Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1243 | 1244 | (Page 1245) | 1246 | 1247 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Muziki Tanzania John Kitime akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ukaribisho wake katika shirikisho hilo leo Jijini Dar es Salaam,kushoto ni Raisi wa Shirikisho Addo November pamoja na Mjumbe wa Bodi wa shirikisho hilo,Daniel Msimamo.

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Shirikisho la Muziki Tanzania limewataka wananchi kuwapuuza wanamuziki wasio na maadili ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na shughuli zao za kimuziki.

  Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Rais wa Shirikisho hilo, Addo November alipokua akimtambulisha Katibu Mkuu wa Shirikisho la muziki ambaye ni John Kitime.

  “Mchakato wa kumtafuta Katibu Mkuu tumeufanya bila kukurupuka, nimefarijika sana kwa kukubali kwake ili kuhakikisha tunawakwamua wanamuziki kwasababu changamoto za muziki tulizokuwa nazo ni nyingi ikiwemo ya wanamuziki wasio na maadili”, alisema November.

  November aliongeza kuwa changamoto kubwa ni Sheria mbovu ya Haki Miliki ambayo mchakato wa kuirekebisha sheria hiyo pamoja na marekebisho ya sera ya utamaduni upo katika hatua za mwisho pia shirikisho limefanya jitihada za kuweka kipengele kinachozungumzia masuala ya sanaa kama haki ya msingi katika mchakato wa katiba mpya.

  Aidha, alisisitiza kuwa shirikisho hilo halipo kwa kumsaidia mwanamuziki mmoja mmoja bali ni kuhakikisha mfumo mzima wa muziki nchini unaweza kuwanasua wanamuziki wote na tasnia kiujumla ili muziki uwe na heshima.

  Naye, Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo, John Kitime amesema kuwa anategemea kutoa elimu kwa wanamuziki kuhusu kazi zao kupitia semina mbalimbali pamoja na kuimarisha shirikisho hilo ili vikundi vya wanamuziki viweze kusimama  na kukuza muziki ili iwanufaishe wanamuziki wenyewe.

  “Sheria ya Haki za Binadamu namba 245 iko wazi kuwa kila mtu anastahili kupata mafao yake yanayotokana na ubunifu wake kwahiyo kutowalipa ni kuvunja haki hiyo ya binadamu, kazi kubwa tuliyonayo ni kuwaelimisha wanamuziki kufahamu haki zao”, alisema Kitime. 

  Shirikisho la Muziki Tanzania linajumuisha mwanamuziki mmoja mmoja pamoja na vikundi ambalo limeundwa na vyama 7 ambavyo vimesajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania vifuatavyo; Chama cha Muziki wa Taarabu, Chama cha Muziki wa Rhumba, Chama cha Muziki wa Dansi, Chama cha Muziki wa Asili, Chama cha Muziki cha Wapiga Muziki wa Diski, Chama cha Muziki wa Kizazi kipya pamoja Chama cha Muziki wa Injili.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii

  HATIMAYE tiketi za mechi ya kufuzu mataifa Afrika 2017 (AFCON) kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) a Egypt unaopigwa kesho katika dimba la Taifa  zimeanza kuuzwa asubuhi ya leo huku kiingilio cha Chini kikiwa ni buku tano kwa viti vya Orange,kijani na Bulu na VIP B&C ikiwa ni 10,000.

  Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 10 jioni na mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa ukipelekea Misri wanahitaji sare ili kujiweka kwenye hatua ya kufuzu nayo Taifa Stars ikihitaji ushindi wa goli tatu na zaidi kufufua matumaini ya kuingia AFCON 2017.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu Jamii

  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kushirikiana na wenye nyumba kuhakikisha wapangaji katika nyumba wanaingia makubaliano ya mkataba na kuwa na picha zao.
  Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa watu wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kushindwa kupatikana pindi polisi wafanyapo operesheni kutokana na kupanga kwenye nyumba hizo lakini wakati akiondoka hawaagi na wenye nyumba wanakosa kuwa na taarifa za watu katika nyumba zao.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa wenye nyumba ambao watashindwa kufanya mkataba bila picha likitokea tukio dhidi ya mpangaji msalaba utamuangukia mwenye nyumba kuhusika katika uhalifu uliofanywa.

