Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1271 | 1272 | (Page 1273) | 1274 | 1275 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda). 
  Akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, “Mabunge yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote muhimu zinatekelezwa;  kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha kutoka kwenye Bajeti ya Serikali”.
  Dkt Ndugulile alisema kuwa muingiliano wa shughuli za kilimo, mifugo na shughuli nyingine za kibinadamu zimesababisha baadhi ya magonjwa ya wanyama kuleta athari kwa binadamu na pia usugu  wa madawa ya aina ya antibiotiki.  Hivyo, kuna haja ya wadau wa sekta hizi kuwa na ushirikiano wa karibu chini ya mpango wa “Afya Moja” (One Health).  
  Alisema kuwaIli mpango wa “Afya Moja” ufanikiwe in lazima maboresho yafanyike  kwenye uratibu wa sekta mbalimbali ndani ya nchi na pia kuandaa mpango wa  pamoja wa udhibiti na kushughulikia majanga.
  Dkt Ndugulile aliyasema hayo kwenye mkutano wa Mpango wa  Usalama wa  Afya Duniani unaofanyika mjini Bali, Indonesia. Mkutano huu ulioanza tarehe 27 Juni unatarajia kuisha tarehe 30 Juni. 
  Dkt Ndugulile mbali ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, ni Mwenyekiti wa  Kamati ya Ushauri ya Mabunge Duniani (Inter Parliamentary Union) kuhusiana na masuala ya UKIMWI, Afya ya Wanawake, Vijana na Watoto.
  ---------------------  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti Mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Bi. Melinda Gates (watatu kutoka kushoto) na ujumbe wake  mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti Mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

  0 0

   Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Geita (GGM), Tenga Tenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Mgodi wa GGM kupandisha watu 100 Mlima Kilimanjaro na wengine watazunguka mlima wa Kilimanjaro kwa baiskeli kwaajili ya kuchangia fedha za mfuko wa Kili challenge ambao ni mapambano dhidi ya Ukimwi. Katikati ni  Balozi wa Kili challenge Msanii, Mrisho Mpoto, Kushoto ni  Mwakilishi wa tume ya Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Peter Dickson.
  Balozi wa Kili Challenge na msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwaajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.

  Julai 16 hadi 22 Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ukishirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi wanatarajia kuwapandisha katika Kilile cha Mlima wa Kilimanjaro watu 50 na wengine 50 watauzunguka mlima kwa baiskeli ikiwa ni kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini.

  Hayo yamesemwa na Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Mgodi wa Geita (GGM), Tenga Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Kilimanjaro Challenge kwa mwaka huu litajumuisha watu kutoka nchi mbalimbali.

  Amesema kuwa Balozi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita kwa mwaka huu ni Msanii wa nyimbo za Mashahiri, Mrisho Mpoto atakuwa na watu watakaoshiriki wa Kili challenge hadi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

  Nae Msanii wa nyimbo za Mashahiri, Mrisho Mpoto amesema kuwa watanzania tuunge mkono kwa pamoja katika sehemu kuchangia au kumuelimisha jamii kuhusina na mapambano dhidi ya UKIMWI yalete mabadiliko.

  “Mimi kama balozi wa Kili challenge, naamini kwamba jitihada zinazofanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na watanzania wote na wadau wenye machungu na nchi hii” Alisema Mpot. Hebu tuungane kwa pamoja kila mmja wetu katika sehemu yake eitha kwa kuchangia au kumuelimisha mwenzake ili mapambano haya yalete mabadiliko” alisema Balozi Mpoto. 

  Fedha zinazopatikana katika mfuko huu zinapelekwa katika kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya ushauri nasaha na upimaji wa ukimwi ambapo baadhi yao ni vie vilivyoko Tanga pale Segera, Manyoni na Geita. Kituo cha watoto yatima Moyo wa Huruma na asasi nyingine zaidi ya 30 zimenufaika na mfuko huu.” Alisema mwakilishi wa TACAIDS, Dickson Peter.

