Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1224 | 1225 | (Page 1226) | 1227 | 1228 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi Dk. Leonard Chamuriho amesema kuwa kasoro ambazo zimejitokeza katika mtambo wa kupima mafuta Bandarini (Flow Meter) zinapatiwa ufumbuzi na mkandasi wa vifaa vya mitambo hiyo.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chamuriho amesema kuwa mtambo huo lazima uangaliwe kwa umakini kutokana na serikali ndipo inapata kodi yake halisi ya mafuta yanayoshuwa na meli.

  Amesema kuwa mkandarasi msambazaji vifaa kutokana na mkataba ni lazima ahakikishe kwa vitu viliyopata kasoro kutatua kabla ya tatizo halijawa kubwa au kutojirudia.

  Aidha amesema kuwa suala la kamera ambazo zimepata hitilafu baada ya kupigwa na radi zitengenezwe mara moja na tatizo lisijirudie wakati mwingine kutokana na umhimu wa kamera katika eneo hilo.

  Amesema kutokana hali hiyo amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari kupeleka taarifa jumatatu ikiwa na ina vitu vyote ambavyo vipo katika mradi wa mtambo huo.
  Kwa upande wa Meneja Mradi Mtambo wa kupima mafuta, Mhandisi Mary Mhayaya amesema kuwa jana kumetokea changamoto katika mtambo iliyotokana na mafuta kukwama kutokana na uchafu ambapo wameweza kusafisha.
  Aidha amesema katika majaribio wa mtambo huo umeweza kuwa na mafanikio baada ya meli tatu kushusha mafuta bila matatizo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi Dk. Leonard Chamuriho akipata maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Mtambo wa Kupima Mafuta wa TPA, Mhandisi Mary Mhayaya leo wakati ziara kushtukiza na katibu Mkuu huyo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi Dk. Leonard Chamuriho akiwa juu ya mtambo akiangalia miundombinu yake wakati wa ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kupima mafuta Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
  Mtambo wa Kupima Mafuta wa TPA,uliopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Zainab Nyamka TIMU ya Abajalo imefanikiwa kutoka na ushimdi wa goli 3-2 dhidi ya The mighty Elephant ya Songea na kufikisha alama 6 zitakazomruhusu kuvuka hadi ligi daraja la kwanza. 
   Abajalo ndio walioanza kufunga dakika ya 10 kupitia kwa Ally Saidi ambaye amefunga mawili na lingine dakika ya 77. 
   Waziri Omary akaipatia timu yake goli kwa mkwaju wa penati huku magoli ya The Mighty Elephant yakifungwa na Simon Minga na Raymond Lwambano dakika ya 46 na 90. 
   Kufuatia matokeo hayo Abajalo wameungana na Mvuvumwa wenye alama 6 sawa nao na kuweza kupanda hadi ligi daraja la kwanza  baada ya timu ya Pamba kuwa na alama 4 huku The Mighty Elephant akisalia na alama 1.

  0 0  Na Zainab Nyamka
  MABINGWA wa ligi kuu bara na wawakilishi wa michuano ya kimatufa timu ya Yanga imefanikiwa kuvuka hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho baada ya kuwaondoa GD Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya goli 2-1.
  Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo umemaliza kwa GD Sagrada Kutoka na ushindi wa goli 1-0 lakini wameshindwa kuvuka hatua hiyo baada ya mechi ya awali Yanga kushinda 2-0 wakiwa nyumbani.
  Kutokana na matokeo hayo, Yanga wameingia hatua ya makundi wakiungana na TP Mazembe pamoja na Etoile Du sahel huku mechi zingine zikiwa zinaendelea kuchezwa.
  Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni kwa saa za  Afrika Mashariki umemalizika huku beki wa Yanga na nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'canavaro' akitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 82 lakini juhudi za golikipa Deogratius Munish 'dida' aliweza kuokoa penati katika dakika za nyongeza na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa Yanga kufuzu hatua ya makundi
  Mechi hiyo ilijaa vurugu sana na mpira kuchezwa takribani dakika 100 huku Sagrada wakitafuta goli la kusawazisha,huku wachezaji wa Yanga Thaban Kamosoku, Amisi Tambwe na Dida wakipewa kadi za njano.