  Wakati huo Jeshi la Polisi linamshirikia Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), MT 66807 SGT, George Kwisema kwa tuhuma za kukutwa na vipande kumi vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. milioni 198 vikiwa katika gari yake yenye namba za usajili T.477 AXS aina ya Suzuki Vitara.

  Katika tuhuma za vipande vya meno ya tembo wanaoshikiriwa wengine, ni Shafi Muhibu pamoja na Asha Hassan ambao walikutwa katika gari iliyokuwa imebeba meno ya tembo.

  Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na sukari mifuko 35 ya Kilogram 50 ambao walikamatwa Chadibwa Mtaa wa Magogoni Kigamboni Mei 31 mwaka huu, ambayo ilikuwa haijalipiwa ushuru na waliokamatwa na tuhuma za sukari ni Said Bakari (25), Mkazi wa Mbagala , Hamadi Selemani pamoja na Bakari Masudi.

  Jeshi la Polisi linafanya upelelezi pia wa mtuhumiwa wa aliyewaleta wahamiaji Haramu na kutoweka katika mazingira ya utatanishi akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa na Katibu Mkuu wa Shiraka la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola, Eng. Shola Taylor wamekutana kwa mazungumzo ofisini kwake,  Mjini Dodoma kuhusu kuipatia Tanzania msaada wa kiufundi wa kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao yaani the National Cybersecurity Strategy na the National Broadband Strategy.

  Tanzania imekidhi vigezo vya kupatiwa msaada huo kwa kuwa tayari nchi ina sera, sheria na kanuni inayosimamia na kuendeleza Sekta ya TEHAMA nchini. Nyaraka hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Pia uwepo wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA kama vile Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo Mahiri cha Kutunzia Data.

   Wadau mbalimbali zaidi ya 60 wa kutoa Taasisi za Serikali, Sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya Serikali wamekutana kwa pamoja na kujadiliana namna ya kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usalama kwenye Mtandao. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam kuanzia tare he 31 Mei, 2016 na kumalizika tarehe 3 Juni, 2016.
  Aidha, Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola ambapo ni mwanachama hai anaestahili kupatiwa msaada huo kutoka Jumuiya hiyo. Nchi nyingine za Afrika ambapo zinaandaa Mkakati huo ni pamoja na Botswana, Rwanda na Malawi na nchi ambazo tayari zina Mkakati huo ni Uganda.

  0 0

  Mtaalamu wa Mazingira,Usalama na Afya wa Vodacom Tanzania,Nashon Mudaka(kushoto)akimuuliza swali mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mlimani jijini Dar es Salaam, Kuhusiana na siku ya mazingira dunia ambapo baadhi ya wafanya kazi wa kampuni hiyo walitembelea shuleni hapo leo kutoa elimu ya Afya na Usalama katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani itakayoadhimishwa rasmi tarehe 5 duniani kote.
  Baadhi ya wanafunzi wa darasa la 6 katika shule ya msingi Mlimani jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Mazingira kutoka Vodacom Tanzania.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika Kitabu maalum cha Kampuni ya Jiangsu Jiangdu construction group inayojenga Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii ya  wanachuo na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli machapisho ya tafiti mbalimbali za madini na mambo mbalimbali ya kimaendeleo zilizofanywa na wahadhiri wa chuo hicho mara baada ya kuwahutubia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha machapisho hayo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kumaliza mkutano huo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
  Viongozi Wakuu  wa Polisi   kutoka  nchi  mia moja  ambazo  zinachangia  polisi wao  kuhudumu katika ulinzi  wa amani  na usalama kupitia Umoja wa Mataifa,  wamekamilisha  mkutano wao wa siku moja  uliofanyika jana Ijumaa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

  Huu ni  mkutano kwa kwanza wa aina yake kuwahi kufanyika,  ambapo wakuu wa  Polisi ( IGPs) wamekutana kwa wingi na kwa wakati mmoja tangu shughuli za  Kipolisi  zilipoingizwa katika  Operesheni za Ulinzi wa Amani kupitia  mwamvuli  wa Umoja wa Mataifa.

  Katika mkutano huu na ambao washiriki walijadiliana, kubadilishana uzoefu, na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kubadilishana za   ulinzi na usalama katika nganzi  ya Kimataifa,  uliandaliwa na  Kitengo cha Polisi cha Umoja wa Mataifa ( UNPOL), kitengo ambacho ni sehemu ya Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa,  na   ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson.

