Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

DIWANI KATA YA CHANG'OMBE AFANYA ZIARA KEKO FURNITURE.

$
0
0
Mwakilishi wa wafanyabiashara Keko, Samuel kushaba akiwaonesha waratibu wa maendeleo maeneo wanayofanyia kazi ambapo amelalamikia gharama ziazowakabili kwa kuweza kukodi maeneo takribani matatu na yote wanayalipia kwa hela nyingi.
 Diwani wa kata ya Chang'ombe,Benjamini Ndalichako (Katikati) akiwa katika ziara ya upekuzi yakinifu katika maeneo ya biashara ya Keko na kuangalia changamoto zinazowakabili wafanyabioshara hao.
Diwani kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake na kueleza changamoto alizoziona na kusema atalifanyia kazi kwa kushirikiana na waratibu wa maemdeleo Manispaa ya Temeke na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wenye eneo kubwa ambalo wanahitaji kufanya uwekezaji wa kujenga maeneo ya biashara na kuwakodisha.
Haya ni mazungira hatarishi yakiwa katikati ya wafanyabishara wa eneo la Keko Furniture ambalo yanaweza kuwa chanzo cha mlipuko wa magonjwa kwa wafanyabishara na wakazi wa eneo hilo.

Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii.
DIWANI wa Kata ya Chang'ombe Benjamin Ndalichako amefanya ziara katika maeneo ya biashara samani za ndani maeneo Keko Furniture na kujionea mazingira hatarishi wanayofanyia kazi na kuweka mikakati ya kuwasaidia wafanyabishara hao akishirikiana na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo wanakadiriwa kuwa na eneo kubwa sana ambalo wanaweza kuwekeza kwa kujenga maeneo yatakayotumika kwa ajili yao.

Ndalichako akiwa ameambatana na baadhi wa wajumbe wanaoratibu maendeleo wilaya na kujionea mazingira wanayofanyia kazi wafanyabiashara hao huku baadhi yao wakiwa hawalipi kodi. Amesema lengo kuu la ziara hiyo ni upekuzi yakinifu  ambapo wameona  vitu vingi sana ikiwemo mazingira hatarishi hasa ukizingatia hawana vifaa vya kujikinga na ajali pamoja na maradhi ikiwemo kifua kutokana na vumbi la mbao pale wanaporanda.

"Mazingira wanayofanyia kazi ni hatarishi na tumeona kwahiyo tunayemuwakilishi wa Salvatory Hinjo na ameahidi kulishughulikia hilo kwa kupeleka kwa mtendaji mkuu kwani wana eneo kubwa sana wanaweza kuwekeza kwa kujenga majengo watakayofanyia biashara,"amesema Ndalichako.

Kutokana na hali aliyoiona Ndalichako ameamua kukaa na wafanyabishara wa eneo hilo na kuzungumzia mazingira hatarishi pamoja na mgogoro uliopo baina ya NHC na wafanyabiashara ambao wamepewa taarifa ya awali ya kuhama kwenye maeneo yao na kuweka msimamo kuwa limeshafika mkononi mwake na atalishughulikia.

Naye mwakilishi wa wafanyabiashara wa Keko Samuel Kashaba  amesema wanachokiomba ni kupatiwa maeneo hayo na sio watakapojenga wapewe watu wengine wakati wao wapo siku nyingi na hata kabla ya kuhamishwa wapatiwa sehemu ambayo watahamishia kazi zao. Hata hivyo amelalamikia mazingira wanayofanyia kazi na kusema hawana budi kukodi maeneo matatu tofauti na gharama zinazidi kuwa nyingi kwa upande wao.

Maafisa Maendeleo ya Jamii Kuchochea ukuaji wa Uchumi.

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo.
MAAFISA Maendeleo ya jamii walioajiriwa katika Halmashauri hapa nchini  wameongezeka kutoka 1,855 mwaka 2005 hadi kufikia 2,675 ikiwa ni ongezeko la asilimia 44 hali inayosaidia kuboreshwa kwa huduma za jamii.

Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Wazee na Watoto wakati wa Mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Wizara hiyo katika kukuza Sekta ya Maendeleo ya Jamii hapa nchini.

