Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO


JTI wazindua mradi kupunguza ajira kwa watoto

$
0
0
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaharu Yoshida(kulia) akimpongeza kwa kumshika mkono Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu, Dk. Abdallah Possi mara baada ya kuzindua Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaharu Yoshida, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa ya kuzindua Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.
Mkurugenzi wa miradi ya jamii Duniani kutoka JTI(Global Director,Social Programs), Elaine McKay, akizungumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.

Na mwandishi wetu, Morogoro

KAMPUNI ya Sigara ya JTI Tanzania imezindua mpango mpya uitwao ARISE wenye lengo la kupunguza ajira kwa watoto kwenye sekta ya kilimo.

ARISE ambapo kwa kirefu inamaanisha (Achieving Reduction of Child Labor in Support of Education) ni mradi endelevu wa miaka mingi ulioanzishwa nchini Brazili na Malawi kwa ajili ya Jamii ambapo zinajiusisha na shughuli za kilimo cha Tumbaku.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

VETA YAWAPA MAENDELEO YA MRADI WA WANAGENZI (DUAL APPREATICESHIP) WADAU WA VIWANDA

$
0
0
MAMALAKA ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA) ikishirikiana na wadau kutoka viwanda vya umeme na umeme wa magari wametoa maendeleo ya mradi huo kwa wadau wa viwanda.
 
Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko wakati akizungumza na wadau wa viwanda vya umeme na umeme wa magari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa mafunzo hayo yanaumhimu mkuwa kwa viwanda kwani mafunzo hutolewa kwa umahili mkubwa kwa walichaguliwa kujifunza mafunzo hayo kutokana na mahitaji ya kiwanda.
 
Bukko amesema kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya vitendo zaidi (Hands & Skills) chini ya Mradi wa ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman.
 
Amesema kuwa utaratibu wa mafunzo hayo yamaendaliwa kutoka na vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi.
Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko akizungumza katika mkusanyiko wa wafanyakazi,viongozi wa Veta pamoja na (Wanagenzi) wanafunzi wanafanya mafunzo yao katika viwanda mbalimbali hapa nchini waliojiunga katika mradi wa wanagnizi(APPREUTICESHIP) jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa mradi huo unawajulisha wanafunzi wanataka kujiunga na mafunzo hayo katika chuo cha Veta na kufanya kazi katika viwanda mbalimbali hapa nchini kuwa mafunzo hayo hayana gharama yoyote na unajifunza katika kiwanda unachohitaji kutokana na taaluma yako.
 

Meneja wa Mradi wa Appreaticeship kutoka kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman, Maltin Mac Mahon akizungumza na wadau wa Veta jijini Dar es Salaam leo na akielezea jinsi alivyowafundisha wanafunzi wa veta ambao wapo na ambao hawapo viwandani hapa nchini kutengeneza vitu vya umeme pamoja na umeme wa magari hapa nchini pamoja na vitu mbalimbali vilivyopo katika viwanda mbalimbali kutokana na mahitaji ya kiwanda husika.
Wanafunzi wanafanya mafunzo katika viwanda mbalimbali hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha mafunzo ya ufundi (VETA) jijini Dar es Salaam leo.

MAJAMBOZZZ: CHUMBA CHA DEREVA TAX CHAZUA KIZAA ZAA MTAA WA MBEZI MTONI GOLD STAR, DAR

$
0
0
Na Ripota maalum, Dar

UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.

Mtandao huu ulipata fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama 'NYATI'.
Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya chumba hicho.

Akizungumza na mtandao huu, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema kuwa siku ya Mei 23, akiwa ameketi uwanjani karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia chini ya mlango.

Kesho yake Mei 24 Baada ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na mashaka na chumba hicho.
Vyupa kila kona

Mei 25 Mama mwenye nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye, kutoa taarifa juu ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na Viongozi wengine, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine  Abdalla Mlaliya na Matrida Paston, waliofika na kujionea hali halisi ya chumba hicho.

