Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakandarasi, 26 mei 2016


Wasanii wa Kundi la Weusi na Isha Mashauzi kuzindua kampeni ya Chandarua Kliniki leo mkoani Mtwara

0
0
Kundi la Wasanii wa Hip Hop Weusi.
Na Mwandishi wetu Mtwara

Wasanii Aisha Ramadhani maarufu Isha Mashauzi na kundi la muziki wa Hip hop la Weusi wanatarajiwa kushiriki katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa malaria katika mradi unaojulikana kama KLINIKI CHANDARUA.

Mradi huo unaotarajiwa kutoa vyandarua bure kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa unazinduliwa jumamosi wiki hii Mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa matekelezo kutoka mradi wa Victor Works Bi, Noela Kisoka amesema wasanii hao watashiriki katika kuhamasisha kampeni hiyo kwa kupitia muziki na wao watashiriki katika uzinduzi wa mradi huo.
Isha Mashauzi

" Tunatarajia kuwa na wasanii kutoka katika kundi la Weusi ambao wanaimba muziki wa kizazi kipya lakini pia tutakuwa na mwanamuziki wa Taarab Isha Mashauzi ikiwa ni hatua ya kuufanya muziki kuwa sehemu ya hamasa ya utekelezaji wa mradi huu" alisema Kisoka.

" Wananchi wa Mtwara wajitokeze kwa wingi kutazama burudani ya muziki wa wasanii hao lakini pia kupata taarifa kuhusiana na Mradi wetu wa KLINIKI CHANDARUA ambao siku hiyo (leo) ndio tutauzindua" alisisitiza Kisoka.

Wasanii hao wamewasili jana jioni mkoani mtwara,tayari kuwasha moto katika uzinduzi wa mradi huo unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani hapa.

Mradi wa KLINIKI CHANDARUA utazinduliwa mkoani mtwara na mkuu wa mkoa huo Halima Dendego na unatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, shirika la Victor Works na kudhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

WANAOKUSANYA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI JIJINI MWANZA LAWAMANI

0
0
Vijana wanaokusanya ushuru wa tozo za maegesho ya magari jijini Mwanza, wamelalamikiwa kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kinyume na taratibu.

Vijana hao wamelalamikiwa kutokana na tabia yao ya kuvizia magari yanayoegeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza huku baadhi ya maeneo hayo yakiwa ni halali kwa ajili ya magari kuegeshwa kwa muda.

Katika mtaa wa Liberty jijini Mwanza, vijana hao wamelalamikiwa kutokana na kuvizia magari binafsi yanayowapeleka wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kwa ajili ya matibabu. Habari na BMG
Gari la mmoja wa wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kilichopo mtaa wa liberty jijini Mwanza likiwa limepigwa cheni.

TPRI YATOA ONYO KWA WANANCHI

0
0




Na Woinde Shizza, Arusha.

Taasisi ya Ukaguzi na Uthibiti wa Viwatilifu (TPRI) imetoa onyo kwa wananchi, kuwa makini na matumizi ya vyandarua vilivyoingia nchini kutoka nje,  huku vikiwa na alama ya uwepo wa dawa ya kuua mbu lakini havina maelezo ya kulinda afya za watumiaji  na havimo kwenye orodha ya msajili wa Viuatilifu.


Msajili wa Viuatilifu, Dkt. Elikana Lekei ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kufuatilia shehena ya vyandarua hivyo kuingizwa nchini, huku vikiwa havina maelezo ya TPRI huku akionesha baadhi ya vyandarua  hivyo.


kwa upande wao wazalishaji wa vyandarua wamesema hali hiyo inatokana na vyandarua vya nje kuingizwa nchini bila ushuru na kwamba imeathiri viwanda vya ndani na kulazimika kupunguza zaidi ya wafanyakazi elfu mbili.


JAJI MKUU AZITAKA MAHAKAMA ZA GEITA KUMALIZA KESI KWA WAKATI

0
0
Na Lydia Churi – Geita

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kuhakikisha zinamaliza kesi kwa wakati ili kutekeleza lengo lililowekwa na Mahakama ya Tanzania.

