Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110164 articles
Browse latest View live

Vyama Vya Siasa Vimekutana Kujadili Mapendekezo ya Mfumo Wa Utatuzi wa Migogoro Ndani na Baina ya Vyama

$
0
0
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini ambalo linaundwa na  wawakilishi wawili kutoka kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa .

Mapendekezo hayo yalitolewa na Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama  vya siasa  nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  na kwa udhamini  wa UNDP  kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa  ya mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini. Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini vikiwemo vyama vya siasa.

Akiwasilisha mapendekezo, Msajili Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa  ilipendekezwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu  wa kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro  ndani ya chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa  na kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa  sehemu ya mapendekezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza.

“Upatanishi ukishindikana mgogoro husika uwasilishwe kwenye Baraza  la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa Baraza  la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa Baraza. Muhusika asiporidhika  na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata  rufaa Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.

Aidha kumekuwa na msisitizo wa kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama  kwenda moja kwa moja  Mahakamani ambako huchukua muda mrefu  na kuathiri ukuaji wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.
Bw. John Cheyo mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.


RC MAKONDA AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI DAR LEO

$
0
0

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na baadhi ya waheshimiwa wengine wakisimama Jukwaa kuu wakati wakipokea rasmi maandamano ya Wafanyakazi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo Mei 1, 2016.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Picha zote na Mafoto Blog
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Raawu......
Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hizo......

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAHALIFU WAWEKEWA MKAKATI MZITO MKOANI DODOMA

$
0
0
Na. Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Dodoma

Katika kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba nchini,  makamanda wa Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha mashtaka wameazimia kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za wahalifu pindi zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa  adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamo katika maazimio ya watendaji hao wa haki jinai nchini katika kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika  mkoani Dodoma na kuwashirikisha makamanda wa polisi wa mikoa,  mawakili wafawidhi wa mikoa  na wakuu wa upelelezi wa mikoa.

Kikao hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wake Mkuu wa Jeshi la Polisi,  IGP Ernest Mangu pia kilihudhuliwa na mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP  Biswalo Mganga, Makamishina wa Polisi, pamoja na taasisi mbalimbali zinazohusika na upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.

Wapelelezi hao na waendesha mashtka walisema wataendeleza  program za mafunzo ya pamoja katika ngazi ya mkoa, kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili  na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano lengo likiwa kuharakisha upelelezi  na kutoa haki kwa watuhumiwa.

Aidha,  wajumbe hao wa haki jinai wameazimia pia kukabiliana na changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi  wa kesi ambapo wamekubaliana kwa pamoja kuzifikisha mahakamani kesi zote zenye ushahidi wa moja kwa moja ili kuondokana na kesi kuchua muda mrefu na kuleta malalamiko kwa wananchi.

HIVI NAVYO NI VIJIPU UPELE VINAVYOTAKIWA KUTUMBULIWA

$
0
0
Katika pita pita za hapa na pale, Kamera ya Globu ya Jamii ilifanikiwa kuzinasa baadhi ya taswira kadhaa katika Barabara ya Morogoro rodi jijini Dar es salaam hasa katika ile njia maalum kwa mabasi ya endayo haraka. 

Njia hii imekuwa ikipendwa sana kutumiwa na ndugu zetu waendesha Bodaboda, kwa madai kwamba hiyo ni njia nyepesi zaidi kwao kwa safari zao. Lakini njia hiyo si yao na wanafahamu fika matumizi ya njia hiyo, lakini bado wao wanaendelea kujiachia tu, kana kwamba hawafahamu lolote au ni njia iliyotengenezwa kwa matumizi yao. 

Ni hivi karibuni Mabasi hayo yaendayo haraka yameanza kufanyiwa majaribio katika njia hizo, ila cha kushangaza kama si chakustaajabisha ni pale ndugu zetu hao wa Bodaboda wanapoendelea na matumizi ya njia hiyo, na wakati mwingine kulazimisha kutaka kulipita hata basi hilo katika sehemu ambayo hata ujiti hauwezi kupita. 

Jambo hili yapaswa kuangaliwa kwa jicho kali sana, maana kama vijipu upele hivi vitaendelea kuwepo, basi kuna siku vitakuja kuwa vidonda vikubwa na vishindwe kutibika.

DKT. SHEIN KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA KILELE CHA WAFANYAKAZI DUNIANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Wafanyakazi wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) na bango lao linalotoa ujumbe"IDARA YA FIDIA NI UTI WA MGONGO WA MAISHA YA WAFANYAKAZI NI MUHIMU KUANZISHWA" wakati alipokuwa akipokea maandamano ya Wafanyakazi wa Taasisi mballi mbali za Serikali na Binafsi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

UMEGUNDUA NINI KWENYE HII PICHA?

HIKI SIO KIJIPU UCHUNGU KWELI???

$
0
0
Kipo eneo la Sinza Bamaga, ubavuni mwa kiota Maarufu cha Hongera jijini Dar es salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WAFANYAKAZI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Rais Dkt.Magufuli ahutubia Mei Mosi, atangaza kupunguza kodi ya mishahara kwa 2%

MIFUKO YA JIMBO IGUNGA YACHANGIA MATENGENEZO YA MADAWATI

$
0
0
WILAYA ya Igunga,Mkoani Tabora imetenga zaidi ya shilingi milioni 73 kutoka katika mifuko ya jimbo la Igunga mjini na jimbo la Igunga magharibi(Manonga) kwa ajili ya ununuzi wa madawati,ukarabati wa nyumba za walimu,ujenzi wa matundu ya vyoo katika baadhi ya shule na zahanati na kufuatilia matumizi ya shilingi milioni 50 zilizotolewa na mfuko wa jimbo kukamilisha baadhi ya majengo ya maabara za shule za sekondari wilayani hapa.

Akitoa taarifa ya mfuko wa jimbo la Igunga Magharibi,Mbunge wa jimbo hilo, Seif Khamis Gulamali amefafanua kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha,zaidi ya shilingi milioni 35 zimetoka katika mfuko wa jimbo la Igunga magharibi na zaidi ya shilingi milioni 38 jimbo la Igunga mjini.

Aidha Mbunge Gulamali hata hivyo amebainisha kwamba lengo la mfuko huo wa jimbo kutoa fedha hizo katika shule za sekondari ni kuzijengea shule hizo mazingira ya kuziwezesha kuwa na sifa ya kupata kidato cha tano na sita katika kipindi cha miaka ijayo.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa wananchi wa jimbo la Igunga magharibi shilingi milioni kumi nyingine zimepelekwa katika shule ya sekondari Mwisi na shilingi milioni tano kwa kuchimba matundu ya vyoo na shimo la kutupia sindano katika zahanati.

Hata hivyo Gulamali ameweka bayana kuwa fedha hizo zilizotumika zimetoka katika bajeti ya mwaka unaoishia juni,30,mwaka huu na kuongeza kwamba katika bajeti ijayo ya 2016/2017 fedha itakayopatikana itazidi kuboresha na maeneo mengineyo ili kuhakikisha kwamba malengo yanafikiwa na kwa wakati uliopangwa.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Igunga mjini,Dk. Peter Dalali Kafumu ameweka wazi kwamba mfuko wa jimbo umedhamiria kutumia shilingi milioni 38 kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika jimbo hilo.

Aidha mfuko huo wa jimbo umetoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya kupaua nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Mwakipanga iliyokuwa imeezuliwa na upepo na hivyo kuwafanya wanafunzi wa shule hiyo kusomea nje kwa kukaa kwenye miti ambako huko nako wamepeleka shilingi milioni 12.

Akibainisha zaidi Dk.Kafumu ameweka wazi pia kwamba shilingi milioni mbili zilipelekwa kujenga matundu ya vyoo katika shule ya Ntobo na shilingi milioni mbili zilizobakia zitatumiwa na kamati iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia matumizi ya shilingi milioni 50 zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara.

