Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

NEWS UPDATES: Lissu aachiwa kwa dhamana

0
0
 Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam

Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum Mohammed.

Kongola alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alinukuu maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia  ndani ya giza nene"

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.

Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo, Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.

Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milini 2.

alitimiza masharti atasomewa maelezo ya awali Agosti 2,2016.

DIASPORA WAHIMIZWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI

0
0
TANGAZO KWA WATANZANIA WOTE NA WALE WANAOISHI NJE YA NCHI (DIASPORA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea na jitihada zake za kuhamasisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya nchi yao. Ili kufanikisha hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikizishawishi taasisi mbalimbali hapa nchini kutoa huduma na fursa za biashara na uwekezaji, ambazo zitasaidia Diaspora kuwekeza kiurahisi hapa nchini. Juhudi hizi ambazo zilianza tokea Serikali ya Awamu ya Nne zimeanza kutoa matunda makubwa ambapo thamani ya uwekezaji kutoka kwa Diaspora inaongezeka kila kukicha.

Kutokana na umuhimu wa Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi na huduma nyingine za kijamii; Serikali inapenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha Watanzania wote wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) umuhimu wa kuheshimu na kutii sheria na taratibu katika nchi wanazoishi. Aidha, Serikali pia inapenda kuwakumbusha tena Watanzania wote wenye nia ya kusafiri nje ya nchi kwa lengo la kupata ajira au kutafuta maisha bora (greenpastures), kuhakikisha kuwa mikataba ya ajira inatambulika na mamlaka za nchi husika. Sambamba na hilo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi za Balozi za Tanzania nje ya nchi zitaendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatua matatizo ya namna hiyo kwa Watanzania; pamoja na Taasisi za Serikali kama vile Wakala wa Ajira Tanzania (TAESA). 


Serikali pia inawakumbusha Watanzania wanaotaka kusafiri nje ya nchi kwa malengo mbalimbali kama vile masomo, biashara, makazi au masuala yoyote binafsi nao kuheshimu sheria na taratibu za nchi husika. Taratibu hizo ni pamoja na:

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar apokea Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu nchini

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akipokea Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu, kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Abdullatif Kadir Mussa iliyomalizika mapema mwezi huu. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho hilo ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Zanzibar Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Nd. Idrissa Kitwana na Katibu Mkuu wa Zahilfe Nd. Juma Omar Ali.
Balozi Seif akiuahidi Uongozi wa Zahilfe kuunga mkono katika kufanikisha malengo yao ya Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud akimpongeza Balozi Seif kwa kusaidia kufanikisha Tamasha la Shirikisho hilo. Picha na – OMPR –ZNZ.

Uongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE }umepata mualiko wa kushiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya Amani ya Dunia unaotarajiwa kufanyika Nchini Benin iliyoko Magharibi mwa Bara la Afrika.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Ndugu Juma Omar Ali akiuongoza ujumbe wa Viongozi wa Shirikisho hilo  alieleza hayo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho hilo iliyomalizika mapema mwezi huu.

Nd. Juma Omar alisema ushiriki wa Viongozi hao katika Mkutano huo wa Kimataifa utaoanza Tarehe 24 hadi 27 Mwezi Agosti mwaka huu utafungua njia kwa wanachama wa shirikisho hilo kupata uzoefu kupitia taasisi nyengine za Elimu ya juu Duniani.

Alisema mpango wa baadaye wa Shirikisho hilo katika kujiimarisha kiajira sambamba na kusaidia Vijana wanaomaliza masomo yao umelenga kutafuta fursa za Taaluma katika sekta ya Uvuvi ili iwafungulie njia ya kuanzisha vikundi vya ujasiri amali.

Alisema Visiwa vya Zanzibar vimebarikiwa kuzunguukwa na Rasilmali ya Bahari ambayo kwa karne nyingi zilizopita bado haijutumiwa ipasavyo tokea kuumbwa kweka ambayo inaweza kutoa mchango wa ajira kwa kundi kubwa la vijana sambamba na kuongeza mapato ya Taifa.

Akizungumzia Tamasha la mwaka huu la Michezo ya Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Nd. Juma alieleza kwamba michezo hiyo ilikuwa ya aina yake kiasi kwamba washiriki wake waliweza kutoa burdani safi iliyoshamiri ndani ya Mji wa Zanzibar.

