Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1237 | 1238 | (Page 1239) | 1240 | 1241 | .... | 3284 | newer

  0 0  0 0


  0 0
 • 05/29/16--03:24: YALE YALEEE...!

 • 0 0

   Hatimaye mpiganaji   Goodchance Monyo na Atilia Magelanga wamefunga harusi katika kanisa la Mtakatifu Peter,Oysterbay jijini Dar hapo jana Mei 28 na baadaye tafrija murua kabisa ikafanyika katika ukumbi wa sabasaba
  Pichani ni Bwana harusi Goodchance Monyo akila kiapo cha ndoa mbele ya Mkewe Bi Atilia Magelanga na wageni waalikwa  mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu katika maisha ya Mwanadamu,ndani ya kanisa la Mtakatifu Peter,Oysterbay jijini Dar.
   Bibi harusi akimvalisha pete bwana harusi ikiwa pia ni ishara ya upendo na wameishakuwa mwili mmoja 
    Bwana harusi akimvalisha pete bibi harusi kuashiria kuwa wameishakuwa mwili mmoja .

   Goodchance Monyo na Atilia Magelanga wakiwa katika picha ya pamoja na mpiganaji Goodfrey Monyo mara baada ya ndoa kufungwa.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo.Baadhi ya maofisa waandamizi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (katikati) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa waandamizi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (katikati) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.

  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imefanya mabadiliko makubwa ya nembo yake pamoja na kuzindua huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE ikiwa ni muendelezo wa mpango wa kufanya mabadiliko ya kibiashara kwa kampuni hiyo. 
  Nembo hiyo mpya ya TTCL na huduma ya 4G LTE vimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa huku akiipongeza kwa hatua hiyo ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na uwajibikaji unaolenga kuonesha tija na ubora. Waziri Mbarawa alisema uzinduzi huo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli la kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na kufikia viwango vya juu kabisa vya kutoa huduma kwa umma sambamba na mpango mkakati wa TTCL kibiashara kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. 
   "Pamoja na pongezi hizi za dhati, naomba mtambue kuwa uzinduzi huu hautakuwa na maana yoyote pasipo mabadiliko ya kiutendaji utoaji huduma kwa wateja. Watumiaji wa huduma zenu wanahitaji mabadiliko ya dhati ya viwango vya huduma na utendaji ili kuwajengea imani juu ya uwezo wenu wa kuwahudumia," alisema Waziri Mbarawa. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe (kulia) wakifuatilia hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani). Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe (kulia) wakifuatilia hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani)

   Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL unaleta muonekano mpya wa kampuni unaoenda sambamba na mageuzi ambayo yanaendelea katika kuboresha miundombinu ya mtandao wa simu na data. 
   Alisema katika safari ya mageuzi TTCL imefanikiwa kuboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G GSM, 3G, UMTS na LTE sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. 
   "...Teknolojia hizi zitaisaidia kuongeza ufanisi, ubunifu katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti zenye ubora wa hali ya juu na ya uhakika na gharama nafuu," alisema Dk. Kazaura. 
   Alisema kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data nchi nzima, hali ambayo itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu wote ndani na nje ya nchi.

  0 0

  Wajumbe wa Mkutano wa Majaji Wanawake Duniani kutoka Mahakama ya Tanzania wakiwa katika ufunguzi wa mkutano huo Washington DC Marekani. Mkutano huo unawakutanisha Majaji na Mahakimu kutoka nchi 92 Duniani kuwezesha kujadili pamoja na mambo mengine wajibu wao katika kuhakikisha kuwa wanatenda haki wanapotekeleza majukumu yao. Ujumbe wa Tanzania una jumla ya wawakilishi 53.
  Ujumbe wa Mahakama ukionekana kwa mbali ukiwa katika ufunguzi rasmi wa Mkutano huo wa Wahe. Majaji Wanawake duniani.
  Baadhi ya Majaji, Mahakimu na Viongozi wawakilishi wa Mahakama ya Tanzania katika picha ya pamoja nchini Marekani.
  Baadhi ya Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi pindi walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini humo, Balozi Masilingi amefurahishwa na ugeni huo nao ujumbe wa Mahakama umesifu mapokezi mazuri yaliyotolewa na ubalozi huo toka walipofika.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusnini Pemba Mei 29, 2015 alipofika kuwashukuru wanachama wa CCM kwa ushindi waliompatia katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu.
  Wanachama cha Mapinduzi CCM wialayanya Chakechake akinyanyua mkono juu kuunga mkono maelezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro kuwapongeza wana CCM kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Wilaya ya Chakechake Pemba akitoa taarifa wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro kuwapongeza Wana CCM kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,(kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia).