  0 0
 • 06/29/16--07:27: WAPIGAPICHA KAZINI
 • Baadhi ya Wapigapicha wa Habari za Michezo, kila mmoja kwa utaalam wake wakiwajibika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuzisaka taswira za mchezo kati ya Yanga na TP Mazembe ya nchini Congo, Juni 28, 2016.


  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kuingwana.

  Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa  Mbunge Lissu kuripoti  katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu  kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekili kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KUFUATIA kutokea kwa vurugu kubwa jana katika mechi yabkimataifa ya kombe la Shirikisho kati ya Yanga na  TP Mazembe na kupelekea kupigwa kwa mabomu ya machozi na kutumika kwa maji ya kuwasha Kamishna msaidizi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke (ACP), Gilles Muroto amesema kuwa jana vikosi vya usalama viliweza kutumia njia hizo kwa ajili ya kutuliza ghasia zilizosababishwa na mashabiki wa mpira waliotaka kuingia ndani na kuzuiliwa kuingia uwanjani.

  Akizungumza na Mtandao huu, amesema kuwa walikamata watu takribani watu 20 lakini wameshawaachia kwani walifanya hivyo kwa ajili ya usalama wao na zaidi hawakuwa pale kwa kwa lengo wa kuwakamata bali ni kulinda amani.

  "Tulikuwa pale kwa ajili ya kulinda amani na zaidi tuliwakata vijana 20 na tumewaachia tayari kwani tulifanya hivyo kwa kulinda usalama wao kwani vurugu zilikuwa nyingi sana, ila kazi kubwa ilifanywa na vikosi vya usalama na wamefanya kazi kubwa sana,"amesema Muroto. Kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa umeweza kuchukua watu wengi zaidi tofauti na idadi inayohitajika na kwa hali hiyo ilikuwa ni hatari sana pale unapozidisha watu,

  Katika mechi hiyo, watu waliweza kujitokeza uwanjani kuanzia majira ya saa 11 alfajiri na kitu kama hicgo hakijawahi kutokea na hata wale mateja pamoja na vibaka walikuwa wengi sana na lazima nguvu ya ziada itumike hasa baada ya wananchi kuvamia geti na kuliangusha na kuanza kuingia ndani kwa nguvu kitu kilichopelekea kuanza kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

  Uongozi wa Yanga uliwatangazia mashabiki wa soka kuwa hakutakuwa na kiingilio katika mechi yao ambapo maelfu ya watu walikuja kwa wingi na kuweka maswali kwa jamii watu hao wote hawana ajira au waliamua kutokwenda kwenye kazi zao kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ambayo ilikuwa katikati ya wiki ila hali ya ndani ya uwanja ilikuwa tulivu na amani.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  JESHI la Polisi Mkoa wa Temeke linawashikilia waendesha bodaboda 35 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutovaa kofia ngumu (Helmet).

  Akizungumza na  Repota wa Globu ya Jamii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,  Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi  (ACP), Gilles Muroto amesema kuwa kukamatwa kwa bodaboda hao kumetokana na opresheni wanayoifanya ya usalama barabarani ambayo ni endelevu.

  Amesema  kuwa  wanawasiliana na mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) juu ya kuweza kuwafikisha mahakamani waendesha bodaboda kwa makosa ambayo wanahusika nayo.
  ‘’Temeke tumejipanga kuhakikisha kila mtu anayetumia chombo cha moto anafuata sheria na kanuni  na wataokwenda tofauti watafikishwa katika vyombo vya sheria’’Amesema Muroto.

  Aidha amesema kuwa opresheni hiyo ni endelevu haishi leo hivyo wale ambao wanajua zimamoto wakikamatwa na makosa ambayo wanapigiwa kelele ikiwa ni usalama wao.

