Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1263 | 1264 | (Page 1265) | 1266 | 1267 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Kama mojawapo ya makampuni ya Afrika yanayoongoza katika sekta ya burudani za video, MultiChoice inatambua kwamba rasilimali watu ni kitovu cha simulizi ya mafanikio yake-ndio maana inawekeza sana katika kutafuta, kuendeleza na kunoa watu bora kabisa katika sekta. 

  Kama kampuni ya kimataifa, falsafa yetu ya kufikiri kimataifa na kutenda kwa ndani ya nchi inaungwa mkono na programu za kuendeleza utendaji wenye nguvu na sera ambazo zimejizatiti katika kuendeleza biashara za ndani na kuajiri watu kutoka miongoni mwa vipaji vilivyolelewa na kukulia nchini. 

  MultiChoice Tanzania inayo furaha kutangaza uteuzi wa Bw. Maharage Ally Chande (pichani) kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania. 

  Chande anajiunga na familia ya MultiChoice baada ya hapo awali kushika wadhifa wa Mkurugenzi Wa Huduma Za Taasisi katika Ofisi Ya Rais-Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi ( President’s Delivery Bureau).

  Mwenyekiti wa MultiChoice Tanzania, Bw.Ami Mpungwe, akiidhinisha uteuzi huo amesema; “MultiChoice Tanzania inaona fahari kuhusu uteuzi huu- hakuna shaka kwamba Bw.Chande ni miongoni mwa watanzania watendaji bora kabisa na anakuja pamoja na uzoefu mkubwa katika masuala ya usimamizi  wa taasisi. 

  Sifa zake kama mtaalamu wa huduma za kibenki na kifedha pamoja na tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ni ujuzi tunaouhitaji katika biashara yetu ili kuipeleka biashara ya Tanzania katika viwango vipya vya hali ya juu. 

  Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya na bila shaka atawahudumia wateja wetu wa DStv kwa nguvu na juhudi mpya.” Bw.Chande ni mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu MultiChoice Tanzania.

  Maharage amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiutendaji kama Afisa Mtendaji Mkuu katika Benki Ya Taifa Ya Biashara(National Bank Of Commerce) kampuni tanzu ya Barclays/ABSA-na pia kutekeleza majukumu ya Meneja Mtendaji wa Tekinolojia na Mawasiliano, Data na Huduma za Ongezeko la Thamani. 

  Ana shahada ya Sayansi katika Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu Cha Afrika Kusini.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BAADA ya kutokutumia jezi zenye mdhamini wao bia ya Kilimanjaro, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limetolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo kwani kutokana na kanuni za michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa timu yoyote inapoingia kwenye hatua ya makundi (nane bora) haki za udhamini za timu zote zinahamia kwa shirikisho hilo kwahiyo wadhamini wote wanatakiwa kuingia makubaliano na CAF na sio klabu tena.

  Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amefafanua hayo mapema leo na kusema kuwa Yanga hawakwenda kwenye vikao vya awali vya timu zilizoingia kwenye hatua ya makundi na ndiyo maana hawakulifahamu hilo ila kwa sasa kama mdhamini atataka aendelee kuweka nembo atatakiwa kukaa chini na CAF na kukubaliana. “Timu yoyote ikifika hatua ya makundi haki za udhamini zote zinahamia kwa CAF, na zaidi Yanga wanaweza kuendelea kutumia jezi zao mpya kama Bia ya Kilimanjaro hawatataka kuweka nembo yao tena.”

  Kwa upande wa klabu ya Yanga, Mkuu wa kitengo cha Haabari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa mkataba wao na Bia ya Kilimanjaro unaelekea ukingoni kwaniyo ni uamuzi wao kutaka kuendelea nao au kuangalia uwezekano wa kupata kampuni nyingine itakayokuwa na maslahi zaidi na itakayonufaisha klabu yao. 

  Amesema wakati wanaenda nchini Algeria hawakuwa wanafahamu kuwa kama kuna mabadiliko ya jezi kwani hawakwenda kwenye kikao cha awali cha timu zilizoingia kwenye hatua ya makundi.”