Baada ya viongozi hao kufika eneo la tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi.

SOMA ZAIDI HAPA

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI (DART) JIJINI DAR LEO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea.

Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa kutumia usafiri huo.

Waziri Mkuu alipanda basi hilo saa 3:30 asubuhi na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine wapande. Kwa wastani ililtumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka kituo kimoja hadi kingine. Basi hilo liliwasili Kimara Mwisho saa 4:23 asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo fupi ya ukaguzi leo (Ijumaa, Mei 27, 2016), Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na pia kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo.

Amesema ameridhishwa na mradi unavyofanya kazi ila ameelezwa kuna usumbufu kwenye mageti wakati abiria wanapotaka kuthibitisha tiketi zao hasa wakati wa asubuhi kunapokuwa na msongamano wa abiria. Pia alielezwa kwamba kuna baadhi ya abiria wanakuja na tiketi za jana yake jambo ambalo linaleta usumbufu kwa sababu hazitambuliki kwenye mfumo wao.

“Nimeridhishwa na uharaka wa njia kwa sababu na mimi mwenyewe nimetumia dakika 50 kufika hapa ingawa kuna maeneo nimeona kuna haja ya kuwa na taa maalum za kuzuia magari (special sensors) wakati mabasi yakipita ili kuepusha ajali,” alisema.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na mtaa wa Samora, Morogoro na Jamhuri na makutano ya Morogoro na Kisutu.

Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waende na tiketi rasmi badala ya kutumia tiketi za jana kwa sababu kufanya hivyo ni makosa na  mtu anakuwa amedhamiria. “Hawa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Mtu akija na tiketi ya jana akamatwe na kupelekwa polisi, huyu atakuwa amedhamiria,” alisema Waziri Mkuu wakati akiongea na mhudumu mmoja katika kituo cha Kimara Mwisho.

“Ninawasihi wananchi wanaotumia usafiri huu wajifunze kufuata utaratibu na kuwasisitizia kuwa kila abiria aje na tiketi ambayo ni rasmi,” alisema na kuongeza: “Haya mabasi nimebaini yako vizuri. Ninatoa msukumo kwa watumishi wa umma wapande mabasi haya ili kupunguza msongamnao wa magari barabarani.”

Katika kupiunguza baadhi ya changamoto, Waziri Mkuu alisema Serikali itasimamia uboreshaji wa ukataji tiketi ili kuondoa usumbufu kwa abiria. Pia alivionya vyombo vya moto viache kutumia njia maalum ya mabasi hayo.

Pia aliwataka polisi wanaofanya doria za usiku kupita kwenye fly-overs na kuwaondoa watu wanaolala kwenye maeneo kwani wanahatarisha usalama wa watu wanaotumia njia hizo. “Zile siyo sehemu za kulala, wanaofanya hivyo wanahatarisha usalama wa watumiaji wa njia hizo, kwa hiyo polisi wakiwakuta watu wa aina hiyo wawakamate mara moja,” alisema.

Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ambaye alifuatana na Waziri Mkuu kaktika ziara hiyo, alisema amepiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali.

“Tulishapiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali, ninawasihi madereva watambue hili na watii,” alisema.

Machi 22, mwaka huu Waziri Mkuu alitembelea soko la Feri kwa lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo (kuzuia moshi) na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.

Aprili 15, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya kikao na kuwaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza pindi majaribio yakianza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja uliopita ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.