  Muroto amesema ametaka wananchi kutoa ushirikiano wa vitendo vya kialifu ili kuweza  jeshi kufanya kazi yake na kuweza kuwakamata wale ambao wanajihusisha na uhalifu mbalimbali ndani ya Temeke.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WATANZANIA wametakiwa kuonyesha ushirikiano kwa kuchukia vitendo wanavyofanyiwa wapelestina katika nchi yao.

  Hayo ameyasema leo, Shekhe Mkuu wa Shia, Ahmed Jalala wakati akizungumza na waandishi wa habari juu matembezi ya amani yatakayofanyika mwisho wa mwezi wa Ramadhan kwa ajili ya kuomba amani kwa nchi ya Palestina.

  Jalala amesema kuwa nchi ya palestina haikaliki na kufanya kuongoza kuwa idadi kubwa ya wajane na yatima kutokana na mauaji yanayofanywa dhidi yao.

  Amesema kuwa vyombo vya kimataifa havijaweka nia dhabiti juu ya kufanya nchi hiyo kuwa na amani kwani vitu vinavyofanya vimeanza muda mrefu lakini hakuna matokeo.

  Kiongozi huyo amesema kuwa Palestina kukiwa na amani hata ugaidi unaweza kuondoka kwani tatizo la nchi hiyo ni kubwa kuliko la ugaidi unaosemwa.

  0 0

  On 20th May 2016 TATOA together with other local and Rwandese stakeholders organized a first of its kind Tanzania - Rwanda Trade Forum in Kigali, Rwanda. The forum was aimed as a networking event for high level Government officials involved in trade facilitation as well as private sector operators from both Tanzania and Rwanda. TATOA delegation was led by its Chairperson Angelina Ngalula ; Board Directors Elias Lukumay, Chief Lusekelo Mwakibete, Rahim Dossa, Saad Ismail and its Chief Executive Officer Emmanuel Kakuyu.

  At the Forum, TATOA was able to hold talks and make tentative cooperation agreements with its Rwandese counterparts. One of these  included a tentative  agreement of cooperation with the Rwanda Transporters Association and Rwanda Freight Forwarders Association. These agreements will see members of the relative associations getting assistance when encountering problems in their counterparts’ respective countries. These agreements will also help boost trade between TATOA and members of the other organizations.

  TATOA also held talks with the Rwanda Private Sector Foundation (RPSF) and agreed on cooperation where the RPSF indicated that they might be interested to enter into an MoU with TATOA to use members’ trucks for their transport needs. The agreement, if finalized, will see TATOA members set special rates for members of RPSF which in turn will help increase trade between members of the two organizations. TATOA also held talks with a number of individual Rwandese businesses for them to use trucks belonging to members.

  The forum which is planned to be held every year was sponsored on behalf of TATOA by Bravo Logistics, Simba Logistics, Usangu Logistics, NAM Enterprises and SIMERA Transport.
  TATOA Chief Executive Officer Emmanuel Kakuyu delivering opening remarks at the Tanzania-Rwanda Trade Forum.
  Participants at the Tanzania - Rwanda Trade Forum, in Kigali.
  Board Chairperson of TATOA, Angelina Ngalula (R) receiving a present from Rwanda Private Sector Foundation Chief Executive Officer.
  Group photo.

  0 0

   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
   Ofisa Masoko Mwandamizi, Amina Mmbaga akimsiliza mmoja wa wanachama wa NSSF.
   Ofisa Mauzo wa NSSF,Abbas Ramadhani (kushoto), akitoa maelezo kwa mmoja wa wanachama waliofika katika banda la NSSF.
   Ofisa Uwekezaji wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Moringe Nyerere (kushoto) akiwaonyesha watu waliofika katika banda la NSSF leo, ramani ya mradi wa viwanja vya Kiluvya vinavyouzwa  na shirika hilo, wakati wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

   Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirikala Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kushoto) akigawa vibeberushi vyenye taarifa za shirika hilo kwawatu waliofika katika banda lao, wakati Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  HAIKUWA hali ya kawaida ila ukihadithiwa ni kama hadithi za sungura na fisi ila umati wa maelfu ya Watanzania ilistaajabisha umma na kila mmoja kujiuliza hivi kweli zaidi ya watu elfu hamsini (50,000) waliojitokeza Uwanja wa Taifa kuishuhudia mechi kati ya Yanga na TP Mazembe, hawakuwa na shughuli za kufanya? Achilia kuajiriwa ila hata kujiajiri pia? 
  Hilo ni swali la kujiuliza kwani majira ya saa 12 asubuhi watu walikuwa wameshafurika kwenye mageti yote ya kuingia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ambayo changamoto mbalimbali ziliweza kuonekana ikiwemo utaratibu wa kuingia kuwa mgumu hasa baada ya uwanja kujaa. Uwanja wa Taifa unachukua watu zaidi ya elfu hamsini (50,000) na kwa hali ilivyoonekana jana kama ungeingia watu zaidi ya idadi halisi, labda pengine hata mchezo wenyewe usingeweza kuchezwa, kwani wangeingia mpaka kwenye dimba la kati unakochezewa mchezo huo.
  Swali la kujiuliza hapa, Je, kujitokeza kule kwa wale watu kunatokana na nini, Je ni kwamba hawakuwa na shughuli za kufanya, na kama wanazo walimuachia nani na kwa nini? na kama ni mapenzi ya Mchezo wa Soka waliyonayo ndio imepeleka kujitokeza kwa wingi wa namna Ile na ndio kuanzia asubuhi yote ile wakati mechi ilichezwa saa kumi (10:00) jioni??  au ndio mambo ya kupenda vya dezo?? nadhani kuna haja ya kujiuliza sana juu ya swala hili, maana kwa siku ya Jumanne tena mwanzoni mwa wiki watu wengi kujitokeza namna ile ni jambo la kushtua kidogo. 

  0 0


  Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.
  Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, 2016 kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).
  Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17, 2016 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), lakini Mheshimiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwa sehemu ya burudani ya burudani mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.
  Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya millennia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.
  Makipa:Fatma Omary, ,Belina Julius, Najiat Abbas; Walinzi:Stumai Abdallah, Fatma Issa,Anastazia Antony, Happuness Henziron, Maimuna Khamis; Viungo:Donisia Daniel, Amina Ali, Amina Ramadhani, Fatuma Bashiri; Wema Richard, Fadhila Hamadi, Mwajuma Abdallah, Anna Hebron, Sophia Mwasikili; Washambuaji: Tumaini Michael, Johari Shaaban, Fatma Idd, Shelder Bonifdace Mafuru, Asha Saada Rashid na Mwanakhamisi Omar.
  ……………………………………………………………….

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

  0 0

  Venue: Paparazzi Club, Slipway - Msasani Bay, Dar es Salaam
  Entrance: 10.000 TSH only
  We are excited to announce the lineup for next edition of #THEBEATFESTIVAL. The program features Jagwa Music (mchiriku / afropunk), Peter Masima (traditional gogo music) and Mzungu Kichaa Unplugged (acoustic performance). Entrance; 10k only. Doors Open 21.00hrs.

   JAGWA MUSIC – afropunk / mchiriku
  Jagwa is the leading exponent of the Mchiriku style, which originated twenty years ago in the poor suburbs of Dar es Salaam. Jagwa and their peers were immediately attracted by the the small Casio keyboards lo-fi sound, adopted it, hooked it up to megaphone speakers, and the resulting gritty, edgy, distortion-laden sound became Mchiriku. Their career, which started in Mwananyamala, one of the poorer suburbs of Dar es Salaam, has taken them to some of the biggest stages across the globe.


  PETER MASIMA – traditional gogo music

  Peter Masima is a talented Gogo musician from Dodoma. He plays Marimba, locally known asilimba and Zeze, a stringed fiddle, and is also a skilled instrument builder. He is fairly unknown on the cultural scene in Tanzania despite his enormous talent. We think it is about time that he is introduced to those who have yet to hear his “voice”. The late Hukwe Zawose who was signed to Peter Gabriels Real World Records made the music of the Wagogo popular globally. It has also been researched by a number of ethnomusicologists due to its rich and unique musical and cultural heritage.


