Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

ukarabati wa Mv magogoni waendelea vyema

$
0
0
 Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Boat yard Ltd jijini Dar es salaam wakiendelea na kazi ya ukarabati  wa kivuko cha Mv Magogoni kilichosimamisha huduma zake kwa ajili ya ukarabati mkubwa.  Picha na Theresia Mwami – TEMESA


Mtanzania Nalimi Mayunga kuzindua video yake na Akon katika fainali za Airtel Trace Music Stars

$
0
0
 Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga anategemea kuzindua video yake  mpya ijulikanacho kama “Please don’t go away” aliyoifanya na mwanamuziki nguli duniani  Akon nchini Marekani. 
Nalimi Mayunga alipata nafasi  ya kurekodi wimbo huo  mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika na kuwashinda washiriki wengi  kutoka  nchi 12 barani Afrika. 
Kibao hicho chenye mahadhari ya R& B  kimeanza kupigwa au kuchezwa leo katika radio mbalimbali nchini wakati ambapo video yake inategemewa kuzinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 20 Mei 2016 wakati wa finali za msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Star 2016 linalowashirikisha washindi watano bora ambao wanashindania kitita cha shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na nafasi kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AfrikaAirtel Trace Star yatakayofanyika hivi karibuni nchini Nigeria. 
Akiongea kuhusu wimbo wake na Akon, Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema “ kwa kweli namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa lakini pia nawashukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii kubwa ya kuweza kurekodi wimbo na Mwanamuziki wa kimataifa Akon. Nafurahi sana sasa video hii iko tayari baada ya mashabiki wangu kuisubiri kwa muda mrefu. Natumaini nyimbo yangu itafanya vizuri ndani na nje ya nchi na kunipa fursa ya kuwa mwanamuziki nyota na hii ndio imekuwa ndoto yangu. Nawaomba watanzania waniunge mkono ili nyimbo zangu na muziki wangu uendelee kufanya vizuri.” 
Aliongeza kwa kusema ”Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza washiriki wa mwaka huu walioingia tano bora na kuwashauri waweke juhudi na nia ili waweze kujinyakulia ushindi na hatimae kutuwakilisha vyema katika mashindano ya Afrika na kurudi na ushindi nyumbani”. Aliongeza Mayunga. 
Naye Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema , tunajivunia kuendelea kuwawezesha watanzania kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi kupitia shindano hili la Airtel Trace Music Stars . Tunaamini video ya Mayunga itafanya vizuri  ikiwa watanzania tutamuunga mkono Star wetu huyu,  nachukua fursa hii  kuwaomba wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki  kuisikiliza na kuipiga katika vyombo mbalilmbali kama radio, TV na klabu za muziki ili iwafikie mashabiki wengi” 
Kufatia ushindi wake Nalimi Mayunga ameweza kupata mafunzo ya muziki toka kwa Akon pamoja na kurekodi kibao hicho kipya cha “Please don’t go away” na pia amepata nafasi ya kurekodi upya wimbo wake nchini South Afrika ujulikanao kama “Nice Couple”ambao unaendelea kufanya vizuri sana kwa sasa
 Mwanamuziki nguli wa miondoko ya R&B duniani Akon akiwa na Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika  mwaka Jana.
Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akirekodi video yake na mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon nchini Marekani.

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA MH DKT REHEMA NCHIMBI (RC NJOMBE)

$
0
0
Kwa niaba ya mama yetu mpendwa Mh Dkt Rehema Nchimbi tunapenda kutoa shukrani zetu za upendo kwa Madaktari na wauguzi wote wa Hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani  kwa kumtibu vyema mama yetu kipindi chote alipo lazwa hospitalini hapo akiwa anauguza jerahaa lililotokana na kukatwa na kioo kichwani, katika ajali aliyopata hivi karibuni Chalinze, Mkoani Pwani.

Tunapenda pia kuishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na viongozi kwa kumpatia mama yetu huduma kipindi chote alicho lazwa hospitalini hapo, kipekee kabisa tunaishukuru familia ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Eng: Evarist Ndikilo, dereva wa Mkuu wa Mkoa Njombe, Bw. Mbunda na Katibu wa Mkuu wa Mkoa Njombe, Bw. Ngalupela kwa kusimama kama sehemu ya familia yetu katika kuhakikisha mama yetu anapata huduma zote muhimu.