Akizungumza na watumishi wa Mahakama mkoani Geita, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania ilijiwekea malengo ya kumaliza kesi katika mahakama zake kwa wakati kulingana na aina ya mahakama.

Alisema kwa mahakama za Hakimu Mkazi, mahakama za Wilaya pamoja na Mahakama za   Mwanzo lengo lilikuwa ni kumaliza kesi zote ndani ya mwaka mmoja ili kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani na mahakama zao kwa kuwa ni zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanahudumiwa na mahakama hizo.  

Jaji Mkuu alisema kwa mahakama za Mwanzo ambazo ziko 970 nchini kote lengo lilikuwa ni kuhakikisha hazikai na kesi kwa zaidi ya miezi sita kwa kuwa ndizo mahakama zinazohudumia wananchi wengi zaidi. 
  
Alisema ili kuziwezesha Mahakama kutekeleza lengo walilojiwekea, tayari Mahakama ya Tanzania imeajiri Mahakimu wapya 107 ambao watasambazwa kwenye Mahakama zote za Mwanzo nchini kwa ajili yakwendakutoa huduma ya msingi ya mahakama ya kutenda haki kwa wananchi wa Tanzania.

Akizungumzia suala la utoaji wa nakala za hukumu, Jaji Mkuu amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kutoa nakala hizo mapema iwezekanavyo ili kutoa haki ya kukata rufaa kwa wananchi ambao hawakuridhishwa na hukumu walizopewa katika kesi zao.

Alisema Mahakama ya Tanzania itaongeza idadi ya Makatibu Mahususi na kuongeza vifaa katika Mahakama zake ili kuongeza kasi ya uchapaji wa nakala za hukumu. Alisema asilimia 80 ya bajeti inayotolewa kwa muhimili huo imetengwa kwa ajili ya kuendesha kesi katika mahakama za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi.

Jaji Mkuu anaendelea na zaira yake katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ambapo anatembelea mikoa Mwanza, Geita na Mara ili kukagua shughuli za kimahakama katika kanda hiyo.

msimu mpya wa Maisha Plus East Africa 2016 waanza rasmi, sasa kurushwa kupitia Azam TV

0
0

 
Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa msimu mpya wa kipindi hicho, uliofanyika jana usiku katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU.
 
Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akifurahi jambo na washiriki wa vipindi vilivyopita vya Maisha plus wakati wa hafla ya ufunguzii uliofanyika katika viwanja vya Studio za Azam Tv na kutegemewa kuanza kuonyeshwa mapema jumapili hii saa tatu usiku katika channel ya Azam Two.Na kauli mbiu ya mwaka huu ni #HAPA KAZI TU.


 
Mkurugenzi wa Azam Media,  Tido Mhando (Kushoto) akiwa na Masoud Kipanya akiongea na wageni waaalikwa waliohudhuriia uzinduzi wa Maisha Plus East Africa 2016 ambaye itaoneshwa katika chaneli ya Azam TWo kuanzia jumapili hii saa tatu usiku.

MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YALIYOANDALIWA NA AGRIPROFOCUS YAFANYIKA UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

0
0
Mgeni Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji ,Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia Wakulima wa AgriProFocus yanayofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
 Afisa Msaidizi wa Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye ndoto wa AgriProFocus ,Hildagard Okoth akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Wenceslaus Lindi wakati akitembelea mabanda katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
 Afisa Ugavi wa SEVIA,Lewis Mlekwa akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mjini Moshi. 

WAHADZABE WALALAMIKA KUTENGWA

0
0
Na Woinde Shizza, Karatu.

Watu wa Jamii ya Wawindaji waokota matunda na walina asali kutoka kabila la Wahadzabe katika kijiji cha Endamagh wilaya ya Karatu, wamelalamika kitendo cha kutengwa kuingizwa kwenye mpango wa ruzuku kwa kaya masikini, unaoendeshwa na TASAF wakati wao ni jamii masikini zaidi, kwani kati yao ni kaya saba tu ndizo zilizo ingizwa kwenye mpango huo, hivyo wanalazimika kugawana kiasi kidogo wanacho  kipata.

