Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1233 | 1234 | (Page 1235) | 1236 | 1237 | .... | 3270 | newer

  0 0   Rais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub, mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1, katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es salaam. Picha na Othman Michuzi.
   Wachezaji wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia bao la kuongoza aliloipatia timu yake dhidi ya Azam FC , katika mchezo uliopigwa jioni hii, ikiwa ni mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1. Picha na Othman Michuzi.

  Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" akiichambua ngome ya Timu ya Yanga, katika mchezo uliopigwa jioni hii, ikiwa ni mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1.
   Mchezaji wa timu ya Yanga Oscar Joshua akimzuia mchezaji wa timu ya Azam FC Himid Mao kwenye mchezo wao wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1.
  Lango la Azam  FC likiwa hatarini kuvunjwa. 


  0 0

   Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.
  Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.
  Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.
  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Dkt. Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani,akiwa  na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Muungano wa Comoro wakati  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani, akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikatki) akifuatana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi (kulia) wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika  sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani,  akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed. Picha na IKULU Zanzibar

  0 0

  Ndoa inayotarajiwa  kufungwa  inaweza kuzuiwa kwa pingamizi. Sheria ilishaweka  utaratibu maalum  wa  kuzuia  ndoa  kufungwa  kwa  wale  wenye malengo  ya  kufanya  hivyo. Badala  ya kutumia  fujo ,mabaunsa na hila zisizo  za kisheria  kuzuia ndoa  au harusi  waweza  kutumia njia halali ya kisheria  na  ukafanikiwa  kuzuia  ndoa  kufungwa.
  Fujo  na hila zisizo  za  kisheria katika kuzuia  ndoa zaweza  kukuletea   madhara makubwa na  hata  jinai. Ya nini  basi ufanye  hivyo   wakati   ipo  namna halali na salama ya  kuzuia .Sababu  zipi  unaweza kutumia kuzuia na  mengine  tutaona  hapa chini. 

  0 0


  0 0

  MADEREVA wa magari waaswa kuwa makini wakati wakiendesha magari hasa katika makutano ya magari ya mwendo wa haraka yanayotoa huduma za usafari jijini Dares Salaam.


  Hayo yamesikika na shuhuda mmoja wakati wa ajali iliyotokea katika makutano ya Barabara ya BRT na Bibititi Mohamed eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.

  Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 katika eneo la Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC na gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.
  Ajali imetokea katika makutano ya barabara ya Bibititi Mohamed na barabara ya BRT  maeneo ya  chuo cha CBE  jijini Dar es Salaam ikiwa ajari hiyo imetokea kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC lililokuwa likitokea Mnazi mmoja kuelekea Maktaba na kugonga gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.
  Chanzo cha ajali hiyo ni Mataa ya makutano ya barabara hiyo kutokufanya kazi ya kuongoza magari.

   Gari lenye namba za usajili T 713 DFC  likiwa limeharibika mara baada ya kugonga gari la Mwendo wa haraka katika eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.
   Gari lenye namba za usajili T 713 DFC ambalo limeharibika kwa kugonga gari la mwendo wa haraka likivutwa na Breakdown kuondolewa eneo palipokuwa na ajali hiyo eneo  chuo cha CBE na katika makutano ya barabara ya BRT na Bibititi Mohamed jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.

  “Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).

  “Hatutaki tabia iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo zamani halikuwepo,” alisema.

  Alisema Serikali imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu,” alisema na kuongeza.

  “Hatutamvumilia mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.” 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


  0 0

  Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
  mganga mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
  Mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.
  Meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima dendego.

  JITIHADA za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.

  Takwimu hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza au kutokomezwa kabisa.

  Takwimu hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.

  “Tunataraji kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa wananchi,”alisema Sichalwe

  Aidha Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje yani OPD sawa na asilimia 17.5.

  Naye Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.

  “Hatutumia wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima

  Akizungumza mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa manufaa ya baba na mama.

