Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1231 | 1232 | (Page 1233) | 1234 | 1235 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

   Mgeni rasmi wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania, lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa huo,John Mongella(watatu kushoto) Mkurugenzi wa Usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kushoto)pamoja na Meneja wa duka hilo,Yohana Mswahili wakifafanuliwa jambo na Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen(kulia) wakati wa uzinduzi wa duka hilo jana.
    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella(watano kushoto) akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Ikiwa ni ishara ya Uzindua wa duka jipya la kisasa la kampuni hiyo lililopo katika sehemu ya maduka makubwa(Rocky City Mall)jijini humo jana.

  0 0

  Peace and Blessing of Allah be with you,

  Alhamdulillah, we are set for another Ramadhan with another Welcoming Ramadhan Conference 1437H.

  Kalamu Education Foundation (KEF) again bringing to you the 8th Welcoming Ramadhan Conferences 1437H - 2016 with the main Theme: “The Role of Family in transforming Community Morals and ethics” ( Familia, kiini cha  Mabadiliko kwa Jamii) the event will be hosted at  Julius Nyerere International Conference Center (JNICC)- Dar es salaam on starting at 08:30am to 04:30pm.

  The Conference is expected to bring together Over 1000 Practitioners, Scholars and Experts to discuss and share their knowledge and experience on the Islamic principles, instruments and issues related to degradation of community morality and how strong family values can transform our ethics in today's world. 

  With the Guest Speaker: Imam Qasim Ibn Ali Khan (U.S.A) will lead the presentations to inspire the fruitful discussion with other Muslim Scholars.
  The participation contribution is TZS 30,000 per person (Lunch and Other Goodies Inclusive)

  Days are numbered Book your Sit NOW,

  Kindly call: 0786 663 666 OR 0763 509 159

  0 0

   Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame  kwenye  Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya  Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
    Baadhi ya Watanzania  waishio Zambia wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa wakatia lipozungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka.  Majaliwa  alikwenda Zambia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye  mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Zambia kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Lusaka Mei 24, 2016. Majaliwa alikwenda Zambia kumwakilisha  Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi. 
   (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  TAWI la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) la Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA-HQ), limepata viongozi wake wapya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Transit uliopo katika jengo la Kiwanja cha Ndege cha Zamani (TBI).

  TAA ni wakala wa Serikali iliyoanzishwa tarehe 29 Novemba 1999 kwa Tangazo la Serikali Na.404 la mwaka 1999 chini ya kifungu cha 3 cha Sheria Na. 30 ya mwaka 1997 ya Wakala wa Serikali. Wakala hii ilirithi majukumu ya iliyokuwa Idara ya Viwanja vya Ndege (Directorate of Aerodromes) chini ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 3 Desemba 1999.

  Viongozi hao wamepatikana baada ya uliokuwepo kumaliza muda wao, na waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango, ni pamoja na Mwenyekiti Bw. Nasib Elias aliyezoa kura zote 28, baada ya kutokuwa na mpinzani, huku katibu mkuu akichaguliwa Bi. Aziza Kipande aliyepata kura 15 akimshinda Bi. Caroline Mntambo aliyepata kura 13.

  Wajumbe watatu ambao ni Bi. Mwanaisha Omari, Bw. Joel Mwakamele na Bi. Frida Omari walipitishwa bila kupingwa na wajumbe waliotoka idara mbalimbali za TAA HQ.

  Naye Bi. Irene Sikumbili alipata kura zote 14 za wanawake na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Katibu Mkuu wake ni Bi. Mwanahawa Mdee aliyepata kura 11 akimshinda Bi. Kipande aliyepata kura tatu.

  Walioshinda katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo ni Bi. Glory Mollel na Bi. Pendo Pascal; wakati Bi. Mntambo ameukwaa uweka hazina na Bi. Magreth Mushi ni mwakilishi wa vijana, huku hakukuwa na mwakilishi wa walemavu kutokana na kutokuwa na mlemavu.

  Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Bw. Abdi Mkwizu alipata nafasi ya kuwapongeza viongozi wateule wa TUGHE na kuwaahidi ushirikiano mzuri kutoka upande wa mwajiri.

  Katika kutoa neno la shukrani kwa wajumbe, Mwenyekiti Bw. Elias aliwashukuru wajumbe wote kwa kuonesha imani yao ya dhati kwake na kuwaahidi kuendeleza mshikamano na mahusiano mema yaliyojengwa na uongozi uliomaliza muda wake baina ya wafanyakazi na mwajiri, lakini pia baina ya wafanyakazi wenyewe.

  Bw. Elias pia ameahidi kuhakikisha wafanyakazi ambao si wanachama wa TUGHE wanajiunga na chama hiki kwani kina manufaa makubwa kwao yakiwemo ya kutetewa pindi mfanyakazi anapokuwa kwenye matatizo na mwajiri wake .

  Naye msimamizi, Bw. Kadyango ambaye aliukabidhi uongozi mpya katiba, aliwashukuru wajumbe wote kwa kumaliza zoezi la uchaguzi kwa amani na kusisitiza kuwa na ushirikiano mzuri na mwajiri, kudumisha uhusiano mwema kazini kati ya waajiri na waajiriwa, kudumisha uhusiano mwema baina ya wafanyakazi wao kwa wao, kusimamia uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi na hali bora za kazi, ili kufikia malengo.

  Viongozi wapya wa TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati), akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kulia ni Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule na Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite.
   Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule  akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati).
  Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite (kulia). akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Wengine ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (kushoto) na Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule.


  Na Mwandishi wetu.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Hedhi Salama Duniani ambayo hufanyika   Mei 28 kila mwaka.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga , Orsolina Tolage amesema kuwa suala hedhi salama wanaliangalia sana katika kuweza mazingira bora ya afya ya wasichana.

  Amesema kuwa Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kwa kushirikiana na wizara ya elimu na Sayansi na Teknolojia juu ya kuangalia watoto wa kike mashuleni wasiweze kukosa kusoma kutokana vifaa vya kumkinga katika hedhi.

  Nae Mratibu wa Maji , Afya na Usafi wa Mazingira Mashuleni wa izara ya elimu na Sayansi na TeknolojiaTheresia Kiuwela amesema kuwa wasichana wanakosa masomo kwa miezi miwili kutokana na hedhi hivyo ni lazima siku hizo zisipotee kwa msichana kukosa kusoma.

  Amesema kuwa wameweka utaratibu wa kupata tauro za kike (Ped) kwa sh.1000 ambapo baadhi ya wasichana hasa katika maeneo ya vijijini wanashindwa kukumdu gharama hizo.

  0 0


  MBUNGE wa Mafinga Mjini Mhe.  Cosato Chumi akizindua 
  gari la kubeba wagonjwa (ambulance) 

  Na fredy mgunda, Iringa

  MBUNGE wa Mafinga Mjini Mhe.  Cosato Chumi kwa kushirikiana na asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

  Gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye thamani ya Sh Milioni 40 lilikabidhiwa jana kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa hospitali hiyo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mashujaa, mjini Mafinga.

  Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na asasi hiyo ambayo mimi ni rafiki yao mkubwa. Uadilifu na uaminifu kwa taasisi hiyo umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

  Alisema  gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

  Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.

  Akishukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, hospitali hiyo ya wilaya ilikuwa na gari moja tu la kubeba wagonjwa.

  0 0


  0 0

  The Assembly late yesterday debated and hailed the Chairperson of the EAC Summit of Heads of State for the concise exposition of the EAC policy contained in the State of the EAC Address delivered to EALA at the March Session.