Akifafanua Bi. Neema amesema kuwa chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru kimepandishwa hadhi  kuwa Taasisi ya Elimu ya Juu inayotegemea kiutendaji hali itakayosaidia kuongeza kiwango wa Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaohitimu katika chuo hicho.

Pia Bi. Neema  amesema kuwa vyuo vinavyosimamiwa na Wizara hiyo vinatoa wahitimu wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira kutokana na umahiri na uzoefu wanaojengewa wakiwa vyuoni.
Aidha wahitimu wa Kidato cha nne na kidato cha sita wenye utashi katika fani ya maendeleo ya jamii wanakaribishwa kutuma maombi yao kwenye “Central Admission System” (CAS),kupitia www.nacte.go.tz.

Taaluma ya Maendeleo ya Jamii inatolewa kwa kuzingatia taratibu na Kanuni zinazotolewa na kusimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).hivyo NACTE inasimamia uandaaji wa mitaala inayotumika katika utoaji wa mafunzo,muda wa masomo,mitihani na Vigezo vyake,pamoja na ubora wav yeti wanavyotunukiwa wahitimu kwa kila ngazi.

MASHAUZI, SNURA, ROMA MKATOLIKI NA WAZEE WA SINGELI KUISHIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII

$
0
0
Jumamosi hii ya Juni 4 mbona ‘kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani mkali kutoka kwa mastaa wa taarab, bongo fleva na singeli.

Ni onyesho kubwa la na mwisho kabla kuelekea mapumziko ya mwezi mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic ataumana jukwaa na Snura, Roma Mkatoliki, Sholo Mwamba na Man Fongo.

Msemaji wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema onyesho hilo la kipekee limezingatia muziki wa kila njanja ili kuleta ladha isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa show.

Mbizo amesema kupitia onyesho hilo mashabiki watajionea wenyewe ni mzuiki upi wenye nguvu zaidi kati ya taarab, bongo fleva, singeli na hata rumba kutokana na ukweli kuwa Isha Mashauzi mbali na taarab lakini pia ana ngoma zake kali za muziki wa rumba.

Naye Isha Mashauzi amesema atalitendea haki onyesho hilo hasa kutokana na ukweli kuwa hajapanda jukwaa la Dar Live kwa takriban miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi pekee ya kutaka kiu ya mashabiki wake watakaofika kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi wa burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.

WACHEZAJI BORA WA MWEZI APRIL NA MEI WAPATIWA VITITA VYAO TOKA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Mchezaji wa Yanga,Juma Abdul, akiwa ameshikilia hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/=baada ya kukabidhiwa rasmi na wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ya kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Mei 2016.
Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/= Mchezaji wa Yanga, Juma Abdul, baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Mei 2016,Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katikati Ofisa wa Ligi, Joel Balisiya.
Mchezaji wa Mtibwa Suger,Chiza Kinyuya akiwa ameshikilia hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/=baada ya kukabidhiwa rasmi na wadhamini wakuu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ya kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi April 2016.
Mchezaji wa Mtibwa Suger,Chiza Kinyuya akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/-toka kwa Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude(kushoto)baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi April 2016,Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Katikati ni Ofisa wa Ligi,Joel Balisiya.

Wizara ya Ardhi yakutana na wadau kutoka TAMISEMI kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya Ardhi

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt Yamungu Kayandabila akizungumza jambo kwenye kikao na wadau kutoka TAMISEMI kuhusu maendeleo ya sekta ya Ardhi nchini.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ATAKA RAIS DKT.MAGUFULI AOMBEWE.

$
0
0
Waziri wa kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizindua tamasha la urafiki katika viwanja vya Ndege mjini Morogoro jana Juni 2 ,tamasha lililoandaliwa na ushirikiano wa makanisa katika mkoa wa Morogoro na kuongozwa na mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren.
Mkazi wa Morogoro aliyekuwa anatembea kwa shida baada ya kuotwa na uvimbe mkubwa eneo la siri akiruka ruka kwa furaha baada ya kuombewa na kupona na mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren.

WAZIRI wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amelaani mauwaji ya kinyama kikatili yanayoendelea kuibuka nchini kuwa yasipewe nafasi na kutaka kila mtanzania kwa imani yake kuliombea Taifa kuondokana na mauwaji hayo pia wakati wote kutoacha kumwombea Rais Dr John Magufuli kwani kazi anayoifanya ni ngumu zaidi.