  “Nawaomba kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa

  Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu

  0 0

  Stanbic Bank Head Capital Markets- East Africa- Wegoki Mugeni (Centre) receiving the award for Best Investment Bank- Tanzania 2016. The other two are officials from the Banker Africa.
  STANBIC Bank Tanzania has scooped the Best Investment Bank 2016 Award at The Banker Africa Awards held in Nairobi, Kenya on Tuesday.Stanbic Bank was voted the Best Investment Bank 2016 in Tanzania by a panel consisting financial industry experts and peers from the banking industry in the region.

  “This is a major endorsement of Stanbic Bank’s expertise and capabilities in spurring investment within Tanzania and the region. We have in-depth understanding of the unique conditions, opportunities and challenges that come with operating in the region, where macroeconomic stability along with institutional and policy reforms are supporting strong development.’’ Said Ken Cockerill, Stanbic Bank Tanzania’s Chief Executive Officer.

  He revealed that the main drivers of growth in the country are telecommunications, transport, financial intermediation, manufacturing, construction, and trade.“Stanbic bank works by understanding all players in the sector value chain and leveraging the global expertise of sector doyens and product specialists at a group level to develop tailor made solutions for our clients across the continent. These unique insights make us the go-to local banking partner with international reach.” He added.

  Stanbic Bank Uganda and CFC Stanbic Kenya were also named best investment bank in their respective countries.Last year, EMEA Finance also named Stanbic Bank Tanzania best investment bank in Tanzania, Uganda and Kenya among other countries where the bank has representation.

  Stanbic Bank Tanzania is part of the Standard Bank Group, Africa’s largest bank by assets.

  Stanbic Bank Tanzania provides the full spectrum of financial services. It’s Corporate and Investment Banking division serves a wide range of requirements for banking, finance, trading, investment, risk management and advisory services. Corporate and Investment Banking delivers this comprehensive range of products and services relating to: investment banking; global markets; and global transactional products and services.

  Stanbic Bank’s corporate and investment banking expertise is focused on industry sectors that are most relevant to emerging markets. It has strong offerings in mining and metals; oil, gas and renewables; power and infrastructure; agribusiness; telecommunications and media; and financial institutions.

  Stanbic Bank Tanzania’s personal and business banking unit offers banking and other financial services to individuals and small-to-medium enterprises. This unit serves the increasing need among Tanzania’s small business and individual customers for banking products that can meet their shifting expectations and growing wealth.

  0 0

  Naomba tuipigie kura Short filamu ya MIKONO SALAMA, Inayowakilisha Tanzania kwenye Shindano la Galway African Film Festival, Ipigie kura kushinda tuzo ya Filamu Bora. 

  Kura yako Moja ni muhimu kwa ushindi, Hii ni kwa ajili ya Uzalendo na Ushindi Kwa Nchi
  Vote, Repost, share kisha Sambaza kwa wingi iwezekanavyo.

  BOFYA LINK HIYO KUIPIGIA KURA FILAMU HIYO.

  Kwa njia Rahisi ya kupiga kura angalia hapo chini.

  IANGALIE FILAMU HIYO HAPA

  0 0

   Mwnyekiti wa TLP, Agustin Mrema akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wananchi wa Zanzibar kudumisha umoja wao na kuachana na kufuata kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochochea vurugu leo jijini Dar es Salaam.
  Mwnyekiti wa TLP, Agustin Mrema akitoka ukumbi wa mikuutano marabadaa ya kumaliza mkutano huu ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  CHAMA cha Tanzania Labour Party (TLP) kimetaka wananchi wa Zanzibar kudumisha umoja wao na kuachana na kufuata kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochochea vurugu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TLP, Agustin Mrema amesema kuwa kauli za viongozi wa siasa visiwani humo zinachochea kuvuruga amani  hivyo wanatakiwa kupuuza.

  Amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea kuvuruga waangaliwe kama wahaini na hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.

  Mrema amesema kuwa hata nchi wahisani waache kuingilia mambo yetu ya ndani kutokana wao hawaishi huku na hata mauaji yakitokea hawaguswi kwa lolote.

