Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1223 | 1224 | (Page 1225) | 1226 | 1227 | .... | 3348 | newer

  0 0

   
   Gari aina ya DCM linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto na Masaki jijini Dar es Salaam likiwa limeinuliwa baada ya kupinduka leo mchana eneo la Kipawa Njia Panda ya Jet Lumo, Dar es salaam. 
  Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa ni kumkwepa mwendesha baiskeli. Watu kadhaa wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamelazwa katika hospitali za Amana na Muhimbili.
   (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
   Wananchi wakiliangalia paa la gari hilo lililokatwa kwa kupata urahisi wa kuwatoa majeruhi waliokuwemo kwenye gari hilo

   Lenzi ya jicho la blog ya ujijirahaa ilipata kuona katika ajali hiyo kitu kinacho sadikika ni hirizi iliyokua juu ya Gari hilo imeshonwa kwa nyuzi nyeusi iliyovishwa kitambaa cheusi
  Gari hilo likitarajiwa kuvutwa kuondolewa eneo la tukio

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetambulisha na kuzindua kampeni yake mpya kwa wateja kupitia huduma yake yake yakifedha kwa njia ya Mtandao ya Airtel Money Kampeni hiyo imezinduliwa katika ukumbi wa burudani/club wa Maisha basement jana usiku mbele ya waandishi wa habari na watangazaji wa vipindi vya redio toka redio mbalimbali 
  Meneja wa huduma ya Airtel Money Moses Alphonce akitoa sababu za ujio wa Mr. Money kwamba amekuja na habari za unafuu urahisi na usalama unaopatikana kupitia huduma ya Airtel Money sasa ambapo huwezi kupata kwingine. 
   Akiongea wakati wa uzinduzi wa Mr Money Meneja huyo alisema "Mr. Money anasema ‘tumia Airtel Money kwa kuwa ndio nafuu na hakika kuliko mitandao yote’ 
  Kutuma pesa popote nchini ni BURE na kwa uhakika Lipia BILI kama LUKU na ujipatie nyongeza za unit za umeme, hii ni kwa Airtel money TU Au lipia Ving’amuzi kwa uhakika na kwa raha bila usumbufu Pia Ongeza salio popote ulipo kwa uhakika, utapata bonasi ya muda wa maongezi BURE Ukiwa na airtel money unaweza kufanya mengi Zaidi 
   Piga *150*60# SASA ujinonee.
   Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi usiku, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi.
   Meneja wa Msoko wa Airtel Money, Moses James (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa.
  Sehemu ya wafanyakazi wa Airtel Tanzania wakifuatilia jambo, wakati wa hafla ya kutambulisha huduma mpya ya Mr. Money, itakayomwezesha mtumiaji wa Airtel Money kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi, iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  UONGOZI wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam umesema kuwa hawawezezi kushushwa daraja kwa ajili ya deni la mchezaji wao wa zamani Donald Musoti ambalo lipo ndani ya uwezo wao.

  Musoti amechezea Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa amelalamika FIFA kwa kumtumia mwanasheria wake Felix Majani, FIFA ambayo imeona Musoti ana hoja, hivyo Simba imetakiwa kumlipa Sh 64.2 milioni.
  Rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema kuwa  klabu yao haiwezi kushindwa deni hilo la Musoti kwani wameshaanza kulizungumza kabla ya kupokea barua kutoka FIFA.
  "Tulianza vikao takribani siku tatu nyuma kabla ya kupokea barua kutoka FIFA na tumebakiwa na mwezi mzima na tutahakikisha tunalipa deni hilo", amesema Aveva.
  Akizungumzia kuhusu fedha za mauzo ya mshambuliaji wao Emmanuel Okwi Aveva amesema kuwa fedha hizo zimeshaingia na zitatumika kwa ajili ya masuala ya ndani ya Simba.
  "Simba ni taasisi na suala la fedha za mauzo ya Okwi zitajadiliwa na ndani ya vikao vya mapato na matumizi na tutahakikisha zinatumika kama zilivyopangwa", amesema Aveva.
  Amesema yapo masuala mengi ya ndani ya klabu ikiwemo ujenzi wa uwanja wa Bunju ambao ulikuwa unasubiri mvua zimalizike.

