Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

NEWS ALET: ZAIDI YA SIMU FEKI LAKI SITA ZAZIMWA USIKU HUU - TCRA

$
0
0
Zaidi ya simu 639,000  hadi sasa zimegundulikwa kuwa ni bandia na TCRA wameanza zoezi  endelevu la  kuzizima moja baada ya ingine usiku huu.
Kwa mujibu wa matangazo ya TBC yaliyorushwa live na kuhusisha maofisa wa TCRA wakiwa studio za  TBC  (kulia)  na  makao makuu ya TCRA barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam, ilipotimia  saa sita na dakika moja simu hizo laki sita zilikuwa zinaendelea kuzimwa.
Dawati la usiku la Globu ya Jamii linaendelea kufuatilia zoezi hili na litatoa updates kila zitapopatikana.

TOWN PLANNERS REGISTRATION BOARD: ANNOUNCING THE 3 RD ANNUAL GENERAL MEETING ON 14 TH – 15 TH JULY, 2016

MERCY KITOMARI, MJASIRIAMALI KIJANA ANAYETAKA KUMUONA ‘ROLE MODEL’ WAKE RAIS MAGUFULI.

$
0
0
Mjasiriamali kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari wakati akizungumza na Meneja Uendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige (hayupo pichani).

MJASIRIAMALI kijana na mmiliki wa Nelwa’s Gelato, Mercy Kitomari amesema anatamani kukutana na Rais John Pombe Magufuli kumwelezea haja ya kukutana na wanawake wajasiriamali vijana wamweleze matatizo yao.

Amesema Rais baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara , inafaa akutane na wajasiriamali wanawake vijana ambao wanapita katika magumu mbalimbali.

Alisema katika mahojiano hivi karibuni ambayo sehemu yake itachapishwa katika mtandao wa Modewjiblog muda wowote kwamba, rais Magufuli akiwa kama ‘Role Model wake’ katika kujituma, anaweza kuwasikiliza wanawake hao vijana na kusaidia kuwasukuma juu zaidi katika kampeni ya kuiweka Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

KOZI YA UKOCHA MWANZA YASOGEZWA MBELE.

$
0
0
KOZI ya ukocha Mwanza wa mpira wa miguu ngazi ya leseni C iliyokuwa ianze Jumatatu Juni 20, 2016 imesogezwa mbele.
Kozi hiyo iliyopangwa kutolewa kwa mtaala wa Shirikisho la Mpira a Miguu Barani Afrika (CAF) na kufundishwa na Mkufunzi wa CAF-Tanzania, Wilfred Kidao, sasa itafanyika kuanzia Agosti 8, 2016 na kufikia kikomo Agosti 22, 2016.

Sababu za kuahirishwa ni kuitikia  ombi la washiriki waliopo jijini Mwanza ambao ni zaidi ya asilimia 75 walituma maombi  Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuomba kusogezwa mbele kwa kozi hiyo kwa sababu za kutumikia vema Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
TFF imekubaliana na maombi yao na hivyo linaomba radhi washiriki wanaotoka nje ya Mkoa wa Mwanza kwa mabadilko hayo. Tunaomba washiriki hao kutoka nje ya Mwanza wasisafiri hadi Agosti, 2016.
Kwa washiriki ambao wamelipa michango yao kwa ajili ya kozi hiyo waendelee kusubiri isipokuwa kwa washiriki ambao hawajalipa michango yao walipe sasa na mwisho ni washiriki 40 tu kwani wakitimia idadi hiyo Idara ya Ufundi ya TFF, litafunga milango.
Hadi sasa waliolipa mchango wa Sh 200,000 kwa ajili ya kozi hiyo ni 29 hivyo nafasi zilizobaki ni 11. Kozi hiyo inaratibwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Vedastus Lufano ambaye anapatikana Mwanza.