  Aidha amesema kuwa amani ikivurugika Zanzibar hata Tanzania bara haiwezi kuwa salama hivyo kauli za kuvuruga amani lazima ziangaliwe katika kulinda masilahi ya wananchi wa pande zote mbili.

  Mrema amesema viongozi wachukue hatua dhidi ya watu wanaochochea vurugu za kisiasa kwa masilahi yao binafsi ya kutaka kuchukua madaraka nguvu kwa kuwaandamanisha wananchi.

  Hata hivyo amesema kuwa Zanzibar ina historia ya mwaka 2001 ya kuuawa watu kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazima kwa sasa suala la uchochezi liangaliwe macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo.

  Amesema mahakama ya ICC haingalii viongozi wa serikali na hata viongozi wa kisiasa ambao kwa namna moja wanakuwa wamehusika katika kusababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto

  BENKI ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kifedha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa Takwimu Rasmi nchini.

  Akizungumza leo alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms. Bella Bird amesema kutokana na umuhimu wa takwimu katika kupanga na kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo, Benki ya Dunia itaendelea kuisaidia NBS ili iendelee kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu kwa wakati.

  “Ili Ofisi ya Taifa ya Takwimu iweze kutoa takwimu kwa wakati, inahitaji kuwekeza katika matumizi ya technolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa takwimu, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kifedha ili kufikia malengo yaliyoainishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya utoaji wa takwimu rasmi nchini”, amesema Ms. Bella Bird.

  Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa takwimu katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kupanga sera na kutekeleza miradi mbalimbali ya nchi husika.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo imeongeza tija katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi nchini.

  “Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kupitia ujio wako kuitembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hii ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi hapa nchini,” amesema Dkt. Chuwa.

  Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu nchini ikilinganishwa na karne zilizopita.Benki ya Dunia inaisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwezi Juni, 2018.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake) alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake), Menejimenti ya NBS na wageni walioambatana na Mkurugenzi Mkazi huyo alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam. ( PICHA NA EMMANUEL GHULA)Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Abina Chuwa akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird (kushoto) alipotembelea leo Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0


  RATIBA

  Ijumaa, 27 Mei 2016

  04:00 Asubuhi  – Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani kwa marehemu Tegeta.

  04:15 – 05:30 Asubuhi;  Nyimbo za maombolezo na sala.

  05:30 – 06.30 mchana; Chakula.
  00;30 – 07:00 mchana;  Safari ya kauelekea Kanisani.

  07:00 – 08:00 mchana; Ibada kanisa Katoliki Mt. Yohanne Mtume na
  Muinjili, Tegeta – Chanika (karibu na Kibo Complex).

  08:00 – 08:45 mchana;  Heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu. (Kanisani).
  09:00 – 10:00 jioni; Safari ya kuelekea makaburi ya Kinondoni.
  10:00 - 11:00 jioni;  Maziko, makaburi ya Kinondoni.


  Bwana ametoa, Bwana Ametwaa, 
  Jina la Bwana lihimidiwe.
  Amen

  0 0

  MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) utaanzisha huduma mpya itakayojulikana kama Mama na Mwana Afya Kadi ili kuboresha huduma za bima ya afya kwa kundi hilo ambalo lipo katika uhitaji maalum.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Kilimanjaro na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bernard Konga alipokuwa akitoa salamu za Mfuko huo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko linaloanza kikao chake mjini hapo.

  Konga amesema lengo la huduma hiyo mpya ni kuwawezesha kina Mama Wajawazito na Watoto kupata huduma za matibabu za uhakika zitolewazo na mfuko wa taifa wa Bima ya afya.

  Chimbuko la hatua hiyo linafuatia matokeo mazuri na mafanikio makubwa ya mradi unaoendeshwa kwa pamoja kati ya NHIF na benki ya maendeleo ya ujerumani ya KfW katika mikoa ya Tanga na Mbeya, hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kupata maoni ya wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha wa 2016/17.