  0 0


  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Watuhumiwa wa Ubakaji Huko Dakawa,Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakipelekwa Kortini Mjini humo kusomewa Mashtaka yao mapema leo.


  Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro imewapandisha kizimbani washtakiwa sita wakikabiliwa na mashtaka matatu tofauti, wakiwemo washtakiwa wawili wanaokabiliwa na mashtaka na kubaka na kumuingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yake binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami Dakawa Wilayani Mvomero.

  Katika kesi hiyo iliyovuta hisia ya mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro, washtakiwa Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi  wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary Moyo, wakikabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti, wanalodaiwa kutenda aprili 27 mwaka huu majira ya usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo Wami Dakawa wilayani Mvomero.

  Upande wa Serikali katika shtaka hilo lililofanyika faragha kwa mujibu wa sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Calistus Kapinga. Washtakiwa wote wawili wamekana mashtaka na kesi hiyo imepangwa kufikishwa tena Juni Mosi mwaka huu  kwa ajili ya kutajwa.

  Upande wa mashtaka umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwa ajili ya usalama wa washtakiwa kwa vile shauri hilo limegusa hisia ya jamii na kwa  vile upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa wanaweza kuharibu upelelezi.
  Katika shtaka jingine lililofikishwa mbele ya Hakimu Ivan Msaki wa Mahakama hiyo, washtakiwa sita wakiwemo Iddi Mabena, Zuberi Thabiti na wengine wanne Rajab Salehe, Ramadhani Ally Makunja anayetetewa na wakili Ignas Punge, Muhsin Ngai na John Petter maarufu kama Paroko, wakazi wa Wami Dakawa wilayani Mvomero wanadaiwa kusambaza picha chafu na za ngono kwa njia ya mtandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka 2015.

  Washtakiwa wote sita wamekana mashtaka ambapo upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili watatu wa serikali uliomba washtakiwa wanyimwe dhamana kwa usalama wao na kutoharibu upelelezi kwa vile bado haujakamilika, huku ule wa mshtakiwa namba nne ukiomba kuwasilisha kiapo cha kupinga mshtakiwa kunyimwa dhamana, ambapo suala hilo la dhamana katika shauri hilo litafikishwa tena juni mosi kwaajili ya kujadiliwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

  0 0

  Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela amedhuria kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Iringa na kutoa rai kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanabuni mbinu mpya za kukusanya mapato zisizo waumiza wananchi, mfano gereji ya manispaa ingeweza kutumika kukagua magari kwa kushirkiana na polisi. 
  Katika hotuba yake alisisitiza suala la Ulinzi na usalama hasa ulinzi wa Mtoto na mama, kwani sasa imekuwa kawaida wanaume kupiga wake zao na kukosa utu. Pia watoto wana bakwa lakini taarifa hazifiki kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, zile zinazo fika ziapungikiwa ushahidi. 
  Mheshimiwa Kasesela amesitiza suala mipango miji endelevu yenye kufikiria mbali zaidi, nyumba zote ambazo hazifai kwa makazi wahusika waambiwe. Vichochoro vyote vilivyofungwa vifunguliwe ili kuondoa hali hatarishi. 
  Kwa upande wa elimu alitoa Msistizo mkubwa kwa kila diwani ulikuwa kuhakikisha kila shule inakuwa na madawati ya kutosha. 
  Baraza hilo lilifunguliwa na Mstahiki meya Mh. Alex Kimbe, pia alikuwapo Naibu meya Bwana Nzala Lyata, Mbunge wa Iringa mjini mh Peter Msigwa. Madwani walijadili mapendekezo ya vikao vya kamti mbalimbali na kupitisha maazimio yote.
  Mstahiki meya Mh Alex Kimbe akifungua baraza
  Mkuu wa wilaya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa rai kwa Manispaa ya Iringa kuongeza kasi ya kukusanya mapato
   Mh Peter Msigwa akichangia hoja
   Mh  Leah Mleleu Diwani viti Maalum (CHADEMA) akisiliza kwa makini
   Mh Nyalusi akichangia hoja