  "Uwanja wa Bunju ulishindwa kushughulikiwa kwa kipindi kirefu kutokana na kusubiri fedha hizi na zimeshaingia na tumekubaliana kuanza ujenzi mara moja, "amesema Aveva.
  Pia ametoa msimamo wa klabu kwa kuwashughulikia wachezaji watano wa kimataifa kwa kosa la kusema uongo na kutokuhudhuria kambini kwa madai ya kutokulipwa mishahara.

  0 0

  0 0


  0 0

  Wakati tukiendelea kuvisaka na kuvimulika vijipu upele, leo tumekutana na taswira hii ya foleni ya watu wenye utulivu wakisubiri kupanda mabasi ya UDART kistaarabu. Utamaduni huu mpya umetupa furaha na faraja sana. Hongera UDART na hongera Abiria wa Dar es salaam.

  0 0

  Shule ya sekondari ya wasichana ya Ilala Islamic iliopo kwenye Msikiti wa Taqwa Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, inateketea kwa moto usiku huu. Chanzo cha moto huo hakijaweza fahamika mara moja na jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea.  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KIKOSI cha timu ya Yanga kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Sagrada Esperanca Kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirishiko barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca nchini Angola.

  Yanga imewasili salama mjini Dundo, Angola jana jioni baada ya safari ya kutwa nzima huku wachezaji wakionekana kupata usumbufu wa kubadilisha usafiri pamoja na baadhi yao kupoteza mabegi.

  Meneja wa timu Hafidhi Saleh amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya wenyeji ambapo anajua mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao.

  Amesema, wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya maandalizi ya kesho ila asubuhi watafanya mazoezi ya mepesi mepesi.

  "Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho lakini kesho asubuhi watafanya yale mepesi mepesi kuelekea mchezo wa kesho ambao ni muhimu sana kwetu,"amesema Saleh.

  Saleh amesema, wanatarajia kesho watahakikisha wanapafa ushindi hasa baada ya wachezaji wao wawili ambao hawakucheza kwenye mechi ya Jijini Dar es salaam watakuwemo kwa ajili ya kuongeza nguvu.

  "Ngoma na Kamosoku wamejumuika katika kuelekea mchezo huu hasa baada ya ule wa awali kuwepo jukwaani wakiwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizozipata kwenye mchezo wa Al Ahly,"amesema Saleh.

  Saleh amesema hali za wachezaji wote zipo vizuri na wamejiandaa kuweza kushinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao na kama watafanikiwa kushinda basi watasonga mpaka hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.

