Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

DAWASCO YAKANUSHA KUSUSIKA NA GARI ILIYOPARAMIA KITUO CHA DALADALA

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro amesema kuwa gari hilo sio mali ya Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam, bali ni moja ya gari linalomilikiwa na watu binafsi ambao wanasaidiana na Dawasco katika kusambaza huduma ya maji maeneo ambayo huduma hiyo bado haijafika kwa kutumia magari makubwa ya kusambaza Maji (maboza) ambayo yamesajiliwa na kuwekwa nembo ya Dawasco.

“Gari hili sio mali ya Dawasco, bali limesajiliwa na Dawasco na kuwekewa viambatanisho vyote muhimu ili kusambaza huduma ya Maji maeneo ambayo mtandao wa Maji haujafika haujafika” alisema Lyaro.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Dawasco ilianza zoezi maalum la kusajili visima pamoja na magari yote makubwa ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es salaam, ambapo tayari magari makubwa takribani 256 ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es Salaam yamekwisha sajiliwa.

Dawasco inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia taratibu za kazi kwa kuandika taarifa zenye uhakika na ukweli ili kuepuka upotoshaji wa habari kwa wananchi.

Everlasting Lyaro 
Kaimu Meneja uhusiano- Dawasco
022-2194800 au 08001164
Dawasco Makao Makuu

30/05/2016

uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara

$
0
0

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo mwaka 2020.

Katika kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.

Akizindua mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.

“kwa mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka 2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”. Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50 vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.

“Marekani inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema Bi Bodipo.

Mwakilishi wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen

Mpango wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.
Mkuu wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NCHINI AKUTANA NA WAFUGAJI WA KIBAHA VIJIJINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kitongoji cha Mlandizi Kati Bw. Ally Nyambwilo akizungumza wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika mikoa ya Pwani na Morogoro.
Mzee wa Jamii ya ufugaji Bw. Lukunati Moreto wa kijiji cha Magindu katika Halmashauri yaWilaya ya Kibaha Vijijini akichangia maoni wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza na Wazee wa Kitongoji cha Mlandizi Kati wakati wa Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Huduma za Jamii kwa Wazee unaondeshwana Tume.

UCHAGUZI MKUU YANGA WASUASUA,HATMA YAKE KUJULIKANA KESHO.

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii.
KATIKA kuelekea uchaguzi Mkuu wa Yanga na dirisha la kuchukua fomu kufunguliwa siku ya Ijumaa na linatarajiwa kufungwa kesho Juni 01 inasadikiwa hakuna mtu yoyote ameyejitokeza tayari kuchukua fomu huku Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF,Aloyce Komba akiwa nje ya mji na anatarajiwa kurejea kesho.

Baadhi ya wanachama wa Yanga wameonesha kutokuelewa uchaguzi kama utafanyika kwani hakuonekani dalili za kuelekea uchaguzi hu Juni 25 na zaidi wanashangaa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF ) ndilo linalohusika na utoaji huo wa fomu na kama serikali wameamua iwe hivyo sawa.

Akitolea ufafanuzi wa uchaguzi, Katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdesit amesema wao wameamrishwa kufanya uchaguzi na serikali na tarehe imeshapangwa watafanya kama walivyoelekezwa zaidi masuala mengine yote anatakiwa kujibu mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi TFF,Aloyce Komba ila wao kwa sasa wapo kwenye majadiliano juu ya kadi za kutumika kwenye uchaguzi huo kati ya za zamani na mpya.

"Suala la uchaguzi hatuwezi kuliongelea sisi tupo kwenye majadiliano ya kadi za kutumika kwenye uchaguzi huo wa Juni 25 na zaidi sisi viongozi wa Yanga ndiyo tunaowajua wanachama wetu na wanavyotaka kusema kuwa tutumie kadi za zamani basi hakuna hata mwanachama mmoja atakayepiga kura kwani toka 2014 hakuna hata mmoja aliyelipia kadi za zamani,"amesema Deusdedit.

Tutatoa tamko baada ya kuhusiana na kadi gani zitatumika siku ya uchaguzi ila wanachama wavute subira kwani sisi tunawatambua kama ni wanachama wetu na watapiga kura.

Rais Dkt. Magufuli afanya uteuzi mwingine leo

$
0
0

 Jaji Shaban Ali Lila
 Mh. Anne Semamba Makinda
Prof. Apollinaria Elikana Pereka

MKURUGENZI WA SMART CODES TANZANIA ATAJWA KWENYE ORODHA YA FORBES AFRICA.

$
0
0
Bwana Edwin Bruno, mjasiriamali wa Kitanzania, mshindi wa tuzo ya kijana mwenye mafanikio 2015, mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Smart Codes (www.smartcodes.co.tz) ametajwa katika jarida la Forbes Africa. Kila mwaka, jarida hilo hutoa orodha ya vijana 30 wenye umri chini ya miaka 30 ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea wa baadaye.

