Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MANISPAA YA ILALA YAUNDA KIKOSI KAZI CHA KUKUSANYA MAPATO.

0
0
 Mkurugenzi wa Manispaa  ya Ilala, Isaya Mngurumi akizungumza na wandishi wa habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Manispa hiyo kwa wadaiwa Sugu wa mapato na ushuru mbalimbali, (Kulia) ni Meya wa Manispaa hiyo Charles Kuyeko na Naibu Meya , Omary Kambilamoto.
Naibu Meya , Omary Kambilamoto Akishusha mabango yaliyowekwa bila kulipa ushuru.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeunda kikosi kazi maalum cha kukusanya mapato ili kuweza kufikia malengo waliyojipangia ya Sh. Bilioni 55.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mungurumi amesema kikosi hicho kimeweza kukusanya sh.bilioni moja kwa wiki huku ikiwa lengo ya kukusamya sh.bilioni 15 kwa mwezi mmoja.

Amesema kuwa katika ukusanyaji wa mapato hayo wamebaini kuwepo kwa watu wenye leseni feki za biashara pamoja na vibali feki vya ujenzi wa maghorofa katika manispaa ya Ilala.
Mungurumi amesema kuwa watu wamejenga maghorofa bila   kuwa na  sehemu ya  kuegesha magari  ambapo ni kosa na kutakiwa wote waliofanya hivyo kujisalimisha.

Aidha amesema kuwa wataendelea kupambana watu wanaokwepa kodi za manispaa ambazo ndizo zinazofanya kuboresha huduma kwa wananchi ya kuweza kupata maji safi na salama, upatikanaji wa madawati pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Naye Meya wa Manispaa hiyo, Charles Kuyeko amesema kuwa manispaa inafatilia vyanzo vyote vya mapato ili kuweza kufikia malengo yao.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Isaya Mungurumi akizungumza na waandishi wa habari juu kikosi kazi cha ukusanyaji mapato katika manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam,

JAMII YAASWA KUTOKOMEZA UNYANYAPAA NA MAUAJI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO

Introducing Moyo Mashine (cover) by Jasu Perfect

BOGA NI ZAIDI YA MBOGA NA CHAKULA

0
0
Geofrey Chambua's photo.
Geofrey Chambua's photo.
Na Geofrey Chambua
Boga na Maboga ni Moja ya Mimea ambayo ni tunu kwa hayawani duniani kutokana na kuwa na tija ya asilimia 100 kuanzia kwenye MIZIZI SHINA JANI TUNDA NYAMA YAKE NA HADI MEBGU.
Bahati Mbaya sana wengi tunalichukulia boga kwa namna nyepesi sana ama kwa kutojua ama kwa kujua lakini tukapuuzia umuhimu wa mmea huu adimu sana kwingineko duniani..........
Mizizi ya maboga ni dawa, shina na jani ni mboga, nyama yake ni chakula na ambacho hushadadiwa sana aghalabu Mwezi huu mtukufu kwa baadhi ya maeneo nchini lakini kama hiyo haitoshi ganda la mboga ndilo eneo lenye virutubisho muhimu sana huku umuhimu mkubwa sana ukiwa kwenye mbegu za maboga msingi hasa wa bandiko langu 
  1. nadamu. Kama utakuwa na mazoea ya kutumia na si kutupa mbegu zake kama wengi wetu tulivyozoea
  2. Mbegu za Maboga ni mojawapo ya mimea ambapo unaweza kupata madini ya Zinc ambayo ni vitamini muhimu katika mwili wa binadamu
  3. Katika tafiti zilizofanyika imethibitika kwamba mbegu hizo zinaweza kusaidia kuuia tatizo la tezi dume (Prostate Cancer) zaidi ya yote zna vitamini nyingine muhimu katika mfumo wa kinga ya mwili (Human Immunity System) kama inavyooneshwa pichani
  4. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako. Pia ni nzuri kwa mama anayenyonyesha.
    Na hizi zinakuwa zipo tayari zimekaangwa tayari kwa kuliwa tu katika ujazo wa kg 1 na bila hata kuwekwa chumvi kama wengi wafanyavyo kwani zenyewe zina chumvi asilia 
Matumizi: Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja.