  0 0

  Mkurugenzi wa Her Initiative Lydia Charles akizungumza na vyombo vya habari

      Her Initiative iliyojulikana mwanzo kama Teen Girls Supportive  Initiative (TGSI) wameandaa mkutano mkubwa ujulikanao kama Panda utaowajumuisha wanafunzi wa kike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari yote katika lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
        Her Initiative ni asasi ya wasichana ambapo wao wenyewe ndio mhimili wa maongezi. Her Initiative inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, elimu, kiutamaduni na kiafya. Zaidi Her Initiative inamjengea uwezo msichana wa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
      Panda ni event inayohusu ujasiriamali, uvumbuzi, ubunifu na matumizi mazuri ya pesa. Kama tunavyofahamu, wasichana tuna matumizi mengi ya pesa na mara nyingi matumizi haya huzidi kipato cha pesa tunachokipata. Kwa kuona hili sisi kama wasichana tumeamua kuandaa event hii ili kusaidiana kuepuka hatari zinazoweza kutokana na kutokuwa na uchumi imara. Madhumuni ni kumjengea msichana hali ya kujitegemea kwa kumfundisha namna ya kuhifadhi pesa kupitia benki tofauti na mifuko mbalimbali ya jamii. Pia tunalenga kuwafundisha wasichana walioanza maswala ya ujasiriamali na uvumbuzi namna ya kuimarisha biashara, mawazo ya biashara na taasisi. Vilevilea kuwahamisha wasichana ambao hawajaanza kujishughulisha kuanza kufanya vitu tofauti tofauti vya kujikwamua kiuchumi.
  Mkutano huu utafanyika ukumbi wa Theatre One katika Chuo Kiuu cha Dar-es-salaam. Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bona Kalua ndio mgeni rasmi katika shughuli hii. Wageni wengine watakaohudhuria na kutoa maneno ya ushauri kwa wasichana ni pamoja na Ruge Mutahaba, Shekha wa Shear Illusions, Jeniffer Shigoli, Rose Ndauka, Dorice Mollel, Aika Navykenzo na Lemutuz.
       “Sisi ni wasichana na tunaimani kubwa ya kwamba tuna uwezo wa kuwahamasisha wanadada wenzetu kujishughulisha na vitu mbali mbali, kujilinda na vile vile kuleta maendelleo katika jamii kwa ujumla. Uwezo tunao na tunaamini Panda ni mwanzo wa maendeleo mengi zaidi kwa wasichana. Nina wasihi wasichana wajitambue, wajithamini na wachakarike” alisema Lydia Charles ambae ni mkurugenzi mkuu wa Her Initiative.
     Waliounga mkono shughuli hii ni Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kupitia serikali ya wanafunzi chini ya wizara ya jinsia.
     Wadhamini wa shughuli hii ya Panda ni GEPF, Shear Illusions, Vijana Inc na AJ Graphics. Tungependa kutoa shukrani za dhati kwenu.

  0 0

  The Benjamin W. Mkapa Foundation (BMF) a non-profit making TRUST has continued sustaining partnership with the Government, Donors, Private sector and Individuals that generously donate and grant finances to the Foundation to implement its 5 years Strategic Plan.

  Since 2012, Bank M has been partnering with the BMF for implementing their programmes targeting to combat HIV and Aids, maternal new born health and crisis of human resource for health benefitting million people in remote communities rural Tanzania.

  Speaking during the post event press conference, the BMF foundation CEO Dr. Ellen Mkondya-Senkoro thanked Bank M for their support, “The Foundation is specifically pleased to benefit from Bank M as our sole partner from the banking industry, whereas through their CSR policy it has for the past 4 years contributed significantly to the Foundation. We are pleased to see our partnership is maturing and further cemented with a signed bilateral memorandum of understanding between the two Institutions.

  We like to take this opportunity to thank Bank M for embracing the cooperation towards this noble course of improving health and well being of Tanzanians, especially in underserved areas” said Dr. Ellen.

  During the recent fundraising event held by BMF on 13 th April 2016 at the Golden Jubilee Towers in Dar es Salaam, BMF raised Tshs 1.17 Billion from different stakeholders, the event was also commemorating the foundation’s 10 year anniversary and launching of the foundation’s new name “The Benjamin W. Mkapa Foundation”.

  “On behalf of the Board of Trustees, Management and Staff of the Mkapa Foundation, we would like to convey our gratitude to all who have made the event a success. Furthermore, our sincere gratitude is extended to all invited stakeholders who attended the event and contributed to the success of raising funds for the good course.” concluded Dr. Ellen”.

  Bank M’s Chief Executive Officer (Designate) Ms. Jacqueline Woiso articulated that Bank M is proud to be part of the successful journey that the foundation has had in the past 10 years. “Our bank is always dedicated to supporting the community based projects. It is our policy to work together with other reputable organization in making a difference to the community and this project is clear confirmation of our commitment. Our bank will continue supporting such projects as our ultimate goal is to enhance community the welfare of the society” said Ms. Jacqueline.

