Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA UTEUZI KWA UMMA


RC MAKALLA AIOMBA BENKI KUU IFANYE UTAFITI KUHUSU UNUNUZI WA MAZAO YAKIWA SHAMBANI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016.
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakiwa makini katika mkutano huo.
Mgeni rasmi katika picha ya Pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo.

Na EmanuelMadafa, JamiiMojablogu Mbeya.
SERIKALI MKOANI Mbeya imeitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya kufanya utatifi juu ya kuwepo kwa ununuzi wa mazao kwa wakulima mapema kabla ya kuanza kukomaa hususani mazao ya ndinzi hasa katika halmsahuri ya wilaya ya Rungwe Mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla wakati akizungumza na wafanyakazi wa benki Kuu Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo yenye lengo la kujitambulisha.

Amesema kwa muda mrefu sasa wakulima wa mkoa huo wamekuwa wakinyonywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakinunua mazao mapema yakiwa shambani na kupangia bei ya chini ambayo haiendani na bei hali ya sokoni.

SHAMO WORLD FOUNDATION YATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu vya msaada kwa  Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif jijini Dar  es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika  kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.

Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.

Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia.
 Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto walio klatika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.

SEKTA YA MAWASILIANO KUPATA MWEKEZAJI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WIZARA YA ARDHI YAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
  Banda la maonesho la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi likiwa limeanza rasmi kutoa huduma katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere vya Sabasaba Dar es salaam.
 Baadhi ya Wananchi wakipata maelezo ya huduma za mipango miji zinazosimamiwa na Wizara ya Ardhi.
 Muoneshaji wa Wizara ya Ardhi bi. Mwanamkuu Ally akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Ardhi kifaa kinachotumika katika upimaji wa Ardhi cha aina ya Total station.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU JUU YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA WA MWAKA 2016

$
0
0
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari "Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba".

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI HAUTAPIMWA NYUMBA KWA NYUMBA bali itafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania kuanzia mwezi Septemba 2016 ambapo UKIMWI utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huu.

Utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.  

Aidha, katika utafiti huu kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo. 

Ifahamike kwamba, utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016 unafanyika nchini kwa mara ya 4 ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili ulifanyika mwaka 2007 na wa tatu ulifanyika mwaka 2011. 

Hivyo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inapenda kuwatoa hofu wananchi kwakuwa utafiti huu sio mpya katika nchi yetu na watanzania ambao wamekuwa wakipitiwa na utafiti huu, wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa zaidi ya asilimia 90.

Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).
Imetolewa na: 
Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Dar es Salaam, 
                             28 Juni, 2016.

TAKWIMU WAZINDUA RIPOTI YA MATOKEO YA UTAFITI WA UONGEZAJI VIRUTUBISHO KWENYE VYAKULA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti Matoke ya Utafiti wa Tathimini ya hali ya uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula hapa nchini kwa mwaka 2015.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa AAPH, Emilian Busara katikati wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ripoti Matoke ya Utafiti wa Tathimini ya hali ya uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula hapa nchini kwa mwaka 2015 jijini Dar es Salaam leo.

YANGA YALALA KWA BAO 1-0 NA TP MAZEMBE UWANJA WA TAIFA LEO

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Obrey Chirwa akiichambua ngome ya timu ya TP Mazembe, katika mtanange uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam, ikiwa ni Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hadi kupanga cha mwisho kinalia, Yanga wamelala kwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa Timu ya TP Mazembe, Mtanzania Thomas Ulimwengu akichuana vikali na Beki wa Yanga, Kelvin Yondani, katika Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa TAifa jijini Dar es salaam. Yanga imelala kwa bao 1-0.
Beki wa TP Mazembe, Christian Nekadio akiruka juu kuondosha hatari iliyoelekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga, Juma Hassan Mahadhi.
Kipa wa Yanga,Deogratius Munish 'dida' akinyaka mpira kwa umaridadi.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA SADC NCHINI BOTSWANA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma (wapili kulia) kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na serikali wa Jumuiya yaMaendeleo kusini mwa Afrika ( SADC ) kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli Juni 28, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA RAIS WA COMORO PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.

Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.

Rais Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii na kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.

Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.

Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka nchini JAPAN.

Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.

Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. 

BALOZI SEIF AFUNGUA SEMINA YA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifungua Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika katika ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na wa Pili kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia ya Rakgas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Kamal Ataya.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbali mbali zilizotolewa kwenye Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Mtaalamu wa utafiti na uchimbaji mafuta na gesi kutoka Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Osama Abdel akityoa mada kwenye semina ya mafuta na gesi ilitotolewa kwa wawakilishi wa Zanzibar.

