha wanachama 36 kutoka idara mbalimbali, ambapo Rweyumamu alishinda kwa kura 18, akimshinda Teobald Benignus aliyepata kura 17.

  Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda kwa Thawabu Njeni aliyemshinda Simon Mbogo baada ya kutumika utaratibu wa kura ya veto, kwa majina yao kuandika kwenye karatasi na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa JNIA, Efatha Lyimo kuokota lililoandikwa jina lake, baada ya kufungana mara mbili na mpinzani wake kwa kura 18.

  Wajumbe wote nane waliogombea na kupitishwa bila kupingwa ni Tobald Benignus, Simon Mbogo, Rehema Ambali, Hussein Msuya, Sadik Milulu, Philbery Lyimo, Mwanaheri Omari na Adventina Rugimbirwa. 

  Uwakilishi wa vijana umekwenda kwa Mwanaisha Athuman aliyepata kura 20, na kumshinda Lydia Mwenisongole aliyepata kura 10; huku nafasi ya uwakilishi wa walemavu umekwenda kwa Baltazar Kidiga.

  Kwa upande wa kamati ya wanawake Uenyekiti umekwenda kwa Sumayi Ngasani, wakati Mweka hazina kachaguliwa Stumai Mbato na mjumbe ni Mastidia Ndyomlwango.

   Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya wanawake ni Justa Emmanuel na Joyce Chisongela.

  Naye mwakilishi wa DNIA, Lyimo mbali na kuupongeza uongozi huo, ameutaka kutenda haki na wasiende kuwa mgombanishi kati ya muajiri na muajiriwa, ila walete ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

  Lyimo pia aliwataka viongozi hao kuweka wazi mapato na matumizi kwa wanachama wake, ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima, na pia waangalie sababu za wanachama wengi kujiengua kwenye chama hicho.
  IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA MAHUSIANO TAA.

  0 0

  Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akijibu maswali mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
    Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti) akiwasikiliza waandishi wa habari wakati wa mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba pamoja na viongozi wengine.
  Mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle umefanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya teknolojia walikutana na kujadili matumizi salama ya mtandao. 

   Mambo makuu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba, ni usalama katika matumizi ya mitandao ya teknojia, Usimamizi wa utunzaji wa data na taarifa za siri na jinsi ya kukabiliana na hasara zinazotokana na matumizi mabaya ya mtandao yenye kuleta athari kwa watumiaji. 

   Imeeleza katika mkutano huo kuwa kila mwaka mabilioni ya dola hutumiwa na taasisi mbalimbali kujiweka salama na athari za kimtandao ambapo hata hivyo imeelezwa kuwa wezi wanaojinufaisha kupitia teknolojia kila kukicha wanabuni mbinu mpya za kufanya uharifu kupitia katika mitandao ikiwemo kuiba taarifa za siri kutoka kwenye makampuni na taasisi.

   Taarifa zimebainisha kuwa hivi karibuni wizi wa kimtandao uliosababisha hasara ya dola za Kimarekani bilioni 300 umefanyika na kiasi cha dola bilioni100 umefanyika kupitia kadi maalumu za mihamala ya fedha na malipo, bara la Afrika likiwa moja ya wahanga wa wezi huu wa kimataifa.

   Ripoti ya mwaka huu kutoka taasisi za Verizon kuhusiana na wizi wa kimtandao imebainisha kuwa kuwa wizi wa siri za makampuni ni wa pili kufanyika baada ya wizi wa fedha japo makampuni mengi hayajawa na mwamko wa kuwekeza katika kupambana na tatizo hili kubwa ambalo hivi sasa ni janga la kimataifa.
   Makamu Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklicki amesema kuwa mikakati ya kuzuia wizi huu kuliko athari zinazojitokeza baada ya kuingiliwa katika mtandao na kuibiwa taarifa za siri za kampuni.

   Alisema wizi huu wa kimtandao ni moja ya changamoto inayozikabili taasisi mbalimbali na makampuni ya biashara na ndio mwanzo wa kutengenezwa bidhaa bandia kwenye masoko na alisisitiza kuwa utunzaji wa taarifa za siri ni jambo la kwanza la msingi kwa kampuni Mkutano huo ambao umedhaminiwa za taasisi za Oracle na CIO Afrika na kuhudhuriwa na watendaji kutoka serikali na taasisi mbalimbali umetoka na maazimio ya kuhakikisha uwekezaji wa kiteknolojia unafanyika katika kuhakikisha wizi huu wa kimtandao unadhibitiwa na makampuni kuwa makini kuhakikisha yanalinda taarifa zake za siri.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu ya Dodoma Julai 1, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu ya Dodoma Julai 1, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uledi  Mussa. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

    MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kushoto akimkabidhi zana za kufanyia kazi mkuu wa wilaya ya Kibiti Gulamu Kifu, baada ya kumwapisha kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa.
   Mkuu mpya wa wilaya ya Kibaha Asumpter Mshama kulia akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kushoto wakati wa hafla iliyofanyika mjini Kibaha ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo ambao waliteuliwa hivi karibuni na Rais Dk John Magufuli
  Mkuu mpya wa wilaya Rufiji Juma Njwayo kulia akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo wakati wakiapishwa wakuu wa wilaya za mkoa huo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa huo iliyopo mjini Kibaha.

  Na John Gagarini, Kibaha.
  MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wakuu wapya wa wilaya wlioteuliwa na Rais Dk John Magufuli mkoani humo kuinua pato la wananchi wa mkoa huo kutoka milioni 1.2 kwa mwaka hadi milioni 3 kwa mwaka.

  Ameyasema hayo leo mjini Kibaha wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya wapya na kusema kuwa pato la mwananchi wa mkoa wa Pwani liko chini sana licha ya kuwa na fursa mbalimbali za kipato.

  Ndikilo amesema kuwa kutoakana na pato hilo la wananchi kuwa dogo kiasi hicho hata mchango wa mkoa kwa Pato la Taifa ni dogo sana la asilimia 1.8 jambo ambalo linapaswa kuwekewa mkakati wa kupandisha pato hilo ili liwe na mchango mkubwa kwa mwananchi na Taifa kwa ujumla.

  “Nawapongezeni kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hizi na mkoa tayari umeandaa mpango kazi wake kwa ajili ya kuinua pato la mwananchi hivyo mnapaswa kuweka vipaumbele ambavyo vitasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya unayoongoza,” alisema Ndikilo.

  Amesema kuwa hakuna sababu ya mkoa kuendelea kuwa na pato dogo huku kukiwa na vyanzo vingi vya mapato ikiwa ni pamoja na rasilimali mbalimbali kama vile uvuvi, kilimo, korosho, maliasili ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama na madini mbalimbali.

  “Mfano ni majumba mengi yanayojengwa Dar es Salaam kokoto na mawe yanatoka mkoa wa Pwani hivyo hakuna sababu ya kuwa maskini tuna zao la korosho ambapo kwa msimu uliopita wakulima waliuza korosho zenye tahamani ya shilingi bilioni 18,” alisema Ndikilo.

  Amewataka wahakikisha wanawajibika na kutowalea watumishi ambao ni kikwazo na wenye urasimu wa kuwahudumia wananchi ambao hufika ngazi ya mkoa kulalamika ili hali ngazi za chini kuna watendaji ambao wangeweza kutatua matatizo hayo.

  “Changamoto ni nyingi ikiwa ni pamoja na suala la ulinzi na usalama, wahamiaji haramu, matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi nisingependa mambo haya yatokee tena hakikisheni mnatimiza wajibu wenu na kuwaondolea kero wananchi,” alisema Ndikilo.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kuwa moja ya changamoto ambazo atakabiliana nazo ni pamoja na wahamiaji haramu kw akudhibiti bandari 19 ambazo zimekuwa ni njia ya wahamiaji hao haramu.

  Naye Asumpter Mshama amesema kuwa moja ya mambo atayapaa kipaumbele ni kuhakikisha fedha kwa makundi ya vijana na akinamama asilimia 10 zinatoka ili wananchi waweze kujenga uchumi wao na ule wa Taifa.

  Wakuu wapya walioapishwa jana ni pamoja na Shaibu Nunduma wilaya ya Mafia, Filberto Sanga Mkuranga, Gulamu Kifu wilaya ya Kibiti, Asumpter Mshama wilaya ya Kibaha, Juma Njwayo wilaya ya Rufiji na Majid Mwanga wilaya ya Bagamoyo huku Happyness William hakuweza kuapishwa kutokana na dharura.

  0 0

  Kufuatia kutimiza agizo la uzimaji wa simu bandia, kutokana na agizo elekezi la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inapenda kuwajulisha wateja wake walio nunua simu orijino kutoka kwa watoa huduma ndani ya maduka yetu ya Airtel, endapo baadhi ya wateja simu zao zitazima kutokana na agizo hilo. 

  Airtel inawatangazia wateja wote watakaoathirika na zoezi hili kutembelea maduka yetu nchi nzima kwaajili ya kuhudumiwa/kurekebishiwa simu zao wakiwa na simu husika pamoja na risiti za manunuzi ya simu hizo.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na zoezi hili.