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Katika  saa  za  kazi  zipo  saa  za  kazi  katika  siku  za  kawaida, saa  za  kazi za  ziada   na  saa  za  kazi  katika  siku  ambazo  ni  za  sikukuu. Kuna  umuhimu  mkubwa  sana  kwa mfanyakazi  kujua  masaa  ya  kazi  . Kama  hujui  masaa  ya  kazi  ya  kisheria  basi ni  vigumu  kujua   usahihi  wa  ujira  unaolipwa .

   Malipo  ya  kazi  hayatokani  na  mshahara  pekee. Yapo  malipo  mengine  ya  ziada  yatokanayo  na  muda  wa  ziada zikiwemo  siku  za  sikukuu. Ili  ujue  usahihi  wa  kile  unacholipwa yakupasa  kujua pia mchanganuo  wa masaa  ya  kazi.  Masaa  ya  kazi  yapo  aina  mbili.

   Yapo  masaa  ya  kazi  ya  kawaida  na  yapo  masaa  ya  kazi  ya  ziada. Sikukuu  nazo  hujumuishwa  katika  masaa  ya  kazi  ya  ziada.


  1.JE  SAA  ZA  KAZI  NI NGAPI KATIKA SIKU  ZA  KAWAIDA  ?.

  Katika  siku  za  kawaida  saa za  kazi  ni 9.  Kwahiyo kwa  siku  mfanyakazi  anatakiwa  kufanya  kazi  masaa  9. Hii  ina  maana  atafanya  kazi  masaa   45 kwa  wiki ikiwa atafanya kazi  kuanzia jumatatu  mpaka ijumaa.

  Muhimu  sana  katika  suala la  saa  za  kazi  ni  kuwa  mfanyakazi asifanye  kazi  zaidi  ya  saa  45 kwa  wiki kwa masaa  ya  kawaida.Hata  siku  zikizidi  lakini  masaa  45  kwa  wiki  yasipite. Hayo  ni  masaa  ya  kawaida.

  2.  JE  SIKU  ZA  KAZI  NI NGAPI ?.

  Siku  za  kazi  zinazoruhusiwa  ni  sita  kwa  wiki. Lakini  itategemea na  taratibu  za  ofisi  yako. Zipo  ofisi  watakwambia tunafanya kazi   jumatatu  mpaka  ijumaaa  na  wapo  wengine  watakwambia  kazi  ni  jumatatu  mpaka  jumamosi. Hawa  wote  watakuwa hawajakosea  kwasababu  bado  wako  ndani  ya  ukomo  wa  siku  za  kisheria.

  Linalopaswa  kuzingatiwa  hapa  ni  kuwa  vyovyote  itakavyokuwa  masaa  ya  kazi  kwa  wiki  yasizidi  45.  Iwe siku  tano  kwa wiki au  sita  muhimu masaa  yasizidi  45  kwa  wiki.  Haya  ni  masaa  ya  kawaida.  Masaa  ya  kawaida  ni  yale masaa  ambayo  sio  ya  ziada.  0 0


  0 0

  Ndege ya abiria ya EgyptAir namba MS804 imepotea asubuhi hii ikiwa angani ikitokea Paris kuelekea Cairo ikiwa na abiria 56 na wafanyakazi 10. Juhudi za kuisaka zinaendelea.
  Ramani inayoonesha njia iliyopita hiyo ndege na chini ni moja ya ndege inayofanana na iliyopotea


  0 0

  Abidjan, May 18, 2016 – The Board of Directors of the African Development Bank Group (AfDB) through its private sector window has approved a USD 120-million line of credit (LOC) to CRDB Bank Plc (“CRDB”) in Tanzania.


