Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

THE TANZANIA GLOBAL DIASPORA CONFERENCE UK 2016

$
0
0
The Tanzania Global Diaspora meeting has just ended in Coventry -UK.

The aims  of  the  meeting  was to  bring  Tanzanians  together ,network and  foster a  feeling  of  belonging, unite  all  Tanzanians in  the  UK  and  beyond, create an  atmosphere of  inclusiveness and  reconciliation and  togetherness, promote  trade  and  Investment ,promote  entrepreneurship.

The conference also provided a platform to showcase exemplary initiatives in international development and diplomacy by diaspora communities around the world, highlight paths to success for diaspora engagement.

 Furthermore, on the  day   we had  the  Tanzania Global Diaspora achievement   awards -  which recognises those individuals who embody the ‘Servant Leader’ – economic success and professional excellence accompanied by moral leadership and service to society. 

The  meeting  was attended  by  the  Mayor  of  Coventry  city and  Hon  Jeremy  Lefroy  MP, Chairman  of  the  All-party  parliamentary  group on  Africa  and  member  of the International development Committee who said  that  he is impressed by  the  current  government’s stand  on corruption.

Because  Coventry is  one  of  the  UK’s  largest  industrial  and  manufacturing  centres it  makes  sense  for  us   as  the  Diaspora to  have  a  significant  presence  here. With  the  Support  of  The Tanzania  Mission  and  Tanzania  Trade  centre  in London, we  want  to  promote Tanzania’s image and goods  extensively  in the  UK ,through our  excellent  networks,  the  good  work  being  done   at  home  to  promote  Tanzania   abroad and  this  is  through a  series  of  tailored  activities, briefings   and   events  like  this  one .By  adopting  this  communications  route  we  will be  able  to  work  with  brands  already based  in  Tanzania  and  use  them to help us  make   the  case   more  widely  in  the  UK

Newdeal  Africa is  a social enterprise   platform based  in the  UK where  Tanzanians  local and  beyond can  showcase social  ,cultural  ,economic  and  political achievements. Its  also a  venue for corporate  organisations to expand their  market  base  by  collaborating with  foreign investors.

Newdeal Africa is made  up of  three divisions which  are: Ethnics  marketing ,Publishing and  media, Public  relations and  Advertising. It  has  branches  in Europe, The  Americas, Scandanavia and Tanzania

Thank you

E.LARUSAI


Chairperson
 Dr  Alex Paurine-lecturer South Bank University ,London receiving  an award  of  excellence  from The Mayor  Of  Coventry
 The Mayor  of  Coventry with Dr  Othman Maganga,lecturer   Coventry University
Hon Jeremy  Lefroy MP ina  group photo with members of the Tanzania Diaspora


INTRODUCING: PYDER FEATY MR T& GODZILLA TONIGHT FREE NATION PROD MR T TOUCH

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

NHIF yazindua huduma Toto Afya Kadi

$
0
0
Na Lilian Lundo – MAELEZO 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepanua huduma za mfuko wake kwa kuanzisha huduma mpya iitwayo “Toto Afya Kadi”. 
Hayo yameelezwa na Meneja Huduma za Dawa NHIF Michael Kishiwa  jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari. 
“Huduma ya Toto Afya Kadi ni huduma ambayo inahusisha watoto chini wenye umri chini ya miaka kumi na nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa kwa mwajiri hasa wale ambao wanalelewa katika vituo vya watoto yatima au wanaolelewa na ndugu waliokosa fursa ya kujiunga na huduma ya Bima ya Afya,” alisema Kishiwa. 
Kishiwa alisema kuwa, mwanachama ambaye ni mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 atatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mdhamini ambaye ni mlezi wake aidha kwenye kituo anacholelewa au mahali anapoishi. 
Aidha, Kawishe alisema kuwa mwanachama wa Toto Afya Kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa huduma ya Bima ya Afya ya NHIF anapata na ambazo zimeorodheshwa katika huduma ambazo zinatolewa na Bima hiyo kwa gharama ya shilingi 50,400 kwa mwaka. Pia alisema kwa kijana ambaye amepita miaka 18 ili kuweza kuendelea kuwa mwanachama wa Bima ya Afya na hajaajiriwa atatakiwa kujiunga katika vikundi vilivyosajiliwa ili aweze kusajiliwa katika mfumo wa kikoi kwa kuchangia kiasi cha shilingi 76,800 kwa mwaka. NHIF ina wanachama asilimia 12 ya watanzania huku ikiwa na jumla ya vituo 6700 nchi nzima, na mpaka sasa jumla ya wanachama 2,000 wa Toto Afya kadi wamesajiliwa nchi nzima tangu ianze Machi, 2016.
Meneja Huduma za Dawa Michael Kishiwa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF)  akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya mfuko huo iitwayo “Toto Afya Kadi” inayohusisha watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa, Kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko huo Bi. Sabina Komba.
Baadhi ya waandishiwa Habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

