Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

TAMKO LA WIZARA KULAANI MAUAJI YA MAMA NA MTOTO, BAGAMOYO, MKOA WA PWANI

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi.

Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu.

Wizara inasisitiza kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa wanafamilia liko mikononi mwa kila mwananchi, hivyo jamii inawajibu wa kusaidia udhibiti wa ukatili na mauaji katika familia na jamii zetu. Jamii ikiwa na uelewa wa pamoja katika haki za wanawake na watoto katika jamii, itawezesha kuwekeza katika haki ya kuishi ya Mtoto, na kuendelea kuwaamini wanawake kwamba wanaweza kutoa mchango mkubwa wa kuendeleza familia zao, na taifa likaweza kupiga hatua kufikia maendeleo endelevu. 
Wizara inapenda kupongeza Polisi mkoa wa Pwani na wananchi walitoa taarifa za kuwakamata watuhumiwa wa mauaji haya, na tunaamini kuwa watakapofikishwa mbele ya vyombo vya sheria haki itaweza kutendeka.
Wizara inapenda kutoa pole kwa familia za marehemu hao waliopoteza maisha kwa kuchinjwa na kuawa, na kuwaombea kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine, na mwanamke na mtoto anahaki ya kuthaminiwa utu wake, bila ubaguzi wowote ambao unaweza kukatisha maisha yao.

Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZUNGUMZIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA AHADI YA UADILIFU KWA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi. Miriam Chisoro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) wakati wakijadili mada kuhusu Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma wakati wakijadili mada hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi.Miriam Chisoro (kushoto) ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA - TFF

$
0
0
VIINGILIO MECHI YA YANGA V/S  ESPERANCA
Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.
Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
 Fuata link chini kwa taarifa zaidi
FIFA YAILIMA FAINI SIMBA, YAPANGA KUISHUSHA DARAJA
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.
Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Fuata link chini kwa taarifa zaidi

VIINGILIO MECHI YA YANGA, ESPERANCE
Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.

UWAKILISHI WA NCHI KIMATAIFA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lingependa kutoa ufafanuzi kuwa iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.Kwa msingi huo, timu ambayo itafungwa katika fainali hizo za Kombe la Shirikisho –ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2016/17

The Government to issue a quarterly report on maternal death

$
0
0
 By Jonas Kamaleki- Maelezo

The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children is set to give a quarterly report on maternal deaths during delivery in order to minimize mothers’ deaths in the country.

This was revealed by the Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Ms. Ummy Mwalimu at the opening of the Health Women Leaders Conference in Dar es Salaam. “My ministry will ensure that all District Councils are providing a quarterly report on the deaths that occur during delivery.” Said Ummy Mwalimu. These reports according to the minister will be in line with maternal deaths reduction.
She also said the 5th Phase Government will construct rooms for operations in all health centres countrywide to rescue women’s life at delivery.
On promoting women in the decision making bodies, Ms. Ummy said she will be appointing 30 percent of women in the boards under her ministry. She mentioned such boards as the Tanzania Food and Drug Authority (TFDA), Medical Store Department (MSD) and Pharmacy Board.

She noted that promotion of women depends largely on the level of education, thus she urged girls to study hard and perform well in order to acquire higher leadership positions. “Fifty - fifty in leadership without education is just politics, so girls you need to be educated so as to be considered in high ranking leadership positions,” added Ummy Mwalimu.
Meanwhile, the Executive Chairperson of the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS), Ms. Fatuma Mrisho urged girls to be busy with studies so as to avoid involving themselves with love affairs thus concentrating with academic issues. She further said that when girls are fully engaged with studies they will be free from HIV/AIDS by about 7 per cent.

Stressing on women empowerment, the Danish Ambassador in Tanzania, Mr. Einar Hebogård Jensen said women need to have equal access to education, healthcare, resources and leadership. He said there was a need to respect and empower them for the betterment of the community.

This was a pre-conference that will be followed by the largest conference on the health, rights and well-being of girls and women that will take place on 16-19 May 2016 in Copenhagen, Denmark. It will attract more than 5,000 people - world leaders, academics, policy makers, activists, media, royalty, civil society and private sector representatives.
 

Mkutano wa Kiroho Columbus-OH unaanza leo Ijumaa

VIINGILIO MECHI YA YANGA, ESPERANCE HIVI HAPA

$
0
0
 Uongozi wa Young Africans ya Dar es Salaam, umekamilisha maandalizi yote muhimu ya mchezo dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola wa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho la Barani Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi Mei 7, saa 10:00 jioni.

Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana ukisimamiwa na kamishna kutoka Ethiopia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa Jukwaa la VIP “A” kuwa ni Sh 30,000; VIP “B” na “C” Sh 20,000 wakati jukwaa la viti Rangi ya chungwa ni Sh 7,000 wakati mzunguko wa viti vya bluu na kijani ni Sh 5,000.
Kwa mujibu wa Muro, Yanga itawakosa wachezaji mahiri wawili, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao watatumia mchezo huo kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano walizoonywa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kushuka kucheza Kombe la Shirikisho.
“Tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi kesho kuishangilia timu yetu kwa nguvu na kasi kubwa,” amesema Muro ambaye alitumia nafasi hiyo kutamba kwamba Yanga ilisajili wachezaji 24 kwenye michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

JENGO LA NSSF LA ENEO LA AKIBA BARABARA YA BIBI TITI JIJINI DAR ES SALAAM LASHIKA MOTO

$
0
0
Jengo la NSSF la eneo la Akiba jijini Dar es Salaam jioni hii limeshika moto ambao kwa bahati nzuri Jeshi la Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti.  Chanzo cha moto huo kinasemekana ni kulipuka kwa mtungi wa gesi katika moja ya vyumba vya ghorofa ya juu katika jengo hilo liitwalo Akiba House.
Magari ya Jeshi la Zimamoto yakiwa eneo la tukio katika harakayi za kupambana na moto huo katika jengo la NSSF  lililopo eneo la Akiba jijini Dar es Salaam muda huu. Moto huo inasemekana hakuna madhara makubwa (ya kibinadamu) yaliyojitokeza baada ya Jeshi la Zimamoto kufika kwa wakati katika eneo hilo. Picha na Prince Ali

RAIS DKT. MAGUFULI AWAONYA WALIOFICHA SUKARI


MAKAMU WA RAIS ASALIMIA WAUMINI WA KIISLAM SALA YA IJUMAA DODOMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya Sala Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa GADAFFI Mkoani Dodoma Leo Mei 6,2016. (Picha na OMR)

TRA YAKUSANYA MAPATO YA SH.TRIRIONI 1.035 MWEZI ULIOPITA

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Mapato Nchini  (TRA)  kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035   ambayo ni sawa na asilimia 99 .5  ya lengo  kukusanya sh.trioni 1.040 .

Akizungumza   na  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Bw. Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi  10  wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92  ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02  katika lengo la kipindi hicho.

Amesema kuwa  TRA imedhamiria  kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika  miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha  ambalo ni sh. Trioni 12.3.

Bw. Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha  inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo. 

Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.

Kamishina Mkuu amesema kuwa wamewakamata wafanyabiashara 300 kwa kuwatoza faini zaidi ya sh. Milioni 746 kwa makosa ya kutotoa risti, kutoa risti zenye bei pungufu pamoja na kutotumia mashine za Kieletroniki  na baadhi yao walihukumiwa kifungo au kulipa faini .

"TRA haitawavumilia wafanyabiashara wanayoikosesha serikali mapato kwa kuuza na kutoa huduma bila risti kwa makusudi yao kamwe hawataachwa", alisisitiza Bw. Kidata.

Mahakama Kuu Yatupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)

$
0
0
Na JacquilineMrisho - MAELEZO

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili. 
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa imekatwa na DPP. 
“Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna. 
Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao. 
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha. 
Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi hiyo.
 Watuhumiwa hao; aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (wa mwisho kulia haonekani pichani), Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania Shose Sinare wakipeana mikono na Mawakili wao,ndugu jamaa na marafiki mahakamani hapo mapema leo mara baada ya Mahakama kuu leo Mei 06 2016 Kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka lao namba nane la utakatishaji fedha.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI MBALIMBALI ALIPOKUWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha
PICHA NA IKULU.

DIALOGUE ON THE ROLE OF TANZANIAN YOUTH IN PEACE BUILDING ORGANISED BY GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA

$
0
0
The Global Peace Foundation Tanzania in collaboration with Tony Inspirational Talk organized a dialogue with the theme “The role of Tanzanian Youth in Peace Building” on 5th May 2016, at the New Montessori College, Mabibo branch, in Dar es salaam. 
The healthy session brought together some 50 youth from the New Montessori College and neighboring college premises, who discussed and came up with a way forward on how they were going to preserve the existing peace and stability in Tanzania. 

Opening of the dialogue, Global Peace Foundation Tanzania representative, Ms Hilda Ngaja said the economic growth of Tanzanian youth depends on the peace of the country. 
Ms Ngaja said that the existing peace in the country gave youth no room for excuses on their personal development, insisting that  without it and economic stability, youth might  involve themselves  in radicalization and violence extremism that ultimately leads to disruption of peace.

