Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Kipaumbele chetu ni kuboresha reli ya TAZARA- Balozi Kijazi.

$
0
0
KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI, ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI AFUNGUA MKUTANO  WA WATAALAM KUTOKA NCHI YA CHINA, TANZANIA NA ZAMBIA WA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA UTENDAJI WA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA (TAZARA) KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MWL. JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (kushoto), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini China ambao wanahudhuria  Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Balozi wa China Nchini Dkt. LU Youqing.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (kulia), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini Zambia ambao wanahudhuria  Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (wa nne kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
SERIKALI  imesema iko tayari kuboresha reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi kwani ni jambo la msingi na itashirikiana na nchi za Zambia na China ili kufanikisha azma hiyo. 

Akizungumza  leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi  John Kijazi wakati akizindua kikao kazi kilicho shirikisha nchi tatu ambazo ni  Tanzania, Zambia na China kuhusu maboresho ya kiutendaji ya reli ya TAZARA.

SUMATRA YATANGAZA NAULI ZA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO HARAKA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen  Kahatano akizungumza na waahabari juu ya nauli za mabasi yaendayo kasi haraka katikati ya jiji la Dar es Salaam,kutoka  Mbezi mwisho –Kimara –Kivukoni nauli ni800 mwanafunzi 200. Mbezi mwisho –Kimara –Kariakoo nauli 800,mwanafunzi200. Morocco-Kimara –Mbezi Mwisho nauli 800,mwanafunzi 200. na Morocco-Kivukoni nauli 650. mwanafunzi 200. Kariakoo – Morocco nauli 650.mwanafunzi 200.viwango vipya vya nauli vinapaswa kuanza kutumika rasmi Mei,12 mwaka huu, mkutano huo umefafanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Traffic  wa Kanda, Magembe Seni.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen  Kahatano leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii.

FIRST NATIONAL BANK YAFUNGUA TAWI MWANZA.

$
0
0
Mkuu wa Biashara FNB Tanzania, Francois Botha akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella jinzsi mashine ya kisasa ya kuolea fedha inavyofanya kazi baada ya mkuu wa mkoa kuzindua huduma za benki hiyo jijini Mwanza. --- Benki ya First National Bank Tanzania (FNB) imeendelea kupanua wigo kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la Rock City Mall jijini Mwanza leo. 

 Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois Botha alisema uzinduzi wa tawi la FNB Mwanza umelenga kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo. “Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. 

Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.” Botha alisema tawi Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mtandao wa matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini. “ First National Bank daima tunafikiri njia mbalimbali za ambazo tunaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. 

Tawi letu la Mwanza litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani yenye biashara inayokua kwa kasi” Botha alisema. Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. 

Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema mkoa wa Mwanza una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza inakua kwa kasi. 

 "Tunakaribisha uwepo wa FNB na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na mikoa mengine," alisema Mkuu wa Mkoa. Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri mkubwa wa rasilimali. “Tunatarajia kuwa mtatoa mchango mkubwa katika utoaji huduma za kifedha mkoani Mwanza kupitia huduma zenu mbalimbali kwa kutumia ubunifu na utaalamu wenu,” Mongella alisema. Tawi hilo lililofunguliwa kwenye jingo jipya la Rock City Mall litatoa huduma za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

TAMASHA LA PILI LA MAVAZI YA STARA KUZINDULIWA.

$
0
0
 Maoneshi ya Mavazi yakiendela.
TAMASHA la pili la Stara, Stara fashion Week 2016 linatazamiwa kuchukua nafasi yake tena mwaka huu katika ukumbi wa City Garden Restaurant Kamata, June 1 hadi 5.

Tamasha hilo ambalo litafunguliwa na Exhibition ya bure, linakaribisha watu mbalimbali wanawake wanaume na watoto kwa manunuzi ya vitu mbalimbali, kama vile Mabaibui,Mitandio Madera kwa ajila ya Mwezi mtufu wa Ramadhani, evening dresses, kanzu, Udi Hena na vitu vingine pia kutakuwa na wachora heena kwa bei nafuu.