Alifahamisha kwamba maandalizi ya Timu za Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kitaifa ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Tanzania nay ale ya Kimataifa yameanza rasmi ili kuwapa muda mrefu zaidi Vijana hao wa kufanya vyema kwenye kinyang’anyiro kinachowakabili.

Nd. Juma alielezea furaha yake kutokana na Uongozi wa Mashindano ya Kitaifa   Tanzania kuiamulia Zanzibar kupeleka Timu Nne za Mpira wa Soka na Timu 3 za Mpira wa wavu kwenye  Mashindano hayo ya Taifa ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania.

Akipokea Ripoti hiyo ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHILFE } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaunga mkono shirikisho hilo kutokana na nia yao nzuri ya kuanza na michezo na baadaye nguvu zao kuzielekeza katika uchumi.

Balozi Seif aliuhakikishia Uongozi wa Shirikisho hilo kwamba atafanya juhudi za ziara wakati atapokutana na Uongozi wa Balozi wa China Nchini Tanzania kuomba fursa za masomo ya fani ya Uvuvi kwa vijana hao kwa lengo la kuunga mkono mawazo yao ya kutumia fursa za ajira katika sekta hiyo.

Alisema ziara za mafunzo ya uvuvi ndani na nje ya nchi ni muhimu kwa vile yatafungua milango ya fursa za ajira kwa kundi kubwa la wasomi wanaomaliza masomo yao ya sekondari badala ya kukaa wakisubiri ajira za Serikali ambazo ni finyu kwa wakati huu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHLIFE } kuendeleza michezo kwa vile inaleta upendo, urafiki, mshikamano na hata ajira kwa Vijana.

Mapema Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud alimpongeza Balozi Seif licha ya kuwa mgeni katika ufungaji wa Tamasha hilo lakini pia alisaidia kuona Tamasha hilo linaanza na kumalizika kwa mafanikio.

Mh. Ayoub alisema mchango wa Balozi Seifm kwa Shirikisho hilo umekuwa Dira na matumaini mapana kwa wana Shirkisho hilo katika hatua ya mtyazamo wa baadaye wa Taasisi hiyo iliyokusanya wasomi wa elimu ya Juu.

TANZANIA AT THE CENTER OF THE AFRICA ENERGY FORUM IN LONDON

0
0
By Ayoub Mzee-London
The critical role of acces to enrgy and power in economic growth is perhaps one of the few core elements of economic development that all economists can agree upon.There are few resources that can benefit the public as a broadly and as effectively as access to power .From Schools to hospitals and homes to offices,the existence of plentiful,affordable and reliable power is the cornerstone of growth in Africa

MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS),JOSEPH MASIKITIKO ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI.

0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Joseph Masikitiko.

KUTOKA BUNGENI: Hatma Ya Vazi La Khanga Kwa Mwanamke Wa Kitanzania

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma lamtia mbaroni Mtu kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria

0
0
Na Abel Daud, Kigoma.

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limemkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamisi Kabateye muha mwenye umri wa miaka 35 na mkazi wa kijiji cha Kitahana Wilaya ya Kibondo kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya SMG yenye namba za usajili 1161293 na magazini 01 yenye risasi 23.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui, amesema kuwa mtuhumiwa alikutwa kilabuni akitumia pombe za kienyeji baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema, ndipo mtuhumiwa alipo hojiwa na asikari na kukiri ambapo alionyesha magazini nyingine ikiwa na risasi 28 iliyo fanya kupatikana kwa risasi nyingine 51.

Katika mahojiano hayo mtuhumiwa, alitoa siri ya siraha zingine mbili ambazo wenzake walikuwa wametangulia nazo katika eneo la magorofani walipokuwa wamepanga kufanya tukio la utekaji wa magari katika barabara ya Uvinza - Mpanda iliyoko wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Aidha askari polisi wakiwa eneo walipokuwa wamejificha majambazi wengine ili kukagua na kuoneshwa siraha zingine ghafra askari walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi waliokuwa wamejificha ambapo katika majibizano hayo licha ya askari kujeruhiwa jambazi mmoja alipigwa risasi bega la kulia na mguu wa kushoto na kufariki wakati akipelekwa hospital. ​

Hata hivyo majambazi wengine walikimbia baada ya kuzidiwa na mashambulizi ya Askari hali iliyopelekea kupatikana magazine nyingine ya tatu ikiwa na risasi 23 ambapo msako mkali wa kuwasaka bado unaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha silaha iliyokamatwa kwa mtu huyo
Maafisa wa Polisi Mkoani Kigoma wakijadiliana jambo.
silaha, risasi na magazine zilizopatikana kwenye tukio hilo.