Amesisitiza kwamba hatua ya kuundwa kwa kamati hiyo kumetokana na idadi kubwa ya wananchi kutoka katika vijiji mbali mbali kulalamikia matumizi ya fedha hizo pamoja na mifuko ya saruji zilizopelekwa kuwa hazijafika.
Mkuu wa wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora, Bi Zippora Pangani akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo uliofanyika mjini Igunga.
Mbunge wa jimbo la Igunga magharibi (Manonga), Mkoani Tabora, Seif Khamisi Gulamali (kulia) pamoja na Mbunge wa jimbo la Igunga mjini, Dkt. Dalali Kafumu (shoto) wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika mjini Igunga.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa kwenye mkutano wa kawaida wa baraza la Halmashauri hiyo uliofanyika mjini Igunga.

UKURASA MPYA WA KIPINDI CHA JOTO LA ASUBUHI CHA EFM 93.7

$
0
0
Watangazaji mahiri Gerald Hando na Paul James (PJ) wameanza rasmi kutangaza 93.7 Efm redio siku ya leo ya tarehe 02/05/2016 katika kipindi cha Joto la asubuhi kilichoboreshwa wakiwa pamoja na Adela Tilya live nje ya jengo la K- net house zilipo ofisi za E fm. Kipindi hiki kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa 3:00 Asubuhi. Usipitwe.
 Kutoka kushoto ni Gerald Hando, Adella Tillya, pamoja na Paul James wakitangaza kipindi cha JOTO LA ASUBUHI live chini ya jendo la K-net house Kawe Beach Dar es salaam leo asubuhi.
  Rdj Spar akisababisha muziki live katika kipindi hicho asubuhi ya leo
  Timu nzima ya Joto la Asubuhi katika picha ya pamoja na baadhi ya mashabiki wa Efm Redio walioshiriki katika kipindi hicho
 Timu nzima ya joto la asubuhi pamoja na Rdj spar,
Gerald Hando akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake mzazi  pamoja na dada yake walipofika katika ofisi za EFM  redio kumpongeza.

Mtoto Getrude ni fahari yetu baada ya kung'aa Umoja wa mataifa.

$
0
0
Mbunge WA jimbo  ilemela na Naibu waziri a Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angeline Mabula amempokea mtoto Getrude mjini dodoma baada ya kuwasili kutoka nchini marekani alipokwenda kuwa wakilisha maripota watoto duniani ktk mkutano WA UN.mtoto Getrude ni mwana ilemela anae soma shule ya mnarani wilayani hapa.awapo bungeni kesho mtoto Getrude atapata nafasi ya kutambulishwa rasmi  bungeni na atakutana na viongozi mbalimbali WA serikali.

Airtel Fursa yasaidia kikundi cha Vijana Wajasiriamali katika mradi wa kutunza mazingira

$
0
0
Airtel Fursa imewapatia pikipiki mbili aina ya Guta, na vifaa vya kufanyia usafi kwa kikundi cha Pambana

Dodoma, Jumapili 1 Mei 2016, Pambana ni kikundi cha vijana 30 wajasiriamali kinachojishughulisha na shughuli mbalimbali katika jamii kama kukusanya taka, kuzalisha na kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini Dodoma, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi, mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na vifaa vingine vya usalama vya kufanyia kazi zao.

Afisa uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa juhudi zao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, " Tumeamua kutoa vitendea kazi vya usafi ili kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia lengo kuu la kuhakikisha maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya usafi na hivyo kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla. Sambaba na hili Airtel imeona nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na kukuza biashara yao".

"Kikundi cha Pambana kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Kaniki."Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao." alisema Kaniki.

Kwa upande mwingine kundi la Pambana waliahidi kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi.Kiongozi wa kikundi hicho, Amasha Zuberi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana zaidi katika Jamii.