Majina hayo yalikusanywa na kuandaliwa na mhariri wa Forbes Afrika, Ancillar Mangena ambaye naye ana chini ya miaka 30. Katika ujumbe wake, anaandika “Orodha inawakilisha vijana ambao tunaamini wana uwezo wa siku moja kuwa kwenye ukurasa wa mbele wa jarida la FORBES AFRICA, ikimaanisha watakuwa na thamani halisi ya si chini ya dola za kimarekani milioni 200, wameajiri maelfu ya watu na kusaidia kukua bara la Afrika.”

Katika mazungumzo mafupi na Edwin Bruno, anasema “Nimepewa heshima kubwa kuwa kwenye orodha hiyo, hata hivyo hii inatokana na juhudi za timu nzima pale Smart Codes. Ni wao ndio wanaofanya kazi kubwa, ambayo inaonekana ndani nan je ya nchi”

Kuhusu mafanikio yake mengine, Bruno anasema “ Ni kweli, mwaka jana programu yetu ya m-paper, ambayo inakupa nafasi ya kusoma magazeti ya Tanzania…sio vichwa vya habari, ila gazeti lote kutokea ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwenye simu yako au kompyuta ilishinda tuzo ya Best Educatinal Innovation Africa, au kwa Kiswahili tuzo ya uvumbuzi bora wa kielimu barani Afrika.”

Bwana Bruno alimalizia kwa kuonesha furaha yake na kuwasihi vijana wengine kufanya kazi kwa kujituma ili waweze kufikia malengo yao au kama yale aliesema mhariri wa Forbes Africa Ancillar, kusaidia kukua kwa bara la Afrika kiuchumi.

ABDULRAHMAN MUSSA MCHEZAJI BORA MWEZI MEI.

$
0
0
SHAMBULIAJI Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei 2016.

 Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.

 Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.

 Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

MISS TANAZANIA USA PAGEANT AEESHA KAMARA AONGEA NA WANAFUNZI WA KENTON HIGH SCHOOL.

$
0
0
Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya.
Miss Tanzania USA Aeesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI ARUSHA.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix  (katikati)  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha leo ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa  Kimataifa wa 'Africa  World Heritage' kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

In Loving Memory

$
0
0
As we mark your second year the memories lingers on,
We know you are in a better place and we pray for you every day
You taught us perseverance, discipline and a giving heart
Today we celebrate your life and know that you are watching over us from heaven.

We miss your wisdom and your kind deeds, time flies but in our hearts you live forever.

You are fondly remembered by your wife Mary, children Billy, Albert, Sia and Beatrice, grandchildren Lynn and Lyssette, relatives and friends

WATOTO MILIONI 2.7 WAMEDUMAA KUTOKANA NA KUKOSA LISHE BORA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo akizungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Lishe nchini.
 Mchungaji wa makanisa ya Kipentekoste, Sixtus Mallya akichangia mada hasa kwenye imani za dini kukataza baadhi ya vyakula na kusema kuwa vyakula hivyo vimekatazwa na Biblia amesema kuwa lishe ni kitu cha mhimu kwa ukuaji wa mwili.
 Baadhi ya Vyakula Lishe ambavyo vinatakiwa kwa kila mlo ambavyo vinatakiwa kila mtu anapokula.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATOTO milioni 2.7  sawa na asilimia 35   wana udumavu kutokana na kukosa lishe hali inayofanya  serikali kupoteza pato la taifa  katika kuhudumia watoto hao.

Utadumavu huo umepungua kutoka asilimia 42  mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 35  mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dini katika suala lishe, Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo amesema viongozi wa dini wana umuhimu kuwa mabalozi wa kuhamasisha lishe katika ngazi ya familia katika nyumba za ibada.

Amesema kuwa  kiwango cha watoto waliodumaa hawawezi kurekebishika kutokana na kuadhiri maumbile ya mtoto pamoja na kinga yake kuwa  duni kwa ugonjwa wa utapiamlo.

Mikindo amesema kuwa suala la lishe haliangaliwi huku likiwa linaadhiri maendeleo ya familia kutokana na malezi ya mtoto aliyedumaa ni tofauti na mtoto asiyedumaa.

Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pazi Mwinyumvua amesema kuwa wanawake wanashindwa kunyonyesha watoto kwa sababu kulinda maumbile kwani mwanamke akinyonyesha kuwa maziwa yanaanguka.

Mwinyimvua amesema wanashindwa kula chakula na mbogamboga kwa madai kula mboga mboga ni suala la watu wenye kipato cha chini.

WADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO WANAOANDAA MKAKATI WA KITAIFA WA USALAMA KWENYE MTANDAO.

$
0
0
 Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Clarence Ichwekeleza akifungua Semina ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini.
Mtaalamu Mwelekezi wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Martin Koyabe akitoa mada kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao. 
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA KUJENGA NCHI (JKT)

MAKAMU WA RAIS, SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akichangia baadhi ya mada zilizowasilishwa kwenye mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016.  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili  unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, katika kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutao huo umefunguliwa leo Mei 31,2016 katika kituo cha mikutano cha ACC mjini Papua New Guinea.                       
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius B. Likwelile.na katibu wake Waziri Rajab. 
(Picha na OMR).