Huku akichangia Tsh milioni 2 ili kuchangia huduma za tamasha la Urafiki la kuliombea Taifa mkoani Morogoro kuendelea mjini Morogoro kwa madai kuwa huduma hiyo ni tiba ya maovu yanayoendelea kujitokeza hapa nchini kwa watu kuchinjwa kikatili kila kona ya nchini.

Waziri Nchemba alisema kuwa tukio la mashekhe na waumini wao kuchinjwa msikitini si jambo ambalo watanzania tumezoea kuliona ama kusikia pia mauwaji ya Mwanamke Aneth Msuya wa Dar es Salaam na watu nane kuchinjwa Tanga na lile la Mwanza si matukio ambayo yamezoeleka Tanzania , hivyo kutaka suala hili lisiachwe kuendelea na badala yake kuzidi kuliombea Taifa . 

“ Tunapokusanyika na tunapokuwa faragha katika ibada zetu tuliombee taifa letu ……jambo la pili kwa uzito huo huo tumwombee Rais wetu mpendwa Dr John Magufuli kazi anayoifanya ni ngumu … kazi anayoifanya ni kwa niaba ya watanzania wote na utashi ule anaoendanao ninyi wenyewe mliomba sana kabla ya kumpigia kura ….uzoefu unaonyesha mabadiliko huwa hayaji rahisi rahisi adui huwa hakubali kushindwa kirahisi kwa hiyo kila tunapoongea na Mungu wetu tukumbuke kumwombea Rais wetu ili kila mema anayoliwazia Taifa yaweze kutimia” alisema waziri Nchemba 

Kuwa kwa upande wake kila anapoona watumishi wa Mungu wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya huduma huwa haachi kuwasogelea japo kushikana nao mikono kama sehemu ya kupokea baraka kutoka kwao kwani wapakwa mafuta wakisema tu ubarikiwe Mungu juu mbinguni huweka tiki ya baraka. 

“Na hivyo ndivyo nilivyopata hata ubunge nilikuwa sina gari wala baiskeli na wazazi wangu walikuwa wanaishi katika nyumba ya tembe wakiwa na maisha magumu nikaenda kanisani kulikuwa na Harambee japo sikuwa na pesa nyingi niliamua kuchangia kidogo tu …..watumishi wale wakasema Ee Mungu mjalie haja ya moyo wake huyu kijana na mimi nilikuwa nikiwaza ubunge kweli ubunge ukatiki …..na hivi leo amekuja mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akasema kwa lugha ya kiingereza kuwa Ee Mungu timiza ndoto ya kijana huyo na mimi ndogo hiyo inaendelea kuota hivyo hivyo kwa hiyo najua na ninyi mtanikumbuka katika majukumu ambayo nimepewa na Rais ……leo baada ya saa 4 asubuhi hatukuwa na ratiba ya vikao vya bunge nimelazimika kuja Morogoro kuifanya kazi hii na leo hii nitageuza bungeni “ 

Kwani alisema majukumu ambayo anayatumikia pia yana harufu ile ile ya ambayo amewaomba kuzidisha maombi kuliombea Taifa kwani yana harufu ya umwagaji wa damu . 
Alisema waziri Nchemba kuwa alipoteuliwa na Rais Dr Magufuli kabla hata ya kuapishwa alipata taarifa ya mifugo kuuwawa na watu kuchinjana kwa kukatana mapanga mkoani Morogoro ambayo yalimkumbusha mapigano ya chuki na wivu kwa Abeli na Kaini mmoja akiwa mkulima na mwingine mfugaji.

“ Tuliombee Taifa letu kila mmoja afanye kazi inayomlete kipato pasipo kuwa na wivu na bila kuwa na dharau kwa kazi ya mwenzake ….kila nikipita huwa nawaeleza watumishi wangu kuwa hakuna mali ,mifugo,shamba ama kitu chochote chenye dhamani kubwa kuliko uhai wa mwa wanadamu” 

Kuwa serikali itatengeneza mazingira bora ya wakulima ama wafugaji kufanya kazi zao kwa uhuru na amani japo kila mmoja anapaswa kutambua kuwa uhai ni zaidi ya yote. 