  Kutokana na kutokujua mabadiliko ya kanuni za CAF kuwa haki za udhamini zinahamia kwao kwahiyo klabu yoyote haitaruhusiwa kutumia nembo ya mdhamini mpaka watakapokubaliana nao, hata hivyo udhamini wetu unamalizika na Bia ya Kilimanjaro na tutaangalia maslahi zaidi,”.

  Mpaka sasa yameshajitokeza makampuni mengi sana na zaidi bado wapo kwenye mazungumzo na masuala yote yakia yamekamilika basi atawataarifu mashabiki na wanachama wa Yanga kuhusiana na ujio mpya wa mdhamini.

  Yanga kwa sasa watatumia jezi hizo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na lina uwezekano wa kuzitumia mpaka kwenye ligi kuu msimu ujao. Jezi hizo kutoka kampuni ya Macron zinazotengenezwa nchini Italy limeingia mkataba na Yanga wa kuwavalisha kuanzia sasa huku ikiwa inawavalisha mabingwa wa kihistoria Afrika Zamaleck ya nchini Misri.

  Muro amesema, wanataka kuwa tofauti na wengine kuanzia mavazi hado utofauti wa kuendesha timu yao kwani hadi sasa wao ndiyo wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na Kati na wanataka kuhakikisha wanafika mbali zaidi na kuweka historia nchini. Ukiachilia mbali hilo amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu yao kuelekea mchezo wao wa pili dhidi ya Tp Mazembe utakaopigwa Juni 28 Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Central Banks Governors from the MEFMI region in a group photo during the Governors Annual Forum held at the Bank of Tanzania in Dar es saaam on Monday 20 June 2016. The event was attended by up to 40 officials comprising 13 Central Bank Governors and Deputy Governors from the MEFMI region, technical experts from Investec Asset Management and the Bank for International Settlements (BIS) in Basel, Switzerland.  The Forum was held back to back with the Bank of Tanzania Golden Jubilee celebrations on 22 June 2016.


  0 0  0 0


  0 0


  0 0

   Wananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 359 DFQ iliyodaiwa kuacha njia na kuparamia daladala namba T 797 DEW eneo la Buza Njia Panda ya Kitunda jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika ajali hiyo watu wawili waliokuwa kwenye Noah hiyo waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
   Noah hiyo ikiwa kwenye mtaro baada ya kutokea ajali hiyo.
   Daladala lililogongana na Noah hiyo likiwa eneo la tukio.
  Wananchi wakiwa eneo la ajali hiyo.
  Picha na Dotto Mwaibale

  0 0

   Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (katikati) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Chacha Wanyancha (kulia) muda mfupi baada ya kufunga mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi hilo yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa jana.  Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa. Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kulia) na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Chacha Wanyancha wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa.  Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua, (wa tatu kushoto) akimkabidhi Cheti Koplo Agnes Amede baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa jana.  Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa, (wan ne kushoto); Mkuu wa Kambi ya JKT Mafinga, Luten Kanali, Hamis Maiga (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mafunzo wa JKT, Kanali Chacha Wanyancha (kushoto).  Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa hafala ya kukabidhi zawadi kwa kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
  Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" akiwa katikapicha ya pamoja na mshindi aliyejishindia simu aina ya iphone 6, Barbara Hassan (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia).
  Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto), akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kwanza wa Kampeni ya "Shinda na TemboCard" kwa upande wa wateja, Ismail Jimroger wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

  0 0

  jame1
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na mfuko huo katika huduma zake mbalimbali nchini kwa jamii Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
  jame2
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
  ...
  NA HASSAN SILAYO
  Mfuko wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo walisajili wanachama 23,228.
  Hayo yamesemwa na Meneja wa Elimu na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe wakati na mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Bw. Mlowe alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye wigo mpana na kugusa moja kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga kufikia wanachama 180,000 kufikia mwezi June 2016.
  Mlowe aliongeza kuwa miongoni mwa sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka 2014/2015 ni Walimu ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na uokoaji wanachama 851, Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza wanachama 205.
  Aidha Bw. Mlowe aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo ulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9, ambapo wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286 billioni kufikia mwezi Juni 2016.
  Pia Mfuko huo umesajili waajiri wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na unategemea kuendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo kuendelea kuboresha huduma zake.

