Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1239 | 1240 | (Page 1241) | 1242 | 1243 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Msemaji wa TFF , Alfred Lucas.

  Na Zainab Nyamka,Globu Ya Jamii.
  TIMU ya Taifa ya Misri  inatua chini kesho kwa ajili ya kuvaana na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) huku   waamuzi wa mchezo huo wakitoka nchini Gabon na timu hizo zitashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa kwenye mchezo huo utakaopigwa Juni 4 mwaka huu.

  Misri ambao wamezoea kuzifunga timu za ukanda wa Afrika mashariki wanatuanchini wakiwa na jumla ya pointi saba huku Stars wakiwa na pointi moja  na katika kuelekea mchezo huo Stars ndiyo haswa itakayohitaji kuibadilisha karata ya mafarao hao kwani kwa hali yeyote kikosi cha timu hiyo kitakuwa inahitaji kuibuka na ushindi tu, kazi ambayo wachezaji itawabidi waoneshe kiwango chao cha juu ili kuweza kupata mabao mengi.

  Endapo  Stars itapata matokeo mazuri katika mchezo  huo na Misri itakuwa imejiweka pazuri kwenda kuikabili Nigeria Septemba mwaka huu na Kocha Mkuu wa  Stars Charles Boniface Mkwasa atakuwa akihitaji ushindi ambapo yupo  katika hali ya matumaini na mbinu atakazotumia kuibika na ushindi katika mchezo huo kwani amesifia maandalizi yanayofanyika kuelekea mchezo huo.

  "Timu tayari imetoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Harambee Stars katika mchezo uliochezwa katika nyasi za ugenini nchini Kenya hiyo ni hatua nzuri katika kuelekea kuona mapungufu ya timu yangu ,"alisema Mkwasa.

  Mchezo wa mataifa yote mawili utakuwa ni mchezo utakao hamua nani ataendelea katika fainali hasa kwa Misri ambayo ikipata sare ya bao moja moja itakuwa imejihakikishia kutinga katika fainali hizo.

  0 0

  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha cha Dar es salaam, wameendelea na Mgomo wao hadi muda katika Hostel za Mabibo jijini Dar es salaam, wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha za kujikimu. 

  Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshangama amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizokuwa zikitolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuhusu lini fedha hizo zitatolewa.

  Inadaiwa kuwa pesa hizo kwa kawaida huingiziwa kila baada ya siku 6o, lakini mpaka sasa ni wiki mbili zaidi ya muda ambao pesa hiyo ilitakiwa iwe imeingizwa.

  Tutaendelea kujuzana zaidi kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.
  Wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam (UDSM), wakiwa katika eneo la Cafeteria maarufu Kama Revolution Square, katika Mabweni yao ya Mabibo jijini Dar es salaam wakiwasikiliza viongozi wao

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa FNB Tanzania, Silvest Arumasi (katikati) akiwa na Meneja Masoko wa benki hiyo Blandina Mwachanga (kulia) na Meneja Mauzo wa benki hiyo, Moise Rajabu (kushoto) wakizindua kampeni mpya ya benki hiyo kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba benki ili waweze kuwekeza na kuwa na kujikimu wakati wa dharula katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
   Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
   Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa FNB Tanzania, Silvest Arumasi (katikati) na pamoja na Meneja Mauzo wa benki hiyo, Moise Rajabu (kushoto) na Meneja Masoko wa benki hiyo Blandina Mwachanga (kulia) wakizindua kampeni mpya ya benki hiyo kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba benki ili waweze kuwekeza na kuwa na kujikimu wakati wa dharula katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. 

  Benki ya FNB Tanzania imezindua kampeni mpya ya kuweka akiba ijulikanayo kwa jina la million a month award (Mama) ili kuwatunuku wateja waliopo na wapya ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuhamasisha Watanzania kuweka akiba kwa ajili ya mustakabali salama wa kifedha. Mkuu wa Huduma za Digitali wa FNB, Silvest Arumasi alisema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba shilingi milioni kumi zitatolewa kila mwezi kwa washindi kumi ambapo jumla ya shilingi milioni 30 zitatolewa kwa wateja katika muda wa miezi mitatu kuanzia Juni mwaka huu.

