Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

DAWASCO YATOA MKONO WA POLE KWA DADA ASHA CHANDE ALIYEPATA ULEMAVU WA MGUU WAKATI WA KUTAFUTA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha Mkandya akimkabidhi hundi ya sh mil 2.5 Dada Asha Chande Ramadhani ikiwa ni sehemu ya kumpa pole kufuatia kupata ulemavu wa mguu wakati wa harakati ya kutafuta maji .Dawasco imetoa mkono wa pole, Mchele Maharage Unga wa Mahindi na Sukari pamoja na hundi ya Sh. Milioni 2.5.
Asha Chande Ramadhani akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa kutoka Dawasco leo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha Mkandya akiwakatika picha ya pomoja na wafanyakazi wa(Dawasco), leo,jijini Dar es Salaam.

WAZAZI WAWALINDE WATOTO NA AJALI BARABARANI.

$
0
0
Na. Catherine Sungura.
Wazazi nchini wametakiwa kuwakinga watoto wao wakati waendeshapo magari kwa kuhakikisha wanawafunga mikanda ili kuwaepusha na ajali za barabarani na kudhibiti madhara yatokanayo na ajali.


Rai hiyo imetolewa leo jijini hapa na kaimu  kamanda kikosi cha usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu    wakati akifungua  mafunzo kwa Mawakili,Mahakimu ,Waendesha Mashitaka na Askari wapelelezi wa kesi za ajali za barabarani,iliyoandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mpango wa Bloomberg Initiative Global Road Safety.


Alisema wazazi wengi wanapokuwa wanaendesha magari hawawafungi mikanda watoto wao na hivyo ajali inapotokea watoto wanakuwa ni wahanga wakubwa kwa kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu

“Wazazi mnawalindaje watoto,baba anaendesha gari,mtoto yupo kwenye usukani anaendesha nae gari,hiyo siyo sahihi ,tuwalinde watoto wawe salama kwa kuvaa mikanda”


Aidha, Kamanda   Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani nchini imekua ikiongezeka kila mwaka na hii ni kutokana na wananchi kutokuona kama ajali ni tatizo kubwa na la haraka ambalo linafanya kuongezeka kwa vifo nchini kulinganisha na magonjwa mengine na hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa kiuchumi.

LAHAULA! KIJIPU UPELE TEMEKE MWISHO...

$
0
0
Kaka Michuzi napongeza kwa idea yako hii, ni kweli sisi wananchi ndio tunaotakiwa tuonyeshe kero zetu. Leo nakuja na hili suala la kuweka dampo la taka katikati ya makazi ya watu.

Hapa Temeke mwisho jijini Dar es salam kuna Dampo la taka kuubwa limewekwa katikati ya makazi ya watu . sababu ya dampo hili kuwepo hapo mpaka sasa hatujui.Madhara ya dampo hili ni makubwa kuliko faida zake.Kwa mfano wakati huu wa mvua dampo hili limekua likitoa harufu mbaya inayokera sana sisi wakazi, Dampo limekua ni mazalio ya inzi na kusababisha kipindu pindu.

Je nauliza viongozi wa Manispaa ya temeke hawalijui hili, au wanasubiri mpaka kiongozi mkubwa awatembelee ndio atoe amri ya nini kifanyake.

Naambatanisha picha uone hali halisi mjionee Kijipu Upele hiki cha huku kwetu.

MUKUTANO WA MWAKA TANZANISKA RIKSFÖRBUNDET(SWEDEN)

$
0
0


TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN!

BAADA YA MKUTANO TUTAKUWA NA BURUDANI !!!

SIKUYA YA JUMAMOSI TAREHE 30/4!

SAA 12 JIONI.

SEHEMU: Bergshamraskolan , Hjortstigen 1 Solna

VINYWAJI/CHAKULA BEI POA KUTOKA FC-KILIMANJARO!

MGENI RASMI: BALOZI H.E DORA MMARI MSECHU

WOTE MNAKARIBISHWA!

TAFADHALI UPATAPO TAARIFA HII MTAARIFU MWENZIO!

Kwaheri Mpendwa wetu Consolata Haika Venance Kimario.