  MZUNGU KICHAA – unplugged performance


  Debuting in 2009 with his album Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa and his band Bongo Beat have created a unique style of live Bongo Flava, which has taken them around the world. Tonight Mzungu Kichaa will perform a selection of old and new songs upfront and personal with a solo acoustic performance with his guitar after a two week songwriting retreat in Morogoro. 


  ABOUT THE BEAT: The Beat is a monthly festival showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is powered by: Caravan Records, Paparazzi Bistro Club, Jameson, and Goethe Institut Tanzania. Info: CRTanzania@gmail.com web:www.facebook.com/TheBeatFestival

  INSTAGRAM: @paparazzi_bistro_club, @thebeatfestival, @CRTanzania, @GoetheTanzania, @MzunguKichaa #thebeatfestival

  FACEBOOK: @paparazzi_bistro_club, @thebeatfestival, @CRTanzania, @GoetheTanzania, @MzunguKichaa #thebeatfestival

  0 0

  Na Sixmund J. Begashe

  Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam imezindua rasmi program ijulikanayo kama Museum Arts Explosion ili kutoa nafasi kwa wasanii wa hapa nchini kufanya kazi zao za sanaa kwenye jumba hilo la Makumbusho ya Taifa kwa malengo ya kuendeleza na kukuza Sanaa na Utamaduni nchini. 
  Akipokea salamu mbali mbali za pongezi kutoka ndani na nje ya nchi baada ya onesho zuri na lililo sisimu wengi waliofika kuliona kwenye Ukumbi wa Makumbusho hiyo, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure ameeleza kuwa, wadau wengi wamependezwa sana na maamuzi haya ya Makumbusho ya kuinua uhai wa Sanaa nchini kwa kupitia Programu hii ya sasa. 
  “Hii ilikuwa ni kiu ya wasanii walio wengi hapa nchini, kiu ya kuwa na sehemu watakayo oneshea kazi zao wanazo zalisha, na si kwa wasanii tu pia kwa watazania na wageni mbali mbali kwani walikuwa wakipata shida sana kuwa na mahali maalumu pakuonea sanaa za jukwaani, lakini sasa tumesha fungua milango kwa wasanii wote hapa nchini ambao watakuwa wamejiandaa vizuri kuja kujisaliji ili kuwekwa kwenye program hii mpya” alisema Bw Bufure. 
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti  Msanii wa Kimataifa Bw Isack Abeneko na Bw Aloyce Makonde wameipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kuwapa heshma ya kuizindua program hio kwa wao kufanya onesho lakwanza na lililo onesha mafanikio makubwa kwa kuudhuriwa na watu wengi, hivyo wametoa wito kwa wasanii hapa nchini kuitumia nafasi hii adhimu ili kuifikishia adhira Mafundisho, Maonyo na Burudani kama yalivyo matarajio yao. 
  Mratibu wa Program hiyo Bw Edgar Chatanda ameielezea program hiyo kuwa kwa sasa itakuwa ikiandaa maonesho  kila Ijumaa ya mwisho wa Mwezi ili kutoa nafasi kwa menejimenti ya Program kujidhirisha na ubora wa onesho kabla ya kupandishwa jukwaani, pia kupata muda wa kutosha wa kufikisha taarifa ya onesho hilo kwa umma ili watanzania wapate hii haki ya kuona kazi za wasanii wa hapa nchini. 
  “Program hii ni endelevu, na tutakuwa na aina mbali mbali za kazi za sanaa zitakazo oneshwa hapa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, tulikuwa na wasanii wa Dance Garage chini ya wasanii wa kimataifa, kwa kweli walifanya vizuri sana, onesho linalofuata litakuwa tarehe 29 Julai 2016 litakalo fanywa na Mwanamuziki wa Kimataifa wa Rege pamoja na Wasanii wa ngoma za ubunifu wa MUDA AFRICA, hivyo nitoe wote kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya kwani onesho lililopita wageni kutoka nje na watu maarufu tu ndio walio uduria”. Alisema Bw Chatanda.