WAENDESHA BODABODA WAFIKISHA FACEBOOK BURE KWA WATEJA WA AIRTEL SOKONI.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akiwa na waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda kabla ya kuingia sokoni kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Airtel wiki hii ilizindua huduma ya facebook bure inayowawezesha wateja wake kuunganishwa na ndugu jamaa na marafiki bure bila kuwa na haja ya kununua kifurushi chochote.
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akinyanyua bendera kuwaruhusu waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda kuingia sokoni na kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla.
 Helikopta maalum ikiruka angani na kusambaza ujumbe wa huduma ya facebook bure kwa wateja wa Airtel na watanzania ili kuwawezesha kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki  na kuendesha shughuli za kijamii, uchumi kupitia huduma ya facebook bila gharama yeyote.
Baadhi ya waendesha pikipiki jijini  Dar es Salaam maarufu kama Bodaboda wakiondoka makao makuu ya Airtel kuingia  sokoni kupeleka huduma ya facebook bure kwa wateja na watanzania kwa ujumla.

Tamasha kupambana na ukatili dhidi ya watoto kufanyika jijini Dar kesho.

$
0
0
Mwenyekiti wa taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) Bi Zainabu Makombe (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto. Wengine ni Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga (kulia) na Mwenyekiti wa taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden Bi.Victoria Lunderberg.

Taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) imeandaa warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho jumamosi ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliodhimishwa kote barani Afrika hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi Zainabu Makombe alisema warsha hiyo itakayohusisha baadhi ya taasisi zinazohusiana na utetezi wa haki za watoto itafanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke kuanzia majira saa 3 asubuni hadi saa 7 mchana.

“Ni kwa kushirikiana na wenzetu taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden tumeweza kuandaa shughuli hii. Tunarajia kwamba shughuli yetu itapambwa na mada mbalimbali za masuala ya afya na haki za watoto zitakazowasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya na mashirika kadhaa yanayohusiana namasuala ya watoto hapa nchini,’’ alitaja.

Aidha Bi Makombe alitowa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo sambamba na watoto wao ili wapate fursa ya kusikikiliza mada muhimu za watoto zitakazoambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga ambaye benki ni sehemu ya wadhamini wa warsha hiyo alisema benki hiyo imeamua kushirikiana na taasisi ya HCT kwa kuwa inatambua umuhimu wa watoto na haki zao ndani ya jamii.

“Si tu kwamba tunashirikiana nao katika kufanikisha maadhimisho haya bali pia tutaendelea kuwa nao pamoja katika mipango yao inayokuja kuhusiana na masuala ya watoto na haki zao...Exim tunaamini watoto ni sehemu ya wateja wetu leo na kesho,’’ alisema.

Mbali na Exim baadhi ya taasisi na kampuni zinazoshiriki katika kufanikisha warsha hiyo ni pamoja na Save the Children, PASADA, SOS, White Ribbon, GUTz, Coca Cola, AAR, YWCA na TTO. 

MTANZANIA MAKALA JASPER ATUNIKIWA TUZO NA NATIONAL GEOGRAPHIC SOCIETY

$
0
0

Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marekani akiwa na Bw. Makala Jasper alipotembelea ofisi za Ubalozi.


Bw. Makala Jasper, Mkurugenzi Mwandamizi wa NGO ya Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI) ametunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award forLeadership in African Conservation. 


Rais wa National Geographic Society Bw. Gary E. Knell  (kushoto) mara baada ya kumkabidhi Bw. Makala Jasper tuzo. Kulia ni Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na afisa wa taasisi hiyo.

Bw. Makala Jasper akitoa shukurani kwa kupewa tuzo.

TANZANIA NA SWEDEN ZATILIANA SAINI KUSHIRIKIANA KIMAENDELEO, MJINI DODOMA

$
0
0

 Benny Mwaipaja, WFM -DODOMA 

SERIKALI za Tanzania na Sweden zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka 4 kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2019 utakaojikita kuimarisha uchumi wa nchi na maendeleo ya watu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, utafiti, nishati jadidifu na kupambana na umasikini.

