Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1232 | 1233 | (Page 1234) | 1235 | 1236 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Baadhi ya Wafanyakazi wa  MultiChoice-Tanzania wakiwa katika vazi la kiafrika siku ya kuazimisha Africa day.

  Jinsi Chaneli za TV za Barani Afrika zilivyofanikiwa kuelezea habari za Afrika katika mtazamo wa Kiafrika. 

  Haukasiriki unapoangalia onyesho katika televisheni au filamu ya kutoka Afrika au kumhusu muafrika na kisha ukatahamaki, “ Hii haina chochote kinachofanana na Afrika ninayoijua?”. Kwa miongo kadhaa, tasnia ya burudani ya filamu na televisheni imetawaliwa na simulizi zenye maudhui ya nchi za Magharibi- hata pale zinapokuwa za kutoka Afrika na kwa ajili ya Waafrika. Kwa bahati nzuri, ndani ya miaka kadhaa iliyopita, tumeona mabadiliko japo ya taratibu lakini ya uhakika, ya simulizi zenye uhalisia kuhusu Waafrika zikisimuliwa kuhusu bara letu.

  MultiChoice tunajisikia fahari kutokana na ushiriki wetu katika mabadiliko na maendeleo haya tangu kuanzishwa kwetu barani Afrika miaka 20 iliyopita. Mojawapo ya malengo yetu ya msingi ni pamoja na kuhakikisha kwamba huduma zetu zinawaendeleza wateja wetu kwa kuwaletea maudhui ambayo wanaweza kuyahusisha nayo na maisha yao ya kila siku. 

  Lengo hili linatukumbusha dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono na kuendelea kuwekeza katika tasnia ya burudani barani Afrika na kuonyesha vipaji vya waafrika kupitia chaneli za hapa barani Afrika za MNet. Kutoka Nollywood mpaka Riverwood, tunaamini katika kusimulia na kuelezea habari au simulizi za Ki-Afrika ambazo watazamaji wetu wanaweza kuzihusisha nazo na maisha yao ya kila siku. Siku ya Afrika inapokaribia tarehe 25 May mwezi huu, tunasheherekea wasimulizi mbalimbali kutoka Afrika ambao wanachangia katika ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni ya Afrika.

  Watazamaji wetu wametuamini kuwa waangalizi na wahifadhi wa simulizi za kiafrika na kuhakikisha panakuwa na simulizi zenye uwiano kuhusu Afrika. Kimsingi hakuna simulizi moja ambayo inafafanua au kuelezea kila kitu kuhusu bara letu na ndio maana chaneli zetu za zinazolenga bara la Afrika ambazo zinajumuisha Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East (E36) na Zambezi Magic, Mzansi Music na Mzansi Bioskop- zimeahidi na kujizatiti katika kuelezea simulizi za Afrika kama zilivyo. Chaneli hizi zinaleta mtazamo tofauti kuhusu maisha ya Afrika ambayo watazamaji wake wanaweza kuyahusisha na maisha yao ya kila siku.


  0 0

  · Music Superstar AliKiba and well-known food personality Marion Elias joined Jamie Oliver’s Food Revolution with a live cooking demonstration on Facebook on Friday 20th May

  · 9 per cent of boys and 12 per cent of girls under the age of 20 in Tanzania are classed as overweight and obese in 2013*

  Tanzania saw the launch of Food Revolution Day on Friday, 20th May 2016 amidst a fanfare of celebrities, live cooking events, a flurry of social media activity and, of course, the British celebrity chef and campaigner Jamie Oliver, who launched the campaign. Jamie and his army of revolutionaries staged a series of live events on Facebook to encourage governments at the World Health Assembly meeting in Geneva on 23rd May to tackle the child nutrition crisis.

