Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Article 16


ARUSHA TO HOST EAC SPEAKERS’ FORUM ON FRIDAY

$
0
0
The 11th Meeting of the EAC Bureau of Speakers is to take place in Arusha on Friday this week (April 29th, 2016).

Speakers from the EAC Parliaments (National Assemblies/Senates) and EALA are expected to be in attendance and shall discuss weighty matters of relevance to the integration process.  The meeting is expected to revisit and make amends to the Rules of Procedure of the Bureau of EAC Speakers that guide the Forum.  The meeting will also see the handover of the Chair of the Bureau of Speakers from the Parliament of Tanzania to the East African Legislative Assembly.

The one day meeting shall be preceded by a meeting of Clerks (April 27th and 28th, 2016) which among other things shall review the mandate of the Bureau, discuss modalities of operationalization of the East African Parliamentary Institute (EAPI) and a number of topical issues on emerging challenges in legislature in the region.  The report of the key meeting will feed into that of the Speakers’ Forum for consideration.

The Bureau of the EAC Speakers is the umbrella body that EALA and the National Assemblies utilise to champion the cause of Parliaments in the region, that of enacting legislation, oversight and representation and plays a key advisory role to the Summit of the EAC Heads of State.

The Bureau holds meetings annually under the guidance of a Chairperson who is elected under the principle of rotation.  The inaugural meeting of the Bureau of Speakers was held in May 2008. The decision making process of the Bureau of Speakers is by consensus.

The Treaty for the Establishment of the East African Community places emphasis on the need for EALA and the National Assemblies of Partner States to liaise in several ways in matters related to the Community. 

Article 49(2) (1) of the Treaty provides that “The Assembly (EALA) shall liaise with the National Assemblies of Partner States on matters relating to the Community”.

Mkutano wa Kiroho Columbus Ohio

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

DAWASCO YATAKIWA KUTUPIA JICHO TABAKA LA WASIOJIWEZA

$
0
0
WANAHARAKATI WA Mtandao wa kijinsia “TGNP” wamepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka.

Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel. Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.

“Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu, tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali wakati wa Mkutano na waandishi wa habari juu ya jitihada zinazoendelea kufanywa na DAWASCO katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini.

Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.

“Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji, hivi ni saa ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amehaidi hadi kufikia Disemba 31 watahakikisha kampeni ya mama tua ndoo ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi wa Dar hususani wale walio katika tabaka la chini, aidha amehaidi kutoa huduma ya Majisafi na salama bure kwa wazee, walemavu na yatima wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha huduma ya Maji, pamoja na kujenga pointi za ya kunywea Maji katika sehemu mbalimbali za Jiji ikiwa ni pamoja na maeneo ya stendi ya Mabasi ya Ubungo, Buguruni chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani.

“Mimi pamoja na menejimenti yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya Maji kichwani mpaka kufikia mwishoni wa mwaka huu, kwani Maji yatakuwa mengi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na Pwani” alimalizia Mhandisi Luhemeja
Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.

NEWS ALERT: Harry Kitilya na wenzake wafutiwa shtaka moja, dhamana yagonga mwamba

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mstaafu, Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania,  Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.

Aidha mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado wakihangaikia kupata dhamana baada ya kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo kikubwa cha dhamana.
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

YANGA YAICHAPA MGAMBO SHOOTING BAO 2-1

$
0
0
Kipa wa Mgambo Shooting, Said Khamis akiokoa moja ya hatari langoni mwake katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara lwenye Uwanja wa Taifa. Yanga imeshinda 2-1.
Beki wa Mgambo Shooting, Salum Mlima akichuana na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kusawazisha.
Mshambuiaji wa Yanga, Amissi Tambwe akiwania mpira.
Kikosi cha Mgambo.
Kikosi cha Yanga.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA MAAFISA KUMBUKUMBU NA TAARIFA ZA AFYA TANZANIA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda akifungua, Mkutano wa Watunza kumbukumbu Jijini Dar es Salaam leo.
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mshauri Mkuu wa Chama cha wataalamu hao na Afisa kumbukumbu na Taarifa za Afya Mwandamizi wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Geofrey Semu akizungumza na washiriki hao kabla ya kufunguliwa Mkutano huo  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo mkutano huo unatarajiwa kufungwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  Baadhi ya washiriki  toka Mikoa Mbalimbali wakimsiliza Mkuu wa Mkoa Paul Mamonda (hayupo pichani) na mwenyeji mwenyeji wao, Elizabeth Mlindoko (wa pili kulia) kutoka  Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI).
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Waajiri Wote Wanaodaiwa Malimbikizo Ya Michango Ya NSSF watakiwa Kulipa Michango Kabla Ya Tarehe 30.06.2016

$
0
0
1
Bw. James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo waliohudhuria katika mkutano huo.
2
Baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo.
_MG_5980
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.
.......................................................................................................................................
Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
  1. Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
  1. Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.

