Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO,JAMES MBATIA AANDAA JIMBO LAKE KUKABILIANA NA MAJANGA (NDENGA).

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akichokoza mada wakati wa kongamano la Elimu juu ya maafa katika jimbo hilo baada ya kukumbwa na mafuriko ,Kongamano lililofanyika katika shule maalum ya Viziwi na kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa,Vijiji na Vitongoji,Maofisa watendaji,Madiwani,wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo hilo.
Baaadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akichangia mada katika kongamano hilo ambalo alikuwa mgeni rasmi pia,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia na kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
 

SERIKALI IMEZITAKA TAASISI ZAKE KUFUATA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA YA MWAKA 2011

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Serikali imezitaka taasisi zake zote kufuata sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na taratibu zake kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi ili kuhakikisha fedha iliyotumiwa inalingana na huduma iliyopatikana.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga kwenye Mafunzo ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kwa Mawakili wote nchini iliyofanyika mjini Dodoma.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yamelenga kuwapa mawakili ujuzi katika utoaji mzuri wa ushauri wa kisheria kwa Taasisi za Serikali.

Wakili Mwandamizi Sanga alisema kuwa msingi mkubwa wa sheria hiyo ni ushindanishwaji wa wazabuni unaoweza kuiletea Serikali thamani ya fedha.“Kila taasisi ya serikali lazima ifuate sheria ya manunuzi kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi,sheria hii imeweka utaratibu wa kuhakikisha fedha iliyotumiwa inalingana na huduma inayopatikana”,alisema Sanga

Akitoa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mikataba (Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) Bi.Monica Otaru alisema mafunzo hayo yatawasaidia mawakili kufanya upekuzi wa mikataba kwa makini na uhakika zaidi.“Pamoja na kuwa kazi ya kupekua mikataba ni sehemu ndogo ya kazi zetu lakini inachukua muda mwingi, hivyo mafunzo haya yatawaandaa Mawakili wa Serikali walioko katika Ofisi za Kanda kuweza kufanya upekuzi wa mikataba kwa umakini na uhakika zaidi”,alisema Bi. Otaru.

Aidha, Bi. Otaru amezitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kazi ya uhakiki wa mikataba kutofanyika kwa usahihi zikiwemo za mikataba kukosa maelezo na maoni kamili ya taasisi husika.Alitaja changamoto nyingine kuwa ni gharama za kusafirisha mikataba kutoka taasisi husika,ugumu wa njia za mawasiliano pamoja na kutoshirikishwa kwa taasisi husika katika mchakato wa manunuzi na uandaaji wa mikataba.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi Divisheni ya Mikataba, Said Kalunde ameelezea juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kufanya upekuzi wa mikataba ya ununuzi ikiwemo ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika katika uhakiki wa mikataba kwa mujibu wa Sheria hiyo ya manunuzi.

“Ni muhimu sana kwa wakili kujiridhisha kama taratibu za ujazaji wa fomu zimefuatwa na fomu zimejazwa kwa usahihi,endapo wakili hatojiridhisha kwa kuhakiki fomu hizo huenda akapatwa na matatizo makubwa ya kiutendaji”,alisema Kalunde.Mafunzo hayo yametolewa kwa mawakili wa serikali divisheni ya mikataba ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza jukumu la kuhakiki mikataba inayotokana na wazabuni.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeundwa chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mshauri wa masuala ya kisheria kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kifungu cha 59(3) cha Katiba ya mwaka 1977.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga akifafanua kuhusu matumizi ya sheria ya manunuzi ya umma na umuhimu wake leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Mawakili wa Serikali waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo yaliyofanyika leo Mjini Dodoma.
 

APPRECIATION

Kipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London
Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.

Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA
Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.
Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.
Karibu

Meya wa jiji Dar aipongeza Klabu ya Yanga kwa kunyakua Ubingwa.