  Now in its fifth year, highlights included chefs and celebrities streaming live on Facebook on 20th May during a seven-hour cooking marathon, calling for people around the world to sign up to the Food Revolution. In India the campaign’s Global Champions - music superstar AliKiba and well-known food personality Marion Elias - were the hosts of the live event on Facebook which took place in Mbuyuni Primary School, Oysterbay.  
  Food Revolution Day, which is saw Jamie joined by a host of well known chefs and personalities, all of whom carried out Facebook Live broadcasts from the around the world to help make history. Some of the notable names included: Jacqueline Fernandez and Chef Kunal Kapur (Mumbai, India); Chef Gennaro, Chef Clodagh McKenna, Charlotte Crosby, Alfie Deyes, Tanya Burr and Jim Chapman (London); Kris Jenner, Wolfgang Puck and Cody Simpson (L.A. USA); Chef Donna Hay (Sydney, Australia); Chef Ali and Juliani (Nairobi, Kenya); Chef Tim Malzer, Chef Steffen Henssler and Janina Uhse (Hamburg, Germany); Chef Ana Luiza Trajano and Chef David Hertz with guests Marina Person and Felipe Solari (Sao Paulo, Brazil); cookery personality Marion Elias and AliKiba (Dar-es-Salaam, Tanzania); Chef Eros and Waje (Lagos, Nigeria); Chef Lynn Crawford (Toronto, Canada); and Bart Van Olphen and Miljuschka Witzenhausen (Netherlands).
  Food Revolution Day was also supported on social media by Coldplay, James Corden, Kate Hudson, Nicole Scherzinger, Rio Ferdinand, Paloma Faith, Niall, Zoella, Jim, Tanya, Louis, Pixi Woos, Haste Kicthen, Olly Murs, Ronan Keating, Marlon Roudette, Cascada, Cornelia Pletto, Palina Rojinski, Holger Stromberg, Chris Mears, Naomie Harris, Jake Paul, Emmanuelle Chriqui and Keltie Knight.

  As part of Food Revolution Day, Jamie also took an International Omelette Challenge global to get people, young and old, experiencing first-hand how super-quick, easy and delicious healthy grub can be wherever you are, and encourage more noise on social media for the Food Revolution. 
   

  0 0

  Kamera ya Globu ya Jamii katika pita pita zake, imebahatika kuinasa taswira hii ya Mdau akijipiga sop sop katika maji yaliyotuama katikati ya Barabara ya Kidogo, Jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi. sina hakika kama kujipiga huku sop sop kunahusiana na uhaba wa Maji mjini.Picha na Othman Michuzi -MMG.
  Hapa inaelekea akimaliza tu, anaingia zake mzigoni kusaka chochote cha kujikimu kimaisha


  0 0  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

   Waimbaji wa Nyimbo za Injili nchini wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kujitolea ikiwa kama sehemu ya ibada ya kumtumikia Mungu kwa kulitangaza neno lake na si kugeuza kazi hiyo kuwa mtaji wa biashara.

  Hayo yamesemwa na Mwalimu wa kwaya ya Wateule Elikana Simatiya kutoka kanisa la Anglikani, St. James lililoko Tabata Segera jiijini Dar es Salaam, maarufu kama  kunyata nyata  jina lililotokana na nyimbo ya kunyata nyata aliyoifundisha akiwa kwaya ya Mennonite. 

  “Waimbaji wengi wa nyimbo za injili wameacha kutumikia Mungu na badala yake   wamekuwa wakiuunda vikundi binafsi vya uimbaji ambavyo hutumika kama vyanzo vya fedha na hualikwa kwenye mikutano ya injili na sherehe mbalimbali kwa malipo maalum,” alisema Simatiya.

  Aidha ameeleza kuwa, uimbaji wa nyimbo za injili ni wito kama ulivyo wito wa uchungaji lakini hivi sasa muimbaji wa injili akialikwa katika mikutano ya injili au sherehe huomba malipo hadi ya shilingi milioni moja.

  Simatiya aliongeza kuwa, ziko gharama ambazo muimbaji anaweza kuomba kupewa kama usafiri kwa ajili ya kumfikisha eneo husika au malazi na chakula ikiwa atahitajika kulala nje ya makazi yake, lakini waimbaji wa leo wamebadilisha wito wa kutangaza injili kwa njia ya uimbaji kuwa biashara.
  Hivyo mwalimu huyo amewataka waimbaji kubadilika kwa kuacha kuharibu kazi ya Mungu na kufanya kazi hiyo kwa kujitolea kwani wapo wanaopokea uponyaji na wanaotiwa moyo kupitia nyimbo za injili.

  Kwaya ya Wateule inatarajia kuzindua albamu mpya ijulikanayo kama Wateule tutakwenda siku ya Jumapili Mei 29, 2016 Tabata Segerea katika kanisa la St. James, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda,huku wakisindikizwa na  waimbaji wa injili ambao ni Ambwene Mwasongwe, Christina Shusho, Edson Mwasabwite pamoja na kwaya za Anglikan kutoka Vingunguti na Ukonga.

  0 0  Ipo kauli isemayo "Mfupa Uliomshinda Fisi" ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyaba bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.

  Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.

  Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.

  Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.

  Baadhi ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.

  Bonyeza HAPA Kwa Picha Zaidi.

  0 0


  · Ni katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

  WAKUU wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.