  0 0  Na Woinde Shizza,Arusha
  CHUO cha ufundi Arusha, ATC, kinatarajiwa kukamilisha matengenezo ya Helkopita na kuirusha angani mapema mwaka 2018 na kuwa ni chuo cha kwanza nchini kurusha Helkopita iliyotengenezwa na Mhandisi mzawa.

  Hayo yameelezwa na Mhandisi wa ufundi aliyebuni na  anayetengeneza Helkopita hiyo, Abdi Mjema, kwenye hafla ya chuo hicho kukabidhiwa maabara ya maji mwendo ambayo imejengwa na serikali ya Japan,kupitia shirika lake la misaada la JICA, chuoni hapo.

  Mhandisi Mjema amemwambia katibu mkuu wa wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi, kuwa matengenezo ya Helkopita hiyo ambayo ameibuni yamefikia asilimia 40, na anafanya matengenezo hayo kwa kuwasiliana na mamlaka ya viwanja vya ndege kwa kila hatua anayofikia.

  Amesema hatua ya majaribio ya kuirusha Helkopita hiyo ambayo inatengenezwa kwa malighafi za nchini anatarajia kuyafanya wiki tatu zijazo  mara baada ya kukamilisha hatua iliyopo sasa ambapo ni 40% ya matengenezo na ambapo utengenezaji wa Helkopita hiyo anatarajia kuukamilisha mwishoni mwa mwaka 2017.
  Mjema, ambae ni mtaalamu wa mitambo aliyebobea  pia mhadhiri wa chuo hicho cha serikali cha ufundi,amesema wazo hilo la kubuni Helkopita hiyo aliibua kutokana na changamoto za usafiri zilizopo nyumbani kwao wilayani Mwanga, ambayo eneo kubwa ni milima na wakati wa masika maeneo mengi huwa hayafikiki.  0 0

   Baadhi ya watumishi na watendaji wa Wizara ya Ardhi, wakimsikiliza Katibu Mkuu Dtk. Yamungu akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwake na watumishi hao kama sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
   Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt. Yamungu Kayandabila akisisitiza jambo kwa watumishi wa wizara hiyo, alipokutana nao katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016. Dkt Yamungu alipokea kero mbalimbali kutoka kwa watumishi hao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
  Mtumishi Beatus Kashangaki akitoa kero zake kwa Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

  0 0

  Na Lilian Lundo – MAELEZO - DODOMA

  Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha bajeti ya shilingi Trilioni 29.5 ya mwaka wa fedha 2016/17 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango June 08, 2016.

  Bajeti hiyo ilipigiwa kura na wabunge waliokuwepo bungeni, ambapo jumla ya wabunge 251 walipiga kura za ndio za kuipitisha bajeti hiyo kati ya wabunge 252 waliokuwepo ukumbini wakati  kura hizo zikipigwa.

  Katika kupiga kura  Hakukuwa na kura yoyote ya hapana au kutokuamua kati ya wabunge waliopiga kura. Jumla ya wabunge 137 hawakuwepo wakati kura zinapigwa.

    “Naipongeza Serikali kwa kutoa hoja ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 na kupitishwa  na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, namtakia Waziri wa Fedha kila la heri katika hatua zinazofuata katika utekelezaji wa bajezi hii,” alisema Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

  Aidha bunge hilo, lilipitisha muswada wa sheria za Serikali kuidhinisha Trilioni 29.5 kwa matumizi ya Serikali kutoka mfuko wa hazina kwa mwaka unaoishia June 30, 2016.

  Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango  amewataka watanzania kulipa kodi na wale wote wanaotakiwa kusimamia ukusanyaji wa kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu ili fedha zilizopitishwa katika bajeti ya mwaka 2016/17.