$
0
0
Na Eliphace Marwa - Maelezo

Meya wa Jiji la Dare s Salaam Mh. Issaya Mwita ameipongeza klabu ya Yanga kwa kunyakua ubingwa huo kwa mara ya Ishirini na Sita tangu kuanzishwa kwa mashindano ya ligi kuu hapa nchini.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mh. Mwita amesema ushindi wa Klabu ya Yanga umeliwezesha Jiji la Dar es Salaam kuendelea kupata sifa katika medani ya Kitaifa na Kimataifa kutokana na ushiriki wa klabu hiyo katika mashindano ya kimataifa.

“Ninaiomba klabu ya Yanga kuthamini ubingwa wao kwa kuonyesha viwango vya kimataifa ili kulifanya jiji hili kuwa chuo cha mafunzo ya mchezo wa mpira wa miguu,” alisema Mh. Mwita.

Aidha aliliomba Shirikisho la Mchezo wa MPira wa Miguu nchini (TFF) kuendelea kusimamia ligi kwa ustadi  zaidi ili kulingana na taratibu za mpira wa miguu kama zinavyoainishwa na Shirikisho la  Soka duniani (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

“Naomba nitoe wito kwa wadau wote katika familia ya mpira wa miguu kushirikiana ipasavyo ili kufanya ligi yetu iwe miongoni mwa ligi bora barani afrika na Duniani kwa ujumla,” aliongeza Mh. Mwita.

Pia aliwapongeza wadhamini wote waliojitolea kusaidia ufadhili kwa vilabu vyote vilivyoshiriki ligi kuu na kuwataka waendelee kuwasaidia ili kuinua soka letu la bongo.

Aidha ameitakia klabu ya Yanga ya Jangwani maandalizi mema katika mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua  za makundi ya kombe la Shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika (CAF) dhidi ya klabu ya Sagrada Esperance huko nchini Angola.

Lady Jaydee - NdiNdiNdi (Official Music Video)

Serikali yakanusha kuhusu Mashine za kukoboa mpunga na mahindi

$
0
0
Halmashauri ya Kahama kufanya kazi saa 24.

Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

SERIKALI imekanusha madai kuhusu mashine za kukoboa mpunga na mahindi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama kufanya kazi wakati wa usiku au saa 24.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali kuviruhusu Viwanda Wilayani Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika wakati wa mchana.

Akijibu swali Mhe. Jafo amesema kuwa, Serikali haijatoa zuio lolote kwa Halmashauri hiyo kwa mashine za kukoboa nafaka kufanya kazi nyakati za usiku ambapo amefafanua kuwa changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vinatumia umeme wa jenereta ambao umekuwa hautoshelezi kuendesha mashine wakati wote hali iliyopelekea kuwepo kwa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.

“Halamshauri imewasiliana na Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) Kahama na yatari tatizo hilo limeanza kushughulikiwa ili kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha usamabazaji kimeanza kujengwa Kahama”, alisema Mhe. Jafo.

Ameongeza kuwa, Halmashauri wilayani hapo inahamasisha Wawekezaji wa viwanda vidogo vikiwemo vya kukoboa mpunga, mahindi pamoja na mazao mengine ili kupanua wigo wa mapato kupitia ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.

“Hakuna sababu yoyote kwa Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekanavyo kwa kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unakuwepo.

kijipu upele katikati ya jiji la dar es salaam, aibu tupu...

$
0
0
Kwa takriban miaka mitatu sasa mtu asiyefahamika na ambaye anasadikiwa ana changamoto ya ufahamu wa akili ,anaishi katika upenyo wa mnara wa saa hiyo iliopo katika makutano ya barabara za Nkrumah, Relwe na Samora katikati ya jiji la Dar es salaam. Hapo anapika, anakula, anafua nguo na analala, ikiwa ni robo kilomita tu kutoka makao makuu ya halmashauri ya jiji. 
Kama hiyo haitoshi mnara huo uko katika hali mbaya na bustani yake inatia huruma. Mnara huu ulijengwa miaka takriban 85 iliyopita kama kumbukumbu ya  Dar es salaam kufanywa jiji.Wahusika mpo?

