Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1256 | 1257 | (Page 1258) | 1259 | 1260 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu 
  ya Jamii, Dar es Salaam.

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,  yatoa hati ya wito kwa Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu (48) na mwenzake, wa kwenda kujibu mashtaka ya kula njama na kutoa lugha ya uchochezi kwa watu wa Zanzibar.
  Mbali na Lissu mshtakiwa mwingine ameyepewa wito huo ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa (52) huku Mhariri wa habari Simon Mkina (44) na Mchapishaji Ismail Mehboob (24) wakisomewa mashtaka hayo.
  Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
  Wakili wa Serikali Paul Kadushi amedai kuwa kati ya Januari 12 na 14, mwaka huu mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikula njama ya kusambaza taarifa ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio lililokuwa na kichwa cha habari cha “Machafuko yaja Zanzibar”.
  Katika shtaka la pili, imedaiwa kuwa Januari 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,washtakiwa wote  kwa lengo la kushawishi uchochezi kwa  Watanzania Visiwani dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Ilidaiwa kuwa  walichapisha kwenye gazeti la Mawio toleo namba 182 la Januari 14 hadi 20, 2016 ikiwa na habari ya uchochezi yenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar”.
  Kadushi amedai katika shtaka la tatu, Januari 13, mwaka huu Jengo la Jamana lililopo Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mehboob, kwa lengo la kushawishi Watanzania wa Visiwani, dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Upande wa huo wa Jamhuri umedai katika shtaka la nne, Januari 13, mwaka huu katika Jengo la Jamana mshtakiwa Mehboob alichapisha gazeti la Mawio toleo namba 182 bila kuwa na kiapo kutoka kwa msajili wa magazeti.

  Shtaka la tano, Januari 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwa makusudi na bila kuwa na mamlaka ya kisheria waliwatishia watanzania wa Visiwani, wasijitokeze kwenye Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
  Ilidaiwa kuwa washtakiwa waliwatishia kwamba uchaguzi huo utasababisha kutokea kwa vita na machafuko utakaosababisha umwagaji wa damu kupitia makala iliyochapishwa na gazeti la Mawio  yenye kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar”.
  Hakimu Simba aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. Milioni 10 kila mmoja walitimiza masharti hayo.
  Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya washtakiwa hayana mashiko ya kisheria mahakama iyafute n kuwaachia huru.
  Amedai kuwa sheria za magazeti za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara haziingiliani na Tanzania Visiwani hivyo kesi hiyo haina mashiko ya kisheria. Wakili Kadushi ameomba muda wa siku saba kwa ajili ya kujibu hoja za utetezi.
  Hakimu amesema kesi hiyo itasikiliza majibu ya hoja za Jamhuri Juni 28, mwaka huu na washtakiwa Lissu na Idrissa wafike mahakamani kusikiliza mashtaka yao.


  0 0
 • 06/14/16--11:09: Introducing Dalali Group
 • In Dalali we always try to make your life easier, whether you are getting rid of an old sofa set at home, selling your old car,  selling a house or renting one. We are a one stop center for connecting you with the potential buyers. 
  Just visit our site www.dalali.co and post any property for free.
  Regards,
  Dalali Group.

  0 0

  • Unapata Facebook na messenger bure kabisa
  • Wateja wa Airtel wanapa huduma hizi bure  bila ya kuwa na muda wa maongezi  au intaneti
  • Huduma hii Inapatikana kwa wateja wote wa Airtel
  Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty akizungumza  kwenye uzinduzi wa kampeni ya  “Bila Salio Wala MB” iliyozinduliwa jana katika hafla iliyofanyika ofisi za makao  makuu ya Airtel, ambapo wateja  wa Airtel
  wanapata huduma ya Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook bure kabisa.
  Dar Es Salaam, 14 Juni 2016 Airtel Tanzania, kwa kushirikiana na Facebook, imezindua huduma ya  Bure  ya Facebook kwa wateja wa Airtel katika kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la  "Bila Salio Wala MB". Lengo la mpango huu ni kuunganisha kila Mtanzania katika intaneti  na, kwa njia hii, kutawezesha kufungua fursa nyingi ambazo hapo awali zimekuwa ngumu kwao kuzitimiza.
   Kama sehemu ya "Bila Salio Wala MB" kampeni, Watanzania wenye kadi ya simu ya Airtel na simu yenye uwezo wa kupokea intaneti wataweza kufurahia Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook
   Ndani ya Facebook, wateja wataweza kuchat, kutuma picha, video , kutoa maoni, kuweka picha, kuangalia picha na mambo mengine mengi.
   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty alisema, "kutokana na maisha ya sasa jinsi yalivyo intaneti ni kitu muhimu sana katika maisha ya watu kwani imekuwa ikileta maendeleo katika Jamii na uchumi duniani kote. Lengo letu ni kuunganisha watu wengi itakavyowezekana na intaneti  na kuwatambulisha katika fursa mbalimbali zilizopo kwa kukuza uchumi wao . Tunaamini kabisa huduma hizi za bure za facebook ni hatua ya kwanza nzuri ya kufikia lengo hili. "
    Free Basics ni seti ya Kiswahili  na tovuti ya kimataifa Tanzania inayotoa Habari za  afya, elimu, biashara na habari za  fedha husiana na watu ili waweze kufanya uamuzi na maamuzi ya kuboresha maisha yao.  Free Basics   ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii duniani kote , inayowawezesha wateja kuwasiliana kwa urahisi na ndugu jamaa na marafiki zao. Kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata huduma hii  bila gharama yoyote  , inatoa fursa kubwa kwa mamilioni ya watu , urahisi zaidi wa kuwasiliana na pia kuweza kutangaza bidhaa mbali mbali na hivyo kuweza kujiongezea kipato huku wakitumia mtandao huo wa facebook kwa kibiashara zaidi ya mawasiliano pekee na kukuza uwezo wao kutokana na utajiri wa habari wanazoweza kupata kupitia mtandao.
    Akitoa maelezo, mkuu wa kitengo cha intaneti Gaurav Dhingra alielezea "utumiaji wake ni rahisi. Popote ulipo Tanzania, ilimradi unakadi ya simu ya Airtel iliyosajiliwa  katika simu yako yenye uwezo wa kupata intaneti , unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook, na kufurahia kabisa, huduma hiyo bila ya kuwa na salio au kifurushi cha intaneti. Kwa wale ambao sio watumiaji wa Facebook wanaweza pia kuomba njia fupi ya kuunda akaunti zao kwa kupiga *148*88 #, "aliongeza Dhingra.

  0 0

  Majaji wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa makini kufuatilia usomani wa Wanafunzi hao katika mashindano hayo. 
  Watoa Aya za Qur-an kwa Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakitoa Aya kwa Washiriki hao.
  Mshinriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Juzuu 10 kutoka Zanzibar Mwanafunzi Khayyam Mohammed mwenye umri wa miaka 13. akisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki leo 14/6/2016.
  Mwanafunzi kutoka Zanzibar Mussa Hamad mwenye umri wa miaka 9 akishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Juzuu 10, yanayofanyika katika Masjid Loota kiembesamaki Unguja 
  Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an kutoka Zanzibar Mwanafunzi Shakir Hamad Juma. akisoma Qur-an katika mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar. yaliowashirikisha Wanafunzi 27 Kutoka Zanzibar, Tanga, Pwani na Morogoro.

  0 0


  Katika Kuonesha Mshikamano Upendo na Umoja Miongoni Mwa Waja wa Mwenyezi Mungu, Wakulima Masikini Waislamu Kwenye Kitongoji Gojra Jimbo la Punjab Huko Nchini Pakistan wamechangia Ujenzi wa Kanisa Kwa Wakristo Waliokua Wanaabudu Nje ya Makazi Yao kama wanavyoonekana Pichani.

  ‘A church is also a house of Allah;
   praying is what matters. 
  We worship the same God’


  0 0

  Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) ameasa wawekezaji katika sekta ya madini, mafuta na gesi kushirikiana na jamii zinazozunguka maeneo yao ya uwekezaji ili kuweza kutunza amani, utulivu na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini na bara la Afrika kwa ujumla.

  Waziri huyo alitoa rai hiyo katika mkutano wa siku moja ya kikanda uliondaliwa na Taasisi ya Uongozi kuhusiana na ‘Leseni za Kijamii za Uendeshaji’. Leseni za Kijamii za Uendesheji ni dhana ya kitaalam inayohusiana na kiwango cha kukubalika kwa kampuni za madini, mafuta na gesi kwa jamii zinazowazunguka katika maeneo yao ya uwekezaji.

  “Migogoro kati ya wawekezaji wa madini, gesi na mafuta na jamii yana madhara mbalimbali ikiwemo ya kifedha, kiutendaji, na kitaswira kwa kampuni husika. Migogoro ya aina hii yakipuzwa madhara yake ni makubwa, na ni kwa sababu hii hii kampuni katika sekta hii zinapaswa kufanya bidii zaidi katika kuhakikisha kwamba shughuli zao za uwekezaji haziwakeri watu,” alisema Simbachawene.

  Aliendelea, “Majadiliano na mashauriano katika ngazi ya wananchi yanaweza yakaleta suluhu katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika ulipwaji wa fidia,  utoaji wa misaada kwa jamii, na utolewaji wa kazi mbadala kwa baadhi ya wananchi ambao wamekoseshwa kazi kutokana na shughuli za kiuwekezaji.”

  Waziri huyo pia alisisitiza dhamira ya serikali katika kugatua madaraka kutoka katika serikali kuu ili kuwawezesha ushirikishwaji wa wananchi kuwa wa urahisi zaidi, yenye uwazi na usawa. 

  “Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tuna uwezo wa kuongeza idadi ya wawekezaji katika sekta tofauti, na kujenga amani, utulivu na maendeleo katika jamii za wananchi,” Waziri alisema.

  Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Dennis Rweyemamu alisema kwamba taasisi hiyo iliandaa mkutano huo ili kuweza kufahamu changamoto za kujenga mahusiano kati ya wawekezaji wa sekta ya madini, mafuta na gesi na jamii zinazowazunguka, pamoja na kutafuta namna bora za kukuza mahusiano hayo.

  “Kampuni katika nchi nyingi sana, hususan katika nchi zinazoendelea, yamewekeza mamilioni ya madola katika kutoa misaada ya kijamii, lakini bado yanakutana na pingamizi kutoka kwa wananchi katika maeneo waliyowekeza,” alisema Rweyemamu.

  Aliendelea, “Mkutano huu unalenga kujenga uelewa wetu ya namna Leseni za Kijamii za Uendeshaji zinapatikana na kukuzwa, kupitia uzoefu wa Tanzania katika dhana hii, na kujifunza pia kutoka katika nchi ambazo zimefanikiwa na zingine ambazo zilijaribu lakini hazijafanikiwa.”

  Mkutano huu wa siku moja imekusanya wadau zaidi ya mia moja kutoka nchini Tanzania na barani Afrika wanaofanya kazi katika serikali, sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za elimu. 

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akifungua rasmi mkutano wa kikanda kuhusu Leseni za Kijamii za Uendeshaji iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi mapema leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili namna ambavyo wawekezaji katika sekta ya madini, gesi na mafuta wanaweza wakaongeza uwajibikaji na kupunguza migogoro kati yao na jamii zinazowazunguka katika maeneo yao ya biashara.
   Mwenyekiti wa McAlister Consulting Corporation na Balozi mstaafu wa Canada nchini Tanzania Balozi Andrew McAlister akizungumzia uzoefu wake kuhusiana na uwekezaji na uwajibikaji wa kampuni za madini, gesi na mafuta katika mkutano wa kikanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi leo jijini Dar es Salaam yenye malengo ya kupunguza migogoro kati ya kampuni hizo na jamii zilizopo katika maeneo yao ya uwekezaji.
   Makamu wa Rais Mwandamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia Mining Plc Bw. Deodatus Mwanyika (kulia) akichangia mjadala katika mkutano wa kimataifa wa kikanda kuhusu Leseni za Kijamii za Uendeshaji iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi mapema leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili namna ambavyo wawekezaji katika sekta ya madini, gesi na mafuta wanaweza wakaongeza uwajibikaji na kupunguza migogoro kati yao na jamii zinazowazunguka katika maeneo yao ya biashara. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TCME Balozi Ami Mpungwe, Mwezeshaji wa mkutano huo Bw. Aidan Eyakuze na Mbunge na Mwenyekiti wa Fedha ya Bunge kutoka nchini Ghana Mhe. James Avedzi. 
   Mtaalam wa kimataifa wa Leseni za Kijamii za Uendeshaji Dkt. Ian Thomson, akiwasilisha mada kuu katika mkutano wa kikanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na namna ambavyo wawekezaji wa madini, gesi na mafuta wanaweza wakajitahidi kuongeza kiwango chao cha kukubalika na kupunguza migogoro kati yao na jamii zilizopo katika maeneo yao ya uwekezaji. 
   aafisa waandamizi wa serikali, sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za elimu wakishiriki mkutano wa kikanda kuhusu Leseni za Kijamii za Uendeshaji iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili namna ambavyo wawekezaji katika sekta ya madini, gesi na mafuta wanaweza wakaongeza uwajibikaji na kupunguza migogoro kati yao na jamii zinazowazunguka katika maeneo yao ya biashara.


  0 0
  0 0

  Zikiwa zimebakia siku mbili tu simu feki kuzimwa nchini kote,Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania,Imewahakikishia wateja wake kwamba fedha zao zote zitakazokuwa kwenye simu kupitia mtandao wa M-PESA watoe shaka kwani pesa zao zitakuwa salama kabisa na vilevile hata kadi zao za simu zitakuwa na usalama wa hali ya juu ila wafanye haraka kununua simu za bei nafuu kabisa kuanzia shilingi elfu 18/-zilizopo katika maduka ya kampuni hiyo ambayo yamesambaa nchi nzima, akiongea na kituo hichi Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia alisema katika kutekeleza agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA)la kuzitaka kampuni za mawasiliano kutoa elimu kwa wateja wao kuhusiana na simu zisizokuwa na kiwango yaani simu feki,Vodacom Tanzania kesho itaendeleza kampeni maalum ya uhamasishaji wa huduma zake mbalimbali ikiwemo kusajili laini kwa wateja kwa njia ya kieletronikali pia kuwauzia wateja simu halisi na za gharama nafuu nchi nzima.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

   Mchumi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Magreth Sembuyagi akifafanua jambo walipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Same Bi. Monica Kwilulihya (hayupo pichani) ili kuendelea na shughuli za kukagua miradi inayotekelezwa na Ofisi hiyo.
   Afisa Mtendaji Kata ya Makanya Bw.Josephat Kitunga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Kata yake alipotembelewa na Wataalamu wa masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kukagua miradi inayotekelezwa, tarehe 14 Juni, 2016.
   Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Herman Kapufi (katikati) akizungumza na baadhi ya Wadau wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame walipotembelea Wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa mradi katika kata ya Makanya, Vunte na Hedaru Mkoani Kilimanjaro.

  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka akizungumza na Viongozi wa vikundi vya mradi huo (hawapo pichani) walipotembelea Kata ya Makanya Wilaya ya Same kukagua utekelezaji wa mradi huo Juni 14, 2016.

  0 0

  Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.  Benjamin William Mkapa akikata utepe kuzindua kitabu cha kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala. 
  Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha ACT wazalendo Bi. Anna Mghwira akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.Picha na Ally Daud-Maelezo

  Na Ally Daud- Maelezo

  Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali baada ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.
  "Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Mhe.  Mkapa.
  Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere. Mbali na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.
  Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi.

  Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.Mbali na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.

  0 0
 • 06/15/16--05:57: KUTOKA CCM LUMUMBA LEO
 • Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya shughuli zake za kiofisi, leo Juni 15, 2016. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Korea Song Geum-Yung, Ofsni kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba ijini Dar es Salaam, leo Juni 15, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Mwenyekiti wa Stand United Amani Vicent akitolea ufafanuzi suala la mgogoro uliopo sasa kwenye klabu ya Stand United

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  UONGOZI wa klabu ya Stand United umesema kuwa hawawatambui wanachama wanaosajiliwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga zaidi wanataka kuja kuiharibu timu hiyo ambayo imetoka kwenye mfumo wa wanachama na kuingia kwenye kampuni huku tayari wakiwa kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 24 mwaka huu na zaidi wamefika mbali na kutishia kwenda kuwashtaki Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

  Mwenyekiti wa Stand United, Amani Vicent amesema kuwa wameshawasilisha malalamiko yao Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kufuatia mchakato unaoendelea kufanywa na kamati ambayo haitambuliki inayowaandikisha wanachama wapya ikiwa wanachama halali walioanzisha Stand United walishakubaliana kwenye mkutano mkuu kuibadilisha timu hiyo kwenda kampuni na tayari wameshasajili.

  "Kuna kamati ambayo imeundwa na Mkuu wa Wilaya ambayo awali ilivua uanachama wa Stand ikiwemo mimi mwenyewe ila baada ya kulifuatilia na kwenda hadi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye na kurudisha mamlaka juu yetu lakini bado wanaendelea kufanya vitu vya kihuni kwa kupita mtaani na kusambaza fomu za kujisajili uanachama,".

  Amesema, wanachokifanya ni kinyume na taratibu na hata ukienda kwa msajili wa klabu utaona ni wanachama gani wanaojulikana wakati wa usajili na zaidi wametangaza hadi tarehe ya uchaguzi ambao hautambuliki ila kwa upande wetu tumeshatangaza na tunafanya Juni 24. Zaidi  klabu yetu kwa sasa iko kwenye mfumo wa kampuni na kama TFF watashindwa kutolea ufafanuzi suala hili la Kamati ya mkuu wa Wilaya badi hatutakuwa na budi na kwenda mbele zaidi kupelekea malalamiko yetu FIFA na ushahidi tunao.

  "TFF wanajua kama tumeshaleta malalamiko kuhusiana na mchakato unaoendelea sasa wa kusajili wanachama wapya na kama watashindwa kutolea ufafanuzi sisi tutakwenda mbele zaidi ambapo tutapeleka na ushahidi ili haki iweze kutendeka kwani katiba yetu inajionesha wazi kabisa kuwa Stand United ipo chini ya kampuni na uongozi wake unajulikana,"amesema Vicent.

  Kwa sasa Stand United ipo chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji, Jonas Tiboroha pamoja na Mwenyekiti Amani Vicent na wapo kwenye hatua za mwisho za kuelekea uchaguzi mkuu na wameshawasilisha tarehe yao TFF na wana imani watashirikiana vizuri.

  0 0
 • 06/15/16--06:08: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. .

   Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa hapo jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la upatikanaji wa madawati, ambao kikomo chake ni mwisho wa mwezi huu. Mashindano haya ya fainali za Copa-UMISSETA yalilenga kuzikutanisha timu za mikoa mbalimbali nchini kwa pamoja Jijini Mwanza, zikiwa zimeundwa na wachezaji mbalimbali kutoka shule za sekondari ili wachuane kwenye michezo na sanaa.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. - “Thamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI iko pale pale, tukiwa tumejidhatiti kuendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha Nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi. Tutaendelea kuunga mkono na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana,” alisema David Karamagi, Mwakilishi Mkazi wa Coca-Cola Tanzania. Karamagi aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola Tanzania inayo imani ya dhati na ikiamini ya kwamba mashindano ya michezo yanayoanzia ngazi ya chini kabisa ndiyo namna thabiti nay a kipekee katika kuibua vipaji vya wachezaji nchini. Pia Karamagi alisema kuwa, wakati wadau wakisubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe mpya za kurejewa kwa fainali za mashindano haya nchini, Coca-Cola Tanzania ilishajipanga kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu za mikoa inayoshiriki. Hivyo basi, kwa udhamini ulioingiwa mwaka huu, Coca-Cola Tanzania itaweza kupanua wigo wa ushirikishwaji wa michezo murua zaidi mbali ya mpira wa miguu, hasa kwa kuweza kujumuisha mpira wa kikapu. “Kampuni ya Coca-Cola nchini tutaendelea na dhamira yetu ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbali mbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na UMISSETA na Copa Coca-Cola’” alimalizia Karamagi.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Benki za Wananchi kwenye Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Juni 15, 2016.
   Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa  Wadau wa Benki za Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Juni 15, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja  na washiriki wa Mkatano wa Wadau wa Benki za Wananchi kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma juni 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipitie upya riba zake ili Watanzania waweze kukopa na kurejesha kwa urahisi.

