Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

APPOINTMENT TO THE CHAIRMAN, VICE CHAIRMAN AND BOARD MEMBERS OF THE TANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA)


Wanafunzi wa International School of Tanganyika watembelea UN Tanzania.

$
0
0
Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN nchini Tanzania (kulia), akitoa somo kwa Wanafunzi wa 'International School of Tanganyika-IST' waliotembelea ofisi hiyo nchini Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali za msingi zinazofanywa na UN.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao mara baada ya ziara yao ya mafunzo kutembelea Ofisi za UN Tanzania.

WADAU WA KAMPENI YA OKOA TEMBO WAZUNGUMZA NA WANA HABARI JIJINI DAR LEO

$
0
0

Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Bw. Shubert Mwarabu (katikati) akielezea kuhus Kampeni yao ya kuokoa Tembo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kampeni hiyo Bw. Lameck Mkuburo pamoja na Bw. Arafat Mtui (wa kwanza kulia).(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

Na Anitha Jonas – MAELEZO

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Okoa Tembo Tanzania imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini kufuatia Tanzania kusaini mpango wa kuwalinda Tembo mwaka 2014 unaozuia uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka 10.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar s Salaam na Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Tanzania Bw.Shubert Mwarabu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Barua ya Wazi waliyomwandikia Mheshimiwa Rais.
Amesema Tanzania inafungwa na mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka (Convetion on International Trade in Endangered Species-CITES) ambao unabainisha kuwa Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala lake la meno ya Tembo.

Amesema uhifadhi wa meno hayo unaigharimu serikali fedha nyingi na kufafanua kuwa kwa sasa Tanzania ina hifadhi kubwa ya meno ya Tembo yaliyokamamwa kutokana na ujangili.
“Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kasi yake ya utendaji tangu kuchaguliwa kwake,tunamuomba atekeleze lengo la tatu la kampeni yetu ya Okoa Tembo wa Tanzania kwa kuliteketeza hadharani ghala la meno ya tembo,tunaona hakuna haja ya kuendelea kuwa na ghala hili” amesema Bw.Mwarabu.
Amesisitiza kuwa ombi lao kwa Rais kutaka ghala la meno ya Tembo liteketezwe kutasidia kutuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa kiasi cha serikali kuona wepesi kuteketeza hazina hiyo.
“ Tunataka ieleweke kwamba kuharibu ghala la meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa ujangili ni kosa la jinai lisilokubalika” Amesisitiza.
Amesema ipo haya ya Tanzania kuunga mkono mpango wao wa kuteketeza ghala la meno ya Tembo kama inavyotarajiwa katika nchi ya Kenya ambayo inatarajia kuteketeza ghala lake la meno ya Tembo hadharani Aprili 30 mwaka huu.Amezitaja nchi ambazo zina mpango wa kuchukua hatua kama ya Kenya kuwa ni Ethiopia,Chad,Gabon, Mozambique na Congo.
Naye mmoja wa wajumbe wa Kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania Bw.Arafat Mtui akizungumza katika mkutano huo amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa ghala hilo nchini Tanzania kunawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno hayo kuona kuwa ipo siku biashara hiyo itaendelea tena.
Amesema Kampeni yao ya Okoa Tembo wa Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa kuwa hatma ya Tembo wa Tanzania iko mikononi mwa watanzania, hivyo ni vema Serikali ikashirikiana na wadau mbalimbali kuchukua hatua madhubuti kuokoa viumbe hao walio hatarini kutoweka kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).Prof. Godius Kahyarara.

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA KATIKA JARIBIO LA UHALIFU WILAYANI CHUNYA MKOANI MBEYA.

$
0
0
 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA.

  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA. 
Mnamo tarehe 27.04.2016 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kijiji na Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu kwenye duka bia la jumla mali ya bwana HAMIS mkazi wa Matundasi.

Inadaiwa kuwa majambazi hao wapatao watano walikuwa wakitumia pikipiki mbili huku pikipiki moja ikibeba majambazi watatu na nyingine majambazi wawili huku wakiwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine walitaka kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuza bia mali ya HAMISI.

Kutokana na taarifa za siri/intelejensia, Jeshi la Polisi lilijipanga kukabiliana na majambazi hao na katika majibizano ya risasi, jambazi mmoja ambaye alikuwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120, risasi 26 kwenye magazine aliuawa baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na mguuni na aliweza kufahamika kwa jina moja BARAKA, anayekadiliwa kuwa na umri kati ya 35 hadi 38, fundi ujenzi mkazi wa Makongolosi.