JERRY MURO AITWA KAMATI YA MAADILI

0
0
Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro ameitwa kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika Juni 28.

 Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai 02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi.

Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na kwa.wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia kupitia vyombo vya habari.

Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili kitaendelea kama kawaida na watatoa maamuzi kama kawaida.

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50. 

Na Emanuel Madafa, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

Awali, akitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.

Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata mkandarasi huyo.

Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa ushindi mfuko huo.

ZOEZI LA UHAKIKI WA SILAHA NCHINI LAFIKIA TAMATI, ANGALIZO LATOLEWA KWA WASIOHAKIKI

0
0
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.

Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza sifa ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.

Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.

Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi

KUFUATIA UINGEREZA KUJITOA UMOJA WA ULAYA, TIMU NYINGI ZAPATA KWIKWI KWENYE SWALA LA USAJILI WA WACHEZAJI

0
0
 Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Timu nyingi zinazoshiriki kwenye ligi kuu nchini Uingereza zimekumbwa na kigugumizi cha kufanya usajili katika kipindi hiki ambacho nchi yao imejitoa katika umoja wa ulaya (EU).

Wakili wa masuala ya michezo, Carol Couse amedai kuwa uamuzi huo tayari umeanza kuleta athali ambapo sarafu ya nchi hiyo imeporomoka na kuzidiwa na sarafu ya Euro, hivyo basi vilabu vyote 20 vya ligi hiyo ambavyo vilikuwa vinapiga kampeni Uingereza isijitoe kwenye umoja huo, kwa kuwa na wasi wasi wa kupanda kwa gharama za vibali vya kufanyia kazi kwa wachezaji wa kigeni watakao sajiliwa.
Msimu mpya wa usajili ulifunguliwa majuma mawili yaliopita, lakini kuna wasi wasi timu nyingi hasa zile zisizo kuwa na uwezo mkubwa kifedha itabidi zisubiri hadi hali ya sarafu hiyo (POUND) itulie ndipo waendelee na mchakato wa usajili.

Carol Couse ambaye hufanya kazi na timu kadhaa kubwa ikiwemo Manchester United amebainisha kuwa hali hiyo itavilazimu baadhi ya vilabu kufanya usajili wa haraka haraka ili kukimbizana na muda kwani haijulikani hali ya thamani ya sarafu hiyo itachukuwa muda gani kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Baadhi ya vilabu ambavyo vimeisha fanya usajili uliokamilika mpaka sasa ni Liverpool waliosajili wachezaji 3 ambao ni kipa wa kimataifa wa Ujerumani Loris Karius, Mlinzi wa kimataifa wa kameruni Joel Matip na Mshambulizi wa kimataifa wa Senegali Sadio Mane. Tottenham wamemsajili Victor Wanyama na Chelsea wamemsajili Mitchy Batshuayi.

Ulinzi vituo vya DART kuimarishwa

0
0
Benjamin Sawe

Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.

Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.

Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.

“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.

Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu.

Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu  iliyojengwa kwa  gharama kubwa  sana.

GAZETI LA MTANZANIA LAZINDUA MWEONEKA MPYA

0
0
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jijini Dar es salaam leo kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya "Mtanzania Limeboreshwa". Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Mtanzania, Dennis Msacky na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Michael Bugidira.
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya "Mtanzania Limeboreshwa"Katikati ni Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira.

EDO CHRISTOPHER ASAINI KAGERA SUGAR.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Simba na Toto African ya Jijini Mwanza, Edward Christopher amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Kagera Sugar baada ya kumalizana na  Toto mwishoni mwa msimu huu huku timu hiyo ikifanikiwa kusalia ndani ya ligi msimu ujao na  aliweza kuisaidia timu hiyo kukusanya alama 30 katika msimamo wa ligi huku wakifunga magoli 26 na Kabla ya kumalizika kwa ligi msimu huu mchezaji huyo alikuwa mguu ndani mguu nje kuachana na timu hiyo.