Mrakibu Msaidizi wa Mafunzo { ASP } Juma Makame wa Pili kutoka kulia mwenye shati la drafti akimpatia maelezo Balozi Seif aliyepo kati kati juu ya harakati za kukamilika kwa matengenezo makubwa ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi hapo Kikwajuni Mjini Zanzibar.Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassan na nyuma ya ASP Juma Makame ni Msimamizi wa ujenzi kutoka KMKM LCDR Hamad Masoud Khamis.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza akimueleza Balozi Seif hatua zinazofanywa za kuimarisha eneo la nje ya Ukumbi huo.Picha na – OMPR – ZNZ.

NEWZZ ALERT:Mahakama Kuu jijini Arusha yamvua ubunge mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole (CHADEMA),yaamuru uchaguzi urudiwe upya

$
0
0
Aliyekwa Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh.Onesmo Nangole

Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.

Akisoma hukumu hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:

1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

Mh. Herman Kapufi aipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

$
0
0
 -Watendaji kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Wakifanya ukaguzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na mifumo ya umeme katika shule kongwe 11 katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa kuzifanyia. 

 Na Hassan Silayo

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Herman Kapufi ameshukuru Jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kutekeleza miradi inayosaidia kuongeza ubora wa elimu nchini ikiwemo utekelezaji wa mradi kukarabati shule kongwe nchini utakaoboresha mazingira ya kufundishia na kusaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo.

Mh. Kapufi amesema kuwa mpango huo umekuja wakati muafaka wakati uongozi wa wilaya hiyo ukipambana kutatua changamoto za elimu na kuwataka wadau kuipa ushirikiano Mamlaka hiyo.

“Kwa kweli napenda kuishukuru Mamlaka ya elimu Tanzania kwa jitihada zake hizi za kuboresha sekta ya elimu nchini, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana katika wilaya hii kwa kipindi chote nilichokuwa hapa kama mkuu wa wilaya, shule zetu kongwe zimechoka sana na zinahitaji ukarabati ili kuweza kuzirudisha katika hali yake ya kawaida kwa utekelezaji wa mpango huu” Alisema Mh.Kapufi.

Naye Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bibi. Sylvia Lupembe amesema kuwa kupitia TEA mpango huo utatekelezwa katika shule kongwe 11 katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa kuzifanyia ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na mifumo ya umeme.

“hali ya shule zetu kongwe kwa kweli sio nzuri tumetembea kwenye mikoa takribani Mikoa sita tumejionea halihalisi ya miundombinu ya shule zetu kongwe hazipo katika mazingira mazuri ya kujifunzia kutokana na kuwa na miundombinu chakavu na kwa mradi huu tunataka kuweka mazingira mazuri ya watoto wetu hawa kujifunzia hasa kwa kuanza na shule hizi kongwe” Alisema Sylvia.

Wakizungumzia ukarabati huo Mwalimu Mkuu wa shule wa Shule ya Sekondari Nganza Bi. Yacinta Lyimo aliishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa Utekelezaji wa mpango huo kwani utasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na hata kusaidia kuinua kiwango cha elimu na ufaulu katika shule hizo.

Aidha, Afisa Elimu wa Manispaa ya Singida Bw. Omari Kisuda Mpango huu wa maboresho ya shule kongwe ni mkombozi katika sekta ya elimu na umekuja wakati uhitaji wa maboresho ya shule hizo unahitajika hasa kutokana na baadhi ya shule kushindwa kufanya ukarabati wa mara kwa mara kutokana na ufinyu wa bajeti.



 

Mchezaji Thomas Ulimwengu amtembelea Mdau wa soka nchini Shaaban Tippo jijini Dar leo.

$
0
0


Mchezaji wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania ambaye kwa sasa anaichezea timu ya TP Mazembe ya nchini Kongo-DRC,Thomas Ulimwengu mapema leo akiwa katika picha ya pamoja na Mdau mkubwa wa Soka hapa nchini (pichani shoto),Othman Shaaban Tippo a.k.a Zizzou.Mchezaji huyo Mshambuliaji wa TP Mazembe amemtembelea mdau huyo anaemiliki duka la vifaa vya michezo lililopo maeneno ya Bamaga,Sinza jijini Dar na kumjulia hali,Ulimwengu amemshukuru na kumtakia afya njema na heri  Mdau Tippo katika shughuli zake mbalimbali,Tippo amempatia vifaa kadhaa vya michezo mchezo huyo Thomas Ulimwengu.