  CRDB, the largest commercial bank in Tanzania, was established in 1969 and listed on the Dar es Salaam Stock Exchange in 2002.  CRDB has a wide geographical coverage of the Tanzanian market where it operates over 120 branches across the country and an additional 3 branches in Burundi. It supports various sectors such as power, manufacturing, agriculture and SMEs over the past years. In 2008, the AfDB provided a risk-sharing facility to promote SMEs in the agriculture sector, through which more than 270 SMEs have benefited.
   
  Since 2008, CRDB has expanded its SME loan portfolio and has partnered with more than 2,125 agents or non-banking intermediaries to widen its reach.  The agency banking has enabled CRDB to provide services in far-flung areas where establishing branches may be uneconomical hence efficiently allowing the financially excluded to access banking services.


  The LOC will help finance infrastructure and SME projects in Tanzania. It will support infrastructure development which is a major constraint for Tanzania’s economic growth. By leveraging CRDB’s branch network and agents, it will also scale up lending to SMEs and women enterprises in both urban and rural areas to create more jobs and to promote inclusive growth for Tanzania’s economy. The LOC will spur regional trade and promote regional integration through expanding capacity of the country’s port and airport, which will also stimulate tourism and government revenues.  


  Dr. Tonia Kandiero, Resident Representative, Tanzania Country Office


  International House, 5th Floor, International House, P.O Box 6024, Dar es Salaaam


  0 0

  Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa  lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL 2016.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi Amewahakikishia  Ulinzi na Usalama wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake pamoja na wageni wote  watakao hudhuria tamasha la Jembeka festival  2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ya tarehe 21 Mei 2016 katika kiwanja Cha CCM Kirumba kilichopo  jijini Mwanza.

  Kamanda Msangi ameyasema hayo  leo ofisini kwake alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (Jembejembe) Alipomtembelea kwa   lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee   nchini Tanzania.

  “Napenda kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza,wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania hili ni tamasha la kipekee hapa mkoani kwetu hivyo napenda kuwaasa wananchi wote kufurahi na kuhudhulia tamasha hilo kwa furaha  pia napenda kutoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani”,Alisema Kamanda Msangi.

  Kwa upande wake Dr. Sebastian Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa ushirikiano aliouonesha tangu awali na hili la sasa kuhakikisha anaimarisha ulinzi na usalama siku hiyo ya tamasha na kuahidi kutumia vyombo vyake vya habari katika kulisaidia jeshi hilo kutoa elimu ya ulinzi shirikishi.
  “Nashukuru sana kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Jeshi la polisi ngazi zote kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mwanza inakuwa salama hivyo mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kusimama bega kwa bega na jeshi letu kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake stahiki linapokuja suala la ulinzi, usalama wa mtu mmoja mmoja na hata utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namna ya kuzuia uhalifu, ili Mwanza yetu iwe mahali salama"
  Aidha Kamanda Msangi ameahidi kuimarisha Ulinzi  wa ndani na nje  kwa maeneo yote ya wilaya ya Ilemela ambako uwanja wa CCM Kirumba ndiko unakopatikana na amewatoa hofu Wananchi wote pamoja na wageni watakaohudhuria tamasha hilo kwa kuhofia usalama. "Atakaye kuja kwa hila tutamdhibiti"
  Tamasha la Jembeka festival 2016 mwaka huu litatumbuizwa na msanii kutoka nchi ya Marekani  Neyo anayetarajiwa kutua nchini kesho usiku.