Shukrani zetu za upendo ziwafikie Viongozi wa CCM taifa na Mkoa wa Pwani, Viongozi wa dini Mkoa wa Pwani Uongozi wa Mkoa wa Njombe, ndugu na marafiki, na wale wote walio mtembelea mama Hospitali ili kumjulia hali na wanaoendelea Kumwombea Mama yetu ili apone kwa haraka.

Mama yetu kwa sasa anaendelea vizuri hivyo tunapenda kuwaondoa wasiwasi wanachi wa Njombe na watanzania kwa ujumla juu ya afya ya mama yetu kwa sasa. Tuzidi kumwombea apone kwa haraka. Tunaomba upendo mliouonesha kwa mama yetu uzidi kudumu na kurithiwa na vizazi vijavyo.

Mama yetu amepata jeraha, baada ya kuchanwa na kioo cha mlango wa moja ya maduka makubwa Chalinze alipo simama kwa mapumziko akiwa safarini kurudi kazini kwake Mkoa wa Njombe tarehe 7 Mei 2016 akitokea Dar es Salaa kikazi.

MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA - SHETTA NDANI YA KIPINDI CHA THE AVENUE

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONDOKA LONDON KUREJEA NYUMBANI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wafanyakazi wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza uliopo London wakati alipoondoka kwenye hoteli ya Intercontinental kurejea Dar es salaam Mei 15, 2016  Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HOW TANZANIAN OIL AND GAS ENTREPRENEURS CAN MAKE MONEY AND SURVIVE THE LOW OIL PRICES

$
0
0
In response to the oil and gas boom. Some Tanzanian entrepreneurs have built their business by offering products and services  __ such as human resources , safety equipment, supply, and logistics, accommodation , IT and telecommunication services__to the oil and gas companies  such as  Maurel et prom, Statoil  BG Group etc.
And they reaped a substantial reward,two years prior to declining in the oil prices.
But times are hard now. The low oil price is biting. International Oil companies shut down projects . And there’s Slow down oil and gas activities in Tanzania and beyond. So, Fewer clients . Business is lower. And their profits are squeezed.
The drop in oil prices since June 2014 from over $100 barrel to $ 45 today is hurting many local businesses.
.
The oil price going down the drain and this present one of the worst oil price downturn in the recent history.
The harsh truth is that nobody knows exactly when the price picks up again. But most economists agree that the road to recovery will be longer and hard.

Feeling down because of the bad oil prices? Don’t panic . Oil price downturn comes and go. And that’s the part of the petroleum industry cycle.
Seriously, I know you love your business. And you don’t want to go back being restricted with month salary again.
So, how do local entrepreneurs keep their business alive during the low oil price? How do you survive the low oil prices? How do you make money?
Read on to find how?
Diversifying Business’s clients
The bad price has changed the entire oil and gas market at a frenetic pace. To reap incredible result, should respond to the market condition and service other industries.
If you were recruiting local workforce for oil and gas sector.
You can offer the same services to the telecommunication, marine perhaps aviation industries.
Flexibility is the mark of successful entrepreneurs. never be rigid.
Fix problems in the downstream segment of the industry
Most Tanzanians investors have been offering products and services to the upstream sector of the industry for some time now. Why? because they had all money.
But that’s not for you. Upstream operators have nothing to do with your products or services now.
The whole east Africa region possesses only two oil rigs. So what business will listen to your products or solution?
To stay in the business line, then solve the problem in the downstream sector__ Downstream operators are making huge cash access benefit weak oil prices.
To stand out in the recent oil and gas market, you products or services must fix an issue in the downstream.
Downstream operators represent things like transportation, marketing, and selling of oil and gas market. So   oil pipeline are booming now
Positive attitude is the critical to survive
In the oil price downturn, people loses jobs. People create jobs. Companies make a huge fortune. Companies go into bankrupt. All in the oil price slump.
So spending the whole day wondering how the prices affecting your business. You’re not helping yourself. Instead .you diminish your creativity and productivity. You must have a positive mindset.
The right attitude helps you to think on how to do to come out ahead. And enables you to fight, work hard and come up with awesome ideas that bring incredible result.
See the weak prices as opportunities and not a problem. In that manner, You’ll be amazing  with the positive result you get.
Surviving is all up to You
Are you going to pay attention and put to use information given to you in this article or you’re going out there and winning how the business is hard in the period of low oil prices.?  Surviving in the current atmosphere is easier than you think. Go out there and make It happen. You’ll thank me later.