  Ujumbe wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania   ni kati ya nchi  ambayo  kwa miaka  kadhaa sasa imekuwa ikitoa  Polisi wake kushiriki katika  misheni za ulinzi wa Amani  chini ya Umoja wa Mataifa,  umeongozwa  na  Naibu Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Maalum  Bw. Daniel Nyambabe.

  Akizungumza kwa njia ya  video  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban   Ki Moon,  amesema. “ Kutoka  Kabul hadi Kishansa na kutoka  Port-au Prince  hadi  Pristina,  Polisi wa Umoja wa Mataifa wanatekeleza majukumu yao katika mazingira magumu, hatarishi   na yenye changamoto nyingi. Lakini pamoja na  changamoto hizo bado polisi hawa welevu na mashuja wameendelea kulinda  jamii,wanaleta  mabadiliko katika  maeneo  hayo  na mengine mengi  kwa kurejesha utawala wa sheria na kufungua njia za upatikanaji wa  usalama na maendeleo  endelevu

  Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu  wa UN, Jan Eliasson,  ambaye alikuwa mgeni  rasmi katika  mkutano  huo , amewaambia  viongozi hao wa Polisi kwamba, kutokana na  changamoto  nyingi na kubwa zinazohusu     Amani na usalama wa Kimataifa,  utekelezaji wa  majukumu ya Polisi na kipolisi  kuanzia wale wanaohudumu na kushiriki katika  operesheni za Umoja wa Mataifa,  na  polisi wote duniani kote unatakiwa kubadilika na kuwa wa kisasa zaidi.

  Maeneo ambayo Polisi wanatakiwa kubadilika katika utekelezaji wa  majukumu yao ni  pamoja na kuwa na zana na vifaa vya kisasa, uwezo mkubwa na weledi wa hali  ya juu katika ukusanyaji  na uchambuzi wa taarifa za kiitelejensia,  uwezo  mkubwa wa kukabiliana  na  kwa wakati na mitandao  ya kihalifu ya kimataifa ukiwemo ugaidi.

  “Kabla ya  kumaliza  hotuba yangu,  ningepeda kusisitiza mambo kadhaa ya msingi ambayo ninaamini mtakubaliana nami. Maafisa wetu ( Polisi) wanatakiwa wawe tayari wakati wowote, wanatakiwa kuwa na vifaa  na zana za kisasa za kazi , wanatakiwa wawe wanaopewa   mafunzo ya hali ya juu,  wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwafundisha wengine, wanaopashwa kuwa na uwezo kuwa na  teknolojia za kisasa, wanatakiwa  wawe na fursa ya  kupata taarifa za kiitelejensia na kuzifanyia kazi ipasavyo,  uwezo wa kupata takwimu za uhalifu na vifaa vya kuzifanyia uchambuzi takwimu hizo” akasema Eliasson.

  Katika  kusisitiza hayo, pia ameongeza na kutilia mkazo nafasi  na fursa ya  Polisi wanawake  ya kushiriki  kwa wingi katika misheni za kulinda Amani. Na kuongeza pia kwamba, maafisa wa polisi wanatakiwa pia wawe ni  viongozi wenye uzoefu mkubwa, na wanatakiwa kuwa tayari kusaidia katika vita dhidi ya  unyanyasaji wa kijinsia na  kingono.
   Viongozi wengine waliowazungumza wajumbe hao ni  pamoja na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani  ( DPKO)  Bw. Herve Ladsous  pamoja na  Bw. Atul Khare Mkuu wa DFS.

  Baadhi ya  Mada zilizojadiliwa katika mkutano wa wakuu hao wa Polisi ni pamoja na  changamoto za uhalifu wa kimataifa na Operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa,  hali ya sasa na  ya baadaye kuhusu Polisi waohudumu katika  Umoja wa Mataifa   pengo,   fursa   nafasi   na  utaalamu wa Polisi katika Umoja wa Mataifa. Baadhi ya mada hizo  zilitolewa na  wataalam kutoka INTEPOL.
  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Operesheni Maalum, Bw. Daniel Nyambabe aliyeongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa kwanza kuwahi kufanyika katika Umoja wa Mataifa ambapo Viongozi Wakuu wa Polisi kutoka zaidi ya nchi 100 zinazochangia Polisi wao katika shughuli za amani na usalama kupitia Misheni za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa walikutana. Pamoja naye ni Lt.Col George Ita'ngare Mshauri wa masuala ya Kijeshi katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

  0 0

  On 28th May 2016, The Economist – English Weekly Newspaper published an article with heading “Government by gesture – A president who looks good but governs impulsively” (CLICK HERE). 