Usafiri wa DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao. Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MZEE MOHAMED SALEHE KAOMBWE ANATAFUTWA NA NDUGU ZAKE

$
0
0
Mimi Mzee Hussein Salehe Kaombwe natangaza kumtafuta kaka yangu mzee Mohamedi Salehe Kaombwe ambaye alitoweka nyumbani kwake magomeni mikumi nyumba namba 191 mtaa wa ifunda, kwasasa nyumba ina namba 9 (mfumo mpya wa namba za nyumba)

Mzee Mohamedi Salehe Kaombwe alikuwa anafanya biashara ya jongoo pwani kati ya Dar es salaa, mafia na kilwa masoko

Tafadhali naomba kwa yeyote anae mfahamu na kumuona alipo atoe taarifa katika kituo cha polisi kilichokuwa karibu nae au atoe taarifa kwa kupiga namba

Mzee Hussein Salehe kaombwe (0712 07 00 19), Salehe Mohamedi Salehe (0754 711 862) Hamisi Mohamedi Salehe (0717 079 124)

MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU UTAWALA WA SHERIA KUFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Mkutano wa Kimataifa kujadili masuala ya Utawala wa Sheria kama chachu ya Maendeleo Endelevu unatarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 1 na 2 Juni, 2016.

Mkutano huo ambao utafanyika katika ngazi ya Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika utafunguliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe (Mb.) na kuhudhuriwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika, Maafisa Waandamizi wa Serikali na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Kimataifa.

Mkutano huo unaolenga kuweka sera, mikakati thabiti, pamoja na kubadilishana uzoefu, weledi na ujuzi miongoni mwa washiriki ili kuwawezesha kutekeleza malengo mapya ya dunia chini ya dira mpya ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Dunia ijulikanayo kama “Agenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030” yenye jumla ya Malengo 17. Malengo hayo yanarithi Malengo ya Milenia yaliyomaliza muda wake mwaka 2015.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Septemba 2015 Jumuiya ya Kimataifa ilifikia makubaliano ya kihistoria kwa kupitisha Agenda mpya ya Maendeleo Endelevu wakati wa Mkutano Maalum wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Mjini New York, Marekani. 

Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa walikubaliana kuwa na Dira Mpya ya Maendeleo ya Dunia ikilenga katika kutokomeza umaskini; kulinda mazingira; kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kushirikisha makundi yote kwenye jamii katika masuala ya maendeleo.

Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sheria (International Development Law Organisation-IDLO) yenye Makao yake makuu mjini Roma, Italia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki takriban 70 kutoka ndani na nje ya Tanzania na umejikita zaidi kwenye lengo Namba 16 linalohimiza haki, amani na jamii shirikishi.

JPM AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JK IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU


MAHAKAMA KUONGEZA MAJAJI MWANZA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman
Na Lydia Churi- Mwanza.

Mahakama ya Tanzania inakusudia kuongeza idadi ya Majaji katika kanda yake ya Mwanza ili kuongeza msukumo wa kumaliza kesi za mauaji kutokana na kanda hiyo kuongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchi nzima.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ataongeza idadi ya majaji katika kanda hiyo ili kesi hizo za mauaji zimalizike kwa wakati.

Jaji Mkuu pia ameiagiza Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kuzipa msukumo maalum kesi za mauaji ili kuhakikisha zinamalizika mapema na kupunguza mlundikano wa kesi katika mahakama za Tanzania.
Awali akisoma taaarifa ya hali halisi ya kesi katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Jaji Mfawidhi wa kanda hiyo Mheshimiwa Robert Makaramba alisema kanda ya Mwanza ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchini ambapo hadi kufikia Aprili mwaka huu kuna jumla ya kesi 512 za mauaji.

Pamoja na mkakati wa Jaji Mkuu kuongeza idadi ya Majaji ili kumaliza kesi hizo, Jaji Mfawidhi wa kanda ya Mwanza alisema wameshachambua kesi hizo za mauaji ambapo Jaji Kiongozi pia aliahidi kuwaongezea jumla ya Majaji 11 ili waweze kusaidia kusukuma kesi hizo.

Jaji Makaramba alisema kati ya mwezi Juni na Julai jumla ya vikao 11 vinatarajiwa kukaa ili kusikiliza kesi 123 zilizopangwa kusikilizwa. Alisema kati ya kesi hizo, 35 ni zile zitakazosikilizwa kwa mara ya kwanza na kesi 88 ni zile zitakazosikilizwa mpaka mwisho.