   

  Bw Chatanda alivishukuru vyombo vya habari vyote hususani MICHUZI BLOG kwa mchango wao katika kufikisha taarifa kwa jamii kuhusiana na program hii ya Museum Art Explosion na kuviomba vyombo vya habari vingine pamoja na wadau mbali mbali kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ili kusaidia kuwapa heshama wasanii na sanaa hapa nchini.
   Msanii wa Kimataifa Bw Aloyce Makonde a.k.a Mkulima akionesha ubunifu wake wa dance alioiita MSOMI MAKOLOLI ionesha kwenye onesho la Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

   Hapo si barabarani bali ni jukwaani, wasanii wa ngoma za ubunifu Bw Tiko Mbepo alie simama kulia na Bw Isack Abeneko alieko juu ya Pikipiki wakimaliza onesho kwa kuwaacha jukwaani baadhi ya adhira walio ichukuwa na kuiweka jukwaani kama sehemu ya onesho lililofanyika kwenye Jukwa la Maonesho la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

   Pichani haya si masumbwi ya kweli bali ni sehemu ya ngoma ya ubunifu iliyo itwa MACHO MATATU ikichezwa na wasanii wa ngoma za ubunifu Bw Tiko Mbepo alie kushoto na Bw Isack Abeneko kulia kweye onesho la Museum Arts Explosion kwenye Jukwa la Maonesho la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaama.

  Wasanii wa kikundi cha DDI wakiwa onesha umahiri wao kwenye ngoma ya ubinifu ijulikanayo kama Freedom (Uhuru) iliyo waliyo ionesha kwenye onesho la Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.


