Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1215 | 1216 | (Page 1217) | 1218 | 1219 | .... | 3272 | newer

  0 0

    Katibu wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Nd. Epi Fania Ngonyani akibadilishana mawazo na Balozi Seif akijiandaa na ujumbe wake kuondoka Bandarini Malindi kurejea Mjini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani mwema. Nyuma ya Ndugu Ngonyaji ni Mwenyekiti wa CCM wa Tawi hilo Ndugu Haroub Othman Mberwa.
   Balozi Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Ndugu Haroub Othman Mberwa aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi kumi wa Kata hiyo waliofanya ziara ya ujirani mwema hapa Zanzibar.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Ujumbe Viongozi wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kinondoni Mjini Dar es salaam katika Banadari ya Malindi baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani mwema Visiwani Zanzibar wakiwa wenyeji wa Tawi la CCM Vikokotoni Mjini Zanzibar.

  Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi mbali mbali Nchini Tanzania wanapaswa kuwa makini katika kuwachangua viongozi imara wakati utakapowadia wa chaguzi za Chama hicho ili kuirahisisha kazi ya ushindi CCM mwaka 2020.

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Haroub Othman Mberwa wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi hapo Bandarini Malindi Mjini Zanzibar.

  Mwenyekiti Mberwa na Ujumbe wake wa Viongozi Kumi wa Kata ya Makangira Msasani ulikuwepo Zanzibar kwa ziara ya kuimarisha uhusiano mwema kati ya kata hiyo na wenyeji wao wa Tawi la CCM Vikokotoni lilioko Mji Mkongwe Zanzibar.

  Ndugu Mberwa alisema wakati umefika kwa wana CCM kuendelea kuongozwa na Viongozi makini waliobobea hekima na busara kuanzia Matawi maeneo ambayo ni chimbuko halisi la upatikanaji wa Viongozi katika ngazi za Majimbo, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.

  Alisema Chama cha Mapinduzi kimepata misukosuko mingi katika awamu tofauti za Uongozi zilizopita iliyosababishwa na baadhi ya Viongozi wenye sura mbili za maamuzi jambo ambalo lilipelekea kuwa na mgawanyiko na hatimae kuzalisha makundi yaliyozaa ufa ndani ya chama hicho.
  Ndugu Mberwa alitahadharisha kwamba Wanachama wa CCM Matawini ndio wenye kauli na rungu za kuwachagua Viongozi watakaokuwa tayari kuwatumikia katika misingi ya uadilifu na ni vyema kuachana na tabia ya kubebana kwa kisingizio cha ukabila, uzawa na urafiki.

  Alieleza kwamba tabia kama hizo ndizo zinazopelekea Viongozi wa Kitaifa kukumbana na wakati mgumu katika kutoa maamuzi ya hatma ya muelekeo wa kumpata Kiongozi wa kubeba dhamana ya kuwatumikia katika masuala yao ya Chama.

  Naye Katibu wa Tawi la CCM la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kiondoni Mkoa wa Dar es salaam Nd. Epi Fania Ngonyani alisema uwepo wa ujumbe wao hapa Zanzibar umejifunza mambo mengi yatakayosaidia kuimarisha chama chao kwa upande wa Tanzania Bara.

  Nd. Ngonyani alisema matembezi ya sehemu za kihistoria pamoja na Mikutano ya hadhara ya kukutana na wanachama wenzao wa baadhi ya Matawi na hata Wilaya za Tanzania Zanzibar imewajengea heshima na upendo kati yao na wenyeji wao iliyopelekea pia kujadili mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

  Alieleza kwamba katika mikutano hiyo ya uhusiano mwema pande hizo mbili zilipendekeza uwepo wa mikakati ya makusudi ya kujengewa uwezo zaidi wa uwezeshaji makundi makubwa ya vijana na wanawake ili washiriki vyema kwenye shughuli za uzalishaji.

  Ziara hizo za kuimarisha uhusiano mwema kati  ya Matawi ya Chama cha Mapinduzi ya Vikokotoni Mjini Zanzibar na Makangira Msasani Dar es salaam hufanyika kwa kutembeleana kila mwaka.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Hapi Salum akionyesha kitu mbele alipotembelea Hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Saaam leo, na kujionea mambo mbalimbali katika hospitali hiyo.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Hapi Salum akizungumza na  Hapi atinga Hospitali ya Palestina-Sinza leo ili kubaini mambo kadhaa ambayo yamemchukiza  katika hospitali hiyo.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Hapi Salum akitembelea na kuwajulia hali wagonjwa katika hospitali ya Palestina-Sinza jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyeshwa barabara zinazopishana ya juu na ya chini, alipokagua daraja ya Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016.
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiuliza jambo, alipokagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016. Kushoto ni Mama Salma Kikwete.
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembea kwenye daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016, walipokagua daraja hilo.
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama moja ya ofisi zitakazotumiwa na magari kulipia ushuru wa kutumia daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0  Dk. Sophia Mlote, mkazi wa Kinyerezi Zimbili jijini Dar es Salaam akiweka sawa vifaa mbalimbali kwenye banda lake la kilimo ambamo amepanda nyanya. Dk. Mlote anatekeleza kilimo hai kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com
  Bw. Hamaro akiandaa tray maalum kwa ajili ya kuwapa wanakikundi kupandikiza mbegu kabla ya kupeleka kwenye vitalu vyao. Hii ilikuwa ni sehemu ya mafunzo ya vitendo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo, Mkuranga
  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.

  Alisema baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.

  “Baba yake Samatt alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.

  Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..

  Alisema SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo.

  0 0

  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanania Dk. Gharib Bilal wa tatu kutoka kushoto na Mama Salma Kikwete wa kwanza kushoto wakishiriki mazishi ya Merehemu Benadette Izengo mama wa Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda aliyekaa katikati yao pamoja na wanafamilia wengine wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanis kuu la Mtakatifu Joseph. 
  Mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Balozi Asha Rose Migiro akiweka mchanga kaburini wakati wa maishi ya marehemu mama Benadette Izengo.
  Fathre Matumaini akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Josepha jana.
  Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana jijini Dar es salaam na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
  Teddy Mapunda na Ndugu yake wakiwa pembeni mwa jeneza la mama yao mpendwa marehemu Benadette Izengo.
   

  0 0


  Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM) akiuliza swali kwa Waziri wa Nnchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), bungeni Dodoma , kwamba ni fedha kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake mkoani Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
   Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (katikati) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum, Kiteto Koshuma kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

  0 0

  Na: Lilian Lundo – Maelezo

  Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa kutuma maombi yao shirika la “Master Card Foundation, Fund For Rural Prosperity” ili kupanua na kuimarisha upatikanaji wa fedha Vijijini Tanzania.

  Hayo yalisemwa na Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti leo, jijini Dar es Salaam katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.


  “Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.  Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.  Aidha, Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .


  Jumla ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaoishi maeneo ya Vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020.
  Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akifafanua jambo katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
  Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .


  0 0

  Katibu mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutozwa kwa vyombo vya usafiri vitavyopita katika Daraja la Nyerere kuanzia jumamosi ya Mei 14.(Picha na Raymond Mushumbusi) MAELEZO

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa kuanzia siku hiyo , vyombo vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.

  “ Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi Nyamhanga.

  Mhandisi Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.Mabasi yanayobeba abiria 15 yatalipia Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15 Sh. 5,000 na yale yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatalipia Sh. 7,000.

  Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.

  Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.

  0 0

  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo, Mkuranga
  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.

  Alisema baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.

  “Baba yake Samatt alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.

  Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..

  Alisema SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo.

  0 0

  John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka (WARAMI) akizungumza na waandishi wa habari Kwenye Hoteli ya Tamarin Mwenge jijini Dar es salaam kuhusu Sakata la Sukari ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyothubutu kuwatetea watanzania waliowanyonge katika masuala mbalimbali na hasa katika suala zima la uhaba wa sukari.

  Kuna tani nyingi za sukari zimekamatwa katika msako maalum ambao Rais aliamrisha vyombo vya dola kufuatilia wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha sukari, baada ya zoezi hilo kuanza sukari nyingi imeendelea kukamatwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa imefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

  WARAMI inapongeza jitihada zote za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha watanzania wanaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo wanapendekeza mambo kadhaa yafanyika na jeshi la polisi

  Mratibu huyo wa Taasisi ya WARAMI amelitaka jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi juu ya wafanyabiashara wanaotamba barabarani kuwa wameliweka jeshi hilo mfukoni kwamba hakuna wa kuwafanya lolote katika nchi hii.
  Taasisi za kiserikali zifafanue juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi kwa maslahi yao kama, ni haki ama si haki.

  Kiongozi huyo wa WARAMI akaongeza kwamba hivi sasa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli anayo vita kubwa kutokana na kazi anayoifanya ya kuwatetea watanzania waliowanyonge anayo vita ndani ya bunge na nje ya Bunge 
  Kutokana Na Hoja Ambazo Zimekuwa Zikitolewa Na Baadhi Ya Wabunge Zikikosoa Utendaji Wa Rais, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifaidika na baadhi ya mambo hivyo wasingependa mabadiliko ya kumkomboa mwananchi wa kawaida yatokee, katika picha kushoto ni Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI
  Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI akifafanua jambo wakati viongozi hao wa taasisi ya WARAMI walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam , kulia ni John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI

  0 0


  Frank Mvungi-MAELEZO

  Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya Mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milioni 30 au vyote viwili.Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

  “Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya Mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016. “Aalisema Mungy.