  Imetolewa na Idara ya mawasiliano 
  Airtel Tanzania

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  KLABU ya Simba imemtambulisha kocha mpya leo na kuingia nae kandarasi ya miaka miwili 2016/2018 huku wakimpa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi. Raisi wa Simba Evance Aveva amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kupitia sifa za Joseph Omog na kuona atakuwa msaada mkubwa sana katika kuisaidia timi ya Simba.

  Akizungumza wakati wa utambulisho wa kocha huyo, Aveva amesema huu ni mwanzo mzuri kwa Simba wana imani ana nafasi kubwa ya kuwasaidia katika namna watakavyobadilisha na kupata mafanikio kwa timu hiyo. " Ni mategemeo yetu kuwa kandarasi hii tuliyoingia na Omog itakuwa na mafanikio na malengo makubwa ya Simba ni kuitoa ilipo na kuirudisha kuwa ya zamani, ". Naye Omog amesema kuwa amekuja Simba kwa ajili ya kuisaidia na kuijenga na atafanya kazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa.

  Wakati huo huo Aveva alimtambulisha katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele ambaye kuanzia sasa atahusika na masuala ya klabu hiyo na zaidi kwa kipindi kirefu hakukuwa na mtendaji mkuu ambaye anakuwa anashughulikia suala la utendaji kiujumla. 

  Kahemele amesema kuwa, Simba kuna changamoto kubwa sana na malengo yake ni kuitoa ilipo na kuirudisha ilipokiwa zamani na amewahakikishia wanachama wa Simba wote kuwa atashirkiana vizuri na kamati ya utendaji katika kulitekeleza hilo na ndiyo maana hata viongz walimfuata ili waweze kusaidiana. "Nawaahidi kufanya kaz usiku na mchana na katika.msimu unaoanza nitahakikisha tunakwenda kwa kasi na zaidi wameleta kocha mzuri anayejua majukumu yake na mimi nitajibika kulingana na nafasi yangu,".

  Kahemele amesema Simba wana mtaji mzuri wa wanachama na watatumia nafasi hiyo kuwa faida kwao kwani wanaweza kufanya mambo mengi kwa fedha za wanachama hao hao.
  Rais wa klabu ya Simba,Evans Aveva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuwatambulisha katibu mkuu mpya wa klabu ya Simba bwana Patrick Kahemele (mwisho kushoto) na kocha mkuu mpya Joseph Omog (pichani kati) ambae ni raia wa Cameroon.Kocha Omog aliwasili jana usiku hapa jijini..
  Pichani wa tatu kulia ni Katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele akifafanua jambi na kwamba kuanzia sasa ndiye atakaehusika na masuala ya klabu hiyo,kwani kwa kipindi kirefu timu hiyo haikuwa na Mtendaji Mkuu ambaye amekuwa akishugulikia masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa ujumla. 
  Kocha Mkuu mpya Joseph Omog,ambae ni raia wa Cameroon akifafanua jambo mbele ya wana habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini  humo .Picha na Michuzi Jr.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki na mameneja wa vyuo na shule binafsi Tanzania (TAMONGSCO) Mrinde Mzanva akiongea na wamiliki na mameneja wa vyuo na shule binafsi kanda ya Dodoma na kuishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kuwa tayari kusaidia chama hicho katika kuhakikisha wanachangia katika ukuaji wa sekta ya elimu nchini.Kushoto Mwekahazina Taifa wa Chama hicho Bw.Yona Mapenzi na Kulia Mwenyekiti wa Chama hicho kanda ya Dodoma Bw.Revocatus Majuto
  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiongea na wanachama wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (TAMONGSCO) katika kanda ya Dodoma na kuwataka kuendelea kuwa karibu na Mamlaka hiyo hasa pale wanapohitaji misaada na mikopo kwa ajili ya kuendeleza shule na vyuo vyao ili kuweza kusaidiana na serikali katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu nchini.
  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (TAMONGSCO) kanda ya Dodoma Leo Mjini Dodoma.

  0 0


  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) akiwapungia wananchi wakati alipomkaribisha Mke wa Rais wa Rwanda Mama Janeth Kagame katika Ofisi zake wakati wa Ziara ya Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini .
  Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisikiliza kwa makini shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati alipotembelea ofisi hizo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiagana na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe - Maelezo

  0 0


older | 1 | .... | 1273 | 1274 | (Page 1275) | 1276 | 1277 | .... | 3348 | newer