  Awali, akifungua kikao cha baraza hilo, mkuu wa wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa, aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki, aliushukuru mfuko huo kwa kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma kwa makundi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wao wa kulipa. Ameutaka mfuko huo kutafsiri hotuba za mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya afya bora kwa wote kwa kuweka mikakati katika eneo hilo.

  Dr Mlingwa pia amesema wilaya ya Siha ni moja ya wilaya zilizofanikiwa sana kuboresha huduma za matibabu ambapo kwa miaka miwili mfululizo imeweza kupunguza sana vifo wa watoto wachanga na kufikia mtoto mmoja kwa kila watoto laki moja.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga, akizungumza wakati akitoa salamu za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko huo lilikofanyika katika ukumbi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaohudhuria.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Bernard Konga,(katikati) akizungumza na baadhi ya wajumbe ndugu Gudluck Kirambe, kulia na meneja wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fidelis Stephen.

  0 0

  President’s Manufacturer of the year (PMAYA) Awards scheduled to be held on May 31, 2016 at the Serena Hotel Dar es salaam which will be graced by HE John Pombe Magufuli, President of the United Republic of Tanzania as the chief guest. Bank M Tanzania plc is the main sponsor of this year’s event.

  Speaking to the press yesterday, The Confederation of Tanzania Industries (CTI) Executive Director Mr. Leodgar said “PMAYA aims to recognize and appreciate the industrial sector’s important role in Tanzania’s economic development process. For the past eleven consecutive years, CTI has been staging this most prestigious members’ event covering all sectors of production and services.

  The main objective of these awards includes recognizing the pertinent role of the industrial sector’s contribution to the national economy, to encourage and motivate investors in the industrial sector, to publicize the importance of the industrial sector in the country, raising the standard of business practices and promote sound corporate governance in the country etc.” Also Tenga thanked Bank M for coming on board to support the awards this year as the main sponsors.

  Bank M’s CEO (Designate) Ms. Jacqueline Woiso said that the PMAYA competition is one avenue that challenges corporate companies to improve on quality of products and services to the public. “Bank M we are proud to support the local manufacturing industry not only financially and in banking services but also through this prestigious competition.” said Ms. Woiso.

  The President’s Manufacturer of the year Awards is an annual event that is organized by the Confederation of Tanzania Industries (CTI) to award the outstanding manufacturers of the preceding year. The competition climaxes with the Annual Business luncheon where winners will be awarded their trophies by the President. The president is also a patron of CTI.

  Regarding this year’s preparations, the CTI Director of Policy and Advocacy Mr. Hussein Kamote assured the press that all the arrangements are going well and all the requirements are in place, “we are ready for the event”, attributed Mr. Kamote.

  The awards introduced in 2005 with the aim of recognizing and appreciating the manufacturing sector’s important role in Tanzania’s economic development process.

  The Awards are given to companies in small, medium and large manufacturer categories that exhibit a high degree of economic impact. This year’s event will gather Tanzania’s most prominent business leaders, corporate executives, industrialists and professionals, about 300 guests from the private sector and government institutions will attend.
  Bank M’s CEO-Designate Jacqueline Woiso giving a brief to the press yesterday in Dsm regarding the Bank in partnership with the Confederation of Tanzania Industries (CTI) in conducting this year’s Presidential Manufacturer of the year ward (PMAYA) which will be held next week in DSM, the event will be graced by the President of Tanzania HE John Pombe Magufuli. She is flanked by the CTI Executive Director Leodegar Tenga (Left) and Serena Hotel Director for Sales and Marketing Seraphin Lusala.
  " The Confederation of Tanzania Industries (CTI) Executive Director Leodegar Tenga giving a brief to the press yesterday in Dsm regarding CIT partnership with Bank M in conducting this year’s Presidential Manufacturer of the year ward (PMAYA) which will be held next week in DSM, the event will be graced by the President of Tanzania HE John Pombe Magufuli. He is flanked by the Bank M’s CEO-Designate Ms.Jacqueline Woiso." 