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana mwishoni mwa wiki amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing na kuzungumzia masuala ya kukuza uwekezaji na ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

  Mheshimiwa Rugimbana amemwelezea Balozi wa China kuwa ameunda kikosi kazi cha Masuala ya Uwekezaji ambacho kina kazi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji, kutambua wawekezaji waliopo na changamoto zinazowakabili na njia bora za kuzitatua kwa lengo la kuboresha mazingira na kukuza uwekezaji kwenye Mkoa wa Dodoma.

  Amesema kwa sasa anataka kuanzisha eneo maalum la uwekezaji kwenye Mkoa wa Dodoma ambapo kitaundwa kituo chenye kutoa huduma zote zinazohitajika kwenye uwekezaji na kutakuwa na taasisi zote zinazohusika na utoaji wa huduma hizo ambapo mwekezaji akifika kituoni hapo hana haja ya kuondoka kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine, mahitaji yake yote yatatatuliwa hapohapo kituoni na mara moja ataanza shughuli yake ya uwekezaji.

  Pamoja na masuala hayo ya uwekezaji, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alimshirikisha Balozi wa China juu ya mpango wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa serikali hapa mkoani Dodoma wenye lengo la kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote muhimu na kuhakikisha serikali inahamia Makao Makuu Dodoma.

  Kwa upande wake Balozi Dkt. Lu Youqing alimshukuru Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa jinsi ambavyo uongozi wake wa Mkoa ulivyoweka utaratibu wa makusudi wa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuanza kushughulikia changamoto zinazowakabili wawekezaji kwa kushirikiana nao na kusema kuwa anapata taarifa nyingi kutoka kwa wawekezaji wa kichina wanaoendesha shughuli mbalimbali Mkoani Dodoma juu ya namna ambavyo uongozi wa Mkoa unashirikiana na wawekezaji hao kutatua changamoto zilizopo.

  Vilevile, Balozi wa China alimhakikishia Mheshimiwa Rugimbana kuwa atasaidia kuzikutanisha Mamlaka zinazoshughulikia ujenzi wa mji mpya wa serikali na serikali kuhamia Dodoma na mamlaka ya Manispaa ya Jiji la Beijing China ambayo inauzoefu na imefanikiwa kujenga mji mpya mbali na ule wa zamani kwa kipindi cha miaka miwili tu, lengo likiwa kubadilishana uzoefu katika kutekeleza mradi huo wenye manufaa makubwa kiuchumi hapa Tanzania.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya uwekezaji na ushirikiano.
  Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing na ujumbe alioambatana nao wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani) wakati walipomtembelea mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake mwishoni mwa wiki kuzungumzia masuala ya uwekezaji na ushirikiano.
  Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing akiagana na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyohusu masuala ya uwekezaji na ushirikiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

  0 0

  Wahitimu wa chuo cha Regional Aviation wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George Sambali (hayupo pichani) kwenye mahafali ya pili ya chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Wahitimu wa chuo cha Regional Aviation wakiwa na vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (hayupo pichani) kwenye mahafali ya pili ya chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0


  0 0

    Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi kompyuta 30 kwa Meneja Msaidizi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  Oscar Mwambene (katikati)   kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
   Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Katikati)
  KATIKA kuendeleza dhamira  yake ya kusaidia Jamii kwa kujenga ubora wa ya elimu ya ICT hapa nchini, Airtel imekabidhi kompyuta 30 kwa Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) ambapo ni sehemu mojawapo ya  mipango yake ya kusaidia vijana wajasiriamali hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA  wa kutoa huduma kwa jamii  katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na ubora wa elimu nchini Tanzania.