Alisema endapo vikao hivyo vitafanyika kama ilivyokusudiwa vitasaidia kupunguza kesi zilizopo mahakamani kwa miaka mingi.

Hadi kufikia mwezi April mwaka huu, Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ina jumla ya kesi 2771 za aina zote zikiwemo zile za Madai ya kawaida, Madai ya Ardhi na za jinai. Ili kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi hizo, kila Jaji amepangiwa kusikiliza kesi 346. Kanda hiyo ina Majaji nane (8).

Jaji Mkuu wa Tanzania ameanza ziara katika kanda ya Mwanza inayohusisha mikoa ya Geita, Mwanza na Mara ambapo atakagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.

TUTAPIGANA KUFA NA KUPONA KUVUKA HATUA YA MAKUNDI -CANAVARO

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
BAADA ya kuiongoza timu yake kutetea ubingwa wa ligi kuu, fainali ya kombe la FA na kuingia hatua ya makundi nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'canavaro' (Pichani)amesema kuwa watahakikisha wanapiga kufa na kupona kuweza kuisaidia timu yao kuingia hatua ya nusu fainali kwani kama watafanya vizuri michezo mitatu ya mwanzo basi watakuwa wameweza kuvuka makundi.

Canavaro amesema mwaka huu wamekuwa na kikosi bora ambacho kimekuwa kinaleta ushindani wa hali ya juu katika kila mechi watakayokuwa wanacheza na hicho kinakuwa ndiyo msingi mkubwa kwao wa kufanya vizuri zaidi.

"Tumeingia hatua ya makundi na tunajua ni moja ya hatua ngumu sana tuliopo ila michezo mitatu ya mwanzo tukipata alama basi tutaingia nusu fainali na hatimaye fainali kabisa na ikiwezekana tutaleta kombe nchini,"amesema Canavaro. 

Na katika kujiandaa zaidi kocha mkuu Hans Van De Pluijm anajua ni wapi atapeleka kikosi kwa ajili ya maandalizi zaidi kwani Juni 17 tunaanza kucheza na Mo bejala nchini Algeria na siku 10 baadae kutakuwa na mechi nyingine dhidi ya TP Mazembe Jijini Dar es salaam.

Amesema, kwa sasa wachezaji wote wanatakiwa kujiweka sawa na kuwazia mashindano yaliyokuwa mbele yao katika kipindi hiki kwani kufanya vizuri kwao kutalitambulisha taifa zaidi.

Wakati huohuo,
Timu ya Taifa imeondoka Alfajiri ya leo huku nahodha huyo wa zamani Canavaro akiwa hajajumuika na kikosi hicho kinachonolewa na Charles Boniface Mkwasa na kuendelea kuweka msimamo wake wa kutokuchezea timu ya taifa kwani ameshaamua na tayari barua ipo TFF.

"Nimeshaweka msimamo wangu kuwa sitachezea tena timu yaTaifa na ndio maana sijajiunga nao kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars,"amesema Canavaro.

Toka kujiengua kwa Canavaro,Mkwasa anamuita kwa mara ya kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi alizocheza akitoka katika majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu bila kucheza.

IDADI YA VIFO KWA WATOTO WACHANGA NA WAKINA MAMA VYAZIDI KUPUNGUA NCHINI.

$
0
0


Na Ally Daud- maelezo

Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .

Akizungumza hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama.

“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii” alisema Dkt. Mbando.

Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.

Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.

Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.

Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mshauri wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.Picha zote na Ally Daud-Maelezo

SHIRIKA LA NDEGE LA SERBIA LAPIGA HATUA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

$
0
0
Ndege kubwa ya kwanza ya shirika la ndege la Serbia, Airbus A330, ikiwa katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla. Ndege hii itakuwa ikifanya safari zake kati ya Belgrade na New York.

