More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 24161 to 24180 of 65393)
- 05/03/16--07:11: _KATIBU WA BUNGE AKU...
- 05/03/16--07:43: _ TAASISI YA MUZDALI...
- 05/03/16--08:00: _KUFUATIA UHURU WA V...
- 05/03/16--08:04: _ Airtel yatoa Furs...
- 05/03/16--08:23: _WADAU WAJADILI TOZO...
- 05/03/16--08:53: _SAFARI YA KUTOKA IF...
- 05/03/16--11:54: _TIZA YA JOTO LA ASU...
- 05/03/16--11:59: _TIRA YAKUTANA NA WA...
- 05/03/16--14:11: _KIJIPU UPELE KIJITO...
- 05/03/16--14:29: _SIMU TV: HABARI KUT...
- 05/03/16--14:35: _UAMUZI WA KAMATI YA...
- 05/03/16--14:40: _Zuriel Wows at Keyn...
- 05/03/16--14:43: _YALE YALEEE...
- 05/03/16--14:45: _shamba mfano la Ofi...
- 05/03/16--14:53: _MBUNGE ABDALLAH ULE...
- 05/03/16--21:00: _ UMOJA NA MSHIKAMAN...
- 05/03/16--22:00: _Vijipu upele nje ya...
- 05/03/16--23:00: _RAIS DKT. JOHN MAGU...
- 05/04/16--00:00: _RAIS DKT. MAGUFULI ...
- 05/04/16--01:48: _INTRODUCING "Ningej...
(showing articles 24161 to 24180 of 65393)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth
0 |
|
0 |
|

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongea na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT kwenye Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam kuhusiana na namna walivyojipanga katika kutekeleza jukumu la utengenezaji wa Madawati ya shule hapa nchini.




0 |
|
0 |
|



0 |
|
0 |
|
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network'– TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
· Airtel yatoa ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi) kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.
Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel imejikita na kushiriki katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.
Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake na ndio mana tunatoa fursa kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi.
Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.
Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel nchini Kenya na India kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi
Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa nchini India na Nairobi, nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu
Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa. Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi, Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi Abubakar Nassor baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi James Kwayu baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika katika makampuni mbalimbali kila mwaka
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na James Kwayu na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na ajira kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Joseph Nyamhanga amewataka watumiaji wa Daraja la Nyerere (Kigamboni) kuzingatia matumizi bora na sahihi ya daraja hilo ikiwemo usafi ili kuliwezesha kukidhi matarajio ya serikali na kudumu kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kikao maalum cha wadau kutathimini viwango vya tozo vitakavyotumiwa katika daraja hilo Eng. Nyamhanga amewataka waendeshaji wa daraja hilo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuimarisha huduma ya ulinzi na usalama na kuwataka watumiaji wa daraja hilo kutumia fursa za uwepo wake kiuchumi na kijamii.
“Hakikisheni tozo zitakazowekwa ziwiane na hali ya maisha ya wananchi ili kuwavutia wengi kupita katika daraja hili na kupunguza msongamano katika vivuko”, amesema Eng. Nyamhanga.Tozo hizo ambazo zitaanza kutozwa kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere hivi karibuni zinalenga kuwezesha NSSF kurudisha gharama za uwekezaji katika daraja hilo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhujumu miundombinu na kukemea vitendo vya watu kufanya biashara katika daraja hilo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara amesema tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere itaanza hivi karibuni baada ya kupitishwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, hivyo amewataka watumiaji wa daraja hilo kutoa ushirikiano kwa watendaji ili kuwezesha huduma kufanyika kama ilivyokusudiwa.
“Tumejipanga Vizuri na tutaanza kutoza watumiaji wa Daraja la Nyerere muda mfupi kuanzia sasa.” amesema Prof. Kahyarara.Zaidi ya shilingi Bilioni 214 zimetumika katika ujenzi wa Daraja la Nyerere ambapo asilimia 60 zimegharamiwa na NSSF na asilimia 40 zimegharamiwa na Serikali Kuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (katikati) akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji katika kikao cha kujadili viwango vya tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Kahyarara na kushoto ni Mkurugenzi wa barabara (Ujenzi) Eng. Ven Ndyamukama.