  Sheria hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai 01, 2017.

   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
    Wabunge wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
   Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na watendaji wakuu wa bungu wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
   Mawaziri  na Wabunge wakimpongeza  Waziri wa Fedha  na Mipango Dkt. Philip Mpango  pamoja na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaju mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali ya Trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17 leo Bungeni mjini Dodoma.
  Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watano kutoka kushoto akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya fedha na Mipango  nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali, leo mjini Dodoma. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts Organization (WAAO).
  Katibu wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga (katikati) akieleza utendaji wa kikundi chao kwa watendaji wa masuala ya Sanaa na Utamaduni wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga. 


  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Naamala Samson

  WAZIRI mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda, amewahimiza vijana wa kitanzania kujishughulisha na kilimo na ufugaji wa kisasa ili kupata matokeo bora na kuinua kipato chao na cha taifa kwa ujumla.

  Mhe. Pinda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki shambani kwake katika kijiji cha Zuzu mkoani Dodoma alipotembelewa na umoja wa wajasiriamali vijana wa GO BIG MOVEMENT wapatao arobaini na mbili (42) waliokuwa katika ziara ya kujifunza kwa vitendo kuhusu ukulima na ufugaji wa kisasa. 

  Aliwahimiza vijana hao kutokata tamaa pindi wanapopata changamoto mbalimbali katika kufanikisha ndoto zao za kumiliki ardhi kubwa nchini na kuitumia kujiajiri na kuwaajiri wengine kupitia kilimo.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Mizengo Pinda akifafanua jambo kwa umoja wa wajasiriamali vijana wa GO BIG MOVEMENT, waliomtembelea shambani kwake katika kijiji cha Zuzu mkoani Dodoma.

  Akizungumza na vijana hao aliwaambia, “Makundi mengi yameshanitembelea hapa na kueleza changamoto zao lakini GO BIG MOVEMENT mmekuja kitofauti sana na kwa siku nyingi tangu nikiwa waziri mkuu nilikuwa natafuta vijana wa mfano kama ninyi” . Aliongezea kwa kusema, “Mna fursa nyingi sana za kufanya kilimo cha kisasa na hata ufugaji wa kisasa zaidi yangu kwani maarifa yapo nje nje na pia mtaweza kusaidiwa na serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha kupitia umoja wenu huu”.

  Katika ziara hiyo iliyochukua takribani masaa nane, vijana hao wakiongozwa na kiongozi wao Bw.Meshack Maganga , walipata nafasi ya kumuuliza maswali mbalimbali Mhe.Pinda na kisha kuzunguka katika shamba la ekari hamsini (50) lenye mazao mbalimbali kama vile mapapai, miembe, zabibu, migomba, maparachichi na viazi. Pamoja na kuona kilimo, waliweza pia kuona ufugaji wa nyuki, bata, kuku, ng’ombe, mbuzi , kondoo na hata uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia upepo na kinyesi cha ng’ombe “biogas”. 

  Aidha, waziri mkuu mstaafu alizidi kusisitiza vijana wa kitanzania kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili waweza kujikwamua kiuchumi. Vilevile katika ziara hiyo, Mhe.Pinda aliweza kuwakutanisha vijana hao na mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.Nehemia Mchechu ambaye nae hakusita kuwapongeza kwa kuthubutu kuanza safari ya kuwekeza kwenye ardhi hasahasa kufanya kilimo na ufugaji wa kisasa. 

  “Kiukweli ninaliona taifa la Tanzania likiwa linainuka na kufanikiwa kufuta umaskini kupitia kwenu. Na nitajitahidi kuwasaidia kadri niwezavyo ili muweze kutimiza ndoto zenu ikiwa hasahasa ya kumiliki ardhi na nyumba za bei nafuu kama ilivyo nia ya Shirika la Nyumba la Taifa” Aliongezea Bw.Mchechu.
  Baada ya kuzunguka shamba hilo, Mhe.Pinda aliwasisitiza vijana hao kuwa wajasiriamali wabunifu na wenye maono ya kuzalisha vitu vyenye ubora ili viweze kukidhi masoko ya ndani na ya kimataifa kwani tatizo lililopo ni wazalishaji kutofikia viwango vinavyotakiwa na walaji.