​ZINGATIA
Kutokana na mtangamano na wanadamu na viumbe, umuhimu mimea mingi unaonekana kupoteza sifa yake ya asili hasa katika ulimwengu huu wa kutegemea kemikali za kukuzia mazao (GMOs World)

Introducing "Kama Ipo Ipo Tuu" by Chemical & Msaga Sumu - Produced By Maxmaizer

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAWAPIGA MSASA MAWAKALA WAKE

0
0
b1
Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akizungumza na Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzo ya mawakala hao katika kutoa huduma bora kwa wateja na mikakati ya kuuza bidhaa za shirika hilo kwa ufanisi mafunzo hao yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya watendaji kutoka vitengo kadhaa ambao pia walitoa mada kadhaa katika kuboresha huduma za shirika la Bima.
b2
Bi. Rose Lutu Lawa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC akifafanua jambo kwa Mawakala wa bima ya Ajali na Mali wakati wa mafunzohayo yaliyofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Bima la Taifa NIC jijini Dar es salaam.
b3Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini maelezo ya Bi Rose Lutu Kaimu Mkurugenzi wa NIC.

b6
Kaimu Mkurugenzi wa MasokoElisante Maleko akimuelekeza jambo kwenye ratiba Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo.
b7
Bi. Tabu Kingu Kaimu Mhasibu Mkuu wa shirika la Bima la Taifa NIC ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo akiandika mambo muimu yaliyokuwa yakijadiliwa katika mafunzo hayo.

Mwigulu Apokelewa Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM MKOA WA DAR ES SALAAM

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shughuli hiyo maalum ya kukabidhi furati na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum, Jangwani jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum.
( Picna na OMR)

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI IKULU JIJINI DAR LEO

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimuapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

NANI ANATOKA NA ANABAKI KUJULIKANA JULAI 01 - AZAM

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

UONGOZI wa klabu ya Azam umeweka wazi kuanzia Julai 01 watataja majina ya wachezaji watakaoachwa na timu hiyo pamoja na wanaotarajiwa kujiunga nao, hilo linakuja katika kuimarisha kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi hasa baada ya kushindwa kufikia malengo waliyoyaweka ya kucheza klabi bingwa Afrika mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habaru, Afisa habari wa Azam, Jaffari Iddy Maganga amesema kuwa wanataka kutengeneza kikosi ambacho kitakuja kuwa na ushindani mkubwa na kufikia malengo waliyojiwekea hususani kucheza klabu bingwa na kufika mbali zaidi. "Azam tumetolewa mapema kwenye kombe la Shirikisho tuhakamishia nguvu zetu kwenye ligi lakini tukaishia kushika Nafasi ya pili".

Amesema Jaffari, Julai Mosi wataweka wazi wachezaji watakaowaacha kwenye timu ya wakubwa na ni wachezaji wangapi wataongezwa kutoka timu ndogo ikiwa pamoja kuwataja wachezaji watakaosajiliwa ili kuboresha kikosi chetu.

"Tutawatumia zaidi wachezaji wetu wa kikosi B kwani umefika muda wa kuwapa nafasi za kucheza timu kubwa kwani wameonesha uwezo wa hali ya juu sana katika michuano ya vijana na wana uwezo mkubwa,"amesema.

Ukiachilia hilo, amewataka mashabiki wa Azam kuwa na subira na kuacha kusikiliza maneno ya watu zaidi ni kuwa wachezaji kwa sasa wapo mapumziko ila watarejea hivi karibuni kwa ajili ya kujiunga na kuanza mazoezi ya pamoja.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ESALAAM

