Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

BENKI YA KILIMO YAASWA KUTOA ELIMU KUHUSU KILIMO BORA.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,  Bw. Lephy Gembe (Katikati) akizungumza na maafisa wa kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (Kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda (Kushoto).
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal (Kushoto) wakati akitoa maelezo kuhusu Wajibu wa TADB katika kuendeleza kilimo nchini.
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal (Kushoto) akimsikiliza i Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (Kulia) walipomtembela Ofisini kwake.

Na Mwandishi wetu.
Benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeaswa kutoa elimu kuhusu kilimo bora ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,  Bw. Lephy Gembe wakati akiongea na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal alipomtembelea Ofisini kwake.

Bw. Gembe alisema kuwa ili kuinua uzalishaji wenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa kuendeleza TADB ina wajibu wa kutoa elimu ya kina kuhusu kilimo cha kisasa kwa kutilia mkazo kuhusu miundombinu muhimu ya kilimo mathalani skimu za umwagiliaji za kilimo ili kuongezea tija shughuli hizo za kilimo.

“TADB muna wajibu wa kuhamasisha kilimo cha kisasa na cha kibiashara kwa wakulima wadogo wadogo ili waweze kubadilisha fikra zao kutoka kilimo cha mazoea na kufikiria kilimo cha kisasa chenye tija kitakachoongeza kipato cha wakulima hao,” alisema Bw. Gembe.

MAMIA KUTOKA KILA PANDE ZA MAREKANI WAMUAGA ANDREW SANGA HOUSTON - TEXAS

$
0
0


Hapa ni mzazi mwenzie Andrew na mtoto wao mpendwa Zoe wakiwa mbele ya mwili wa marehemu.Mwili wa marehemu utawasiri Dar Es Salaam siku ya jumanne na jumatano ndugu na jamaa wa Dar_Es_Salaam wata Ibada ya misa na kuaaga mwili ndani ya kanisa la Lutheran nyuma ya Ubungo Plaza siku ya jumatano asubuhi kisha safari ya Dodoma jioni na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis May 05.

Mwakilishi wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani angeongea mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa na kuaga mwili wa Andrew.

Mzazi mwenza wa marehemu Andrew akitoa neno mbele ya watu waliojitokeza kuja kuaga mwili wa marehemu. 

MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

$
0
0
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.
Katika Tukio la Kwanza:

Mtoto wa miaka mitatu aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN mkazi wa Matemela Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu Journey ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ELIABU MYEKO (33) mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.


Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko katika Kijiji cha Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.


Aidha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo. Dereva alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na mmiliki wa Gari zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhi Kituo cha Afya Ipwani Wilayani Mbarali kwa uchunguzi wa kitabibu.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu azitoe kwa mamlaka husika ili akamatwe.


Katika Misako:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche 25 ya Bhangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.

Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.02.2016 majira ya saa 16:00 jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.


Aidhakatika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19) mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram 10.


Mtuhumiwa alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.

Imesainiwa na:

(EMANUEL G. LUKULA – ACP)

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KIJIPU UPELE ENEO LA TABATA MWANANCHI

Makamba awasilisha Bajeti ya wizara yake na kusisistiza umuhimu wa mazingira.

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma).

MKUU WA MKOA WA MWANZA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UNDP

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez, wakati akimkaribisha Ofisini kwake, leo Mei 2, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akimsikiliza Mkuu wa idara ya Siasa, Mawasiliano wa Umoja wa Ulaya, Luna Deals alipokuwa akizungumza jambo, leo Mei 2, 2016 wakati walipofika ofisini kwake. Ugeni huo ulieleza kusudio lao la kutembelea, MWAUWASA, SAUT, pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Jijini Mwanza.
Mazungumzo ya pamoja baina ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez.

Mara baada ya mazungumzo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akalazimika kuchagua kibao kinacho onesha ni maeneo gani kama mkoa wangepeda nguvu za uwekezaji zielekezwe.

UJENZI WA NYUMBA ZA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC WAKWAMA KWA ZAIDI YA MIAKA 21

$
0
0

Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe wakitoka kukagua nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.