JK asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa Kenya

$
0
0
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Mkewe, Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya hapa nchinikufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Nwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki kilichotokea wiki iliyopita nchini Uingereza. Mwingine katika picha ni Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Boniface Muhia. Dkt. Kikwete anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mazishi ya Mama Kibaki yatakayofanyika Nairobi, Kenya.
Mama Salama Kikwete naye akisaini Kitabu cha Maombolezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Aziz Mlima naye akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais Mstaafu, Dkt. Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Naibu Balozi, Mhe. Boniface Muhia (wa pili kutoka kulia), mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo, Mama Salama Kikwete (wa kwanza kushoto) na Balozi Mlima nao wakimsikiliza Naibu BaloziPicha na Reginald Philip

Appreciation Note

$
0
0
Mrs. Sylvia Francis Shao 03-Nov-1952 – 02-Mar-2016

The Family of Dr. Francis Shao of Regent Estate – Dar-Es-Salaam would like to express our heartfelt appreciation for the outpouring of sympathies and comforting support received during the time of our loss. Thank you to all those who visited, called, sent prayers, cards, memorials, flowers, or helped in any way. Your kind words of comfort have been a powerful remedy to our wounded hearts. 
With utmost gratitude we would like to extend a special Thank You to the following:

The Prayer Communities of  St. Elizabeth of Hungary, St. Monica and St. Josephine of Bakhita and Choir, The St. Peter’s Catholic Church Oysterbay, Dar-Es-Salaam, in particular Rev Frs. Kwembe, Aaron and Gerald who led the Requiem Mass and Rev. Fr. Tingo of Keni-Aleni Parish Rombo,who led the burial mass, RESEWO,. The Management and Staff of TFNC, Board and Management of TIC  and TACRI. All the Doctors and Medical Staff who attended her at Muhimbili National Hospital and all other Medical Institutions where she was cared for during her illness, and Dr Maria Kamm and Weruweru Girls High School Alumnae.


Finally, We  extend our sincere appreciations to all relatives and friends from Marangu, Moshi and Arusha and all community members in, Keni Rombo,who poured in for the burial ceremony.  There will be a Thanks giving Mass on Friday 6th May, 2016, at 17:00 p.m. at St Peter’s Catholic Church Oysterbay Dar-Es-Salaam. 
“He will wipe every tear from their eyes. There will be no more death’ or mourning or crying or pain, for the old order of things has passed away.”                                                                                                                 Revelation 21:4


With Warm Regards,



Husband, Children, Grandchildren and all the members of the family.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza huku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga wakisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye tukio la kumuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi mpya nchini Uingereza . PICHA NA IKULU. 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.

Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Mei, 2016

TEASER JOTO LA ASUBUHI MAY 6 IJUMAA


SHIRIKA LA NDEGE LA NCHINI MAURITIUS LAZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA MAURITIUS KUJA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi wa Safari za ndege za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo. shirika hilo limezindua safari za ndege za kutoka nchini Mauritius kwenda jijini Dar es Salaam na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius ndege hizo zitaanza safari zake kesho.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akizunumza katika uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leoikiwa na lengo la kuunganisha ushirikiano kati ya nchi za bara la Afrika hasa Tanzania na Nchi ya Mauritius. Safari hizo ni za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Shamlashamla za uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

BRITAM YAZINDUA HUDUMA ZAO NCHINI TANZANIA.

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara ya Bima Britam group Bw. Steven Wandera muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni hiyo ya Bima hapa nchini, uzinduzi uliofanyika juzi Hyatt Regency hotel jijini Dar es salaam.
 Mgeni rasmi Jaji (mstaafu) Joseph Sinde Warioba akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Group Dk. Benson Wairegi muda mfupi baada ya mheshimiwa huyo kuzindua rasmi Kampuni ya Britam Tanzania inayojishughulisha na masuala ya bima katika soko la Tanzania, uzinduzi huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

YALIOJIRI BUNGENI

$
0
0
SIMU.TV: Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mhe. Vedasto ahoji mpango wa serikali wa kutengeneza barabara ya kiwango cha lami katika eneo la kihistoria la vita vya maji maji.     https://youtu.be/mN6_ACXc2YA