  The article, inter-alia misinformed the public and readers that since Dr. John Pombe Joseph Magufuli came into powers last year “the country has become totally uninvestable”. The Tanzania Investment Centre (TIC) would like to point out that the information portrayed by the newspaper is inaccurate, misleading and distortion of facts.

  TIC wishes to inform the public and readers of the following facts:-

  1.Since President John Magufuli came into power (from December 2015 to May 2016) TIC has registered 551 investment projects worth $ 9,211.88 million. Of all these projects 229 are owned by Tanzanians, 215 projects are owned by foreigners while 107 projects are owned through joint ventures.The projects are expected to employ 55,970people and bring multiplier effects to Tanzanians.

  The above registered projects by TIC for the past six months (December 2015 – May 2016) shows an increase of 20.31% compared to six months before President Magufuli came to power i.e. June-November 2015 where TIC registered 458 investment projects worth $ 5,727.29 million. Of all these projects 201 are owned by Tanzanians, 159 projects are owned by foreigners while 98 projects are owned through joint ventures. The projects are expected to employ 39,361 people and bring multiplier effects to Tanzanians.

  Generally, investments have increased during President Magufuli’s era which shows high investor confidence towards his Government. Attractive laws, peace, stability good and friendly policy as well asconducive investment environment are other major factors that have attracted both FDI and domestic investment during this period in Tanzania.

  2.The World Investment Report 2015 indicates that FDI rose by 14.5% in the United Republic of Tanzania. The Report noted that Tanzania, in 2014, regained its FDI inflows compared to the previous three years. In fact, its FDI inflows represented its highest level in 2014 given that it attracted slightly $ 2,142 million compared to $ 2,131 million recorded in 2013. This amount is significantly higher than the very low level of $ 640 million between 2005-2007 (pre-crisis). This achievement is due to natural gas reserves discoveries in the United Republic of Tanzania. Indeed, Tanzania remains the leading FDI’s recipient in the East African Community.

  3.       It is true that, the World Bank Doing Business Report 2016 ranked Tanzania 139 out of 189 countries compared to 145 out of 189 in 2014. TIC wishes to clarify thatDoing Business provides an aggregate ranking on the ease of doing business based on indicator sets that measure and benchmark regulations applying to domestic small to medium-size businesses through their life cycle. Economies are ranked from 1 to 189 by the ease of doing business ranking. Therefore this has nothing to do with the leadership of Dr. John Magufuli.

  4.TIC reaffirms  the  public and readers that  Tanzania is still the best place in East Africa to invest due to the fact that the country is peaceful and stable. Tanzania has a friendly business environment supported by good investment policy and legislation.  The Fifth Phase Government under the leadership of President Magufuli continues to take measures to improve investment climate as and when need arises.  Tanzania’s investment environment continues to offer predictable, transparent and strong long-term proposition to investors. Investment is legally protected against expropriation and nationalization. In terms of investment facilitation, the Tanzania Investment Centre (TIC), Zanzibar Investment Promotion Agency (ZIPA) and Export Processing Zone (EPZA) promote, coordinate and facilitate all investments in Tanzania. These are premier ports of call for investors coming to Tanzania through their well-established one-stop shop facilities. Tanzania’s geographic location position makes her as a natural regional business hub.  Tanzania borders 8 countries, 6 out of which namely Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia and Eastern part of the Democratic Republic of Congo, uses the Dar es Salaam port and Tanzania’s railways and roads for their sea freight.   This presents good opportunities for investment in infrastructure development, trade, transport and logistics.

  Therefore the statement that our country has become totally uninvestable has no truth in it and should be completely ignored by the public and readers.

  Issued by:

  ACTING EXECUTIVE DIRECTOR,

  TANZANIA INVESTMENT CENTRE (TIC),

  SHAABAN ROBERT STREET,

  P.O. Box 938,

  DAR ES SALAAM

  TANZANIA

  Date: 3rd May, 2016

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wakazi wa mikoa ya Dodoma na Iringa kutumia fursa ya kukamilika kwa kiwango cha lami barabara ya Dodoma Iringa kufanya shughuli za uzalishaji ili kujiletea maendeleo.

