Mamlaka ya Biashara Tanzania, TANTRADE, imepongezwa kwa kuichagua sekta ndogo ya ngozi, na kuifanyia maboresho, katika kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano, ya kujenga Tanzania ya Viwanda.
Pongezi hizo zimetolewa na wadau wa ngozi wa machinjio ya Vingunguti na Ukonga, wakati wa kufanya tathmini ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, yaliyofanywa na Tantrade kwa ushirikiano na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam, DIT, Kampasi ya Mwanza, ambapo kimeendesha mafunzo ya nadharia ya utunzaji ngozi, yakafuatiwa na mafunzo kwa vitendo ya unjinjaji, uchunaji, na utunzaji bora wa ngozi, na kukamilishwa na mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa bora za ngozi yaliyofanyikia DIT kampasi ya Mwanza.
Wadau hao wameipongeza TANTRADE kwa kubaini fursa zilizopo kwenye sekta ndogo ya ngozi na kuamua kutoa kipaumbele maalum kuiendeleza sekta hiyo, kwa kuwaelimisha wafugaji, wasafirishaji, wajinjaji, na wasindikaji ngozi, ili Tanzania itoe mazao ya ngozi yenye daraja la juu.
Akizungumzia uamuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka amesema “Sisi kama taasisi tumijipanga kuwajengea uwezo wajasiriamali, waweze kutumia vizuri fursa za biashara zilizopo kupitia sekta hii muhimu ya ngozi na hatimaye kuwaongezea kipato binafsi na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wetu kwa ujumla, ili kufikia malengo ifikapo mwaka 2025 nchi iwe na uchumi wa kati,” alisema Rutageruka.
Pia aliiomba serikali ya mikoa na wilaya kupitia manispaa na halmashauri zao, kutenga maeneo maalum yatakayotumiwa na wajasiriamali wadogo na wa kati , kuzalisha bidhaa za ngozi, ambao TANTRADE kwa upande wake itawapatia fursa za kuyafikia masoko kupitia fursa mbalimbali zikiwemo za maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, DITF, ambapo TANTRADE itawatengea maeneo maalum ya kuonyesha bidhaa za ngozi.
Tantrade kwa ushirikiano na Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam kampasi ya Mwanza, wameamua kuitekeleza kwa vitendo kauli ya rais Magufuli ya Tanzania ya viwanda, kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo Watanzania kuweza kuendesha viwanda vidogo vidogo vya sekta ya ngozi nchini.
Mafunzo hayo ya unjinjaji wa kisasa yalitanguliwa na mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa kutunza ngozi, na kufuatiwa na mafunzo ya utengenezaji bidhaa za ngozi, yatakayoendeshewa mjini Mwanza.
Mkufunzi na mtaalam wa ngozi, Patrick Mshana, mwenye uzoefu wa zaidi miaka 40 akiwafunda wachinjachi na wasindikaji ngizi wa mchinjio za Vingunguti na Ukonga, wakati wa mafunzo ya uchinjaji, uchunaji na usindikaji bora wa wanyama ili kuzalisha ngozi bora, yaliyoendeshwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Chuo cha DIT Kampasi ya Mwanza, yaliyoendeshwa katika katika machinjio ya Vingunguti hapa Jijini Dar es Salaam, na kuhitimishiwa Mwanza kwenye Kampasi ya DIT, yalihudhuriwa na wachinjaji na wasindikaji wa ngozi kutoka machinjio Vingunguti na Ukonga jijini Dar es Salaam wajasiliamali wa bidhaa za ngozi wa Kanda ya Ziwa.
Mkufunzi na mtaalam wa ngozi, Patrick Mshana, mwenye uzoefu wa zaidi miaka 40 akiwafunda wachinjachi na wasindikaji ngizi wa mchinjio za Vingunguti na Ukonga, wakati wa mafunzo ya uchinjaji, uchunaji na usindikaji bora wa wanyama ili kuzalisha ngozi bora, yaliyoendeshwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Chuo cha DIT Kampasi ya Mwanza, yaliyoendeshwa katika katika machinjio ya Vingunguti hapa Jijini Dar es Salaam, na kuhitimishiwa Mwanza kwenye Kampasi ya DIT, yalihudhuriwa na wachinjaji na wasindikaji wa ngozi kutoka machinjio Vingunguti na Ukonga jijini Dar es Salaam wajasiliamali wa bidhaa za ngozi wa Kanda ya Ziwa.
Wachinjaji wa ng'ombe wa machinjio ya Vingunguti, wakifundishwa mbinu mbalimbali za kumbembeleza mnyama kabla ya kumchinja, ili asikarike, mnyama akichinjwa kwa ukatili, harisa zinaingia kwenye nyama, hivyo walaji kujikuta wanakula nyama yenye hasiri na wao kupata hasira, Mafunzo ya uchinjaji, uchunaji na usindikaji bora wa wanyama ili kuzalisha ngozi bora, yaliyoendeshwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Chuo cha DIT Kampasi ya Mwanza, yaliyoendeshwa katika katika machinjio ya Vingunguti hapa Jijini Dar es Salaam, na kuhitimishiwa Mwanza kwenye Kampasi ya DIT, yalihudhuriwa na wachinjaji na wasindikaji wa ngozi kutoka machinjio Vingunguti na Ukonga jijini Dar es Salaam wajasiliamali wa bidhaa za ngozi wa Kanda ya Ziwa.
Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda akifungua semina ya siku tano ya mafunzo ya bidhaa za ngozi kwenye chuo cha DIT Mwanza jana,akiwa ameshika kiatu kilichotengenezwa hapa nchini chenye viwango vya kimataifa,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha DIT tawi la Mwanza Dk Albert Mmari na Kaimu Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka.