Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1257 | 1258 | (Page 1259) | 1260 | 1261 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Sikonge

  WAZEE wanaonufaika na fedha zinazotolewa na serikali katika mpango wake wa kunusuru kaya maskini kupitia mradi wa TASAF III wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameanza kufunguka juu ya manufaa wanayopata kupitia mpango huo.

  Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili juzi wakati wa zoezi la kugawiwa fedha hizo ikiwa ni mgao wa 6 tangu kuanza kwa mradi huo, wazee hao walisema wazi kuwa mpango huo umeanza kuboresha maisha yao sambamba na afya zao.

  Walisema fedha hizo zimewawezesha kuwa na uhakika wa maisha sambamba na kupata milo 3 ya chakula na sasa wana afya njema sana.

  Mzee Nikulao Hussein (75) mkazi wa kijiji cha Chabutwa Mashariki katika kata ya Chabutwa wilayani Sikonge alisema mwanzoni alipewa sh 30,000 akazitumia kwa chakula tu lakini mgao uliofuata alinunua kuku 2 baadae 3.
  Mratibu wa TASAF wilayani Sikonge Mkoani Tabora Claud Nkanwa (wa pili kutoka kulia) akisimamia zoezi la uhawilishaji fedha kwa kaya maskini katika kijiji cha Mitwigu wilayani humo.

  Aliongeza kuwa fedha hizo japo ni kidogo lakini zinawasaidia sana kimaisha kwani zamani alikuwa anaishi maisha ya taabu sana ikiwemo kuomba omba lakini sasa haombi tena kwa watu.

  ‘Sasa siombi tena chakula kwa watu, naomba serikali iache mradi huu uendelee, wasiuondoe,' aliongeza.

  Mzee Magubika Andrea (80) mkazi wa kijiji cha Mitwigu anaeleza kuwa tangu aanze kupata hela za TASAF III maisha yake yamebadilika sana kwani ana uhakika wa kupata chakula kila siku na tayari amefuga kuku 10 na amepanga kununua bati moja moja ili kuezeka nyumba yake, anataka kuondoa nyasi.
  Wananchi wa kijiji Mitwigu wilayani Sikonge Mkoani Tabora wakiwa kwenye foleni ya uwezeshwaji fedha za TASAF juzi.

  Mzee Mrisho Athuman (74) wa kijiji cha Kikungu alieleza bayana kuwa alikuwa anaumwa sana na chakula kilikuwa hamna, lakini baada ya kupata hela hizo akanunua dawa na chakula, sasa ameshapona na afya yake imerudi vizuri hana wasiwasi tena ameanza kunawili.

  ‘Kama sio hizi hela za serikali ningekufa mapema, nilikuwa naumwa sana, ndani chakula hamna, watoto hawaendi shule hata nguo walikuwa hawana, baada ya kupewa hela sasa watoto wanasoma, na mimi nimepona kabisa na nina kuku 6’, aliongeza.

  Bi.Anet Joel Sangira (74) mkazi wa kitongoji cha Magharibi kata ya Chabutwa anasema hali yake ilikuwa duni sana lakini baada ya kuwezeshwa 40,000 za awali watoto wake 3 na wajukuu 2 waliokuwa wameacha shule sasa wanaenda wote na mmoja amekuwa wa kwanza darasani kati ya watoto 60.
  Wazee wa kijiji cha Chabutwa wilayani Sikonge Mkoani Tabora wakisubiri mgao wa fedha za TASAF(Picha na Allan Ntana).

  ‘Nyumba yangu ilikuwa ya nyasi sasa nimebadilisha nimeweka bati upande mmoja nitamalizia upande mwingine kidogo kidogo nikipata hela nyingine’, alisema Salome.

  Mratibu wa Mradi wa TASAF wilayani Sikonge Claud Nkanwa anaeleza kuwa mradi huu umewasaidia sana wananchi wengi kwani wengi wao walikuwa wanakula mlo mmoja tu kwa siku kutokana na kuishi maisha ya umaskini.

  Anaelezea changamoto kubwa anayokumbana nayo kuwa ni baadhi ya wananchi kuomba kuongezewa hela kwa msingi kwamba hela wanayopewa ni kidogo na kwamba wanashindwa kuigawa kwa chakula na kuanzisha miradi.

  0 0

   Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya watanzania wajitokeze  kwa wingi kufanya mazoezi siku ya Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani)  nembo ya Yonga, leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya watu waliofika kufanya mazowezi ya Yoga, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  MAZOEZI ya viungo vya mwili yenye asili ya Indi nchiniIndia yanatarajia kufanyika Juni 19 mwaka huu katika viwanja vya ufukwe wa Cocobeach jijini Dar es Salaa ikiwa ni kuadhimisha siku ya Utamaduni wao na kimataifa kwa ujumla.

  Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Yogo ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya uhindi kwa mda wa miaka mingi.

  Alimnukuu Waziri Mkuu wa India, Shri Narendra wakati akihutubia mkutano wake wa 69 wa Baraza Kuu la Umojawa Mataifa Septemba 27, 2014 alipendekeza jumuiya yakimataifa kupitisha siku ya Kimataifa ya Yoga.

  Aidha ameeleza kuwa siku ya Yoga sio tu kufanya mazoezi bali mbinu ya kujitambua na kutambua mahusiano ya mtu na dunia na mazingira yake.

  Balozi huyo amewaomba watanzania kujitokeza kwawingi kufanya mazoezi siku ya Juni 19 mwaka huu kwenye ufukwe wa Cocobeach Dar es Salaam huku akisemamazoezi ni uhai wa binadamu hivyo siku hiyo watawezakufundishwa mbinu mbalimbali za kufanya mazoezi yaviungo kutoka kwa wataalamu kutoka nchini India.

  0 0


  0 0

   Katikatika pita pita za Kamera ya Globu ya Jamii, imeweza kuzipata taswira hizi za Wafanyakazi wa kampuni moja ya Usafi jijini Dar, wakiwajibika kwa ushirikiano mkubwa katika Mtaa wa Chimala, katikati ya Jiji ili kuhakikisha barabara zinakuwa safi.
   Usafi umepamba moto.


  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametengua AMRI ya kuvifungia viwanda vidogo 28 vya kukoboa mpunga eneo la Sido iliyotolewa na jiji la Mbeya kupitia idara ya mazingira sababu ya kuvifungia viwanda hivyo zikielezwa kuwa ni mlundikano wa pumba katika maeneo hayo
  Uamuzi wa kutengua amri hiyo ametoa leo kwenye ziara ya kutembelea ofisi ya Sido  Mkoa na kisha kutembelea karakana ya sido, viwanda vidogo vya uzindikaji na ukamuaji mafuta ya alizeti na viwanda vya kukoboa mipunga eneo la sido na hapo ndipo alipokutana na umati wa wananchi wakiomba msaada wake kwakuwa viwanda hivyo vimebeba ajira ya watu zaidi ya 2000
  Baada ya kuwasikiliza wananchi hao alitangaza kutengua amri hiyo kwa kuwa kuvifunga viwanda hivyo kutafanya mchele kuadimika na bei itapanda na si jambo jema hasa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu
  Pili ametengua amri hiyo ikizingatia kuna ajira zaidi ya watu 2000 .

   "Kwa amri hii ya kufunga ukoboaji hivi Hawa watu 2000 wanakwenda wapi? Kama si kurudi mtaani na kwa vijana ni hatari. Hii kauli ya hapa kazi tu kwa Hawa watu 2000 wataifanyia wapi?"
  Ameagiza Mkuu wa wilaya, jiji , jumuiya ya wakoboaji washirikiane na uongozi wa Mbeya cement ambao ndiyo watumiaji wa pumba hizo kuongeza uwezo wa kusomba pumba hizo
  Akiwa eneo la Sido magari ya Mbeya cement yaliendelea kusomba pumba na wamemuhaidi Mkuu wa mkoa ndani ya wiki mbili pumba zote zitakuwa zimesombwa

    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiangalia ukoboaji mpunga katika mashine moja katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido jijini  Mbeya 
     Wanancnhi wakimngoja mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ili kutatua changamoto ya  ukoboaji mpunga  katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido jijini  Mbeya 
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akkwasili kutatua changamoto ya  ukoboaji mpunga  katika eneo viwanda vidogo eneo la Sido  jijini  la Mbeya

  0 0


  0 0

  Nineteen Tanzanian secondary school students who recently completed a year-long academic exchange in the United States visited the U.S. Embassy this week and met with Deputy Chief of Mission Virginia M. Blaser.  The students attended U.S. secondary schools through the Department of State’s Kennedy-Lugar Youth Exchange and Study (YES) program.  The participants came from Pwani, Tanga, Kilimanjaro, and Zanzibar.  While abroad, they attended schools in the states of California, Connecticut, Georgia, Indiana, Iowa, Michigan, Missouri, Montana, Ohio, Pennsylvania, Texas, Washington, and Wisconsin.
  The YES program was established by the State Department’s Bureau of Educational and Cultural Affairs in October 2002 and more than 150 Tanzanians have participated since 2007.  The YES program provides scholarships for high school students, (ages 15-17 years) to spend up to one academic year in the United States.  Students live with host families, attend high school, engage in activities to learn about American society and values, acquire leadership skills, and educate Americans about their countries and cultures.  Approximately 900 students worldwide travel to the United States through the YES program each year.
  Tanzanian secondary school students who recently returned from a year-long academic exchange in the United States share a light moment with U.S. Embassy Regional English Language Officer Scott Chiverton.  The students, who come from Pwani, Tanga, Kilimanjaro, and Zanzibar, were participants in the Department of State’s Youth and Exchange Study program, and attended secondary schools in the states of California, Connecticut, Georgia, Indiana, Iowa, Michigan, Missouri, Montana, Ohio, Pennsylvania, Texas, Washington, and Wisconsin.

  0 0
  0 0

  • Simu za Bure zinapatikana katika maduka yote ya Airtel
                •Utapata vifurushi vinavyodumu kwa muda wa miezi minne na muda                       wa maongezi zaidi ya dakika1000

  Kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeanzisha ofa kabambe ya “simu za bure na halisi" zinazopatikana katika maduka yote ya Airtel. Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana kwa wateja wote wenye simu bandia na  ambazo sio za viwango vinavyokubalika  katika soko la Tanzania  , kwa kununua kifurushi chenye dhamani  ya sh. 22,000 / = Tshs tu.   Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa  na Airtel ikiwemo  ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika  550  kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne.
   Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha  Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema "tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu  bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika siku ya Alhamisi, Juni 16.  Tunachukua fursa hii kuwahakikishi wateja wetu kuwa simu zao zitazimwa lakini laini zao hazitahadhirika  na katika kuwasaidia wateja kuweza  kununua simu zenye kiwango kinachokubalika, tumeamua kutoa simu zenye uhalisi bure pindi mteja atakaponunua kifurushi kitakachodumu kwa muda wa mienzi 4
   Dhingra aliendelea kufafanua kuwa, ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua simu zinazokidhi mahitaji yao ,  tumeongeza simu za aina mbalimbali ikiwemo Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3  ambapo mteja akinunua anapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000 . "Tunatoa wito kwa wateja wetu wa Airtel wenye simu bandia kufika kwenye duka letu lolote la Airtel na simu yake ili ajipatie  simu yenye kiwango kinachokubalika kwa gharama nafuu zaidi kwa kununua kifurushi cha Airtel na kupata simu bure. "alinukuliwa Dhingra
  Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kwa kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.
  Mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Gaurav Dhingra akionyesha simu zinazopatikana kwenye maduka yote ya Airtel katika ofa iliyozinduliwa hivi karibuni kufuatia tamko la serekali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Simu hizo zinauzwa kwa gharama nafuu kabisa.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela ametoa rai kwa wananchi wa wilaya ya Iringa kuchangamkia fursa ya kilimo cha viazi vitamu. Alitoa rai hiyo katika siku ya Wakulima katika kijiji cha Luganga kata ya Ilolo Mpya tarafa ya Pawaga. 
  Hafla hiyo iliyoandaliwa na mradi wa Viazi Lishe "Viable Sweet Potato Technlogies in Africa-VISTA na kufadhiriwa na seriakli ya watu wa Marekani (USAID) unajumuisha Halmashauri 7 ikiwemo IRinga, Wangingombe, Gairo, Mufindi, Ulanga,Mbozi na Chunya. 
  Katika mradi huo wakulima wanahamasishwa kulima viazi lishe kwa ajili ya afya ya mama na mtoto na pia kwa ajili ya biashara ambapo bidhaa kama juice, chapati, kakau(clips), tambi, mkate , maandazi na bidhaa zingine nyingi huweza kutengenezwa ili kukuza kipato. 

  Akimkaribisha mgeni rasmi Meneja wa Mradi wa VISTA Bwana Fred Grant alisema mradi huu uko katika mwaka wa 2 na ni wa miaka 3 ni muhimu Tanzania ikaanza kufikiria jinsi ya kuuendeleza nchi nzima kwani manufaa yake ni makubwa. Sherehe hizo pia zilihidhuriwa na waakilishi kutoka Halmashaurizote 7 zinazonufaika na mradi huo.
   Meneja mradi wa VISTA Fred Grant akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi Mh Richard Kasesela

   Mh Kasesela akifurahia Juice ya Viazi Vitamu na watoto Fabiana na Telephina wa Kijiji cha Luganga


  Meneja Mkuu kiwanda cha Tosti ambao ndio wanunuzi wakubwa wa viazi akitoa melezo. Kiwanda hiki kipo Iringa na kina mahitaji ya viazi kiasi cha tani 150 kwa wiki za viazi mbalimbali.
   Mh Kasesela akifurahia kiazi kitamu

  Mh Kasesela akifurahia Juice ya Viazi Vitamu na watoto

  0 0

  SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo yote ya mji wa Kibaha mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 72, kuanzia siku ya Ijumaa 17/06/2016, Jumamosi 18/06/2016 na Jumapili 19/06/2016.

  Akizungumzia kukosekana Kwa huduma hiyo ya Maji, Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza  sababu ya kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Juu, ni kumruhusu Mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani, ambapo baada kukamilika kwa kazi hiyo, uzalishaji wa Maji utaanza mara moja.“Tuko kwenye hatua ya mwisho ya kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani, kazi hii ikikamilika, uzalishaji utapanda kutoka wastani wa lita Milioni 70 hadi kufikia lita Milioni 106 kwa siku hivyo kuweza kutimiza lengo letu la kumtua mama ndoo ya Maji kichwani” alisema Lyaro
  Lyaro, ameeleza kuwa kuzimwa kwa mtambo huo, kutasababisha maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata, Segerea hadi Kinyerezi kukosa huduma ya Maji.Hivyo,ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi muhimu na lazima ili kukidhi mahitaji yao kwa kipindi  chote cha kukosekana kwa huduma hiyo.
  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuzima simu feki  leo  Juni 16 mwaka huu.
  Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.
  SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi leo,  katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye  kiwango kwa usalama  wa afyanyake na ulinzi wa nchi.
  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.
  Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kwani  kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10 jela.
  Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.
  Aidha amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.
  ‘’Simu feki kesho kuzimwa. Hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya  feki ambazo baada soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba  .

  0 0

  Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.
  Sensei Rumadha Fundi, alipokea na kukubali mwaliko kama mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania akiwa natumaini la usajili wa chama hicho hapa Tanzania.
  Hivi karibuni Sensei Rumadha alikuwa  nchini Ureno hivi sasa kuishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan  Gasshuku 2016". 
  Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" kimefanya mabadiliko hivi karibuni yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa katika michezo ya  Olympics.
  Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayoonekana katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.

  Pia, kuhakikisha  kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani Okinawa duniania kote. 
  Hivyo imeteuliwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayotambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

  Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu ( Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa,Japan.
  Inatumainiwa  kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na Kati. "Endapo usajili utalegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza" amesema sensei Rumadha.
   Yoshihiro Miyazato, mkuu WA Jundokan duniani, na Sensei Rumadha
   Tuka shoto ni  Tsuneo Kinjo sensei 9 Dan , OKINAWA  BUDOKAN " Certified overseas trainer", Gima Sensei 9 Dan , OKINAWA BODOKAN "Overseas trainer, Yoshihiro Miyazato, mkuu wa Jundokan duniani, na Sensei Rumadha.
   Sensei Rene , miaka 78 anaishi Paris kwa zaidi ya miaka 45 sasa ni mzaliwa wa Madagascar,  anashikilia Dan 8 toka Jundokan Karate. Pia ana dojo na wanafunzi wenye  ngazi za juu za  Karate huko Madagascar.

  Miyazaki Sensei 5 Dan, aliyekulia katika Jundokan dojo tokea yupo shule us vududu " Kindergarten" huko Okinawa, Sensei Rumadha kati na Sensei Kinjo kulia.

  Picha ifuatayo:

  0 0

  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika foleni na wageni wake kwenda kuchukua chakula wakati wa kufuturu katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipongezwa na kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo baada ya kuongea machache katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' na wagemi wengine wakipakua chakula katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.


  0 0


  0 0

  Assalaam alaykum,
  Aisha Sururu Foundation ina furaha kuwaalika kwenye fainali ya mashindano ya mwaka 2016 (1437 AH) ya kuhifadhi Qur’an tukufu itakayofanyika Jumapili ya tarehe 19/06/2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es salam, ambapo vijana wanawake na wanaume watakaoshiriki katika mashindano haya watapigania nafasi zao za kwanza kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur’an katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
  Mashindano ya kuhifadhi Qur’an ya mwaka huu yatakuwa ni mashindano ya kumi na nne (14) tangu mashindano ya kuhifadhi Qur’an yanayoandaliwa na Aisha Sururu Foundation yaanzishwe, Alhamdulillah.
  Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 24 ya Tanzania pamoja na visiwa vya Zanzibar, Unguja na Pemba, kwa nia ya kuwashajiisha watoto kuhifadhi Qur’an katika viwango vya juu vya kuisoma Qur’an tukufu.
  Kauli Mbiyu ya Mwaka Huu: Tuwathamini Waalimu Wetu wa Qur’an Tukufu, Tupate Radhi za Mola Wetu Ra’ufu.
  Tukio: Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu.
  Tarehe: 19/06/2016.
  Ukumbi: Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam, Tanzania.
  Wakati: Saa 2 Asubuhi Mpaka Saa 8 Mchana (8am – 2pm).
  Mgeni wa Heshma: Mheshimiwa Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu.
  Shukran.
  Wabillahi Tawfeeq,
  AISHA SURURU FOUNDATION

  0 0

  MWALIMU HOUSE

  NAFASI ZA UPANGAJI.


  Kampuni ya Walimu ya (Teachers’ Development Company Limited) inayo furaha kuutangazia umma nafasi za upangaji katika jengo la MWALIMU HOUSE lililopo  Kiwanja Namba 48 Kitalu ‘Y’, ILALA BOMA jijini Dar es Salaam.  Jengo linapakana na Barabara ya Uhuru na Kawawa Mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Soko la Karume na Ilala maarufu kama Ilala Boma.


  Nafasi zilizopo katika jengo zinaweza kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za kiofisi, maduka, bank, zahanati, mgahawa, chuo nk.


  Nafasi za upangaji zinapatikana kuanzia ghorofa ya kwanza hadi ya nane kwa ukubwa wa kuanzia square mita 42 hadi 218. Gharama ya Upangaji ni Tshs. 24,000 (Bila VAT) kwa square mita moja ikijumuisha kodi ya pango (rent) na huduma zinazotolewa katika jengo (service charge).


  Huduma zifuatazo zinazotolewa katika jengo letu la Mwalimu House;-

  (i)   Genereta (Stand by Generator) (Mpangaji atachangia fedha kidogo ya mafuta ya Generator)

  (ii) Tenki kubwa la kuhifadhi Maji

  (iii)               Lifti ya kubeba watu 10 kuanzia ghorofa ya chini (Basement) hadi ya nane

  (iv)                Eneo kubwa la Parking (Inalipiwa)

  (v)  Usafi na Ulinzi (Masaa 24)


  Kwa maelezo zaidi au kuona maeneo yanayopangishwa, Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia:-

  Simu ya Mkononi: 0769084939, 0713495603

  Simu ya Mezani: 0222203063


  0 0  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mapendekezo ya Tume hiyo kwa Serikali na Jamii katika kuhakikisha Ulinzi na Usalama kwa Mtoto unaimarika. Katikati ni Kamishna wa Tume hiyo Bi. Salma Ali Hassan.

  Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Salma Ali Hassan akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani) kuhusu hali ya mtoto wa Tanzania na mazingira hatarishi wanayokutana nayo ikiwemo ubakaji, ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Francis Nzuki .


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.

   Mkuu wa Shule ya msingi Bunge, Khadija Telela akisoma hotuba kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa shule ya bunge wakiwa katika furaha baada ya kupokea  madawati katika hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  UMOJA wa wanafunzi waliohitimu shule ya msingi bunge mwaka 1991 wameikomboa shule hiyo kwa kutoa msaada wa madawati 70 yenye thamani ya milioni saba.

  Akizungumza na wakati wa makabidhiano ya madati  hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanafunzi waliosoma bunge wametambua umuhimu wao katika kusaidia shule waliosoma kwa kwenda na kampeni ya madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam.

  Makonda amesema kila mmoja kwa makundi waliosoma shule zao wanawajibu wa kwenda kusaidia katika mapungufu katika shule hizo.
  Aidha amewataka wanafunzi kuiga mfano wa wanafunzi wenzao waliosoma hapo kuwa wakihitimu wanaweza kutatua baadhi ya changamoto katika shule ya bunge.

  Mwenyekiti wa umoja wanafunzi waliohitimu mwaka 1991, Eliapenda Lyimo amesema  kuwa wametambua kampeni ya madawati katika mkoa wa Dar es Salaam kuona shule ya bunge wanauhitaji wa madawati.

  Eliapenda amesema kuwa shule ya bunge kwa msaada wa madawati hayo bado wanaupungufu wa madawati 50  ambapo wakipata madawati hayo, shule itakuwa imeachana upungufu wa madawati.

older | 1 | .... | 1257 | 1258 | (Page 1259) | 1260 | 1261 | .... | 3283 | newer