Watu hao wa kabila la Wahadzabe wametoa kauli hiyo  katika kijiji cha Endamash, walipotembelewa na maafisa wa TASAF kutoka Makao Makuu, pamoja na wawakilishi wa Benki ya Dunia, ambapo wamedai sasa wanalazimika kugawana fedha zinazo tolewa kwa kaya saba kwakuwa wote hawana uwezo na matunda na wanyamapori wameadimika kutokana na ukame.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Billar Bird amesema amesikitishwa na hali waliyo nayo watu hao, lakini amechukua maombi yao na atayafikisha kwenye kikao cha nchi wafadhili wanaotarajia kukutana mwezi ujao.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema kasoro hizo zimetokana na tabia ya jamii hiyo ya kuhamahama ndiyo maana walikosa fursa hiyo lakini  TASAF itaangalia namna ya kuwasaidia.


BARAZA LA WAZEE YANGA, WATAKA MKUTANO MKUU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BARAZA la wazee wa Yanga wameomba kupewa ufafanuzi na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) pamoja na Baraza la Michezo nchini (BMT) kuhusiana na matumizi ya kadi zitakazoruhusiwa kupiga kura siku ya uchaguzi, kwani hilo limekuja baada ya taarifa kutolewa kuwa kadi za zamani ndizo zitakazotumika katika siku ya kupiga kura.

Katibu mkuu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali amesema wanataka ufafanuzi zaidi kwani toka kuanza kwa mfumo wa kadi mpya za benki ya Posta wanachama wengi walibadilisha na kuondoka kwenye mfumo huo zamani na kadi hizo wanazitumia kwa miaka miwili sasa.

"Kutokana na tamko lao la kutumia kadi za zamani na kuwabagua wale wenye kadi mpya na kusema walio na kadi za zamani ndiyo wanahaki ya kupiga kura kiuhalisia inaweza kuleta mgogoro kwa wanachama,"amesema Akilimali. Kwahiyo tunaomba TFF na BMT kuweza kutoa tamko la kutumika kwa kadi zote mbili kwani hata katika uchaguzi wa mwaka 2006 zilitumika kadi mbili Yanga kampuni na Yanga Asili.

Pia, Baraza la wazee limeombaTFF na BMT kuipa ruhusa Sekretarieti ya Yanga kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wenge Ajenda ya uchaguzi mkuu ili wanachama wapewe taarifa kuhusu uchaguzi, na katika mkutano huo sekretarieti iwaalike viongozi kutoka wizara husika, TFF, DRFA (chamacha mpira wa miguu mkoa wa Dar es salaam) na wadau wote ili kushuhudia maamuzi ya wanachama wa Yanga huku wakiomba busara itumike na kudumisha umoja, amani na utulivu uliopo ndani ya klabu hiyo.

WAGANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS NA HARAMBEE KESHO

0
0
Waamuzi watatu wa soka kutoka Uganda, ndio wakaochezesha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Harambee Stars ya Kenya utakaofanyika Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi, Kenya.

Waamuzi hao watakaochezesha mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Azam Tv kwa kushirikishi na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) ni Brian Nsubuga atakayepuliza kipenga na wasaidizi wake ni Bugembe Hussein upande wa kulia (line 1) na Katenya Ronald kwa upande wa kushoto (line 2).

Kamishna wa mchezo atakuwa Amir Hassan kutoka Somalia ambako Meneja wa Uwanja wa Moi Kasarani, Lilian Nzile amesema kwamba mazingira uwanja ni mazuri na mipango yote ya mchezo huo imekaa vema ikiwa ni pamoja na usalama uliothibitishwa pia na Kanali wa Jeshi la Polisi, Muchemi Kiruhi OCS wa Kasarani.
Kwa upande wa Kocha Mkuu Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Charles Boniface Mkwasa atawakosa washambuliaji wake watatu katika kikosi ambacho kitaivaa Harambee Stars.

Washambuliaji hao ni Mbwana Samatta kutoka Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na John Bocco ambaye ni majeruhi wa mguu aliumia wakati wa fainali za Kombe la FA kati ya Yanga na Azam Jumatano wiki hii.