Kutowasilisha michango kwa wakati husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.
Ili kuendana na kasi ya Mh. Rais John Pombe Magufuli na “motto” wake wa “Hapa kazi tu” shirika limeandaa mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika jiji la dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya wafanyakazi wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa kuwatembelea waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa shirika watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata mmoja atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya wafanayakazi.
Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye jumla ya shs milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.
Shirika linatoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.
Itakapofika mwezi julai, 2016 shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo mengine lengo la nssf siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho (Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii – NSSF katika kutekeleza majukumu yake.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya nssf, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
  1. Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
  1. Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya nssf no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya nssf na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.
Kutowasilisha michango kwa wakati husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.
Ili kuendana na kasi ya mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli na “Motto” wake wa “hapa kazi tu” shirika limeandaa mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika jiji la dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya wafanyakazi wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa kuwatembelea waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa shirika watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata mmoja atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya wafanayakazi.
Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye jumla ya shs. milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.
Shirika linatoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.
Itakapofika mwezi julai, 2016 shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo mengine lengo la NSSF siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho (Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano kwa hsirika la taifa la hifadhi ya jamii – NSSF katika kutekeleza majukumu yake.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mkutano wa Kiroho Columbus, Ohio, Marekani

MATUKIO YA WATENDAJI WA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma tarehe 27, Aprili, 2016
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi (kushoto) akizungumza na Kamshna Msaidizi Kitengo cha Wenye Ulemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 27, 2015 Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa saba kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo, kulia kwake ni Naibu Waziri (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na kushoto ni Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi katika viwanja vya Bunge Dodoma.
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Musa Uledi mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 27, 2015 Mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza Mratibu wa Taifa wa Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARAF) Bw.Walter Swai nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa shughuli za Bunge Aprili 27, 2016. Picha na PMO

Profesa Mugongo asaini kibali cna kuhamisha leseni.

$
0
0
Na Zuena Msuya
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesaini
kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka

ampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia  Geo-

Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu

ZEM Tanzania Limited.

Akizungumza mara baada ya kusaini kibali hicho leo, jijini Dar es

salaam,Profesa Muhongo amesema kampuni hiyo itaanza shughuli za

uchimbaji mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu 2016, katika

ijiji cha Nyasirori wilayani Butiama Mkoani Mara.

Alifafanua kuwa kusaini kwa kibali hicho kunatoa fursa kwa kampuni

ya china ya uchimbaji wa madini ya ZEM,ambayo iliingia

makubalianao ya kufanya kazi na kampuni ya Henan AfroAsia  Geo-

Engeneering ( Tanzania) mwezi Desemba mwaka 2015.

Gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha dolla za

Marekani mlioni43.3. 

 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo akisaini kibali cha
kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati  wa madini kutoka

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia

Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa

Dhahabu ZEM Tanzania Limited, tukio lililofanyika katika ukumbi

wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini 
 Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini
kitabu cha wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa

Nishati Profesa Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza

kutano wao.

 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela
wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na  Maneja wa

ampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa

pamoja wakionesha kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa

kati  wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China

ya Henan AfroAsia  Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda

Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM Tanzania

Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha

Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba

mwaka 2016.

 Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kulia),
Wakibadilishana mawazo na Kansela wa ubalozi wa China, Gou

Haodong(wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na

Madini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni

chimbaji wa madini katika kijiji cha Nyasirori wilayani

Butiama utakaoanza mwezi Desemba mwaka huo, Maneja wa

Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia

Zhang Jiangbo(kulia)