  Akizungumza wakati akikagua barabara ya Dodoma Iringa KM 260 Profesa Mbarawa amesema Barabara hiyo imelenga kufufua uchumi wa mikoa ya Iringa na Dodoma hususani hifadhi ya Ruaha na Vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa.

  “Barabara hii tuIiigawa katika sehemu tatu Iringa-Migori KM 95.2, Migori- Fufu KM 93.8 na Fufu –Dodoma Km 70,9 ili ikamilike kwa haraka na hivyo kuharakisha maendeleo ya watu wa Dodoma na Iringa “. Amesema Profesa Mbarawa.

  Profesa Mbarawa amesema kiasi cha sh. bil 4.6 itatolewa na Serikali ili kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa barabara ya Iringa mchepuo KM 7.3 itakayoanzia Kihesa –Kilolo kupitia Chuo Kikuu cha Iringa hadi Igumbilo ili kuondoa msongamano wa magari katikati ya Mji wa Iringa.

  Waziri Mbarawa amesisitiza nia ya Serikali ya kuukarabati uwanja wa Ndege wa Nduli mkoani Iringa ili kuwawezesha watalii wanaokwenda katika hifadhi ya Ruaha na Vivutio vingine vya Utalii Mkoani Iringa kutumia uwanja huo ili kuhamasisha uchumi wa mkoa wa Iringa.

  Naye Mbunge wa Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa kwa kukubali kujenga barabara ya Mchepuo ya Iringa na kumuomba aangalie uwezekano wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Iringa-Kalenga hadi katika hifadhi ya Taifa Ruaha yenye urefu wa KM 104.

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupanua barabara ya TANZAM eneo la Mlima kitonga na kumalizia ujenzi wa barabara ya Tosamaganga –Ugwachanya kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa daraja la Tosamaganga ili kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Iringa.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano yupo katika Ziara ya siku nne mkoani Iringa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu mkoani humo.
  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Eng. Daniel Kindole wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma –Iringa KM 260 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoani Iringa.
  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Iringa. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Kushoto Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuanza ziara ya siku nne mkoani Iringa.

  0 0

  Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

  Hatimaye utepe wa mtanange wa michuano ya Copa Amerika umekatwa alfajiri ya kuamkia leo, mishale ya saa 10:30 kwa saa za hapa nyumbani na kushuhudia wenyeji wa michuano hiyo, Marekani wakianza vibaya kwa kuchabangwa mabao 2-0 na watukutu wa Colombia.

  Mchezo ulianza kwa kasi na kumilikiwa zaidi na Colombia ambao iliwachukuwa dakika 8 tu kujipatia goli la kwanza, goli lililotokana na uzembe wa walinzi wa Marekani kushindwa kuokoa mpira wa kona iliyochongwa na Edwin Cardona's na kumkuta Christian Zapata na kuuweka kambani mpira huo.

  Wenyeji walijitahidi kufurukuta ili kusawazisha bao na kunako dakika ya 36 Clint Dempsey mchezaji aliye wasumbua sana Colombia alikosa bao baada ya shuti lake kuokolewa na golikipa Aspira, mpira huo ulisababisha Colombia kufanya shambulizi la kushitukiza (counter attack) na katika harakati za kuokoa mlinzi wa Marekani Yedlin akaunawa mpira na mwamuzi Roberto Gacia toka Mexico akaamuru upigwe mkwaju wa penati.
  Wachezaji wa Marekani pamoja na kocha wao Jurgen Krinsman walijaribu kugomea penati hiyo kwa kumzonga mwamuzi lakini haikusaidia kitu maana refa ndiyo mwamuzi wa mwisho, unajua akisema nyinyi ni nyani basi ni nyani, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez akaukwamisha mpira kimiani kiufundi kabisa na kufanya ubao usomeke 2-0.

  Kipindi cha pili Marekani walijitahidi angalau kupata hata goli la kufutia chozi lakini bahati haikuwa yao maana kunako dakika ya 58 Clint Dempsey aliyekuwa akilitia njaa goli la Colombia alipiga kichwa mpira wa kona na kumpita kipa Aspina lakini mpira huo uliokolewa kwenye mstari na mlinzi Perez na kunako dakika ya 64 Clint Dempsey alipiga free kick matata sana iliyookolewa na golikipa Aspina, hivyo kipyenga cha mwisho kilipopulizwa COLOMBIA 2 MAREKANI 0.