Exhibition hiyo ambayo itakuwa inaanza tarehe 1 June asubuhi ya saa nne hadi saa 12 jioni, itafungwa na maonyesho ya mavazi ya stara kwa wanawake pekee siku ya Jumapili ya tarehe 5 kuanzia saa nne hadi saa 11 jioni.

Katika kilele cha maonyesho hayo kazi za mikono ya wabunifu wa hapa nyumbani wanaobuni mavazi ya stara zitaonyeshwa pamoja na warsha itakayojadili mada mbalimbali ambazo ni pamoja na
1. Jinsi ya kumpata mwenza na kudumisha ndoa
2. Matumizi na Mipango ya Fedha
3. Ujasiriamali Na nyinginezo
Kongamano hilo la wanawake, litakuwa na kiingilio cha shilling elfu 35 VIP na Elfu 50 viti maalum Kwa kujumuisha chakula cha mchana kwa wote na zawadi mbalimbali zitatolewa.

Stara fashion week imedhaminiwa na  Maximalipo, Hijab Couture, Hijabi Central Tz, Kanzu Point, Cordoba School, Speedy Print, I-view Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden Restaurant, Event Lights, Sofia Production,  Clouds Media na wengineo.

TSN SUPERMARKET/HYPERMARKET YAMWAGA “LOYALTY VOUCHERS’ KWA WATEJA WA MARA KWA MARA.

$
0
0
 Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy akitambulisha Vocha hizo zilizogaiwa Mwanza kwa Wateja. Afisa Mwajiri wa TSN Group Amos Paul akikabidhi Vocha hizo za punguzo la manunuzi ya bidhaa, kwa wateja wa kwanza kufurahia punguzo hilo TSN hypermarket Mwanza. 
Meneja Uhusiano wa TSN Group, amesema mpango wao wa kuendelea kuboresha biashara kwa kutangaza kwenye mitandao ya kijamii. Sasa unaweza kufollow TSN Group TZ kwenye mitandao ya kijamii kwa promotion mbalimbali zitakazoendelea kutambulishwa. 

Sasa unaweza ku’bargain’ kwenye supermarket, Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy ameelezea kuhusu mikakati ya kuboresha biashara za TSN kwa kutambulisha Loyalty Gift Vouchers kwa wateja.

Wateja sasa wanaweza kuomba na kupata punguzo la bei ya bidhaa walizonunua katika maduka yao yaliyopo, Kibo Complex-Tegeta, Bamaga Petrol station-Mwenge, Baraka Plaza-Mikocheni, Tancon House-Posta, Swiss Tower -Upanga Dar es Salaam pamoja na Rock City Mall-TSN Hyprmarket Mwanza iliyofunguliwa hivi karibuni.

Meneja Uhusiano huyo ambaye alizitambulisha Voucher hizo kwa mara ya kwanza Mwanza amewataka wateja kumiminika katika maduka yao kupata punguzo hilo la kwanza kufanyika katika supermartket. 

Alisema TSN inatoa punguzo la manunuzi kwa wateja wanaonunua bidhaa zisizopungua chini ya laki tatu ndani ya wiki moja. Alisema kupata punguzo la bei mteja atalazimika kujisajili na kuacha mawasiliano yake ya simu na kuhakiki mauzo yake kwa wiki. 

Katika promotion hiyo ambayo itadumu  miezi mitatu kuanzia sasa hadi mwezi wa saba, kwenye checkout point ya maduka ya TSN, utatakiwa kuomba kitabu na ujisajili kwa kuandika jina lako, kiasi cha manunizi uliyofanya na mawasiliano yako ukisubiri kufikia kiwango kinachostahiki ili uweze kukabidhiwa vocha hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA MFUKO WA PENSHENI PPF JIJINI ARUSHA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. 
Picha zote na Mafoto Blog.
Jengo hilo lililozinduliwa leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.

TFDA YAKUTANA NA WADAU WA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO.