Tukio hilo limefanyika leo Juni 16, 2016, mjini Dodoma kati ya Katibu Mkuu na mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Sweden, Mhe. Ulrika Modeer.

Dkt. Likwelile ameeleza kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2019, Serikali ya Sweden itatoa ruzuku ya fedha za Kiswidi, SEK 5.5 Biln, sawa na shilingi Trilioni 1.42 za Kitanzania.

Amesema kuwa kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano huo kutafuatiwa na utiwaji saini wa mikataba ya kifedha ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika miradi kadhaa ikiwemo kusaidia Elimu, Maendeleo ya Jamii-TASAF, Utafiti, Nishati, Demokrasia, Haki za Binadamu, na Sekta Binafsi.

"Ushirikiano huu umelenga kusaidia kujenga mazingira ya maendeleo endelevu na kuwapatia Watanzania maskini fursa za kujikwamua katika umaskini kwa kujipatia ajira na kuweza kuanzisha biashara za kujipatia kipato ambapo vikundi vinavyolengwa zaidi ni wanawake, watoto na vijana" Alisema Dkt. Likwelile

Dkt. Servacius Likwelile ametoa wito kwa Serikali ya Sweden na nchi nyingine duniani kuwekeza katika biashara na vitega uchumi ili ziweze kunufaika na rasimali kubwa ambazo nchi imejaaliwa ikiwemo maliasili, ardhi yenye rutuba na jiografia ya kimkakati inayochochea uwekezaji na biashara

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ushirikianno na Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer, amepongeza uongozi mahili wa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupambana na vitendo vya kifisadi ikiwemo rushwa.

"Sweden inaunga mkono kwa nguvu zote hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli kupambana na mauvu nchini na tunaamini nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo" Alisistiza Modeer.

Mhe. Ulrika Modeer ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa fedha kupitia mfuko mkuu wa Bajeti ili kuwezesha kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa hifadhi ya mazingira, kilimo endelevu, kuwawezesha wananawake kiuchumi na kumsaidia mtoto wa kike na kiume kielimu.

"Tunataka kuona kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda sambamba na maendeleo ya wananchi wake ambapo tunaamini kuwa utafiti utasaidia kupata njia bora za kupambana na umasikini"Alisisitiza Mhe. Modeer

Amesema kuwa pamoja na nchi yake kutaka kuyasaidia makundi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu, wanataka kuona suala la demokrasia na utawala bora vinapewa kipaumbele katika mipango mbalimbali ya maendeleo

"Vilevile uwekezaji wetu mkubwa wa fedha katika maendeleo ya Taifa hautakuwa na maana sana kama suala la hifadhi ya mazingira halitapewa kipaumbele kwa kuanzisha miradi ya nishati jadidifu "Renewable energy" ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi: aliongeza Mhe. Ulrika Modeer

Uhusiano wa Tanzania na Sweden umedumu tangu mwaka 1960 ambapo katika kipindi chote cha miaka 50, serikali hizi mbili zimeshirikiana katika kubuni na kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo

Programu na miradi itakayotekelezwa katika ushirikiano uliosainiwa leo unaendena pia na Mpango wa Taifa wa Pili wa Miaka Mitano unaoanzia mwaka 2016/17 hadi 2020/21 na unalenga kuondoa utegemezi wa misaada kwa Tanzania. 


Katibu Mkuu Wizara ra Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa maendeleo wa miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka mine kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo, wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016.


NHIF MOROGORO WASHEREKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA ELIMU JUU YA FAO LA TOTO AFYA.