TANZANIAN WINS HER MAJESTY THE QUEEN’S YOUNG LEADERS AWARD

$
0
0



By Ayoub Mzee-London 
Her Majesty The Queen, Head of the Commonwealth, accompanied by Prince Harry, has hosted a special ceremony in the Ballroom at Buckingham Palace to present medals to the 60 winners of The Queen's Young Leaders Awards for 2016.
Among them was Rachel Nungu from Tanzania a doctor and the national co-ordinator of a medical programme to help children who are born with clubfoot. The programme uses a non-surgical method called the Ponseti method to treat patients. Children born with clubfoot are often hidden away, so Rachel has built good relationships with community leaders to spread awareness of the condition and its treatment.
 She has contributed to the establishment of partnerships with clinics in different regions and has trained staff. So far, more than 100 children have been treated, and in the future the group hopes to help more of the 3,000 children who are born with the condition each year. Chairman of The Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust, Sir John Major, David Beckham and Sir Lenny Henry were also in attendance. 
The Queen’s Young Leaders Award is a prestigious Commonwealth project which recognises and celebrates exceptional young people from across the Commonwealth who are taking the lead in their communities and using their skills to transform lives. The Queen’s Young Leaders programme aims to discover, celebrate and support young people from every Commonwealth nation. The awardees are chosen for having transformed their own lives and the lives of those around them, despite challenges they may have faced along the way.

ATE WAWAASA WANACHAMA KUACHANA NA UWAKALA WA RUSHWA KATIKA SEHEMU ZAO ZA KAZI.

$
0
0
WANACHAMA wa chama Waajiri Tanzania waaswa kuachana na uwakala wa Rushwa katika nafasi zao wakati wa kuaajiri wafanyakazi katika sehemu zao za kazi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha waajiri Tanzania(ATE), Agrey Mulimuka wakati akizungumza na wanachama hao katika mkutano mkuu wa mwa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Pia amesema kuwa waajiri waajiri wafanyakazi wenye kibali cha ukazi na kuwa na mabadili katika sehemu zao za kazi.

Nae Kamishna wa kazi wa Wizara ya Ofisi ya Waziri  Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Hilda Kabisa wakati akizungumza na wanachama wa chama cha waajiri Tanzania jijini Dar es Salaam leo kwenye mkutano wa Mwaka wa Chama cha waajiri Tanzania. 

Amesema kuwa waajiri wengi huwa hawana tabia ya kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini.
Kamishna wa kazi wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Hilda Kabisa akizungumza kwa niaba ya Wizara wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa chama cha waajiri Tanzani (ATE) jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa chama cha waajiri Tanzania, Almas Maige na Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa chama cha waajili Tanzania jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wadau na wa chama cha waajiri Tanzania(ATE) wakisikiliza katika mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

UCHAGUZI JUDO JULAI 06, FOMU KUANZA KUTOLEWA KESHO

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa Martina Maurizio (kulia), akiwaelekeza jambo wachezaji.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo nchini (BMT) limetangaza tarehe ya uchaguzi wachama cha mchezo wa JUDO ambao unatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu huku nafasi mbalimbali za wagombea zikitangazwa na kuwataka klabu kujitokeza kuja kuchukua fomu zitakazoanza kutolewa kesho Juni 30 katika ofisi hizo.

Akizungumza na Michuzi blog , Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika hapa hapa Jijini Dar es salaam na kila klabu itatakiwa kutuma wawakilishi watatu wakiambatana na barua za utambulisho pamoja na cheti cha usajili wa klabu hiyo.

“kila Klabu inatakiwa kutuma wawakilishi watatu ambao wataingia kwenye mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba yatakayofanyika Julai 5 ambayo ni siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, ila wawakilishi hao wanatakiwa kuja na barua za utambulisho na cheti cha usajili wa klabu hiyo,”.

Ametaja nafasi zinazogombaniwa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, Muhasibu, Mkurugenzi wa Ufundi ambapo gharama za uchukuaji wa fomu hizo itakuwa ni kiasi cha shilingi 20,000.

Katika nafasi yaKamishna wa waamuzi, kamati ya fedha na masoko, kamati ya kujitolea na ustawi na kamati ya elimu na michezo gharama yake itakuwa ni shilinngi 10,000 huku akiwataka wanachama waje kwa wingi kujchukua fomu kwani kila kitu kinahitaji waendeshaji ili kukijenga zaidi na kukiletea maendeleo pia amesema kuwa mwisho wa kuchukua fomu hizo ni Julai 01.

"Fomu zote zitakuwa zinapatikana hapa na mwisho wa kuchukua ni Julai 01 na kisha watafanya mchakato wa mabadiliko ua katiba na kisha kueleka siku ya uchaguzi ambapo utafanyika hapa hapa Jijini Dar es salaam ila sehemu husika haijajulikana bado,"amesema Najaha.

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi

$
0
0
Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi.

"Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume)

"Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa kuwapo," alisema Msangi.

Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu wote.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images