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Daud Ntibenda akifungua kikao kazi cha wadau wa TFDA katika sekta ya Habari mkoani Arusha.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Said Mecki Sadiki akizungumza na maafisa wa TFDA ofisini kwake walipokwenda kumtembelea ofisini kwake na kujadili masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika mkoa wake.
Picha ya Pamoja.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAENDELEA KUPUNGUA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja.Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 umepungua hadi asilimia  5.1  kutoka asilimia 5.4.
 Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja akifafanua  jambo  kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania.kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii). 

Na. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
OFISI ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.

Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.

Amesema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.

Akizungumzia Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.

Amesema kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa ya ungana na matunda aina ya machungwa.

Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11  wa mwezi Machi 2016.

“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza  ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi " Amesema Kwesigabo.

Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.

Wadau wa maji kujadili rasilimali za bonde la Mto Rufiji

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeandaa warsha kwa wadau wake juu ya tathmini ya kimkakati ya athari za kimazingira na jamii juu ya mpango jumuishi wa usimamizi na maendeleo ya rasilimali maji za bonde la Mto Rufiji zitakayofanyika Jijini Dar es salaam na mkoani Iringa.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mbogo Futakamba alipokua akifafanua kuhusu mpangilio wa warsha hizo zitakazofanyika katika mikoa miwili ambapo kwa Jijini Dar es salaam warsha hiyo itafanyika Mei 20 mwaka huu na mkoani Iringa itafanyika Mei 23 mwaka huu kuanzia sa 3 kamili asubuhi hadi sa 10:30 jioni.

"Wizara yetu inawakaribisha wadau wake wote kushiriki warsha hii na mada zitakazotolewa zitahusisha maelezo ya jumla juu ya mipango ya maendeleo ya muda mrefu ya rasilimali za maji ya bonde la mto Rufiji na athari zake tarajiwa za kimazingira na kijamii, kuwapa fursa ya kutoa maoni na mitazamo yao juu ya mipango inayokusudiwa pamoja na kutoa ufafanuzi kuhusu maamuzi na taratibu zinazofuata,"alisema Mhandisi Futakamba.

Aidha, Mhandisi Futakamba ameongeza kuwa warsha hizo zitaandaliwa na kuwezeshwa na washauri elekezi kutoka Kampuni ya uingereza ijulikanayo kama Environmental Resource Management ikishirikiana na kampuni za JSB Envi-Dep na eMjee Consult za Tanzania.

Warsha hizo zitaruhusu wadau kujadiliana kwa pamoja na kutoa maoni ya kutosha juu ya mada zitakazoongelewa ili kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania kupitia rasilimali maji zilizopo kwenye bonde la mto huo.

UPDATES: MSIBA WA MTOTO WA ANKAL

$
0
0
Familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini.

Msiba sasa umehamishiwa Tegeta Wazo Hill, Nyumbani kwa Mama Mzazi wa Marehemu (likiwa ni ombi maalum la Mama), na taratibu zote zinafanyika huko.

 Mipango ya kuusafirisha Mwili wa Marehemu kutoka nchini Afrika Kusini na kuja nyumbani kwa mazishi, inafanyika na taratibu za  mazishi zitatolewa mara tu baada ya mwili kuwasili nchini.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

TANZANIA-RWANDA TRADE FORUM: REGISTRATION DEADLINE: 10TH MAY (1600HRS EAT)