$
0
0
Tungependa leo kusoma risala na kusema jinsi ambavyo umekuwa ukituletea furaha kila wakati lakini wapi leo tarehe 30 April 2016 tukiwa na moyo wa majonzi twashiriki na ndugu, marafiki pamoja na mwanao mpendwa Beno kusema kwaheri ya kuonana.

Kweli ni huzuni kubwa na ni ngumu kuamini kuwa hatutaona tena tabasamu lako na ucheshi wako.

Tulikupenda sana, ila Mwenyezi Mungu amekupenda Zaidi. Bwana ametoa bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

wana KIFUNGILO.

TANZANIA SISI NYUMBANI (TSN) YAFUNGUA HYPERMARKET JIJINI MWANZA

$
0
0
Ufunguzi wa Hypermarket kubwa kuliko Mwanza unaendelea hivi sasa katika Mall ya Rock City Mwanza.
Hypermarket hii ambayo ni tawi jingine jipya la TSN linatazamiwa kuwahudumia wakazi wa Mwanza waliokuwa wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zikiwemo mbogamboga fresh kutoka hapa hapa nyumbani.
Akizungumza katika ufunguzi huo masaa machache yaliyopita Mkurugenzi wa TSN alisema,Tanzania Sisi Nyumbani  TSN itatoa zawadi kwa watu 100 wa mwanzo kufika katika uzinduzi huo. 
"Hii ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh.. kutoka nyumbani tena kwa bei nafuu.Tanzania Sisi Nyumbani tunahakikisha Watanzania wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni katika Hypermarket hii.. Wateja wetu ni majirani zetu... karibuni sana TSN Hypermarket Mwanza." alisema.
 Sehemu ya mpnagilio wa bidhaa kwa ndani kama zinavyoonekana. 
 Sehemu ya malipo kwa ndani kama inavyoonekana
 Bidhaa ain ya mboga mboga fresh kabisa 
 Bidhaaa mbalimbali zikiwa ndani ya TSN,tayari kwa wateja kuanza 
Watu na wateja mbalimbali wamefika kujionea Hypermarket hiyo ya kisasa kabisa ndani ya jiji la Mwanza.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI IJUMAA APRIL 29, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho kilicho fanyika ofisi ya kata ya Kahe ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini ,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.

Mbunge wa Viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akitoa salamau za pole kwa wakazi wa kata za Mabogini na Kahe walioathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
 Wananchi katika kata ya Kahe wakifurahia pamoja na Wabunge James Mbatia na Lucy Owenya, wakati wa kukabidhi msaada uliotolewa kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


TPDC yatolea ufafanuzi Akaunti za Escrow katika benk ya Stambic

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia. 

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

 Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:
1.Akaunti ya Mapato ya Gesi 
Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2.Akaunti ya Uendeshaji 
Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3.Akaunti ya Kulipia Deni
Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

RC PAUL MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR LEO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda (wa pili kushoto),akiwa sambamba na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Wilaya ya Kinondoni,Ilala pamoja na Temeke wakishiriki kwa pamoja kufagia ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mh Paul Makonda kuzindua kampeni ya Usafi wa jiji la Dar Es Salaam,uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika mapema leo asubuhi Katika viwanja vya .Lidaz Club,Kinondoni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serikali,dini na makundi mengine yakiwemo makundi ya michezo na waendesha boda boda.Mkuu wa Mkoa alizindua kampeni hiyo ya Usafi kwa kuwakabidhi Wenyeviti hao kila mmoja ufagio wa ajili ya kwenda kuwahamasisha wananchi wao katika mitaa yao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda akiwahutubia Wananchi mbalimbali mapema leo asubuhi katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar mara baada ya kumaliza kufanya usafi na hatimae kukusanyika kwenye viwanja hivyo,ambapo Mh.Paul Makonda alizindua kampeni ya Usafi kwa jiji la Dar.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke ndugu Bakari Makere,kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa Paul Makonda katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Usafi kwa jiji hilo.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Juma Mgendwa.
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliokuwa yakijiri uwanjani hapo.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NEWS ALERT: ABIRIA WANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE MJINI BUKOBA LEO

$
0
0
Watu kadhaa wamenusurika kufa, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria mali ya Shirika la Ndege la Auric Air kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa Bukoba, Mkoani Kagera ilipokuwa ikitua. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutokea Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30, 2016. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa. Pichani ni Rubani wa Ndege hiyo akiwasaidia abiria wake kutoka kwenye Ndege hiyo. 