Aidha majambazi wengine wanne walifanikiwa kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo na ndipo askari polisi waliendesha msako mkali kuelekea kijiji hicho na majambazi hao baada ya kuwaona Polisi waliwasha pikipiki zao kwa nia ya kukimbia huku wakirusha risasi ovyo ndipo Polisi walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili na kukamata Pikipiki moja yenye namba ya usajili MC 761 AFS aina ya Sanlg iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hao.

Majambazi wengine wawili walikimbia na msako mkali unaendelea ili kuwakamata. Miili ya marehemu imehifadhi katika Hospitali ya Wilaya Chunya.

Wito:
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Butusyo A. Mwambelo anatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri ili kuzuia vitendo vya kihalifu mapema kabla ya kutokea.

Imesainiwa na:
 [BUTUSYO A. MWAMBELO – SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. 

WANAMITINDO 3 KUTOKA TANZANIA KUFANYA ONYESHO KWENYE JUKWAA LA "DICOTA" MAREKANI

$
0
0
Katika ulimwengu wa Fashion, bendera ya Tanzania yazidi kupeperushwa kimataifa, wanamitindo maarufu nchini Tanzania ambao kwa sasa wanaishi nchini Marekani yaani hapo namzungumzia Mama wa mitindo Asya Idarous khamsin, Judy & Flora wanategemea kufanya maajabu yao kwa kuonesha mitindo kwenye Onesho kubwa 'Dicota 2016' ambalo linategemea kufanyika Ijumaa ya Tarehe 29 April 2016 "Hyatt Regency North Dallas".

Hivyo kwa wadau wote wa mitindo na watanzania kwa ujumla suport yenu kwa wanamitindo hao, itapelekea ongezeko la ukuaji wa Tasnia ya mitindo Tanzania kwa pamoja tunawatakia Kila la kheri Kwenye onesho hilo.
By Victor Petro

waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi kuwa ya biashara kuchukuliwa hatua

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Rehema Kilonzi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka fedha 2015/2016 ambapo Serikali imekusanya zaidi ya Bilioni 60 kati ya bilioni 70 zilizopangwa.kulia kwake ni mwanasheria toka Wizara hiyo Bw.Seif Hiza na mwisho ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Mboza Lwandiko.

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi na kuyageuza kuwa maeneo ya biashara na kuisababishia Serikali kukosa mapato ya kodi ya Ardhi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Rehema Kilonzi wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka fedha 2015/2016.
Amesema kuwa baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wameyageuza maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya makazi ya watu kuwa nyumba za kulala wageni,hosteli, maeneo ya biashara kinyume cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.

“Rai yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na kumilikishwa kisheria,tunawaomba walipe kodi ya Pango la ardhi kwa wakati kuepuka usumbufu wa kufikishwa Mahakamani .”alisisitiza Kilonzi.
Amesema katika kipindi cha mwaka wa 2015/2016 Serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 60 kutokana na kodi ya Pango la Ardhi ambazo ni sawa na asilimia 85 ya lengo lililowekwa la kukusanya shilingi bilioni 70.
Amesema mkakati wa wizara hiyo ni kuhakikisha kuwa inafikia lengo la kukusanya Kodi hiyo na kuongeza kuwa hiyo imesambaza maafisa wake katika Ofisi zote za Kanda ili kuhakikisha kuwa Halmashauri na Manispaa zinasambaza hati za madai ya Kodi ya pango la Ardhi na kuwafikia wadaiwa wote kwa wakati muafaka.
Amesema wizara hiyo inaendelea na mkakati wa kufungua mashauri ili kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali za wadaiwa sugu na kuwapokonya hati milki katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia hatua hiyo amesema kuwa katika jiji la Dar es salaam mashauri yataanza kusikilizwa katika Baraza ya Nyumba na Ardhi La Wilaya ya Kinondoni kuanzia mwezi Mei 2016, kisha zoezi hilo litaendelea kwa Mikoa na Wilaya zote Jijini hilo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu Kodi ya Ardhi inayotozwa na wizara hiyo amesema kuwa inatozwa kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.
Amesema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu ( kuanzia Februari 2016) Wizara imewafikia wamiliki wa Ardhi 679 katika Maeneo ya Sinza na Kijitonyama Jijini Dar es salaam na kufanya uthamini wa maendelezo kwa kwa wale waliokiuka masharti ya matumizi yaliyopangwa ambapo ilibainika kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Uendelezaji kwa kubadili matumizi yaliyoainishwa katika milki zao.
Aidha, amesema kutokana na uthamini uliofanyika mwezi Februari Serikali inatarajia kukusanya jumla ya milioni mia nane kama faini kutokana na ubadilishaji wa matumizi ya maeneo usiozingatia Sheria za Ardhi katika maeneo ya Sinza na Kijitonyama.