Kwa upande wake mhubiri wa huyo kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren limpongeza waziri Nchemba kwa kujiweka mbele katika huduma.

WADAU WATAKIWA KUTOA MCHANGO WA KUBORESHA KANUNI ZA UPATIKANAJI WA MBOLEA NCHINI.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Wadau wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.

Gharama hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu ya kilimo.Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa wakati.

“Wakulima hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.Kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala wadogo 500.

Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.Mawakala hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.

Aidha, shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.Vile vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.

Dkt. Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na Nigeria.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka akifungua warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu akibainisha baadhi ya changamoto zinzoikabili sekta ya mbolea nchini ikiwemo bei ya mbolea kulingana na uwezo wa wakulima wengi na muda mrefu wa majaribio kwa mbolea inaingia nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa mbolea kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla. Wa kwanza kushoto Mgeni rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka.
Mtaalamu wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt. Consolatha Mhaiki akichangia mada juu ya matumizi ya mbolea ni yanavyopaswa kuendana na aina ya udogo kwa uzalishaji bora wa mazao wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.

'KAKA' KUIKOSA COPA AMERIKA CENTENARIO 2016, MESSI NAYE TIA MAJI TIA MAJI.....

$
0
0
Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Yakiwa yamesalia masaa machache kipyenga kupulizwa kuashiria ufunguzi wa michuano ya Copa Amerika, kiungo mahili na mkongwe wa timu ya taifa ya Brazil Ricardo Kaka ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuumia kifundo cha mguu. Kaka ambaye naye alichukuwa pahala pa kiungo wa Bayern Munich Douglas Costa, sasa na yeye nafasi yake itazibwa na kiungo kutoka klabu ya Sao Paulo, Henrique Gauso.
Kwa upande mwingine mchezaji bora wa Dunia mara tano, Lionel Messi aliwapa wakati mgumu mashabiki wake na waargentina kwa ujumla kuwa naye angekosa michuano hii kufuatia kupandishwa kizimbani katika mahakama moja nchini Hispania baada ya kushitakiwa kwa kosa la kukwepa kodi. 
Messi ameshitakiwa pamoja na Baba yake kwa kosa hilo, wote wawili wakana kosa hilo na Messi amesema yeye hafahamu chochote kinachoendelea kwa sababu kazi yake ni kucheza mpira tu na mambo yake mengine ya nje ya uwanja yanafanywa na watu wengine wakisimamiwa na Baba yake, Baada ya hapo Messi alipanda ndege kuelekea Marekani ili kujinga na wenzake kwa ajili ya mtanange huo wa michuano ya COPA AMERIKA CENTENARIO.

Kwa ufupi tena tuzidadavue timu mbili ambazo nchi zao zinadaiwa kwa kuwa na magenge makubwa ya wauza dawa ya kulevya (kwa lugha ya mtaani wanaita ngada), lakini sisi hayo hayatuhusu.
MEXICO

Kwenye viwango vya ubora wa soka vya shirikisho la soka duniani FIFA, mexico inakamata nafasi ya 16. Ikiwa kundi C na nchi za Jamaica, Uruguay na Venezuela, Mexico itawategemea sana nyota wake vijana kama vile mshambuliaji Javier Hernandez'chicharito' wa klabu ya Bayer Leverkeusen, mlinzi Paul Aquilar kutoka Club America, kiungo wa Porto Hector Herrera na Oribe Peralta wa Club America, chini ya kocha JUAN CARLOS OSRIO wanazungumziwa kuwa wataleta ushindani sana.
COLOMBIA

Chini ya kocha mzoefu JOSE PEKERMAN colombia ikiwa na wachezaji wanyumbulifu na vijana wengi ambao hutumia zaidi mchezo wa kumiliki mpira watatoa upinzani mkubwa katika kundi lake na hasa katika mechi ya ufunguzi kati yao na wenyeji Marekani.Ikiwa katika nafasi ya 4 ya ubora wa viwango vya FIFA, colombia itawategemea zaidi akina James Rodriguez wa Real Madrid, mshambulizi Roger Martinezwa Rancing Club, kiungo wa Juventus Juan coudrado na mshambulizi Carlos Barca wa As Milan.

Kipyenga kinapulizwa leo hivyo pitia kurasa hii ili upate kila kinachojiri huko Marekani.

