Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1258 | 1259 | (Page 1260) | 1261 | 1262 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterprenuers) imezaa matunda baada ya kikundi hicho kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya biashara na Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of Women Entreprenuers in Comoro).

  Makubaliano hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Comoro tarehe 14 Juni 2016. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za Tanzania nchini Komoro, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Comoro.

  Tukio hilo la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi hivyo vya Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Comoro lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kilumanga aliwapongeza wajasiriamali hao kwa hatua hiyo muhimu waliofikia na kuwa ana imani ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na wenye manufaa kwa pande zote mbili.

  Alieleza kuwa Tanzania na Comoro zinaweza kushirikiana katika nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa hii itakuwa ni chachu kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Comoro kwa ajili ya kuekeza.
  Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Chabaka F. Kilumanga na Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania Komoro wakishuhudia utiaji saini mkataba wa ushirikiano baina ya vikundi vya wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania na Komoro.
  Bi. Naila Thabeet wa Association of Women Enterpreneurs akibadilishana mkataba na Bi. Anna Matinde kutoka Tanzania Saccoss for Women Enterprenuers.
  Wadua wakishuhudia tukio la kihistoria ambapo ni mara ya kwanza vikundi vya akina mama kutoka Komoro na Tanzania wamekubaliana kushirikiana katika nyanja za biashara.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa wadau mawasiliano juu uzimwaji wa simu feki leo katika ukumbi wa Anatoglo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau wa mawasiliano wakimsikiliza mkuu wa  mkoa hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Watanzania wametakiwa kutumia simu zenye viwango na kuachana simu bandia ambazo hata kiafya si salama kwa matumizi ya binadamu.

  Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati mkutano wa wadau wa mawasiliano kuelekea uzimaji wa simu leo usiku wa kuamkia kesho, Makonda amesema TCRA imethubu kutoa huduma bora  kwa wananchi katika mawasiliano.

  Amesema TCRA imeweza kupambana tangu uzimaji wa analojia kuingia digitali ambapo Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika utekelezaji wa vitendo katika masuala mawasiliano.

  Makonda amesema hata katika sheria ya mtandao baadhi ya watu walikuwa wanapinga ili kuweza kuendelea kutukana katika mitandao ambapo TCRA imeweza kufanikiwa kufanya hivyo.
  Makonda amewataka wadau kuja na mawazo ya kuboresha huduma ya mawasiliano nchini katika ulinzi wa taifa.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuanza kazi mara moja kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo hapa nchini.

  Akizungumza na bodi hiyo kupitia Teknolojia ya Video (Video Conference) toka mjini Dodoma Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kufahamu kuwa miundombinu ya banadri nchini iko katika hali duni, isiyo uwiana na malengo ya Serikali ya kuwa na bandari itakayoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

  “Kazi yenu kubwa ya kwanza ni kurudisha uadilifu na ufanyakazi wa uzalendo na unaozingatia weledi kwa watumishi wote wa bandari nchini”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Amesema TPA inakabiliwa na changamoto nyingi  zikiwemo watu kuajiriana kindugu, utendaji usiozingatia matokeo, mifumo mibovu ya ukusanyaji mapato, baadhi ya watendaji kuwa na maslahi binafsi katika kampuni zinazofanya kazi bandarini na utendaji dhaifu wa matumizi ya mifumo ya elektoniki hali inayosababisha utendaji usio na ufanisi.

  Aidha Prof. Mbarawa amezungumzia umuhimu wa bodi hiyo kuangalia upya muundo wa bodi ya zabuni ya bandari na namna kampuni zinazopewa zabuni zinavyopatikana ili kuondoa manung’uniko na mikwamo katika utekelezaji wa miradi.

  “Hakikisheni mnaweka watu waadilifu, wasio na maslahi binafsi katika bodi za zabuni ili kuiwezesha bandari kushindana na bandari za nchi nyingine na hivyo kuvutia wasafirishaji wengi hali itakayoongeza mapato ya bandari na  kukuza uchumi wa nchi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TPA Prof. Ignas Rubaratuka amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kubadili changamoto zote za bandari nchini kuwa fursa na kazi hiyo itafanywa kwa weledi na kwa muda mfupi.