Moja ya nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu /Mkurugenzi rasilimali Watu na Uendeshaji wa TBC Bi.Joycelin Lugora akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi wa wilaya ya Kisarawe (DED) Kisarawe Bi. Mwanamvua Mlindoko na kushoto ni Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBC na Wanahabari wakitoka kujionea hali halisi wakati Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe alipokwenda kukagua nyumba za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.PICHA NA ANNA NKINDA.


Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili zichezewe.

Na.Daudi Manongi-WHUSM

Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.

Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.

“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.

Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YATOA HATI YA KUKAMATWA KWA MEYA WA KINONDONI,BONIFACE JACOB

$
0
0
Na MweneSaid, Blogu ya Jamii, Dar.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani.

Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.

Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.

Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.
Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji.

Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jana, maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha Udiwani kata ya Ubungo.Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali.

Shitaka la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication Limited.

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOTEMBELEA BANDA LA SSRA KATIKA MAONESHO YA MEI MOSI YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JAMHURI MJINI DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akimpatia maelezo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo, katika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma jana.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akimsalimia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo, katika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akiwasalimia baadhi ya Maofisa wa Mamlaka hiyo, alipotembelea banda la mamlaka hiyo, katika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma jana.

MZIBUAJI BORA WA MWAKA

WIZI MTANDAO KWENYE TAASISI ZA FEDHA BADO NI CHANGAMOTO

$
0
0
Teknolojia imeendelea kurahisisha maisha na kwa sasa kumekua na ukuaji wa matumizi ya simu za viganjani kufanya miamala ya fedha maeneo mengi ya bara la Afrika. Kufuatia ongezeko kubwa la watumiaji wa simu, mabenki na kampuni za simu zimeendelea kuhakiki simu zinatumika kufanya miamala ya kifedha.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana (2015) ya GSMA State of the industry, huduma za kifedha kupitia simu kwa sasa zinapatikana katika nchi 93 duniani ikiwa na jumla ya huduma 271 kwa ujumla wake, kwa wastani watoa huduma za kifedha kupitia simu wana safirisha kiasi cha dola milioni 33 kwa siku. Takwimu hizi  zinategemewa kuendelea kukua.

Aidha, Mwaka jana (2015), European investment bank ilianisha Afrika kuongoza duniani kwa matumizi ya Simu za viganjani kufanya miamala yakifedha. Kwa Upande wa Nchi ya Kenya, asilimia 62 (62%) ya watu wake wamekua wakitumia simu za viganjani kufanya miamala ya kifedha.

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

$
0
0
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.

Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Jaji Mstaafu kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume kwa sasa.

Mheshimiwa Jaji Mstaafu Lubuva amesema Tume yake imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ya Kwanza ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa Taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais mapema mwezi Julai mwaka huu.

Aidha pongezi kama hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhan Kailima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume akieleza kufurahishwa kwake na namna ambavyo dhana ya ushirikishwaji imetumika katika kuandaa Rasimu hiyo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliratibu na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuanzia Otoba 25 mwaka jana na kuhitimisha rasmi zoezi hilo Machi 20 mwaka huu kwa Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele mkoa wa Kaskazini Unguja.

RC Morogoro aamuru kukamatwa kwa mwalimu aliepokea mshahara bila kufanya kazi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe ameamuru kukamatwa kwa Mwalimu Hamisi Salumu Mkoleme kwa tuhuma za kulipwa mishahara ya mwaka mmoja na nusu bila kufanya kazi katika kituo chake alichopangiwa baada ya uhamisho kutoka mkoa wa Tanga kwenda mkoa wa Morogoro bila kuripoti katika kituo alichopangiwa.

Akizungumza na walimu waliofika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mvomero ili kuhakikiwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Stephen Kebwe ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mvomero kusimamia kwa ukamilifu zoezi hilo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema wameamua kuchukua hatua za kupitia upya orodha aliyokabidhiwa na Halmashauri ili kujiridhisha na kwamba iwapo itabainika mwalimu yeyote amefanya kosa kama hilo, hatua kali zitachukuliwa.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho. PICHA NA IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.

Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016

Kamati ya maandalizi siku ya Utamaduni Duniani yaanza maandalizi

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Hajjat Shani Kitogo (aliyesimama) akiongoza majadiliano jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe ya 21 Mei.
Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Sefania Motela (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Bw. John Mponda (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
 

BUNGE LAOMBWA KUUNGA MKONO SERIKALI YA JPM KATIKA KUKUSANYA KODI KWA MAENDELEO

WAKAZI WA TEMEKE WAMIMINIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII 'NSSF'

$
0
0
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande)
Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

BUNGE LAOMBWA KUUNGA MKONO SERIKALI YA JPM KATIKA KUKUSANYA KODI KWA MAENDELEO

YANGA KUPATA UONGOZI MPYA MEI 27 MWAKA HUU

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BODI ya Wadhamini ya Timu ya Yanga imetakiwa kuwaarifu wanachama wao juu ya uchaguzi utakaofanyika Mei 27 mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa timu hiyo, Baraka Deusdedit ilisema kuwa utawala wa uongozi wa yanga ulimalizika Julai 14,  2014.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) iliitaka Kamati ya utendaji wa timu hiyo kufuata maadili ya katiba ya Klabu hiyo kutokana na maagizo ya FIFA ya kufanya uchaguzi Juni 30, 2014.

Hata hivyo uongozi wa yanga uliweza kufanya mkutano wa dharula wa wanachama na kushindwa kutimia kwa akidi ya bodi ya wadhamini pamoja na wanachama na kufanya Mwenyekiti na Makamu wake kuendelea na uongozi pamoja na kufanya marekebisho ya katiba ya uongozi huo kuendelea na kazi.

Katika taarifa hiyo ilisema  klabu ya yanga ilitakiwa kufanya uchaguzi katikati ya Mei mwaka jana lakini serikali iliwataka kuahirisha uchaguzi wao na timu hiyo haikuweza kufanya pingamizi hilo  kutokana na kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge pamoja na madiwani.

Timu hiyo katika taarifa yake ilieleza kuwa watafanya uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo na mamlaka yake bila kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maagizo hayo yalitolewa na TFF pamoja na mamlaka za michezo ya kufanya uchaguzi ndani ya siku 33 ambapo kipindi hicho si sahihi kwa klabu ya yanga huku timu yao ikiwa katika mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la FA pamoja na  Mashindano ya Kombe la Afrika.

Wanahabari waashwa kushirikiana na Wadau wa Afya kuelimisha Jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

$
0
0
 Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Wanahabari nchini wametakiwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na afya.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Bi. Neema Rusibamayila wa Wizara hiyo, Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia amesema kuwa suala la kuielimisha jamii lina umuhimu ndo maana kuna haja ya Wizara kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza suala hilo.

Ameeleza kuwa Shughuli za kibinadamu zinachangia kwa kiasi cha asilimia 95 katika kuzalisha na kuongeza kiasi cha gesi joto katika kwenye anga hewa ambapo amezitaja baadhi ya shughuli hizo zikiwemo za uzalishaji viwandani, uzalishaji nishati, kilimo,ufugaji, ukataji miti, uchomaji misitu, usafirishaji, pamoja taka. 

Akitaja athari za mabadiliko ya tabianchi, Dkt. Azma ameeleza kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa joto juu ya wastani, ukame, mafuriko, vimbunga, kubadilika kwa mgawanyo na muda mvua kunyesha pamoja na kuongezeka kwa kina cha bahari.

‘’Sisi sote ni mashahidi wa mabadiliko ya hali hewa yalivyokuwa tishio katika afya ya binadamu. Mabadiliko hayo yameendelea kuleta athari mbalimbali kwa jamii, mazingira na afya ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, hewa safi, uhakika wa upatikanaji wa chakula na makazi salama’’, alisema Dkt. Azma.

Ameongeza kuwa athari hizo zimepeleke uwepo wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza ikiwemo malaria, kuhara, kipindupindu, homa ya bonde la Ufa, denge, utapiamlo, magonjwa ya mfumo wa upumaji na magonjwa ya mfumo wa fahamu.

‘’Jamii ina fursa ya kuboresha afya yake na vizazi vijavyo endapo itaamua kubadilisha mfumo wa maisha unaochangia uzalishaji na ongezeko wa jotogesi unaoharibu (ozone) yaani tabaka hewa’’, aliongeza Dkt. Azma.
 Msimamizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Geofrey Mchau akitoa mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
 Afisa Habari toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bwana Saidi Makola akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi akisoma taarifa ya Mkurugenzi toka Wizarani leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Afisa Habari toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Catherine Sungura akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.

 

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images