TANROADS yakanusha kudaiwa fidia

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO


Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wamekanusha kudaiwa fidia na wananchi wa Kijiji cha Mazingira,Wilaya ya Handeni mkoani Tanga waliovunjiwa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa TANROADS Mhandisi Alfred Ndumbaro alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya malalamiko ya wananchi wa Kijiji hicho kuhusu kutolipwa fidia zao.

”Sheria iko wazi kuwa wanaojenga karibu na barabara wakivunjiwa hawalipwi fidia yoyote lakini wale ambao ujenzi wa barabara uliwafuata katika maeneo yao wana haki ya kulipwa fidia”, alisema Mhandisi Ndumbaro.

Mhandisi Ndumbaro ameongeza kuwa zoezi la malipo ya fidia kwa wanakijiji waliokuwa na uhalali wa malipo hayo lilishakwisha zamani kwa hiyo, wanaodai sasa ni wale ambao nyumba zao zilivunjwa kutokana na kujenga eneo la barabara.

Aidha, Mhandisi huyo ametoa rai kwa wananchi kufuata sheria za ardhi ili kupata uhalali wa viwanja vyao pamoja na kuepuka usumbufu na gharama za kuvunjiwa nyumba zao.

Nyumba hizo zilivunjwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami yenye Kilomita 54 kutoka Mkata hadi Handeni iliyojengwa na Kampuni ya Synohydro Corporation Limited ya China.

TWIGA STARS KUKIPIGA NA RWANDA MECHI YA KIRAFIKI JUNI 17.

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
TIMU ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars inatarajia kucheza mechi ya kitaifa ya kirafiki dhidi ya timu ya wanawake ya Rwanda mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 17 katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam  leo  Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa Twiga imeshathibitisha kukubali mwaliko huo na katika barua waliyoituma, wameomba mechi hiyo ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za fainali za Mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake.

"Wenzetu wameomba mchezo huu kwa ajili ya kuandaa kikosi chao baada ya kufuzu kuelekea katika mashindano fainali za mataifa ya Afrika", amesema Lucas .
Rwanda wameona kuwa kiwango kizuri kilichooneshwa na stars katika mechi zake mbalimbali ikiwemo ile ya kuwania kufuzu kucheza fainali hizo ni kizuri kwa timu yao,"Timu hiyo iliona kiwango kilichooneshwa na Twiga ni kipimo kizuri kwa timu yao kuelekea katika fainali hizo kwa upande wa wanawake", amesema Lucas. K utokana na mechi hiyo Twiga itaingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya kuwavaa Rwanda".

UCHAGUZI YANGA UKO PALE PALE, SIKU YA KUCHUKUA FOMU ZASOGEZWA MBELE.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewatuhumu baadhi ya watendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kutaka kukwamisha uchaguzi wa Klabu ya Yanga kwani kwa kipindi kirefu klabu hiyo ilikuwa ikitumia uongozi wa zamani baada ya kutofanya uchaguzi wake mkuu kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na hali hiyo uongozi mpya wa BMT ulitoa agizo kwa vyama vyote vya michezo ikiwemo klabu za mpira za miguu ikiwemo Yanga kufanya uchaguzi kwa ajili ya kupata viongozi wapya lakini baraza liliitaka Yanga kufanya uchaguzi kabla ya Juni 30 baada ya kuomba kusogezewa mbele tarehe iliyopangwa awali kutokana na kushiriki mechi za kimataifa.

Akizungumzia tuhuma hizo Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa anasikitishwa na baadhi ya watu ikiwemo watendaji wa TFF kutaka kukwamisha zoezi la uchukuaji fomu wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo lakini kutokana na hali hiyo wangependa wanayanga kujua kuwa uchaguzi upo palepale kama walivyoeleza awali.

"Licha ya baadhi ya watu kutaka kukwamisha mchakato huu lakini tunapenda tu kuwajuza kuwa uchaguzi unatakiwa kufanyika kabla ya Juni 30", amesema Kiganja.

Kwa upande wake Afisa habari wa TFF, Alfred lucas alisema kuwa hadi sasa watu waliojitokeza kuchuakua fomu hizo ni watatu huku mbili zimetolewa kwa watu wanaogombea nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji huku Aron Nyanda akijitokeza kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo.

"Hadi sasa wamejitokeza kuchukua fomu ni watu watatu  wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga huku zoezi likiwa linaelekea ukingoni", amesema Alfred.

Aidha BMT imetangaza zoezi hilo kumalizika Jumapili badala ya leo kama ilivyotangazwa na TFF.

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli afanya uteuzi wa Jaji wa Rufani, Mwenyekiti DIT na Mwenyekiti NHIF

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA KWA MWAKA 2015.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi mbalimbali waliopata tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa viwanda kwa mwaka 2015. 
PICHA NA IKULU.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 'AFRICA WORLD HERITAGE' JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa 'Africa World Heritage' kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumaane Maghembe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati alipomkaribisha kufungua Mkutano wa "Afrca World Heritage' kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa wa' Africa World Heritage ' wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Mei 31, 2016.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images