0
0
KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(pichani) amewataka Maafisa na Askari wote wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi kudumisha nidhamu wanapokuwa wakitekeleza majukumu ya kazi za kila siku. 
 Meja Jenerali Rwegasira ameyasema hayo leo katika hafla ya ufungaji Mafunzo ya Uongozi wa ngazi za juu kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam. 
 "Katika muda mfupi niliofanya kazi katika Wizara hii nimeambiwa kuna watumishi wanakataa kwenda kwenye vituo vipya kwasababu ya kutopatiwa fedha za uhamisho, huo ni utovu wa nidhamu," alisema Meja  Jenerali Rwegasira. 
 Alisisitiza Mtumishi anapopatiwa uhamisho ndani ya Jeshi jambo la kwanza ni Utii kwanza wa Utekelezaji wa Amri hiyo na siyo sababu au madai mengine ambayo ni kinyume na Utendaji wa Taasisi za Kijeshi. 
 Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP. John Casmir Minja alisema Jeshi hilo limeitikia wito wa kubana matumizi kama inavyosisitizwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Joseph Pombe Magufuli ndiyo maana katika hafla hiyo imehusisha Maafisa wachache wa Gwaride ili kupunguza gharama zisizo za Msingi. 
 "Katika Sherehe za kufunga Mafunzo ya Uongozi kwa mwaka huu Gwaride limepunguzwa kwa kujumuisha Maafisa na Askari wachache zaidi na pia hata Wageni Waalikwa utaona wamekua ni wachache sana ili kuitikia wito wa Rais wa Awamu ya tano kama anavyosisitiza kupunguza matumizi yasiyoyalazima", alisema Kamishna Jenerali John Casmir Minja.
 Aidha, alisema Chuo hicho kina changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na uchakavu wa Miundombinu baada ya kupewa hadhi ya kuwa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na kwamba anaamini Serikali ya awamu ya tano itazifanyia kazi changamoto hizo. 
 Hata hivyo Kamishna Jenerali Minja aliwapongeza wahitimu hao kwa kuchangia Tsh. Milioni 2.4 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya chuo hicho kwa ridhaa yao ambapo walichangishana fedha hiyo ili kuboresha hali ya chuo hicho. 
 Jumla ya Wahitimu 98 wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za Juu wamehitimu Kozi hiyo na kutunukiwa cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza ambapo Idadi hiyo inajumuisha Wahitimu 93 kutoka Tanzania Bara ikiwa Wanaume ni 83 na Wanawake 10 pamoja na Wahitimu 05 kutoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar ambao ni Wanaume 04 na Mwanamke 01.



Gwaride la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la uvishaji cheo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Kaya 60 zaondolewa katika mpango wa Tasaf III Halmashauri ya Mji Kibaha

0
0
Jumla ya Kaya 60 katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha zimeondolewa katika mpango wa kunusuru kaya maskini nchini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) kutokana na kutokidhi vigezo.

Akiongea kwa njia simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Innocent Byarugaba amesema kuwa jumla ya kaya 2,388 zimekuwa zikinufaika tangu kuanza kwa awamu hiyo lakini kwa sasa ni kaya 2,328 ndio zitaendelea kunufaika na ruzuku hiyo baada ya kaya 60 kuondolewa katika mpango huo.

“Katika awamu hii, kaya 60 zimeondolewa katika mpango huo baada ya kutokidhi vigezo, ikumbukwe kuwa fedha hizi za ruzuku zina masharti tofauti na ruzuku za awamu ya kwanza na pili ambapo kama mnufaikaji hajakidhi vigezo hakuna namna nyingine zaidi ya kumuondoa kwenye mpango,” alisema Byarugaba.

Byarugaba aliendelea kutaja vigezo ambavyo vimefanya kaya hizo kuondolewa kwenye mpango huo kuwa ni pamoja na kaya zilizoshindwa kufuatilia watoto wao kwenda shule, kaya zilizoshindwa kuwapeleka watoto chini ya miaka mitano kliniki na zile kaya ambazo hazikustahili kupata ruzuku lakini ziliingia kwenye mpango.

Vile vile Byarugaba amesema kwamba, mpango huo unalenga kuwainua wananchi katika sekta ya afya, elimu pamoja na kuwawezesha wananchi kupata milo mitatu.

Tangu kuanza kwa TASAF III jumla ya Tshs. milioni 572,840,680 zimeshatolewa kwa walengwa.

Aidha Fedha hizo zimekuwa zikitolewa kwa awamu tofauti tofauti ambapo jumla ya Tshs. milioni 87, 608, 295 zimegawiwa katika awamu ya sita kwenye mitaa 40 huku kaya 2,328 zikinufaika ukiondoa kaya 60 zilizoondolewa.

Awamu ya kwanza Fedha zilizotolewa ni Tshs. Milioni 106,574,159, awamu ya pili Tshs. milioni 96,354,886, awamu ya tatu Tshs. milioni 94,426,568, awamu ya nne Tshs. milioni 95,276,818 na ya tano Tshs. milioni 92,599,954.

Serikali yapiga marufuku uagizaji wa transfoma za umeme kutoka nje ya nchi.

