Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1265 | 1266 | (Page 1267) | 1268 | 1269 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  BENCHI la Ufundi la Kikosi cha Yanga limeweka wazi kuwa hali ya beki wake wa kushoto Oscar Joshua aliyeumia katika mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia anaendelea vizuri na atarejea uwanjani tena Jumanne kukipiga na TP Mazembe huku beki wa kulia Juma Abdul anaendelea vizuri na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mepesi.

  Abdul alikosa mechi ya awali baada ya kuwa majeruhi kwa kuumia sehemu ya kifundo cha mguu na kuukosa mchezo wa kwanza na nafasi yake ikichukuliwa na Mbuyi Twite. Hata hivyo kwa sasa anaendelea vizuri na daktari ameweka wazi kuwa anaweza kuanza mazoezi na timu itakaporejea ataungana na wenzake.

  Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro (Pichani)amesema kuwa Joshua anaendelwa vizuri na watakaoukosa mchezo huo ni Beki wa kushoto Mwinyi Haji aliyepata kadi nyekundu pamoja na mshambuliaji Amisi Tambwe mwenye kadi mbili za njano alizozipata kwenye mchezo wa marudiano na Segrada Esperanca ya Angola na wa hatua ya makundi na Mo Bejaia.

  "Ni wachezaji wawili tu ndiyo watakaokosa mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao ni Mwinyi anayetumikia kadi nyekundu na Tambwe mwenye kadi mbili za njano, kwahiyo katika mchezo huo Oscar atarejea tena uwanjani na Abdul anaendelea vizuri ameanza mazoezi mepesi mepesi na pindi timu itakaporejea ataungana nao,"amesema Muro.

  Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika jiji la Antalya nchini Uturuki ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao utapigigwa Siku ya Jumanne Juni 28 na unatarajiwa kuwa wa ushindani wa hali ya juu hasa baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa awali na wakihitaji matokeo na TP Mazembe wakitaka ushindi ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe, Wilayani Kondoa.

  Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
  Mbunge wa Kondoa,Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara hiyo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.

  0 0

  Na Eliphace Marwa - Maelezo            
  Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) imeandaa utaratibu wa kutembelea wateja wake ambao  ni taasisi za umma ili kusikiliza na kutatua   changamoto  zinazo tokana na huduma wanazotoa,huduma hizo ni pamoja na mfumo wa barua pepe unaorahisisha mawasiliano  serikalini. 
  Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wataasisi hiyo Bi Suzan Mshakangoto, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salam na kutaja baadhi ya taasisi 34 zitakazoanza kutembelewa kuanzia tarehe 22 Juni hadi Juni 23.
  Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari,utamaduni Sanaa na  Michezo, Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika  Mashariki Kikanda na Kimataifa.       
  Aidha aliongeza kuwa huduma nyingine zinazotolewa  na wakala wa serikali ni pamoja na uhifadhi wa mifumo ya tovuti  za serikalini, utoaji huduma za simu za mikononi, Uratibu wa  mitandao serikalini, Ugawaji wa masafa ya internet, huduma za ujumbe mfupi wa maandishi (sms) pamoja na utengenezaji wa mifumo ya tovuti na usajili anuani  za tovuti.  
  Hiyo ni kutimiza Agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Angela Kairuki la kutaka kila Wizara, wakala na Taasisi za Serikali katika kipindi cha Wiki ya Utumishi wa Umma kukutana na wateja wao na kusikiliza kero walizonazo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi, aidha kauli mbiu ya mwaka huu ni, “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.
  Kila taasisi itatembelewa na wataalam  wawili wa wakala wa serikali watakao sikiliza maoni na kutoa  msaada wa kiufundi na ushauri wa kitaalamu katika kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeza juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na wakala.  
  Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Wakala wa Serikali Mtandao Bi Suzan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa taasisi yake kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya wiki ya Utumishi wa Umma.

  0 0

  Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo akimkabidhi vielelezo vya CCM vya matumizi ya Uchaguzi mkuu uliopita, kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Bashir Nkoromo)

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana,  na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.

  Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene.
  Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.
  "Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa ", alisema Mamilo.
  Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
  Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
  Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
  Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni  saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.

  0 0


    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni akizungumza na waandishi habari juu ya utapeli unaofanywa na watu kwa kutumia majina ya viongozi akiwemo, Waziri Mkuu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni hayupo pichani leo  jijini Dar es Salaam,.
  (Picha na Emmanuel Msaaka,Globu ya Jamii).