  Amesema watahakikisha kuwa malalamiko yanayotokana na bandari yanashughulikiwa kwa weledi na kwa kufuata sheria ili haki itendeke na kuiwezesha  bandari kuwa na hadhi inayostahili.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho ameitaka bodi hiyo kujifunza majukumu yake kwa haraka na kutenda kazi kwa mujibu wa sheria.

  Bodi Mpya ya Bandari nchini ambayo imeanza kazi rasmi Juni 14, 2016 inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu na inaundwa na  wajumbe nane ambao ni Mwenyekiti Prof. Ignas Rubaratuka, Dkt. Jabir Bakari, Bw. Azizi Kilonge, Eng. Deusdedit  Kakoko, Bw. Masanja Kadogosa, Bw. Japhary Machano, Bw. Malata Pascal, Dr. Francis Michael na Bi Jayne Nyimbo.
  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Prof. Ignas Rubaratuka (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) kwa njia ya teknolojia ya video (Video Conference) katika kikao kazi kati ya Waziri na Bodi hiyo. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Sekta ya Uchukuzi Dr. Leonard Chamuriho.
  Kikao kazi cha Bodi Mpya ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani), Kikao hicho kimefanyika kwa njia ya teknolojia ya video (Video Conference). Bodi ikiwa jijini Dar es Salaam na Waziri na Naibu wake wakiwa mjini Dodoma.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea kwa njia ya simu na Suzan Lukindo,Mkazi wa Tabora aliyeibuka mshindi shilingi Milioni 5/- katika droo ya wiki ya promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 16 wameibuka katika droo ya wiki ya kwanza.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Kushoto ni Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
  Ofisa wa masuala ya Usalama kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Neema Mgombelo(kushoto)Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kulia) wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa droo ya wiki ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Suzani Lukindo, mkazi wa Tabora,aliibuka mshindi wa wiki wa kitita cha shilingi Milioni 5/- kupitia promosheni hiyo inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 16 wameibuka katika droo ya wiki ya kwanza.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali .

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Simon Delens (wa pili kushoto), akikabidhi cheti mmoja wa watengeneza matofali 200, Hoit Macha baada ya kumalizika kwa mafunzo juu ya utengezeji bora wa matofali yaliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mhandisi wa Mafunzo, Emmanuel Owoyo na Meneja Afya na Usalama, Jerome Mwakabaga.
  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Simon Delens (wa pili kushoto), akikabidhi cheti mmoja wa watengeneza matofali 200, Mohamed Ali, baada ya kumalizika kwa mafunzo juu ya utengezeji bora wa matofali yaliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mhandisi wa Mafunzo, Emmanuel Owoyo na Meneja Afya na Usalama, Jerome Mwakabaga.
  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Simon Delens (kulia), akizungumza katika semina waliyowaandalia watengeza matofali kuhusu ubora wa matofali na usalama mahali pa kazi. Zaidi ya watengeza matofali 200 walihudhuria jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Meneja Masoko wa Twiga Cement, Martha Haule (kushoto), akizungumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa semina hiyo wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na maofisa wa kampuni ya Twiga Cement.

  0 0


  0 0


  0 0  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
  Imeelezwa kwamba , upatikanaji wa vifaa saidizi  ( assistive divices) kwa watu wenye  ulemavu wa aina mbalimbali   siyo tu,  utawawezesha  kushiriki katika  shughuli  za  kiuchumi, kijamii na maendeleo bali pia utawaondolea  hisia za kunyanyapaliwa na  kubaguliwa.
  Hayo  yameelezwa na siku ya  jumatano na   Dkt. Abdallah Possi ( Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri, wakati alipokuwa akichangia  majadiliano  kuhusu  mada ya  uondoaji wa umaskini  na kukosekana kwa usawa    kwa watu wote wenye ulemavu. Mhe Possi alikuwa mmoja wa  wanajopo  watano, walioongoza  majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya pili ya mkutano wa tisa  wa Mkataba wa Watu Wenye Ulemavu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
  Katika mchango wake,  Naibu Waziri amesisitiza kwamba suala la    upatikanajji wa vifaa saidizi  kwa watu wenye ulemavu ni muhimu sana  kwa kile alichosema  ukosefu wa vifaa  hivyo  ni  moja wa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu.
  Akatoa wito  kwa  serikali, jumuiya ya kimataifa na asasi   za kiraia  kuangalia ni kwa namna gani katika wa umoja wao  wanaweza kushirikiana ili kukabili changamoto hiyo ya upatikanaji wa  vifaa saidizi wa watu wenye ulamavu.
  Mhe Possi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu, pamoja na kuzungumza  uhaba wa vifaa saidizi pia amezungumzia kwa uzito wa aina yake kuhusu pamoja na mambo megine fursa ya upatikanaji wa ajira  kwa watu wenye  ulemavu, unyanyapaji na mitizamo  hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.
   Akasema      mitizamo  hasi  dhidi ya watu wenye  ulemavu, ubaguzi na uyanyapaji  umekuwa  kikwazo kikubwa katika    siyo tu, utekelezaji wa sera na mipango ikiwamo ya  fursa za ajira kwa walemavu, bali pia katika kufungua  fikra na  mitizamo  mipana  na jumuishi kuhusu watu wenye ulemavu.
  Aidha  Mhe. Naibu  Waziri amerejea kauli yake kwamba  inakuwa vigumu kutenganisha  ulemavu na umaskini kwa kile anachosema vinakwenda pamoja.
  Akasisitiza ili watu wenye ulemavu waweze kushiriki katika utekelezaji wa Agenda 2030, kujipatia fursa za ajira kama  ilivyo kwa watu wengine pamoja na  kuondokana na umaskini, jamii inao wajibu  mkubwa wa kutoa ushirikiano  kuacha kuwabagua, kutowanyanyapa  na kubwa zaidi   kwa watendaji na wenye mamlaka serikali kuandaa na kutekeleza  mipango ambayo ni  jumuishi  na yenye kuzigatia maslahi , mahitaji  na  mazingira halisi ya watu wenye ulemavu.
  Hoja ya  vifaa saidizi kwa watu wenye  ulemavu  iliungwa mkono na wanajopo wengine  kwa kile walichoeleza kwamba ni muhimu sana katika  kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa huru na kuondokana na utegemezi.
  Wanajopo hao mbali ya  Dkt. Possi  walikuwa ni  Bi. Asa Regner, Waziri  wa   Waziri wa Watoto,  Wazee na Usawa wa Jinsia  kutoka Sweden,  Bw. Joelson Dias ambaye ni  Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati ya  Haki za watu wenye ulemavu kuotka Brazil,  Bi, Silvia Quam kutoka Guatemala na  Bi Emi Aizawa, kutoka Japan.
   Mhe. Dkt. Abdallah Possi, (Mb) Naibu Waziri, Ofisi  ya Waziri Mkuu akichangia  majadiliano kuhusu  mada ya  kuwaondololea umaskini na   kukosekana kwa usawa kwa  watu wenye ulemavu. Mhe. Possi alikuwa mmoja wa wanajopo watano walioanzisha majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya pili ya  Mkutano  wa Tisa wa Mkataba wa Watu  wenye Ulemavu unaoendelea hapa  Umoja wa Mataifa.
   sehemu ya  washiriki  wa  majadiliano kuhusu kuwaondolea umaskini na kukosekana kwa usawa  kwa watu wenye  ulemavu ikiwa ni sehemu ya  mwendelezo wa  majadiliano kuhusu  ajenda kuu ya mkutano wa tisa wa mkataba wa watu wenye ulemavu. 
   Ujumbe wa Tanzania ambao umeongoza na  Mhe, Naibu  Waziri katika  mkutano wa Tisa  wa  Mkataba kuhusu Watu wenye  Ulemavu. 
   Naibu Waziri Possi  akibadilishana   mawazo na   Bi. Asa Regner Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Jinsia  kutoka Sweden muda mfupi  kabla ya kuanza kwa majadiliano kuhusu kuwaondolea umaskini na kukosekana kwa usawa kwa watu wenye ulemavu.
  Ujumbe wa Tanzania ambao umeongoza na  Mhe, Naibu  Waziri katika  mkutano wa Tisa  wa  Mkataba kuhusu Watu wenye  Ulemavu.  kati ya wajumbe  hao ni,   kutoka kushoto mstari wa nyuma ni  Bi. Ngusekela Karen Nyerere ( Mambo ya Nje) Mhe. Stella Ikupa Alec ( Mb, CCM), Mhe. Riziki Said Lulinda( Mb,CUF) na Mhe. Dkt. Elly Marko Macha( Mb. CHADEMA)  aliyekaa mbele ni  Bi Josephine Makunzo Lyengi, Kaimu Kamishna kuhusu Watu wenye Ulemavu