  0 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kupanga Miji mingine  Miwili Midogo ya Wete Kisiwani Pemba na ule wa Makunduchi Unguja katika azma yake ya kuhimiza matumizi bora  na ya kudumu  ya ardhi hapa Nchini.
  Mipango hiyo itaenda sambamba na kufanya mapitio ya mpango wa maendeleo ya Utalii katika eneo la Pwani ya Mashariki ya Kisiwa cha Unguja  inayoanzia kutoka Chwaka Wilaya ya Kati hadi Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A”.
  Akifunga  Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanmzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba migogoro ya ardhi bado imekuwa changamoto kubwa inayoisumbua Serikali kwa muda mrefu sasa.
  Balozi Seif  alionya kwamba Wananchi wengi hawataki kuheshimu Sheria ya Ardhi jambo ambalo linaibuwa migogo ya ardhi kila uchao. Hivyo katika kumaliza au kupunguza migogoro hiyo aliiomba Mahkama ya Ardhi kuzishughulikia Kesi za migogoro ya Ardhi haraka iwezekanavyo.
  Akizungumzia tatizo la ajira kwa watoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwanasihi wazazi  kuwacha kuwatumikisha  kazi watoto wao  hasa zile hatarishi kwa kisingizio cha kujiongezea kipato cha familia ili kupunguza tatizo hilo lililolikumba Taifa kwa hivi sasa.
  Balozi Seif alisema Familia bado zina jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wao wanapata haki zao za msingi ikiwemo elimu na malezi bora kwa lengo la kuwajengea mazingira mazuri ya maisha yao ya baadaye.
  Alifahamisha kwamba kuwepo kwa ajira za watoto hapa Zanzibar bado ni suala kubwa na Serikali inaendelea na jitihada za kulitafutia dawa ya kulikomesha kabisa  ili kuendana na sera na miongoizo ya Kimataifa juu ya kuondokana na tatizo hilo sugu.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunga Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunga Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
   Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kufungwa kwa Baraza la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kufungwa kwa Baraza la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani. Picha na  OMPR – ZNZ.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 
   BAADA YA kupoteza michezo miwili sasa kikosi cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Julai mosi kwa ajili ya maandalizi yao ya mechi zake za kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo kambi hiyo itakuwa nje ya Jiji la Dar es salaam huku wakiwa hawajaweka bayana ni wapi wataelekea. 
   Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry muro amesema kuwa wachezaji wamepewa siku mbili za mapumziko na Julai mosi kikosi kitaingia kambini. na tayari benchi la ufundi limeshakutana na uongozi na kuzungumzia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo na baada ya kuona makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao uliopita dhidi ya TP Mazembe sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo wao huo ili kuhakikisha wanafanya vizuri. 
   Kwa sasa timu yao imebakiza mechi nne katika hatua hiyo hivyo maandalizi yatakayofanywa ni makubwa na watahakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao uliosalia dhidi ya Medeama pamoja na mechi za marudiano. 
  "Kikosi kitaingia kambini kujiandaa na michezo yetu na tutahakikisha maandalizi yanayofanyika yanakuwa ya hali ya juu ili kuweza kupata pointi tatu katika kila mchezo", amesema Muro.
   Mechi inyofuata ya Yanga ni dhidi ya Medeama ya Ghana huku pia ikisubiri michezo yake ya marudiano na kufanya idadi ya michezo hiyo minne. 
   Licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu yao kwa nguvu zote lakini walishindwa kutumia nafasi walizozipata katika dakika 45 za kwanza na matokeo waliyoyapata ndo yameshatokea na hawawezi kubasilisha ukweli kuwa wamepoteza mchezo huo muhimu kwao tena katika uwanja wa nyumbani na zaidi uongozi wameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wao hivyo hawana sababu ya kumlaumu mtu kwa kupoteza mchezo huo. 
   Katika hatua nyingine Jerry alisema kuwa anataka wanayanga watambue kuwa madai ya wao kutakiwa kulipa deni la zaidi ya milioni 530 hazina ukweli wowote kama mchezo huo ulikuwa bure na hawakuingiza mapato yoyote, watatakiwaje kulipa deni hilo, 
  "Kinachotuhusu sisi ni kulipia gharama za uwanja pamoja na vivu vingine muhimu hivyo kama kuna uharibifu wowote basi asilimia 15 ya fedha tunazolipa yatatumika kwa ajili ya uharibifu huo".

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.

  Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es salaam ni Dkt. Binilith Satano Mahenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Charles Ogesa Mlingwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Bi. Zainab Rajab Telack ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

  Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Mikoa imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya wateule ambao waliteuliwa na Rais Magufuli Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.

  Aidha, miongoni mwa wakuu wa wilaya 139 walioteuliwa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika wilaya tatu ambapo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mteule Mhe. Fatma Hassan Toufiq na badala yake amemteua Bi. Agness Elias Hokororo kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mteule Bw. Emile Yotham Ntakamulenga na badala yake amemteua Bw. Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mteule Bw. Fikiri Avias Said na badala yake amemteua Bw. Miraji Mtaturu kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao huku wakizingatia kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.

  Rais Magufuli pia amewataka kusimamia ukusanyaji mapato ya serikali na matumizi ya fedha na rasilimali nyingine za umma, kuhakikisha wananchi wapo salama na pia kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali.

  "Katika kazi hizi wapo watakaowakejeli, katika kazi hizi wapo watakaowadhihaki, nyinyi kavumilieni na mmuweke Mungu mbele na mkawaweke watanzania mbele, mkafanye kazi kadiri Mungu atakavyokuwa amewaongoza.

  "Nataka kuwahakikishia tunawaunga mkono kwa nguvu zote, mkafanye kazi bila uwoga wowote, katembeeni kifua mbele, kwa sababu tumewaamini wala msiwe na wasiwasi, ukifanya kitu kizuri kwa dhamira yako iliyo njema kitazaa matunda mazuri, ukifanya kitu kwa unafiki hakitafanikiwa" Amesema Rais Magufuli

  Katika hafla hiyo, wakuu wa mikoa walioapishwa na wakuu wa wilaya wateule wamekula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

  Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates ambapo Rais Magufuli amemuhakikishia mwenyekiti mwenza huyo kuwa serikali ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na taasisi hiyo ambayo imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Afya, Uongozi na Kilimo.