  Kwa upande wake Bw.Maganga alimshukuru waziri mstaafu huyo kwa kuwapokea kwa heshima kubwa na kuahidi kuendelea kujifunza daima kupitia wakulima, wafugaji na wajasiriamali wengine wakubwa. “Mheshimiwa waziri mkuu mstaafu tukuhakikishie tu haya tuliyojifunza kwako hatutayaacha yapotee, bali tutayafanyia kazi ili kuhakikisha tunajiinua kiuchumi na kuendeleza taifa letu.”

  0 0

  KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, 21 Juni, 2016)  wakati akijibu maswali ya watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma katika  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.

  Kila mwaka Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika  ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.“Nitafuatilia michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi wasihangaike,” amesema.

  Katika hatua nyingine Uledi amewataka Wakuu wa Idara kuandaa  mpango wa mafunzo kwa watumishi na washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa wakati.


  Pia mtumishi mwingine Ernest Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.
  KATIB1 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21,2016).  
  KATIB2 
  Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM  anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo  kwenye  kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
  KATIB3Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Aziz Mlima akiwa katika na mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India, Mhe. Amar Sinha, Mazungumzo hayo yalijikita katika kuboresha na kukuza mahusiano kati ya Tanzania na India hasa kwenye nyanja ya Viwanda ambayo itazalisha ajira kwa vijana na kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili.
  Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ally Kondo na Bi. Mercy Kitonga wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo hayo.
  Sehemu ya Ujumbe ulioambatana na Mhe. Sinha ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Mlima na Mhe. Amar Sinha. Wa kwanza kulia ni Baloizi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya.
  Mkutano ukiendelea. 
  Dkt. Aziz Mlima na Mgeni wake, Mhe. Amar Sinha wakiwa katika picha ya pamoja. 

  0 0

  East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: June 21, 2016: The second week of the sensitisation of stakeholders in the Partner States has commenced and will see EALA Members continue with its outreach to regional stakeholders.  The sensitisation activities which run up to the back-end of next week are themed: ”EAC Integration Agenda: Accessing the Gains”.

  Last week, the Members met a number of stakeholders.  In Kigali, the EALA Chapter led by the Chairperson, Hon Patricia Hajabakiga, addressed over 1000 representatives of the National Youth Council in Huye, Southern Province at the weekend. 

  A number of issues were raised at the outreach programme including youth involvement in strengthening of the integration process, with the Members urging the stakeholder group to take advantage of cross-border opportunities in the region.  Earlier on, the Chapter held an interactive session with representatives and the membership of the Private Sector Federation (PSF) Rwanda led by the Chief Executive officer, Stephen Ruzibiza.
  EALA Members with Hon Kahinda Otafire (2nd from right), Minister for Justice and Constitutional Affairs in Uganda. The Members are from left, Hon Frederic Ngenzebuhoro, Hon Dora Kanabahita, Hon Dr Martin Nduwimana and Hon Nusura Tiperu. On right of the Minister is Hon Bernard Mulengani.

  The PSF members urged EALA to ensure the total and complete elimination of NTBs on the corridors especially the Northern Corridor.  Last year, EALA enacted the EAC Elimination of Non-Tariff Barriers (NTBs) Bill 2015 and the piece of legislation is currently undergoing assent in the Partner States.


  0 0

  KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.

  Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, 21 Juni, 2016)  wakati akijibu maswali ya watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma katika  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.

  Kila mwaka Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika  ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.

  “Nitafuatilia michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi wasihangaike,” amesema.

  Katika hatua nyingine Uledi amewataka Wakuu wa Idara kuandaa  mpango wa mafunzo kwa watumishi na washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.

  Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa wakati.

  Pia mtumishi mwingine Ernest Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21,2016). Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1263 | 1264 | (Page 1265) | 1266 | 1267 | .... | 3278 | newer