Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1244 | 1245 | (Page 1246) | 1247 | 1248 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi wakiwa katika picha ya Pamoja na jamii ya watu wenye ulemavu leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
   

  0 0

  KIKOSI CHA KWANZA

  1. Deogratius Munish 'Dida'
  2.Juma Abdul 
  3. Mwinyi Haji
  4. Aggrey Morris
  5. Erasto Nyoni
  6. Himid Mao
  7. Thomas Ulimwengu
  8. Mwinyi Kazimoto
  9. Elius Maguli
  10.Mbwana Samatta
  11.Farid Mussa

  Akiba

  1. Aishi Manula
  2. Mohamed Hussein 
  3. David Mwantika
  4. Shiza Kichuya
  5. Jonas Mkude
  6. Deus Kaseke
  7. John Bocco

  Benchi la ufundi

  Kocha. Charles Boniface Mkwasa
  Kocha msaidiz. Hemed Morroco

  0 0

  Bingwa wa zamani wa mchezo wa Masumbwi Dunia kwa uzito wa juu (World Heavyweight Champion) aliyeaminika kuwa mmoja kati ya Mabondia bora zaidi kuwahi kutokea, Muhammad Ali maarufu kama "The Greatest" amefariki Dunia leo katika hospitali ya Phoenix-area iliyopo Phoenix, Arizona alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 
  Ali ambaye alikuwa ni Bingwa mara tatu wa  ngumi za Uzani wa Juu Duniani, amefariki akiwa na umri wa Miaka 74.

  Muhammad Ali aliyestaafu ndondi za kulipwa mwaka 1981 aligundulika kuwa na ugojwa wa Parkinson (Parkinsons Disease) Mwaka 1984 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo hadi alipopatwa na mauti.

   Mbali na ugonjwa huo pia Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja na maambukizi katika njia ya mkojo.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina

  **********  *********
  HISTORIA FUPI YA MUHAMMAD ALI.

  Muhammad Ali alikuwa bondia kwa sababu kuna mtu aliyemuibia baskeli yake. Alikuwa na umri wa miaka 12 wakati ule na alikuwa akiishi Louisville katika jimbo la Kentucky akijuilikana kwa jina la Cassius Mercellus Clay Jr.

  Joe Martin, aliyekuja kuwa kocha wake baadaye, anaelezea jinsi kijana huyo alivyokuwa akilia huku akiahidi kumtandika magumi aliyemuibia baskeli yake pindi akimpata. Kocha huyo wa ubondia alimchukua Clay, kijana mweusi anayetokea katika familia ya watu maskini, na kumjumuisha na watoto wengine aliokuwa akiwafundisha.

  “Alikuwa na bidii zaidi kuliko waatoto wote wengine niliokuwa nikiwasimamia,” anasema Joe Martin.
  Ingawa Clay wakati ule hakuwa na nguvu ya kuvurumisha masumbwi, alikuwa mwepesi wa kuranda randa kupita kiasi. Mnamo mwaka 1960, akiwa na umri wa miaka 18, alishinda katika pambano la ndondi la michezo ya Olympiki mjini Rome, Italia. Medali yake ya dhahabu inasemekana aliitupa ndani ya Mto Ohio kwa sababu alikasirishwa na jinsi watu weusi wanavyobaguliwa nchini mwake.

  Cassius Clay alikamilisha michuano ya wasiolipwa baada ya kuibuka na ushindi mara 100 katika jumla ya mapambano 108 aliyopigana. Wafanyabiashara 11 wa Kizungu kutoka Louisville walishirikiana ili kumfungulia njia Cassius Clay ya kuingia katika ulingo ya mabondia wa kulipwa.

  Bondia huyo mwenye kipaji alikuwa akitajikana pia kuwa ni mtu aliyekuwa na majivuno na mdomo mpana. Kabla ya mapambano yake, Cassius Clay daima alikuwa akijinata kuwa yeye “ndie mbabe wa wababe na mzuri kuliko mabondia wote na kuwakejeli wapinzani wake.

