Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1204 | 1205 | (Page 1206) | 1207 | 1208 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Baada ya jana kuiripoti habari ya lile dampo haramu la temeke mwisho, sasa kijipu upele kilichokuwa kikisumbua na kukera watu wa Temeke Mwisho, Kimetumbuka kabla hata ya kupakwa kitunguu swaumu. Lile dampo korofi limesafishwa usiku mzima wa kuamkia leo, na hali sasa ni kama unavyoiona katika picha.

  Somo hapa ni kwamba;

  1. Tusifanye kazi kwa mazoea, mpaka watu walalamike baada ya kudhurika- reactive mode 
   2. Kama uwezo wa kusafisha uchafu ule kwa usiku mmoja upo, kwa nini msingefanya hayo tangia siku za nyuma

  SISI WAKAZI WA KARIBU NA ENEO HILI, TUNAOMBA DAMPO HILI LIONDOLEWE HAPA, NA KIWANJA HIKI CHA WAZI KILICHOVAMIWA WARUDISHIWE VIJANA WETU WA TEMEKE WAENDELEE KUKITUMIA KWA MATUMIZI CHANYA.
  Najua wahusika mnaisoma Globu hii ya Jamii na suala hili linaloharibu mandhari nzuri ya temeke mwisho mtalifanyia kazi.
  Malori yakipishana kuondoa uchafu uliokuwa umerundikwa kwenye dampo hilo.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) Bw. Erick Chrispin akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa hilo unaofanyika kila mwisho wa mwezi jana jijini Dar es Salaam. Mada kuu katika mjadala huo ilikuwa ni “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake”
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Asasi ya Open Mind Tanzania (OMT) ambaye pia ni Mratibu wa Programu ya Kukuza Ajira zenye staha jijini Dar es Salaam(YEID) Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha maada kuhusu misingi ya ujasiriamali wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
  Meneja Matukio na Ushirikiano wa Asasi ya Buni Innovation Hub Bi. Maryam Mgonja akielezea kuhusu namna asasi yao inavyofanya kazi wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).


  0 0

  Na John Nditi, Morogoro 

  SERIKALI ya mkoa wa Morogoro imetoa Sh milioni kumi kwa ajili ya kununua unga na maharage kwa ajili ya waathirika  8,800 wa mafuriko  yalitotokea katika vijiji kadhaa vya  halmashauri ya wilaya ya Morogoro.

  Mbali na mkoa pia halmashauri ya wilaya  imetoa Sh milioni tatu kwa ajili  kununua mahitaji muhimu kwa waathirika wa mafuriko  hayo  kwa wananchi wa vijiji vya kata tatu  zilizopo katika halmashauri hiyo.

  Hatua  hiyo imetokana na Mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Steven Kebwe na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa  kutembelea eneo la mafuriko  Aprili 26, mwaka huu  kwa kutumia helikopta  ya Polisi na kujionea hali halisi , ambapo pia aliongea  na waathirika wa kijiji  cha Bwila juu , Kubulumo na Kiganila.

  Mkuu wa mkoa , Dk Kebwe alisema na kiasi hicho cha fedha , zimewezesha kununua   tani sita za unga wa sembe na tani mbili  za maharage , mafuta ya kupiki na  chumvi  na kupekewa kwa waathirika kwa kutumia magari makubwa mawili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).


  Mkuu wa mkoa kabla ya kukabidhi msaada huo wa awali kwa mkuu wa wilaya ya Morogoro, Muhingo Rweyemamu, alisema licha ya  wananchi hao kupatwa na mafuriko ,aliwataka  eneo wanaloishi kuhama  kwa kuwa tayari walilipwa fidia kupisha ujenzi wa bwawa la Kidunda.

  “ Tunatoa mdaada huu kutokana na hali ya kibinadamu ingawa tayari walitakiwa kuhama maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa bwawa la Kidunda  baaada ya serikali kupita fidia ...lakini wamendelea kubakia na sasa wamekubwa  na mafuriko haya” alisema Mkuu wa Mkoa.

  “ Hiki chakula kinatolewa kwa awamu ya mwisho , hakitatolewa kingine , na nina agiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri , Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na Mkuu wa Polisi wilaya , watu hawa waondoke maeneo hayo kwa kuwa tayari wamepimiwa viwanja na kulipwa fidia zao” alisisitiza Dk Kebwe.

  Alisema ,kama zilipitika siasa wakati wa uchanguzi mkuu uliopita na kuwafanya waendelee kubakia maeneo hayo kwa  sasa imekwisha na hawana budi kuyahama maeneo hayo wakati taratibu za kumaliziwa malipo y ao za ziada zilifanyiwa kazi na Serikali.

  Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Yona Maki , alisema licha ya  kupatiwa msaada wa awali, pia  mahitaji muhimu yanahitajika kwa haraka  lambayo ni mahema 20 kwa ajili ya makazi kwa waathirika 200 waliotoka kijiji cha Bwila chini na kuhamia eneo la muinuko katika kijiji cha Msonge.

  Maki pia alitaja mahitaji mengine ni  pamoja na kupatiwa boti mbili za kuvusha waathirika na kuwapekelea mahitaji yao ng’ambo ya pili yam to  sambamba na mbegu za mahindi tani 26 na mtama  tani 1.4 ikiwemo muhongo na viazi vitamu na dawa za binadamu.

  “ Waathirika wanaohitaji msaada hadi sasa ni 8,795  kutoka vijiji vitano vya Kata ya Serembara, vijiji viwili kata ya Mvuha , kijiji kimoja kata ya Tununguo na kijiji kingine kimoja kutoka kata ya Mkulazi” alisema Maki.

  Kwa upande wake , Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Kibena Kingo, alisema kuwa pamoja na wananchi walioathiriwa na mafuriko kulipwa fidia inayikadiriwa Sh bilioni saba  na kupewa viwanja kwa ajili ya kuhamia  kupisha ujenzi wa bwawa la Kidunda.

  Pamoja na hayo alisema ,wananchi wa vijiji Kibulumo, Bwila chini , Bwila juu na Vidunda waliolipwa fidia  walishindwa kuyahama makazi yao  baada ya kuwasilisha madai mapya  kuwa  wamepunjwa fidia zao

  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mkurugenzi mtendaji wake kwa nyakati tofauti walisema wananchi waliotakiwa kuhama eneo hilo la bonde  ili kupisha ujenzi wa bwawa la Kidunda walilipwa fidia jumla ya Sh bilioni saba na b ado kulipwa nyongeza ya fidia ya Sh bilioni nne.
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe ( wapili kushoto) akikabidhi kiroba cha sembe kilo 50 ikiwa ni sehemu ya tani sita ya unga huo, kwa Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Muhingo Rweyemamu ( watatu kulia) Aprili 28, mwaka huu baaada ya Ofisi ya Mkuu mkoa kutoa Sh milioni kumi ya kununua vyakula kwa ajili ya kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji kadhaa vya Halmashauri ya wilaya ya Morogoro. (Picha na John Nditi).
  Sehemu ya chakula cha msaada kilichotolewa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa kusaidia waathirika wa mafuriko.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016. nyuma yake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  ​Mstahiki Meya wa Manipsaa ya Iringa, Mh. Alex Kimbe na Mkuu wa Wilaya ya Iring, Mh. Richard Kasesela, Aprili 30, 2015 waliungana na walimbwende walio shiriki na wale watakao shiriki mashindano ya ulimbwende mjini Iringa kufanya usafi katika hospitali ya Rufaa ya Iringa. Zoezi hilo lilianza saa 2 asubuhi hadi saa 4. 

  Mwandaaji wa ulimbwende Iringa Miss Maya alisema wameamua kuhakikisha Iringa inakuwa safi na watafanya usafi kila mara mpaka mji ung'are. 

  Naye Meya wa Manispaa ya Iringa, Mh. Kimbe aliwaomba wadau wote wajitokee kufanya usafi kwa nguvu zote. Mkuu wa wilaya alisema zoezi hili endelevu na wataendelea kuhimiza usafi kwa nguvu zote . Pia alimuomba mstahiki meya kutunga sheria ndogo ndogo kali zenye faini kubwa kwa wanao kaidi suala la usafi.


  0 0


  0 0

  Gisenyi RWANDA

  Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016,kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda,ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

  Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John PombeMagufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

  Wakati wa ziara hiyo,wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

  Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njeya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.

  Kwau pande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Njeya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.

  Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushorobawakati (Central Corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (Standard Gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.

  Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati yaPamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.

  Aidha, Serikaliya Rwanda imeonesha utayari wake wakuleta nchiniMaafisa na Watumishi waSerikali kwalengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).

  Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.

  Mkutano ujao wa kuminatano waTume ya Pamoja yaKudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
  30 Aprili, 2016

  Gisenyi RWANDA

  0 0
 • 04/30/16--23:29: UCHAMBUZI WA MAGAZETI

 • 0 0

  SERIKALI imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani. 

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

  Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.

  Hata hivyo, Dokta Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia  Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo  Tanzania.

  "lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa  na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kulia) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Keneth Kiseke.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam. Kikao kilijadili masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) waliofika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini. Wa kwanza  kushoto ni Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Nishati, Stella Mandago na katikati ni Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tonia Kandiero.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongoza kikao kati ya watendaji wa Wizara, Taasisi zilizo chini ya Wizara na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam. Kikao kilijadili masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini. Kulia kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tonia Kandiero.

  Na Teresia Mhagama

  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeipongeza Tanzania baada ya nchi ya Uganda kuamua hivi karibuni kuwa Bomba la Mafuta Ghafi lenye kipenyo cha inchi 24 kutoka Hoima nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzania hadi  bandari ya Tanga.

   Pongezi hizo zilizotolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, Tonia Kandiero wakati alipofika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam  na kuzungumza na uongozi wa Wizara ukiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

  “Tunawapongeza sana kwa kupata mradi huu muhimu kwa nchi ya Tanzania, napenda kukutaarifu kuwa Benki  ya Maendeleo ya Afrika ipo tayari kufanya kazi nanyi ili mradi huo uweze kutekelezeka kama ilivyopangwa,” alisema Kandiero.

  Akizungumzia utekelezaji wa bomba hilo la mafuta litakalokuwa na urefu wa kilometa 1403, Profesa Sospeter Muhongo  alisema kuwa, hatua inayofanyika sasa ni majadiliano ya wataalam kutoka nchi hizo mbili juu ya mpango wa utekelezaji wa mradi huo ikiwemo masuala ya fedha na watatoa taarifa yao kwa viongozi wa juu wa nchi hizo.

  Alisema kuwa pia kitajengwa kiwanda kwa ajili ya kusafisha mafuta ghafi katika eneo la Hoima nchini Uganda ambapo mradi huo utagharimu Dola za Marekani bilioni 4.7  na kila nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki atakuwa na hisa ya asilimia 8 na kuwajibika kuchangia Dola za Marekani milioni 150.4  ili kutekeleza mradi huo.

  “ Sisi kama nchi tunajipanga kuchukua asilimia zote Nane (8) za hisa hizo na  fedha ambazo tunapaswa kutoa kwenye mradi huu zinaweza kutoka serikalini au Sekta Binafsi hivyo tunaweza kuja AfDB kuzungumza suala hili,” alisema Profesa Muhongo.

  Aidha katika kikao hicho, AfDB iliipongeza TANESCO kwa kutekeleza mikakati mbalimbali inayopelekea deni la Shirika kupungua.

   Watendaji wa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika pamoja Wizara pia walijadiliana  masuala mbalimbali yaliyolenga  kuendeleza miradi ya  Nishati nchini  pamoja na upunguzaji wa deni la TANESCO ili kuliwezesha Shirika hilo kufanya kazi zake kwa ufanisi.

  Aidha Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, alieleza kuwa AfDB inatoa kipaumbele katika uendelezaji wa miradi ya Nishati ili kuliwezesha Bara  la Afrika kuwa na nishati ya  umeme ya uhakika na kwamba wataendelea kutoa ushirikiano  kwa Wizara ya Nishati na Madini ili kuendeleza miradi ya Nishati pamoja na mafunzo.

  0 0

  Na Benedict Liwenga, Maelezo.

  Kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945) alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu kuwahi kutokea katika karne ya 20. 

  Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mbabe huyo aliamka kwa nguvu kupitia Chama hiko cha Wafanyakazi wa Ujerumani na kuchukua udhibiti wa Serikali ya Ujerumani mnamo mwaka 1933.

  Hitler aliamuru uanzishwaji wa kambi za mateso dhidi ya Wayahudi na makundi ya watu wengine huku akiamini kuwa kufanya hivyo ilikuwa chachu na tishio tosha dhidi ya ukuu wa himaya ya Aryani na hatimaye kusababisha vifo vya zaidi ya Wayahudi wapatao milioni Sita.