KONGAMANO LA JESHI LA POLISI (MEDICAL WING) LA KUJIPIMA UTENDAJI KAZI NA CHANGAMOTO LAFANYIKA MJINI TABORA

$
0
0
LAPF imedhamini kongamano la Jeshi la Polisi (Vikosi vya masuala ya tiba) uliofanyika mjini Tabora. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umetoa kiasi cha Shilingi milioni 6,200,000/= katika kufanikisha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania maalum kwa ajili ya kujipima na kujadili changamoto mbalimbali za kitengo cha tiba ndani ya jeshi la polisi (medical wing) Wawakilishi kutoka mikoa yote Tanzania walishiriki katika kongamoano hilo wakiwa ni maofisa waandamizi wa jeshi hili la polisi. katika kongamano hilo Mfuko ulipata wasaa wa kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko lakini pia mada ya maandalizi kabla ya kustaafu ilitolewa katika mkutano huo , udhamini huu una synergy kubwa na mfuko katika kusajili wanachama wapya ndani ya jeshi la polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi ACP Paul Kasabago akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya TZS. 6,200,000/= iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni LAPF kuwezesha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania (medical wing) mjini Tabora. Wanaokabidhi kutoka LAPF ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama Bw. Valerian Mablangeti, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Desdery Sigonda pamoja na Meneja Kanda ya Dar es Salaam Bi. Amina Kassim.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa mada kuhusu Mfuko ikijumuisha maandalizi kabla ya kustaafu, Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi wakisiliza kwa makini katika kongamano la jeshi hili lililofanyika mjini Tabora hivi karibuni.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini mada toka Mfuko wa Pensheni LAPF kwenye kongamano la Jeshi hili lililofanyika mjini Tabora ambapo maafisa hao walivutiwa na kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari ikiwa ni maandalizi kabla ya kustaafu.
Mmoja ya Maafisa waandamizi walioshiriki kongamamo la jeshi la Polisi mkoani Tabora hivi karibuni akiuliza namna ya kujiunga kwa hiari na Mfuko wa Pensheni wa LAPF mara baada Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitoleawazo na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

MAPITIO YA HOJA MBALIMBALI ZA WABUNGE MJINI DODOMA.

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani akijibu baadhi ya hoja za Wabunge zilizoihusu Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kipindi cha jioni Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) (kulia)
akijibu baadhi ya hoja za baadhi ya Wabunge wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali jioni bungeni mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mapitio ya baadhi ya hoja za Wabunge leo jioni Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mhe. Amina Makilagi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali za Wabunge leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) akijibu hoja za Wabunge mbalimbali wakiochangia hotuba ya Wizara yake leo jioni Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa mapitio ya hoja za Wabunge jioni Bungeni mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma)

SHAKA: KIKWETE AMEITUMIKIA NCHI HII KWA UWEZO WAKE,BASI MEMA YAKE YAHESHIMIWE

$
0
0
Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa tanga
……………………………………
Na Woinde Shizza,Tanga

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM )umevitaka vyama vya
upinzani wanaopika maneno ya majungu yenye lengo la kuwagonganisha viongozi wa CCM,Waache kumsumbua sumbua Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete astaafu kwa heshima, kwa sababu ameitumikia nchi yake kwa kutoa jasho jingi miaka kumi iliopita, Aidha umoja huo umesisitiza kuwa kazi aliyoifanya Dk Kikwete katika uongozi wake wa miaka kumi kisiasa na kiserikali utabaki kwenye vitabu vya kumbukumbu ya historia iliotukuka, hususan kila utakapokumbukwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2015.

Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati alipozungumza na viongozi na wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbi wa TANU Hall mjini Tanga.Alisema baada ya upinzani kubaini kukosa hoja na hawakubaliki katika jamii maadui wa kisiasa wanotimiwa na nafisadi wamekuwa wqkijaribu kupika uzushi na kutaka kuionyesha jamii kwamba viongizi wa chama tawala hawana maelewano.

“Nakupeni usia viongozi wa Ukawa ambao sasa mmekuwa wakiwa , mambo ya ngoswe waachieni ngoswe wenyewe, viongozi wa ccm hawagombani, hawajawahi kugombana na kamwe hawatagombana milele “alisema shaka Aliwataka viongozi hao kutazama mustakabali wao kisiasa na kuachana na ccm kwa sababu chama hicho tawala haiwezekani kubomoka kwa maneno ya jikoni , vijiweji au vichochoroni.