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  JESHI la Polisi Mkoa Ilala linamshikilia mkazi wa Pugu, Imarock  Paula Rutashabya ‘ Issa Mohamed Jiunga’ kwa tuhuma za kutumia jina la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kujipatia kipato kwa kupiga simu kwa watu wenye nafasi zao kwa kuomba fedha.
  Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es  Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema tukio hilo lilitokea Juni 16 mwaka huu maeneo ya mtaa wa Samora  Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
  Kamanda, Hamduni  amesema mtu alikamatwa baada ya kumpigia simu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jones Logistics LTD , James Rodrick Luponda  na kujitambulisha kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam lengo la kumsaidia kijana wake aliyepata ufadhili wa kusoma lakini anahitaji achangie asilimia 30 sawa na dola za Kimarekani 35,000 ya gharama za chuo kilichoko nchini Ufilipino baada ya kupata ufadhili wa asilimia 70.
  Amesema mtuhumiwa katika maongezi yake alimueleza mkurugenzi huyo kuwa fedha hizo atumie benki ya Eco akaunti Kenya au kutoa pesa taslim kwa  kumpa namba za simu 0717 338 473 ya kijana anayehitaji msaada kuwa atafika ofisini kwake baada masaa mawili akiwa na nyara zote za fursa ya hayo  masomo pamoja na akaunti namba ya benki alizozitaja.
  Mtuhumiwa alikamatwa na anahojiwa  ili kuweza kupata mtandao wake ambao wanatumia majina ya viongozi kujipatia kipato.
  Majina ya viongozi ambayo yanatumika kwa watu kujipatia kipato  kwa njia ya utapeli  ni Waziri Mkuu , Mkuu wa Mkoa na wengine na kuahidi wananchi kutoa ushirikiano dhidi ya watu wanaotumia majina hayo.

  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo
  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha  usafiri wa anga ili luleta huduma bora na kuwapa amani  wananchi wanaotumia usafari wa anga katika Jumuiya hiyo.
  Hayo yamesemwa  leo na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mheshimiwa  Makame Mbarawa alipokuwa  akifungua  Mkutano wa 19  wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es salaam. 
  “Mkutano huu unalenga kuadhimia kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa unahitajika sana kwa wananchi  ili kuongeza shughuli za kiuchumi na kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
  Ameongeza kuwa “ni lazima tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi zetu.”  
  Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo  Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma  za usafiri huo.
  “Ni lazima tuyafanyiekazi   maadhimio ya  mkutano huu  ili kuboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga” alisisitiza  Bw. Johari.
  Naye,  Mwenyekiti wa SADC Bw. Geoffrey Moshabesha amesema  kuwa  kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
  Jumuiya ya SADC imeweka  mikakati ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga kwa nchi wanachama.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
   Wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa hayupo pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa  akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) baada ya ufunguzi wa mkutano wa 19  wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Picha zote na Ally Daud- Maelezo.


  0 0

   Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti. tzNIC inapenda kuuarifu umma wa watanzania kuwa imetenga siku za Jumatatu (27 Juni 2016) na Jumanne (28 Juni 2016) kutoa elimu kwa umma juu ya kazi zake, manufaa ya matumizi ya majina ya kikoa cha dot tz (.tz domain names) na namna bora ya kuhama kutoka matumizi ya majina mengine ya vikoa kama dot com na dot org kwenda kikoa cha dot tz. Katika kipindi hicho tzNIC pia itapokea maoni mbalimbali juu ya uboreshaji  wa huduma zake na nini kifanyike ili watanzania wengi wasajili na kutumia majina ya kikoa cha dot tz kwa ajili ya biashara zao, huduma zao na matumizi binafsi. 
  Tukio hili litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa tzNIC, Ghorofa ya 8, LAPF Millennium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia saa 3 mpaka saa 10 jioni. Kabla ya tukio hili tzNIC itatoa maelezo ya utangulizi kupitia kipindi cha Jambo Tanzania (TBC) siku ya Ijumaa (24 Juni 2016) au Jumatatu (27 Juni 2016) asubuhi. 
  Kwa wale wa mikoani na watakaoshindwa kufika wanaweza kutupigia simu (022 2772659 au 022 2772660) au kutuandikia barua pepe kupitia manager@tznic.or.tz) au info@tznic.or.tz
   WOTE MNAKARIBISHWA

  0 0

   Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi
   
   Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi
   
   Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.
   
   Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki
   
  Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

  0 0


  0 0
  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa WKAC Tanzania Bi THEODOSIA NUHULO akiizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu ukandamizwaji wa wanawake hususani wajane nchini Tanzania ikiwemo sheria kandamizi ya mirati ya kimila nchini sheria ambayo imetajwa kuwaumiza wajane wengi 
  PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI
  Na Exaud Mtei

  Serikali ya Tanzania imetakiwa kufanya marekebisho makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo imetajwa kuwa ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa unawaelekeza wanachama kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za kisiasa,kiuchumi,na kijamii ili kuletwa usawa.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa yanayotetea haki za wanawake Tanzania kwa namna mbalimbali.
  Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo yote mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC ambao wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa mnamo mwaka 2005 WLAC  kwa kushirikana na wadau wengine watetezi wa haki za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya mirathi (Tamko la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006 ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni vya kibaguzi kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la kisheria.
  Mkurugenzi wa umOja wa wajane nchi i Tanzania ROSE SARWAT akizngumza na wanahabari wakati Tanzania ikiingia kuadhimisha siku ya wajene nchini ambapo amewataka wajene na watanzania kujitokeza kwa wiingi kesho katika viwanja vya mnazi mmoja kuadhimisha siku hiyo ili kupata Fursa ya kujadili kwa pamoja kuhusu haki zao hususani sjheria hiyo kandamizi kwa wajane.
  Ameeleza kuwa WLAC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali tena kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na tarehe mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.
  Amesema kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi ameeleza kuwa serikali ya Tanzania kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo kikubwa cha wanawake wajane nchini Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi zikiwemo za mirathi baada ya vifo vya wenzi wao
  Mkutano huo ukiendelea
  Bi Theodosia ameendelea kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali zinazofanywa na WLAC na wadau mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado serikali haijaonyesha jitihada za maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba wajane wanapata haki zao.Aidha WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea uwezo majaji na waendesha mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu mkataba wa CEDAW na umuhimu kwa kuzingatia haki za binadamu katika maamuzi yao.
  Pamoja na hayo WLAC wameitaka serikali kuchapisha taarifa hiyo ya kamati ya CEDAW na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila potofu dhidi ya wanawake na kuwatendea haki badala ya kuwanyanyasa kwa namna mbalimbali.
  Hata hivyo WLAC wameitaka serikali kutoa fidia ya kutosha kwa wajane waliohusika katika kesi mkakati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki zap.


  0 0

   WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mh. Issa Haji Ussi (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Welezo,Mh. Hassan Khamis Hafidh (kulia) na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Mh.Nassor Salim nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Chukwani Wilaya ya Magharib ‘B
  KAIMU Mkurugenzi wa Tume ya Uratibu Athasri na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya Dk.Mahmoud ussa,akifungua mafunzo kwa maafisa wa Chuo cha Mafunzo kujua athari za matumizi ya Madawa ya Kulevya,wakati wa wiki ya siku ya kupambana na madawa hayo Duniani.
   KAIMU Mkurugenzi wa Tume ya Uratibu Athasri na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya Dk.Mahmoud ussa,akifungua mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka,juu ya athari za matumiziya Madawa ya Kulevya,wakati wa wikiya siku ya kupambana na madawa hayo Duniani.
   Swali kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Chuo cha Mafunzo kujua athari za matumizi ya Madawa ya Kulevya,wakati wa wiki ya siku ya kupambana na madawa hayo Duniani.

  0 0


  0 0

  God Made Dutch and Dutch Made Holland!!!!

  1. Ni nchi ya kwanza kugeuza eneo la bahari kuwa eneo la makazi (Land Reclamation)
  ​ Yasemekana kwamba Uwanja wa Ndege wa Schipol uko Mita 4.5 chini ya usawa wa Bahari ​

  >2. Nchi Inayoongoza kwa kuwa na watu warefu zaidi duniani, wastani wa urefu wa wanaume ni sm 184 (karibu mita 2) ilihali wanawake ni sm 170
  ​. Inasadikika kwamba sababu kuu mchanganyiko wa vinasaba pamoja na unywaji wa maziwa kwa wingi ​tangu mwaka 
  400 AD. 

  >3. Nchi ya Kwanza Duniani Kuhalalisha Ushoga Mnamo Mwaka 2001

  >4. Nchi Yenye Idadi Kubwa ya Baiskeli Kuliko Hata Idadi ya watu, sensa ya mwisho inaonesha nchi hiyo ina Baiskeli milioni 18 sawa na zaidi ya baiskeli moja kwa kila raia
  ​. Kwa wastani wadachi huendesha baiskeli umbali wa km 2.5 kila siku sawa na km 900 kwa mwaka​

  >5. Nchi ambayo imehalalisha haramu nyingi kiasi cha kuwafanya watu wawe huru sana na hivyo kupunguza kama si kuondoa wafungwa kabisa. Hii ni nchi pekee ambayo imelazimika kuazima wafungwa toka mataifa mengine maana jela zao zipo tupu