  At debate, Hon Shyrose Bhanji termed the speech as enlightening and said it had laid ground on a number of important matters in the integration agenda.  The Speech cited the implementation of the Customs Union as key but added that a number of agencies should be able to issue the certificate of origin so that accessibility is realised. 

   Hon Abubakar Zein reiterated that it was necessary for the region to contain corruption and remove bad governance in order to realise progress of the EAC.  Hon Mike Sebalu termed disasters as a matter that the region must collectively address. 
  Hon Shyrose Bhanji contributes to the debate in the House late yesterday

  “There is no soveregnity when it comes to matters concerning disasters”, he said.  Hon Mumbi Ngaru on her part termed sensitization as fundamental and said there was need for more adequate funding, a sentiment that was echoed by Hon Bernard Mulengani and Hon Frederic Ngenzebuhoro as well.   On her part, Hon Judith Pareno said that East Africans continued to face a number of challenges at the borders citing frequent stops by the authorities while Hon Dora Byamukama called for closer working relations between the Private Sector under the East African Business Council and the Assembly.

  The Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Rt Hon. Majaliwa, Kassim Majaliwa delivered the State of EAC Address on behalf of the President of the United Republic of Tanzania, and Chair of the Summit of EAC Heads of State, H.E. John Pombe Joseph Magufuli, at the commencement of the 5th Meeting of the 4th Session of the 3rd Assembly in Dar es Salaam, Tanzania on March 8th, 2016.

  The Speech, gave a score-card on a number of areas related to the pillars of integration.
   
  Hon Frederic Ngenzebuhoro addresses the Assembly.

  The Speech highlighted the adoption of the use of One Stop Business Posts (OSBPs) as a trade facilitation concept to minimize delays at the border posts and on the major corridors in the region. The House was informed that out of the 15 borders earmarked to operate as OSBPs, 7 had been completed and 4 others were operating as OSBPs using bilateral agreements.

  READ MORE HERE

  0 0

  KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam Mei 24, 2016 kujadili masuala mbalimbali.
   
  A; Tuzo za Wanamichezo Bora
   Kikao kilikubaliana Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA, safari hii zifanyike Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali. 
  TASWA imeuanda kamati maalum kwa ajili ya kusimamia upatikanaji wa wanamichezo hao bora, kamati ambayo inajumuisha waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wataalamu kutoka vyama mbalimbali vya michezo. Sekretarieti ya TASWA inaendelea kufanya mawasiliano na wateule wa kamati hiyo kabla ya kuwatangaza.
   
  Kwa kawaida kila mwaka TASWA inatoa tuzo kwa wanamichezo bora wa kila mchezo na pia kunakuwa na mwanamichezo bora wa jumla kwa mwaka husika. 
  Baadhi ya waliopata kutwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Tanzania wa jumla kwa miaka kumi iliyopia na miaka yao katika mabano ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wanariadha.
  Mwaka 2009 tuzo ilienda kwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan, ambaye pia alitwaa tuzo hiyo mwaka 2010, wakati mwaka 2011, ambapo tuzo yake ilitolewa mwaka 2012 mshindi alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe. Mwaka 2013/2014 ilienda kwa mwanasoka Sheridah Boniface. 
  Mwaka 2015 tuzo ilifanyika katika aina nyingine,  ambapo walizawadiwa wanamichezo 10 tu waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya urais wa Mhe. Jakaya Kikwete na pia TASWA ilitoa Tuzo ya Heshima kwa Mhe. Kikwete. 
  B; Media Day
  Kama inavyojulikana chama chetu kimekuwa kikiandaa bonanza maalum likihusisha waandishi na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, lakini kwa miaka miwili bonanza hilo limekwama kufanyika kutokana na sababu mbalimbali. Kikao kimekubaliana nguvu zaidi ielekezwe ili jambo hilo lifanyike na kuwapa raha wadau. Taarifa zaidi kuhusu Media Day itatolewa Jumamosi wiki hii. 
  C: Changamoto kwa waandishi 
  Kikao kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi wa habari za michezo na chama kwa ujumla, ambazo zimewekewa mikakati ya muda mfupi na mrefu na utekelezaji wake utaanza kuonekana siku chache zijazo.
   Ahsanteni,
   Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  25/05/2016

  0 0
 • 05/25/16--02:01: BEI YA MADAFU LEO.