  Katika pambano lake la kwanza la kuwania ubingwa wa dunia Februari 1964 dhidi ya mtetezi wa taji hilo, Sonny Liston, Clay hakuwa akijulikana ni nani na watu waliamini angeshindwa tu. Lakini baada ya raundi ya sita, Liston aliungama. “Mie ndie mbabe,” alinguruma Cassius Clay kupitia kikuza sauti.

  *Mwaka huo huo, alisilimu na kujiunga na kundi la Nation of Islam lililokuwa likiongozwa wakati huo mwanaharakati wa haki wa Wamarekani Weusi, Malcolm X. Akabadilisha jina la Cassius Clay na kujiita wakati huo huo Muhammad Ali*
  Muhammad Ali hakuwa bondia tu, alikuwa mwanaharakati pia. Alipinga vita vya Marekani nchini Vietnam na alikataa kutekeleza sheria ya kutumikia jeshi. Mnamo mwaka 1967, akapokonywa sio tu leseni yake ya ubondia, bali pia alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, ingawa baadaye bondia huyo wa aina pekee aliachiwa kwa dhamana.

  Wasanii na wasomi mfano wa Richard Burton na Henry Fonda au mwandishi vitabu Truman Capote wakampigania mpaka Muhammad Ali akaruhusiwa tena kurejea ulingoni baada ya kulazimika kukaa nje kwa miaka mitatu.

  Machi 8, 1971 Muhammad Ali aliteremka ulingoni Madison Square Garden mjini New York kwa kile kilichotaajwa “kuwa pambano la ndondi la karne” dhidi ya bingwa wa wakati ule, Joe Frazier. Lilikuwa pambano kati ya mafahali wawili, kati ya mpinzani na yule aliyekuwa akiangaliwa kama mwakilishi wa mtindo wa maisha wa Kimarekani. Katika pambano hilo la kusisimua la zaidi ya raundi 15, Frazier akashinda kwa pointi. Ali akalazimika kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ubondia kunusa jamvi.

  Yakafuata mapambano mengine ya kusisimua mfano wa lile la mjini Kinshasa dhidi ya George Foreman mnamo mwaka 1974, ambapo Muhammad Ali anasema “aliranda mfano wa kipepeo na kuuma kama nyuki”

  Muhammad Ali alilipiza kisasi dhidi ya Joe Frazier mwaka 1975 na kumlazimisha kusalimu amri mnamo rauni ya 14. Mohammed Ali alistaafu mwishoni mwa mwaka 1981 baada ya kuranda kwa karibu miaka 40.

  Wakati huo tayari alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Parkinson. Licha ya maradhi hayo, Muhammad Ali ndiye aliyewasha mwenge wa Olimpiki huko Atlanta mnamo mwaka 1996 na kuusisimua ulimwengu mzima. Mwaka 1999 aliteuliwa na kamati kuu ya michezo ya Olimpiki kuwa “mwanaspoti bora wa karne.”

  Mpinzani wake wa zamani George Foreman amegeuka hivi sasa kuwa rafiki yake mkubwa na kuungama “Muhammad Ali ndie bingwa wa mabingwa.”


  Mpaka leo june 4 2016. Muhhamad Ali anapoteza maisha ndie mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. aliepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu.

  0 0

   Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,  Dk. Juliana Pallangyo pamoja na ujumbe wake.
   Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja,na  Kaimu Kamishna wa Petroli ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya   Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mwanamani Kidaya wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (hayupo pichani) kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.
   Meneja Uendeshaji  kutoka   Kampuni ya  Puma  Energy Lameck Hiliyai (katikati)  akielekeza  jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile (aliyekaa katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) katika kikao hicho kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Mratibu wa Jr NBA Bahati Mgunda akizungumzia kuhusu mafunzo wanayoyapata vijana takribani 100 katik mchezo wa mpira wa Kikapu chini ya mchezaji wa kimataifa anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet na kusema kuwa itakuwa moja ya mchango mkubwa sana kwa vijana hao.

  Mgunda amesema vijana wanapewa mvbinh mbalimbali za kuujua vyema mchezo huo na watakuja kuwa msingi mkubwa sana wa maendeleo ya baadae.