   Arumasi alisema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo itakayochukua miezi mitatu kwamba kwamba wateja wapya na waliopo watapata nafasi ya moja kwa moja kushiriki kwenye droo kutokana na kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao na kuweza kujishindia zawadi kila mwezi kwa miezi mitatu ya kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki. “Kila mwezi tutafanya droo moja na kuchagua washindi kumi kati ya wateja wetu ambapo washindi hao kumi na kila mmoja atajipatia zawadi ya shilingi milioni moja”. 

   Arumasi alisema kampeni hii inafungua milango ya fursa kwa Watanzania kujiwekea akiba kwa faida ya badae na inawapa fursa ya kusimamia vizuri matumizi ya fedha zao na hatimaye kuwa na utamaduni wa kuweka akiba huku wakizidi kujijengea nidhamu katika mapato na matumizi “Kupitia kampeni hii tunataka kuhimiza utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa wateja wetu ili waweze kuwekeza na kuwa na msaada wakati wa dharula. Hii ni njia mojawapo ya kujenga jamii imara yenye uhakika wa kuishi maisha bora,” alisema.

  0 0

  Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wametembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni chini ya kampuni ya Songoro Marine katika Bandari ya Dar es Salaam.

  Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Herbert Mrango ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati wa kivuko hicho na kuushauri uongozi wa TEMESA kuharakisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

  “Nakuagiza Kaimu Mtendaji uhakikishe malipo kwa kampuni hii yanafanywa kwa wakati na ukarabati huu kukamilika mapema ili kuwapa fursa wananchi kutumia kivuko hiki”alisema Balozi Mrango.

  Aliongeza kuwa ni muhimu wananchi kurejeshewa huduma ya kivuko hicho ili kuondoa kero inayowakabili kwa sasa kwa kuwa na kivuko kimoja chenye uwezo wa kubeba magari ambapo kukamilika kwa ukarabati wa huu utakuwa umerahisiha shughuli ya usafirishaji.

  Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan amesema atahakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwezesha mkandarasi huyo kumaliza kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kurejesha huduma ya kivuko hicho kwa wananchi.


  Aidha aliongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni, ukarabati wa “Body” pamoja na mifumo ya umeme unaofanywa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Songoro Marine huku TEMESA ikihusika na ukarabati wa mitambo ya kuongozea kivuko.

  Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa huduma katika maeneo ya kigamboni na Magogoni Jijini Dar es Salaam kilisimamisha rasmi kutoa huduma hiyo mapema Mei mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya Songoro Marine kukiongezea ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi.
  Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan (Kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango (katikati) wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango( wa tatu kulia) akiongoza na wajumbe wa bodi hiyo wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silvester Simfukwe (katikati walio chuchumaa) akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) sehemu ya kivuko cha Magogoni inayoendelea kufanyiwa ukarabati. Picha na Theresia Mwami-TEMESA.

  0 0

   Katibu Mkuu Baraza la Tiba Ushauri Utafiti wa Dawa Asili Tanzania BAWATA, Shariff  Karama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kutoa wito kwa waganga wote kutii agizo la Serikali la kujisajiri ili kureta ufanisi katika taaluma ya Tiba Asili hapa nchini, leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Taifa wa Baraza la Waganga Watafiti Tiba Asilia Daud Wiketye.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Baraza la Tiba Ushauri Utafiti wa Dawa Asili Tanzania BAWATA, Shariff  Karama.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

  0 0

  The European Commission has announced additional €10 million in humanitarian aid to help the increasing number of displaced Burundians. This comes on top of the €12.2 million already provided since the beginning of the year, bringing total EU humanitarian aid for the Burundi crisis in 2016 to over €22 million so far.

  More than 260 000 people, over half of whom are children, are estimated to have left Burundi since April 2015, seeking refuge in neighbouring countries.

  "The EU is committed to support the Burundian people at these difficult times. The humanitarian situation affecting Burundians remains a cause of great concern. More than a quarter of a million people have now fled their homes.

  The neighbouring countries' hosting capabilities have been stretched to the limit, with the situation in Tanzania especially worrying. The additional EU funding will help get essential aid to those in need and improve refugees' living conditions, notably in Tanzania," said EU Commissioner for Humanitarian Aid and Crisis Management Christos Stylianides.

