Na Editha Karlo blog ya Jamii, Kagera.
WAKAZI wawili wa Mkoa wa Kagera wameshinda fedha taslimu kupitia shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB katika matawi yake yote nchini.
Wakiongea na mtandao huu mara baada ya kushinda fedha hizo mmoja wa washindi hao Jafram Mohamed ambaye ni askari polisi Wilayani Ngara alisema kuwa anaupongeza uongozi wa NMB kwa kuanzisha shindano hilo kwa wateja wao kwani lina lenga kuwahamasisha kujiwekea akiba mara kwa mara.
Mohamed alisema kuwa yeye ni mtumishi wa serekali lakini amekuwa akijiwekea akiba mara nyingi kadiri awezavyo katika akaunti yake hali iliyopelekea kuingia katika droo ya kucheza bahati nasibu hiyo.
"Nilifurahi sana baada ya meneja kunipigia simu na kuniambia nimeingia faini za bahati nasibu ya shindano la pata patia, hizi fedha nilizoshinda shilingi laki nane ntazifanyia jambo la msingi na ambalo ni kumbukumbu kwangu na familia yangu"alisema Mohamed.Naye mshindi mwingine Philbert Robart mjasiliamali na mkazi wa Wilaya ya Muleba alisema kuwa amefarijika kushinda kiasi cha shilingi laki nne katika bahati nasibu ya pata patia toka bank ya NMB.
"Kwakweli bank ya NMB unatujali sana wateja wake, hizi fedha nilizoshinda leo zitanisaidia katila biashara zangu, nina wasihi wateja wote wa bank ya NMB nchi nzima wale wapya na wazamani kujiwekea fedha mara kwa mara katika akaunti yao itawapa nafasi ya kuingia katika shindano hili"alisema Rogati
Meneja wa NMB Mkoa wa Kagera Victorine Kimario alisema kuwa shindano hilo la pata patia kwa wateja wao ni endelevu hivo amewataka wateja kujiwekea fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili waweze kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda.
''Kampeni hii ya pata patia ya kuwataka wateja wetu kuweka fedha katika akaunti zao imeanza mwezi wa pili mwaka huu, wateja wanatakiwa kuweka fedha katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi elf hamsini na kuendelea mara kwa mara ili aweze kuingia katika faini za kushinda"alisema Meneja
Alisema kila mteja ambaye anaingia fainali lazima ashinde sababu atatakiwa kuzungusha gurudumu lenye lenye nba kuanzia laki moja hadi milioni tatu na mshale wa gurudumu utakaposimama ndiyo kiasi ambacho atakuwa kashinda.Meneja Kimario amewataka wateja wapya na wazamani wa bank ya NMB kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili kujiweka katika nafasi ya kushinda bahati nasibu ya pata patia.
Mshindi wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB matawi yote nchini Jofram Mohamed akizungusha gurudumu na kushinda shilingi laki 8 taslimu.
Mshindi mwingine wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ys NMB kwa matawi yote nchini kutoka Mkoa wa Kagera Filbert Rogati akizungusha gurudumu na kushinda shilingi laki 4
Washindi wa shindano la pata patia wakisikiliza maelekezo toka kwa meneja wa NMB Mkoa wa Kagera kabla ya kuzungusha gurudumu la bahati nasibu
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa bank ya NMB tawi la bukoba mjini wakishuhudia washindi wanavyojipatia fedha zao kwa kuzungusha gurudumu