  This is the 3 rd Fundraising event to be hosted by the Foundation with the aim of raising funds from Corporates, Parastatals and Individuals to support the health programme it undertakes across the country. This year’s purpose of raising funds is to co-support the Foundation’s five years Strategic Plan of 2013 – 2018 which is costed at Tshs136 billion and aims to benefit directly and indirectly at least 20 million people by 2018 through reinforcing HIV and AIDS services; Reproductive, Maternal, New born and Child health services; improving health workforce policies, systems and practices and enhancing community health education, promotion and awareness.

  The event was mainly sponsored by Bank M, other sponsors included Montage Limited, PSPF and Mwananchi Communication Limited.
  Bank M CEO (Designate) Ms. Jacqueline Woiso speaking during the post event press conference held at Hyatt Regency today, Bank M and Mkapa foundation were announcing the success of their partnership over the recently held fundraising dinner organized by the foundation in partnership with the Bank whereby a total of TZS 1.17Bln was raised. She is flanked by the Mkapa foundation CEO Dr. Ellen Mnkondya Senkoro.
  Benjamin Mkapa foundation CEO Dr. Ellen Mnkondya Senkoro giving a brief to the press during today’s post event press conference held at Hyatt today.

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  1.NINI MAANA  YA  KUUMIA  KAZINI.

  Kuumia  kazini  kunajumuisha  kila  jeraha  analolipata  mfanyakazi  wakati  akitekeleza  majukumu  yake  ya  kazi. Jeraha  laweza  kuwa  dogo  au  kubwa   lakini  litaitwa jeraha  tu. Katika maana  hii  yapo  mambo mawili  kwanza  jeraha  na  pili   wakati  ukiwa  kazini.  Ili  mfanyakazi  apate  stahiki  zake  ni  lazima  haya mawili  yatokee.

  ( a ) JERAHA  HUJUMUISHA  NINI.

  Jeraha  ni  pamoja  na  kidonda, kukatika  kiungo iwe  mkono ,  mguu,  kidole  au  vinginevyo, kuathirika  akili, magonjwa yaliyotokana  na  kazi  kwa  mfano  kansa  inayotokana  na  kemikali  za  viwanda, magonjwa  ya  ngozi, na athari  nyingine  za  kimwili  au  kiakili  zilizotokea   wakati  mfanyakazi  akiwa  kazini au  zilizosababishwa na  kazi   ya  mfanyakazi. 

  ( b ) NI  WAKATI  UPI  NI  WA  KAZI.

  Wakati  wa  kazi  ni  wakati  wote  ambao  mfanyakazi  atakuwa  akitekeleza  majukumu  yake  ya  kazi kwa  mujibu  wa  ratiba  ya  ofisi. Kuumia  ukitekeleza  kazi  za  kiofisi  nyumbani  kwako  hakuwezi  kuhesabika   kama  kuumia  kazini /wakati  wa  kazi. 

  Lakini  kuumia  ukiwa  safarini  kuelekea  mkoa  au  nchi  fulani  kutekeleza  majukumu  ya  kazi  ni  kuumia  wakati  wa  kazi.  Hii  ndiyo  tafsiri  yake.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya anapenda kuwatangazia Wananchi wa Bukombe na umma wote kwa ujumla kuwa maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Walimu Wilayani hapa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 18/05/2016 ni batili na hayana msingi wowote kwani hoja zote 17 ambazo waliziorodhesha zilishajibiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia barua yenye Kumb. Na. A.30/3/84 ya tarehe 16/05/2016. 
   Aidha Mkuu wa Wilaya amekitaka chama cha Walimu kama hakikuridhishwa na majibu ya hoja zao, bado kina nafasi ya kukutana tena na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Kuzungumzia masuala hayo badala ya kufanya maandamano ambayo yataathiri shughuli za mitihani ya “Mock” kwa kidato cha nne iliyoanza tarehe 10 hadi 20/05/2015 na ile ya “STEP” chini ya BRN kwa shule za sekondari iliyoanza tarehe 16 hadi 20/05/2016. 
   Kamati kuu ya Ulinzi na usalama ipo imara kudhibiti maandamano hayo na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa Amani katika Wilaya ya Bukombe. 