  Akizungumazia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.
  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu tathmini ya hali halisi kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini ifikapo mwezi june 2016 ambapo kiwango cha simu Bandia Kimepungua kutokana na Elimu inayotolewa na Mamalaka hiyo kwa wananchi. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
  Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Injinia Gabriel Mruma akiwaeleza waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia simu zenye ubora unaokubalika ili kuepuka athari zinazotokana na matumizi ya simu Bandia. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy .(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO ).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA  0 0

  Mimi Mama Bishanga, Prisca Zenda na wanachuo wenzetu watanzania wa Cleveland State University, Cleveland, Ohio, tumesikitishwa sana na kifo cha ghafla cha  mwanao Maggid Michuzi  kilichilichotoke South Africa. Pokea pole zetu na tunamuombea marehemu amani ya kudumu katika usingizi wake wa milele: Na mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu unachopitia.
  AMINA
   Mrs Marolen a.k.a  Mama Bishanga (kulia) na Prisca Zenda wananchuo wa Cleveland State University. kilichopo Cleveland, Ohio, USA.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa Jumatano.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).

  “Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri Mkuu.

  Amesema anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. “Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.

  Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.

  Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari nchini linakwisha ifikapo 2019. “Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.

  “Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.

  “Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.
    

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, MEI 10, 2016.

  0 0

  Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI, ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.


  Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza, ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi kila mwaka.  "Nimeshtushwa na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo, hongereni sana", alisema Mavunde.

  Mavunde amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja tu kubwa na ya msingi ya utanzania.
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI Shannon Kiwamba(kushoto)
  Mh Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
  Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini.
  Mh Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM

  0 0

  Yanga yaibuka Kidedea Mara baada ya Kuibugiza Timu ya Mbeya City Fc Goli Mbili kwa Sifuri, (2-0) katika Mchezo ulio Chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya huku wafungaji wakiwa ni Vicent Bossou Goli la Kwanza na Amis Tambwe Goli la Pili..
  Kikosi Kazi cha Timu ya Mbeya City Fc Wakoma Kumwanya.
  Baadhi ya Waamuzi wakisalimiana kabla ya Mtanange huo kuanza.
  Goli Kipa machachali na Mkongwe katika Soka Nchini Juma Kaseja akiwa katika Mkao wa kiufundi lango la Mbeya City Fc.
  PICHA ZOTE NA MR,PENGO MMG MBEYA.

  0 0


  Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe akifungua warsha ya siku mbili kwa Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini (LNG) jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Utafiti (TPDC), Bw. Kelvin Komba akielezea mbele ya waandishi wa habari lengo la warsha ya siku mbili kwa Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini (LNG) jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini (LNG) wakifuatilia warsha hiyo.

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendesha warsha ya siku mbili ya Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika nchi (LNG). Akifungua Warsha hiyo kwa Niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe alisema warsha hiyo inalenga kuwakutanisha wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi huo.

  Aliongeza kuwa warsha hiyo pia imekusudia kutengeneza mazingira shirikishi kwa wadau hao kabla ya kuanza kutekeleza ujenzi wa wa Mradi huo. Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika gesi asilia kwa matumizi ya ndani na kusafirisha nje ya nchi unatarajiwa kujengwa eneo la Likong’o katika Manispaa ya Lindi.

  Warsha hiyo inawakutanisha wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TPDC, Taasisi kutoka Serikalini na Makapuni ya Wawekezaji ya Mafuta na Gesi Nchini.

  0 0

   Ni miaka mitatu imepita tangu ulipotwaliwa Mpendwa Mama yetu Victoria. Ni Roho Mtakatifu pekee anayetufariji kila mara majonzi na huzuni vinapotujaa mioyoni. Tunaamini  kuwa Mama umepumzika katika utukufu wake Mungu.

  Unakumbukwa sana na mumeo Thomas Kiama, wanao Evelyn, Grace, Mary, Agnes, Esther na Stella,wakwe zako Wilfred, Noel na Richard, wajukuu zako Clifford, Ian, William, Eleon, Mainda, Kandi, Agness, Mboni, Lincoln na Lucas.

  Upendo, ucheshi, ukarimu na tabasamu lako vitabaki kuwa nguzo katika maisha yetu siku zote.Kipenzi Mama tulikupenda sana lakini Mungu Mwenyezi alikupenda zaidi. Umepumzika kwa amani!

  Familia ya Thomas M. Kiama

  0 0  0 0
 • 05/10/16--22:54: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

older | 1 | .... | 1215 | 1216 | (Page 1217) | 1218 | 1219 | .... | 3272 | newer