0
0

Jonas Kamaleki-Maelezo

Serikali imeliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutoagiza transfoma nje ya nchi na badala yake kutumia zinazotengenezwa hapa nchini na kampuni ya Tanalec.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Iddi Mpakate aliyetaka kujua ni lini Serikali itatoa pesa kukamilisha miradi ya umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Dkt. Kalemani alisema uzalishaji wa transforma ni mkubwa ikilinganishwa na mahitaji ya bidhaa hizo kwa mwezi, hivyo hakuna sababu ya kuagiza transforma hizo kwa bei kubwa wakati zinapatikana hapa nchini.

Kuhusu suala la kugharamia nguzo kwa Mpango wa REA Dkt. Kalemani alisema mteja hatakiwi kutozwa gharama yoyote ziadi ya Tshs. 27,000 fedha ya kuunganishiwa umeme kwa mpango huu.Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali inatekeleza Mradi wa REA Awamu ya II katika Wilaya ya Tunduru na kazi hii inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2016.

Alisema Kazi ya kupeleka umeme katika wilaya hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa Kilomita 293. 2, na ujenzi wa njia nyingine yenye msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 76.1 na ufungaji wa transfoma 38 pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wa awali 3,330

“Gharama ya Mradi kwa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Wilaya ya Tunduru ni Tsh. Bilioni 32.56,” alisema Dkt Kalemani na kuongeza kuwa mkandarasi amekwishalipwa bilioni 27.22 sawa na asilimia 83.6 ya fedha.
Dkt. Kalemani amesema kuwa katika Wilaya ya Tunduru ni vijiji vinne ambavyo vimeunganishiwa miundombinu ya umeme na kufanyiwa majaribio kabla ya kuwashiwa umeme.

Kwa mujibu wa Dkt. Kalemani mkandarasi anaendelea kufunga transforma na Mita za Luku katika vijiji 34 vilivyosalia kwa Wilaya ya Tunduru ili viweze kupatiwa huduma ya umeme ifikapo tarehe 30 Juni, 2016.

YANGA YAJIFUA USIKU WA MANANE NCHINI UTURUKI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Yanga kilichopo nchini Uturuki hivi sasa, kimeendelea kujifua usiku ikiwa ni moja ya mkakati wa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm katika kuelekea mchezo wao dhidi ya Mo Bejala unaotarajiwa kuchezwa usiku nchini Algeria.

Pluijm ameonekana kutumia njia hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali kwani ameweka wazi kuwa anajua aina zote za hujuma zinazotumiwa na mataifa ya kiarabu. 

Yanga ipo nchini Uturuki ikijiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo bejala ambapo ikishamaliza mchezo huo itarejea tena Uturuki na kumalizia kambi hiyo kabla ya kuja kuvaana na TP Mazembe Julai 28 jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Hans Van De Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake, wakati wa Mazoezi yao ya Usiku huko nchini Uturuki.
Wachezaji wa Yanga wakimsikiliza mwalimu wao.

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA RASMI KESHO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

DIRISHA la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) na ligi Daraja la kwanza (FDL) litafunguliwa rasmi kesho huku timu zikishauriwa kufanya usajili kwa umakini mkubwa na linatarajiwa kufungwa Agosti 6 ambapo usajili huo utaenda sambamba na semina elekezi kwa viongozi wawili wa timu zinazo shiriki ligi kuu, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la pili na  wanaotakiwa kuhudhuria semina hiyo ni Katibu mkuu wa klabu pamoja na Afisa usajili.

 Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa semina hiyo itahusu matumizi ya mifumo ya usajili kwa njia ya mtandao (TMS) kwani msimu ujao ni lazima kila timu iwasilishe usajili wa wachezaji wake kwa mfumo wa TMS kama FIFA walivyoelekeza.

"Misimu miwili iyopita tulianza kuutumia mfumo huu lakini haujaonesha kufanikiwa sana na ndio maana imeitishwa semina hii kwani kwa msimu ujao wachezaji watakaotambuliwa ni wale watakaosajiliwa kwa mfumo wa TMS", amesema Alfred. Semina hiyo itaanza siku ya jumatatu semina itakayowahusu viongozi wa ligi kuu, Jumanne itakuwa kwa ajili wa viongozi wa Ligi daraja la kwanza huku ikimalizika kwa viongozi wa ligi daraja la pili siku ya Jumatano.

Kuanzia leo hadi Juni 30 kutahusisha uhamisho wa wachezaji huku timu hizo pia zikitakiwa kuweka wazi wachezaji wanaowaacha  ili waweze kusajiliwa na timu nyingine endapo wanawahitaji. Kipindi cha Agosti 7 hadi 14 kitatumika kwa ajili ya mapingamizi kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, huku hatua ya pili ikianza Agosti 17 hadi Septemba 7. 