  Tanzania has received the highest number of Burundians so far (nearly 140 000) mostly to Nyarugusu refugee camp, which has subsequently become one of the largest and most overcrowded refugee camps in the world. Even though additional camps have been set up (Mtendeli and Nduta) to accommodate the continued influx, living conditions in the camps need to improve.

  Risks of infections and epidemics are high. Sheltering conditions also involve considerable risks for the most vulnerable.

  The European Commission has been supporting the Burundian people since the beginning of the crisis.

  In total, EU humanitarian assistance released to respond to the Burundi crisis amounts to €36.2 million since May 2015.

  0 0

  UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa naShirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Musoma mkoani Mara siku ya Jumanne na Jumatano, Mei 31-Juni 1, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

  PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Magesa Mulongo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah.

  Watu takribani 200 walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Mara, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.

  Mkoa wa Mara una Halmashauri tisa, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Mji wa Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.

  PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.

  Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.


  Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza ambapo alisema kuwa PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
  Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.

  Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.
  Mtaalam kutoka TMA, Paul Chikira ambae ni mmoja wa wawezeshaji akifuatilia tukio hilo la uzinduzi wa mradi. 
   
  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

  0 0

  Barclays Bank Tanzania Head of Human Resources, Mrs Eutropia Isaack Vegula, talking to some University of Dar es Salaam students during the banks career fair event at the UDSM Business School hall  in Dar es Salaam at the weekend.
   Barclays Bank Tanzania Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joe Bendera (left) talking to some University of Dar es Salaam students during the banks career fair event at the UDSM Business School hall in Dar es Salaam at the weekend.

   Some University of Dar es Salaam students together with Barclays bank officials posing for a group photograph, during the bank career fair event in Dar es Salaam.

  0 0

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya MINJINGU Mines & Fertliser Ltd ya Arusha wametia sahihi Hati ya Makubaliano (MoU) kushirikiana katika kufanya tathimini za kina katika kitalu cha Songo Songo Magharibi.

  Akiongea baada ya kutia sahihi hati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema makubaliano kati ya TPDC na Kampuni ya Minjingu yanafungua fursa ya kufanya tathmini za kitaalamu kwa pamoja juu ya takwimu zilizopo za kitalu cha Songo Songo Magharibi ambacho kinamilikiwa na TPDC nia ikiwa ni kutafuta mashapo ambayo yanaweza kuhifadhi mafuta au gesi asilia.

  “TPDC tayari ina takwimu nyingi kuhusu Kitalu cha Songo Songo Magharibi na itafanya kazi kwa karibu na Kampuni ya MINJINGU kuhakikisha kunakua na mafanikio katika mradi huu” amesema Dkt Mataragio.

  Dkt. Mataragio amesisistiza kuwa makubaliano hayo yanatoa wajibu kwa pande zote mbili kufanya kazi kwa pamoja ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kutathmini uwezekano wa mashapo ya kitalu cha Songo Songo Magharibi kuhifadhi mafuta au gesi.

  “Iwapo kutakua na matokeo chanya basi hatua zingine za utafiti ikiwemo kuchimba kisima zitafuata” aliongezea Dkt. Mataragio.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Minjingu, Ndugu Pardeep Hans alisema wao kama kampuni ya kizawa wamefurahi sana kuaminiwa na Serikali na watafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu wa kushirikiana na TPDC ili kuhakikisha wanafikia lengo la ushirikiano wao.

  “Endapo gesi itagundulika basi itatumika kutumika katika mradi wa mbolea ambao MINJINGU wako ubia na TPDC” pamoja na Ferrostaal kutoka Ujerumani, Haldor Topsoe ya Denmark na Fauji ya Pakistani” alisema Bw. Hans.

  Makubaliano hayo ya awalia yanafungua fursa ya TPDC pamoja na MINJINGU ya ushirikiano wa utafiti katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi, Kampuni ya Mijingu ikiwa Kampuni ya kwanza ya Kizawa kushirikiaa na TPDC katika utafiti wa mafuta na gesi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (kushoto) na Mkurugenzi wa Minjingu, Bw. Pardeep Hans wakipeana mikono mara baada ya kutiliana sahihi Mkataba wa Makubaliano (MoU) katika utafiti wa mafuta na gesi na kufanya tathimini za kina katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mke wa Rais.
  Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Magogoni jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU

  0 0

  Shirika la ndege la RwandAir kuongeza ndege kubwa mbili aina ya Airbus A330 mwezi wa Tisa mwaka huu na kuanzisha safari zake mpya za Mumbai, Indina na Guanghzou - China. Shirika hilo linaendelea kupasua anga kwa kuongeza safari mpya, kusafiri kwa raha kwenye ndege zao mpya, pia kwa bei nafuu.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa bidii.