  Kama kampuni yenye kutoa huduma bora za simu za mkononi, Airtel itaendelea kusaidia sekta ya ICT hapa nchini kwa kuwawezesha  vijana kupata elimu iliyobora  na kuwa vijana wenye mafanikio katika Jamii yao.

  Akizungumza wakati wa sherehe za makabidhiano hayo  yaliyofanyika katika Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) kilichopo Temeke, meneja huduma kwa jamii wa Airtel,  Hawa Bayumi alisema kuwa Airtel itaendeleza dhamira yake ya kuunga mkono juhudi ya kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.

  “ Leo hii tumekabidhi kompyuta hizi tukiamini  kwamba tunachangia nchi yetu kuwa na elimu bora, ni jambo la muhimu kwa wanafunzi na walimu kuwa na vifaa bora mashuleni. Ndio maana Airtel imeweka mkazo katika swala la kusaidia Jamii kwa upande wa elimu  kwa kutoa vitendea kazi vitakavyoweza kusaidia kujifunzia na kupata elimu ya ujasiriamali na hatimaye kuchangia vyema na kupata matokeo bora. Kutokana na msaada huu kwa NCT tunaamini kabisa kwamba kiwango cha elimu kwa Wanafunzi kitaongezeka na hata urahisi wa walimu katika ufundishaji utaongezeka kwa kiwago kikubwa, na vile vile tunawawezesha kizazi kijacho kujikita zaidi katika teknolojia na kujua mambo mengi zaidi yanayoendelea dunia nzima kutokana na technolojia inayokuwa kila siku, "alisema Bayumi

  Akizungumza kwa niaba ya chuo, mkurugenzi wa Mafunzo wa NCT, Eunice Nderingo Ulomi, aliwashukuru Airtel kwa kwa msaada huo wa kompyuta , na kubainisha kuwa kompyuta hizo zitachangia kuongeza kiwango cha elimu kwa mwanafunzi kitaaluma. "Mara nyingi kompyuta huwa inatazamwa kama si kitu cha muhimu katika Jamii yetu, ila ni kifaa muhimu sana kinachomuwezesha mwanafunzi kupata habari nyingi sana za masomo na hata kujua mambo mbalimbali yanayoendelea dunia nzima hasa katika karne hii ya 21," alisema Ulomi.

  "Lengo letu ni kuhakikisha tunatoa elimu iliyobora katika  sekta ya utalii . Kupokea kompyuta hizi kutaboresha hali ngumu  tuliyakuwanayo ya upungufu wa vifaa hivi hapa chuoni na tunaamini tutatoa elimu iliyobora ambayo itasidia kupunguza changamoto tulizakuwanazo, ambazo zimekuwa zikitufanya tukwame katika mambo mengi sana, hivyo zitatusaidia  kukuza ujuzi wa kila mtu hapa chuoni, vile vile zitasaidia kuongeza mapato ya serikali, kukuza nchi yetu  katika ushindani wa kitalii na kuongeza uingizaji wa watalii ambapo itasaidia kuongeza sekta nyingine za kiuchumi katika upande wa maonyesho ", aliongeza Ulomi

  0 0
 • 05/30/16--02:45: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kulia) akikabidhi zawadi ya nguo, Mzee Filipo Mchopa (katikati) wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwenye kituo cha wazee wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki (kushoto) ni Meneja Operesheni wa AAR, Harold Adamson.
   Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kushoto) akimsalimia, Shida Uwesu, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Ofisa Madai wa Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR, Louisa Mwinchumu (katikati) akimkabidhi msaada wa chakula, Hidaya Othuman, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