AMERICAN REGULATORS WIELD A BIG STICK, BUT NOT ALWAYS FAIRLY

$
0
0
LIKE politicians, financial regulators know that late on a Friday is a good time to slip out bad news. The Financial Crimes Enforcement Network (FinCEN), part of America’s Treasury, chose February 19th to announce it had rescinded a devastating finding against a European bank suspected of facilitating money-laundering. The withdrawal, less than a year after the designation, looks like a climbdown.

In March 2015 FinCEN branded Banca Privada d’Andorra (BPA) as a “primary money-laundering concern”, saying its top managers had moved cash for criminal groups. This so-called “311” measure (after the relevant section of the Patriot Act of 2001) is usually crippling for the bank concerned, because in effect it cuts it off from the American financial system and any banks that participate in it. 

BPA was no exception: the government of Andorra, a mountainous financial haven nestled between France and Spain, ended up taking over the bank despite objections from its majority shareholders, the Cierco family; its Madrid-based wealth-management arm was liquidated. The Ciercos, insisting there was no legal basis for FinCEN’s move, sued in the American courts.

GEPF WATOA MSAADA WA BAISKELI MAALUM KWA WALEMAVU (WHEELCHAIRS) KWA KIKUNDI CHA TANZANITE DISABLED ARTS GROUP KILICHOPO JIJINI DAR

$
0
0
Balozi wa Mfuko wa GEPF,Rose Ndauka akielezea majukumu yake kama balozi na msanii wa filamu katika kuyaunganisha makundi mbalimbali ya kijamii kujiunga na Mfuko wa GEPF. Meneja Masoko na huduma kwa wateja wa Mfuko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina.
Balozi wa Mfuko wa GEPF, Rose Ndauka akikabidhi rasmi zawadi hizo kwa mwenyekiti wa kikundi huku akishuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Bw Aloyce Ntukamazina. Kulia ni Meneja Masoko na huduma kwa wateja wa Mfuko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina 
Katibu wa kikundi cha Tanzanite Disabled, Saidi Machako akitoa neno la shukurani kwa ujumbe kutoka GEPF kwa msaada wa baiskeli za kutembelea walizozipata, ambazo zitawasaidia katika shughuli zao za kila siku.
Pichani wasanii wa kikundi cha ngoma cha Tanzanite Group wakitoa burudani kwa wageni wao kabla ya kupokea msaada huo.
Mmoja wa wanufaika wa msaada huo akifurahia zawadi hizo na Rose Ndauka.

Banc ABC yaanzisha huduma ya kukuza biashara Afrika

$
0
0
Bank ABC imeanzisha huduma mpya kwa wafanyabishara wakubwa kuhamisha and kuingiza mitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya elektroniki.Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumatano hii, Mkuu wa kundi la Benki hiyo katika ukanda wa Afrika, Dk. Mabouba Diagne alisema wametenga Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya Sh billion 40) kwa ajili ya mpango huo unaolenga kuimarisha biashara miungoni mwa nchi za Afrika.

“Tumeanzisha huduma hii mpya kwa ajili ya kurahisisha na kukuza biashara miungoni mwa wafanyabishara wakubwa barani Afrika. Tunataka wafanyabiashara waweze kufungua milango yenye fursa nyingi za kibishara barani Afrika,” Dk. Diagne alisema.Alisema Banc ABC imezimia kuwawezesha Watanzania kutumia teknolojia mpya ya kuhamisha mitaji na fedha nyingi si ndani ya nchi tu bali nje ambako kuna fursa nyingi za biashara zisizotumika.

“Mara nyingi wafanyabishara wengi wa hapa nchini wanaofanyabishara nan chi jirani wamekuwa wakilalamika kukosekana kwa huduma bora za kuhamisha fedha kwa wingi. Sasa jawabu limepatikana kwa Banc ABC kuanzisha huduma za kisasa za kuhamisha mitaji,” alisema.

Alisema watu wanaweza kuhamisha mitaji hata fedha nyingi nchi za nje kwa kutumia simu za mkononi bila kuathiri biashara.“Tumeanzisha huduma hii kwa sababu biashara baina ya nchi za Afrika ni jambo muhimu la kuwezesha nchi na wafanyabishara waweze kutumia fursa nyingi zilizomo barani Afrika kutokana na bara hili kuwa na rasilimali nyingi asilia,” alisema kiongozi huyo msomi mwenye shahada ya juu ya uzamili ya hisabati.