  “Nimefarijika sana kuoana suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu, lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
   
  Akizungumza kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
   
  Pia amesema katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto .Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.

  Katika kikao, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo Leo kwenye hospitali hiyo.
  Kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo, Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.
   

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
  SERIKALI kupitia Baraza la Michezo (BMT) limefungia Shirikisho la mchezo wa Ngumi za Kulipwa nchini (PST) kujihusisha na ngumi hadi kuanzia jana Mei 31 hadi Mei 2019, PST wameshushiwa rungu hilo baada ya kuchezesha watoto wenye umri chini ya miaka  10 na kumuajiri mnadi miunguko(Card Girl) mtoto mwenye umri chini ya miaka nane kinyume na sheria.

  Mbali na kufungiwa kwa shirikisho hilo pia Serikali imesitisha uteuzi wa PST, Emmanuel Mlundwa kama mjumbe wa kamati ya kutengeneza katiba, kanuni na taratibu za kufuatwa katika michezo ya ngumi za kulipwa.

  Akitoa tamko hilo Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa Katika pambano lililofanyika Mei 14 kati ya Thomas Mashali na bondia wa Iran, Sadjadi Meherab waliwachezesha watoto hao huku kitendo kama hicho pia kikiwahi kutokea Juni 18 mwaka 2002. "Katika pambano hilo PST walimtumia mtoto Joyce Francis ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kama mnadi mizunguko katika pambano hilo", amesema Kiganja.

  Amesema kuwa Mlundwa na katibu wake Anthony Rutta hawatapewa kibali chochote na serikali cha kuratibu mapambano hayo ndani wala nje ya nchi.

  "Tumewafungia kina Mlundwa kuanzia leo hivyo mialiko yote ya mabondia itapitia mezani kwangu na kamati itayashughulikia bila kuathiri haki za mabondia na hao washiriki katika mashindano", amesema Kiganja. Baada ya kusikiliza utetezi wa Mlundwa juu ya suala hilo  PST wamesema wapo tayari kusitisha mapambano ya watoto ikiwa ni maoni kama kusitisha huko kutazorotesha maendeleo ya mchezo huo.

  Amesema kuwa BMT walitegemea kukuta utetezi wake utataja mamlaka yaliyomruhusu kuandaa ngumi za watoto lakini kwa bahati mbaya hawakukutana na kipengele hicho katika utetezi wake kutokana na suala hilo Serikali imevitaka vyama vyote vya michezo kuheshimu na kuepuka kufanya kazi bila kufuata kanuni za mchezo husika.

  0 0
 • 05/31/16--13:30: elimu sasa


 • 0 0

  MCHAKATO wa usajili wa washiriki wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, umezidi kushika kasi, huku siku tatu zikiwa zimesalia kabla ya kufanyika kwake Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto wao.

  Gidabuday alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100 na mita 50.Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

  Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na kushinda zawadi.Naye, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank inayodhamini mashindano hayo, Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusajili watoto wao katika Azania Bank Kids Run, ili kufikia lengo lao la kuibua vipaji vipya vya riadha.

  Jibrea alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao.Alizitaja zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo (track suit).
  Jibrea alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.

  Katika mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh. 75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo."Pia, washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh. 15,000, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo. Nia ni kuwafanya watoto watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano," alisema Jibrea.

  0 0

  East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: June 1, 2016: In a memorable occasion for the East African Legislative Assembly, founding First Ladies of the EAC late yesterday delivered motivating addresses at a Special Sitting held in Arusha.

  Looking graceful yet resplendent, Kenya’s Mama Ngina Kenyatta and Uganda’s Mama Miria Obote brought back the good old memories of the first EAC and challenged EALA Members to ensure the future of integration is both guaranteed and realised.  The United Republic of Tanzania’s Mama Maria Nyerere sent her apologies. Her family was however represented at the occasion of the Special Sitting by Hon Makongoro Nyerere, who is an elected Member of EALA.