SIMU.TV: Je kwa nini serikali inachukua muda mrefu kurekebisha mishahara ya walimu baada ya kupandishwa vyeo? Mhe. Angela kairuki afafanua.     https://youtu.be/vBJhmrQSQq8

SIMU.TV: Haya hapa majibu ya serikali juu ya ushirikiano wa ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali katika ukaguzi wa taasisi za muungano.      https://youtu.be/b88YuNv7kdw

SIMU.TV: Mhe. Charles Mwijage atoa ufafanuzi juu ya mpango wa serikali kujenga viwanda katika mkoa wa Katavi na kutoa mafunzo ya ujasiliamli kwa vijana; https://youtu.be/ipc_QTZAxD0

SIMU.TV: Mbunge wa viti maalum Mhe.Upendo Peneza aitaka serikali kutekeleza ahadi yake ya kupunguza misamaha ya kodi hadi asilimia 1 ya GDP; https://youtu.be/AH0xHUvlWGM

SIMU.TV: Waziri wa katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amesema serikali itaendelea kuratibu mfumo wa uimarishaji wa sheria za nchi.https://youtu.be/wJV91GwUSIA

SIMU.TV: Watoto 4 wa familia moja wilayani Same wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa usingizini na mtu anayedhaniwa kuwa ni ndugu yao; https://youtu.be/wSny4bwyYjQ

SIMU.TV: Nini hatma ya wananchi wafanyabiashara  baada ya ujenzi wa masoko ya kimataifa kusimama Kyerwa.      https://youtu.be/0qVNQ5M1rmY

SIMU.TV: Sikiliza mpango wa serikali katika kutatua kero za maji safi na salama katika jimbo la Nanyamba na sehemu mbalimbali nchini;https://youtu.be/sy3sM1gCxYA  

SIMU.TV: Fahamu mpango wa serikali katika kukabiliana na kesi za unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto nchini;https://youtu.be/dOsctJ2YzGg

TANZANIAN CLUBS COMPETE FOR UNIQUE SUNDERLAND PRIZE

$
0
0
Football clubs in Tanzania are being offered the opportunity to visit Sunderland as part of the club’s partnership with Acacia Mining.

The unique partnership with Acacia is the club’s first ever football partnership and sees SAFC work with local schools and football clubs in the Kahama and Tarime districts of North West Tanzania, working to deliver Acacia’s Maendeleo Fund dedicated CSR programmes.

A selection of nine local football teams from these areas have been selected to participate in a unique competition that will see representatives from their club visit Sunderland and partake in a week-long knowledge sharing tour, which includes attending a match at the Stadium of Light alongside visiting the club’s state-of-the-art Academy of Light.
Sunderland AFC’s Head of International Football Development, Graham Robinson, has been working with the local football teams in Tanzania this past week as the club continues its commitment to help improve football in the community.

As part of the club’s visit, Graham has spent time with local team, Kakola Sports Club at Bugarama School, supporting the club on all aspects of its football operations from training schedules to creating business plans.

Graham said: “The overall aim of the competition is to help the different clubs create a more sustainable environment for its players and staff by creating a plan that not only benefits the club’s performance on the pitch but also the business side off it.”

Alongside supporting Kakola Sports Club off-field activities, Graham also delivered a number of training sessions with the club’s coaching staff, which was watched enthusiastically by over 200 adults and children from nearby villages.
SAFC's Graham Robinson delivering coaching session.
This was followed by taking in a friendly game between the club and local rivals Home Boys in which Graham was guest of honour.

Graham will also be working with Bugarama FC, Ilogi Yossi FC and Stand United in the coming days as the club continues its operations in Tanzania.

For more information about Sunderland AFC in Africa please visit www.safc.com/the-club/safc-global.

Timu ya Taifa ya mchezo wa Roll kwenda Kenya.

$
0
0

 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo, Ismail Bura (kulia) akionesha Kocha Mkuu wa mchezo wa Roll, Aurher Haule sampuli ya sare za Taifa zinazofaa kuvaliwa na wachezaji wanapokuwa nje ya nchi.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty ,Nadia Azmat akimkabidhi jezi kocha Mkuuwa timu ya Taifaya Tanzania ya mchezo waRoll, Aurther Haule  zitakazotumika kuchezea mchezo wa Roll kwa nchi zaAfrika utakakaofanyika Kenya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty ,Nadia Azmat akionesha viatu vitakavyotumika kuchezea mchezo wa Roll kwa nchi zaAfrika utakakaofanyika Kenya.

Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Taifa ya Mchezo wa mpira wa kuteleza(Roll Ball) imeondoka jana ikiwa na wachezaji 12 kwenda Kenya kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayoanza leo mjini Nairobi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Arthur Haule alisema jana Dar es Salaam kuwa wamejiandaa kutwaa ubingwa wa mchezo huo utakaoshirikisha timu kutoka mikoa sita.

Alisema safari yao ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Nadia House of Beuty inaondoka na wachezaji 12 na viongozi wawili.

Aliwataja wachezaji watakaowakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Mohammed Athumani, Emmanuel Thomas, Hamisi Salum, Rajab Kassim, Omari Madohola, Yakhe Shaaban,Jonas Emmanuel, Fahadi Waziri, Said Abdallah,Kassim Rajab, Feruzi Juma na Clement Andrea.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty, Nadia Azmat akikabidhi vifaa vya michezo kwa safari hiyo aliwataka watanzania wengine kusadia michezo ambayo haina umaarufu ili kuibua vipaji mbalimbali vya vijana.

Nchi zinazoshiriki mashindanoi hayo ni wenyeji Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO MAALUMU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

$
0
0
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahama Mkoani Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.

Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma iliyo bora kwa wananchi.

Mwenyekiti wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za siri.

“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini zinatenda haki.

Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.PICHA NA
BMG
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.

UN NA EU WAFURAHISHWA NA MIRADI WALIYOIFADHILI JIJINI MWANZA

$
0
0
RC Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya.

MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo kadhaa jijini Mwanza.

Wakizungumza baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa), Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo imewatia hamasa kubwa.

Awali akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.

“Mradi ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.Akizungumzia hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.

“Timu yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta, alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.

“Ufadhili umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.Aidha, alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na upatikanaji wa mashine.
Luana Reale, EU Tanzania
Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

Hospitali ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.Hospitali hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.
Toka mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.

Wataliano wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa patholojia na utafiti.Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
Hoyce Temu
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).


WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO YAPOKEA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.4 TOKA WHO.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dkt. Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.

‘’Ni msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’, alisema Dkt. Rusibimayila.

Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo nchini.

Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.


Kwa upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi nchini.

Aidha, ameongeza kuwa spesimeni za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa maabara.‘’Wanufaika wa huu msaada kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.

Kupitia wadau mbalimbali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.


Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakikabidhiana hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro (kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
 

RITA yaanza kukusanya ada za Usajili kwa njia ya kielekroniki.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Serikali inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

Hatua hiyo imefikiwa na Wizara Katiba na Sheria ili kuhakikisha Serikali inakusanya mapato kuanzia sasa na mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwahudumia wananchi.

“Tayari wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli” alisema Dkt. Mwakyembe.Katika kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.

Wilaya ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.Zoezi hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma, Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara, Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.

Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.Kwa mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni asilimia 79.

Ili kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.

Kampeni hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa asilimia 8.7.Kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera na Dodoma.

POINTI 3 ZA AZAM FC SAWA, BADO ZA COASTAL UNION

$
0
0
Muda mfupi uliopita Mapunda ameimbia mbeyacityfc.com kwamba kwa kosa hilo City ilistahili kupata ushindi huo wa bao 3 na pointi 3 kama ambavyo kanuni za ligi zinavyoelekeza na kutoa angalizo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kuongeza umakini katika kutunza kumbukumbu za adhabu au makosa mbalimbali kwa wachezaji wake.
“Kwenye hili nalipongeza shirikisho, hakika wametenda haki, na ninawaomba waendelee kusimama kwenye misingi ya haki, ni haki yetu kupata pointi 3 baada ya Azam fc kuchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kadi 3 ambaye ni wazi hakustahili kucheza mchezo ule, hata sisi tumekutana na hali hii katika nyakati tofauti lakini hatukuwahi kuthubutu kumchezesha mchezaji mwenye adhabu hata kama alikuwa ni muhimu kikosini” alisema.
Akiendelea zaidi Mwenyekiti Mapunda alisisitiza vilabu kuwa makini na matukio ya aina hii huku pia akiikumbusha TFF kuendele kuchukua hatua kama hizi.

Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa bado anaamini TFF itaitendea haki City kwa kuchukua hatua kama hizi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliovunjika dakika mwisho za kipindi cha pili baada ya kutokea kwa vurugu kubwa uwanjani zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo ya Tanga.

