Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1264 | 1265 | (Page 1266) | 1267 | 1268 | .... | 3272 | newer

  0 0

  WAAMUZI WA MECHI ZA JUMAPILI
  Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.

  Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
  Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
  Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba  ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
  Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
  Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
  Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.
  MZAMBIA KUWAAMUA YOUNG AFRICANS, 
  TP MAZEMBE
  Mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.

  Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.

  SUALA LA STAND UNITED YA SHINYANGA
  Kutokana na mkanganyiko wa uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi katika Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF), limeagiza michakato yote miwili inayoendeshwa sambamba ndani ya klabu ya Stand United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo mengine.

  …………………………………………………………………….
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA


  0 0

  Wizara ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi. 
  Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika  kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
  Alisema Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa  kuwajengea miundombinu rafiki sehemu za kazi ili  kuongeza ufanisi kazini.
  "Wizara pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake" . Alisisitiza James
  Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa  bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
  Kwa upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.
  Maadhimisho hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla katika maeneo yao ya kazi.
  Imetolewa na:
  B. Mwaipaja
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo akiongea na watumishi wa wizara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James 
   Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
   Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifanya sala wakati wa kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
   Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
  Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja. Hapa baadhi yao wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang wakibadilishana mawazo leo  kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo  leo kabla ya kuanza  kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za  Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.

  Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.

  0 0


  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) kulia akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India, Bw. Amar Sinha alipokuja kumtembelea Ofisini kwake na Kufanya naye Mazungumzo kuhusu umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na India.
  Mhe. Waziri akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambapo walijadili namna Tanzania na India zitakavyoweza kushirikiana katika sekta mbalimbali kama vile uwekezaji, elimu, afya, TEHAMA na ufundi.
  Bw. Sinha akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo.
  Mhe. Waziri akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India zawadi yenye picha za wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi za taifa hapa nchini.


  0 0

  Na Sixmund J. Begashe
  Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, imefungua mlangoa kwa wasanii wa ndani ya nchi na marachache wa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuwapa nafasi wasanii wa wakitanzania kuibua na kuendeleza vipaji vyao kwa kufanya maonesho ya mara kwa mara katika kumbi za maonesho zilizopo katika Makumbusho hiyo.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure kwenye mazungumzo na muandishi wa habari hizi baada ya kikao walicho kaa na wasanii wa Ngoma za Ubunifu ambao hufanya kazi zao kimataifa na marachache ndani ya nchi .
  Bw, Bufure alisema kuwa kwa sasa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imeanzisha Progaram Maalumu inayoitwa MUSEUM ARTS EXPLOSION ambapo kila mwisho wa mwezi wasanii watapata nafasi ya kufanya Maonesho kwenye Ukumbi wa kisasa wa Makumbusho hiyo na kwa mwezi huu wa Juni Wasanii wa Kimataifa Bw Aloyce Makonde na Bw Isack  Abeneko pamoja na wasanii wengine watafanya onesho kubwa siku ya tare 24 jioni. 
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti Bw Aloyce Makonde na Bw Isack Abeneko wameitaja program iliyo anzishwa na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kuwa ni ya kizalendo na itarudisha heshma ya kazi za sanaa na wasanii kwenye fikra za watanzania na ulimwengu kwa ujumla.

  ‘’Naipongeza sana Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha program hii, kwa sababu kilikuwa ni kilio cha muda mrefu cha wadau wa sanaa na wasanii nchi kutokuwa na sehemu yenye heshma zaidi itakayoweza kuwakutanisha wasanii na wapenzi wa sanaa zenye asili ya utamaduni wa kitanzania, lakini kilio hicho kimefutwa machozi na serikali kupitia Makumbusho ya Taifa na ninaomba program hii iwe endelevu” Alisema Bw Makonde.
  Nae Bw, Abeneko aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa watanzania kuona sanaa zenye ubora zaidi kupitia ukumbi wa Kisasa wa makumbusho hiyo kwani niimani yake kuwa wasanii wote watajiandaa vya kutosha kabla ya kupandisha kazi zao kwenye stage hiyo ya kisasa hapa nchini. “Hivi juzi mimi nilikuwa Ujerumani kwa maonesho ya takribani mwezi mzima, nimeona namna sanaa yenye vionjo vya utamaduni wetu inavyo pendwa na kuheshimiwa huko nje, naamini kwa mlango huu sasa watanzania nao watapata nafasi ya kuidhamini” aliongeza Bw Abeneko.
  Bw. Bufure ametoa wito kwa wasanii na watanzania wote kujitokeza siku ya Tarehe 24 June saa moja jioni kushuhudia onesho hilo la Contemporary Dance litakalofanywa na DANCE GARGE chini ya Msanii Aloyce Makonde na Isack Abeneko, kama onesho la ufunguzi wa program hiyo ambapo kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= (elfu kumi) kwa wakubwa na wanafunzi Ths 5000 (elfu tano) 
   Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bw Achiles Bufure, akifafanua jambo kwenye Mkututano na wasanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu na Muziki, awapo pichani.
   Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bw Achiles Bufure, pamoja na wajumbe wa kikao wakisikiliza kwa makini ufafanuzi kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa ngoma za Ubunifu na Muziki Bw Isack Abeneko (walipi kushoto) kwenye Mkutano maalum wa maandalizi ya Onesho la sanaa litakalofanyika Tar 24 June 2016  kwenye Ukumbi wa Makumbusho Posta mjini Dar es Salaam.
   Msanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu Bw Aloyce Makonde akifafanua jambo kwenye Mkututano na Uongozi wa MakumbushonaNyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
  Msanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu na Muziki wa asili Bw Isack Abeneko akifafanua jambo kwenye Mkututano na Uongozi wa MakumbushonaNyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

  Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (pichani) ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.
  Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.
  "Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo"Alisema Dkt. Mpango
  Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria
  Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.
  "Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa" Aliongeza Dkt. Mpango
  Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje
  Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha
  Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.
  Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.


  0 0

  Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania (DPP), ameiondoa mahakamani rufani aliyoikata dhidi ya Mawaziri Waandamizi wa zamani, wa Fedha Basil Mramba na wa Madini Daniel Yona iliyopangwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani Tanzania.

  Rufani hiyo iliondolewa jana kabla ya kuanza kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na Profesa Ibrahim Juma.
  Mapema Juni 20, mwaka huu, DPP aliwasilisha kusudio la kuondoa rufani hiyo chini ya kanuni ya 77(1) ya Mahakama ya Rufani pamoja na nakala kuwakabidhiwa kwa mawakili wa utetezi.
  Hata hivyo, jopo hilo lilisema kwamba kifungu alichokitumia DPP kuwasilisha kusudio hiyo siyo sahihi kwa kuwa kinatumika kabla ya shauri halijapangwa kusikilizwa.
  Jaji Mbarouk alisema DPP alitakiwa kutumia kanuni ya 4(2)(a) ya Mahakama ya Rufani kuomba kuondoa rufani hiyo.Mawakili wa Serikali Waandamizi, Theophil Mutakyawa na Shadrack Kimaro, walieleza nia ya DPP ya kuondoa rufani hiyo, jambo ambalo halikuwa na pingamizi kwa upande mwingine.

  Jopo hilo lilikubali maombi ya kuondoa rufani hiyo. Mapema mahakamani hapo DPP alikata rufani kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 2, mwaka 2015 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi chini ya Jaji Projest Rugazia.

  Jaji Rugazia alisema mawaziri hao walitakiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na siyo miaka mitatu kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ilivyowahukumu,dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka.Kadhalika, Jaji Rugazia alikubaliana na hukumu ya kumwachia huru Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

  Hata hivyo, DPP alikata rufani Mahakama Kuu, kupinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwamba ni ndogo kwa sababu jopo la mahakimu watatu waliotoa hukumu hiyo walikosea kumwachia huru Mgonja.

  Mbali na kupinga adhabu hiyo, DPP aliomba mahakama kuwaamuru washtakiwa kulipa fidia ya fedha walizosababisha hasara.Mahakama ya Kisutu, iliwahukumu Mramba na Yona kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya sh. milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
  Kwa sasa mawaziri hao wanatumikia kifungo cha nje baada ya kupendekezwa kuwa miongoni mwa wafugwa wanaohitaji kumalizia sehemu ya kifungo chao wakiwa nje, ikiwamo kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokea Mwenge wa Uhuru toka kwa Mkuu wilaya ya Mufindi Jolwika Kasunga katika kijiji cha Ikungwe kata ya Wasa tarafa ya Kiponzelo. 
  Mwenge huo ambao ulikimbizwa zaidi ya Km 11.5 katika vijiji 7, kata 4 na tarafa 2. katika mbio hizo jumlay amiradi 5 ya wananchi ilizinduliwa, miradi 5 ya vijana ilizinduliwa pia klabu 2 za Rushwa na mapambano ya madwa ya kulevya harikadharika vilizinduliwa. 
  Kiasi cha shilingi milion 15 zilitolewa kwa vikundi 5 vya vijana kama ilivyo kauli mbiu ya Mbio za Mwenge mwaka 2016 VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA WASHIRIKISHWE NA KUWEZESHWA. 
  Taarifa yake Mkuu wa wilaya Iringa pamoja na risala ya Utii kwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh Kasesela alisema Halmashauri ya Iringa vijijini imetenga hekali 198 kwa ajili ya shughuli za maendeleo za vijana, katika vijiji 10 kwa ajili ya ujasiliamali. 
  Halmashauri imefanikisha  vijana 1321 kupata ajira kwenye miradi ya kijamii, 1230 walipata ajira zilizo tokana na wazabuni hasa hasa wa ujenzi wa barabara na miundo mbinu ya mwaji. sambasamba na hilo pia vijana 28, 783 wamewezeshwa kujiajiri ambapo wengi ni katika kilimo. 
  Mwenge ulifanikiwa kuonwa na kuguswa na watu karibu 1880 kwa kadirio la haraka. Mwenge wa uhuru ulilala Ifunda ambapo mkesha wa Mwenge uliudhuriwa na watu karibu 300 mpaka asubuhi. 
  Kivutio kikubwa kilikuwa watoto wa halaiki walivyoonyesha ukakamavu . Mwenge ulikabdhiwa wilaya ya kilolo kuendelea na mbio hizo. Unatarajiwa kurudi Iringa Manispaa tarehe 22/06/2016 na kupokelewa tena na Mh Richard Kasesela eneo la Tagamenda saa 2 asubuhi.
   Mh Jolwika Kasunga DC wa Mufindi akimkabidhi DC wa Iringa Mh Richard Kasesela Mwenge wa uhuru.
   Mwenge ukianza mbio rasmi Iringa
   Mzee chavala ambaye ni mstaafu aliwahi kufanya kazi na Bwana George Mbijima mkimbiza mwenge Taifa.
   Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwapagaisha wananchi wa Ifunda kwa kuchana mistari na kuzindua wimbo alioshirki kuimba wa Mwenge Tanzania alioimba na msanii D Money. Vumbi lilitimka vilivyo.


  0 0
  0 0

  Dkt.Jim James Yonas   0 0


  0 0


  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
   Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa kwenye mkutano huo. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.

  ·         Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka  chakula mara tatu kwa siku.
  ·         Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.
  Kwanini Hospitali imechukua hatua hii
  Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

  “Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” amesema Bw. Aligaesha

  0 0

   As part of its mission to digitalize Tanzania, Vodacom Tanzania has today announced that all smart phones including iOS and feature phones can now access its M-Paper platform that allows its customers to read newspapers and magazines on their phones at nearly half a price.Previously the M-Paper application could only accommodate Android phones. With M-Paper, Vodacom Tanzania is aiming to digitalize the way of accessing information in real time by enabling people to read any newspaper and magazine of their choice from first to last page at their fingertips at anytime.
  The application, which was developed by Smart Codes in partnership with Vodacom Tanzania can be downloaded for free on any App store or the web platform www.mpaper.vodacom.co.tzAfter downloading the app,selected newspaper or magazine one chooses to read can be paid for via M-Pesa or airtime, while for those outside the country can pay for the service with their debit or credit cards. 
  “Vodacom Tanzania has once again managed to use innovation to simplify life of Tanzanians with the introduction of this incredible platform. Once you download the M-Paper app on your phone you can read all your favourite newspapers at half a price anywhere all you need to do is download the app in your phone,” said Matina Nkurlu, Vodacom Tanzania Public Relations Manager.
  He said the app now has more than 52 newspapers and magazines which people can choose to read at nearly half a price of the hardcopy and even cheaper if they opt to buy via daily, weekly or monthly subscriptions available. 
  For his part, Smart Codes Chief Executive Mr. Edwin Bruno said they decided to partner with Vodacom Tanzania to develop the M-Paper app after seeing how much Vodacom has been thriving in applying technology to provide solutions and give their customers the best services.“We live in fast paced world where technology  has changed how we do things- almost everything being digitalized, therefore, our partnership with Vodacom Tanzania to develop the M-Paper app and make the service available to all smartphones is our way of using innovation to better the flow of information,” said Mr. Bruno
  About M-Paper
  M-paper is your personal digital newsstand. M-paper allows you to read all Tanzanian newspapers and magazines in the exact same way you would read them in hardcopy: from the first to the last page.  All newspapers and magazines are sold for nearly half the retail price. 
  We are happy to announce that,
   M-Paper is now officially launched!
  "As part of its mission to digitalize Tanzania, Vodacom Tanzania has today announced that all smartphones including iOS and feature phones can now access its M-Paper platform that allows its customers to read newspapers and magazines on their phones at nearly half a price.Previously the M-Paper application could only accommodate Android phones."


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.(PICHA NA OMR).
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.

  Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.

  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.

  Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  ZIKIWA zimesalia  siku saba kwa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza(FDL) pamoja na daraja la pili(SDL) kuweka wazi wachezaji wanaowaacha kuelekea msimu ujao wa ligi kwa mujibu wa kalenda iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa Miguu nchini(TFF) inaonesha kuwa kuanzia Juni 15 hadi 30 timu hizo zinatakiwa kuweka wazi wachezaji wanaowaacha kwani jambo hilo ni muhimu ambalo linaweza kuwapa fursa timu nyingine kusajili wachezaji waliotoka ndani ya timu hizo kama wanawahitaji.

  Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas (Pichani) amesema kuwa hadi sasa hakuna timu iliyotoa majina ya wachezaji waliowaacha kwani siku zilizobaki ni saba tu hivyo timu zinazishiriki FDL na SDL zinatakiwa kufanya zoezi hiyo mara moja kabla ya juni 30.

  Amesema baada ya kumalizika kwa mapumziko yaliyomalizika Juni 10 kipindi kilichofuata ni usajili kilichofunguliwa Juni 15 huku kikitarajiwa kumalizika Julai 30. "Kwa mujibu wa Kalenda tuliyoitoa inazitaka timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15 hadi Juni 30 ili kuwapa fursa ya kuchukuliwa na timu nyingine", amesema Alfred.

  Akizungumzia timu kutoka Ligi kuu timu zilizoshuka daraja ambazo ni Coastal Union, African Sports na Mgambo JKT zote za Jijini Tanga amesema kuwa katika ratiba pia iliyotolewa timu hizo zimewekwa makundi tofauti huku kila kundi likibeba timu nane. Huku kundi A likiundwa na timu za Abajalo ya Dar es Salaam, African Sports ya Tanga,  Ashanti United ya Dar es Salaam, Kiluvya United ya Pwani, Friends Rangers ya Dar es Salaam, Lipuli  ya Iringa, Mshikamano FC ya Dar es Salaam na Polisi Dar ya Dar es Salaam

  Kundi B lina timu za JKT Mlale ya Ruvuma
  Coastal Union ya Tanga, Kimondo FC ya Mbeya, Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam Kurugenzi ya Iringa, Mbeya Warriors ya Mbeya, Njombe Mji ya Njombe na Polisi Morogoro  ya Morogoro na Kundi C linabeba timu za Alliance Schools ya Mwanza, Mgambo Shooting ya Tanga, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya Dodoma, Polisi Mara ya Mara, Rhino Rangers ya Tabora na Singida United ya Singida.

  0 0

    Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia  magari katika bandari ya Dar es Salaam.
  Habari Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  KUTOKANA na mkanganyiko wa uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi katika Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF), limeagiza michakato yote miwili inayoendeshwa sambamba ndani ya klabu ya Stand United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo mengine. 

  Hilo limekuja baada ya kuwa na sintofahamu kwa pande mbili tofauti kufanya uchaguzi kwa  nyakati tofauti moja ikiwa Kampuni na wengine wakijiita wanachama wa Stand United.

  Akizungumza na Globu hii, Mkurugenzi wa Ufundi Muhibu Kanu kwa niaba ya Stand United Kampuni amesema kuwa wamesitisha uchaguzi huo mpaka pale watakapopewa angalizo na TFF kwani wao wanafahamu mchakato mzima jinsi ulivyo ndani ya klabu hiyo pamoja na hao wanaojiita wanachama. "Tumepokea barua kutoka TFF ikituambia kuwa tuache mchakato wa uchaguzi na sisi tumetii kwani tunachofahamu sisi ndiyo wenye haki na mamlaka zaidi tunachosubiri ni maamuzi yao".

  Kanu amesema, baadhi ya watu hawaitakii mema klabu hiyo zaidi wanachotaka ni kuona  ni kila siku kuwa katika migogoro itakayokuwa haina manufaa na kudhoofisha maendeleo, kitu ambacho si kizuri na wanachotakiwa ni kuacha uongozi unaotambulika kufanya kazi yake kwa ufasaha  na kuitoa timu mahala ilipo na kuipeleka juu Zaidi.

  "Wanachoona ni kuwa timu imepata mdhamini na ametaka kuleta maendeleo kwenye klabu yetu wanaanza kujitokeza kwa kuanzisha mchakato wa uchaguzi na wakijiita wanachama wa Stand ilihali kuwa wanafahamu kuwa kwa sasa tumesajili kama kampuni na wale wanachama wote wa halali tulioanza na timu tulikaa chini kwenye mkutano mkuu na kukubaliana kwa pamoja,"amesema Kanu.

older | 1 | .... | 1264 | 1265 | (Page 1266) | 1267 | 1268 | .... | 3272 | newer