MAPENDEKEZO YA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

$
0
0
NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni.“Mimi pamoja na Waziri wangu, Ummy Mwalimu baada ya kupewa jukumu la kuongoza wizara tuliunda kikundi cha wazee kwa ajili ya kuamua mambo makubwa mawili ambayo tutayatekeleza likiwemo la pensheni kwa wazee wote,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema suala jingine ambalo wamepanga kulitekeleza ni utoaji wa huduma ya bure kwa wazee, ambapo watawapatia bima ya afya ili wasiendelee kusumbuka.Kwa upande wake Waziri Mkuu aliwahakikishia wazee hao kwamba Serikali inawatambua na ndiyo sababu ya waliamua wawe na sehemu ya kufikishia malalamiko yao ambayo ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Kuhusu ombi la wazee hao kwa Rais Dk. John Magufuli la kuwa na uwakilishi Bungeni kwa kupitia nafasi zake 10 za uteuzi, Waziri Mkuu alisema amelipokea na atalifikisha kwa Mhe. Rais.Pia amewataka wapanue taasisi yao na kuimarisha mtandao uweze kujulikana na wazee wengi zaidi, wawe na viongozi kuanzia ngazi za vijiji ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na utoaji wa huduma za afya kwa wazee katika hospitali mbalimbali alizotembelea na kukuta yameanzishwa madirisha maalumu ya kuhudumia.Akizungumzia kuhusu suala la wazee kupewa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI aliwataka waandaaji wa matamasha na semina za mafunzo hayo kujumuisha watu wote wakiwemo wazee.

Naye Mwenyekiti wa mtandao huo , Bw. Sebastian Bulegi alisema lengo la kumtembelea Waziri Mkuu ni kumuomba awafikishie shukurani zao kwa Rais Dk Magufuli kwa kuwapatia wizara maalumu inayoshughulikia masuala yao.“Vile vile shukurani hizi tufikishie kwa mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli kwa kufanya wazee kuwa agenda yake ya kwanza na tayari ameshatembelea makazi ya Nunge Kigamboni (Dar es Salaam) na Bukumbi (Mwanza),”alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na wajumbe wanane wa mtandao huo unaoundwa na Asasi 26 za wazee katika ngazi za wilaya na mkoa kutoka mikoa ya Kigoma, Tanga, Arusha, Mwanza, Lindi na Dodoma, aliiomba Serikali isimamie kutokomeza mauaji ya wazee.Ombi jingine alilolitoa kwa Serikali ni utekelezwaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003, Sera ya Matibabu bure kwa wazee, mafunzo ya kupambana na UKIMWI pamoja na uwakilishi katika ngazi za kutoa maamuzi.

Pia wazee hao wamemhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamekubali ombi linalotolewa na viongozi wakuu wa nchi la kuwataka wawaombee ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA. 
JUMAMOSI, APRILI 30, 2016.

Madereva Pikipiki Waombwa Kufuata Sheria Za Usalama Barabarani

KUNA LUGHA GONGANA HAPA

$
0
0
Dereva wa gari la ubalozi lililogongwa kwa nyuma akijaribu kuongea na dereva na konda wa daladala lililosababisha ajali hiyo. Haikujulikana mara moja kama waliweza kuelewana na yaliishaje maana ripota wetu aliyekuwa anapita kwa gari hakuweza kusimama maeneo ya Msasani jirani na ofisi za ZANTEL jijini Dar es salaam leo.