Mkurugenzi wa Barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Ven Ndyamukama (Kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha wadau kujadili tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Eng, Joseph Nyamhanga
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara (kulia) akitoa taarifa ya namna tozo zitakavyokusanywa kwa wadau mbalimbali wanaotumia Daraja la Nyerere zoezi litakaloanza hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli akitoa maoni ya namna ya kuwahudumia waendesha baiskeli katika kikao cha kujadili tozo zitakazotumika kataka Daraja la Nyerere.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kujadili tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere, Tozo hizo zitatangazwa hivi karibuni.
Akizungumza katika kikao maalum cha wadau kutathimini viwango vya tozo vitakavyotumiwa katika daraja hilo Eng. Nyamhanga amewataka waendeshaji wa daraja hilo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuimarisha huduma ya ulinzi na usalama na kuwataka watumiaji wa daraja hilo kutumia fursa za uwepo wake kiuchumi na kijamii.
“Hakikisheni tozo zitakazowekwa ziwiane na hali ya maisha ya wananchi ili kuwavutia wengi kupita katika daraja hili na kupunguza msongamano katika vivuko”, amesema Eng. Nyamhanga.Tozo hizo ambazo zitaanza kutozwa kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere hivi karibuni zinalenga kuwezesha NSSF kurudisha gharama za uwekezaji katika daraja hilo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhujumu miundombinu na kukemea vitendo vya watu kufanya biashara katika daraja hilo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara amesema tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere itaanza hivi karibuni baada ya kupitishwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, hivyo amewataka watumiaji wa daraja hilo kutoa ushirikiano kwa watendaji ili kuwezesha huduma kufanyika kama ilivyokusudiwa.
“Tumejipanga Vizuri na tutaanza kutoza watumiaji wa Daraja la Nyerere muda mfupi kuanzia sasa.” amesema Prof. Kahyarara.Zaidi ya shilingi Bilioni 214 zimetumika katika ujenzi wa Daraja la Nyerere ambapo asilimia 60 zimegharamiwa na NSSF na asilimia 40 zimegharamiwa na Serikali Kuu.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (katikati) akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji katika kikao cha kujadili viwango vya tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Kahyarara na kushoto ni Mkurugenzi wa barabara (Ujenzi) Eng. Ven Ndyamukama.

Mkurugenzi wa Barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Ven Ndyamukama (Kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha wadau kujadili tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Eng, Joseph Nyamhanga

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara (kulia) akitoa taarifa ya namna tozo zitakavyokusanywa kwa wadau mbalimbali wanaotumia Daraja la Nyerere zoezi litakaloanza hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli akitoa maoni ya namna ya kuwahudumia waendesha baiskeli katika kikao cha kujadili tozo zitakazotumika kataka Daraja la Nyerere.

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kujadili tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere, Tozo hizo zitatangazwa hivi karibuni.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
"Safari ya kutoka Ifakara kwenda wilaya za Malinyi na Ulanga ni ngumu kuliko unavyoweza kuelezea, kukwama barabarani na kulala njiani sasa ni vitu vya kawaida kama inavyoonekana hapa" Picha kwa hisani ya Vedasto Msungu Technologies.
Baadhi ya Abiria wakijishughulisha namna ya kujinasua kwenye eneo hilo kutokana na hali halisi ionekanavyo pichani
Meneja wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa wadau wa soko la Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya).
Wadau wa soko la Bima Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juuu Kusini,Mbeya,Iringa,Njombe ,Rukwa ,Songwe na Katavi wakiwa katika umakini kufuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo ulioandaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (TIRA).
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 |
|
0 |
|
Kamera ya mulika "Vijipu Upele" leo imeinasa taswira hii ya vijana wanaojihusisha na shughuli ya ubebaji taka katika ameneo ya makazi ya watu, wakiumwaga uchafu huo katika dampo kivuli eneo la Kijitonyama kando ya Barabara inayoelekea Sayansi kutokea Tandale kwa Alimaua, Jijini Dar.
0 |
|
0 |
|