  Imetolewa na:
   Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
   Geita 
  17 Mei, 2016

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja (pichani) leo tarehe 18 Mei, 2016 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.

  Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
  Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 5/2015/2016 kilichofanyika tarehe 13 Mei, 2016 chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 310 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Mei, 2016.
  Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 45, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 37, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 90 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 138.


  Imetolewa na:
  Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje, 
  Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
  Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
                  DAR ES SALAAM
                     18 Mei, 2016.

  0 0

   Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif lililopo katika mtaa wa Mansfield  jijini Dar es Salaam. 
   Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif.
   Wafanyakazi wa duka la vifaa vya elimu la Tahfif wakiwa kazini.
   Baadhi ya vifaa vya elimu.
   Wafanyakazi wa duka la Tahfif wakiwa katika picha ya pamoja.


  Na Maria Inviolata
  “Lengo la kuuza vifaa vya shule kwa bei rahisi ni kutoa mchango wetu katika elimu kwa kuwauzia wateja wetu vifaa hivyo kwa bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi nchini” ni kauli ya Mkurugenzi wa duka  la vifaa vya shule na ofisini la Tahfif, Mohamed Merali.

  Kwa kuthibitisha kauli yake Merali anafafanua kwa lugha ya Kiarabu neno Tahfif maana yake ni “Rahisi”. Duka hilo linajihusisha zaidi na kuuza vifaa vya shule, ofisini, vifaa vya kompyuta na vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho.
  Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugenzi huyo anasema kuwa Tahfif ilianzishwa  kwenye miaka ya 1972 na baba yao na kukabidhi duka hilo mikononi mwa wanafamilia ili kuundeleza adhma yake ya kusaidia elimu nchini, wakisimamiwa na hayati Jargis Merali, ambaye alibuni mpango mwingine wa kudhamini burudani na michezo.

  Awali duka hilo lilikuwa maeneo ya Kariakoo tu, kwa juhudi za wanafamilia hao kuenzi kauli ya baba yao ya kuchangia elimu wakafungua duka lingine katikati ya jiji maeneo ya Posta.

  Mwandishi wa makala hii alipotaka kujua siri ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi kama haiathiri biashara hiyo au labda kuna njia nyingine  mbadala inayofidia gharama hizo, Mohamed anasema kuwa siri yao kuu ni kuuza kwa urahisi vitu vingi kwa muda mfupi na kuagiza vingine, kwani ukiuza kwa bei kubwa itakugharimu muda mrefu kumalizia bidhaa zako zilizo sokoni.
  Mkurugenzi huyo anasema kuwa ukiwa makini na faida ambayo kwa macho ya wengi inaoneka ni kidogo, lakini kwa wao ni faida inayojitosheleza kabisa.
  Mwandishi alipouliza inakuwaje  baadhi ya wateja wa Tahfif wa bidhaa za jumla wanauza ghali bidhaa hizo kwenye maduka yao, Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja hao kutoongeza sana bei, kwani jambo hilo linawaumiza wazazi walio wengi kwa kushindwa kununua mahitaji ya vifaa vya shule, ingawa kibiashara faida inatakiwa ili kulipa gharama na lengo la kibiashara, lakini kwa mfanya biashara makini haitaji kuweka bei ya juu katika biashara zake, jambo hilo linawaathiri wateja wake kwa njia nyingi.
  Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja wake wenye maduka ya vifaa vya shule na ofisini, kuuza vifaa hivyo kwa bei ambayo haiwaumizi wateja, lengo  kuu liwe ni pamoja na kusaidia wanafunzi ili wapate vifaa shule kwa urahisi, kwani jambo hilo litasaidia kuinua elimu nchini.