 • 0 0

  Dada yetu wa mtaa leo akiwa katika harakati za akimwaga maji pembezoni mwa mtaro  akiwa na nia ya kumwaga maji machafu ambayo ameshayatumia kwa kusafisha vyombo vyake ila faida yetu ni kupunguza mavumbi katika kipindi hiki cha upepo mkali jijini Dar.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi, wakati Balozi Saud alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Mei 25,2016 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
  (Picha na OMR).

  0 0

   Meneja wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Yasini Silayo.
  Baadhi ya Waandishi wahabari wakifuatilia mkutano huo.
  Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.

  Frank Mvungi-Maelezo
  SHIRIKA la Umeme Tanzania limewataka wateja wake kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini Mhandisi Majige  Mabulla wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
  Majige amesema kuwa moto hauwezi  kutokea endapo mtumiaji wa umeme atahakikisha kuwa mfumo wa umeme katika nyumba yake umesukwa na fundi ama mkandarasi aliyesajiliwa.

  “Kuwa makini katika matumizi bora ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi,hita za umeme,kuchaji simu,kompyuta kutasaidia kupunguza au kuondoa tatizo la majanga ya moto” alisisitiza Mabulla.
  Akizungumzia hatua nyingine zinazoweza kusaidia kuzuia majanga ya moto Mhandisi  Majige ni kuepuka kuweka vitu vinavyoweza kushika moto kirahisi karibu na nyaya ama maungio ya nyaya za umeme ndani ya nyumba .

  Majige alitoa wito kwa watumiaji wa umeme kutoa taarifa pale wanapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa ndani ya makazi ya watu ili tathmini ya uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji yaliyoongezeka ifanyike.

  Katika kuzuia matukio ya moto TANESCO imekuwa ikihakisha kuwa inamfikishia mteja umeme ulio salama na usiokuwa na madhara kwa mtumiaji kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye mita.
  Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwepo na matukio ya ajali za moto katika makazi ya watu ambayo yamekuwa yakisababisha madahara  ikiwemo kusababisha vifo,majeruhi  na uharibifu wa mali.

  0 0

  Mwandishi Wetu-Geneva
  TANZANIA imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

  Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto  Ummy mwalimu (Pichani) wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.

  Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua  katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia  vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000

  Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.

  “Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania  ambapo hadi kufikia  tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia wizara ya afya  itaimarisha  na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema

  Kwa upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar  imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa  hadi kufikia asilimia 0.6.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  MSHAMBULIAJI wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi amesema, kuelekea katika usajili  wa wachezaji wapya viongozi  wanaqtakiwa kuangalia ambao wanahaki ya kuitetea simba na sio kusajili mchezaji kwa sababu ya jina lake.

  Mgosi amesema, Klabu inatakiwa kusajili wachezaji ambao wataipa Simba kile kitu ambacho kinakihitajika ili kuiweka timu katika nafasi nzuri.

  Mgosi amesema, wachezaji wa kigeni wanahitajika lakini waangaliwe kama ni watu aina gani wanahitajika na wanauwezo wa kuitetea timu kwa kazi watakayoifanya.

  "Mchezaji wa kigeni anatakiwa kufanya kazi ya ziada ambayo itamzidi yule mchezaji mzawa ili kuweza kuweka utofauti kati ya mchezaji wa kimataifa na mzawa katika klabu,"amesema Mgosi. Hilo limekuja baada ya wachezaji wa kigeni wa timu hiyo kucheza chini ya kiwango ukilinganisha na wazawa na wengine kuishia kuishia kukaa benchi.