WADAU MBALIMBALI WAOMBWA KUJITOKEZA KUWASAIDIA WALEMAVU

$
0
0
Katibu Mkuu akiwa anatoa msaada katika shule ya watoto wenye ulemavu wa akili  na viungo katika shule ya msingi mreyai iliyoko ndani ya wilaya ya rombo.
 Shaka akiwa anapanda MTI katika shule ya watoto wenye ulemavu mreyai rombo
Shaka akiwa na baadhi ya wanafunzi

Na Woinde Shizza, Rombo.
 
Viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani wao pia ni binadamu wanao sitahili kupata haki na mahitajj muhimu ya kibinadsmu

Hayo yamebainishwa  leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro yenye  huduma ya watoto wenye ulemavu wa viungo na Mtindio wa akili.

Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu watakuwa viongozi wazuri wa baadae. 

Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa hata sehemu ambayo haitakiwi siasa.

"Napenda kuviambia vyama vingine vya siasa, sasa hivi uchaguzi umeisha, ni kipindi cha kufanya kazi na kuachana na  mambo ya siasa, sasa hivi ni kipindi cha kufanya kazi na kutatua matatizo ya wananchi " alisema Shaka.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao ni walemavu wa viungo,amesema kuwa shule hiyo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baiskeli kwa ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.

Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika mabweni hapo shuleni, lakini wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro,  kwani vitanda ambavyo wana vitumia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja kuvichukuwa.

Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto wengine."watoto hawa wana wazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wamewaleta hapa ili wapate elimu, hivyo tunaomba sana serekali na wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema laizer

Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi, sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.

Kikao cha Mwaka cha Menejimenti ya Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika cha UNICEF, kuhitimishwa leo jijini Dar es Salaam

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amelihakikishia Shirika La Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (The United Nations Children's Emergency Fund-UNICEF) kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na shirika hilo katika harakati zake za kuboresha ustawi, kutetea na kulinda haki za watoto duniani.


Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika cha Shirika hilo kilichoanza tarehe 25 Aprili na kinahitimishwa leo kwenye Hoteli ya Ramada.

Dkt. Mahiga alisema kuwa UNICEF ni shirika kubwa linalojulikana duniani kwa mchango wake katika ustawi wa nchi zinazoendelea, hususan katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za kimsingi.

Waziri Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kuhakikisha kuwa watoto wanapatiwa haki zao ipasavyo, hakuna budi UNICEF ikashirikiana na Serikali husika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma harakati hizo. Alizitaja changamoto kubwa kwa ustawi wa watoto ni pamoja na sera, mifumo ya kisheria, ufinyu wa bajeti na urasimu katika taasisi za Serikali. “Tunakabiliwa na changamoto nyingi katika harakati za kuimarisha ustawi, kutetea na kulinda haki za watoto ambazo ili ziweze kutatuliwa kwa wepesi lazima Serikali, UNICEF na wadau wengine tufanye kazi kwa pamoja”.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RC.MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA WAMILIKI WA BENDI KUPELELEKA MAPENDEKEZO MAPYA SHERIA YA KUFANYA BIASHARA HIYO.

$
0
0
Sehemu ya wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika ukumbi wa Vijana leo kuwasilikiliza juu ya kilio wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki juu ya agizo la kufunga kumbi hizo saa sita leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WADAU wa Muziki na wamiliki wa bendi wamekutana kwa ajili kuangalia jinsi ya kuweza kuendesha shughuli zao kutokana na sheria ya muziki kufungwa saa sita.

Akizungumza na Wamiliki wa Bendi na Wanamuziki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watu hao kuunda kamati ya kuona jinsi watavyoweza kubadili sheria kutokana na mazingira ya sasa.Makonda amesema kuwa Watu wenye bendi wanamchango mkubwa katika pato la taifa kutokana na vinywaji kunywewa katika kumbi hizo wakati bendi hizo zikifanya kazi.

Aidha amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa watu wafuate sheria  na amri zikitolewa watu wakubali na sio kila mtu kuamuka kufanya yake pamoja na kuangalia haki ya mtu mmoja inayoadhiri watu wengine

Amesema katika watu wanaofanya biashara hiyo wanatakiwa kuangalia katika vipengele moja ni ya muda gani wa kufanya biashara ,wamiliki wa baa ni muda gani wanaweza kuanza , wapi watu bendi wanaweza kufanya muziki.