GEITA GOLD MINE(GGM) YASHIRIKI MAONYESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI MJINI DODOMA

$
0
0
Kampuni ya Dhahabu ya Geita(GGM) imeshiriki maonyesho ya  usalama na afya mahala pa kazi kwenye viwanja vya Jamhuri  mjini Dodoma.Maonyesho hayo yameratibiwa na wakala wa usalama na Afya mahala pa kazi(OSHA) kuelekea maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi Duniani.
Akizungumza kuhusu ushiriki wa Geita Gold Mine(GGM) kwenye maonyesho hayo,Ofisa mawasiliano mwandamizi wa Geita Gold Mine(GGM)  Bw Theophil Pima amesema kuwa kampuni ya GGM ni mdau wa usalama na afya mahala pa kazi na ndiyo sababu ya  kushiriki maonesho hayo.
“GGM inatambua usalama ni kitu muhimu kuliko hata uzalishaji na ndiyo maana imeshaweka tamko kabisa kuwa Usalama ndicho kipaumbele chake kikubwa kuliko vyote katika shughuli zake.Tumekuwa tukishirikiana kwa ukaribu na wakala wa usalama na afya mahala pa kazi na kupatiwa vyeti mbalimbali”alisema Bw Theophil Pima na kuongeza kuwa wafanyakazi wote wa GGM  kabla ya kuanza kazi hupatiwa mafunzo maalumu ya usalama mahala pa kazi ili kuepusha ajali ambazo ni changamoto kubwa kwa migodi mingi Duniani.
Akizungumzia kauli mbiu ya maonesho hayo kuwa "Msongo wa mawazo mahala pa kazi ni changamoto yetu sote", Bw Theophil Pima amesema kuwa Kampuni ya GGM kama zilivyo kampuni zingine inayo changamoto ya baadhi ya wafanyakazi wake kuwa na tatizo la msongo wa mawazo na ndiyo maana wanayo program maalumu ya kuleta madaktari bingwa kutoa ushauri na utaalamu wa kisaikolojia kwenye hospitali yao hapo mgodini.

“Msongo wa mawazo ni changamoto kubwa kwa sababu husababisha mfanyakazi awe na mawazo na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.Wakati mwingine msongo wa mawazo hasa kwa wataalamu wanaoendesha mashine migodini unaweza kusababisha ajali”alisema Bw Theophil Pima na kuwaomba watanzania mkoani Dodoma wajitokeze kwa wingi kwenye banda lao ili kuona vifaa vya kisasa vinavyotumika kwenye masuala ya afya na usalama kwenye kampuni yao.

Akizungumzia maonyesho hayo Mkurugenzi wa usalama na afya kutoka wakala wa usalama na Afya mahala pa kazi(OSHA) Mhandisi Alex Ngata amesema maonyesho kama hayo ni fursa ya kutoa mafunzo  kwa waajiri na wafanya kazi ili watambue nafasi ya afya na usalama mahala pa kazi na namna ya kukabiliana na chngamoto mbalimbali ukiwemo msongo wa mawazo.


 Afisa mawasiliano mwandamizi wa Kampuni ya Geita Gold Mine(GGM) Bw Theophil Pima akizungumza na vyombo vya habari kwenye maonesho ya usalama na afya mahala pa kazi.Pembeni yake ni Afisa Utumishi wa GGM Bw Joseph Mgire(wa kwanza kushoto) na Bw Chacha Magige ambaye ni mratibu wa masuala ya usalama mahala pa kazi GMM.Wengine ni wataalamu kutoka GGM.

 Wakazi wa Dodoma wakitembelea banda la maonyesho la Geita Gold Mine

 Bw Mohamed Mwaimu(katikati)kutoka kitengo cha dharura na uokoaji cha GGM akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya msingi waliotembelea banda la Geita Gold Mine jinsi ya kumuokoa mtu aliyepata ajali ya kumwagikiwa kemikali mgodini.

 Mtaalamu wa afya mahala pa kazi Bw Shija Ayoub akionyesha upimaji wa kelele na vumbi kazini


MJANE WA BABA WA TAIFA MAMA MARIA ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI LEO

$
0
0
Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 27, 2016. 
Mama Maria, ambaye hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo akisema kuwa  ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa hili la Tanzania.
Mama Maria Nyerere na msaidizi wake pamoja na Mwanae Mh. Makongoro Nyerere wakitembelea  Daraja hilo leo kwa furaha na fahari.

Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongolo Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.
Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.
"Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?" Amesisitiza Mama Maria Nyerere.
Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 32, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

KAMPUNI YA “GE POWER” KUPUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI BAKHRESA

$
0
0
Injini ya gesi ya GE aina ya Jenbacher ambayo itauzwa kwa kampuni ya Said Salim Bhakhresa ili kupunguza gharama za uendeshaji.

KAMPUNI ya GE ambayo imejikita kwenye biashara ya uvumbuzi na usambazaji wa nishati (NYSE: GE) leo imetangaza kuipa mamlaka Kampuni ya Clarke Energy inayojishughulisha na masuala ya Nishati. Kampuni hiyo ambayo huuza injini hizo kwa niaba ya GE itasambaza injini ya gesi aina ya Jenbacher na itaiuza injini hiyo moja yenye ufanisi wa hali ya juu kwa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (Bakhresa) ili kukamilisha kituo cha kufua Nishati ya joto. Kituo hicho kitasambaza umeme huo kwenye Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha Azam kilichopo Dar es Salaam, Tanzania na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji za kampuni hiyo kwa mwaka.
"Sisi tuliwachagua GE pamoja na Kampuni ya Clarke Energy hapa Dar es Salaam kutokana na utendaji wao wenye ufanisi mkubwa katika maeneo mengine nchini Tanzania pamoja na urahisi na upatikanaji wa huduma zao kwa wateja hapa nchini" alisema Rajesh Nair, Meneja Ufundi, Said Salim Bakhresa & Co Ltd.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi ndani ya mwambao wa Pwani na kusini, kumekuwa na mabomba mawili ya gesi ambayo yamejengwa nchini ili kusafirisha gesi kutoka kitovu cha uzalishaji kuelekea kwenye maeneo ya matumizi. Bomba la kwanza lilikamilika miaka michache iliyopita na idadi ndogo ya viwanda na wauzaji wa matumizi binafsi waliunganishwa katika bomba hilo. Bomba la pili la gesi ndiyo limemalizika hivi karibuni na kufungulia fursa ya ununuzi wa gesi kwa viwanda vingi zaidi.