Shirika la ndege la Serbia, ambalo ni shirika la ndege la Taifa la Serbia, lilisherehekea hatua nyingine katika mabadiliko kama shirika la ndege linaloongoza katika kanda, kwa kuwasili kwa ndege yake kubwa ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla jana.

Ndege aina ya Airbus A330 itatumika katika ruti za shirika la ndege la Serbia kati ya Belgrade kwenda New York, Ambayo itazinduliwa tarehe 26 Juni 2016, ikiunganisha Serbia na Marekani kwa huduma ya ndege ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika miaka 24.

Baada ya kutua Belgrade, ndege hiyo ililakiwa kwa salamu za kitamaduni za urushaji wa maji na kukabidhiwa kwa wawakilishi wa ndege hiyo. Waliokuwa katika safari ya kwanza ya ndege hiyo ya kihistoria ni kundi la wadau wakubwa wakiongozwa na Siniša Mali, Mwenyekiti wa shirika la ndege la Serbia na Meya wa Belgrade, na Dane Kondić, Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Serbia. 

NECTA SASA KUFUNGA MITIHANI KWA KUTUMIA MASHINE.

$
0
0
Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejipanga kuanza kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani kwa kutumia mashine maalum ili kuondokana na hatari ya kuvuja kwa mitihani hiyo na gharama za ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/2017, jana Bungeni Mjini Dodoma.

Prof. Ndalichako alisema kuwa katika kuimarisha utendaji kazi wake NECTA itanunua mashine mbili za kufunga mitihani (Auto Poly Wrapping and Packing Machine) ili kuimarisha usalama wa mitihani kwa kupunguza watu wanaoshiriki kwenye maandalizi ya mitihani hiyo.

“Katika mwaka 2016/2017 Baraza litasimika mashine mbili za kufunga bahasha za mitihani hivyo kuondoa hatari zinazoweza kujitokeza kwa kuwa idadi ya watu wanaofanya kazi hiyo itapungua.” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako aliongeza kuwa Baraza litaboresha mfumo wake wa ukusanyaji na uchakati takwimu na kuweka Mfumo wa Kielektroniki wa kumtambua mwanafunzi kwa namba maalum tangu anapoandikishwa shuleni hadi atakapomaliza mzunguko wa masomo yake.

Alisema kuwa mfumo huo wa utambuzi utaunganishwa nchi nzima ili kuwezesha kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi kwenye shule yoyote atakayoenda kusoma ndani ya nchi kwa kuwa namba hiyo atakayopewa na Baraza ataitumia hata kwenye shule nyingine atakazohamia.

“Wizara itaweka Mfumo wa Kielektroniki wa ukusanyaji taarifa za wanafunzi chini ya Baraza la Mitihani ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo wakati wa mitihani na utaratibu huu utapunguza matumizi makubwa ya fedha kupitia mfumo wa TSM9.” alisema Prof. Ndalichako.

Pia alieleza kuwa katika kufanikisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), mwaka wa fedha uliopita Mamlaka ya Elimu Tanzania imechapisha vitabu 558,720 vya jinsi ya kujibu mitihani ya Kidato cha Pili na Kidato cha Nne ili kuwawezesha wanafunzi watahiniwa kujibu maswali vizuri katika mitihani yao hatimaye kuongeza ufaulu.

NIPO TAYARI KUKAA MEZANI NA TIMU YOYOTE - HUMUD.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIUNGO wa Coastal Union Abdulhalim Humud (Pichani)amesema yeye ni mchezaji huru na anaweza kukaa mezani na timu yoyote kwa sasa kwani mkataba wake na Coastal Union umekwisha kwa sasa huku timu hiyo ikiwa tayari imeshashuka daraja.