VIJIPU UPELE KWENYE NJIA YA MABASI YAENDAYO HARAKA YA DART JIJINI DAR ES SALAAM - WATANAANIA TUMEROGWA NA NANI??

$
0
0
 Basi la DART likiwa limegongwa na gari  ndogo leo asubuhi katika makutano ya barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es salaam na kuzua mtafaruku mkubwa
 Gari linalosadikiwa kugonga basi la DART leo
 Dereva akiripoti ajali makao makuu
Jana Magomeni Mapipa kijana mmoja aligonga basi la DART wakati akivuka. Chini ni taswira iliyosambaa mitandaoni bila maelezo ya kina ila inaonesha kuloikuwa na tatizo 

UTATA KABURI LA MWANAFASIHI SHAABAN ROBERT KUSHUGHULIKIWA

$
0
0

 Shaka akiwa na ujumbe wake  waliozuru katika kaburi la mwandishi gwiji wa vitabu vya fasihi andishi na simulizi marehemu Shaaban Robert kijiji cha Mjimwema mkoani Tanga

Na Woinde Shizza,Tanga
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) umesema utaieleza serikali mkoani Tanga kuondosha utata na mivutano iliopo katika kijiji cha Mjimwema kati ya familia mbili husika mahali ambako  amezikwa mwandishi bingwa wa vitabu vya fasihi simulizi na uandishi Marehemu  Shaaban Robert.
Tamko hilo limetamkwa na Kaimu katibu Mkuu wa Uvccm Shaka Hamdu Shaka aliyefika katika kaburi la Mwandishi huyo nguli katika  Afrika mashariki aliyezaliwa January 1, 1909  na kufariki  Juni 20,  1962 .
Shaka mara baada ya kusafisha kaburi la marehemu na kuomba duwa akiwa na ujumbe wake alielezwa na mjukuu wa marehemu Khatib Mwinjovu kwamba mahali hapo alipozikwa babu yake Shaaban Robert pamekuwa na mivutano isio na ulazima toka upande wa familia ya mke wa marehemu Robert.
Alisema kaburi hilo ni alama kuu katika Taifa letu  hivyo halipaswi kuandamwa kwa mivutano au misuguano isio na sababu na kuahidi kwamba seeikali itatumia uwezo wake kuleta mapatano haraka.
"Nitaongea haraka na mkuu wa mkoa wa Tanga kuhusu utata huu. UVCCM ingependa kuona kaburi la mwandishi huyo bingwa anayetajika duniani linatunzwa kwa heshima zote. Huyu mtu ametumia maisha yake yote kuandika ili kuvielimisha vizazi na vizazi hadi sasa.
Aidha  shaka aliitaka jamii kutambua na kuheshimu nguvu alizozitumia marehemu Shaaban Robert  katika uhai wake ambazo sasa alisema zinafaa katika kizazi hiki hadi kingine wakati yeye akiwa hapati  tija wala faida.
Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa Tanga Shija Othman Shija alisema uamuzi wa UVVCM kuja kulizuru kaburi hilo ni tendo la kiungwana hivyo akatoa wito kwa jumuiya nyingine nazo kuiga mfano huo.
Shija alisema ni jambo lisilowezekana kuzungumzia nchi yetu kabla na hata baada ya uhuru bila kulitaja jina la marehemu Shaaban Robert kutokana na mchango wake mkubwa hasa katika mitaala ya elimu na ukuzaji lugha ya kiswahili.
"Shaaban Robert amekuwa nguzo na kioo ambacho hakutavunjika wala kuingia nyufa wakati wote, maandiko yake yatabaki katika kurasa muhimu toka kizazi kimoja hadi kingine "alisems katibu huyo wa ccm mkoa.

Introducing Ajira App - Ajira moja kwa moja kwenye simu yako ya kiganjani...