Alisema suala la kubadilishana na kuhamisha mitaji ni biashara kubwa duniani kwa sababu mitaji ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu.Mapema mkurugenzi wa Banc ABC Tanzania, Bw Dana Botha alisema tayari benki hiyo imeanzisha mtandao wa matawi 100 hapa nchini na kuwa miungoni mwa benki imara.Naye Mtendaji Mkuu wa kundi la benki hiyo Dk. Blessings Mudavanhu alisema kuwa benki hiyo ambayo imesajiliwa katika soko la fedha la London, ilizindua aina ya bidhaa yake mpya na kujitanua kimataifa baada ya kuungana na Atlas Mara.

“Tutatumia jamvia la teknolojia ya habari na mawasiliano. Tunataka watu waanchane na kuandika cheki nyingi na kutumia gharama kubwa za miamala ya katatazi badala yake watumie simu za mkononi,” alisema Dk Madavanhu.Alisema benki hiyo ambayo inaendesha biashara katika nchi za Tanzania, Nigeria, Afrika kusini, Botswana Zimbabwe, Rwanda, Burundi na Zambia imedhamiria kuwa benk kubwa inayokuza biashara miungoni mwa nchi za Afrika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto, Jones Mwalemba, naJohn Du Toit.

Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akibadikishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo, John Du Toit katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni  BancABC Tanzania, Khalifa Zidadu (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa Superdoll, Sateesh Babu Desu na Prasanthar Govinder pia wa Superdoll.
 

TANGAZO LA WASTAAFU WOTE KUTOKA LAPF

$
0
0

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAANDAA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA MFUKO HUO

 
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA LAPF KUWA KUTAKUWA NA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHI NZIMA KUANZIA TAREHE 13.06.2016 HADI TAREHE 24.06.2016 KUANZIA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI. TAREHE KAMILI KWA KILA WILAYA INAPATIKANA KWENYA MAGAZETI YA MWANANCHI YA TAREHE 06.06.2016, 08.06.2016 NA 10.06.2016, DAILY NEWS LA TAREHE 07.06.2016 NA 09.06.2016 NA TOVUTI YA MFUKO www.lapf.or.tz KILA MSTAAFU ANATAKIWA KUFIKA NA PICHA MOJA NDOGO (PASSPORT SIZE) NA KITAMBULISHO CHOCHOTE.

KILA MSTAAFU ANAYELIPWA PENSHENI NA LAPF UNAOMBWA UJITOKEZE KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI ZILIZO KARIBU NAWE.

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0767-600043 AU 0753-999991.

“STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF”

MABILIONI YA JK YAKUMBUSHWA BUNGENI LEO

MKWASA AWAPA ONYO MAFARAO, ASEMA ANAJUA MBINU ZAO ZOTE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars",  Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anazifahamu mbinu zote wanazotumia timu za Ukanda wa kiarabu na ameshajizatiti kuweza kupata matokeo kwani ana wachezaji wa kila aina wanaoweza kutumia mfumo wa aina yoyote.

Stars wanakabiliwa na mchezo wa kufuzu kwenda kwenye fainali za mataifa Afrika AFCON 2017 wakiumana na Mafarao wa Misri mechi itakayopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema kuwa, wachezaji wake wote wanajua umuhimu wa mchezo huo na wanataka kufungua ukurasa mpya katika historia ya soka la hapa nchini kwa kufuzu kwani kama wakifanikiwa kupata matokeo dhidi Misri na hilo linawezeka kama kipindi cha kwanza wakiweza kupata goli la kuongoza ambalo anaamini litawaondoa mchezoni.

"Tumejiandaa kikamilifu na kama tukipata matokeo kipindi cha kwanza tutawaondoa mchezoni na kikubw zaidi wachezaji wanajua kinachowapelekea na kama tukifanikiwa kushinda kwa goli tatu na zaidi tutapata nguvu zaidi ya kuwafunga Nigeria hata kama watakuwa nyumbani,"amesema Mkwasa. Najua Misri wamekuja na nia ya kutaka sare tu lakini wasione kama mechi hii itakuwa rahisi sana zaidi tunajua mbinu zao wanazotumia kipindi cha kwanza na hata cha pili.