  Patashika hiyo itaendelea leo kwa michezo mitatu

  COSTA RICA vs PARAGUAY
  BRAZIL vs EQUADOR
  HAIT vs PERU

  0 0


  0 0

  Wadau kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson Mwanyika akiwashukuru wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakati wa ufungaji jan 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga akitoa neno la sukurani kwa mtoa mada (hayupo pichani) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.


  0 0

  EALA has granted leave to Hon Dora Byamukama to introduce a Bill entitled the East African Community Prohibition of Female Genital Mutilation Bill, 2016.

  The Bill which outlaws the cultural practice is seen as critical and in essence numbers the days of those that still engage in the cultural practice.

  Hon Byamukama states that the culture of FGM brings with it a number of complications including early child marriage and defilement, health complications that sometimes lead to transmission of HIV and AIDS, death and injuries to those who bear the practice.
  Hon Saoli ole Nkanae makes his contribution to the House.

  According to Hon Byamukama, with the advent of the Common Market Protocol which necessitates free-movement and cross-border nature, the influence of culture and hence spread is expected to increase if not checked.

  Contributing to the debate, Hon Judith Pareno remarked that surveys show an estimated 200 Million women in 27 countries in the Continent have undergone FGM.  Hon Saoli ole Nkanae noted that the practice is prevalent among the Maasai people in East Africa, terming it a serious matter. Also rising in support of the Motion was Hon Frederic Ngenzebuhoro.  

  Female genital Mutilation (FGM), is the ritual removal of some or all of the external female genitalia. UNICEF estimated in 2016 that 200 million women had undergone the procedures in 27 countries in Africa, as well as in Indonesia, Iraqi Kurdistan and Yemen, with a rate of 80–98 percent within the 15–49 age group in Djibouti, Egypt, Eritrea, Guinea, Mali, Sierra Leone, Somalia and Sudan. .The practice is also found elsewhere in Asia, the Middle East, and among communities from these areas around the world.

  Hon Dora Byamukama, has been granted leave to introduce the EAC Prohibition of Female Genital Mutilation Bill, 2016

  The practice is rooted in gender inequality and attempts to control women’s sexuality and ideas about purity, modesty and aesthetics. It is usually initiated and carried out by women, who see it as a source of honour, and who fear that failing to have their daughters and granddaughters cut will expose the girls to social exclusion.

  The health effects can include recurrent infections, difficulty urinating and passing menstrual flow, chronic pain, the development of cysts, an inability to get pregnant, complications during childbirth, and fatal bleeding.

  0 0

  By a Tanzanian
  The article which appeared in the Economist of May 28th 2016  (CLICK HERE) about the Tanzanian leader and government was both distasteful and amateurish to say the least. 
  The fact that the arguments advanced are full of insults and belittles a Head of State of a country with no shares in the Economist, is a sign of not only disrespect but a loss of focus by an otherwise “respected” international paper. 
  No wonder the current feeling worldwide is that The Economist we all used to almost adore is nowadays a mere Tabloid devoid of decency, quasi combative and totally disingenuous.
  Certainly, the Tanzania leader does not govern impulsively. Neither does he lead the government by gesture. To the contrary, he is fully committed to strengthening democratic principles of good governance and rule of law, leads a sustained fight against corruption and brings about efficiency and accountability in delivery of services to the people, subsequently lifting the majority of them out of poverty. 
  These efforts are what the Economist does not appreciate. Instead, the author of the article shows a high degree of ignorance and ineptness and intentionally attempts to mislead the world of a well thought through President Magufuli’s vision. 
  The President is evidently taking measures and carrying out reforms that strongly support favorable business climate that will spur speedy economic growth. He firmly thinks things through and with high degree of clarity for that matter. The majority of the people of Tanzania embrace what he is doing and stands for. Understandably the few, who have ripped off our resources unchecked over centuries and take them away to develop Europe, are not amused.
  The article fails to sharpen the arguments by showing reasons behind what it terms tax irrationality, claims of a country becoming uninvestable, but even discussing in all fairness America’s usual double standards in respect to upholding of human rights and arrogance of interfering in internal matters of other sovereign states. However, overall the investment climate in Tanzania continues to improve considerably. 
  The Dar es Salaam port is currently one of the most efficient and corrupt free ports in this part of the world. Cargo handling is done electronically and on a 24 hour basis. Meanwhile, businesses can now be registered on line. Air and surface transport network especially roads, offer the most cost effective connectivity in the region. Power supply is stable and connectivity has reached 40% which is one of the highest on the continent. The development budget for 2016/2017 focuses mainly on wealth creation and laying foundation for industrialization and has been increased from 27% the previous fiscal year to 40% this year. Surely, it is inconceivable to allege that this government is being led by gestures!
  On the other hand, it is a blatant and an unqualified lie to assert that the country has expelled thousands of Kenyan teachers who purportedly did not have proper working permits. Arguably Tanzania is one of the few countries with very liberal immigration and labor laws making it a favored destination for people from all over the world including conservative UK. Of course since the author might have been paid to insult us, it is not surprising that some disgruntled and erratic opposition leaders are being quoted to paint a negative image of the country.
  Yes Africa needs strong men and strong women to lead strong institutions. 