  First to take the podium was Mama Miria Obote who was emphatic that the EAC must re-energise itself and strive to be a fully functioning integration bloc.   The former First Lady called for prioritisation of economic investment projects including oil refineries, the Standard Gauge Railway, agricultural research, food security and climate change.
  A birds eye view of the proceedings

  The founding First Lady called for creation of employment opportunities especially for the youth in the region.

  “This can be achieved through joint or common East African Community investments such as the ongoing projects between Uganda and Tanzania for the proposed pipeline, Uganda, Rwanda, Tanzania and Kenya for the Standard Gauge Railway; Kenya, Ethiopia and the new South Sudan for the Lamu Port. The clear call should be an intensification of efforts across various fields to make our region more integrated”, H.E. Mama Obote said.

  She further called for the region to move faster to have an integrated syllabus and curriculum to stabilise the labour market within the EAC.
  H.E. Mama Miria Obote delivers her remarks as H.E Mama Ngina Kenyatta pays attention at the Special Sitting in Arusha.

  “For instance, a majority of Ugandans have never learnt proper Swahili. We are now learning proper Swahili in schools and in the public engagement. This is the best way towards integration”, Mama Obote said.

  Mama Miria Obote was full of praise for the EALA for recognising the contribution of the founding families.

  “We are very grateful for EAC and EALA for recognising the contribution of our founding Fathers, Comrade Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Jomo Kenyatta & Comrade Dr. Apolo Milton Obote and we are also thankful to the Almighty God for having kept us alive as former First Ladies of the Independent East African Community, Mama Miria Nyerere, Mama Ngina Kenyatta and I”, Mama Obote said. 
  EALA Speaker presents a plaque to Hon Makongoro Nyerere, Member of EALA and son of the founding father of the United Republic of Tanzania, H.E. Mwalimu Julius Nyerere and H.E. Mama Maria Nyerere.

  She further appreciated the Governments of the United Republic of Tanzania, Kenya and their people who as the original Members of the East African Community, understood the social-political challenges of Uganda.


  0 0

  Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika Kusini waliouawa kinyama na iliyokuwa Serikali ya Makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 Juni, 1976.

  Watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu. Kwa kutambua umuhimu wa mtoto, Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kitaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kutumia njia mbalimbali ikewemo vyombo vya habari (magazeti, redio runinga).

  Pia itaendesha kampeni katika mitandao ya kijamii (Intagram na facebook) iliyopewa jina la “#NAMPENDANITAMLINDA” ambayo itatoa fursa kwa watu mbalimbali Tanzania kupiga picha wakiwa na watoto na kuzituma “kupost” kwenye mitandao yao ya kijamii (Instagram na Facebook) na kisha kuandika (hush tag) “#NAMPENDANTAMLINDA”.

  Lengo la kampeni ili kuimarisha juhudi za wadau mbalimbali katika kulinda na kuendeleza haki na maslahi ya watoto nchini. Kampeni hii itaanza Juni 1 na kuhitimisha kilele tarehe 16 Juni ambayo ni siku ya Mtoto wa Africa.

  Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni “Migogoro na machafuko Afrika: Tulinde haki za Watoto”

  TAMWA inawaomba wadau mbalimbali wakiwemo wazazi, waalimu, viongozi, wasanii na wanajamii kwa kuonyesha upendo kwa watoto kwa kuithibitishia jamii kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwa wanawapenda na watalinda haki zao.

  0 0

  MCHAKATO wa usajili wa washiriki wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, umezidi kushika kasi, huku siku tatu zikiwa zimesalia kabla ya kufanyika kwake Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto wao.

  Gidabuday alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100 na mita 50.
  Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji. Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na kushinda zawadi.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Kwanza Napenda kuchukua Nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuniwezesha kuiona siku ya Leo maana Si kwa uwezo wangu bali ni kwa Uwezo wake Muumba wetu aliye Juu. 

  Leo ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.

  Napenda Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema. Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana. 

  Nakukabidhi wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5 Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.

  Naomba pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi 37:23 Kuwa "Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake"Hakika wewe ni Mungu wa Wote.

  Nachukua fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata marafiki zangu. Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi sio mwema sana kuzidi wengine.

  Wewe Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea Nayaona na kuyafurahia.

  Asante sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu. Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.

  Happy Birthday to You Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  0 0


older | 1 | .... | 1239 | 1240 | (Page 1241) | 1242 | 1243 | .... | 3270 | newer