Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1202 | 1203 | (Page 1204) | 1205 | 1206 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Chabaka Kilimunga alikutana na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Comoro (TADICO), tarehe 27 Aprili 2016 katika ofisi za Ubalozi jijini Moroni.

  Pamoja na mambo mengine, uongozi huo mpya wa TADICO uliwasilisha katika yake mpya na kueleza mikakati iliyonayo ya kuboresha utekelezaji wa shughuli za TADICO kwa manufaa ya wanadiaspora waishio Comoro.

  Aidha kwa upande wake Mh. Chabaka alieleza kufurajika na uongozi huo mpya kuja kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha ambapo aliuambia uongozi huo kuwa, Serikali inatilia mkazo mkubwa sana wa ushiriki wa wanadiaspora katika maendeleo ya nchi wanazotoka, hivyo ni muhimu kwa uongozi huo kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuchangamkia fursa mbalimbali zinazoibuka kutoka nyumbani.

  Sambamba na hilo Mhe. Chabaka aliendelea kusisitiza juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya Ubalozi na uongozi wa TADICO.
  Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Comoro (TADICO), mara baada ya kukutana nao kwa mazungumzo. Kutoka kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ahmed Mzee Mbaba, Mweka Hazina wa Jumuiya, Suzan Harun Kalambo, Afisa Ubalozi, Thabit A. Khamis, Mkuu wa Kanseli Ubalozi, Mudrick Soragha, Mwenyekiti wa Jumuiya, Omari Kombo Hussein pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Frank John Kalambo.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Kufanikiwa kwa juhudi za Kutokomeza ugonjwa wa Malaria kutaufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri na salama pa kuishi kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuwawezesha mamilioni ya watu kufikia malengo yao kimaisha.

  Hivi karibuni Tanzania imeungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Malaria duniani ambapo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.

  Takwimu kutoka Shirika la Afya ulimwenguni WHO za mwaka 2002 zinaonyesha kuwa kila mwaka watu kati ya milioni 300 hadi 500 duniani wanapata ugonjwa wa malaria, kati yao watu milioni moja na nusu hufariki kutokana na ugonjwa huo.

  Kulingana na takwimu hizo katika bara la Afrika watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano ndiyo wanaathirika zaidi na ugonjwa wa malaria ambapo kila mwaka watoto milioni tano wanakufa kwa ugonjwa huo barani Afrika.

  Kwa mujibu wa WHO idadi  vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hadi kufikia mwaka 2013 vilipungua kwa takriban asilimia 20 tu duniani kote katika muongo mmoja uliopita ambapo theluthi moja ya nchi 108 ambazo malaria ilikuwa imeenea zilitarajiwa kutokomeza ugonjwa huo katika kipindi cha miaka 10.


  0 0

  Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, aliwasili nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake kwa lengo la kushiriki Kikao cha Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao hicho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia ) akizungumza na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni (kushoto) mara baada ya Waziri huyo pamoja na ujumbe wake kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.
  Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia) akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya ujenzi wa mabomba kutoka Uganda, Habumugisha Johnbosco (kushoto) aliyeambatana na ujumbe wa Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
  Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi Cheti cha Ushiriki Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika wakati wa kilele cha Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi yanaondelea mkoani Dodoma.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika, akikionesha cheti cha ushiriki wakati wa Maonyesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi, yanaondelea mkoani Dodoma.
  Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bw. Athuman Juma akitoa maelezo kwa wananchi , kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamkala hiyo, wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi.
  Afisa Uhusiano na Uhamasiahaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga akifafanua jambo kwa moja wa wadau waliohudhuria Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika mkoani Dodoma.
  Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA, wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa SSRA, Bw. Ally Masaninga katika maonesho hayo.


  0 0
 • 04/29/16--02:12: KUMBUKUMBU
 • Mpendwa wetu Pius Wilfred Shangali, leo ni miaka 8 tangu ulipotuacha katika simanzi isiyoweza kuelezeka kwa maneno wala vitendo, kwa mema yako, tutaendelea kukuenzi na kukumbuka hadi tutakapo kutana tena paradiso.

  Unakumbukwa na wazazi wako Baba Wilfred Shangali na Mama Shangali, wadogo zako Theophil, John, Christer na Bertha pamoja na dada zako Jane na Suzy bila kuwasahau marafiki zako.