Akizungumza na Michuzi Blog Humud amesema kwa atakayehitaji huduma kutoka kwake basi watakaa mezani na kuingia makubaliano nao na kuweka wazi changamoto alizokutana nazo katika timu ya Coastal Union mpaka kupelekea kushuka daraja na chanzo kikuu kikiwa ni ubovu wa uongozi uliopo pale.

"Nimemaliza mkataba wangu na Coastal Union na nipo huru kujiunga na timu yoyote kwa sasa na watakaonihitaji nitakaa nao mezani na kuweka makubaliano kwa kila upande kuridhika na makubaliano hayo,"amesema Humud. Kiungo huyo ameweka wazi matatizo yaliyopo kwenye timu ya Coastal Union na kusema viongozi ndiyo wamefanya mpaka timu hiyo kushuka daraja kwani wameshindwa kuiongoza kipindi chote na hata chama cha mpira wa miguu mkoa nao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana.

Amesema, wamekuwa na kikosi kizuri sana katika ligi ila wakashindwa kujituma sana kwani walikuwa hawapati stahiki zao kama inavyotakiwa na kuishia kucheza mpira wakiwa wameshavunjika moyo na kuona bora liende.

Humud amewahi kukipiga katika timu za Simba na Azam na baadae Sofapaka ya Kenya na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu alizopitia katika kipindi chote.

EAC TABLES USD 100 M BUDGET TO EALA

$
0
0
The EAC today presented Budget estimates for the Financial Year 2016/2017 totaling $101,374,589 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha. Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon Dr Susan Kolimba presented the Budget speech to an attentive House on behalf of the substantive Minister and Chair of the EAC Council of
Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.

The 2016/2017 Budget is adrop down from $110,660,098 Million presented to the House in the previous Financial Year. The Budget prioritizes the full implementation of the EAC Single Customs Territory, enhanced implementation of the EAC Common Market Protocol especially additional commitments and interconnectivity of border immigration systems and procedures acrossn Partner States and enhancement of productivity and value addition in key productive sectors.

The budget also takes cognisance of development of cross-border infrastructure and harmonisation of laws,policies and standards in respective sub-sectors, implementation of a liberalised EAC airspace, enhanced implementation a One Area Network in telecommunications and the implementation of EAC Peace and Security initiatives.

According to the Minister, other key specific priorities are strengthening of the legal and judicial systems, enhancement of Information, Communication and Education to promote popular participation of the citizenry in the EAC integration process and promotion of education, science and technology for creative and productive human resources.
Hon Dr Susan Kolimba, Deputy Minister, Foreign Affairs and East African
Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko.
The deputy Minister of Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the
EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.
 

VOLVO SHOWCASE THEIR PRODUCTS AT CONTRACTORS INTERNATIONAL CONFERENCE.

$
0
0
AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) gestures with President of Tanzania, Dr.John Pombe Magufuli (left) and other delegates regarding construction equipment and trucks during Contractors International Conference in Dar es Salaam recently.

WAZIRI PROFESA MAKAME ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE NA KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na MawasilianoProfesa Makame Mbarawa.
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es salaamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
 

KAMANDA SIRRO ATINGA MTAANI KUTOA SOMO LA ULINZI NA USALAMA, AWANYOOSEA KIDOLE WANAOJIFUNZA MAMBO YA KIVITA SEHEMU ZA IBADA

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na wanachi wa maeneo ya Manzese, wakati akitoa wito wa kuwataka wanaojifunza mambo ya kivita katika sehemu za ibada kuacha mara moja, kwani hiyo si kazi yao na wala hailipi. Kamanda Sirro aliingia mtaani kutoa somo hilo kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuendeleza jitihada za kuimarisha ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.
Kamanda Sirro akiendelea kutoa somo kwa wamazi wa maeneo ya Manzese, Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wananchi walioitikia wito wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, alipokuwa akitoa somo kuimarisha ulinzi na Usalama Jijini. Mkutano huo ilifanyika kwenye viwanja vya Manzese jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

HIZI SASA SIFA......

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images