$
0
0
 NHIF Mkoa wa Morogoro washerekea siku ya Mtoto wa Afrika kwa Kutoa elimu juu ya fao la TOTO AFYA. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Morogoro Bi. Agnes Chaki akitoa maelezo  kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko huo , katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoa wa Morogoro.
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza wananchi  walifika kwenye banda la NHIF  Mkoani  Morogoro  kutoka  (kushoto) ni Afisa matekelezo Enock Humba, Agnes Chaki na Hamidu Mwambungu, katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Morogoro.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Agnes Chaki pamoja na Afisa matekelezo wa ofisi hiyo Bw. Enock Humba wakiendelea kuhamasisha wazazi juu ya umuhimu wa Fao la TOTO AFYA, katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Morogoro.

TEA KUJENGA NYUMBA 40 ZA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent (katikati), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa na Watumishi Housing Company katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. Kushoto ni Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa TEA, Julius Rugemalila. (Picha na Francis Dande)
Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati) akizungumza wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati), wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia), akibadilishana hati na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa wakipongezana.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

RC WA MWANZA MHE JOHN MONGELLA APOKEA GARI LA WAGONJWA

$
0
0
Na Atley Kuni RS Mwanza. 
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella amepokea gari la Wagonjwa kutoka kwa Surgical Rafiki Mission kwaajili ya kuhudumia wananchi wa mkoa huo ambalo amelikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekouture na kuwataka kuitunza kwa maslahi mapana ya wananchi wa mkoa huo. 
 Akizungumza kabla yakupokea gari hilo mkuu huyo wamkoa amesema, msaada walio upokea kutoka kwa Rafiki Mission ni masaada wakupigiwa mfano kwakuwa watu wengi wanabarikiwa vitu vingi lakini suala lakutoa misaada wameshindwa. 
RC  Mongella amesema kama mkoa ukipata marafiki wa aina ya Rafiki hawana budi kuwa ng’ang’ania wasiondoke kwenye himaya yao. 
“ Nafahamu hata sisi tunabarikiwa sana lakini hata siku moja hakuna mtu aliwahi kuleta hata mkasi, hivyo lazima tufahamu kutoa ni moyo na sio utajiri. Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amesema, karibu asilimia tisini ya matatizo ya afya yanayo ikabili jamii ya kitanzania yamejikita katika suala la afya ya mama na mtoto ambayo kama taifa tukifanikiwa kuwekeza katika hili, basi matatizo mengine ya afya yataondoka yenyewe 
“ Najua suala la mama na mtoto ni tatizo mtambuka kwa taifa, hivyo tukiwekeza zaidi katika afya ya mama na mtoto tutakuwa tumekabili changamoto kubwa ya masuala ya afya na itawawezesha wananchi kujikita katika shughuli za maendeleo”, alisema Mongella 
 Awali akitoa salama za Rafiki Mission, Balozi Issaya Chialo, alisema wao kama Rafiki Mission, wanatambua matatizo yanayo ikabili jamii ya kitanzania hususan masuala ya afya, na kwamba wao kama Rafiki Surgical mission, hawana ubaguzi katika utoaji wa misaada kwa jamii nzima ya kitanzania.
 “ Mkuu wa mkoa sisi shughuli zetu zipo katika mkoa wa Mtwara tukijikita katika zaidi katika utafutaji wa mafuta na Gesi, lakini hiyo haituzuii sisi kupeleka misaada pembe zingine za nchi na ndio maana leo tupo katika mkoa wako wa Mwanza” alisema Balozi Chialo na kuongeza kuwa, wanajisikia fahari katika hilo. Chialo ameutaka uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture kulitunza gari hilo la wagonjwa lenye thamani ya Mil. 40, ambalo litasaidia katika kuwakimbiza wagonjwa wenye mahitaji maaluma sehemu mbali mbali za mkoa huo na mikoa ya jirani. 
 Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Subi, amesema hivi sasa hospitali ya mkoa huo inakabiliwa na changamoto ya chumba cha kutolea huduma ya upasuaji kwa akina mama, ambapo mkuu wa mkoa amemtaka Mganga huyo wa mkoa kutenga kiasi cha Mil. 5 kutoka katika makusanyo ya ndani ya hospitali ya mkoa huo na Mkuu wa mkoa kupitia wadau wa maendeleo atahakikisaha kiasi kingine cha fedha kinacho salia kinapatikana kwaajili ya ukarabati wa chumba hicho ambacho kinahitaji Mil.20 ili kiweze kufanya kazi ya upasuaji kwa akina mama. 
 Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture, imekuwa msaada kwa wagonjwa wa mkoa huo na mikoa ya jirani kutokana na huduma zake kuwa nzuri na madaktari mabingwa wanaopatikana katika mkoa huo.