  Kauli hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.

  Wakishiriki kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.

  Akichangia mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.

  Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

   Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo, Theophil Makunga (kushoto) akimkaribisha Mohamed Omari wakati alipofika katika ofisi hiyo Dar es Salaam leo (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

   Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo linalomilikiwa na Kampuni ya Quality Media Group, Anicetus Mwesa (wa nne kushoto) akimkabidhi zawadi maalumu, wakala wa magazeti, Mohamed Omari baada ya kufanikiwa kuuza nakala nyingi zaidi kwa mwezi Aprili. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
  Mohamed Omari wa tatu kushoto na mwenzake Fikirini Shabani wa tatu kulia, wakiliangalia Gazeti la Jambo Leo mara  baada ya kuibuka mshindi kwa kuuza kopi nyingi kwa Mwezi wa Aprili 2016 .

  0 0

  TAWI la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) la Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA-HQ), limepata viongozi wake wapya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika jengo la Kiwanja cha Ndege cha Zamani (TBI).

  TAA ni wakala wa Serikali iliyoanzishwa tarehe 29 Novemba 1999 kwa Tangazo la Serikali Na.404 la mwaka 1999 chini ya kifungu cha 3 cha Sheria Na. 30 ya mwaka 1997 ya Wakala wa Serikali. Wakala hii ilirithi majukumu ya iliyokuwa Idara ya Viwanja vya Ndege (Directorate of Aerodromes) chini ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 3 Desemba 1999.

  Viongozi hao wamepatikana baada ya uliokuwepo kumaliza muda wao, na  waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango,  ni pamoja na Mwenyekiti Bw. Nasib Elias aliyezoa kura zote 28, baada ya kutokuwa na mpinzani, huku katibu mkuu akichaguliwa Bi. Aziza Kipande aliyepata kura 15 akimshinda Bi. Caroline Mntambo aliyepata kura 13.

  Wajumbe watatu ambao ni Bi. Mwanaisha Omari, Bw. Joel Mwakamele na Bi. Frida Omari walipitishwa bila kupingwa na wajumbe waliotoka idara mbalimbali za TAA HQ.

  Naye Bi. Irene Sikumbili alipata kura zote 14 za wanawake na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Katibu Mkuu wake ni Bi. Mwanahawa Mdee aliyepata kura 11 akimshinda Bi. Kipande aliyepata kura tatu.

  Walioshinda katika nafasi  ya ujumbe katika kamati hiyo ni Bi. Glory Mollel na Bi. Pendo Pascal; wakati Bi. Mntambo ameukwaa uweka hazina na Bi. Magreth Mushi ni mwakilishi wa vijana, huku hakukuwa na mwakilishi wa walemavu kutokana na kutokuwa na mlemavu. 

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA
   SHERIA NA MAHUSIANO TAA

  0 0
  0 0


  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee na Viongozi wa Serikali, wakati akiondoka Zanzibar kuelekea Nchini Comoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteuli wa Muungano wa Visiwa vha Comoro akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangana na Viongozi wa Serikali, waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kumuaga akielekea Nchini Conoro kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteule wac Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe.Azali Assouman Boinakher
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assouman Boinakher. akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Ikulu, Zanzibar

  0 0


  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (pichani) amesema ujangili nchini hufanyika katika ngazi tano ukiwahusisha baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi na watumishi wasio waaminifu.
  Ngazi nyingine ni wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja na kuua wanyama, wasafirishaji na madalali; wawezeshaji kwenye ngazi ya nchi zinakonunuliwa nyara na wasambaza silaha ambao ni kiungo kati ya majangili nguli na watakatishaji fedha. Ngazi ya mwisho ni majangili nguli wa kimataifa.
  Profesa Maghembe ambaye alitaja ngazi hizo jana bungeni alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17, alisema kutokana na hali hiyo, wizara imeimarisha kitengo chake cha intelijensia na kufanya doria kwa kuzingatia mfumo wa makundi hayo.

  Alisema kesi 161 zilimalizika kwa wahalifu 53 kuhukumiwa kifungo cha jumla ya miezi 6,360 na Sh363.9 milioni kulipwa kama faini.
  “Kati ya wahalifu waliohukumiwa, wanane ni majangili nguli wenye mitandao ya kimataifa,” alisema Profesa Maghembe.
  Alisema katika doria zilizofanyika, nyara mbalimbali za Serikali zilikamatwa ambazo ni pamoja na mijusi 315, kobe 202, tumbili 81 na nyani mmoja.
  Profesa Maghembe alisema vipande 253 vya meno ghafi ya tembo vyenye uzito wa kilo 634 na vipande 34 vya meno ya tembo yaliyochakatwa vyenye kilo mbili, vilikamatwa.
  “Vilevile, kilo 10,096 za nyamapori ya wanyama aina mbalimbali na ngozi 39 za wanyamapori zilikamatwa. Pia, bunduki 85 na risasi 1,235 za aina tofauti zilikamatwa,” alisema.
  Majangili watajwe
  Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mhe. Catherine Magige alisema haiwezekani Serikali na Bunge wakawa wanapambana na ujangili huku baadhi ya wabunge wakidaiwa kuhusika.
  Magige alitaka Bunge lifanye uchunguzi na kujua wabunge majangili ni kina nani ili waweze kutajwa kwa kuwa tembo wanakaribia kuisha nchini.
  “Hakuna mbunge ambaye yuko juu ya sheria, hivyo watajwe kwa kuwa haiwezekani tunapambana na ujangili halafu kumbe wengine wapo humuhumu,” alisema Magige.
  Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa wizara hiyo, Esther Matiko alisema suala la ujangili nchini limekuwa ni tishio kwa wanyama na hata binadamu wanaofanya shughuli ndani ya hifadhi.
  “Ujangili nchini umeiletea nchi sifa mbaya kimataifa. Serikali hii yenye falsafa ya kutumbua majipu lazima sasa ijielekeze katika kuwatumbua wale wote wanaohusika katika kukwamisha kesi za ujangili ili zisimalizike kwa wakati,” alisema Matiko.

  0 0
 • 05/25/16--20:21: Article 18


 • 0 0


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Be.Sabasaba Moshingi,(kushoto), akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam  Mei 25, 2016. 
  Wajumbe walipokea taarifa ya uendeshaji Benki hiyo kwa mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na mipango ya uendeshaji wa Benki kwa mwaka huu wa 2016. 
  Pamoja na mambo mengine, Bw.Moshingi alisema benki inampango wa kuingia kwenye soko la his a(Dar es salaam stock exchange), sambamba na kuongeza Huduma za ATM kwenye matawi yake mbalimbali kote nchini. Katikati no Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, na kulia in Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki hiyo, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.
  Wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupokea taarifa ya mahesabu ya fedha iliyosomwa na Meneja wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Nexia SJ Tanzania, Bw.Fulgensio Mgaya, ambaye alisema mahesabu ya Benki hiyo hayakukutwa na dosari, wajumbe wa mkutano huo, Bi.Theresia A Chitumbi na Bw. James Sando, wameupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa usimamizi thabiti na uendeshaji mzuri wa Benki. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Hamisi Mussa Omar. 
   Wakurugenzi wa idara mbalimbali za TPB, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi ameshukuru AZAM TV kuwa kituo cha kwanza cha Habari hapa nchini kuchukua jukumu la kushirikiana na mamlaka hiyo ili kutimiza viwango vya mamlaka ya hali ya hewa duniani katika kutangaza taarifa za hali ya hewa. Dokta Kijazi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya wiki tatu ya kutangaza Taarifa za hali ya hewa kwa watangazaji wapya wa habari ya hali ya hewa ambazo huandaliwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini.
  Mafunzo ya hali ya hewa kwa jamii kwa wanahabari wa Azam yamefanyika kwa kuandaliwa na TMA na WMO, lengo ni kuimarisha uhusiano kati ya mtoa huduma na jamii kupitia vyombo vya habari.
  Wanahabari wa Azam walipata wasaa wa kujifunza namna ya kurekodi na kutangaza utabiri wa hali ya hewa ili kuweza kuboresha vipindi vyao vya kwa jamii hususan kipindi cha habari.katika picha hapo wakatikati mbele ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi.

  Pichani kutoka kulia ni mkuu wa chuo cha hali ya hewa Kigoma Joseph Aliba, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnes Kijazi, Samuel Muchemi (mwakilishi kutoka mamlaka ya hali ya hewa Duniani),   Mwanga Kirahi Mkurugenzi wa mafunzo Azam TV nyuma yao ni watangazaji wapya wa habari za hali ya hewa. Kutoka kushoto ni Mohamed Mohamed, Jamaly Hashim, Fatuma Mohamed, Sophia Kilumanga, Halima Shebuge, Rajabu Mbogo na Nuru Mbura.

  0 0


  Mr. Moustafa Khataw

  0 0


  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1232 | 1233 | (Page 1234) | 1235 | 1236 | .... | 3278 | newer