  Kwa upande wake Bi. Melinda Gate amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania na ameahidi kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates itaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  29 Juni, 2016 .

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zainab Telack kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Hili ni Jambo la kushangaza sana tena ni jambo la Aibu kwa Uchafu kama huu kuwa Pambo mbele ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa bila hata jitiada za makusudi kufanyika, Jamani hii si Aibu hii tena bila kuwa na hofu takataka zimejazwa kwenye mifuko katika Ofisi ya kata ya Iyela Jijini Mbeya kama mapambo ya Sherehe, wahusika wa hili kitumbuweni Kijipu hiki kabla hamjatumbuliwa.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willium Lukuvi wakati  akifungua mkutano wa Kujadili Matatizo na Ufumbuzi wa Utekelezaji wa Sheria ya Umiliki wa Sehemu za Jengo (Unit Tittle Act) iliyofanyika na wadau wa ardhi kutoka taasisi na makapuni mbali mbali ya ujenzi katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
  Baadhi ya wawakilishi wa taasisi na makapuni mbali mbali ya ujenzi yakiwa katika mkutano huo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Nchini(TFF) kuanza kusimamia rasmi mechi zote za kimataifa zitakazofanyika hapa nchini, Kuanzia sasa TFF itahusika na kuratibu mechi hizo, kusimamia mapokezi ya timu, usalama wao, sehemu za kufikia, viingilio pamoja na uuzwaji wa tiketi za mchezo husika na maamuzi hayo ni kama yamekuja baada ya Yanga kuruhusu wapenzi wa soka nchini kuingia bure katika mchezo wao dhidi ya TP Mazembe hali iliyozua tafrani.

  Katika mchezo huo vyombo vya usalama vilipata wakati mgumu kuzuia mashabiki wa timu hiyo baada ya kutaka kuingia uwanjani ikiwa tayari ulikuwa umejaa na Vurugu hizo ziliwalazimu wanausalama kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha ili kuwatawanya mashabiki hao waliofikia hadi hatua ya kuangusha moja ya geti la uwanjani hapo.

  Kwa mujibu wa kanuni ya FIFA kifungu cha 67, CAF kifungu cha 59 na TFF kifungu cha 52 kinalipa mamlaka shirikisho husika kusimamia kila kitu ikiwemo maandalizi ya machezo, mapato, matangazo na vingine muhimu katika mchezo huo namba 107 wa Yanga dhidi ya Mazembe Yanga walishapanga viingilio lakini walibadili maamuzi na kuamua kuingiza watu bure na kurusiwa na CAF kwa masharti ya kuingiza mashabiki elfu 40 tu lakini walizidi hadi 60 elfu.

  Pia TFF kupitia kwa Wizara yenye dhamana iliruhusu mchezo huo lakini nayo ikitoa masharti ya kutoharibu miundombinu ya uwanja, kulipa gharama za uwanja, gharama za CAF pamoja na TRA na walikubaliana na kwa sasa wanafanya mawasiliano na watu wa Wizara, CAF na TRA kujua Yanga wanatakiwa kulipa kiasi gani. 

  Pia kunasubiriwa ripoti kutoka CAF juu ya matukio ya ndani na nje ya uwanja yaliyojitokeza katika mchezo huo dhidi ya Mazembe na zaidi TFF wanaitakia Yanga kila la kheri kuelekea katika mechi zake zilizobaki kwani matokeo ya mchezo kati ya Mo Bejaia na Medeama yanaipa Yanga matumaini ya kusonga mbele endapo watafanya vizuri katika mechi zake zilizobaki.

older | 1 | .... | 1271 | 1272 | (Page 1273) | 1274 | 1275 | .... | 3353 | newer