Mkwasa ameweka wazi kwa watanzania wote kuja kwa wingi kwani kikosi chake kipo kamili kuwavaa mafarao hao na anataka kuvunja historia iliyokuwa inawasumbua kwa kipindi kirefu cha kufunga na mataifa ya kiarabu. Stars inawakilishwa na nyota kutoka Genk Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu kutoka TP mazembe ambao wameshajiunga na wenzao n tayari wameshakuwa fiti kuwakabili waarabu hao.

wataalam wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini wakutana

$
0
0
Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor akizungumza na wadau na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao (hawapo pichani) mbele ya vyombo vya habari.
Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bibi Kitolina L. Kippa. akimkaribisha Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor kuzungumza na wadau na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini (hawapo pichani).
Wadau na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor (hayupo pichani).
Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor (wa nne kutoka kushoto) waliopo mbele akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wataalam wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA " THE ECONOMIST" GAZETI LA KIINGEREZA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa " The Ecomist" Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Liganda. 
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Liganda (kulia), akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.

Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa "Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively"

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.

"Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma" alisema Zamarad.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.

Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Picha yenye Nembo inayotumika Nchini Papua New Guinea kutoka kwa Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana. (Picha na OMR).

TIMU ITAKAYOWEKA DAU NONO MEZANI NITAJIUNGA NAYO - MGOSI

$
0
0
MSHAMBULIAJI mkongwe wa timu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kuna baadhi ya timu zinahitaji huduma yake ingawa hajataka kuziweka wazi kwani wapo kwenye maongezi na kikubwa zaidi anaangalia maslahi baina yake na timu hizo zinazomuhitaji.

"Nimemaliza mkataba wangu na Simba kwahiyo ni mchezaji huru naweza kujiunga na timu nyingine yoyote ila kwa sasa nipo kwenye maongezi na baadhi ya timu zinazohitaji huduma yangu,"amesema Mgosi. 

Kwa sasa yupo mapumziko baada ya kuwa na majukumu ya kimpira kwa muda mrefu lakini yupo kwenye maongezi na timu itakayoweka dau kubwa atajiunga nao ila ni mapema sana kuzitaja timu hizo.

Mgosi alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa lakini aliweza kukabidhiwa Kitambaa cha kuiongoza timu hiyo kama Nahodha huku katika baadhi ya mechi ambapo kocha Mkuu Jackson Mayanja akitumikia kadi nyekundu na Mgosi  kuchukua majukumu hayo ya kuongoza kikosi cha Simba. 

Hata hivyo Mgosi amekuwa na historia nzuri na wanamsimbazi hao kwani amechezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa sana kabla ya kutimkia katika timu zingine lakini umuhimu wake ulionekana na uongozi kuamua kumrudisha.

JUDICIARY EXCELLS IN WORLD DOING BUSINESS RANKING

$
0
0
By Nurdin Ndimbe

The World Bank has just released a World doing Business report where Judiciary has attained high ranking on enhancing business environment in doing business for 2016.Tanzania is among the 189 World economies that are evaluated by the World Bank on the easiness and conduciveness of their business regulatory system necessary for investment attraction.

Presenting a paper on Doing Business Report 2016 in Dar Es Salaam recently, the Court Administrator of High Court -Commercial Division, Mr Willy Machumu said that, the trend for doing business and service within the Judiciary has significantly improved better than before. According to reports released by the World recently, Tanzania has improved in service delivery in recent years.
The World doing Business report is a series of cumulative report which presents quantitative indicators on business regulations which can be compared within 189 economies of the World. The World Doing Business Report broad objectives are to inform various policy makers to improve quality of rules and regulation which aims on improving private Sector economic understanding.

“It depicts how easy or difficulty for local entrepreneur to open and run small to medium sized business when complying with relevant regulations, in short it is matter of measuring regulatory quality and efficiency in a given country how conducive is the country for business grounds and investment attractions” he said.

JK AOMBELEZA MSIBA WA RAIS WA SAHARA MAGAHARIBI

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete.
Mke wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikete.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa nchi ya Sahara Magharibi Brahim Salem Buseif mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images