  Wakali wengine kutoka hapa nchini Tanzania akiwemo Diamond, Juma Nature, Ney wa Mitego, Maua Sama, Ruby, Fid q, Mo Music, Baraka da prince, na wengine kibao,  wanatarajiwa kumwaga mvua ya burudani siku hiyo.
  JEMBEKA FESTIVAL linaloandaliwa na Jembe ni Jembe Entertainment kupitia Jembe FM, hufanyika kila Mwaka  mkoani Mwanza na  tamasha hilo kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu sabini toka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
  Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Katibu wa Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa  lengo la kumkaribisha kuwa miongoni  mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee  nchini Tanzania.
  Aksante sana Gazeti la Mwananchi toka Mwananchi Communication kwa kutusaidia kufikisha taarifa mlango kwa mlango PAMOJA SANA.
  Jumamosi hii, May 21,2016 itakuwa ni Jembeka Festival Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao. 
  Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so huu ni muda wa kununua tiketi mwana wa kwetu.
  Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi Blog, Michuzi Blog, DjChokaMusic.com, Lakairo Hotel na wadau wengine.


  0 0


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohammed akionesha mkoba wenye Bajeti ya Serikali ya Zanzibar ya mwaka wa Fedha 2016/2017 wakati alipokuwa akiingia Baraza la Wawakilishi kwa kuiwasilisha Bajeti hiyo.
   Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
   Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wakifuatilia Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 wakati Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Khalid Salum alipokuwa akiwasilisha Hutuba hiyo. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar. 
  Baadhi ya Mabalozi wadogo wanaowakilishi nchi zao Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohammed kuhusu mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serekali kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

  0 0

  The Board of Directors of the African Development Bank Group (AfDB) through its private sector window has approved a USD 120-million line of credit (LOC) to CRDB Bank Plc (“CRDB”) in Tanzania. 

  CRDB, the largest commercial bank in Tanzania, was established in 1969 and listed on the Dar es Salaam Stock Exchange in 2002.  CRDB has a wide geographical coverage of the Tanzanian market where it operates over 120 branches across the country and an additional 3 branches in Burundi. 

  It supports various sectors such as power, manufacturing, agriculture and SMEs over the past years. In 2008, the AfDB provided a risk-sharing facility to promote SMEs in the agriculture sector, through which more than 270 SMEs have benefited. 

  Since 2008, CRDB has expanded its SME loan portfolio and has partnered with more than 2,125 agents or non-banking intermediaries to widen its reach.  The agency banking has enabled CRDB to provide services in far-flung areas where establishing branches may be uneconomical hence efficiently allowing the financially excluded to access banking services.

  The LOC will help finance infrastructure and SME projects in Tanzania. It will support infrastructure development which is a major constraint for Tanzania’s economic growth. By leveraging CRDB’s branch network and agents, it will also scale up lending to SMEs and women enterprises in both urban and rural areas to create more jobs and to promote inclusive growth for Tanzania’s economy. 

  The LOC will spur regional trade and promote regional integration through expanding capacity of the country’s port and airport, which will also stimulate tourism and government revenues. 

  0 0
 • 05/19/16--00:50: BIASHARA ASUBUHI....


 • 0 0

  Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

  Maji ni rasilimali muhimu kwa maisha ya viumbe vyote pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote, ubora wa afya na mazingira kwa ujumla vinategemea kuwepo kwa maji yakutosha na yenye ubora unaotakiwa.

  Maji yana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii kwa kuwa hutumika kwa matumizi mbalimbali kama vile kuzalisha umeme,kupika, kuoga na kufua nguo, katika ujenzi na kusaidia maisha ya viumbe hai, matumizi ya viwandani pamoja na kilimo hivyo usimamizi na utunzaji wake lazima uzingatiwe.

  Serikali ina malengo ya kuwapatia maji wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, Mkoa wa Pwani, Kibaha pamoja na Bagamoyo kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2025.Hakika aja ya mja hunena, muungwana ni vitendo. Hii imethibitika kuwa kweli Serikali ya Awamu ya Tano inajali watu wake hasa wa hali ya chini kama Rais John Pombe Magufuli ambavyo hupenda kuwaita wanyonge. Watu wengi wanahitaji kuwa na maji ya bomba lakini uwezo wa kuunganisha ulikuwa mgumu kwani gharama wengi waliiona kuwa ni kubwa sana.