  Mteja wa duka hilo wa muda mrefu ambaye hakutaka jina lake litajwe, anasema kuwa alianza kununua vifaa vya shule tangu mwanae akiwa darasa la Kwanza hadi sasa ambapo mtoto huyo yupo Kidato cha Tatu, mteja huyo anatoa shukrani kwa duka hilo kwa kuuza vifaa hivyo kwa bei nafuu  na jirani yake aliyemuelekeza ilipo Tahfif, naye mteja mwingine Joseph Mwalugenge anasema kuwa  yeye ananunua vifaa hivyo dukani hapo kwa sababu mahitaji yake yote yanapatikana hapo. 

  Mteja mwingine wa muda mrefu dukani hapo, anasema inambidi kutoka Kigamboni ili kukidhi mahitaji yake ya kupata vifaa hivyo hapo Tahfif.
  Hivi sasa Tahfif inatoa huduma ya kuuza vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho, kama vile Kompyuta maalum na vifaa vyote vya kisasa vinavyohitajika watu hao.
  Tahfif inaagiza bidhaa zake kutoka katika nchi za China, Dubai na India, licha ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi, Tahfif hutoa misaada mbalimbali kwa watoto na watu wenye uhitaji kama vile kwenye vituo vya kulelea watoto yatima nakadhalika.
  Lengo kuu la maduka ya Tahfif ni kuendelea kutoa huduma ya kuuza vifaa vya kisasa zaidi vya Shule na  Ofisini ili kukidhi mahitaji ya Wanafunzi kwa kuinua elimu nchini, pia kutoa udhamini wa michezo na burudani kwa lengo la kuzalisha wanamichezo bora, anasema Mohamed Merali.

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya msingi Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameondokana na adha ya ukosefu wa madawati baada ya kukabidhiwa madawati 60 na kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris.

  Hivi karibuni, wanafunzi wa shule hiyo, pia walikabidhiwa madawati 100 na diwani wa kata hiyo ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Maridadi) ambaye alidhibitisha kwa vitendo adhma yake ya kuona tatizo la madawati linamalizika.

  Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahmoud Kambona, akizungumza jana wakati akipokea madawati hayo 60 kwa mkurugenzi wa kampuni ya Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, alisema huu ni wakati wa jamii ya wafugaji kupata elimu.

  Kambona aliwataka wazazi wa jamii ya wafugaji wa eneo hilo kutumia fursa ya kuwepo kwa madawati hayo kwa kuwahimiza wanafunzi wasome kwa bidii ili wapate elimu bora itakayowasaidia kwa siku za usoni kwani elimu ndiyo hazina.

  “Nimetembelea shule nyingi za msingi kwenye hii wilaya yangu lakini sijaona shule yenye maktaba kama yenu hivyo hongereni, ila wazazi mjitahidi kuwapa chakula wanafunzi wanaotoka mbali ili wasome vizuri,” alisema Kambona.

  Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hizo, Harpreet Brar alisema hiyo siyo mara ya kwanza kusaidia jamii inayozunguka eneo hilo kwani alishachangia sh10 milioni za ujenzi wa maabara na kusomesha wanafunzi wawili kila mwaka.

  Brar alisema pia katika kuhakikisha anaendelea kusaidia jamii ya eneo hilo alishatoa sh500,000 za ujenzi wa choo, alitoa madawati 75 na chakula kwenye shule ya Namelock na ataendelea kushirikiana kwenye suala maendeleo.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Sipitieck alitoa wiki mbili kwa uongozi wa kata ya Loiborsiret, kuhakikisha wanajenga nyufa zilizojitokeza kwenye baadhi ya madarasa ya shule hiyo.

  “Sisi jamii ya wafugaji ni matajiri mno kwani tuna mifugo mingi sasa itakuwa jambo la kushangaza kusikia eti darasa limeanguka na kusababisha matatizo kwa watoto wetu, hivyo mkarabati haya madarasa,” alisema Sipitieck.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar, wakiwa na moja kati ya madawati 60 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwenye shule ya msingi Loiborsiret.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar, wakifurahia jambo baada ya kampuni hiyo kugawa madawati 60 kwenye shule ya msingi Loiborsiret
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri, baada ya kumkabidhi madawati 60 ya shule ya msingi Loiborsiret yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar.