  0 0
   Viongozi na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, wakijiandaa kushuka chini kwenye jengo la Lumumba ili kuwapokea watoto kwa sherehe ya Siku ya Mtoto Afrika iliyosherehekewa tawini hapo leo mchana. Wazazi kote nchini, wamehimizwa kuwajengea watoto, tabia ya kuweka akiba, kwa kuwafungulia Akaunti maalum za Watoto, ili kuzitumia fedha hizo katika kugharimia Elimu. 
  Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba,  Bibi Pendo Assey wakati wa kuadhimisha siku ya  Mtoto wa Afrika, katika Tawi hilo hapo.
  Bibi  Assey amesema, Tanzania ina watu wengi, lakini watu wanaohudumiwa na huduma za kibenki ni watu wachache, kutokana na Watanzania kutokuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba, hivo kuwafungulia Watoto akauti, kutawajengea utamaduni wa kujiwekea akiba.
   Viongozi na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, wakijiandaa kuwapokea watoto kwa sherehe ya Siku ya Mtoto Afrika iliyosherehekewa tawini hapo leo mchana.
    Mkurugenzi wa Utawala na Manunuzi wa Benki ya CRDB, Beatus Segeja,(Kulia) akikata keki wakati wa sherehe ya Siku ya Mtoto wa Africa, CRDB Bank, Tawi la Lumumba.
   Baadhi ya watoto na mabango yenye ujumbe muhimu
  Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba,  Bibi Pendo Assey akikata keki wakati wa kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo tawini hapo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akitizama maendeleo ya ujenzi wa daraja Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu  wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambalo ujenzi wake ulikwama kutokana na ukosefu wa fedha hali ambayo iliwalazimu wananchi wa kijiji hicho kupita juu ya daraja hilo kwa kutumia kamba kitendo ambacho kilikuwa kikihatarisha maisha yao.(PICHA E.MADAFA JAMIIMOJABLOG) .

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mwenye miwani akijaribu kupita kwa lengo  kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbaka katika kijiji cha Kibhundughulu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambalo  ujenzi wake ulianza toka mwaka 2015 na  ulishindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 58 ambapo katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa wa mbeya aliambatana na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo.

  Mafundi wa kampuni ya Richer Ivestment ya Mkoani Mbeya ambao ndio wanajenga daraja hilo wakiendelea na ujenzi daraja hilo ambapo hadi kukamilika kwakwe linataji kukagharimu kiasi cha shilingi milioni 58 .

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibhundughulu  Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambao ndio watumiaji wa daraja hilo la Mbaka ambalo lilikwama kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha hali iliyopelekea wananchi wa kuanza kutumia daraja hilo kwa kupita juu kwa kutumia kamba hali ambayo iliatalisha maisha yao.
  Katika mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano mafundi wanaojenga daraja hilo ili liweze kukamilika kwa wakati .
  Aidha Makalla amekemea baadhi watu wasio waaminifu ambao walikuwa wakipita juu ya daraja hilo kabla ya kukamilika kwakwe kitendo ambacho kilikuwahatari kwa maisha ya wananchi hao.