$
0
0
Ajira ni application pekee ya simu ambayo inakutafutia mtumiaji kazi and inakwambia kwa kiwango gani umekidhi mahitaji ya  kazi iliotangazwa. Ajira imebuniwa hapa tanzania kwa watanzania, ni rahisi sana kutumia. Zahidi ya kukutafutia kazi mtumiaji, Ajira pia ina huduma ya mawasiliano yani messaging system ambayo inakuwezesha mtumiaji kuwasiliana na muajiri moja kwa moja kupitia application bila hata kuhitaji email au simu ya muajiri.
Ajira pia itakufahamisha kupitia simu yako kwa njia ya notification japo kazi ikitangazwa ambayo umekithi mahitaji yake.  Ajira inarushwa hewani Jumatatu ya tarehe 16 mwezi huu wa mei, lakini kabla hata ya kutangaza rasmi application yetu watu wengi tayari wanaitumia na pia watu zaidi ya elfu hamsini wanatufollow kwenye social media channel zetu.
Ajira inapatikana kwenye google play store kwa kuandia "Ajira Job" au kwa kupitia link ya hapa chini
Na pia unaweza kutembelea www.ajirascore.com
kupata maelezo zaidi.

MKUTANO WA WAMILIKI WA MAGAZETI NA MSAJILI WA MAGAZETI

MAKONDA ASHITUKIA MCHEZO MCHAFU WA KUFANYA GARI ZA SERIKALI KUUZWA.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
BAADHI ya watumishi Serikali wamekuwa wakifanya ujanja ujanja wa kuharibu magari ya Serikali ili waweze kutengeneza mazingira ya kuyauza kwa watumishi   hao wa ndani ofisi hiyo  hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitoa magari nane yaliyoenda kutengenezwa na Umoja wa Mafundi Gereji wa Wilaya Kinondoni ikiwa ni kujitolea ili watumishi waweze kutekeleza majukumu yao bila kuleta vizingizio vya kukosa usafiri.

Makonda amesema kuwa gari zinaharibika kitu kidogo lakini hayatengenezwi kwa muda muafaka na kufanya gari hizo kuharibika wakati zikiwa zimegeshwa na baadae kufanya mnada na wanunuzi wa gari hizo ni watumishi.
Amesema kuwa gari hizo zikitengenezwa, na madarevawakiziharibu kwa makusudi basi mshahara wake utakatwa kwa ajili ya kutengeneza gari ambalo limeharibiwa naye.
Aidha amesema kuwa watumishi wanashindwa kuwatembelea wananchi kutokana na kukosa usafiri wakati magari yamekaa kwa muda mrefu na kuendelea kaharibika.
Nae Katibu wa Mfundi Gereji Wilaya ya Kinondoni, Abdallah Rashid amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano na mkuu wa mkoa katika kuhakikisha magari yanakuwepo na watumishi waweze kuwatembelea wananchi kujua matatizo  yao.

DIRA YA DUNIA JUMATATU 16.05.2016

SERIKALI KUWAWEZESHA WANANCHI KUPATA TAARIFA NA HUDUMA MBALIMBALI KUPITIA SIMU ZAO.

$
0
0
 Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
17/5/2016.

SERIKALI kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia kazi suala la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi kupata huduma na taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi mahali popote walipo kwa njia ya mtandao.

Utaratibu huo pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini Tanzania kupata taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba nafasi hizo, kufuatilia majibu ya usaili walioufanya na kupata taarifa za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia ujumbe mfupi (sms).

Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa   mfumo huo utamuwezesha mwananchi kupata huduma za Serikali mahali popote alipo kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na kubadilishana taarifa.

Amesema kuwa dhana ya Serikali Mtandao  ni kuwa na matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli zote za Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kwenye huduma za Afya, Utalii, Malipo ya tozo za huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma mbalimbali za Serikali.