  0 0

  Sehemu ya Watendaji wakuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wao, Francis Senguji (wa pili kushoto) wakiwa katika tafrija ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
   Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
   Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Francis Senguji akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Furaha Samalu.
   Burudani ya Ngoma za Kiafrika ikitolewa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizugumza na wadau mbalimbali wa sanaa katika hafla ya uzinduzi wa siku ya msanii, leo jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu ameiagiza BASATA kuangalie namna bora na kuhakikisha maazimisho ya siku ya Msanii yanaadhimishwa nchi nzima na kwa mafanikio makubwa, pia amesema Makampuni na mashirika mengi yamekuwa yakiwatumia wasanii kwenye kazi zao mbalimbali ni vyema wajitokeze pia kwenye kudhamini maazimisho ya siku ya Msanii na kuzienzi kazi zao.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza akimkaribusha mgeni rasimi katika uzinduzi huo wa siku ya msanii leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau mbalimbali wa sanaa waliofika katika uzinduzi wa siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francoise leo jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 05/26/16--23:05: TASAF KUWANUSURU WAHADZABE
 • Mfuko wa Maendeleo ya jamii –TASAF-umeanza mkakati maalumu utakaowezesha jamii ya Wahadzabe walioko katika mikoa ya Arusha,Manyara na Singida kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na mfuko huo nchini kote.

  Wakizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unavyotekelezwa katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha,viongozi wa TASAF walioambatana na wadau wa maendeleo walioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchi za Tanzania Bi.Bella Bird,na baadhi ya maafisa wa benki hiyo kutoka Marekani ,baadhi ya wahadzabe waliomba kuorodheshwa katika Mpango huo ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo kupitia utaratibu wa kuhawilisha fedha.

  “ baadhi ya wananchi wenzetu wameandikishwa kwenye mpango huku wengi wetu hatujapata fursa hiyo na tumeanza kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo’’ alisisitiza mmoja wa wahadzabe katika kijiji cha Endamaghan umbali wa kilometa 70 kutoka makao makuu ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

  Akizungumza baada ya kutembelea makazi ya wahadzabe Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- kwa kuweza kuwafikia wananchi ambao wanakabiliwa na umaskini nchini kote.

  ‘’Benki ya Dunia inatambua na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kukabili tatizo la umaskini miongoni mwa wananchi wake,umuhimu mkubwa pia unapaswa kuwekwa katika kunusuru jamii za watu walioko katika mazingira magumu wakiwemo wahadzabe” alisisitiza Bi. Bird.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-Bwana Ladsilaus Mwamanga alisema zoezi la kutambua na kuziandikisha kaya maskini katika jamii ya Wahadzabe lilifanyika. Hata hivyo alisema zoezi hilo liliathiriwa kwa kiwango kikubwa na mfumo wa maisha ya jamii hiyo wa kuhamahama kutafuta chakula kwa kuwinda wanyama na kuokota matunda na asali.

  “Hatukuweza kuwaandikisha wote ingawa kimsingi wanastahili kuingizwa kwenye Mpango,hii ilitokana na kuhamahama kwa wananchi hao kujitafutia chakula hususani matunda, asali na mizizi” alisisitiza Bwana mwamanga.

  Hata Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa kazi ya kuziandikisha kaya za walengwa katika jamii hiyo ya wahadzabe na nyingine zenye maisha ya kuhamahama itafanyika upya na kwa haraka ili waweze kuziingiza kwenye Mpango wa Kunusuru na Kaya Maskini unaotia mkazo katika kuboresha maisha ya walengwa hususani kupitia sekta za elimu, afya,lishe na kukuza kipato kwa kaya za walengwa.

  Zifuatazo ni picha za ziara ya viongozi wa TASAF na Wadau wa Maendeleo katika maeneo ya wahadzabe,wilayani Karatu Mkoani Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa Kaunda suti) akiwasikiliza baadhi ya wananwake wa jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha Endaghan wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na TASAF kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .
  Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird ( hayupo pichani) alipotembelea kijiji cha Endamaghan kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akiwahutubia wakazi wa Endamaghan katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha juu ya utekelezaji wa Mpango 
  Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Endamaghan kutoka jamii ya Wahadzabe akipokea fedha za ruzuku kupitia mpango huo.
  Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji cha Endamaghan wakiwemo jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani) juu ya utekelezaji wa Mpango huo.
   