  Mgosi amesema, viongozi wanatakiwa kuangalia makosa yaliyotokea katika msimu uliopita na kupelekea timu kushindwa kufikia malengo ili kuyarekebisha na hata usajili utakapofanyika uwe wa kueleweka.

  0 0

  The Contractors Registration Board (CRB) annual general meeting is set to take place this coming Thursday and Friday on 26th and 27th May respectively at Diamond Jubilee hall.

  Sponsored by TIB Corporate bank, the meeting will be the winding up of the Annual General Meeting following the first meeting, which took place in Mwanza at Malaika Beach Hotel on May 5th and 6th. 

  The event will carry the theme 'Deliberate Capacity Building of Contractors for Sustainable Economic Development; Challenges and Way forward'.During the Mwanza consultative meeting, contractors underscored the importance of financial empowerment as a means to enable local contractors to compete in the construction industry particularly in bidding, securing and executing contracts. 

  This was amid reports that at least 65 per cent of projects undertaken by indigenous contractors were shoddy due to poor financial base and lack of professionalism.In its bid to support the performance of local contractors, TIB Corporate Bank introduced hassle-free loans to local contractors of various works aiming to build and strengthen contractors’ financial capacity and create a bigger room for them to play in the construction industry. 

  The loan is extended for meeting working capital needs; purchase of construction equipment; and for providing bank guarantees for the purpose of earnest money deposit or security deposit. 

  ‘This special loan facility for the local contractors is tailor made in order to support and create a favourable operating enviroment, and thus enable them to compete with international contractors and thus contribute to the economy of the country’ said Frank Nyabundege, TIB Corporate Bank Managing Director.

  The meeting in Dar es Salaam will also host an international Construction technology, products and services Exhibition

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.

  Na. Aron Msigwa - Dodoma.

  Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 8 kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika mazingira mazuri.

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake. 

  Dkt.Kigwangala amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi milioni 680.Aidha, ameeleza kuwa vyuo vya Afya vimekuwa vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula waliokuwa wakiidai Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka 2009 hadi 2015.

  Amebainisha kuwa tayari Serikali imekwishahakiki madeni yote ya wazabuni ili yaweze kulipwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi ili zifanye kazi hiyo.

  Katika hatua nyingine Dkt.Kigwangala amesema Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.

  " Niko tayari nikishirikiana na waheshimiwa wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo" Amesisitiza Dkt.Kigwangala.

  0 0

  Mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji akichangia mada ndani ya bunge hilo 

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Serekali imekuwa ikipoteza kodi nyingi zitokanazo na ushuru wa mazao hasa kutokana na kuwa na mzabuni mmoja ambaye anakusanya kodi za mazao kwa nchi nzima .

  Hayo yamebainishwa na mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge hil, ambapo alisema kuwa kuna changamoto kubwa ya utekelezaji wa umoja wa forodha hapa nchini Tanzania.

  Alisema kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazofikia kiwango staili cha asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa hawatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao katika nchi za jumuiya wanachama .

  Aidha alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande wa Tanzania, kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi au kubaini viwango vya kusamehewa kodi zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya TCCIA.Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa upya katika nchi yetu na serekali kwa sababu TCCIA haipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni mikoa tu huku katika ngazi za wilaya pamoja na vijiji hawapatikani.

  Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na pia wananchi wengi pamoja na wafanya biashara wengi kutokujua thamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha mfanyabiashara kujua unafuu wa kodi.

  “sasa hivi ili kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa kutoa hati hizo kwa wadau wengine ili kuleta unafuu wa ulipaji kodi “alisema Bhanji

  Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za biashara za manispaa pamoja na ofisi za biashara za wialaya nawao waweze kupewa ili jukumu na wao waweze kutoa hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .

older | 1 | .... | 1231 | 1232 | (Page 1233) | 1234 | 1235 | .... | 3285 | newer