  Mashambulizi ya Ujerumani dhidi ya nchi ya Poland mwaka 1939 ndiyo yaliyoanzisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo mpaka kufikia mwaka 1941Ujerumani iliteka sehemu kubwa ya ardhi ya Ulaya na Afrika Kaskazini. 

  Ili kuepuka kukamatwa kwa kukwepa utumishi katika jeshi la Austria-Hungary, Adolf Hitler aliondoka toka Vienna na kuelekea Munich mnamo Mei 1913 lakinibaadaye alilazimika kurudi tena.

  Taarifa za kihistoria zinasema kuwa Kiongozi huyo wa Nazi alijiunga na jeshi la Bavaria na kuanza kufanya kazi za kujitolea ambapo mwaka uliofuata alishiriki kikamilifu katika vita ya Kwanza ya Dunia akiwa mstari wa mbele upande wa Magharibi ambapo uzoefu wake katika vita na mapambano uliathiri mawazo, fikra na mitazamo yake yote baada ya hapo.

  Baada ya Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, Hitler alichukua udhibiti wa chama hiko cha wafanyakazi wa Ujerumani kama kiongozi hivyo alitumaini kingemwezesha kushika dola ya Ujerumani punde si punde.

  Aliposhindwa kwenye jaribio la Mapinduzi la mwaka 1923 yeye na wenzake walikamatwa na kufungwa jela na baada ya kutoka jela alijitahidi kukijenga chama hiko na kuanza mikakati ya kukamata dola kwa njia zilizo halali.

  Hitler alikusudia kufanya mageuzi na kuendesha sera za kibaguzi ambazo zingetoa nafasi ya kutosha kwa Wajerumani kuweza kuishi katika himaya kubwa duniani.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (katikati) akifuhia jambo na wanawake wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Iringa Mjini baada ya kumaliza mkutano wake na wanawake hao kwa lengo la kujiwekea mikakati ya kukuza ujasiriamali kupitia Saccoss ya UWT.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) akisalimiana na mkazi wa Iringa mjini, Rebeca Mkwavi ambaye ni mlemavu wa macho jana alipokutana nao katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini, mbunge huyo alitoa msaada wa Sh 1 milioni kwa wanawake walemavu 20 kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiujasiriamali.
  Mkazi wa Iringa Mjini ambaye ni mlemavu wa macho Anna Kaheya (kulia) akipokea kitita cha Sh 1milioni kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) jana kwa niaba ya wanawake wenzake 20 wenye ulemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya ujasiriamali. Mbunge huyo alikutana na wanawake hao Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini zilizopo Sabasaba.

  0 0

   kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaonyeshwa moja ya miradi ya UVCCM wilaya ya Same.

  Na Woinde Shizza, Same

  Wabunge wa upinzani wametakiwa kuwatetea wananchi, kutatua kero zao pamoja na kuwawakilisha vyema wanapokuwa bungeni na sio kufanya kazi ya kutoka nje ya bunge kwa mambo ya siyokuwa ya msingi.

  Hayo yamebainishwa leo na kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Same katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa standi ya Same.

  Alisema kuwa ni jambo la kuchekesha na kushangaza kuona kiongozi ambaye amechaguliwa na mwananchi ili akamuwakilishe kwa kupeleka kero zao bungeni anafika bungeni na kutoka nje kutokana na sababu zisizo za msingi.

  "unajua ni jambo la kushangaza kuona mbunge anasusia kikao cha bunge kisa eti serekali imekata a kurusha vikao vya bunge live sasa jamani uyu mbunge katumwa kuuza sura kwenye televisheni au kupeleka kero za wananchi, mbona awa Wabunge watakuwa kama harusi iliyokosa Vyombo "alisema shaka

  Alibainisha kuwa wananchi wa nataka kutekelezewa ahadi zao na sio kuona sura zao kwenye tv, na kuaidiwa ahadi zisizo tekelezwa.

  Alisema kuwa wananchi wa sasa hivi wanataka maendeleo, na viongozi kuona Sura zao bungeni wakiwa wanafanya mambo ya ajabu na ya kutia aibu wanapokuwa bungeni.

  Aliongeza kuwa iwapo kama viongozi wa upinzani wameshidwa kufanya kazi waliotumwa na wananchi wao basi waachie ngazi kwa kujiuzuru ili waweza kufanya kazi na wanaotambua nini wajibu wao bungeni.