Na pingamizi la hatua ya pili zitaanza  Septemba 8 hadi Septemba 14 na Septemba 15 hadi 17 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili.

TFF pia imezitaka klabu zinazoshiriki ligi kuu (VPL), ligi daraja la kwanza (FDL) pamoja na daraja la pili (SDL) kutaja viwanja vyake vya nyumbani kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Timu hizo zinatakiwa kuwasilisha taarifa ya viwanja watakavyovichagua kabla ya Juni 20 mwaka huu.

Klabu hizo zinatakiwa kupeleka vipimo vya viwanja husika ili TFF kupitia kamati ya mashindano ijiridhishe kama vitafaa kutumika kwa ajili ya ligi husika na timu zinazoshiriki mashindano hayo pia zinatakiwa kuambatanisha vipimo hivyo na aina ya nyasi, idadi ya vyumba, uwezo wa mashabiki wanaoweza kuingia pamoja na jina la mmiliki.

"TFF itahitaji kupata taarifa mapema na iweze kufanyia kazi kwani ni muhimu kukagua viwanja hivyo kama vina sifa zinazostahiki na hata kama ikitokea mechi zimepangwa usiku basi timu ziweze kucheza", amesema Alfred.


Tumezielekeza kwamba iwapo timu haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa wa jirani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (3) Ligi Kuu Tanzania Bara toleo la 2016/17.


ZIARA YA SERIKALI YA JIMBO LA PUNTLAND-SOMALIA NCHINI TANZANIA

0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland -Somalia walipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiukaribisha ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland - Somalia, ulipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle akiwa na Maafisa alioambatana nao.
Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland –Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle akizungumzia lengo la Serikali yake kuitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Maafisa aliombatana nao.

MAHAKAMA YA KISUTU YATENGUA UDIWANI WA CHADEMA KATA YA SARANGA

0
0
Na Mwene Said, Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetengua matokeo ya kiti cha  diwani wa Kata ya Saranga, Efraim Kinyafu (CHADEMA),  baada ya kubaini kwamba uchaguzi ulikiuka taratibu katika  kuhesabu kura.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Mdoe dhidi ya diwani huyo Kinyafu na msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema ambaye kwa sasa amehamishiwa kituo kingine cha kazi na ilisomwa kwa niaba yake na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

“Mahakama baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili, imebaini kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika kuhesabu kura inatengua matokeo ya uchaguzi wa kata ya Saranga” alisema Hakimu Mashauri.

Mdoe alifungua kesi hiyo akidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura akilalamikia kituo kimoja na kuiomba mahakama kuamua vyovyote itakavyoona inafaa na itamke uchaguzi haukuwa wa huru na wa haki.

Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Fredrick Kihwelu, alidai mteja wake hajaridhika na hukumu hiyo hivyo watakata rufani kuipinga.

Alidai wataomba mahakamani wapatiwe mwenendo wa kesi ili waweze kuwasilisha sababu za kukata rufani.

Wakili huyo alidai mdai huyo alikuwa halalamikii kushindwa kwa kuwa wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, alikiri kushindwa kwa tofauti ya kura zaidi ya 500.

Alidai katika kituo ambacho alikuwa akilalamikia mdai huyo kulikuwa na wapigakura 68, hivyo hata kama kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura kusingeweza kubadili matokeo yote.

Wakili huyo alishauri kwamba aliyepaswa kusahihishwa kwa kukiuka taratibu ni  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kesho na keshokutwa iwe makini kwa kutorudia  makosa na sio mdaiwa wa kwanza (Kinyafu).

MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA PENSHENI PPF AKABIDHI VYETI KWA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2015/16

0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Khijjah, akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakati wa zoezi la kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano Dar es Salaam, (DCC). Tukio hilo lilifanyika wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi. Picha na Mafoto Blog.
 
************************************

Akizungumza baada ya kukabidhi Vyeti hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Khijjah, aliwapongeza Wafanyakazi bora wa 2015/16 wa Mfuko huo kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini na kuwataka Wafanyakazi wote wa PPF kufanya kazi kwa bidii bila kurudi nyuma ili kuendelea kutimiza malengo.