Hussein Boffu
Petroleum Geoscience Graduate
   Hussein.Boffu@Tanzaniapetroleum.com
0655 37 65 43

2nd Anniversary of the late Private R. Brian Salva Rweyemamu

$
0
0
Private R. Brian Salva Rweyemamu
December 27th 1987 - May 15th 2014

It is hard to believe and, indeed, difficult to comprehend that 24 months have now passed since you departed us on that fateful early morning of unbearable sorrow of May 15th, 2014. Though we accept God’s Wish of that reality, sights and memories of that early morning will vividly remain with us until we finally join you.
To say that the family misses you, R. Brian Salva Rweyemamu, is a gross understatement. Our hearts have bled and bled uncontrollably in the last two years and continue bleeding. Tears have turned into rivers as we seek human explanations of your untimely death at that very tender age. We, however, still thank God for the fruitful, precious short time you spent with us.
Brian, you forever remain the Joy of the family and we continue to hold dear the responsibility of our unshakable loyalty and deep love for you. Your father, Salva Rweyemamu, your mother Isabella Kafumba Rweyemamu, your loving younger sisters – Brenda and Sonia, your dear friend Bridgety Kizenga, your many cousins, uncles, aunties, and friends and friends of the family, continue to pray for you. 

Rest in Peace Brian.

SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA ANKAL KUFUATIA MSIBA WA MWANAE MAGGID

$
0
0
Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue  pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa  kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...


Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi  wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...


Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote.  ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...


Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani  za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba  mfiwa Ankal ni mwanachama. 
Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, Ruby 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na  Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani pamoja na Ras Makunja Na Ngoma Afrika Band wa Ujerumani na Jeff Msangi wa Canada. 

TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA  KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.


HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...


Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!






SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Shirika la umeme TANESCO limewatahadharisha wamiliki wa mabango ya matangazo ya umeme ambao hawajalipia kujisalimisha kabla sheria haijafuta mkondo wake. https://youtu.be/FMQOVY654WQ
 SIMU.TV: Fahamu sababu iliyopelekea mechi ya mwisho ya ligi ya Uingereza kuharishwa katoka uwanja wa Old Trafford; https://youtu.be/IN7rk1jEjyU
 SIMU.TV: Michuano ya mchezo wa golf  uliyojumuisha washiriki 100 kutoka mikoa mbalimbali wahitimishwa rasmi katika viwanja vya Lugalo.   https://youtu.be/03qfyNqmgVY
 SIMU.TV: Hivi ndivyo uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ulivyochimbika wakati  Simba na Mtibwa Sugar wakilisakata kabumbu.  https://youtu.be/TJ-hv35kPjw
 SIMU.TV:  Mwenge wa auhuru unaoendelea kukimbizwa visiwani Zanzibar kufungua miradi ya maendeleo itakayogharimu Sh.bil.3 .7;https://youtu.be/XtTgkl2pkgI
 SIMU.TV:  Wakulima wa korosho katika wilayani Lindi wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa madai yao ya malipo ya korosho. https://youtu.be/N--vkxTO1NA
 SIMU.TV: Yajue mengi kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya kisiasa na uchumi akikufafanulia kwa undani kabisa kuhusu tatizo la sukari nchini.  https://youtu.be/CTvpJdxg1d4
 SIMU.TV: Fahamu mambo mengi kutoka wataalamu wa kutatua matatizo ya kijamii wakikujuza kuhusu  kwa athari za malezi duni kwa mtoto.  https://youtu.be/3_2RamGPhdU

SWAHILI TV: ZAIDI YA MILIONI MIA MOJA TSHS. ZILIVYOCHANGWA KWA KING DREW

TANAPA YAKABIDHI MCHANGO WA MADAWATI 16,500 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA KWA WILAYA 55 ZINAZOPAKANA NA HIFADHI ZA TAIFA

$
0
0
Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh,Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Hundi za fedha kiasi cha Sh Bilioni moja zilizo tolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa wakuu wa mikoa 19 kwa ajili ya Madawati katika wilaya 55 zinazopakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero ,Betty Mkwasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mara ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa ,Kamishna wa Polisi Mstaafu,Zelothe Stephen ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.


MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO MHE JAMES MBATIA AANDAA JIMBO LAKE KUKABILIANA NA MAJANGA (NDENGA).

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo, Mhe. James Mbatia akichokoza mada wakati wa kongamano la Elimu juu ya maafa katika jimbo hilo baada ya kukumbwa na mafuriko ,Kongamano lililofanyika katika shule maalum ya Viziwi na kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa,Vijiji na Vitongoji,Maofisa watendaji,Madiwani,wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo hilo.
Baaadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus Makunga akichangia mada katika kongamano hilo ambalo alikuwa mgeni rasmi pia,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia na kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.

MAKALA YA SHERIA: JE, NI HALALI KUMWACHISHA KAZI MFANYAKAZI KWA KOSA LA KWANZA?

$
0
0
Na  Bashir  Yakub
Sheria  ya  Ajira  na  Mahusiano  Kazini  ya 2004 ndiyo  sheria  mama  katika  masuala  ya  ajira. Kwa  anayetaka  kujua  haki  na  wajibu  wa kazi  na  mfanyakazi,  mwajiri  na  mwajiriwa  basi  na  asome  sheria  hii.  Sheria  hii  ilianza kutumika  rasmi tarehe  5/ 1/  2007.


Misingi  mikuu  ya sheria  hii  ni  usawa  wa  ajira kwa  jinsia, ujira  unaolingana  na kazi  inayofanywa  na  mfanyakazi, haki  na  maslahi  bora  kwa  mfanyakazi, mazingira  bora  na  salama  ya  kazi  na  mengine  mengi  hasa  yanayoshabihiana  na  haki  za  binadamu.


Kumwachisha  kazi  mfanyakazi  ni  moja  ya  maeneo  muhimu  katika  sheria  hii. Wakati  gani  mfanyakazi  aachishwe  kazi,  kwa  kosa  gani, utaratibu wa  kumwachisha  kazi,  stahiki  zake  baada  ya  kuachishwa  kazi,  uachishwaji  kazi  haramu, utaratibu  wa  hatua  za  kuchukua  panapo  uharamu  katika  kuachishwa  kazi  ni  sehemu ya  mambo  muhimu  katika  sheria  hii.

Makala  haya  yataeleza  habari  hii  ya kuachishwa  kazi  lakini  yatalenga  kipengele  kimoja  tu  cha  uhalali wa  kumwachisha  mfanyakazi  kwa kosa  la  kwanza.

1.NI  IPI  TAFSIRI  YA  KUACHISHWA  KAZI.

Kuachishwa  kazi  ni  hatua  ambapo  muajiri  husitisha  mkataba  wa  ajira  kwa  notisi  au  bila  notisi  kwasababu  mbalimbali  zikiwemo  za  utovu  wa nidhamu.



KIJIPU UPELE MTAA WA CHATO JIJINI DAR ES SALAAM.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA PROMOSHENI YA MILIONI 100 NA TUSKER - FANYA KWELI UWINI.

$
0
0
MILIONI MIA MOJA  KUSHINDANIWA KUPITIA BIA YA TUSKER LAGER

 Kwa kutambua thamani ya wateja wake Kampuni ya Bia ya Serengeti imezindua promosheni maalum ya kutoa shukrani kwa wateja wake ambao ni watumiaji wa bia ya Tusker Lager, ambapo watajishindia pesa taslimu Milioni 1 kwa washindi kumi (10) kila wiki kwa muda wa wiki kumi na kufanya jumla ya Milioni mia kushindaniwa na Zawadi za bia kibao. 

Uzinduzi huo uliofanyika kwa aina yake katika mikoa miwili tofauti kwa wakati mmoja, mikoa hiyo ni Dar es Salaam na Kilimanjaro hii ni tofauti na ilivyozoeleka kwani uzinduzi hufanyika Katika sehemu moja tu. Promosheni hii imeanza rasmi leo na itaendeshwa kwa muda wa wiki kumi. Uzinduzi ulipambwa na maonyesho ya barabarani, msafara ulianzia kiwandani Chang’ombe na kuishia Fyatanga Bar Tegeta huku ukipokelewa na shamrashamra za aina mbalimbali.