  WAFANYAKAZI wa AAR Insurance Tanzania wametoa msaada wa vyakula, mavazi pamoja na vifaa vya matumizi ya nyumbani kwa kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kupitia programu maalum ya kusaidia jamii ijulikanayo kama Jaza Kikapu. Akiongea kwenye makabidhiano ya msaada huo jijini Dar es salaam leo, Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR, Hamida Rashid amesema kwamba kwa muda wa miaka 17 AAR imekuwa na utamaduni wa kuhamasisha wafanyakazi wake kutumia fursa mbalimbali kujitolea kuisaidia jamii hususani makundi ya watu wenye mahitaji maalum kupitia program ya wafanyakazi kujitolea ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakisaidia watu wenye shida mbalimbali. 

   “Sisi AAR Insurance tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu kwenye mambo yanayoigusa maisha ya watu ikiwa ni kwa wafanyakazi wetu pamoja na jamii nzima. Tunatazamia kuendelea na uhusiano mzuri na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kwa miaka mingi ijayo.” 

   Rashid alitaja baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada kuwa ni pamoja na nguo pamoja na vyombo vinavyotumika kwenye matumizi ya kila siku majumbani ambavyo vilikusanywa kutoka kwa wafanyakazi wa AAR kupitia kampeni yao ya Jaza Kikapu ambapo wafanyakazi walijitolea kutoa vitu mbalimbali kusaidia wenye shida.

   Akizungumzia msaada huu, Meneja Mauzo wa AAR Insurance Tanzania, Bi Tabia Masoud alisema“ni utamaduni wetu kama kampuni kuwajali wateja wetu na jamii iliyotuzunguka kama jinsi tunavyojali familia zetu. Tunafanya hivi ili kuona watu wote katika jamii wakiishi maisha bora.” “Tunaona fahari kuweza kutoa msaada kwa wazee kwani kundi muhimu katika jamii yetu. Wazee hawa wanaishi katika mazingira magumu, hivyo ni matumaini yetu kwamba msaada huu utaleta utofauti katika maisha yao na kuwawezesha kuendelea kufurahia maisha ipasavyo.”

  0 0

  Mtaalam wa utengenezaji wa maua yenye mchoro wa Moyo, Simon kutoka Tukuyu Mkoani Mbeya akiwa katika kazi yake ya Kutengeneza Moyo wa Maua kama alivyokuwa na kamera ya MMG Mkoani Mbeya leo.
  Mtaalamu wa Makopa simon akiwa kazini kwake leo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa Akizungumza na wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na masuala ya Afya – ICAP  kutoka chuo cha Colombia New youk, Dkt. Fernando Morales akizungumza mbele ya wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau ha oleo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa NBS jijini Dar Es Salaam leo.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (wa kwanza kushoto )akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wadau wa agenda ya Hedhi salama nchini alipokuwa akitembelea vibanda vya maonyesho ya wadau hao kwenye viwanja vya mnazi mmoja  wakati Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   WADAU wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Raymond Mushi wakati wa maadhimisho ya hedhi salama hapa nchini  wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Wizara ya Afya,  kampuni ya Kasole Secrets Company pamoja na wadau wengine wa Elimu na Usafi wa Mazingira yakiwemo mashirika ya ACRA, WSSCC, SAWA, UNICEF, WaterAid, GIZ, SNV, Plan International, Flaviana Matata Foundation, Msichana Initiative, JALI INTERNATIONAL, FLAVIANA MATATA FOUNDATION, MSICHANA INITIATIVE, JALI Project, TAYOA,  VIGOR na TMARC Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (katikati)aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya wasanii maarufu nchini, Kajala Masanja na Queen Darleen (wenye fulana nyeusi) wakiwa pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maandamano ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Na Mwandishi wetu.
  WADAU wa kutetea agenda ya hedhi salama hapa nchini wamemuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu  kutetea vikali  masuala yanayohusu  hedhi salama ikiwemo  uwepo wa mitaala ya elimu iliyo wazi juu ya hedhi salama na usafi kipindi cha hedhi katika shule zote za Msingi na Sekondari hapa nchini.