ACACIA ILIYOSHIRIKI MAONYESHO YA MEI MOSI MJINI DODOMA

$
0
0
  Ofisa Afya na Usalama mahali pa kazi kutoka kampuni ya kuchimba madini ya Acacia Bulyanhulu, Michael Nota (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa ya usalama kwa watu waliofika katika banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya sherehe za mei mosi kitaifa mjini Dodoma jana, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakaz Tanzania (TUCTA).  
Watu wakitoa maoni yao walipofika katika banda la ACACIA 
 Ofisa Afya na Usalama mahali pa kazi kutoka kampuni ya kuchimba madini ya Acacia, Michael Nota akionyesha ramani inayoonyesha maeneo yanayopatikana madini.
 Baadhi ya watu wakipimwa HIV walipofika katika banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Emergency Purpose Officer wa GGM,  Mwaimu Mohamed (kulia) akionyesha vifaa vya kutoa huduma ya kwanza. 

KAMBI TIBA YA GSM na MOI: Oparesheni 55 za vichwa vikubwa zafanikiwa Bugando

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Jumla ya watoto 55 wamenatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo,  chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima. 

Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii,  jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.
Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.

"Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina", alifafanua Dk Kiloloma.

Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio washamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM. 

Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya.

Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.

Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.

Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho juijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.

Kikao cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda, chafanyika mjini Gisenyi

DKT. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Raya Issa Msellem kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.

GALA DINNER, FASHION SHOW, BURUDANI NA KUTOA VYETI KWA WADAU MBALIMBALI DICOTA 2016 DALLAS, TAXAS

$
0
0

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi na wageni wao wakihudhuria gala Dinner ya DICOTA  2016 iliyofanyika siku ya Ijumaa April 29, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency Dallas, Texas nchini Marekani. Katika gala Dinner kulikuwepo Balozi alishiriki utoaji vyeti kwa wadau mbalimbali na yeye mwenyewe kupewa zawadi kutoka menej wa Turkish Air ambao walikua nikati ya wadhamini wa kongamano la DICOTA 2016. Picha na Vijimambo/Kwanza Production.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye gala dinner ya kongamano la DICOTA 2016.
Wadau waliohudhuria kongamano la DICOTA 2016 wakiwa kwenye Gala Dinner siku ya Ijumaa April 29, 2016 katika hotel ya Hyatt Regency Dallas, Texas nchini Marekani.
Gala Dinner ikiendelea.

Compare the Kenya Building Collapse to The SCOAN Building Incident

$
0
0
On April 29th 2016, a seven storey residential building in Nairobi, Kenya collapsed. The structure had failed after days of heavy rains and flooding. Following the collapse, parts of the building remained upright leaving room for rescue teams to save many people from the wreckage.

"Seven people are confirmed dead and 121 people have been rescued and rushed to various hospitals in Nairobi," the Nairobi County police chief told Reuters.

This clearly contrast to the building that collapsed in Lagos, Nigeria at The SCOAN in September 2014. Many have since argued that the collapse at The SCOAN was not as a result of structural failure, but a controlled demolition.

When comparing the two incidents there are notable differences. It can be seen that The SCOAN building did not fall to one side as most do when there is a defect in the structure, but rather it fell on it’s own footprint, on top of itself leaving a slim chance for survival.

On the contrary, when the structure of the Kenyan building failed, it came down on one side leaving parts of the building still standing. This made room for more than 121 people to be rescued from the wreckage leaving only seven people confirmed to be dead as at the time of filling this report.

Another noticeable difference between the two cases is that the Kenyan building did not collapse suddenly but there were warning signs that the structure was failing. Residents were complaining that the building was shaking and making noise before it finally collapsed. "They told me that the house was shaking. When I arrived here I found that the house had collapsed." a resident explained.

Operation Centre director Colonel Nathan Kigotho, told reporters at the scene, "The biggest cause of this was that the building was next to the river. The water most likely undermined the foundation," he said.

Lower floors of the building crumpled, leaving some of the top storey almost intact. Broken bed frames, mattresses and clothes protruded from the wreckage.

Clear CCTV footage of the SCOAN building collapsed shows that the building suddenly came down within a matter of seconds without any previous warning.

Lets not forget the fact that residents of the collapsed Huruma building, Kenya were able to rescue household equipments such as furniture, mattress, kitchen utensils and other household appliances from the debris. Opposite was the case with The SCOAN building incident as there was no trace of the furnitures or household appliances. The entire building came down in dust making it impossible to recover any item from it.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images