  Aidha amemtaka mkarandasi anaye jenga daraja hilo kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo katika kipindi cha wiki mbili ili kutoa fursa kwa wananchi hao kuanza kulitumia . 

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akisiadiana na mafundi wa kampuni ya Richer Investment ambao wanajenga daraja la Mbaka kwa kiasi cha fedha shilingi Milioni 58 mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kibhundughulu ambao ndio watumiaji wa daraja hilo.

  Baadhi ya akinana wakazi wa kijiji cha Mbaka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakikatiza katika ya mto kutokana na Daraja walilokuwa wakitumia kuzuiwa na serikali ili kupisha ujenzi wake.
  0 0

   Keki ya Siku ya Mtoto wa Afrika toka Benki ya CRDB, Tawi la Azikiwe Premier, la Jijini Dar es Salaam.
   Mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Tawi la Azikiwe Premier, Nelwike Mwambapa, akiwasha mshumaa kuashiria uzinduzi wa sherehe za Siku ya Mtoto wa Afrika tawini hapo.
   Watoto wakishangalia fash fash za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kwa Benki ya CRDB, Tawi la Azikiwe Premier, jijini Dar es Salaam.
   Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, ambaye ni mteja wa CRDB Bank, Emmanuel Kawishe, akimlisha keki mmoja wa watoto waliohudhuria sherehe hiyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula, na kushoto ni ofisa wa tawi hilo, Nelwike Mwambapa.
   Mfanyakazi wa Benki ya CRDB, Tawi la Azikiwe Premier, Nelwike Mwambapa, akimlisha keki mmoja wa watoto, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika tawini hapo.

  0 0
  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Hawa Ng’humbi akizungumza na baadhi ya wataalam wa masuala ya maafa walipomtembelea ofisini kwake ili kufanya tathimini ya utekelezaji wa  mradi wa  Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Juni 16, 2016.
   Mnufaika wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa Bi. Juliana Peter akifurahia mbuzi wa mradi huo wakati wa zoezi la Tathimini ya utekelezaji wa mradi huo lililofanywa na Wadau wa masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 16, 2016.
   Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akifuatilia mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kujadili utekelezaji wa mradi huo, Wilaya ya Kishapu tarehe 16 Juni, 2016.
   Baadhi ya wanakikundi cha Muungano wakifurahia mafanikio ya kuongezeka kwa mbuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa wakati wa tathimini ya utekelezaji wake iliyofanywa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri mkuu tarehe 16 Juni, 2016 Wilaya ya Kishapu Shinyanga.
  Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Mazingira Bi. Juliana Peter akichangia hoja wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Manisapaa ya Morogoro mjini Ndugu Fikiri Juma mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa chuo cha Mzumbe mara baada ya kuwasili mkoani hapo ambapo atahudhuria sherehe ya siku wahitimu wa chuo cha Mzumbe ,juni 17, 20016 mjini hapo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma, Alhaj Adam Kimbisa na Wapili kushoto ni Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, January Makamba.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John Malecela  katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 16, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika futari aliyoianda kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson katika fuatari aliyondaa kwenye makazi kake mjini Dodoma Juni 15, 2016.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni. PICHA NA IKULU.


  Tanzania inatarajia kufungua Ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.

  Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).

  "Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" Amesema Rais Magufuli.

  Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania.

  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  16 Juni, 2016.

  0 0
  0 0


  Wasomi hao wametoa maoni hayo baada ya mwanaharakati, Jenerali Ulimwengu kusema juzi kuwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anapaswa kushtakiwa kama viongozi wengine walioisababishia hasara Serikali. Wasomi wametafsiri maoni hayo ya Ulimwengu kuwa hayakuwa ya kichambuzi, bali ya kiunaharakati.