“Naamini TFF watatutendea haki kwenye hili pia,mchezo ule ulikuwa na matukio mengi ya ajabu ambayo yalimfanya mwamuzi kushindwa kumaliza mchezo, risasi za moto zilipigwa uwanjani, , sisi bado tunasubiri pointi tatu zingine kutoka kwenye mchezo ule, kwa sababu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”, alimaliza.
Mwenyekiti wa Mbeya City fc, Mussa Mapunda amelipongeza shirikisho la soka Tanzania TFF kwa hatua yake ya kuipoka pointi 3 timu ya Azam Fc na kuziweka kwa timu yake kufutia makosa yaliyofanywa na timu hiyo ya Chamazi Complex kumchezesha mchezaji Erasto Nyoni aliyekuwa na zuio la kadi tatu za njano.

zanchick yajipanga kushirikiana na wizara ya kilimo,maliasili,mifugo na uvuvi kuwasaidia wafugaji na wakulima wadogowadogo.

$
0
0
Uongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanchick } umejipanga kushirikiana na Wizara ya Kilimo,  Maliasili, Mifugo na Uvuvi katika kuwasaidia wafugaji na wakulima wadogo wadogo Nchini ili waendeshe miradi yao ya uzalishaji katika misingi ya kitaaluma.

Mkuu na muanzilishi wa Shamba hilo Dr. David Elua akiuongoza ujumbe wa Viongozi watatu wa shamba hilo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar.

Dr. David Elua alisema mpango huo uliolenga kutekelezwa pande zote mbili za Muungano, Tanzania Bara na Zanzibar utawanufaisha wanachi wa kipato cha chini zaidi ya 45,000 kwa kupata ajira katika uendeshaji wa miradi ya ufugaji kuku kwa kutumia njia ya kisasa.Alisema katika hatua ya awali shamba hilo tayari limeshatoa ajira zipatazo 300 katika kiwanda chake cha kutotoa vifaranga vya Kuku kiliopo Maruhubi juhudi zikiwekwa zaidi katika kuunga mkono azma ya Serikali Kuu katika uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

Dr. David alimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Sera hiyo iliyoanzishwa na Serikali na kuanza kukubalika kwa baadhi ya mashirika na taasisi za uwekezaji ndani na nje ya nchi itawasaidia zaidi vijana kupata ajira badala ya kusubiri ajira za serikali ambazo ni finyu kwa miaka ya sasa.

Akizungumzia ugonjwa wa kuambukiza wa kipindupindu ulioikumba Zanzibar katika Kipindi hichi Mkuu na Muanzilishi wa Shamba hilo la Kuku Maruhubi Dr. David alisema Uongozi wake umepata mshtuko kutokana na janga hilo linaloendelea kusumbua wananchi hasa Watoto wadogo.

Dr. David alisema Zanchick imeahidi kutoa mchango wa shilingi Milioni 10,000,000/- ili zisaidie nguvu ya Serikali katika mapambano yake dhidi ya maradhi hayo yaliyopoteza maisha ya watu wasiopungua 53 tokea yavikumbe Visiwa vya Zanzibar mwezi septemba mwaka uliopita.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Ujumbe wa Viongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanzchick } uliofika ofisini kwake kubadilishana mawazo juu ya sekta ya uwekezaji.Aliyempa mkono ni Mkuu na muanzilishi wa shamba hilo Dr. David Elua, wa kwanza kutoka kulia ni Meneja operesheni wa Shamba hilo Bw. Christopher Kontonasios na wa kwanza kutoka kushoto ni Nd. Issa Kassim.
 Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanzchick } ukiongozwa na Mkuu na muanzilishi wa Shamba hilo Dr. David Elua.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Shamba la Kuku Maruhubi { Zanzchick } mara baada ya mazungumzo yao.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu na muanzilishi wa Shamba hilo Dr. David Elua, Bwana Michael Mantheakis, Nd. Issa Kassim na kushoto ya Balozi Seif ni Meneja operesheni wa Shamba hilo Bw. Christopher Kontonasios.Picha na – OMPR – ZNZ.

msaada kwenye tuta: Watu hawa Wanatafuta ndugu zao

$
0
0
Ndugu Ally Said (40) amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu anatafuta ndugu zake ambao amepotezana nao . Kwa yoyote atakayemtambua afike Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Uhusiano.
Mwenye picha hapo juu ambaye jina lake halijafahamika amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, anatafuta ndugu zake ambao amepotezana nao .Kwa yoyote atakayemtambua binti huyu afike Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Uhusiano.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images