  Amesema riba kubwa zinazotozwa na baadhi ya benki, huduma zisizokidhi mahitaji na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wananchi wanapotaka huduma za kifedha.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT) mjini Dodoma.

  Mkutano huo ulijumuisha wajumbe kutoka mikoa 10 ya Kigoma, Lindi, Simiyu, Manyara, Katavi, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma kati ya mikoa 18 ya Tanzania Bara ambayo bado haina Benki za Wananchi ila ipo katika hatua za kuanzisha.

  Amesema changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za sheria na taratibu ambazo zinakwamisha ufanisi wa kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hasa zile zinazolenga kuwahudumia watu wa kipato cha chini.

  “Tunahitaji kutafuta njia bora ya kutatua changamoto hizi, na Benki za Wananchi ni kiungo muhimu katika kushughulikia changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za kifedha,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema ni muhimu kuanzisha Benki za Wananchi katika kila Mkoa ili kuweza kusambaza huduma hizo karibu zaidi na walengwa, hali ambayo itasaidia kupunguza umasikini kupitia ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

  Amesema Serikali itaangalia uwezekano wa kuiwezesha mikoa ambayo itaonyesha ari zaidi ya kuanzisha benki zao na akatoa wito waandae mikakati ya kuhamasisha wananchi ili wakusanye mitaji ya kutosha.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa COBAT, Bibi Elizabeth Makwabe amesema Jumuiya yao ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanachama saba na sasa hivi wamefikia 10 huku wananchi wanaowahudumiwa na benki hizo ni zaidi ya milioni mbili.

  Amesema Jumuiya za Benki ya Wananchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mfumo hafifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ufinyu wa mitaji.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,    
  DODOMA.

  JUMATANO, JUNI 15, 2016.

  0 0


  Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Ulinzi na Usalama wa Mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika inayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa na kulia ni Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala Bw. Waziri Nashiri.

  Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala Bw. Waziri Nashiri (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mipango ya Manispaa hiyo katika kuwasaidia watoto walio kwenye mazingira hatarishi. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu na katikati ni Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa.

  Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa akieleza kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu taratibu za kufuata ili kupata huduma katika kituo cha Amana One Stop Centre ambacho kinahusika na kutoa msaada kwa watoto wanaofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu.Picha na Fatma Salum (MAELEZO) 

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA
   


  WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI WILAYANI ILEMELA NA NYAMAGANA.

  KWAMBA MNAMO TAREHE 14.06.2016 MAJIRA YA SAA 10:30HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA JONATHAN GABRIEL MIAKA [31] MKAZI WA BUGOGWA AKIWA NA MISOKOTO MIA NNE [400] YA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.

  INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAFANYA BIASHARA YA KUUZA MADAWA HAYO YA KULEVYA KATIKA MITAA MBALIMBALI YA IGOMBE NA ILEMELA PIA, NA PINDI MTUHUMIWA ANAKAMATWA ALIKUWA AKIFANYA MAWASILIANO NA WATEJA WAKE JINSI YA KUWAPATIA BHANGI HIYO.

  KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA SAA 13:30HRS KATIKA ENEO LA MWANANCHI WILAYANI NYAMAGANA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA RAMADHANI HAMAD MIAKA [24] MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA BHANGI KILO TATU [03] KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.

  AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA BIASHARA YA KUUZA BHANGI KATIKA MITAA HIYO WANAYOISHI, NDIPO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA POLISI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KILO HIZO ZA BHANGI.

  WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA BHANGI UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO NI HARAMU NA BATILI KATIKA USTAWI WA NCHI YETU, KWANI JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATAFUTA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO NA KUWAKAMATA KISHA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA AJILI YA KUPEWA ADHABU KALI ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENGINE.

  IMESAINIWA NA:
  SACP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

older | 1 | .... | 1256 | 1257 | (Page 1258) | 1259 | 1260 | .... | 3286 | newer