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Fiji zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kudiplomasia katika ngazi ya Mabalozi.

  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, na Mwakilishi wa Kudumu wa Fiji katika Umoja wa Mataifa Balozi Peter Thomson ndio waliotia sahihi hati za kuanzishwa kwa uhusiano huo kwa niaba ya serikali zao katika hafla fupi iliyofanyika siku ya Alhamisi katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania.

  Fiji inakuwa nchi ya tatu baada ya Malta na Equador ambazo tayari zimekwisha anzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania katika ngazi ya Mabalozi. Kama ilivyokuwa kwa nchi hizo mbili hati za makubaliano hayo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  Wakizungumza mara baada ya kubadilishana hati , wawakilishi hao pamoja na kuonyesha kufurahishwa na uhusiano huo, pia walielezea namna gani wanavyoweza kukuza ushirikiano katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande hizo mbili hapa Umoja wa Mataifa na nje ya Umoja wa Mataifa.

  “ Ni kwa muda mrefu serikali yangu ( Fiji ) imekuwa ikitamani sana kuwa na uhusiano wa Tanzania, labda pengine niongeze kwamba sisi wananchi wa Fiji baadhi ya vizazi vyetu asili yake ni Tanganyika ( Tanzania) kwa hiyo uhusiano huu utaimarisha zaidi siyo tu kutambua na kuthamini kule tulikotoka, lakini pia tunayo mambo ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu kwa manufaa ya nchi zetu na watu wake”. Akasema Balozi.

  Kwa upande wake, Balozi Tuvako Manongi amemwambia Balozi Thomson kwamba, nchi hizo mbili zimefungua ukurasa mpya. Na akaongeza . “ nimewahi kutembelea Fiji, ingawa ilikuwa ni kwa muda mfupi lakini niliweza kujionea nakujifunza kilimo cha kisasa na endelevu na pia zao la nazi ambalo hata kwetu ( Tanzania) ni moja ya zao muhimu sana, kwa niyo ninaamini kwamba kwa kuanzisha uhusiano huu tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwetu.”

  Jamhuri ya Fiji ni Kisiwa kilichoko katika Bahari ya Pacific ya Kusini ( South Pacific Ocean) na lilikuwa koloni la Uingereza kabla ya kujipatia uhuru wake mwaka 1970. Uchumi wa nchi hiyo pamoja na mambo mengine, unaendeshwa kwa kiasi kikubwa na sekta za utalii, madini, bidhaa za misitu, uzalishaji wa sukari, mazao yatokanayo na nazi, pamoja na viwanda vidogo vya pamba na pia Fiji inatengeneza nguo…..
  Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Fji katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Peter Thomson, wakitia sahihi Hati za kuanzisha Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Nchi hizo Mbili katika nganzi ya Mabalozi. Hafla hiyo fupi ilifanyika siku ya Alhamisi katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania. Kushoto kwa Balozi Manongi ni Afisa wa Uwakilishi Bi, Tully Mwaipopo akimwelekeza Balozi sehemu ya kuweka sahihi yake.
  Balozi Tuvako Manongi na Balozti Peter Thomson wakipongezana mara baada ya kubadilishana hati za kuanzishwa kwa ushirikiano wa kidiplomasia katika ngazi ya Mabalozi. Hati hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
  "Unajua baadhi ya raia wa Fiji walitoka Tanganyika, kwa hiyo hii ni hatua muhimu sana kwetu ya kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania" hiyo ilikuwa ni kauli ya Balozi Thomson akimweleza Balozi Manongi na kuwafanya waangue kicheko cha furaha.

older | 1 | .... | 1233 | 1234 | (Page 1235) | 1236 | 1237 | .... | 3270 | newer