  Wadau hao walitoa ombi hilo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Kupitia risala iliyoandaliwa na wadau hao na kusomwa na mmoja wa wanafunzi, Halima Akida Mwanafunzi shule ya msingi Tandale wadau hao walimuomba makamu wa Rais Mama Samia Suluhu apiganie kuona kwamba masomo yanayofundishwa mashuleni kuanzia darasa la nne yanajumuisha elimu ya kina juu ya hedhi salama na usafi kipindi cha hedhi ikiambatana na mazingira sahihi ya usafi wa vyoo bora ili kuleta mchango mkubwa katika kunyanyua ubora wa elimu ya mtoto wa kike nchini.

  “Vilevile, ipo haja ya kuwepo kwa uwezeshwaji mkubwa baina ya Wizara zote ambazo zina dhamana kubwa katika masuala ya Jinsia, Elimu, Afya, Ardhi na Maji. Pamoja na wadau wa maendeleo ambao wanamaslahi katika suala la upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa vyoo bora, ili waweze kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja,’’ aliongeza mwanafunzi
  Aidha wadau  hao waliongeza kuwa kuna haja ya  kufanya marekebisho ya sheria ya kodi kwa kuondoa Ongezo la Kodi ya Thamani (VAT) katika bidhaa zote zinazohusiana na usafi wa ndani wa mwanamke.

  “Kwa kuzingatia unyeti wa uharaka na athari chanya za suala hili, tunatoa wito kwa suala hili kupewa nafasi na kujadiliwa katika Mkutano wa Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mkoani Dodoma,’’ aliongeza. 

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi alisema tayari serikali imeanza kuoangalia  ni jinsi gani itazileta pamoja TAMISEMI na Wizara tatu, ambazo ni Wizara ya Maji, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kufahamu namna zinavyoweza kutengeneza nia ya pamoja katika kutafuta suluhusho la kudumu.

  “Aidha Serikali itahimiza wananchi kupitia kamati za shule kuanzisha mfuko maalumu katika shule zote nchini ambao utasimamia mahitaji yote ya lazima yanayohusu maji na usafi wa mazingira mashuleni,’’ alibainisha.

  Zaidi Bw Mushi aliwapongeza wadau wao ikiwemo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Wizara ya Afya kwa kushikirikiana na kampuni ya Kasole Secrets Company pamoja na wadau wengine wa Elimu na Usafi wa Mazingira kwa kuandaa na kuadhimisha maadhimisho hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa mkoa wa Dar es Saalam na kwa ngazi ya kitaifa.

  Wadau hao ni pamoja mashirika ya ACRA, WSSCC, SAWA, UNICEF, WaterAid, GIZ, SNV, Plan International, Flaviana Matata Foundation, Msichana Initiative, JALI INTERNATIONAL, FLAVIANA MATATA FOUNDATION, MSICHANA INITIATIVE, JALI Project, TAYOA,  VIGOR na TMARC Tanzania.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akiongoza kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kikao hicho kimefanyika leo Mei 30, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma(kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
   Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri w Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Maauni(hayupo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP, John Casmir Minja(kulia) ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, DIGP, Abdulrahmani Kaniki(wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Adengenye.
  Watendaji Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini kikao kazi kilichofanyika chini ya Uenyekiti wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo Mei 30, 2016 Mkoani Dodoma.
  (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0
 • 05/30/16--05:28: TAARIFA YA MSIBA
 • MAREHEMU JACKLINE OSWALD KAPINGA

  Familia ya Marehemu Mzee Oswald Kapinga ya Sinza - Dar e salaam (karibu na  white inn) inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Jacqueline kilichotokea jana tarehe 29/05/2016 katika hospitali ya muhimbili jijini Dar es salaam. 

  Familia inapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ya kuwa, msiba utakuwa nyumbani kwa wazazi wake hapo sinza. 

  Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika, taarifa ya awali kutoka kwa familia, Marehemu wanategemea kumuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele siku ya kesho (Jumanne) ya Tarehe 31/05/2016 katika makaburi ya sinza karibu na Ukumbi wa mwika kuanzia saa 8.00 Mchana. 

  Kwa taarifa zaidi na maelekezo mbali mbali unaweza kuwasiliana na makaka wa marehemu hapo chini: 

  JOSEPH O. KAPINGA (Mwananchi communication)  - 0788617654

  GOSBERT O. KAPINGA - 0754286301

  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, 
  JINA LAKE LIHIMIDIWE
  AMEN.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
  UONGOZI wa Yanga umekana taarifa za kuwa timu ya Zamaleck ya nchini Misri kuleta ofa ya kuwataka wachezaji wake watatu na kusema kama watapata barua kutoka huko hawana budi kukaa mezani nao.

  Akizungumza Katibu Mkuu wa Yanga  Baraka Deusdedit amesema ameshapokea simu za watu wakimuuliza kuhusiana na hilo lakini ukweli kuwa hawajapata barua yoyote kutoka Zamaleck na kama kweli wanawahitaji wachezaji basi watakaa mezani na kukubaliana. Taarifa zinazosambaa ni kuwa Zamaleck wametuma barua ya kuwataka Golikipa Deogratius Munish 'dida', Juma Abdul na Vicent Bossou.

  "Nimesikia kwa baadhi ya watu na wengine wamenipigia simu juu ya hilo kuwa wachezaji watatu wanatakiwa na Zamaleck na tayari wameshatuma barua na kusema kuwa uongozi wa Yanga umeshapokea na suala liko mezani,"amesama Deusdedit. Nataka niwahakikishie tu mashabiki wa Yanga kuwa suala hilo halipo na wao kama sekretarieti hawajapokea ila litakapofika watapata taarifa kwani mpira ni kazi.

  Akijibu suala la usajili wa mchezaji wa Azam, Kipre Herman Tcheche amesema kuwa hana taarifa hiyo na anazidi kushangaa kuona taarifa hizo zinasambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kudai."Nasikia tu kuwa Yanga wamemsajili Tcheche lakini sina taarifa hizo kwa sasa na zaidi mimi ndio mtendaji Mkuu wa Yanga suala lolote lazima lije mezani kwangu,"amesema Deusdedit.

  0 0

  WAKAZI wa Kijiji la Mnavila, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, wamefanikiwa kuwaua Mamba wawili waliokuwa wakisumbua kijijini hapo kwa matukio ya kudhuru watu kwa kuwajeruhi na wengine kuuwawa kwa kuliwa na Mamba hao.

  Wananchi hao ambao makazi yao yapo kando kando ya Mto Ruvuma, wamekuwa wakipatwa na majanga hayo kwa kipindi kirefu, hali iliyowapelekea kuomba msaada kwa Kampuni ya OnTour Tanzania yenye makazi yake jijini Dar es salaam ambayo ina kibali cha kuwinda Mamba wahalibifu hasa katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara. 

  Mamba hao wamekuwa ni tishio sana kwa binadamu, hasa wale wanaotumia Mto huo kwa matimizi mbalimbali, na kupelekea watu wengi kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamepoteza viungo na kuwafanya wawe na vilema vya kudumu.
  Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mnavila, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakishirikiana na Maafisa wa Kampuni ya OnTour Tanzania, kumshusha mmoka wa Mamba hao, baada ya kuwaua kutoka na madhara ya kuwadhuru wakazi wa kijiji hicho.
  Sehemu ya Wanakijiji hao wakiwa wamewazunguka Mamba hao baada ya kuwaua ili waweze kutoa miili ya watu walioliwa.
  Mtaalamu wa kuwapasua Mamba hao, akiendelea na kazi yake ikiwa ni jitihada za kuutoa mwili wa mmoja wa Wanakijiji hao alieliwa na Mamba hao hivi karibuni.

older | 1 | .... | 1237 | 1238 | (Page 1239) | 1240 | 1241 | .... | 3284 | newer