Makonda amesema kuna vitu vya kuangalia katika kufanya biashara hiyo kuwa ni sehemu gani watapiga na mazingira je kuna hospitali,shule ,kanisa, msikiti.Amesema kamati lazima iwe na majibu ya vitu ambavyo ni vya msingi katika kuendesha shughuli zao bila kuathiri watu wengine.

Hatimaye mwili wa Papa Wemba wafikishwa Kinshasa

$
0
0
Sehemu ya Waombolezaji nchini Congo, wakipokea Jeneza lenye Mwili wa aliekuwa Mwanamuziki Mkongwe wa Rhumba, Marehemu Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba Maarufu kwa Jina la Papa Wemba, ulipowasili kwenye Uwanaj wa Ndege wa Kimataifa wa Kinshasa, Nchini Congo ukitokea Nchini Ivory Coast. Marehemu Papa Wemba alifikwa na Umauti, katika moja ya Onyesho la Muziki wake, Jijini Abidjan Ivory Coast, hivi karibuni.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinshasa.

KONGAMANO LA MAFUNZO YA UFUNDI YANAYOKIDHI VIWANGO BORA KWENYE SOKO LA AJIRA NCHINI LAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi na Mafunzo ya Ufundi,Prof.Simon Msanjila,akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la Mafunzo ya ufundi yanayokidhi viwango bora kwenye soko la ajira lililoandaiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku mbili la Mafunzo ya ufundi yanayokidhi viwango bora kwenye soko la ajira,wakimsikiliza kwa umakini Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi na Mafunzo ya Ufundi,Prof.Simon Msanjila(hayupo pichani)wakati akizindua kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi na Mafunzo ya Ufundi,Prof.Simon Msanjila,akiongea na waandishi wa habari baada ya kuzindua kongamano la siku mbili la Mafunzo ya ufundi yanayokidhi viwango bora kwenye soko la ajira,lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)jijini Dar es Salaam leo,wapili toka kushoto Mwenyekiti wa bodi ya elimu ya mafunzo,Dkt. Rebecca Sime na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),Dkt.Adolf Rutayuga.

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu.

 Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. 

 Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini. 

 "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena. 

 Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
   Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima. 

MVUA KUBWA YALETA ADHA YA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM

Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu yakikabidhi waendesha bofboda vikoti maalum vya salama barabarani

$
0
0
KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imetoa msaada wa vifaa kusaidia waendesha bodaboda  Mtaa Mbezi A, katika kujiepusha na ajali katika siku  ya usalama  duniani.

Akizungumza wakati wa kakabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Erick Sambu amesema kuwa vifaa walivyopewa vitasaidia katika kujiepusha na ajali kutokana na dereva wa gari kuona kifaa hicho.

Amesema kuwa vifaa hivyo vina thamani ya sh.milioni Nne na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika makundi mbalimbali kutokana na kazi yao ya kuangalia usalama.

Sambu amesema kuwa SGA  katika kuadhimisha siku ya usalama duniani na kuwataka wadau wengine kuunga mkono katika kuwangalia watu bodaboda.

Naye Mwakilishi wa Mwanyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbezi A, Carolyne Ngoda amesema kuwa SGA wameokoa maisha ya vijana wao wanaoshughuli na biashara ya kusafirisa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


 

SGS01
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti maalum la usalama barabarani Bw. Thobias Msua  mmoja wa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4 na wametoa msaada huo kwa waendesha  bodaboda zaidi ya 4000, makabidhiano hayo yamefanyika Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam.
SGS1Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti maalum la usalama barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4
SGS2SGS4
Waendesha Bodaboda wakiwa wamejipanga mara baada ya kukabodhiwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani.
SGS5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi  vikoti maalum vya usalama barabarani  kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni nne.