Edward amesema kuwa ameamua kuingia mkataba na timu hiyo baada yaw kukubaliana katika baadhi ya matakwa yake huku akiahidi kuitumikia kwa juhudiw zake zote na toka awali alishasema atafanya kazi na timu yoyote itakayokuwae tayari kukubaliana na matakwa yake lakini nafasi kubwa akiipa Toto.

"Nilikuwa tayari kufanya kazi na timu yoyote msimu ujao ili mradi tu tukubaliane na wawe tayari kunipa kile ninachokitaka", amesema Eddo.

Kwa sasa ataendelea na mazoezi ili kuhakikisha Kagera hawajuti kumjumuisha ndani ya kikosi chao na anachokisubiri ni ripoti ya kambi ya timu hiyo ili kuanza kambi rasmi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Mshambuliaji huyo ni moja ya zao la Simba lakini alishindwa kuendelea baada ya uongozi kutokuwapa nafasi katika kikosi hata baada ya kuonesha uwezo mzuri.

SERIKALI YATANGAZA KIAMA CHA WAUZA DAWA NA VIPODOZI HATARI MITANDAONI.

0
0
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza.

Na Fatma Salum (MAELEZO).
Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema hivi karibuni itaanza msako mkali wa kuwatafuta na kuwakamata wauzaji wa dawa zinazokatazwa pamoja na vipodozi vikali ambao wanajitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii kuhusu kuibuka kwa watu wanaotangaza  biashara ya dawa na vipodozi ambavyo Serikali imevipiga marufuku. 

Akitaja bidhaa hizo Bi. Simwanza alisema ni pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa viungo vya mwili, kupunguza uzito wa mwili na vipodozi vyenye kemikali za kuchubua ngozi bidhaa ambazo zinasababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa Saratani.

“Kumezuka wafanyabiashara holela wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Whatsup Groups na kwengineko  kutangaza biashara ya dawa na vipodozi vyenye kemikali hatari ambavyo vimepigwa marufuku na TFDA hivyo wanaohusika wajiandae, hivi karibuni tutaanza kuwashughulikia.” Alisema Simwanza. 

Alibainisha kuwa bidhaa hizo nyingi hazijathibitishwa na kupewa kibali na TFDA hivyo wauzaji wanakiuka Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura ya 219 inayowataka wafanyabiashara wote wa bidhaa hizo kuzisajili kabla hazijaenda kwa  mtumiaji na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na Sheria.

Alieleza kuwa TFDA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameandaa mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanawabaini na kuwakamata wafanyabiashara wote wanaouza dawa na vipodozi hivyo kupitia mitandao na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani au kuwatoza faini. 

“Wengi wa wafanyabiashara hao hawaweki anuani za maeneo wanayopatikana na hawana maduka rasmi bali huweka namba za simu za mkononi lakini kwa kutumia vyombo vya dola tutawabaini tu na kuwatia mbaroni.” Alisisitiza Simwanza.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy amewatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano hasa matangazo ya biashara kuwa makini na matangazo hayo kwani baadhi ya wafanyabiashara hizo wanaweza kuwa ni watu wenye nia mbaya. 

Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa mbalimbali pamoja na vipodozi ambao wanajitangaza kupitia mitandao ya kijamii na kuna baadhi ya watu wananunua bidhaa hizo bila ya kuhakikisha usalama wake jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

WODI ZA KISASA ZA AKINA MAMA WAZAZI ZINATARAJIWA KUJENGWA KATIKA HOSPITALI ZA RUFAA JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa hali ambayo ilikuwa imefikia katika wodi za wazazi ni mbaya, kwa kulala chini ya sakafu baada ya kujifungua  au kulala wazazi wane katika kitanda kimoja.

Makonda amesema kuwa hata Rais Dk.John Pombe Magufuli kitendo hicho hafurahishwi hivyo jitihada lazima zichukuliwa kwa wazazi kuwa kitanda mmoja kwa mzazi mmoja katika hospitali ya Amana,Mwananyamala na Temeke.

Akizungumza leo wandishi wa habari wakati wakati akipokea mchoro wa ghorofa tatu zitazojengwa kila Hospitali za Rufaa katika jiji la Dar es Salaam kwa kubeba wazazi 150 kwa kitanda kimoja mazazi mmoja zitajengwa na muungano wa makampuni ya amsons, Makonda amesema  watashirikiana  na wadau ili kuhakikisha wanamaliza tatizo la mazingira mabaya katika utoaji wa huduma za afya.