  0 0


  0 0

  KIJANA RAJAYI AYOUB MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA DUNIA YA USOMAJI QUR'AN KWA TAJWEED AMESHINDA NA KULITAKATISHA JINA LA TANZANIA KATIKA ULIMWENGU WA QUR'AN.

  HONGERA SANA RAJAYI AYOUB, HONGERA FAMILIA YA RAJAYI, HONGERA WAALIMU WA RAJAYI. KARIBU NYUMBANI UKIWA NA AMANI NA FURAHA. ALHAMDULILLAH.

  0 0


  Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipanda ngazi kuelekea kwenye pampu na valvu zilizofungwa kwenye mita ya kupimia mafuta(Flow Meter) wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji kazi wa mita hiyo.
  Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya(kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho ( wa pili kushoto) kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika moja ya valvu zilizoko kwenye mita hiyo, upande unaoendeshwa kwa kutumia mfumo wa digitali hali iliyosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Mita hiyo sasa inatumia mfumo wa analojia na hatua ya urejeshaji wa valvu hiyo katika hali yake ya awali inafanyiwa kazi na mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga mita hiyo.
  Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho ( wa pili kulia) akitoa maagizo kwa Mamlaka ya Bandari kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ikiwemo hitilafu ya kamera za ulinzi na baadhi ya valvu kwenye mita ya kupimia mafuta na kuwasilisha taarifa ofisi kwake ndani ya siku sita juu ya namna ya watakavyoshughulikia mapungufu yaliyojitokeza.
  Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho mwenye Kaunda suti) kuhusu ufanyaji kazi wa mtambo unaochuja mafuta kwa lengo la kudhibiti na kuzuia mafuta machafu kuingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
  Mita ya Kupimia Mafuta (Flow Meter) iliyojengwa eneo la kwa mwingira, mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam . Utaratibu wa kujenga uzio na paa kufunika mtambo huo unaendelea kupitia mkandarasi aliyepewa jukumu la kujenga mradi huo ili kukuimarisha ulinzi na usalama wa mita hiyo. Picha/Raymond Mushumbusi na Aron Msigwa.


  Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho (kushoto) kuhusu mfumo wa kompyuta wa mita ya kupimia mafuta unavyofanya kazi kwa kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa wa utendaji kazi wa mita hiyo.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Hebel Mhanga( wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho( wa pili kulia) kuhusu ufanyaji kazi wa mifumo ya kuendesha mita ya kupimia mafuta (flow meter) uliojengwa eneo la Kwa Mwingira Mji Mwema Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na katibu Mkuu huyo leo Mei 18,2016.
  Habour Master Kapteni Abdul Mwengamuno kutoka Mamalaka ya Bandari ya Dar es Salaam(kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho (kushoto) hatua za kuzingatia wakati wa upakuaji wa mafuta kutoka kwenye meli mpaka kwenye mita za kupima mafuta ambapo mafuta hayo huchujwa kuondoa uchafu kwa kupitia mitambo maalum iliyofungwa kwenye mita hiyo.

  Na. Lorietha Laurence - Dar es salaam.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi Dkt. Leornad Chamuriho ameupa siku mbili uongozi wa Bandari unaosimamia Mita ya Kupimia mafuta nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni jijini Dar es salaam kuhakikisha kuwa unatoa taarifa ndani ya siku mbili kuhusu hitilafu iliyojitokeza kwenye mfumo wa kufungua valvu za mita hiyo upande wa umeme.

  Aidha, ameuagiza uongozi huo kutoa taarifa kuhusu hitilafu ya kamera 2 za usalama zilizoungua na kushindwa kufanya kazi kwa takribani mwezi mzima. Katibu Mkuu huyo ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mita hiyo eneo la mji Mwema Kigamboni leo jijini Dar es salaam na kubaini upungufu wa utendaji wa baadhi ya maeneo.