  "Vijana wanapatiwa mafunzo na Hasheem na kama wakiendelea kupata fursa hiyo basi watakuj kuwa wachezaji wazuri sana,"amesema Mgunda. Vijana  hao wamepatikana baada ya kuwa na ligi iliyokuwa inaendelea katika viwanja vya JMK Park ambayo kwa mujibu wa kituo hicho itakuwa ni endelevu na itaibua vipaji vingi.
   Hasheem Thabeet akiwaelekeza jambo watoto hao
  vijana takribani 100 wakipatiwa mafunzo katik mchezo wa mpira wa Kikapu chini ya mchezaji wa kimataifa anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani Hasheem Thabeet iliyokuwa inaendelea katika viwanja vya JMK Park ambayo kwa mujibu wa kituo hicho itakuwa ni endelevu na itaibua vipaji vingi.PICHA HABARI NA ZAINAB NYAMKA,GLOBU YA JAMII.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga mara baada ya tukio la uapisho kukamilika.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tatizo la uhujumu wa miundombinu ya Mwendokasi.
  Katika taarifa yake Mh. Hapi ameeleza kuwa katika kipindi cha siku mbili watu 49 wamekamatwa na polisi wilayani Kinondoni wakiwemo wamiliki wa magari, bajaji na bodaboda kwa makosa ya kuingilia miundombinu ya Mwendokasi kinyume cha sheria. 

  Kati yao watuhumiwa 43 watapelekwa mahakamani siku ya jumatatu ijayo hali inaowafanya kuyatumia mapumziko ya Juma wakiwa mahabusu.

  Mh. Hapi amewataka wananchi wa Kinondoni na hasa madereva kufuata sheria, vinginevyo watakabiliana na rungu la dola.

  Aidha, Mh. Mkuu wa Wilaya ameagiza Polisi wilayani Kinondoni kuendelea na zoezi la kuwakamata wale wote wanaogeuza vivuko vya barabara za DART kuwa sehemu za kulala na kujisaidia.

  "Tumewaagiza Polisi kuwakamata wote wanaolala na kujisaidia kwenye vivuko vya barabara. Hata wale ambao wamesimama kule juu saa za usiku bila kazi yoyote wakamatwe na washitakiwe kwa sheria za uzembe na uzururaji. Wengine hawa ni vibaka na wengine ndio wanaolala na kujisaidia huko usiku." Alisema Hapi.

  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli akizungumza na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam alizungumzia juu ya uhujumu wa miundombinu ya mwendokasi na kuagiza watu hao kushughulikiwa ipasavyo.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya aliutaka uongozi wa DART kuchukua tahadhari za kiusalama katika vituo vya mabasi ili kuzuia uwezekano wa kutokea tishio la usalama. Hapi aliwataka DART kuweka utaratibu wa kuwakagua abiria kwa mashine za mikono za ukaguzi ili kuhakikisha usalama wa wananchi wanaopanda mabasi hayo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa Wananchi  wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira. Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.

  Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia Wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.

  Wakisoma Risala yao , Wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi  kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.

  Mwisho Waziri aliwahukuru Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5 juni kila mwaka.
      Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni kesho
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya  Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya mazingira hapo tarehe 5 juni.
   . Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ambao walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya Mbweni.


  0 0

   Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni  Boniface Jacob  akizungumza na  Mafisa Watendaji  juu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  na kuwafukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.
  (Picha na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  HALMASHAURI ya Manispaa ya kinondoni imefukuza kazi mafisa watendaji kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.

  Akizungumza leo na maafisa watendaji kata, meya wa kinondoni boniface jacob amesema kuwa hawatavumilia  watendaji wanaofuja fedha za umma.

  Watendaji waliofukuzwa ni Ernest Misa na Ally Bwanamkuu na wengine wawili wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi ambao ni Shaban Kambi pamoja na Bernard Supu. 

  Aidha Meya huyo amesema zipo kata tano ambazo zimekusanya mapato vizuri na kata tano zingine zimefanya vibaya hivyo wanatafuta dawa ya kuwaondoa watendaji waliofanya vibaya.