  Kwa kulitambua hilo Serikali imeamua kuingia gharama za kuwaunganishia maji wateja wake na wenyewe watalipia kidogo kidogo gharama hizo. Hili ni jambo la kuungwa mkono sana.Hapa tunamsikia mkazi wa Mbweni, Jijini Dar es Salaam, Bi Fatuma Iddi akisema,“Kwa kweli serikali hii imetukumbuka, mimi nilishapoteza matumaini ya kupata maji kwangu kwani sikuwa na uwezo wa kulipa malaki hayo kwa ajili ya kuunganishiwa. Lakini kwa kulipia kwa awamu hilo nitalimudu. Heko Mhe. Rais Magufuli kwa kutujali hasa sisi wanyonge.”

  Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Mkoa wa Dar es Saalam zinaeleza kuwa Mkoa unapata maji kutoka katika mito na visima ambapo eneo kubwa la Mji huo linahudumiwa na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) ambayo imepewa mkataba na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASA) na kwa maeneo yasiyo na mtandao wa DAWASA hupata maji kutoka kwenye visima vinavyoendeshwa na vyombo vya watu binafsi.


  0 0

  Khadija Khamis na Mariyam Kidiko – Maelezo Zanzibar 19/08/2016.

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupandisha kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 150,000 cha sasa hadi TZS300,000 kuanzia mwezi April mwakani .

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati akisoma Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016-2017 katika Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje kidogo wa Mji wa Zanzibar .

  Alisema serikali imekusudia kutekeleza ahadi yake ya kuimarisha maslahi ya wafanyakazi hususan wa kipato cha chini ili waweze kumudu vyema maisha yao na kuhamasika kufanya kazi kwa bidii.

  Aidha alisema kuwa serikali imekusudia kupunguza kodi katika kipato cha mshahara wa wafanyakazi na kuweka viwango vyake sawa na Tanzania Bara ili kwenda sambamba na hatua ya kupandisha kima cha chini cha mshahara

  Pia aliwataka wafanyakazi kujituma zaidi kwa ufanisi ili kuongeza tija na kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kukuza kwa haraka uchumi wa nchi na kuongeza wigo wa mapato ya serikali na kupunguza mzigo mkubwa wa matumizi yasiyo ya msingi.

  Dkt Khalid alisema kwa kuzingatia malengo makuu ya Serikali na mustakabali wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha katika kila shilingi inayotumika senti 58.7 ziende katika sekta tano zinazobeba malengo makuu ya serikali .

  Akizitaja sekta hizo ni Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji ,Elimu na Mafunzo ya Amali ,Afya ,Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira na Kilimo ,Maliasili , Mifugo na Uvuvi ambapo zinatarajiwa kutumia jumla ya shilingi TZS 494.2 bilioni kati ya TZS841.5 bilioni za matumizi ya Serikali .

  Aidha Waziri huyo alisema Serikali haikusudii kupandisha kodi yoyote katika vianzio vyake vya mapato ya ndani zaidi na kurekebisha viwango vya ada mbali mbali vilivyopitwa na wakati na badala yake inatajia kupanua wigo wa kodi kwa kuimarisha ufanisi katika ukusanyaji na kuongeza uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato.

  Aidha alifahamisha kuwa kutokana na hali ya muelekeo wa fedha sera kuu ya matumizi inahitaji kubana zaidi matumizi kulingana na vianzio vya mapato vilivyopo kwa kupunguza madeni hasa ya kiinua mgongo, walimu, wazabuni na Dhamana za hazina .

  Hata hivyo waziri Khalid alieleza serikali itaendelea na jitihada zake za kuwaenzi wazee kwa kuendelea kutoa pencheni maalum kwa wazee waliofikia umri wa miaka sabini na zaidi kwa kiwango cha TZS 20,000 kwa kila mwezi kwa wazee wote wa Unguja na Pemba.