Amesema ufadhili wa ujenzi wa majengo hayo umetolewa na Kampuni ya Amsons ambao watajenga majengo yote kwa gharama zao.
Amsema ujenzi huo  kina mama na watoto wamekuwa wakitseka wanalala kitanda kimoja wawili hadi wanne naona mwisho umefika naomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia sekta mbalimbali hasa  huduma za afya," alisema Makonda.

Aliongeza kuwa kukmilika kwa ujenzi huo kutasaidia wakina mama 450 watkaofikishwa katika hospitali  hizo.

Katika hatua nyingine, Makonda alikabidhi magodoro 100 katika Hospitali ya Amana ambayo yayatumiwa na wazazi ambao wamekuwa wakilala wawili hadi watatu katika godoro moja.

Kwa upande wake, Meneja wa ukuzaji biashara wa kampuni ya Amsons Group,Suleiman Amon, alisema ujenzi huo utakuwa na ghorofa tatu katika hospithali ya Amana, Temeke na Mwananyamala.

Alisema ujenzi wa majengo hayo utagharimu kiasi cha Sh. Milioni 4.5 na utaanza ndani ya wiki sits kuanzia sasa na utachukua wiki nane hadi kukamilika kwake.

" Msaada huu ni kama kurudisha shukrani kwa jamii hivyo tutaendelea kuahirikiana na kuhakikisha kwamba akina mama wanapata huduma bora wakati na baada ya kujifungua,"alisema Amon.

Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe, alisema wanashukuru kwa msaada huo ambao umetolewa kwasababu utasaidia kupunguza mzigo wa changamoto waliyokuwa nayo  kwani hata watu wa mikoa ya jirani wanatumia hopspitali ya Amana kupata huduma.

"Tutatoa ushirikiano kutunza majengo hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu, na magodoro yaliyoyolewa yatapunguza changamoto kwa wazazi ambao wamekuwa  wakilala watatu hadi wanne katika godoro moja,” alisema.

WANANCHI WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA ZA 4G YA TTCL, KATIKA VIWANJA VYA SABASABA.

0
0
 Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.
 Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.

Wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kununua bidhaa bora za  4G katika viwanja vya Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba. 

Akizungumza katika Maonesho hayo, Emerco Mashele Afisa kutoka TTCL amesema kuwa katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya SabaSaba, kampuni imeendelea kuwaletea watanzania bidhaa nzuri za 4G – LTE, zenye kiwango kikubwa cha ubora, bei nafuu na uhakika. 

“Safari hii tumewaletea Wananchi bidhaa bora na nzuri katika matumizi ya mawasiliano ya simu. Kwa huduma zetu tunatoa fursa kwa wateja wetu kupata intaneti yenye kasi ya 4G ukiwa na Laini za 4G ambazo zinapatikana hapa katika Banda TTCL na ofisi za TTCL katika jiji la Dar es salaam” amesema Emerco. 

Aidha, Bw. Emerco aliongeza kuwa katika Maonesho haya ya SabaSaba, TTCL inatoa fursa ya wananchi kupata   laini ya 4G, Modemu ya 4G, Mi-Fi ya 4G na Routers ya 4G.

Katika maonesho haya tuna laini za 4G ambazo zinapatika hapa na katika ofisi zetu za TTCL, Mteja anaweza kifaa cha 4G Mi-Fi ambapo mteja anaweza kuunganisha watu wengine 10 na kupata intaneti katika ubora ule ule. 4G Routers inauwezo wa kuunganisha watu 32 na inauwezo kwenda katika ubora ule ule, Aidha pia Routers inatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma simu ya Mezani. 

MTU MMOJA ANAYEDAIWA JAMBAZI SUGU ADAKWA DAR

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kuwa jambazi sugu Abdallah Said (45) kwa  makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na uvamizi kwenye vituo vya Polisi ikiwemo kituo cha Stakishari na taasisi mbalimbali za fedha  zikiwemo benki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la Kariakoo baada ya askari kufanya upelelezi wa kuwasaka watuhumiwa sugu wanaojihusisha na makosa yakiwemo ujambazi wa kutumia silaha.