Hii si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kuendesha promosheni kama hii kwani ni wengi wameshanufaika kupitia promosheni mbalimbali za mfumo huu na hata kubadili maisha ya watumiaji wa bidhaa zake kwa kiasi kikubwa. Kupitia bia ya Tusker Lager Kampuni hiyo inaendeleza kile kilichokuwepo cha kurudisha fadhila na kutoa shukrani kwa watumiaji wa bia ya Tusker Lager. 

Wateja wanaweza kujaribu mara nyingi kadiri wawezavyo. Ili kuwa mshindi wa Tusker milionea, washiriki wataweza kujishindia pesa taslimu kupitia droo zitakazochezeshwa kila wiki. Unapofungua bia ya Tusker Lager (500ml) chini ya kizibo ukapata kizibo cha Tusker Milionea hii inakuingiza Katika droo ya kupata Milioni moja, au unaweza kupata Bia ya Zawadi – hii inampa mteja wa Tusker bia ya bure papo hapo alipohudumiwa na ikiwa utapata jaribu tena utaendelea kuburudika kistaarabu ili kuongeza nafasi yako yako kuibuka mshindi. Promosheni hii itasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini ili kuleta ufanisi zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti alisema promosheni hii si kwa ajili ya kuongeza mauzo tu bali ni kutoa shukrani kwa wateja wao kwa kuwaunga mkono na kusapoti bidhaa zao.

“Kupitia Bia ya Tusker Lager wateja wetu wanaweza kujishindia shilingi Milioni Moja kwa washindi kumi kila wiki kwa muda wa wiki kumi ambao tutawapata kutoka Katika droo za kila wiki nchi nzima. Lengo kubwa ni kumwezesha mnywaji na mdau wa bia ya Tusker kufanya kweli kupitia bia yetu ya Tusker Lager”aliongeza Bi. Cesear Mloka.

Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro uzinduzi ulifanyika katika manispaa ya Moshi huku ukihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wasambazaji na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti na wana habari. Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mauzo bwana Alain Tsageutayo ambae alisema “Wakati wa kuchagua zawadi za kushindaniwa pesa taslimu ilichukua nafasi ya juu – na kiwango cha Milioni moja kinaweza kusaidia kujikwamua kwa namna moja au nyingine. Wateja wetu ndio wametufikisha hapa tulipo basi nasi hatuna budi kurudisha shukrani kwako mtumiaji wa bia yetu ya Tusker Lager na ndio maana tunatoa kwa washindi 100, milioni 1 kila mmoja katika kipindi cha promosheni.”

Milioni 100 na Tusker Lager - Fanya kweli na Uwini itadumu kwa muda wa wiki kumi nchi nzima. Kwa washiriki wa Tusker milionea wataweza kushuhudia droo zitakazofanyika kila ijumaa na kuonyeshwa kwenye runinga. Washindi watakaopatikana watakabidhiwa pesa zao kila ijumaa inayofuatia kwenye sherehe maalum ya promosheni.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Kaskazini Amoni Kabagi(kushoto) akieleza jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa 'Tusker Fanya Kweli Uwini' mjini Moshi, pamoja nae ni Meneja wa Mauzo wa Kilimanjaro, Godwin Seleli.
Msafara maalum ukielekea katika Bar ya Fyatanga tayari kwa uzinduzi rasmi kwa wateja wa bia ya Tusker
Mkurugenzi wa Masoko Cesear Mloka (katikati) pamoja na wafanyakazi wengine wa SBL wakishangilia uzinduzi rasmi wa Tusker Fanya Kweli Uwini kwa wateja uliofanyika katika Bar ya Fyatanga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Basilla Mwanukuzi ashiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilaya ya Kinondoni

$
0
0
Mkurugenzi wa taasisi ya Basilla Mwanukuzi Foundation na Miss Tanzania 1998, Basilla Mwanukuzi akiungana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi pamoja na viongozi wa vyama na serikali na wananchi wa kinondoni katika kuupokea Mwenge wa Uhuru jana Mei 16, 2016 kwenye uwanja wa shule ya Bunju. Mwenge huo umeanza kukimbizwa katika wilaya ya Kinondoni ukitokea Mkoani Pwani.
Basilla Mwanukuzi akipokea mwenge.