The Director of Tony Inspirational Talk, Anthony Luvanda inspired the youth to strive for personal responsibilities on their daily activities,  decisions and behaviours with the view to avoiding  the possibility of them engaging on issues of radicalization.

 He told them to be proactive and think beyond employment for their personal development. Luvanda asserted that the youth are a group which can be easily brainwashed because of their economic status. He also advised them to practically implement their entrepreneurship ideas so as to  stabilize their economic status.
On the other hand, the Montessori College Principle, Denis Jonas applauded the Global Peace Foundation Tanzania on their role of educating the youth in sustaining and promoting peace in Tanzania.

He also said that it was high  time now for the youth to accept responsibilities, work hard, learn more in order to cope with the world challenges, calling them to stand up and  speak up, as well as offer their  opinion on the way forward towards that goal, rather than constantly complaining while engaging in the blame-game.

Dialogue organisers, participants and presenters pose for a souvenir photo at the end of the exciting session. For mor photos CLICK HERE

TANZANIA UK DIASPORA TASKFORCE YATOA PONGEZI KWA BALOZI MPYA UK DKT. ASHA ROSE MIGIRO

WANANCHI MKOANI TABORA WATAKA MIGOGORO YA ARDHI IMALIZWE NA SERA MPYA YA ARDHI

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.

Na kwa sasa kamati maalumu ya kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera iliyoridhiwa na wengi.Katika sekta ya Ardhi Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kwa takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo zimejitokeza changamoto nyingi ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera hiyo.

Migogoro na malalamiko yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi kubwa katika jamii yetu na imekuwa ikiigharimu kwa kiasi kikubwa katika kuitatua.Kuongezeka kwa migogoro hii imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi pamoja na watumiaji mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji, wawekezaji, wananchi, vijiji na hifadhi.

Hata hivyo, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan katika sekta za kilimo, madini, viwanda na wananchi kutonufaika na uwekezaji unaofanywa katika ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.Aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini na hata sekta ya ardhi kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya Serikali kuamua kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.

Changamoto zote kwa pamoja, zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa ya watanzania wote.Ardhi ni Sekta mama na hivyo basi Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala yote ya maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake zinafanyika kwenye ardhi.

Na sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Hamisi Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.Shakira Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.Hanifa Selengu Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi.

YANGA YAWATUNGUA WAANGOLA BAO 2-0 TAIFA LEO

$
0
0

Wachezaji wa Timu ya Yanga, Juma Abdul (kushoto) na Simon Msuva (kulia) kwa pamoja wakishangilia baada ya kupata goli la pili lililotiwa kimiani na Matheo Anthony (kati), wakati wa Mchezo wa Makundi wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Beki wa Yanga, Juma Abdul, akijaribu kumtoka Mchezaji wa Timu ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akiipachikia timu yake bao la kuongoza wakati wa Mchezo wa Makundi wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe, pamoja na Beki wa Timu ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, wakiwania mpira wa juu, wakati wa Mchezo wa Makundi wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 2-0.
Kipa wa tiku ya GD Sagrada Esperanca ya nchini Angola, Roadro Juan Da Semero akiusindikiza mpira kwa macho ulipokuwa ukiingia langoni kwake, ikiwa ni mkwaju mkali uliopigwa na Matheo Anthony wa Yanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Zaidi Ya Tani 4579 Za Sukari Zilizofichwa Zakamatwa Dar

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AFUNGUA SEMINA KWA WABUNGE YA UELEWA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Mhe. Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.
 Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifungua semina hiyo

 Baadhi ya wabunge wakihudhuria kwenye semina hiyo

 Mhe. Zedi akiongoza majadiliano wakati wa semina hiyo
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
KAMANDA WA MATUKIO BLOG


SIMU TV: Habari kutoka vituo vya televisheni

KAMBI YA MADAKTARI WA MOYO WA NCHI TATU TOFAUTI YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar na nchini Uingereza waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
 Picha ya pamoja ya madaktari bingwa wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti za nchi tatu.
Daktari bingwa wa kufanya oparesheni ya BAY PASS kwa watu wenye matatizo ya moyo(Jina lake halijpatikana mara moja) akizungumza katika hafla ya kuwaaga madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam leo.

MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia, Uingereza na Qutar na baaadhi ya madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo  kutoka nchi za Saudi Arabia, Uingereza na Qutar jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja taasisi nne kutoka nchi tatu tofauti.
Abri amesema taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya hapa nchini na Taasisi ya Jakaya Kikwete.
Amesema kuwa kambi  hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa  nje ya nchi kwaajili ya matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.
Kwaupande wake Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao wametibiwa hapahapa nchini.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live


Latest Images