“Madaktari wamempa Bocco saa 72 za mapumziko. Bila shaka kabla ya kucheza na Misri atakuwa amepona,” alisema Mkwasa leo Mei 28, 2016 asubuhi na kuongeza kuwa Samatta ametuma taarifa kukosa mchezo dhidi ya Kenya kwa kuwa ana ratiba ya kucheza mchezo muhimu Mei 30, mwaka huu na matarajio ni kujiunga na timu Juni 1, 2016 kabla ya kuivaa Misri Juni 4, mwaka huu.
Kwa upande wa Ulimwengu, uongozi wa TP Mazembe nao waliomba kumtumia Ulimwengu katika mchezo wa ushindani wa mpinzani wake AS Vita. TP Mazembe na AS Vita ni timu pinzani huko DRC Congo na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ukaridhia na Mkwasa sasa amejipanga kukiandaa kikosi bila nyota hao mahiri.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

TEA KUENDELEA KUJENGA MABWENI YA WASICHANA

0
0
KUELEKEA maadhimisho ya hedhi salama itakayofanyika Mei 28 , Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imesema itaendelea kujenga mabweni na chemba za kuhifadhi na kuchomea taulo za kike ili kuwafanya wanafunzi wa kike kusoma katika mazingira mazuri.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo iliyoko wilayani Ilala, Meneja Mawasliano na Uhusiano wa TEA, Sylvia Lupembe alisema wanafunzi wa kike wamekuwa na wakati mgumu katika masomo yako kutokana na hedhi.

“ Wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria masomo kwa zaidi ya siku 80 kwa mwaka jambo ambalo linarudisha maendeleo ya mazomo yao, kwa kushirikina na wadu wa elimu tumeona tuangalie suala la kuwasaidia, hasa wale alioko kwenye shule ambazo ni vigumu kufikia,” alisema.

Alisema kwa mwaka huu wa fedha, TEA kwa kushirikiana na wadu wa elimu wanakamilisha ujenzi wa mabweni 11 ya wanafunzi wa kike hapa nchini.

Lupembe alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuwezesha kupatikana na taulo hizo za kike sambamba na mchango wao katika ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Pangani ambalo limegharimu sh milioni 20.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo Christine Kasyupa, aliwashukuru TEA na benki ya CRDB kwa mchango wao ambao wamekuwa wkaiutoa katika shule hiyo kwani awali walishopokea dawati.

Naye Mwanafunzi Monica Singano anayesomba darasa la Saba A katika shule ya msingi Yombo, alisema msaada huyo umekuja wakati mzuri hasa kutokana na wanafunzi wengi kutoka kwenye familia mabazo hazina uwezo wa kugharamia kununua taulo za kike.

“ Wengi wa wanafunzi hapa wanatoka familia zisionauwezo wa kununua taulo za kike, wengi wanatumia vitambaa ambavyo haviwezi kuwafanya wanafunzi kukaa shule kuanzia asubuhi hadi mchana, hivyo kulazimika kwenda kubadili huku masomo yakiwa wanaendelea,” alisema
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya kujihifadhi wanawake vilivyotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Ofisa wa TEA, Happines Tandari, Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad na Mwalimu Emily Salumu. (Picha na Francis Dande) 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiimbo nyimbo katika hafla hiyo. 
Ofisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Happines Tandari akizungumza kaba la makabidhiano ya vifaa hivyo.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa (katikati) na mwalimu Salumu sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Monica Singano sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE MAKWAIA

0
0
likuwa siku, miezi na leo hii ni mwaka wa tatu tangu ulipotuacha kwa machungu mengi siku ile ya tarehe 30th May 2013 ukiwa Jaslok Hospital, India. Kimwili haupo nasi bali kiroho tupo nawe, Daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi, Sio tu kuwa Baba mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu. Uliyebarikiwa kwa mambo mengi, ucheshi wako, hekima na busara zako, na juu ya yote hayo ulikuwa unafanya jambo kwa kusudi maalumu kwa kupenda usawa kwa kila binadamu, na kuwataka watoto wako tuwe na upendo na kutambua umuhimu wa elimu katika familia na jamii.