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwasili katika ghala la kuhifadhia bidhaa la Kampuni ya Marenga Investment alipofanya ziara ya ghafla kwa lengo la kujionea hali ya upungufu wa sukari pamoja na kufanya ukaguzi mwingine.aliiongozana nao ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwa katika ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali la kampuni ya Marenga Investment.kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa.

Mmiliki wa Ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali za kampuni ya Marenga Investment,Joseph Kimosso akimuongoza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky kutembelea maeneo zilipohifadhiwa bidhaa mbalimbali.

AIRTEL YATAMBULISHA MR. MONEY.

$
0
0
 Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma ya MR. MONEY  ambayo itaendeleza kurahisisha matumizi ya huduma ya kifedha kupitia simu za mkononi kwa uhakika katika kufanya miamala mbalimbali kwa gharama nafuu na kuhakikisha muamala wako unakamilika kwa usalama kabisa.
amesema kuwa huduma ya Airtel Money Tap Tap ni huduma nyingine inayowasaidia wateja wakeinayotoa nafasi kwa wateja kufanya malipo kupitia kadi maalumu bila kuwa na haja ya kuwa na simu ya Mkononi.
 Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao wa simu wa Airtel huduma ya MR. MONEY.
Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa udiznduzi wa huduma ya MR.MONEY jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa huduma ya MR. MONEY inawezesha wateja wake kupata mkopo ya Timiza isiyo na harama kwa wateja na mawakala wa Airtel Money. 
Amesema kuwa wateja wa Airtel wanaweza kununua Luku na kupewa muda  unit nyingine za ziada endapo mteja akitumia airtel Mone kununua Umeme. usikose kupata nafuu ya fedha zako unapomtumia pesa wapendwa wako kwa kutumia Artel  Money bila gharama yoyote.
 Kwa kutumia huduma mbalimbali za MR. MONEY piga *150*60# kufurahia huduma.

Wakulima wawe makini na mvua hizi za masika.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania, Kilimo kimetajwa kuwa uti wa mgongo wa Taifa. Ikumbukwe kuwa miaka ya Sabini za mwanzoni kuliwahi kuwepo kauli kuhusu kilimo iliyosema “Kilimo cha Kufa na Kupona”. Kauli hii ililenga kuondoa njaa iliyokuwa inalikabili Taifa. Kwa miaka  ya hivi karibuni, serikali ikaja na Kauli Mbiu ya “Kilimo Kwanza”. Hizi zote ni jitihada za kuinua kilimo ambacho kinategemewa na walio wengi hapa kwetu.

Kilimo ni eneo la kipaumbele katika uchumi wa Tanzania licha ya kuwa  kilimo nchini bado kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua na hali ya hewa kwa ujumla .
 
Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa iliyotolewa na  Mkurugenzi Mkuu Dkt. Agnes Kijazi zinasema mvua za masika zimeshaanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Hata hivyo maeneo machache yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
 
Hali ya unyevunyevu wa udongo inatarajiwa kuwa ya kutosheleza shughuli za kilimo katika maeneo mengi.Hata hivyo, mvua za juu ya wastani zinazoendelea kunyesha zinaweza kusababisha hali ya unyevunyevu wa udongo kupita kiasi hivyo kuathiri mazao na hata kusababisha mafuriko na kuharibu mazao.
 
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, msimu wa mvua za Masika katika kipindi cha miezi ya Machi hadi Mei, 2016 ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), Pwani ya Kaskazini, (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-Kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani kwa maeneo mengi ya ukanda huo isipokuwa maeneo ya Kusini mwa ukanda huo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
 
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha tahadhari imetolewa kwa wakulima wote kuwa makini na mvua hizi za masika zinazoendelea kwani zinatarajiwa kunyesha kwa wingi katika baadhi ya maeneo kulingana na uelekeo wa upepo katika maeneo mengi ambayo yanayopata mvua za msimu wa masika.
 
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images