  Tutakukumbuka daima Pius. 

  Pumzika kwa Amani.

  Amin.

  0 0

  Wasimamizi wa uchaguzi wakiwa pamoja na mawakala wa wagombea wakihesabu kura mara baada ya kukamilika zoezi la upigaji kura.
  Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wakijumuisha kura ili kujua mshindi katika uchaguzi huo.
  Rais mpya wa ZIFASO na Makamu wake Juma Shirazi Hassan na Makamu wake Zuwena Jaku Hassan wakitoa shukrani na nasaha zao baada ya kuchaguliwa kuongoza Jumuia hiyo kwa mwaka 2016/2017. 
  Wagombea wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa ajili ya kupiga kura.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi . 
  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akiongoza zoezi la ugawaji wa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ,Magonjwa hayo ni Minyoo ya Tumbo,Matende ,Ngirimaji na Usubi, ambapo dawa hizo zinatolewa kwa wananchi wote kuanzia miaka Mitano (5)na kuendelea . 
  Wananchi eneo la kwabwe jijini Mbeya stendi wakisubiri kwa hamu kupatiwa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi mei 2 hadi 5 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa,Jamiimojablog-Mbeya .

  0 0

  Muwakilishi wa Globu ya Jamii Bwana Fadhiri Atick a.k.a Mr.Pengo ambae pia ndiye Msimamizi Mkuu wa Timu ya Vijana wenye Umri wa Chini ya Miaka 18 akikabidhi Jezi kwa Vijana wa timu ya M.P FC (Mr.Pengo Football Club) Waliopo Jijini Mbeya wenye Vipaji vya kucheza Mpira wa Miguu.
  Kutoka Kulia ni Fadhili Atick a.k.a Mr.Pengo akiwa na Kijana wake Dominick katika Picha ya pamoja mara baada ya Kuwakusanya Vijana wenye Vipaji vya Kucheza Mpira wa Miguu na kuunda Timu kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 18 kwa Lengo la Kuwaandaa na  kuwaepusha Vijana kutofikiri au Kutenda Mambo Mbalimbali yasiyo faa katika Jamii kama kuvuta Bangi, Kucheza Kamali, Wizi na Udokozi, kuwaweka vijana kuwa Ngangari na pia kuendeleza Vipaji kwa Vijana hao.
  Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Mr.Pengo Football Club (M.P FC) wakiwa katika Pozz

  0 0

  Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili. 
  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi utakaochangia maendeleo katika sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
  Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov akizungumza kwenye kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo jana Jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana  Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi, anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.Picha zote na (Fatma Salum- MAELEZO)

  0 0

  Tanzania has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the country including rural areas with the aim of achieving gender balance by availing opportunities for girls to acquire skills in science and technical subjects including Information and Communication Technology (ICT).

  The compliments were given yesterday (April 28, 2016)  by the International Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew Rugege when officiating at the opening ceremony of the International Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in Addis Ababa, Ethiopia.

  “ Your Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to convey my regards to your government for its efforts in promoting ICT education for girls as witnessed by four girls who travelled all the way  from Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls, excelled in ICT competition organized by ITU,” he said praising the girls for successful creating useful IT applications that could be used for provision of social services. 

  The four girl students from Tanzania who were invited for the occasion in the Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school in Dodoma.

  READ MORE HERE

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani Serengeti.

  Na Jacquiline Mrisho – Dar es Salaam

  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara 15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.

  Akikabidhi msaada huo Meneja ujirani mwema wa Tanapa, Ahmed Mbugi amesema TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo ya Elimu na Afya katika wilaya hiyo.

  “Mabati haya ni msaada ambao tumeutoa kwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni muendelezo wa misaada tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za maendeleo wilayani hapa” alisema Mbugi.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Naomi Nnko aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za sekondari wilayani humo.

  Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Juma Keya alishukuru kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika mengine ndani na nje ya Wilaya ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri hiyo kuleta maendeleo katika jamii.


  Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Maftah Mohammed aliliomba shirika hilo kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo.


  Mpaka sasa TANAPA imeisaidia Halmashauri hiyo kwenye ujenzi wa maabara katika Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule za Sekondari.

  0 0

  KAMPUNI ya Aspro Capital Limited ni kampuni inayoingia ubia na wajasiliamali kwa kutoa huduma za kitalaam ili kuweza kutatua changamoto zinazomkabili mjasiliamali.