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo Mei 3, 2016 imetupilia mbali rufaa saba kati ya nane zilizowasilishwa mbele yake na viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016 maarufu kama StarTimes League.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati, Wakili Revocatus Kuuli ametangaza uamuzi mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo unatokana na kikao cha akidi iliyotimia ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati, Wakili Revocatus Kuuli pamoja na wajumbe wawili, Dk. Francis Michael na Abdallah Shaweji. Kadhalika warufani wote walihudhuria kikao hicho kilichojadili rufaa hizo Jumapili Mei mosi, 2016.
Kamati imemtoa hatiani Kipa wa Geita Gold, Denis Richard Dioniz baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa jukumu lake kupanga muda wa mchezo kwa mujibu wa kanuni kutokana na kutumia muda mrefu maliwato baada ya kuugua tumbo kama ilivyoripotiwa na mwamuzi na kamisaa wa mchezo.
Dioniz alifungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000). Adhabu hiyo alipewa na pamoja na Kipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa. Mohamed hakukata rufaa baada ya kuadhibiwa Aprili 3, 2016.
Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Ambao rufaa zao zimetupwa ni:
Timu ya Geita Gold
Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
Timu ya Soka ya Polisi Tabora
JKT Oljoro Fc ya Arusha
Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Katika adhabu hizo leo Kamati ya Rufaa ya Nidhamu imebariki adhabu kwa Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC aliyetiwa hatiani kwa kumshawishi Mohammed - kipa wa JKT Kanembwa FC kukaa golini ili penalti aliyogomea kabla ipigwe.
Awali, Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
Kuhusu Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora na Fatel Rhemtullah ambaye ni Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora hao imeamuriwa kuendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu kama Mwenyeakiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian
Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zilikutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao, hivyo kamati imeamuru adhabu hiyo iendelee.
Uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya TFF Aprili 3, 2016 ilitoa uamuzi wa shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza. Aliyesoma hukumu hiyo ni Wakili Jerome Msemwa ambako alisema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.
Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C sambamba na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu kamisaa wa mchezo wa Geita Gold na JKT Kanembwe, Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji matokeo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge, Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu ya JKT Kanembwa Basil Matei waliachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.
Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde walifungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.
Katibu wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro, Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba, na Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Mrisho Seleman, waliachiwa huru na Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.
The sleepy coastal and seaside resort town of Ocean City - Maryland in the North East corner of the United States plays host once a year at the end of April to the annual Maryland State Conference of Child Educators. It is the learning, audit, and re-tooling program where the states frontline childcare Educators and policymakers gather to grade their performances and get ready for the new challenges of raising the next generation of Maryland States global citizens.
This year however, the organizers wanted something new, something different, revitalizing, and a strong shot in the arm of those saddled with the responsibility of shaping the future of the states human capital.
Fresh off her interview 3 weeks ago of meeting her 19th World Leader - Nigeria's President Muhammadu Buhari in Washington DC, Zuriel was invited and gave the Keynote address earlier today to a gathering that was unsuspecting and non expectant of this 13 year old Girl, who astounded them with her command of related issues, and challenged her audience to be different, creative and more engaging going forward.
She addressed the conference both in English and in Chinese, underscoring the need for the learning of more global languages, if their students are to be competitive in tomorrows new business word.
A film maker and a girl child education advocate, she recieved a standing ovation from the 600 plus delegates at the end of her 45 minutes presentation, with the theme "How to Effectively Educate" the next generation of Americans.
Ofisa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Claudy Losiock (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya madiwani na mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Kambona (kushoto) kwenye shamba lake ambalo ni darasa kwani amelima na kupanda kitaalamu.
(Picha na Woinde Shizza, Simanjiro).
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.
Na Owen Mwandumbya,
Midland Afrika Kusini.
Midland Afrika Kusini.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili.
“ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai





Uchafu wa aina mbalimbali ukiwa umeziba kabisa mitaro pembeni mwa barabara ipitayo pembzoni mwa uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo. Uchunguzi unaonesha kuwa karibu mitaro ya mji mzima wa Dodoma imezibwa hivyo.
Hatukufanya juhudi za kuwatafuta wahusika kwani kama mtu anajua wajibu wake kwa nini akumbushwe?? Na kama hajui wajibu wake na anafanya kazi kwa mazoea....Wahusika mpo??
Hatukufanya juhudi za kuwatafuta wahusika kwani kama mtu anajua wajibu wake kwa nini akumbushwe?? Na kama hajui wajibu wake na anafanya kazi kwa mazoea....Wahusika mpo??
Ngoma inaishia hapa....
0 |
|
0 |
|


PICHA NA IKULU
0 |
|
0 |
|
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.