  Jacob amesema migogoro ya ardhi imepungua kutokana na kila watendaji kuwajibika katika zao awali migogoro ilikuwa inasababishwa na wenyewe

  Amesema kinondoni wanataka kuibadili katika kuhakikisha watendaji wanawahudumia wananchi kuachana kufanya kwa mazoea.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China, ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini lu youqing aliyeambatana na Kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  pamoja na Balozi wa China hapa nchini lu youqing mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Salum Hapi   akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika barabara  ya mabasi yaendayo haraka.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza 

  Mkuu wa wilaya ya kinondoni,Salum Hapi amewataka wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika barabara  ya mabasi yaendayo haraka.

  Hapi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi juu ya utekelezaji wa agizo la Rais, amesema kuwa  watu 49 wamekamatwa ambao wamekuwa wakitumia vyombo vya moto katika barabara  ya mwendokasi

  Hapi amesema kuwa barabara hiyo watu waheshimu sheria za nchi na watu watakaokiuka watachukuliwa hatua.

  Aidha amewataka DART kuongeza ukaguzi  wa abiria katika vituo vyake kwani sio watu wote wanasafiri wengine ni wahalifu,

  Hapi amesema watu wote ambao wamekamatwa wafikishwa mahakamani kujibu mashitaka  yao.

  0 0

   Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  KIKOSI cha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa amekubali matokeo baad ya kufungwa goli 2 - 0 na Misri huku akisifia kikosi chao kuwa ni kizuri na wana wachezaji wazuri na wamecheza kwa nidhamu kubwa sana.

  Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa amesema wachezaji wake wamecheza vizuri ila wameshindwa kutumia nafasi walizozipata katika kipindi cha kwanza na makosa madogomadogo kutoka kwa wachezaji na hasa ukiangalia goli la pili lilikuwa ni kosa la mabeki katika kufanya marking ya mwisho. Hata hivyo nawapongeza sana Misri kwani wamepata alama tatu na kuweza kufuzu Mataifa Afrika 2017 nchini Gabon.

  "Wachezaji wamejituma sana na siwezi kuwalaumu kwani wamecheza na timu yenye uwezo mkubwa sana na wana wachezaji wa kimataifa wengi wanaocheza soka la kulipwa nje,"amesema Mkwasa.Baada ya matokeo hayo Stars wamesalia na pointi moja na Misri kujiongezea alama tatu na kufikisha saba ambazo zimempa nafasi ya kufuzu AFCON.
  Benchi la ufundi la Taifa stars, Charles Boniface Mkwasa kushoto, Hemed Moroco kocha msaidizi Peter Manyika kocha wa makipa na Mkurugenzi wa Benchi la ufundi Abdala Kibadeniwa (kwanza kulia).


  Mchezo ukiendelea jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


  Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa Misri jijini Dar es Salaam wakati wa kicheza kati ya timu  ya Taifa Taifa Stars na Misri.  Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.

  NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amemuomba Nadir Haroub 'Canavaro'arejee kwenye kikosi cha Stars kwani bado ana uwezo wa kucheza na uwepo wake kwenye kikosi hicho ni muhimu ukizingatia uzoefu wa muda mrefu katika michuano mbalimbali ya kimataifa.
  Samata amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhid ya Misri uliomalizika kwa Taifa Stars kufungwa goli 2-0 na kufuta matumaini ya kufuzu michuano ya mataifa Afrika AFCON 2017 nchini Gabon. 

  Amesema uwezo wa kumshawishi mchezaji kurejea kwenye kikosi hicho ila Canavaro ni mtu mzima na ana maamuzi yake ya nini anachotaka kufanya ambacho kina faida kwake.

  "Ninao uwezo wa kumshawishi mchezaji yoyote yule kurejea kwenye kikosi ila kila mmoja ana maamuzi yake na ukiangalia Canavaro ni mtu mzima na anajua nini anachofanya zaidi nachoweza kusema tunaomba aje kwenye timu kwanza ana uzoefu wa siku nyingi hasa michuano ya kimataifa,"amesema Samatta.