   Sekta binafsi  zaaswa kutoa huduma wanazotoa ziwanufaishe wajasiliamali wadogo kama serikali inavyotarajia na inavyofuatilia kwa karibu huduma zinazotolewa na sekta binafsi kwa wajasiliamali.

  Hayo yamesemwa na 
  Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi wakati akizungumza na wajalisiamali waliokusanywa na kampuni ya 
  Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa serikali imekuwa inafanya jitihada mbalimbali za kuendeleza wajasiliamali wadogo ikiwa ni pamoja kuanzisha mikakati na programu zinazolenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

  Naye 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki amesema kuwa kampuni yao ni muunganiko wa wanahisa ili kusaidia wjsiliamali wadogo kwa upande wa vifungashio pamoja na masoko ya bidha za wajasiliamali wadogo.
  Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi akizungumza na wajasiliamali katika mkutano ulioandaliwa na Kampuni ya Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na uendelezaji wajasiliamali wadogo ambao wanataka kuendelez biashara zao.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki akizungumza na wajasiliamali wadogo ambao wanafanya kazi za mikono katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki na Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi wakiwa katika picha ya pamoja na wajasiliamali wadogo katika mkutano wa Kampuni ya Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga  litakuwa limekamilka kufikia 2020 hivyo kilichobaki ni kuanza utekelezaji wa kuanza kujenga bomba hilo.

  Profesa Muhongo ameyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na waandishi wa habari  juu ya mikakati walioweka katika kutekeleza ujenzi wa bomba hilo, amesema kuwa wataalam katika sekta mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wamekutana leo jijini Dar es Salaam kuweza kuweka mikakati hiyo ya kuanza kutekeleza bomba hilo.

  Muhongo amesema kuwa  kutokana na maagizo  ya Rais Dk.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Mseveni  ya  mradi wa bomba la mafuta watendaji kazi yao ni kuanza kufanya utekelezaji na wataweza kumaliza kabla ya mwaka huo baada ya kupata muongozo wa wataalam wataowasilisha Mei 26  Oima nchini Uganda.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

  Waziri huyo amesema kuwa Uganda imetoa asilimia 40 kwa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweza kununua hisa hizo ili kuwa na sehemu ya kunufaika na bomba hilo ikiwa hisa hizo zinauzwa kwa Dola za Kimarekani Bilioni 4.7.

   Amesema kuwa kwa nchi makini haiwezi kuacha kununua hisa hizo kutokana na faida ya mradi huo na  nchi itakayoacha kununua hisa hizo sio makini.

  Amesema bomba hilo lina umuhimu kwa kujengwa nchini ambapo Tanzania itaweza katika kujenga bomba la gesi kwenda uganda kutokana na uhitaji wa Waganda wa gesi inayozalishwa nchini.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini Profesa James Mdoe ( wa kwanza kushoto, waliokaa mbele); Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kushoto waliokaa mbele) pamoja na wataalam wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni (hayupo pichani) katika mkutano kati ya nchi ya Tanzania na Uganda lengo likiwa ni kujadili mpango wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi, Isack Kamwela akijibu swali la Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam. 
    Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum) alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo Bungeni mjini Dodoma.
  (Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge  wa Ilala  Azzan  Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
  SERIKALI itaendelea kutekeleza ahadi zake ilizoahidi ya kuwapatia maji wananchi wake ikiwemo wakazi wa jiji la Dar es salaam ili kutatua adha ya maji inawakabili katika maenneo yao. 

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack Kamwela wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Ubungo jijini Dar es salaam Saed Kubenea lenye vipengele (a), (b), na (c) lililohoji ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.

  Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali imekamilika na kufanikisha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini na ulazaji wa bomba kubwa lenye kipenyo cha mm 1800 kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 56.

  “Hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam inaendelea kuimarika kwa kuzingatia kuongzeka kwa uzalishaji maji kutoka Ruvu Chini ambao una uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 za maji kutoka lita milioni 180 za awali kwa siku” alisema Mahandisi Kamwela.  

  Katika kuhakikisha jiji hilo linakuwa na maji ya kutosha kwa wakazi wake, Mahandisi Kamwela amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu nao umekamilika na una uwezo wa kutoa maji lita milioni 196 kutoka lita milioni 82 za awali kwa siku.