Supastaa wa Malawi Tay Grin awapania Diamond na Vanessa Mdee

$
0
0
Rapper na supastaa wa Malawi, Tay Grin, amedai kuwa ana mpango wa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. Tay ambaye hivi karibuni aliachia video ya wimbo ‘Chipapapa’aliomshirikisha msanii wa Nigeria, 2 Face Idibia, amesema kuwa hao ni wasanii wa Tanzania anaowakubali zaidi. “Ningependa sana kufanya kazi na wasanii wa Tanzania,” anasema Tay. 
 “Napenda jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoimba. Ni kimuziki sana hata kama sizungumzii Kiswahili, muziki wao unasikika vizuri na ni mtamu. Nimesikiliza wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Alikiba na muziki wao wa Bongo Flava. 
Nadhani Nyau Music inaweza kuchanganyikana vizuri na wasanii hawa wakali. Kwa sasa ninafanyia kazi wimbo na Vanessa Mdee na nina matumani ya kumpata Diamond Platnumz kwenye wimbo huo,” ameongeza. 
 Tay amesema anawakubali wawili hao kutokana na jinsi wanavyojituma na mapenzi yao makubwa kwenye muziki. “Nimekuwa nikifuatilia kazi zao kwa muda sasa na naweza kusema kuwa wamenishika.” 
 Tay ni msanii anayeheshimika zaidi nchini Malawi na amewahi kutumbuiza mara mbili kwenye shindano la Big Brother Africa na amewahi kutajwa zaidi ya mara tano kuwania tuzo za Channel 0. Amewahi kushirikisha wasanii kama Sway (UK), Brick & Lace (Jamaica), Naeto C, Ice Prince, na 2face wa Nigeria), Wahu na Nameless wa Kenya, Double HP, Da Les na Lira wa Afrika Kusini na wengine.

NEWS ALERT: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela Alishiriki katika kufunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD)

$
0
0
​Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela Alishiriki katika kufunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti. 
Mafunzo hayo yenye lengo la kuhimiza mijadala na mazungumzo kati ya sekta binafsi na serikali yaleindeshwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam- Shule ya Boiashara (UDBS) na kudhaminiwa na mradi wa BEST-PPD. Katika hotuba yake ya ufungaji Kasesela alisisitiza sana suala la nidhamu ndio msingi wa kujenga sekta binafsi iliyo imara. 
Pia aliwaasa kupunguza utitili wa jumuiya za sekta bianfsini muhimu zikaungana na kujenga moja yenye nguvu. 
Aliwashauri halmashauri zote kufungua dawati kwa ajili ya mijadala na sekta binafsi. 
" Bila sekta binafsi imara uchumi wa nchi hauwezi kukua, ni muhimu sekta binafsi ikaanza kuchukua nafasi stahiki ikiwemo kutekeleza majukumu mengine kwa niaba ya serikali mfano ukuaji wa michezo mabayo inahitaji uwekezaji ili serikali iondokane na kuwekeza, nchi kama Marekani hazina wizara ya michezo" alisema, baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wadau kutoka wilaya za Njombe, Kilolo, Mfundi na Iringa.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiufunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti mjini Iringa leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



RAIS DKT. JOHN Pombe MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

$
0
0
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kwa barabara kutokea jijini Dar es Salaam leo Aprili 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mango

GLOBU YAKO YA JAMII INAKULETEA MAKALA MPYA YA "MULIKA VIJIPU UPELE"

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Katika kunogesha Libeneke hili, Globu ya Jamii kuanzia leo linazindua makala mpya maalumu itakayojulikana kama “MULIKA VIJIPU UPELE”,  lengo kuu likiwa ni kuanika mambo ya  uzembe, kutowajibika, kujisahau, huduma mbovu, kufanya kazi kwa mazoea na madudu mengine mengi yanayokera jamii. Hii ni katika kutoa mchango wetu mdogo katika kuisaidia serikali ya awamu ya tano kuweka mambo sawa.

Makala hii itakujia wakati wowote “Vijipu Upele” vitapoonekana popote pale nchini. Na katika kutekeleza na kufanikisha hili, pia tunakaribisha michango ya picha na habari kutoka kwenu waheshimiwa wadau wetu. Tuma kwa kupitia email address ya issamichuzi@gmail.com au kwa WhatsApp namba +255 754 271 266, nasi tutairusha hewani mara moja. Hakikisha unataja nini, wapi na lini.

Kwa kuanzia na kama mfano wa zoezi hili, mmulika “Vijipu Upele” wetu ametembelea mji wa Dodoma na kuvinjari katika bustani maarufu  ya  Nyerere Square, na kukuta wana Dodoma wengi wako pale wakipunga upepo ama utengeneza kucha zao na urembo mwingine ama kupiga picha kama ilivyo ada ya mahali hapo.
Lakini  lahaula! Hali aliyoikuta mmulikaji "Vijipu Upele" wetu kwenye mnara wenyewe wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni ya kusikitisha.... 
Wanasema bandubandu humaliza gogo. Na endapo hakuna juhudi za makusudi za kuuokoa mnara huo hazitafanyika haraka, basi mambo yatakuwa mengine, maana  karibu sakafu ya mnarani hapo sio tu inameguka na kuvunjika, bali pia karibu slabs za sakafu yote zimelegea. Hatuna uhakika kwamba tatizo ni kutumika sana kwa watu kutembelea kila siku kwa wingi, ama mafundi waliofanya kazi hiyo alilipua kazi. 
Jionee mwenyewe taswira hizi.....






Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images