Tutaendelea kukumbuka na kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha, na daima tutaendelea kukumbuka busara zako Baba na tutaendelea kukuenzi hadi tutakapo kutana tena paradiso.

Daima unakumbukwa sana na mke wako Mama Thecla Makwaia; watoto wako Stella Makwaia, Frank Makwaia, Robert Makwaia na Christopher Makwaia (MK), wajukuu zako Magdalen Christopher Makwaia pamoja na Madeleine Christopher Makwaia, unakumbukwa sana na ndugu zako, marafiki zako, majirani zako wote, wafanyakazi wenzako na Idara mbali mbali ulizowahi kufanyakazi kipindi cha uhai wako.

Tutakukumbuka daima Baba.

PUMZIKA KWA AMANI. AMEN.

*Misa ya kumbukumbu itafanyika tar 29/05/2016 saa 2.30 asubuhi katika kanisa la St. Maximilian Kolbe – Mwenge Afrika Sana.

WASHIND KUMI WA KWANZA WA PROMOSHENI YA MILLIONI 100 NA TUSKER FANYA KWELI UWINI WATANGAZWA

0
0
 Ni wiki mbili tangu promosheni ya TUSKER FANYA KWELI UWINI ilipozinduliwa kiaina yake mikoa miwili tofauti kwa wakati mmoja, Dar es Salaam na Moshi. Leo washindi kumi wamepatikana katika droo ya kwanza na ya kusisimua. Milionea hawa walitangazwa leo katika droo iliyorushwa moja kwa moja na kushuhudiwa na waangalizi kutoka Bodi inayosimamia michezo ya kuigiza Tanzania, wana habari nan a wahusika wakuu wa promosheni hii ambao ni timu nzima ya Tusker lager. 

Washindi kupitia maongezi ya simu walionesha mshangao na furaha kubwa kushinda kitita cha Tsh. 1,000,000 ambapo wamekiri hawakutegemea kupata kiasi hicho cha pesa kwa hivi karibuni. Ukiachilia mbali washindi wa kila wiki wanaopatikana kupitia droo pia wapo watumiaji wa bia ya Tusker wanaojipatia bia kibao za bure kila siku. Promosheni bado ina wiki tisa mbele.

Washindi kumi wa kwanza ni Rehema Matemba, Elias Poto, Deogratius Shayo kutoka Kilimanjaro, Vestina Mainde, Doru B. kutoka Morogoro,  Sebastian Joseph, Michael Mwinuka,  Albert Tarimo na Festo Silvester ambaye ameshinda Millioni 2 wote kutoka Dar es Salaam.

Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa kwanza Rehema Matemba ambaye ni mfanyabiashara katika manispaa ya Moshi alishikwa na mshangao kwani hakutegemea na anaona kama ndoto kuwa mshindi wa Milioni 1 kutoka Tusker kwani alishiriki promosheni hii wiki moja iliyopita na kuwa kati ya wale waliobahatika.

Naye mshindi wa pili Albert Tarimo alielezea furaha yake na kuishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake kwa kugusa maisha yao ambapo kila mara huja na promosheni za kuvutia kwa wateja wake. “Nilishiriki kujaza vocha ya promosheni hii nilipokua bar nakunywa bia yangu ya Tusker sikutegemea kushinda kwani siku zote huwa sina mazoea ya kushiriki mashindano yeyote yale, nafuraha sana ni mara yangu ya kwanza kushiriki na kuwa moja ya washindi. Milioni 1 niliyoipata itanisaidia kuwalipia wanangu ada za shule kwangu ni faraja sana imekuja kipindi ambacho nauhitaji mkubwa wa pesa.” Alisema Tarimo.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela alieleza kuwa promosheni hiyo iliypo maalum kwa watumiaji wote ina faida kubwa kwa watumiaji wa bia zao za Tusker kama ilivyoanza kwa wateja kumi wa kwanza leo ambao wameguswa kwa namna tofauti nay a kipekee. “Ikiwa tu hapa ni hatua za mwanzo za promosheni hii kumekuwa na zaidi ya washindi 1000 wa bia za bure na maelfu wameshashiriki. 