Amesema  katika uchunguzi wa  wamebaini kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya  ujambazi wa kutumia silaha ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji ya kutumia silaha.

Kamanda, Sirro amesema mtuhumiwa baada ya kufikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa, alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji katika kituo cha Polisi Stakishari na taasisi za fedha ambazo ni  Benki ya Access Mbagala, Benki ya NMB Mkuranga, Benki ya CRDB na CBA Chanika, Road Block ya Polisi Kongowe na matukio mengine.  

Aidha kamanda huyo  maesema kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwataja baadhi ya viongozi waanzilishi wa mipango ya uvamizi na uporaji wa silaha na mauaji kwa kutumia pikipiki ambao ni Abdulaazizi  Ndobe, Sheykh Mtozeni, Omari Matimbwa,Haji Ulatule,Nasoro Utaule Sasoro Mpemba na wenzake.

Mtuhumiwa huyo pia alitaja mipango yote ilifanyika katika msikiti wa Kitonga na yeye akiwa mtaalam na mshauri wa kitaalam kwa upande wa utumiaji wa silaha.

Wakati huo huo.Jeshi hilo  linamtafuta, Heri Mpopezi mwenye umri kati ya miaka 35-45 kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Mtuhumiwa huyo ameshiriki katika matukio mbalimbali ya uvamizi wa vituo vya Polisi, na taasisi za kibenki na kupora fedha pamoja na mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mfanyakazi wa chuo  cha JKU Zanzibar na anapendelea kutembelea na kuishi Zanzibar, Chanika, Mbagala, Mbande, Kimara, Kitonga, Mwamdimkongo, Bupu, Bagamoyo,Tanga, Kilwa, Ikwiriri, Rufiji na Dondwe.

Amesema  kuwa muonekano wa mtuhumiwa huyo ni Maji ya kunde, urefu wa wastani, kipara kidogo na anapendelea kuvalia vazi la Kanzu na mavazi mengine ya kawaida. Hivyo basi, natoa rai kwa wananchi raia wema watoe taarifa za uhakika za kukamatwa  kwa mtuhumiwa huyo  kituo chochote cha Polisi.

Akizungumzia suala la Mbunge wa Singida  Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema walimkamata mbunge huyo Juni 29 mwaka huu  na wamemhoji kutokana na kutoa maneno ya uchochezi na  kutoa lugha za kashfa dhidi ya Rais Pombe Magufuli ambayo aliyatoa baada ya kutoka Mahakamani Kisutu juzi.

Tundulisu alikuwa akituhumiwa kwa kosa la uchochezi na alikuwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipotoka alitoa maneno ya kumkashifu Rais na maneno ya kichochezi sasa leo(jana) tumempeleka Mahakamani kujibu mashtaka hayo.  

WAKAZI WA ZANZIBAR WANUFAIKA NA KAPU LA VODACOM FOUNDATION.

0
0
 Mkazi wa shehia mahameni mjini Zanziba, Bi.Mwajuma Juma(katikati) akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali kutoka kwa Meneja mauzo wa kanda hiyo wa Vodacom Tanzania, Mohamed Mansour(kulia)ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation ,kushoto ni mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid.
 Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar, Mohamed Mansour(kushoto)na mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid(kulia)wakimkabidhi kapu lenye vyakula mbalimbali Bi.Mwamvua Makame mkazi wa mji huo, ikiwa ni msaada uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mkazi wa Masingini Zanzibar,Mzee Mtumwa Haji Mustafa (kulia) akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali kutoka kwa mwakilishi wa Doris Mollel Foundation, Warda Walid(kushoto)na Meneja mauzo wa kanda hiyo wa Vodacom Tanzania, Mohamed Mansour(katikati)ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation.

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea watoto yatima nchini na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha wamiliki na vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha Mboni Show hafla iliyojumuisha watoto yatima 283 kutoka Vituo vitano vya Mkoa wa Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea watoto yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watoto hao na sio vinginevyo. Kuhusu malezi ya Watoto yatima, Makamu wa Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu bora,upendo na si kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali. 

Aidha, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba jamii kuweka mipango mizuri ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto yatima kwa kuwa nao wana haki ya kuishi vizuri kama watoto wengine. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images