"Bakhresa ni moja ya kampuni inayoongoza katika sekta ya viwanda Tanzania na ufungaji wa mtambo huu wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia, utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa,” alisema Hugh Richmond, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Clarke Energy. "Huu ukiwa kama mradi wa kwanza wa kampuni yetu nchini Tanzania, utasaidia kupunguza gharama ya kiwanda kujiendesha huku ukifua umeme wa kuaminika utakaotosheleza mahitaji," alisema Richmond.

Ufungaji wa mtambo huu utaiwezesha Kampuni ya Bakhresa kutumia gesi hii mpya kupata nishati za umeme na joto kwa ufanisi na uhakika. Kampuni ya Clarke Energy huuza kwa niaba ya GE aina ya injini ya gesi Jenbacher J612 yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.82 (MW) za nishati ya umeme. 

Mtambo huu utazalisha pia nishati ya joto ambayo itaingizwa kwenye jiko la mvuke lenye uwezo wa kuzalisha kilowati 1,040. Clarke Energy itakua mvumbuzi kwa kuzalisha nishati ya umeme na joto ambapo hili litafanikiwa kwa kufunga mitambo ya umeme kwenye gridi ya taifa ili kuweza kubeba mzigo wa kilovolti 33”.

"Injini za mtambo wa gesi aina ya Jenbacher J612 huzalisha hewa chafu kidogo, ila huzalisha umeme kwa ufanisi wa hali ya juu,” alisema Oluwatoyin Abegunde, Mkuu wa Biashara GE Distributed Power kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa nishati katika Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika. Alisema," Kwa kuchanganya teknolojia yetu ya uhakika na utaalamu wa Kampuni ya Clarke Energy, kwa pamoja tutazalisha umeme wa uhakika pamoja na suluhisho la kupunguza gharama kwa Kampuni ya Bakhresa na hivyo kuwasaidia kuwa mbele ya viwanda vingine nchini Tanzania.”

Kampuni ya Bakhresa, ni moja ya viwanda vinayoongoza nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo ilizinduliwa mwaka 1970. Leo hii familia ya viwanda vya Bahkresa imezidi kujizolea umaarufu kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwamo nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi. Pia nchi za Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini. Tayari kuna makampuni kadhaa chini ya mwamvuli wake na imewekeza hasa kwenye sekta ya vinywaji, ufungaji vifaa, huduma za baharini, mafuta ya petroli na burudani.

GSM FOUNDATION NA MOI WAANZA KAMBI ZA UPASUAJI BUGANDO

$
0
0
Jumla ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima.

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta (kulia) akiongea na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma (katikati) pamoja na Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba.
Mtaalamu wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando.
Meneja Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba.

SIMU TV: YALIYOJIRI BUNGENI LEO

$
0
0

SIMU.TV: Mhe.Shangazi aihoji serikali juu ya kurejesha silaha kwa wananchi waliopokonywa silaha wakati wa oparesheni tokomeza;  https://youtu.be/fuOH6fmxTmg
 SIMU.TV: Mhe.Mwita aitaka serikali kusimamia wakandarasi kuhakikisha wanajenga mifereji mikubwa katika barabara zote ili kuzuia mafuriko; https://youtu.be/PfxQ7FT8hx8  
 SIMU.TV: Mhe.Kuchaukaa aihoji serikali juu ya utekelezaji wa sera ya ujenzi kama alivyoahidi rais Magufuli katika kampeni; https://youtu.be/AsXZhKe8nPY
 SIMU.TV: Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa atoa ufafanuzi juu ya kukabiliana na balaa la njaa kwa wananchi wa Igunga waliokubwa na mafuriko. https://youtu.be/wPzB45nqFi4

Nape Apania Kuiboresha Tasnia ya Habari

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.

Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.

WAZIRI MKUU KATIKA MATUKIO YA BUNGENI LEO.

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi  (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images