Tangu tuzindue Tusker Fanya Kweli Uwini wiki mbili zilizopita tumepata muamko mkubwa kutoka kwa wateja wetu. Leo tumepata washindi wetu kumi wa kwanza ambao watakabidhiwa million 1 kila mmoja na kufanya jumla ya Million 10 kutolewa wiki ya kwanza. “Alisema Nandi.

Aliongeza kuwa “promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini inaendelea na tumebakiwa na wiki tisa, tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado tuna Million 90 na bia kibao za kushinadaniwa! Kutakua na shughuli mbalimbali za burudani kila wikend yaani Ijumaa na Jumamosi kipindi chote cha kampeni yetu katika bar mbalimbali nchi nzima, hivyo mjitokeze kwa wingi muweze kufanya kweli. 

Katika huu mwanzo mzuri wa promosheni yetu napenda kuwashukuru sana wateja wetukwa kutuunga mkono na walivyoipokea kwa mikono miwili promosheni hii ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli na Uwini.” Aliongeza Nandi

Droo za promosheni hii zitaendeshwa kila wiki na hiyo italeta msukumo kwa wateja na watumiaji wa bia ya Tusker kushiriki zaidi. Kwa utofauti kabisa hii ni promosheni ya kwanza iliyoangalia na wahudumu wa bar pia ambapo wahudumu watapata Tsh 100,000 endapo aliyemuhudumia akishinda. Hivyo leo washindi kumi wamepata Million 1 kila mmoja na wahudumu kumi pia wamepata 100,000 kila mmoja.
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akitoa maelezo ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, pembeni yake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua.
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi kumi wa kwanza wa promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo, akishuhudiwa na afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua (katikati), pamoja na muongozaji wa shoo hiyo Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni mtangazaji wa ITV wakati wa droo ya kwanza inarushwa moja kwa moja kupitia ITV.
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela akiokota kuponi ili kujua mmoja wa washindi kumi wa kwanza.

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BENKI YA NMB KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

0
0
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji,Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Benki ya NMB katika maeonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya biashara na Kilimo wa Benki ya NMB,Oscar Rwechungura (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi (aliyekunja mikono) katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia wakulima wa AgriProFocus.Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi,Emanuel Kashusho akikabidhi zawadi ya T-shirt ,Kalamu na Key holder kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi mara baada ya kutembelea banda la Benki hiyo na kupata maelezo namna inavyoshirikiana na wakulima katika kukuza mitaji yao.


KONGAMANO LA KUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUFANYIKA KESHO

0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na rais wa kef mohamed kamilagwa(kushoto) akimuonesha imam qasim ibn ali khan baadhi ya vivutio vilivyopo nchini kupitia jarida
 Imam Qasim Ibn Ali Khan (katikati) akibadilishana mawili matatu kwaajili ya kongamano la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na rais wa kef mohamed kamilagwa na kushoto kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Juma Nchia
 Imam Qasim Ibn Ali Khan pamoja na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani mohamed kamilagwa.
Mke wa imam hasaina m.khan (wakwanza kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwl. j.nyerere akiwa na baadhi ya wanakamati waliojitokeza kumpokea alipowasili nchini tanzania. 
 Imam Qasim Ibn Ali Khankutoka usa akiwa pamoja na baadhi  ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la nane la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani mara baaada ya kuwasili nchini tanzania.

WANAMICHEZO WAASWA KUWA WABUNIFU

0
0
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Viongozi  wa  Timu ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo wameaswa kuwa wabunifu na kuongeza jitihada za kuunda timu bora za michezo zitakazo jipatia ushindi katika mashindano mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mhazini  kutoka Shirikisho la Michezo,Wizara na Wakala wa Serikali (SHIMIWI) Bw.Brown Nyamtiga mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na washindi kutangazwa. 