Katika Kikao hicho jumla ya Wafanyakazi 22, kutoka Kurugenzi na Idara mbalimbali walikabidhiwa vyeti vya Wafanyakazi Bora na Mwenyekiti huyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa William Erio, akizungumza na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano Dar es Salaam, (DCC) jijini, leo Juni 14, 2016.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Mganga, akizungumza wakati wa Kikao hicho.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Uwekezaji, Agustine Paul, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Huduma za Sheria, Enelia Majo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

POSHO ZA WATENDAJI WA MANISPAA YA KINONDONI KUTENGENEZA MADAWATI 28000.

0
0
 Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa kusaini mkataba na wazabuni 10 wa kutengeneza mdawati 28000 leo jijini Dar es Salaam.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob  Boniface akisaini mkataba  wa kutengeneza madawati na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Edosama Hardware,  leo jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya watu waliokuwa wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa kutengeneza madawati wa shule za msingi na Sekondari katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar  es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imekata posho za watendaji wa idara zake kwa muda wa miezi miwili  na kuweza kupata sh.bilioni 1.8 ambazo zitamaliza tatizo la madawati 28000 kwa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Kinondoni.

Kuondosha kwa posho hizo kulitokana na manispaa  kubaini kuwa hawana uwezo wa kununua madawati 28000  kwa kukosa bajeti hiyo katika mwaka fedha 2015/2016  na kuona posho za watumishi zitumike kununua madawati hayo.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mkataba  wa kampuni 10 za kutengeneza madawati  28000, Meya wa Manispaa Kinondoni, Jacob Boniface amesema kuwa kwa kuingia mkataba huo kinondoni inachana na tatizo la madawati.

Jacob amesema kuwa Kinondoni wanafunzi kukaa chini ni aibu kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na vyanzo mapato vingi.
Amesema kuwa waliongia mikataba kuhakikisha kufikia juni 30 mwaka huu wazabuni wote kuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati.

Jacob amesema kuwa madawati yanayokusanywa na wadau mbalimbali wanayahitaji kwa ajili kuweka akiba ili yakiharibika kuweza kutumika pale penye upungufu.

Ameasema madawati hayo yanatengenezwa kwa bei ndogo kuliko na awamu zote kwani kwa sasa yanatengenezwa kwa sh.85000, wakati kwa manispaa hiyo ilishatengeneza dawati moja kwa sh.400,000.

KANISA LA THE SILOAM LAKABIDHI HUNDI YA SH.MILIONI 19 KWA MKUU WA WILAYA KINONDONI.

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amezitaka Taasisi mbalimbali  za Dini kujitolea katika kuchangia madawati ili iweze kukabilina na changamoto za madawati katika wilaya hiyo.

Hapi, ameseyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokabidhiwa hundi ya sh. Milioni 19 kutoka kwenye kanisa la The Pool of Siloam Church kwa ajili ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati.

Amesema kitendo cha Kanisa hilo kusaidia tatizo la madawati ni jambo jema ambalo litasaidia kumalizana na changamoto ya madawati huku akitaka taasisi zengine kuiga mfano wa kanisa hilo.

Amesema kwa sasa Wilaya yake inakalibia kumaliza changamoto ya ukosekanaji wa madawati ambapo amedai mpaka kufikia mwisho wa mwezi uwenda tatizo la madawati akatika wilaya hiyo litakuwa limekamilika.

Hata hivyo, Hapi amewataka watendaji wa manispaa hiyo kuhakikisha wanazipeleka pesa hizo zilizotolewa kunakohusika na sio sehemu nyingine.

Aliongeza kuwa yeye yuko tayari kuwafuata viongozi wa dini ili waweze kumsaidia katika kampeni ya madawati katika kumaliza tatizo hilo katika halmashauri ya Kinondoni kwa wanafunzi kuachana na kukaa chini ya sakafu.

Amesema kanisa kujitoa huko atafikisha salamu kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutokana na mwitikio wa kutambua umuhimu wa elimu na kukubali kuchangia.

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya  amesema kuwa mchango wa fedha hizo kwa ajili ya madawati imetokana na mchango wa waumini wa kanisa hilo kwa kuguswa na madawati.

Eliya amesema ataendelea kuchangia katika hatua mbalimbali kutokana nafasi ya kanisa katika jamii hasa katika matatizo mbalimbali.
 Mkuu wa Wilaya, Ally Hapi akizungumza  na waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church ambao wamefika katika viwanja vya manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Jacob  Boniface.
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumkabidhi  hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church waliofika kushuhudia makabidhiani ya mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images