  And yes, Tanzania is just doing that for the benefit of her citizens. Those businessmen or so called foreign investors who used to siphon our resources with absolute impunity using corrupt government leaders and politicians, who do not what strong men and women, should count themselves unwanted. 
  They will continue to use Tabloids like the Economist to discredit committed and honest governments such as that led by President Magufuli. Definitely time is running out for them and Africa is no longer the same old highly indebted and dependent continent. 
  Tanzania’s new vision and economic model will work for our people and not foreigners seated in London who still think the continent can relapse into absurdity under crocked white stocky colonialists. The country is taking its destiny in its own hands by instilling a culture of high degree of discipline, accountability and efficiency with emphasis on prudence, proper collection and utilization of revenue, control government expenditure and allow private and public investments to flourish. 
  These agents of change stand out high on the current government’s development agenda.  President Magufuli remains focused and is firmly in charge of the destiny of Tanzania and God bless him abundantly.

  It is time we completely stop begging sprees to 
  London, Washington, Brussels etc.
  ONLY IN TANZANIA: Out-going President Jakaya Mrisho Kikwete hands over power with a smile and huge laugh from his predecessor Dr. John Pombe Joseph Magufuli. 

  0 0

  Kundi la pili la washindi wa mamilioni ya Tusker watangazwa.
  Wiki iliyopita ilishuhudiwa washindi kumi kutoka mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Kilimanjaro wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni inayoendelea ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli na Uwiniinayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti. 

  Katika droo ya pili iliyochezeshwa leo, washindi wengine kumi walitangazwa. Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha walitangazwa washindi kumi ambao ni Rose Mkwizu, Sijali Ally, Anna Lazaro kutoka Dar es Salaam, Elizabert Wiliam kutoka Mlandizi –Pwani, Josephat Lukindo,George Mlay kutoka Kilimanjaro,Geofrey Manangwa kutoka Tanga, Wanzagi na Lucas Fransis kutoka Mwanza na Umoja Nyakwa kutoka Morogoro. 

  Mbali na washindi hao ambao walijipatia zawadi ya pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure tangu promosheni ilipoanza. Bado kuna wiki nane ambapo zimebaki Millioni 80 kushindaniwa kwa kipindi hicho kilichobaki cha promosheni hiyo.

  Naye mmoja wa washindi Elizabert Wiliam alisema kuwa Shoo ya kwanza iliyorushwa kupitia runinga ya ITV ndiyo iliyomsukuma kushiriki promosheni hiyo. “Nilitazama droo ya kwanza wiki iliyopita na siku zote mimi ni mtumiaji mzuri wa bia ya Tusker, baada ya muda punde tu nilienda kunywa huku nikiwa na shauku ya kushinda tu na kuingia kwenye droo” alisema bi Elizabeth. Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wao kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla. Aliongeza kuwa pesa aliyoipata ataitumia katika kukuza biashara zake.

  Naye Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tannzania ambako sasa mikoa ya kanda ya ziwa imeungana nasi katika promosheni hii wiki iliyopita. Tuna washindi kutoka nchi nzima, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Dar es Salaam. 

  Tunapenda kuwathibitishia wateja wetu kuwa promosheni hii si ya watumiaji wa bia ya Tusker waliopo Dar es Salaam tu bali kwa ushahidi huu wa washindi kutoka mikoa mingine unatosha kuthibitisha kuwa ni ya nchi nzima.