  Akizungumza katika Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juzi, Ulimwengu alisema Kikwete anastahili kushtakiwa kwa kuwa fedha nyingi zimepotea wakati wa kuunda Katiba Mpya, ambayo haikupatikana.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana akizungumza na gazeti hili jana, alisema anamheshimu Ulimwengu kama mchambuzi wa kimtazamo, lakini katika suala hilo hakuwa sahihi.  “Ulimwengu ni kati ya watu kumi kwa mitazamo ya kimsimamo na wachambuzi wazuri lakini katika hili nadhani maoni yake yalikuwa ya kiuanaharakati zaidi na sio ya kichambuzi makini kama tulivyomzoea,” alisema Dk Bana.
  Alisema mchakato wa Katiba, ulienda kwa mujibu wa sheria na Bunge ndiyo lenye dhamana ya kutunga sheria na siyo Rais huyo mstaafu, ambaye yeye alianzisha tu na kwamba Kikwete alifanya kila njia, kuhakikisha anawaridhisha watanzania kupata katiba.
  Hata hivyo, alisema Watanzania wanatakiwa kumpongeza Kikwete kwa kuanzisha mchakato wa Katiba kuliko kuwa na mawazo kwamba anastahili kupelekwa mahakamani.
  “Bunge lile la Katiba lilijadili na kufikia lilipofikia na katiba iko uwanjani, tunachosubiri ni kupiga kura ya maoni, Kikwete kosa lake nini? Mchakato ule ulikuwa wa Watanzania wote na siyo wa Kikwete,” alisema Dk Bana.
  Aidha alisema Kikwete kama Rais wa wakati huo, alipoitisha Bunge la Katiba lilionekana ni jambo jema kwa Watanzania wote kwani ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kupata Katiba Mpya, “sio vizuri kutanguliza maoni ya kiuana harakati katika midahalo ya aina hii,” alisema.
  Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba la Kanisa Katoliki, Methodius Kilaini alisema mchakato wa kupata Katiba Mpya, hauhitaji haraka ni mchakato wa muda mrefu ambao unahitaji uvumilivu ; na hilo limejidhihirisha katika nchi mbalimbali zilizopitia jambo hilo.
  “Katiba sio jambo ambalo unaanza tu na unapanga kumaliza ndani ya muda fulani, ina mchakato mrefu, jambo la msingi ni kuwa wavumilivu inaweza kuchukua hata hatua tisa kumi,” alisema Askofu Kilaini.
  Alisema suala la katiba lilikuwa ni la nchi nzima na Serikali kwa ujumla, halikuwa la mtu mmoja ambaye ni Rais wa wakati huo Kikwete.
  Alisema kwa maoni yake ni kitu cha kawaida utayarishaji wa Katiba mpya, kuchukua zaidi ya mihula kadhaa na wakati mwingine isifanikiwe.
  “Tuangalie historia katika nchi nyingine wamefanyaje, tena tupongeze sisi hatuna mauaji wengine wameingia mpaka kwenye migogoro na mauaji lakini sisi tunaenda polepole,” alisema Askofu Kilaini.
  Msomi mwingine ambaye hakutaka jina lake kuandikwa ambaye pia alishiriki katika Bunge la Katiba, alisema mchakato wa kupatikana Katiba mpya haukuwa wa Kikwete ni wa nchi nzima ambao ulihusisha wadau wengi.
  Alisema Kikwete alifanya kazi yake ipasavyo, hivyo haoni sababu ya kusema kwamba Rais wa wakati huo anastahili kushtakiwa badala yake angepongezwa.
  “Kwanza tungempongeza kwa kutumia rasilimali za ndani pekee kwa sababu hakuna mchakato kama huu ambao ungeendeshwa bila rasilimali, na tulizotumia hazikuwa za kutoka nje,” alisema.
  Aidha alisema katika watu ambao walishiriki kuchelewesha mchakato wa Katiba mpya ni pamoja na wajumbe kutoka vyama vya siasa, ambao walijali zaidi maslahi ya vyama vyao.

older | 1 | .... | 1258 | 1259 | (Page 1260) | 1261 | 1262 | .... | 3270 | newer