 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa mapokezi ya Gari la Wagonjwa kutoka Rafiki Surgical Mission.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akikabidhi cheti cha Shukrani kwa Balozi Issaya Chialo, kama sehemu ya shukrani kwa kutambua mchango wa Rafiki Surgical Mission, walio utoa kwa Mkoa huo wa Gari la Wagonjwa.
Hilo ndilo gari lililotolewa na Rafiki Surgical Mission.
(Habari na picha zote na Afisa habari wa mkoa wa Mwanza)

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO JIJINI TANGA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akimvisha nyota mmoja wa wahitimu 156 wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Gwaride la heshima likipita mbele ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasiara, wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa Mahafali ya kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uongozi Daraja la Pili , yaliyofanyika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo, Wilayani Handeni, jijini Tanga.Ambapo aliwaasa wahitimu kwenda kulihudumia Taifa kwa uadilifu.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

JK BALOZI WA HESHIMA MAENDELEO YA KILIMO, AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO.

KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasifiki.
Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.


Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018.

DAWA ZA MILIONI 294 ZILIZOKAMATWA KATIKA OPERESHENI ZAKABIDHIWA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.

$
0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea dawa kutoka kwa Msajili wa baraza la Famansia , Elizabeth Shakalaghe ambazo walizikamata katika operesheni safisha maduka ya dawa   leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymont Mushi akipokea baadhi ya maboksi ya dawa jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BARAZA la  Famasia Tanzania  limekabidhi dawa  kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda zenye thamani ya Sh. milioni 294 zilizokamatwa katika operesheni safisha maduka ya dawa  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi dawa  hizo Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shakalaghe amesema operesheni hiyo iliyofanyika katika Mikoa tisa na walifanikiwa kukamata dawa  zenye thamani ya zaidi ya  Sh. milioni 336 na kati ya dawa  hizo dawa  zenye thamani ya zaidi ya  Sh milioni 11 hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Alisema dawa hizo zitasambazwa katika hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam na zimehakikiwa.

Amesema katika Mkoa wa Dar es Salaam majalada 10 yamefunguliwa  mahakamani kwa wale waliokamatwa  na dawa  za serikali ambayo kwa sasa yapo katika hatua za upelelezi. 

"Bado kumekuwa na ongezeko  la maduka ya dawa ambayo yanaanzishwa kinyume na sheria na taratibu hususani katika Mkoa huu na tumebaini kwamba maduka yaliyofugwa wakati wa operesheni yanafunguliwa wakati wa usiku na kuendelea kutoa huduma za dawa .amesema.

Elizabeth amesema lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kuvunja sheria ya famasi katika uendeshaji na utoaji wa huduma za dawa nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa dawa hizo, Mkuu wa Mkoa huu,Paul Makonda alisema wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali wanatakiwa kufunga maduka hayo mara moja au kuzirudisha walikonunua  huku wengine wakifanya huduma nyingine ambayo ni tofauti na leseni walizoomba.

Makonda amevitaka  vyombo vya dola na watendaji wa ngazi ya mkoa , manispaa, kata na mitaa kuhakikisha wanayafunga na kuyaondoa maduka yote ambayo hayana vibali na yanayoendeshwa kinyume na sheria ya famansi nchini.

Aidha amevitaka vyombo vya dola kufanya operesheni nyakati za usiku ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki kwa wale watakaokaidi maagizo ya awali na kufanya biashara wakati wa usiku kwa kizingizio serikali imelala wakati huo.