  >6. Nchi ambayo wanawake hufurahia maisha kuliko nchi nyingine yoyote duniani kwa kupewa kipaumbele cha kwanza, wakifuatiwa na mtoto, Mbwa, Baiskeli na Mwanaume kipaumbele cha mwisho
  Inline image 2
  >7. Nchi yenye maduka ya ngono (sex shops) na vioski huru vya kuvutia bangi (maarufu kama coffee shops) ambapo unaingia na kuvuta bangi utakavyo kisha unarudi kitaa...yaani ukiingia coffee shop unakutana na menu za bangi tu
  ​ na watu wanavuta bila hata kupata mawenge​
  Inline image 1
  >8. Miongoni mwa nchi maarufu kwa starehe duniani kwani licha ya kuongozwa kwa unywaji wa pombe yao maarufu ya Heineken pia inachagizwa na kauli mbiu ya S 3 (SAND, SUN AND SEX)

  >9. Nchi inayoongoza kwa unywaji wa kahawa duniani (wastani wa vikombe 3
  ​ na zaidi ​
   kwa siku kwa mtu) sababu ni kwamba licha ya baridi kahawa inawafanya wasilale ili waendelee na starehe

  >10. Likizo ya uzazi ni siku 57 kwa wote baba na mama na inaweza kuchukuliwa muda wowote hadi mtoto anapofikisha miaka 8!!

  11. Ni moja ya nchi pekee duniani ambapo makaburi hukodishwa kwa kati ya miaka 5 hadi 10 kutegemea pochi lako na hii inatokana na uhaba wa maeneo ya kuzikia nchini humo 

  0 0

   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Utumishi na Utawala Bora,  George Simbachawene (wapili kulia)  na Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama   watatu kulia) bungeni mjini Dodoma Juni 22, 2016.  Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Babati Vijijini  Jitu Vrajlal Son, , Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Mbunge wa Korogwe Stephen Ngonya na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
     Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Utumishi, na Utawala Bora , George Simbachawene  (kulia) na Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei  Massay (kushoto) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wapili kushoto ni Mosses Kirway  na wapili  kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa ya  CCM, Thomas Lulu, wote  wakiwa ni wageni waliotembelea Bunge wakitoka Mbulu
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi kutoka jimbo la Ukongwa waliotembeklea  bunge  kwa mwaliko wa Mbunge  (wapili kulia)

  0 0

  Hi,
  This could be one of the poorest marketing mails you have ever received, but the intention is so simple.
  If you are looking for a job, simply click the link and apply for any position you qualify: https://adopto.eu/careers/jobs/qKVQxNAvwkSns0Rf-eJrfw
  I will be contacting only shortlisted candidates.
  Regards,
  Hilary
  Skype: hillieskom

  0 0

  Na Eliphace Marwa- Maelezo
  Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.
  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
  “Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.
  Balozi Maiga aliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi. 
  Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.

   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima  mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima  wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo


  0 0

   Will be happening on 24th June, 2016 this friday, at National Museum and House of Culture, Dar es Salaam from 07.00PM to 09.30PM

  Entrance fee is 10,000 TZS, and Students 5,000 TZS  and Tickets are available at Museum and House of Culture and Epidor Masaki.

  For more information please call/text the numbers: 0719083050 and 0714940690.

  Thanks and Regards 
  Museum and House of Culture.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na Madaktari  wa MNH  ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
  Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza  madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
  Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali na kufikia Shingili Bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
  Amesema kutokana na mafanikio hayo,  MNH imewaongezea madaktari  wake posho mbalimbali  ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali  imeamua  kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake  jambo ambalo awali halikuwapo.
  Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki  za wafanyakazi wake ikiwamo  pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.
  “ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
  Akielezea mipango ya MNH  Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
  Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH kesho Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru LEO amekutana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwasikiliza na kujibu kero mbalimbali.
   Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru baada ya kukutana nao LEO kwenye ukumbi wa CPL katika hospitali hiyo. 
   Madaktari Bingwa wakimsikiliza Profesa Museru LEO kwenye ukumbi wa CPL.
   Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo.
  Dk Moa akiuliza swali baada ya kupewa nafasi kwenye mkutano huo.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na  Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile (wa pili kulia) , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Zanzibar Mhe Khamis Mussa Omar (kushoto Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu (wa pili kushoto) , na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda  (kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Zanzibar Mhe Khamis Mussa Omar na kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua Kitabu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Bodi ya wakurugenzi wa BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1265 | 1266 | (Page 1267) | 1268 | 1269 | .... | 3272 | newer