  Canavaro aliamua kuachana na timu hiyo miezi sita iliyopita na ameweka wazi msimamo wake wa kutokucheza timu hiyo hata baada ya kuitwa tena na kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa.

  0 0

  Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmed Abdulrahman Rashid akitoa maelezo juu ya Mpango Mkuu wa matumizi ya Ardhi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Mradi wa Mji mpya wa Zanzibar uliofanyika Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Mjini Zanzibar.
  Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
  Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akitoa maelezo namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyojiandaa katika kuwapatia wananchi nyumba bora za kuishi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ngambo Tuitakayo.
  Mkurugenzi wa mipango Miji na Vijiji Dkt. Mouhammed Juma akimunyesha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud namna ya Mji mpya utakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
  Watoto wakiangalia na kufurahia mji mpya wa Zanzibar utakavyokuwa kupitia Mradi wa Ngambo tuitakayo wakati wa uzinduzi wa maonyesho katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

  0 0  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (kulia), akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star 2016, Melisa John, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika fainali za mashindano ya Afrika zitakazofanyika Lagos nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu. Wanaoshuhudi ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Ngereza.  · Mshindi anaenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika nchini Nigeria

  Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imekabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars ambaye ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika inayotegemea kufanyika Lagos Nigeria

  Melisa John mwenye umri wa miaka 22 anayetokea mkoa wa Dar es Saalam aliibuka mshindi katika fainali zilizoshirikisha washiriki tano bora walioingia kwenye kinyanganyiro hicho. Melisa ataondoka nchini tarehe 4 Juni 2016 kwaajili ya mandalizi ya awali na mazoezi ya muziki yatakayoshirikisha washiriki wengine 8 kutoka nchi za Afrika ambazo Airtel inayoendesha biashara zake kisha kushiriki kwenye fainali zitakazofanyika 11 Juni 2016

  Akiongea wakati wa kukabidhi bendera, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi alisema Sanaa ni Kazi ,ajira na ni bidhaa yenye thamani kubwa. Muziki kama tanzu mojawapo ya Sanaa ina nafasi kubwa katika kubadili maisha ya mtu na nchi kiuchumi endapo itatumika vizuri. ile dhana kuwa kazi ya Muziki ni kuburudisha imepitwa na wakati.Wanamuziki sasa tuingie kazini.

  Ninawapongeza Airtel wamelielewa hili na kuamua kuunga mkono Serikali kwakuwa na mpango kabambe wa kuibua vipaji vya Vijana kupitia Sanaa ya Muziki uitwao Airtel Trace Music Stars wenye lengo la kuwawezesha Vijana,wanamuziki chipukizi kushiriki na kufikia ndoto zao, ikiwa pia ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni inayosisitiza Mashirika na Taasisi kushiriki kikamilifu katika kukuza na kuendeleza Sanaa na Wasanii.

  “napenda kumpongeza Melisa kwa ushindi huo na kumuhasa kuonyesha nidhamu na kuwa na mwelekeo wa kufikia lengo lake wake wote wa mashindano kwani mashindano haya yanatoa fursa pana zaidi ya ushindi hivyo hii ni nafasi ya pekee sana kwako kuitumia fursa hii ipasavyo na kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri ya kudumu, kuongeza wigo mpana wa marafiki na mashabiki na pia kuonyesha uwezo/ talanta yako katika mziki” aliongeza Kihimbi

  Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “tunajivunia kuanzisha mpango huu kabambe ambao si tu unawawesha vijana kubadili maisha yao bali unawapa nafasi ya kufanya muziki na kuonyesha vipaji vyao nje ya mipaka ya nchi. Tunafurahi kuwawezesha vijana wanamuziki chipukizi kupata nafasi hadimu za kufanya kazi na magwiji wa muziki duniani kama Akon na Keri Hilston hivyo tunaomba watanzania watumie fursa hizi kupitia programu zetu za kijamii chini ya mpango wetu wa Airtel Fursa kujikwamua kimaisha wao pamoja na jamii inayowazunguka.”