WAZIRI SIMBACHAWENE AWASHA MOTO KWA WAFANYABIASHARA WA MAENEO YASIYO RASMI, AAGIZA KUONDOLEWA MARA MOJA.

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (Mb), Katikati akizungumza wakati  wa ziara  ya kukagua mradi wa mabasi yaendayo haraka  leo  jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kushirikiana na viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia leo  hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya makutano ya barabara na katikati ya jiji.

Pia amemtaka Makonda kuhakikisha anawaondoa ombaomba wote  walipo katika makutano hayo pamoja katikati ya jiji kuweza kusaidiwa na sio kuomba hawawezi kujikwamua na umasikini.

Simbachawene alitoa agizo hilo  leo  alipofanya ziara katika mradi wa Mabasi yaendayo haraka UDART na kudai kwamba bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kutokana na watu  kushindwa kufuata sheria ambazo zimewekwa.

Amesema  lengo la kuwaondoa wafanyabiashara na ombaomba hao ni kutaka kuhakikisha kwamba jiji la Dar es Salaam linakuwa katika muonekano mzuri na usafi  na kuweza kufuta mbinu nyingine ya kuwasaidia kupitia mfuko wa TASAF.

"Kuanzia  leo  sitaki kumuona mfanyabiashara katika maeneo hayo ya makutano na pembezoni mwa barabara watafutieni utaratibu ambao utawafanya wakae maeneo  salama  kutokana kila manispaa ilivyoanisha "amesema Simbachawene.

Aliongeza kuwa anataka katika maeneo hayo kuwepo na askari saa  24 ambao watahakikisha hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara baada ya kuondolewa.
"Acheni kukamata mama ntilie nataka askari hao watumike kuwakamata wafanyabiashara hao wakae hapo saa  24" amesema Simbachawene.

Amesema kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya jiji  kunachangiwa na uwepo wa biashara zinazofanywa katika mazingira ambayo sio rasmi na ndia chazo cha uchafu.

Kwa upande wa usafiri wa Mabasi yaendayo haraka UDART,Simbachawene pia amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na kuacha kutumia Barabara za mwendo haraka hususani pikipiki na maguta.

Amesema serikali imejipanga  kukabiliana na changamoto  foleni kusimamia utekelezaji wa barabara  za mabasi ya  mwendo wa haraka awamu ya pili unatarajia kuanza  mwakani.

Simbachawene amesema tayari wameshafanya tathimini na utatumia miaka miwili hadi kukamilika kwake pia wapo  katika mchakato wa kumtafuta mkandarasi kwaajili ya ujenzi.

Amesema awamu ya pili itaanzia katika Barabara ya sokoine kuelekea barabara  ya Kilwa hadi  Mbagala na kutakuwa na barabara  za juu katika makutano ya barabara  ya Kawawa na Nyerere,
Nae  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuahidi Waziri huyo kuwa watatekeleza maagizo yote na kuahidi kuanzia oparesheni hiyo  leo.

INTRODUCING VIDEO MPYA YA Jerry Bwax Latino #ELERII TOKA CREW YA #BADSPENDERZ

KAMPUNI YA TING YATOA MAGETI YA CHUMA KUDHIBITI WEZI WA KOKI ZA MAJI UWANJA WA TAIFA

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez, wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Juni 17, 2016. Kampuni hiyoimetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44.