Dkt. Jabiri amesema  moja ya vitu vinavyosababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosekana kwa Serikali mtandao ni pale wanapohitaji kupata huduma za Serikali ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika kwenda Idara ya Uhamiaji kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi ya wiki moja ili taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za Serikali wakati suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.

“Matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa taarifa  kwa kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa haimlazimu mwananchi kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma yake” Amesisitiza Dkt. Jabiri.


Dkt. Kigwangalla awataka wanafunzi kupenda kusoma masomo ya Sayansi nchini.

$
0
0

Baadhi ya wanafunzi wa waliohitimu kidato cha Sita katika Mahafali ya 19 ya Shule ya Wasichana ya St. Marys Mazinde Juu wakiwa katika mahafrali hayo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mku wa shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba wakati wa kuwasili katika eneo la Mahafali ya 19 ya kidato cha Sita ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Lushoto Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea hutuba ya wanafunzi hao wa kidato cha sita.
 (Picha zote na Andrew Chale.Lushoto Tanga).
Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.


Rai hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.

SERENGETI BOYS WATAKATA INDIA, WASUBIRI MECHI MOJA KUINGIA HATUA YA NUSU FAINALI.

$
0
0

Na Zainab Nyamka,wa Globu ya Jamii.

Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 17, 2016 imechanua vema baada ya kuilaza India mabao 3-1 katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani katika dakika ya 21 wakati lile la pili India walijifunga baada ya beki wake kuhangaika kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28 wakati lile la tatu lilifungwa na Asad Juma katika dakika ya 48 huku lile la India likifungwa na Komal Thatal katika dakika ya 38.

Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa wanasubiri angalau sare au ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini utakaopigwa Alhamisi Mei 19, 2016 na Malaysia Mei 21, 2016 ili icheze nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Mei 12 kabla ya kufikia fainali zake Mei 26, mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoka sare ya Marekani ya bao 1-1.

Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliwakilishwa na Ramadhani Kabwili, Ally Nganzi, Ally Msengi, Asad Juma, Dickson Job, Issa Makamba, Maziku Amani, Nickson Kibabage, Shaaban Ada, Syprian Mtesigwa na Mohammed Abdallah.

India: Mohammed  Nawaz, Reamsochung Aimol, Boris Singh, Mohammed Khan, Juendra Singh, Suresh Wangjam, Amarjit Kiyam, Khumanthem Meetei, Sandjev Staldi, Aniket Jadhav na Komal Thatal

VIJIPU UPELE BADO KERO BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

$
0
0
Hivi jamani baadhi yetu tutabadilika lini? Kwa nini hatutaki kuyaelewa ama kuyakubali mabadiliko ya kimazingira. Wewe umeambiwa hiyo ni barabara maalum ya magari ya mwendo kasi lakini bado kutokana utashi wako unaoujua wewe unaona aaahh.. kawaida tu.
Tazama hilo gari la wagonjwa tunaweza kusema lilikuwa linakwepa foleni kwa sababu maalum, lakini hilo gari la nyuma unaweza kujiuliza lilikuwa likifuata nini kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi. Tukisema hiki ni kipele na kikiachwa kitakuwa jipu ni kosa? Wahusika tuongeze bidii kidogo kupambana na hivi vijipu upele ambavyo dawa yake si ni kuvibinya tu.

KESSY ADAIWA KUIHUJUMU SIMBA, AJIB KUADHIBIWA NA KAMATI YA MAADILI, MAFISANGO AKUMBUKWA

$
0
0
Rais wa Simba Evance Aveva akifafanua jambo
NA Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Simba umelaani vikali kitendo cha Hassan Kessy na Ibrahim Ajib kufanya vitendo nje ya mkataba wao na kusema ni usaliti kwa klabu hiyo.