  Kwa upande wake Melisa John amewashukuru Airtel na Serikali kwa ushirikiano katika kukuza tasnia ya muziki na kuchochea ajira kwa vijana wengi, “nimejipanga vyema kukabiliana na changamoto iliyoko mbele yangu na ninawaahidi kuipeperusha vyema bendera ya nchi yangu. 

  Napenda kuwaomba mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla kunipigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno MEL kwenda namba 15594 kura yako ni muhimu na itachangia kunipa ushindi”

  0 0

   Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. Sendeka amesema, Wapinzania wanadai kwamba Rais Dk. John Magufuli uongozi wake ni wa Kidikteta, wameamua kujaribu hoja hiyo kwa kuwa wameishiwa hoja na hata hivyo hoja yao hiyo haiwezi kuwa na mashiko kwa Watanzania ambao wanaamini Rais Dk. Magufuli anavyofanya sasa kupasua majipu na kupambana na vitendo vya ufiadi, kufuja rasilimali za nchi, uzembe na umangimeza ni sahihi. 
   Wananchi wakimshangilia Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipoingia kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi leo jioni
   Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. Sendeka amesema, Wapinzania wanadai kwamba Rais Dk. John Magufuli uongozi wake ni wa Kidikteta, wameamua kujaribu hoja hiyo kwa kuwa wameishiwa hoja na hata hivyo hoja yao hiyo haiwezi kuwa na mashiko kwa Watanzania ambao wanaamini Rais Dk. Magufuli anavyofanya sasa kupasua majipu na kupambana na vitendo vya ufiadi, kufuja rasilimali za nchi, uzembe na umangimeza ni sahihi.  
  Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiwaaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO


  0 0


  Je, unateseka na msongo wa Mawazo? Je, unajua watu ambao wateseka? Unaweza kuokoa maisha leo!Video hii inatahadharisha kuhusu afya ya akili watu mbalimbali wanapatwa na matatizo haya ya akili yanayowapelekea kuchukua maamuzi mabaya yakiwemo hata kuchukua hatua ya kujiua.

  #Kwenye kampuni ya METL inaamini, kwamba wafanyakazi wake ni mali yao hivyo inawapatia elimu hii na inaendelea kuwasaidia kwani wasingeweza kufikia hapo bila watu wake hao.Kamwe hujachelewa kuomba msaada andika maoni yako na tuendeleze mjadala huu."it's never too late to get help,Write your views in the comments and let's take this discussion ahead."

  Nawe msomaji wetu unaweza kuandika maoni yako na tuendeleze mjadala huu, baada ya kuiona video hii hapa chini:
  Video:
  Afya ya akiliTanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watu wake wanakabiliwa na matatizo ya akili huku wengi wa wanaopatwa na matatizo haya ukimbizwa kwa waganga wa kienyeji kupatiwa tiba za asili wakiamini kuwa wamelogwa.

  0 0


  0 0

  Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.

  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kusimamia vyema utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza mipango iliyojiwekea kwa wakati ili kuimarisha ustawi wa wananchi wanaowawakilisha na taifa kwa ujumla.

  Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati akifungua semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).

  Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge wana jukumu la kuzingatia malengo hayo na kuhakikisha yanatekelezwa kwa kuwa mipango yote na mikakati ya maendeleo hupitia Bungeni hivyo hawana budi kusimamia malengo hayo ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

  Akizungumza wakati wa semina hiyo Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inafanya kazi nzuri katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia na kuwataka Wabunge kuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa malengo hayo.Bw. Rodriguez ameongeza kuwa ni muhimu sana kwa Wabunge kuweza kuyaelewa malengo hayo ya Dunia ili waweze kufanikisha utekelezaji na ufuatiliaji wake katika ngazi zote za Taifa.


  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro (kulia) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez Alvaro (kulia) akimwonesha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) sehemu ya taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
  Wabunge Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga, Mwenyekiti wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja kwenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini iliyofanyika Bungeni, Dodoma.
  Mtaalam wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo hayo mjini Dodoma.
  Mtaalam wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo hayo mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.


older | 1 | .... | 1244 | 1245 | (Page 1246) | 1247 | 1248 | .... | 3353 | newer