Shaka alisisitiza kuwa mwenyekiti wa ccm Dk Kikwete wakati akiwa Rais ameitumikia nchi yake kwa kadri ya uwezo wake kama ambavyo walivyotenda na kuitumikia nchi viongozi watangulizi wake akiwemo baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na yeye ametenda kwa uwezo wake kama atakavyotenda Rais Dk John Magufuli katika kipindi chake.

“Mtu mwenye akili timamu kila atakaposafiri akiizunguuka nchi yetu na kupita juu ya barabara za lami, ujenzi wa madaraja, kutanuka kwa mawasiliano, kukua uchumi wa Taifa na wa mtu mojmoja na wananchi kiushi katika nyumba za kisasa lazima utamkunbuka Kikwete taka usitake
“alieleza Kaimu huyo katibu mkuu . 

Alisema kila zama ina kitabu na Nabii wake hivyo mema yaliofanywa na kiongozi mmoja aliyemaliza muda wake yanahitaji kuheshimiwa kwa sababu  Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni watoto wa baba na
mama mmoja.

Jecha atembelea NEC

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Jecha Salim Jecha akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva ,Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi walipokutana makao makuu ya NEC kuzungumzia maswala mbali mbali ya Demokrasia na mustakabali wa Siasa za Tanzania hapo jana tarehe 9-5-2016.
 
 Picha ya pamoja



RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AAGWA LEO NA BALOZI WAPYA CHIKAWE NA KISAMBA

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam,jana, Mei 9, 2016.Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba, Balozi huyo alipofika kumsalimia katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.(Picha na Bashir Nkoromo).

TANZIA UK DIASPORA GLASGOW.

$
0
0
Tunasikitika kuwatangazia msiba wa Mtanzania mwenzetu 
Bi Mwasaburi Hajikilichotokea Jumamosi jioni huko Glasgow Scotland.

Mipango ya mazishi inaendelea na mtajulishwa tarehe ya mazishi.
Msiba uko nyumbani kwa Marehemu
2/1, 105 Mcculloch St. Glasgow, G41 1NT.

Kwa wale mlioguswa mnaweza kutuma rambi rambi zenu kwenye account ya
ndugu wa marehemu 

A. AZIZ.
Nationwide.
Account No: 01491791
Sort code: 07 04 36.
Kwa mawasiliano zaidi mnaweza kumpigia ndugu wa Marehemu
A. AZIZ - 07411445644

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

YALE YALEEEE.....

$
0
0
 Yale mabasi yaendayo haraka, tuliyokuwa tukiyasubiri kwa hamu kwa kipindi kirefu, hatimae leo yameanza kazi rasmi kwa ruti zote zilizopangiwa. pamoja na kuanza kwa kazi, lakini bado wanachangamoto ya matumizi ya njia yake, kwani bado kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vimekuwa vikiitumia njia yake hiyo kana kwamba ni jambo la kawaida tu. Leo Kamera ya Mtaa kwa Mtaa imezungukia eneo la Kariakoo na kujioneka hali halisi katika barabara hiyo na kukuletea wewe mdau ujionee mwenyewe na kutoa maoni yako ya nini kifanyike ili jambo hili likae kwenye mstari ulionyooka. Picha na Emmanuel Massaka.
Daladala hili likiwa limeifunga kabisa njia hiyo kwa lengo la kukatisha barabara hiyo kurudi lilikotoka baada ya kuona chombo chenye njia yake kikichomoza mbele yake.
Bodaboda na Watembea kwa miguu wakijidai katika barabara hiyo.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI LONDON.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei  12, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu amesema anaenda kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

“Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.

“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema.

Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

Shirika la ndege la Etihad latoa taarifa kuhusiana na msukosuko wa Ndege yake Indonesia.

$
0
0

Timu ya wataalamu kutoka shirika la ndege la Etihad leo wametembelea abiria tisa waliolazwa baada ya Ndege aina ya EY474 ya shirika hilo kupatwa na msukosuko mkali katika anga la wazi ambapo walitoa huduma endelevu, ushirikiano na msaada.

Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote za matibabu.

Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”

Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images