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo Majengo jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) MANGULA AKUTANA NA WAZIRI MAMBO YA NJE KUTOKA CHINA MJINI DODOMA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara ) Mhe. Philip Mangula akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo wa CPC Mhe. Guo Yezhou mjini Dodoma ambapo walizungumzia mahusiano imara kati ya Tanzania na China pamoja na mipango mbali mbali ya kimaendeleo.
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mbao ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China Mhe. Guo Yezhou mjini Dodoma.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NGOMA AFRICA BAND YAWATAKIA HERI YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki aliens inayoongozwa na mwanamuziki mashuuri Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja inaungana na wadau wote wa habari duniani kwa kuwatakia kila la heri na baraka wanahabari na vyombo vyao kwa kusherehekea siku ya Uhuru wa Habari duniani.Bendi inaungana na wadau wote wa habari kwa wimbo maarumu wa "Uhuru wa Habari" utunzi wake kamanda ras Makunja . Sikiliza song: Uhuru wa Habari.

Wanadiaspora watakiwa kuwekeza nyumbani

$
0
0
Nembo ya ZADIA
Na Mwandishi wetu Washington

Wazanzibari waishio nchi za nje wametakiwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa.

Wito huo ulitolewa jana na maofisa kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zaznzibar (ZSSF) wakati wakizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliondaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), Meneja wa Mipango na Uwekezaji kutoka ZSSF Bwana Khalifa Muumin Hilal alisema kuwa Taasisi yake ina miradi kadhaa ya uwekezaji inayoendeshwa kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar, na kwamba inawahamasisha Wazanzibari waishio Ughaibuni kuwekeza katika miradi hiyo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ambao ujenzi wake tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

TAARIFA YA MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI KUTOKA WIZARA YA AFYA

MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV ILIVYOSHUHUDIA DAMPO KOROFI LA KATA YA MAANGA JIJINI MBEYA LIKIPIGWA MSASA SIKU YA USAFI

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI,MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika leo katika ukumbi wa Tamisemi Mjini Dodoma,(wa pili kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016.
[Picha na Ikulu.]

WAKUU WA IDARA WA MANISPAA ZA JIJINI LA DAR ES SALAAM WALA KIAPO KUTAFUTA WATUMISHI HEWA.

$
0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugeni pamoja na wakuu wa idara mabalimbali za manispaa na jiji la Dar es Salaam leo.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakisaini mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa zao jijini Dar es Salaam, na atakaye shindwa kuwajibika  katika kufanya kazi  na baadae wakija kujulikana atawajibishwa yeye.
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakiapa kiapo cha mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jijini la Dar es Salaam leo walipo apishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa mkataba wa wiki moja wakuu wa Idara za Manispaa za jiji la Dar es Salaam kutafuta watumishi hewa.

Wakuu wa Idara za Manispaa watakaoshindwa kufanya hivyo wataundiwa tume ambayo itapita katika manispaa hizo kuhakiki watumishi hewa na endapo watumishi hewa wakibainika kuwepo mzigo utabebwa na wakuu wa Idara kulipa mishahara hewa hiyo.

Makonda ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Pamoja na Wakuu Idara mbalimba za manispaa za jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa mkataba huo kila mtu lazima afanye kazi  na sio  na  kukimbizana au kuamrishishana.

 Amesema kuwa mara ya kwanza walipatikana watumishi 71 lakini baada ya kuweka mkazo wamefikia 209 ambao wanalipwa zaidi ya sh.bilioni 2.9 ambapo fedha hiyo zingefanya kazi nyingine ya kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa kusukumana wakati kazi hiyo waliomba wenyewe na kuahidi kutekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa kwenda kuangalia vitu vya kihuduma kwa wananchi sio yake, lakini inatokana na wale wenye wajibu wa  kutekeleza majukumu yao kufanya uzembe tu.

 Makonda amesema kuwa zoezi la kutafuata watumishi hewa lazima lifike kikomo na kuweza kufanya mambo mengine ya kutatua changamoto za wananchi ambazo zimetokana na watu kujisahau kutimiza wajibu wao.
Viewing all 110164 articles
Browse latest View live




Latest Images