“Mkiwa kama Wizara yenye jukumu la kusimamia masuala ya Michezo nchini  ni vyema muwe mfano kwa taasisi zote za serikali kwa kuwa na timu imara zenye uwezo wa kupata ushindi pamoja na hili linawezekana pale mtakapoamuwa kuweka jitihada za dhati katika kusimamia hilo”,alisema Bw.Nyamtiga.

Akiendelea kuzungumza katika uchaguzi huo Bw.Nyamtinga alisema anatambua changamoto ya pesa iliyoko serikalini kwa sasa,hivyo viongozi wanapasawa kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuisaidia serikali suala hilo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Timu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo Bw.Modest Mfilinge kutoka Utawala alisema katika uongozi wake anatarajia kufanya mageuzi chanya katika sekta ya michezo kwa wafanyakazi wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuunda mabonaza yatakayo kuwa yakifanyika kila mwisho wiki.

“Awali ya yote nitafanya jitihada za kutambua wanamichezo katika Wizara na kwa hili naamini ndipo nitakapopata wachezaji mahari watakao unda timu bora ya michezo katika Wizara na kikubwa nitakachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wenzangu”,alisema Bw.Mfilinge.

 Pamoja na hayo Bw.Mfilinge alisema mabonanza anayotarajia kuanzisha ni endelevu na anaimani kubwa na viongozi wenzake waliyochaguliwa kuwa watashirikiana vizuri na kufanya kazi nzuri yenye kuleta matokeo chanya katika timu ya wizara. 

Hata hivyo uchaguzi huo wa Wizara umesaidia kupatikana kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Timu Bw.Jackson Manyika kutoka Kitengo cha Uhasibu,Katibu Mkuu Msaidizi Bw.Mfaume Said Mfaume kutoka Utawala,Makamu Mwenyekiti Bw.Francis Songoro,Mweka Hazina Bi. Flora Mwenyembegu, Mjumbe Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa SHIMIWI Bw.Carlos Mlinda pamoja na Wajumbe wa Idara .

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA BUNGE CHAPATA MWENYEKITI MPYA

0
0
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bw. Mchenya John akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge (hawapo pichani) kabla ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUGHE tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi hiyo Bibi. Emma Lyimo.Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Abdallah Hancha (wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wenzie wa Ofisi ya Bunge kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Walioambatana naye ni wajumbe wa Kamati Kuu ya TUGHE tawi la Bunge.Wasaidizi wa kamati ya Uchaguzi wakihesabu kura wakati wa Uchaguzi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Chacha Nyakega akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.

PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-MAELEZO

NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA UDOM

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akishirika kufanya usafi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom wakati usfi wa mazingira kitaifa iliyofanyika, Dodoma jana
Luaga Mpina akiongozana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati wa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana
Luaga Mpina akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana

TAWLA YAWATAKA WANAWAKE KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIUCHUMI ILI KUNDOA UTEGEMEZI

0
0
Wanawake wametakiwa kushiriki shughuli za kiuchumi ili kujikomboa na kukandamizwa na mifumo ya kijamii iliyopo sasa nchini.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Bi Tike Mwambipile leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa chama hicho.

Bi Mwambipile amesema kuwa wanawake wa Kitanzania wananyanyasisika sana kwani hawana vipato vya kutosha, hivyo inabidi waongeze juhudi katika kuibua na kubuni miradi endelevu ya ujasiriamali ili kukuza vipato vyao.“Wanawake mnapaswa kujiunga na VICOBA na Saccos ili muweze kupata mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kufanyia biashara,”alisema Bi Mwambipile akiongeza kuwa kipato kinachopatikana inabidi wanawake wawe na maamuzi ya kukitumia bila kusubiria maelekezo ya waume zao.

Naye Mwenyekiti wa TAWLA, Bi Asia Bade amesema kuwa wakati umefika kwa wanawake kujitambua kuwa ni sehemu muhimu katika jamii hivyo kutumia uwezo wao kujikwamua kiuchumi pasipo kutegemea wanaume.Bi Bade ameongeza kuwa suala la ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za kiuchumi litawakomboa na utumwa wa kipato ambao umewatesa kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake mjumbe wa Mkutano huo, Dkt. Pindi Chana ameishauri Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuweka sharti la mkakati wa kuwainua wanawake na vijana kwenye mabenki yanayoomba usajili. Ameongeza kuwa bila kuonyesha makakati huo, BOT isitoe kibali kwa benki yoyote.