  Washindi wetu wa wiki iliyopita watapokea zawadi zao za fedha taslim Million 1 katika hafla fupi ya makabidhiano itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam na Moshi.
  Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akiokota vocha ya ushindi katika droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akitazama kwa makini mchakato mzima, anayefuata ni muongozaji wa shoo hiyo Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni mtangazaji wa ITV
  Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akimkabidhi vocha ya mshindi afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua ili kuhakiki taarifa za mshindi wakati wa droo ya pili ya promosheni ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo hiyo, pembeni yake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akifurahia jambo alilosikia kutoka kwa mmoja ya washindi kupitia njia ya simu.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki (katikati) akiwa na mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (Kulia) na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi wakishiriki zoezi la Usafi katika eneo la Feri.Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Kyuki akiwa na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi wakizoa taka katika eneo la FerWatumishi wa Tume wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi eneo la Feri.
   

  0 0

  Katika kutambua mchango wa Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na kuweka mbele utu wa binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, wajumbe kutoka nchi 44 za kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua na kuiidhinisha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo utakaofanyika mwaka 2018.

  Katika Mkutano Mkuu wa Abuja changamoto iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia wananchi wake nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa serikali zao kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu. Aidha, wajumbe wa Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi wa Afrika kuweza kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo unaotokana na vipato vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki nyumba za gharama nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya gharama nafuu, riba kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na ukosefu wa ardhi ya kujenga nyumba hizo.

  Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu umeazimia nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano Saguya, Abuja, Nigeria).

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia). Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.

  Mchoro huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.


  0 0

  Hivi ndivyo lionekanavyo Daraja la Mungu lililopo nje kidogo ya Mji wa Kiwira, Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, ni Daraja ambalo lilijitengeneza lenyewe kwa maajabu ya Mungu na hakuna mtu au mafundi walio husika katika ujenzi wa daraja hilo.

  Baadhi ya wenyeji wa eneo lililopo Daraja hilo, wanasema kwamba kipindi cha nyuma (yaani enzi za mababu zetu) walikuwa wakihangaika sana kujenga daraja katika eneo hilo na jitihada za ujenzi wa daraja katika eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kutokana na kila walipokuwa wakijenga wanakuta pana bomoka bila ndoto yao hiyo kutimia.

  Ila siku moja wa walipo rudi tena kuendelea na ujenzi wa daraja lao, ndipo walipolikuta daraja hilo lililo jitengeneza kwa miujiza ya Mungu, ndipo hapo lilipopewa jina la Daraja la Mungu.

  Daraja hilo lenye ukubwa wa aina yake lililo katiza juu ya maji katika mto wa Rungwe linapitisha watu kwa kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine. 
  Pichani ni sehemu ya pili kutoka juu ya Daraja hilo la Mungu ambapo maji yake huwa yanatowa mvuke muda wote.
  Sehemu ya upande mwingine wa daraja hilo la Mungu kukiwa na daraja lingine lililojengwa baadae.
  Upande wa chini wa daraja lingine lililo jengwa na binadamu lipo Sanjari na Daraja la mungu.
  Hii ni moja ya alama yenye kuonyesha tarehe ya mtu mmoja mwenye asili ya India anae sadikiwa kupoteza maisha juu ya daraja hilo kwa kukosea masharti ya daraja hilo miaka ya nyuma, hivyo baadhi ya wahindi huja katika eneo lilipo jiwe hili na kufanya ibada zao. jiwe hili lipo juu ya daraja la mungu.
  Muonekano wa daraja lilojengwa na watu lililopo mkabala na daraja hilo la mungu.PICHA ZOTE NA MR. PENGO WA MMG, Nyanda za Juu Kusini.

  0 0
 • 06/04/16--03:25: TAARIFA YA MSIBA
 • Eng Joseph Shega na Mkewe wa Nyumbu Kibaha wananasikitika kutangaza kifo cha Mzazi wao Mwalimu Francis Temba kilichotokea  tarehe  June 3, 2016 saa 1 jioni katika Hospitali ya Mpanda

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu wilayani mpanda mkoa wa Katavi

  Habari ziwafikie  Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Loide Ipinge aliyoko nchini Namibia, Dr Nima Shidende wa UDOM, Dr Mary Sangu wa Dodoma ,Dr Frenk Shega wa Maunt meru Hospitol arusha Wanafunzi wote waliofundishwa na marehemu Mwalimu Francis Temba wana mpanda na wana Rukwa ndugu na jamaa wote wanao husika na msiba huo

  Bwana ametotoa Bwana ametwa Jina lake lihimidiwe

older | 1 | .... | 1243 | 1244 | (Page 1245) | 1246 | 1247 | .... | 3348 | newer