Kessy (kulia) alisimamishwa na uongozi wa Simba baada ya kukutwa na kosa la kufanya madhambi kwa makusudi na kupelekewa kupatiwa kadi nyekundu katika mchezo wao dhidi ya Toto uliomalizika kwa Simba kupoteza mechi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Simba Evance Aveva amesema kuwa kitendo cha Kessy kusaini katika klabu nyingine akiwa bado ana mkataba na Simba kinaonekana ni kitendo cha kihuni na kinachothibitisha kuwa amekuwa anahujumu timu.
Ajibu  (kulia) naye amefanya kosa lililopelekea kupata kadi nyekundu na usiku huo huo majira ya saa 3 usiku anapiga simu na kusema kuwa amepata timu anakwenda kufanya majaribio nchini Afrika kusini amesema  Aveva.
"Hawa wachezaji wawili wameonyesha ni wamekuwa wanahujumu timu na tumeona makosa wanayoyafanya ni ya wazi kabisa,"amesema Aveva.
Aveva amesema kessy amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu lakini ameshasaini kwa wapinzani wetu na tumeliona hilo na ligi ikiwa bado haijaisha na ushahidi upo kutokana na matendo yake yote aliyokuwa anayafanya.
Kwa upande wa Ajib, kamati ya maadili itaangalia namna gani watamuadhibu kulingana na kitendo cha kufanya kosa na kisha kuaga kwenda nchini Afrika kusini.
Wakati huohuo, klabu ya Simba inafanya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mchezaji wao Patrick Mutesa Mafisango aliyefariki Mei 17 2012 kwa ajali ya gari.
Mafisango (kushoto) alifariki mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu iliyoishia kwa Simba kuwa mabingwa huku akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli na katika ligi pamoja na kufunga goli la mwisho.
Akitoa salamu hizo za maombolezo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kuwa bado watakuwa na kumbukumbu hiyo daima kwani Mafisango alikuwa ni moja ya wachezaji  waliokuwa na kipaji kikubwa sana."Daima tutaendelea kumkumbuka sana kwani ni moja ya wachezaji wenye kumbukumbu kubwa sana katika klabu yetu ya Simba na mpira kwa ujumla,"amesema Manara
Manara amesema kuwa wataendelea na utaratibu wao wa kumuombea kila mwaka ikiwa ni moja ya kumbukumbu yao muhimu, Baada ya kufariki kwa Mafisango, Klabu ya Simba waliamua kuweka heshima kwa kutokuitumia tena jezi namba 30 ambayo ilikuwa inavaliwa na mchezaji huyo mwenye asili ya Kongo.

YANGA KAMILI KUWAVAA WAANGOLA KESHO KOMBE LA SHIRIKISHO

$
0
0

Na Zainab Nyamka 
wa Globu ya Jamii

KIKOSI cha timu ya Yanga kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Sagrada Esperanca Kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirishiko barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca nchini Angola.
Yanga imewasili salama mjini Dundo, Angola jana jioni baada ya safari ya kutwa nzima huku wachezaji wakionekana kupata usumbufu wa kubadilisha usafiri pamoja na baadhi yao kupoteza mabegi.
Meneja wa timu Hafidhi Saleh amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya wenyeji ambapo anajua mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao.
Amesema, wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya maandalizi ya kesho ila asubuhi watafanya mazoezi ya mepesi mepesi.
"Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho lakini kesho asubuhi watafanya yale mepesi mepesi kuelekea mchezo wa kesho ambao ni muhimu sana kwetu,"amesema Saleh.
Saleh amesema, wanatarajia kesho watahakikisha wanapafa ushindi hasa baada ya wachezaji wao wawili ambao hawakucheza kwenye mechi ya Jijini Dar es salaam watakuwemo kwa ajili ya kuongeza nguvu.
"Ngoma na Kamosoku wamejumuika katika kuelekea mchezo huu hasa baada ya ule wa awali kuwepo jukwaani wakiwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano walizozipata kwenye mchezo wa Al Ahly,"amesema Saleh.
Saleh amesema hali za wachezaji wote zipo vizuri na wamejiandaa kuweza kushinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao na kama watafanikiwa kushinda basi watasonga mpaka hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images