  Maeneo hayo ni pamoja na kamera za kufuatilia mwenendo wa usalama wa mita hiyo, valvu zilizoshindwa kufanya kazi upande wa mfumo wa umeme hivyo kubakiwa na njia ya analoji kutokana na hali ya mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha jijini Dar es salaam. “Ifikapo Jumatatu nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua zilizochukuliwa na mnieleze lini ukarabati wake utakamilika pia ujenzi wa paa kuzuia athari ya mvua kwenye mita hii” amesema Dkt. Chamuriho.

  Ameongeza kuwa dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi katika viwango vinavyostahili ili kulinda mapato yanayotokana na mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali na hivyo kuongeza mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.Kwa upande wake Meneja Mradi wa Ujenzi wa Mita hiyo kutoka Mamlaka ya Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa hivyo vimeanza kukabarati.

  " Kisichofanya kazi ni mfumo wa kufungua mafuta upande wa umeme kwenye baadhi ya valve, upande wa analoji unafanya kazi vizuri na kazi ya upakuaji mafuta kupitia mfumo wa analojia inaendelea kama kawaida" Amesisitiza.Amesema kuwa tayari wamemweleza mkandarasi aliyefunga vifaa hivyo kuvifanyia marekebisho haraka iwezekanavyo.

  Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema kuwa ofisi yake inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja wanaotumia mitambo hiyo iliyopo bandarini hapo na Serikali inapata mapato kulingana na huduma iliyotolewa.Mita ya Kupimia Mafuta yalnayoingia nchini iko katika hatua ya majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa majaribio ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.

  0 0

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo ya siku tano, tarehe 16 – 20 Mei, 2016, kwa wadau wa udhibiti katika mnyororo wa Usalama wa Chakula hususan upimaji katika maabara Barani Afrika.
  Akifungua mafunzo hayo yaliyowashirikisha wadau wapatao 50 kutoka nchi 15 za Afrika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, alisema kuwa Lengo kuu la mafunzo na mkutano ni kujadili majukumu, wajibu na mchango wa kila mdau katika suala zima la kuhakikisha chakula ni salama kwa walaji.


  Dr. Mpoki alisema, “ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa wa namna bora ya usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa Chakula Salama kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau mliopo hapa’ .

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, wakati wa kutoa maelezo ya awali kuhusu mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za mionzi (IAEA), alieleza kuwa kufanyika kwa mafunzo haya nchini Tanzania ni heshima kubwa na ishara ya mwendelezo wa TFDA kufikia Dira yake ya kuwa taasisi inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa Tiba.


  Nchi zinazoshiriki katika mafunzo haya ni pamoja na Algeria, Benin, Botswana, Cameroon, Egypt, Ethiopia, Mauritius, Mali, Chadi, Namibia, Sudan, Tunisia, Uganda, Zimbabwe na Tanzania.
  Matokeo ya mafunzo haya yatakuwa ni dira ya utekelezaji wa mradi wa udhibiti wa mnyororo wa Usalama wa Chakula kabla ya kufikia mwisho wa mwezi Disemba 2016.

  Wadau wa mnyororo wa udhibiti wa Usalama wa Chakula walioshiriki katika mafunzo haya wanatoka kwenye maeneo ya maabara, ukaguzi, uzalishaji wa vyakula na walaji.


  Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akitoa maelezo ya awali katika ufunguzi wa mafunzo kwa washiriki wa Kongamano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Bara la Afrika. 


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya siku tano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Afrika. Wengine waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Bi. Charys Ugullum, Mwakilishi wa FAO na Mwakilishi wa IAEA, Bw. Alex Mulori. 

  0 0

  SHIRIKA la  Taifa la  Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.

  Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero. Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
  Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
  Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1223 | 1224 | (Page 1225) | 1226 | 1227 | .... | 3348 | newer