Dkt. Chana ameonyesha kukerwa na riba za mikopo kuwa juu sana kwa wakopaji na kusema, “Watanzania tunayafanyia mabenki kazi kutokana na riba kubwa wanazotuwekea kwenye mikopo, hii haitunufaishi bali inatutesa katika kurejesha.”Akionyesha kukerwa na utegemezi wa wanawake, Mjumbe wa Mkutano huo, wakili Mary Kessy amesema ni wakati wa wanawake kuacha kubweteka wakisubiri kupokea kutoka kwa waume zao bali wachangamkie fursa zilizopo ili wawe na kipato cha uhakika.

Bi Kessy amesema kwamba kuna fursa nyingi za kuwainua wanawake kiuchumi ambazo ni pamoja na ushiriki katika shughuli za madini, kilimo, mifugo na uvuvi pia kutumia mabenki ya wanawake.“Huu sio wakati wa kuchagua kazi, wanawake tujitume, fursa ziko nyingi sana hapaTanzania, kama ni kwenye migodi tuwemo, biashara za kimataifa tufanye na kwenye nafasi za uongozi tujitokeze badala ya kulalamika” amesisitiza Bi Kessy.

Huu ni Mkutano wa 25 ambao unawajumuisha wanawake wanasheria nchini kuweza kubainisha namna ya ushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuweka mikakati ya kutoa elimu endelevu ya uzalishaji mali.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Ms. Aisha Zumo Bade akisoma hotuba yake waakati wa wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
Mtoa Mada Agustus Emmanuel Fungo akiwasilisha mada ya masuala ya kiuchumi kwa wanasheria wa Chama cha wanasheria wanawake TAWLA wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.

Mtoa Mada Dr. Elie Waminian Akizungumza wakati akitoa mada wanawake kujiamini katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kutokuwa wavivu.

Baadhi ya wanasheria wanawake walioshiriki katika mkutano huo wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa.
 

VIJANA WAHINIZWA KUDUMISHA UZALENDO

0
0
Na Lorietha Laurence

Vijana wamehimizwa kuendeleza upendo na uzalendo katika kutambulisha Taifa la Tanzania ikiwemo kutangaza utamaduni wake kwa mataifa mengine  Barani Afrika na Duniani kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi, Lilian Beleko jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuzindua klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere chini ya usimamizi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika ikiwa na lengo la kuwapatia vijana elimu ya msingi kuhusu historia ya ukombozi wa bara la Afrika na masuala mbalimbali ya kijamii.

“Klabu ni jambo jema na zuri kwa vijana wa sasa ukizingatia wengi wao hawakuwepo wakati ukombozi wa bara la Afrika hivyo kupitia klabu hizi mtajifunza mengi” alisema Bi.Beleko.

Aidha aliongeza kuwa viongozi wa Afrika walijitolea kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo kwa kuwaunganisha waafrika katika kupigania uhuru wa bara la hilo ili kuwakomboa kutoka mikononi mwa wakoloni na kuweza kujitegemee kwa kuwa na viongozi wake.

Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi Kulthum Maabad ameleza kuwa ili vijana waweze kujikomboa kutoka katika umaskini ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra kwa kupata elimu muhimu ikiwemo ya uzalendo wa kuitumikia nchi zao kwa uaminifu.

Kwa upande wake Msaidizi Maalum wa mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nchini ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kujifunza na kuujua mchango mkubwa uliofanywa na Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika kwa kusoma vitabu vyake na kupitia nukuu zake

Uzinduzi wa klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere umeenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya wiki ya ukombozi wa afrika ambapo hukumbukwa kwa kuwaenzi waasisi wa upigania uhuru kwa kuwepo kwa maonyesho mbalimbali ya Sanaa,Lugha na Utamaduni.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images