  Ili kuhakikisha maji yanawafikia walengwa, Mahandisi Kamwela kazi za ulazaji za ulazaji wa mabomba mawili kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tenki jipya la maji eneo la Kibamba na ukarabati wa matenki ya Kimara zimefikia wastani wa asilimia 98, hatua hiyo imewezesha majaribio ya uendeshaji wa mitambo hiyo kuanza mapema Aprili mwaka huu.

  Aidha,  Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Kimbiji na Mpera  ambapo hadi sasa mkandarasi amekamilisha uchimbaji wa visima tisa kati ya visima 20 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu, hadi kukamilika visima hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 260 kwa siku. 

  Hadi sasa uzalishaji wa maji katika jiji hilo umefikia lita milioni 390 kwa siku ikilinganishwa na mahitaji ya lita milioni 450 ya sasa.

  Akijibu swali la nyongeza la Kubenea alioitaka kujua maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ya maji, Mhandisi  Kamwela ameyataja maeneo hayo yatakayonufaika ni pamoja na maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.

  Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.

  Kukamilika kwa miradi yote itaongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam hadi kufikia lita milioni 750 ambayo yatakidhi mahitaji ya wakazi hao hadi kufikia mwaka 2032.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.(Picha na OMR)

  0 0

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob akizungumzana wa wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa kuhama katika eneo hilo na kuhamia katika kituo cha mabasi Simu 2000, leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakijibapanga kwenye maeneo yao waliypewa bure na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo amefanya ziara katika eneo la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la kufanya biashara zao.

  Amewataka wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuwataka kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani wasipofanya hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na imepanga kuwaondoa.

  Meya alieleza kuwa isingekuwa busara kuwaondoa bila kuwaeleza watakwenda wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha ili wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa walipie maeneo ya biashara waliyopewa.

  Pia amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo watalipia,Meya huyo amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa hakuna atakayekosa eneo la kufanya biashara.

  Afisa biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara hao kutokaidi agizo hilo la Meya,hivyo kuanzia kesho wataondolewa kwa nguvu.

  Meya amesema kuna maeneo wamepewa madiwani akiwemo yeye na hayafanyiwi biashara, hivyo sio sawa maeneo hayo wapewe wafanyabiashara.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila pamoja na Kaimu Mthamini Mkuu wa Serikali Bi. Evelyin Mugashwa wakifuatilia taarifa ya viwango elekezi vya bei ya soko la Ardhi nchini katika mkutano na wataalam wa Uthamini Aprili 29, 2016.
   Watalaam wa uthamini wa Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi wakijali taarifa ya viwango elekezi vya bei ya soko la Ardhi nchini iliyowasilishwa kwao na ofisi ya mthamini mkuu wa Serikali Aprili 29, 2016.

  0 0

  WAZIRI wa NCHI ofisini ya WAZIRI Mkuu, Jenista Mhagama(wakwanza kulia), na naibu wake, Dkt. Abdallah Possi.(wapili kulia), walipotembelea banda la WCF, kwenye maonyesho ya Siku ya Usalama na afya mahala pa kazi mjini Dodoma Aprili 28, 2016.Kushoto ni afisa uhusiano mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence.WCF inashiriki maonyesho hayo yaliyoratibiwa na OSHA kwa ushirikiano na TUCTA, ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya Siku ya wafanyakazi Duniani(Mei Mosi).
  Afisa uhusiano mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya OSHA.
  Wananchi wakipatiwa MAELEZO kuhusu mafao ya fidia kwa wafanyakazi kutoka kwa maafisa wa WCF(kushoto).


  0 0

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kushiriki vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kurudi salama mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.

  Pongezi hizo za Spika zimetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kwa niaba ya Spika alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge hadi jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.

  Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni timu za mpira wa miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa kuishinda timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15 wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1 Kushiriki kwa Wabunge katika mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo kati ya pande mbili za Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya zao.

  Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo. Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi mbalimbali katika kujenga na kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani mwema.

  Ushiriki wa Wabunge kwenye mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki michezo mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi mazoezi ya viungo (Gym).
  Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
  Mbunge wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
  Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon aliloliteua Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016 Hyatt Hotel Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016. 
  (Picha na OMR)

older | 1 | .... | 1202 | 1203 | (Page 1204) | 1205 | 1206 | .... | 3348 | newer