  Katika kutekeleza malengo Waziri Khalid ameliomba Baraza hilo liidhinishe Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 yenye mapato ya jumla TZS 841.5 bilioni zikiwemo TZS 482.4 bilioni za mapato ya ndani, TZS 324.8 bilioni kutokana na Ruzuku na Mikopo ya nje, TZS 1.3 bilioni kutokana na misamaha ya madeni na bilioni 33.0 bilioni za mikopo ya ndani.

  Pia ameomba kuidhinishwa matumizi ya 841.5 bilioni ikiwa TZS445.6 bilioni kwa matumizi ya kawaida na TZS 395.9 bilioni kwa kugharamia Mpango wa Maendeleo.

  0 0


  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rshid Ali Juma akizungumza na wafanyakazi na wananchi walioshiriki maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazi mmoja Zanzibar.


  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya kudumu ya sanaa katika maadhimisho ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

  Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdalla akimuonyesha Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo sanaa ya ufumaji kofia za asili ya Zanzibar katika maonyesho ya sanaa yanayofanyika makumbusho ya Mnazimmoja.

  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akiangalia kazi ya ubunifu iliyofanywa na msanii Naaman Ali Khamis wa kwanza (kulia) anaetumia majani makavu ya migomba.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
   

  0 0

   
  Jacquiline Mrisho-MAELEZO, Dodoma
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amewataka Mawakili wa Serikali kuwa makini na kutoa ushauri kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu pindi wanapotoa ushauri wa kisheria kuhusu mikataba mbalimbali.Mhe. Masaju ameitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na Mawakili wa Serikali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayohusu uhakiki wa mikataba ya ununuzi wa umma leo Mjini Dodoma.

  Alisema ni vyema wakatekeleza jukumu hilo kwa makini kwani ushauri unaotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia mawakili hao ndio msimamo wa Serikali.“Ninapenda kuwakumbusha kwamba ninyi ni watumishi wa umma na mnaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na kanuni zake za mwaka 2003” alisema Mhe. Masaju na kuongeza kuwa:

  “Kama walivyo watumishi wengine wa umma na kwa msingi huu, ninyi ni sehemu ya Serikali na nafasi yenu katika Serikali ni kubwa”.Pia aliwataka wanasheria wa Serikali kujengewa uwezo kuhusu uhakiki wa mikataba na iwapo watashindwa kutekeleza wajibu huo ipasavyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu.

  Alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa thamani ya mikataba inayohakikiwa na wanasheria wa taasisi ya manunuzi ni wazi kwamba kuna umuhimu wa Maafisa Sheria kupatiwa mafunzo hayo.“Wanasheria wa Serikali wanaohakiki mikataba hii wanawajibika kuzingatia sheria zinazohusiana na mikataba husika pamoja na maadili ya Wanasheria wa Serikali katika Utumishi wa Umma kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 27 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 2005”,alisema Mhe. Masaju.Mhe. Masaju alishauri utaratibu wa mikataba yote kuhakikiwa Dar es Salaam ubadilike kwani unasababisha ongezeko la gharama kwa taasisi za Serikali na kuchelewesha miradi.

  Alifafanua kuwa Divisheni ya Mikataba iko Makao Makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee hivyo, mikataba yote ya mikoani ni lazima ipelekwe Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikiwa.“Hii inasababisha wadau hasa wa kwenye Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa, Jiji na wengine walioko mikoani kusafiri na kupeleka mikataba Dar es Salaam kwa ajili ya uhakiki” alisema Mhe. Masaju.

  Hivyo alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeona umuhimu wa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko Mikoani ili hatimaye baadhi ya Mikataba kutoka kwa wadau walioko wilayani na mikoani iwe inapelekwa katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko mikoani.

  0 0


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo leo Bungeni mjini Dodoma 19 Mei, 2016.
  Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mhe. Cecilia Paresso wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.
  Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
  Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (mwene gauni la kitenge) akiwa na baadhi ya Wabunge wakielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA. MAELEZO, DODOMA.

older | 1 | .... | 1224 | 1225 | (Page 1226) | 1227 | 1228 | .... | 3283 | newer