  Aidha Alibainisha kuwa viongozi wa CCM pamoja na serekali wamejipanga vyema kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuwatimizia yale  yote ambayo waliahidi kwa wananchi wakati wa kipindi cha kampeni.

  0 0

  NA EVELYN MKOKOI

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano za Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki usafi wa mazingira wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, mara hii mkoani Simiyu katika wilaya ya Meatu jimboni Kisesa.

  Akizungumza na wananchi wa eneo la Mwandoya wilayani Meatu, Mhe. Mpina amewaasa wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuitunza miti 4820 iliyopokelewa na kupandwa wilayani hapo baada ya serikali ya awamu ya tano kutekeleza ahadi yake ya kuupatia Mkoa wa Simiyu idadi hiyo ya miti.

  Naibu Waziri Mpina, alisema kuwa kwa kuwamkoa wa simiyu huko kwenye hatari kubwa ya kuwa janga na umesha wahi kukabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula, kabla ya uchaguzi uliopita, kwa kuitunza miti hiyo ya matunda wakazi wa mkoa huo watanufaika na miti ya matunda hayo ya muda mfupi kwa kufanya biashara ili kuweza kukuza uchumi na kuongeza kipato cha kila mmoja.
  Aliongeza kuwa, zoezi la upandaji miti mkoani simiyu katika ma shule, maeneo ya makazi ya watu na mashamba yanahitaji utunzani mkubwa kwani miti hiyo ina uwezo mkubwa wa kuboresha uoto wa asili ambao mpaka hivi sasa umetoweka.

  Aidha Mhe. Mpina amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu kuchukua nafasi yao kusimamia wanachi wafanye usafi ikiwa ni agizo la serikali la kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi na kuwa viongozi ambao watakuwa wazembe katika suala zima la usimamiaji wa usafi wa mazingira watachukuliwa hatua.

  Alipoongea na wanachi wa Jimbo La Kisesa, Naibu Waziri Mpina aliwaasa wananchi wa Kisesa wa sapoti jitihada za serikali za kupanda miti na kutunza mazingira, na kuwa hakikishia wapiga kura wake kuwa pamoja na kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, nafasi za kazi yake kama Mbunge wa jimbo hilo ipo pale pale na ataendelea kuwapigania wana Kisesa.

  Aliwaomba wana Kisesa wawe mfano wa kupanda miti iliyotolewa na serikali na kuitunza na kwa aliokosa miche ya miti hiyo iliyogawiwa ame ahidi kuwapatia miche mingine kwani shabaya yake kubwa ni kuwezesha mkoa wa simiyu kupata miti hasa ya matunza na mbao ili kuboresha uchumi binafsi na pato la taifa.

  Mhe. Mpina Amefanya usafi wa mazingira leo katika eneo la hospital ya Mwandoya pamoja na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya utekekezaji wa kampeni ya kitaifa ya kupanda miti.

  0 0
 • 05/01/16--04:30: Article 11
 • FUATILIA HOTUBA YA MHE.RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ''LIVE'' KUPITIA TOVUTI RASMI YA RAIS  

  WWW.IKULU.GO.TZ  

  KUANZIA SAA 3:30.

  NI SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KITAIFA ZINAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JAMHURI MKOANI DODOMA LEO  (MEI MOSI).

  0 0

  Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( wa tatu toka kushoto) pamoja na wafanyakazi wenzake wakifurahia moja ya nyimbo za mwanamuziki Nasib Abdul”Diamaond Platinum’s” alipokuwa akitumbuiza wakati wa hafla ya kuwatunuku zawadi wafanyakazi bora wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Msanii mahiri wa Mziki wa kizazi kipya,Nasibu Abdul 'Diamond Platinum’s ' akitumbuza vilivyo wakati wa hafla ya kuwatunuku zawadi wafanyakazi bora wa Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakicheza na Mwanamuziki anayetamba katika medani ya muziki wa kitaifa na Kimataifa ,Nasibu Abdul 'Diamond Platinum’s ', wakati wa hafla ya kuwatunuku zawadi wafanyakazi bora wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016.  Matembezi hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.  WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.  Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.

   Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani

   Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1204 | 1205 | (Page 1206) | 1207 | 1208 | .... | 3348 | newer