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
KAMPUNI YA kusambaza ving'amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam, imekabidhi mageti ya chuma  27 kwa uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo, Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini
“Mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu waziri.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungungaji Dkt. Veron Fernandos, alisema kampuni yake ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema, Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu miundombinu mingine.
K-VIS MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Vernon Fernados, akimuonyesha moja ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
 Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo, Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzima
 Mkazi wa jiji akijisaidia kwenye moja ya vyoo hivo huku upande wa kushoto bomba linaonekana likiwa limeng'olewa koki.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MKUTANO WA 68 WA KAMATI KUU YA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI JIJINI GENEVA, USWISI

$
0
0
Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa,Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Mjumbe wa “WMO Excecutive Council” na Bw. Wilbert Timiza Muruke, Meneja Mahusiano ya Kimataifa wa TMA katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Excecutive Council-68) unaondelea, Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 15-24 Juni 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi alikuwa miongoni mwa wajumbe 37 wa Mkutano wa Sitini na Nane wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization Executive Council WMO-EC 68) unaofanyika makao makuu ya Shirika hilo, Geneva nchini Uswisi kuanzia tarehe 15 hadi 24 Juni, 2016. Pia Dkt. Kijazi anaingia katika Kamati Kuu ya WMO akiwa kati ya wanawake wawili (2) kutoka Afrika na watano (5) kati ya thelathini na saba (37) kuwakilisha Dunia nzima. 
Mkutano wa WMO-EC-68 pamoja na masuala mengine unajadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Duniani sambamba na kutimiza Makubaliano ya Kikanda na Kimataifa katika kukabiliana na athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. 
Aidha masuala yanayojadiliwa ni sehemu ya Mpango Mkakati wa WMO na vipaumbele vyake katika kipindi cha mwaka 2015-2019 unaojumuisha utekelezaji wa programu za utoaji wa huduma bora zaidi za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services”, Utekelezaji wa programu ya uboreshaji wa vituo vya upimaji wa hali ya hewa na ubadilishanaji wa data za hali ya hewa “WMO Integrated Global Observing System and Information System (WIGOS/WIS), utoaji wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na maafa “Disaster Risk Reduction, Resilience and Prevention”, Uboreshaji wa huduma za usalama na usafiri wa anga “Aviation meteorological services”, Kuboresha huduma za hali ya hewa kwa maeneo ya Dunia yenye barafu ya asili ikiwa ni pamoja na milima mirefu kama Kilimanjaro “Polar and high mountain regions”, Kujenga uwezo wa rasilimali watu na vitendea kazi hasa kwa nchi zinazoendelea na visiwa vidogo na tafiti za hali ya hewa. Aidha Mkutano huu unajadili pia namna ya kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa kama njia ya kuboresha huduma za hali ya hewa kote duniani na kutatua changamoto za athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi na uhifadhi wa mazingira.

IMETOLEWA NA: 
MONICA MUTONI-AFISA UHUSIANO TMA

MADRASA RAHMAN SEGEREA MWISHO IMEFIWA NA MWANAFUNZI BI.SALAMA JUMA NYAMBI

$
0
0


ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU 
Madrasat Rahman iliyopo Segerea mwisho, Dar es salaam  tunasikitika kutangaza kifo cha mwanafunzi wetu marehem Bi.Salama Bint Juma Nyambi (pichani kushoto mwenye gauni la bluu na mtandio mweupe). Msiba upo Segerea mwisho kwenye mtaa wenye madrasat Rahman. Maziko  ni Jumamosi 18.7.2016

 Allah amlaze mahala pema peponi- Amiin

NEWS ALERT: Ndege ya Precision Air yanusurika kuwaka moto Zanzibar

$
0
0
Ndege ya Precision Air ikitokea Kilimanjaro kuelekea Dar es salam kupitia Zanzibar usiku wa Alhamisi ili pata hitilafu ya injini yake moja kushika moto wakati ikitaka kuruka Uwanja wa Kimataifa wa Karume wa Zanzibar na kupelekea abiria  kushuka haraka na kurejea sehemu ya mapokezi. Hakuna madhara ambayo yameripotiwa na abiria wote walishuka salama,
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, mojawapo ya injini ilishika moto  na kulazimisha marubani  kusimamisha ndege na kuirudisha sehemu ya kupakia abiria, baada ya kuchukua hatua za dharura za kuuzima moto huo kabla ya kuleta madhara.  
Kampuni ya Precision imethibitisha tukio  hilo na hii hapa tarifa yake rasmi:
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images